Sura ya 25

Muda unapita, na kufumba na kufumbua leo imefika. Chini ya uongozi wa Roho Wangu, watu wote wanaishi katikati ya mwanga Wangu, na hakuna anayefikiria yaliyopita ama kuiwekea jana maanani. Nani hajawahi kuishi katika wakati wa sasa? Ni nani ambaye hajapitia katika siku na miezi ya ajabu katika ufalme? Ni nani hajaishi chini ya jua? Ingawa ufalme umeshuka miongoni mwa mwanadamu, hakuna ambaye amepata kupitia ukunjufu wake; mwanadamu anautambua tu kutoka nje, bila kufahamu dutu lake. Wakati ambapo ufalme Wangu unatengenezwa, ni nani asiyefurahi kwa sababu yake? Je, nchi katika dunia zinaweza kuutoroka kweli? Je, joka kubwa jekundu linaweza kutoroka kwa msaada wa ujanja wake? Amri Zangu za utawala zinatangazwa katika ulimwengu wote, zinaasisi mamlaka Yangu miongoni mwa watu wote, na zinatumika katika ulimwengu wote; hata hivyo, mwanadamu hajawahi kweli kuyafahamu haya. Wakati amri Zangu za utawala zinafichuliwa kwa ulimwengu ndipo pia wakati kazi Yangu duniani itakuwa karibu kukamilika. Nitakapotawala na kuonyesha nguvu miongoni mwa wanadamu wote na Nitakapotambulika kuwa Mungu mmoja Mwenyewe, ufalme Wangu utashuka duniani kikamilifu. Leo, watu wote wana mwanzo mpya kwenye njia mpya. Wameanza maisha mapya, ilhali hakuna yule ambaye amewahi kwa kweli kuyapitia maisha duniani sawa na mbinguni. Je, mnaishi kweli katika mwanga Wangu? Je, mnaishi kweli miongoni mwa maneno Yangu? Ni nani asiyetilia maanani matarajio yake mwenyewe? Ni nani asiye na wasiwasi kuhusu hatima yake? Nani hapambani katika bahari ya mateso? Ni nani asiyetaka kujiweka huru? Je, baraka za ufalme ni kwa sababu ya bidii ya mwanadamu duniani? Je, tamaa zote za mwanadamu zinaweza kutimizwa jinsi anavyotaka? Siku moja Nilionyesha mandhari mazuri wa ufalme mbele wa mwanadamu, ilhali aliuangalia tu kwa macho ya ulafi na hakuna aliyetamani kuingia. Wakati mmoja “Niliripoti” hali ya kweli ya dunia kwa mwanadamu, ila hakufanya chochote zaidi ya kusikiza, na hakutazama maneno yaliyotoka katika mdomo Wangu na moyo wake; siku moja Nilimwambia mwanadamu kuhusu hali ya mbinguni, ilhali aliyachukua maneno Yangu kama hadithi za maajabu, na hakukubali kweli kile ambacho mdomo Wangu ulieleza. Leo, matukio ya ufalme yanaangaza miongoni mwa mwanadamu, lakini kuna mtu ambaye amewahi “kuvuka kilele na bonde” akiutafuta? Bila wito Wangu, mwanadamu asingekuwa ameamka kutoka kwenye ndoto zake. Je, ametekwa sana na maisha yake duniani kwa kweli? Kweli hakuna kiwango cha juu katika moyo wake?

Wale ambao Nimewaamulia kabla kama watu Wangu wanaweza kujitoa Kwangu na kuishi kwa maelewano Nami. Ni wa thamani machoni Pangu, na wanang’aa na upendo Kwangu katika ufalme Wangu. Kati ya watu wa leo, ni nani anayetimiza masharti hayo? Nani awezaye kufikia kiwango kulingana na mahitaji Yangu? Mahitaji Yangu kweli yanaleta ugumu kwa mwanadamu? Je, Ninamfanya atende makosa kwa makusudi? Mimi mwenye huruma kwa watu wote, na Mimi huwachukulia kwa hali ya mapendeleo. Hata hivyo, hii tu ni kwa watu Wangu wa Uchina. Si kuwa Nawachukulia kwa hali ya chini ama kuwa Nawaangalia kwa wasiwasi, bali ni kwamba Mimi Nawachukua kwa matendo na hali halisi. Watu hukutana na vikwazo katika maisha yao bila kuepuka, kama ni kuhusu familia zao ama dunia kwa upana. Ilhali ugumu wa nani umepangwa kwa mikono yao wenyewe? Mwanadamu hana uwezo wa kunijua. Ana ufahamu wa mwonekano Wangu wa nje, ilhali hajui dutu Yangu; hajui viungo vya vyakula akulavyo. Ni nani anaweza kuona kwa uangalifu moyo Wangu? Nani anaweza kuelewa kweli mapenzi Yangu mbele Yangu? Nikija chini duniani, giza limetanda na mwanadamu “amelala fofofo.” Natembea miongoni mwa mahali pote, na yote Nionayo ni yaliyoraruka na matambara na yasiyoweza kuvumilia kuyaona. Ni kana kwamba mwanadamu yuko radhi tu kufurahia, na hana tamaa yoyote kufuata “vitu vya nje, ya ulimwengu.” Bila kujulikana kwa watu wote, Ninaaua ulimwengu mzima, ilhali sioni mahala popote ambapo pamejaa uzima. Hapo papo, Ninaangaza mwanga na joto na kutazama dunia kutoka mbingu ya tatu. Ingawa mwangaza unaanguka juu ya ardhi na joto inatawanyika juu yake, mwangaza na joto pekee ndizo zinaonekana kufurahi; haziamshi chochote kutoka kwa mwanadamu, ambaye anafurahia kwa raha. Ninapoona haya, Ninarejesha mara moja kwa mwanadamu “fimbo” ambayo Nimetayarisha. Fimbo inapoanguka, mwangaza na joto vinatawanywa hatua kwa hatua na dunia mara moja inakuwa ya kuhuzunisha na yenye giza—na kwa sababu ya giza, mwanadamu anatwaa nafasi kuendelea na raha. Mwanadamu ana busara ndogo kuhusu kuwadia kwa fimbo Yangu, lakini haonyeshi hisia, na anaendelea kufurahia baraka zake duniani. Inayofuata, mdomo Wangu unatangaza adhabu kwa wanadamu wote, na watu katika ulimwengu wote watasulubiwa msalabani vichwa vikiangalia chini. Adhabu Yangu inapokuja, mwanadamu anatingizwa na kelele ya milima ikitikisika na ardhi ikipasuka, na baadaye anashtuliwa. Akiwa ameshtuka na mwoga, anatamani kutoroka, lakini ameshachelewa. Adhabu Yangu inapoanguka, ufalme Wangu unashuka juu ya dunia na nchi zote zinapasuliwa kuwa vipande, vikipotea bila kueleza na kutoacha chochote nyuma.

Kila siku Natazama juu ya uso wa ulimwengu, na kila siku Nafanya kazi Yangu mpya kati ya mwanadamu. Ilhali watu wote wanazama kwa shughuli za kazi, na hakuna anayetilia maanani mienendo ya kazi Yangu ama kugundua hali ya vitu zaidi ya wao wenyewe. Ni kana kwamba watu wanaishi katika mbingu mpya na dunia mpya waliotengeneza wenyewe, na hawataki mtu mwingine kuingilia kati. Wote wameshiriki katika kazi ya kujifurahisha, wanajitamani wakifanya “mazoezi ya kimwili.” Kweli hakuna mahali Pangu katika moyo wa mwanadamu? Mimi hakika sina uwezo wa kuwa mtawala wa moyo wa mwanadamu? Roho ya mwanadamu kweli imemwacha? Nani amewahi kuyatafakari kwa makini maneno kutoka kwa mdomo Wangu? Nani amewahi kutambua ombi la moyo Wangu? Je, moyo wa mwanadamu kweli umechukuliwa na kitu kingine? Wakati mwingi sana Nimepaza sauti Nikimwita mwanadamu, lakini je, kuna yule ambaye amehisi huruma? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuishi katika ubinadamu? Mwanadamu anaweza kuishi katika mwili, lakini hana ubinadamu. Je, alizaliwa katika ufalme wa wanyama? Ama alizaliwa mbinguni, na anamilikiwa na uungu? Ninafanya madai Yangu kwa mwanadamu, ilhali ni kana kwamba haelewi maneno Yangu, kana kwamba Mimi ni jitu la kutisha, lililo geni kwake. Mara nyingi Nimevunjwa matumaini na mwanadamu, mara nyingi Nimekasirishwa na utendaji kazi wake duni, na ni mara nyingi Nimesikitishwa na unyonge wake. Mbona sina uwezo wa kuibua hisia ya kiroho katika moyo wa mwanadamu? Mbona Sina uwezo wa kuvuta upendo katika moyo wa mwanadamu? Mbona mwanadamu hataki kunichukulia kama kipenzi chake? Je, moyo wa mwanadamu sio wake mwenyewe? Je, kitu kingine kimechukua makao katika roho yake? Mbona mwanadamu anaomboleza bila kukoma? Ni kwa nini yeye ana taabu? Mbona, wakati yuko na huzuni, hajali uwepo Wangu? Je, inaweza kuwa kwamba Mimi nimemdunga mwanadamu? Je, inawezekana kwamba Nimemwacha mwanadamu kwa makusudi?

Machoni Pangu, mwanadamu ndiye mtawala wa vitu vyote. Nimempa mamlaka si haba, Nikimwezesha kusimamia vitu vyote duniani—nyasi iliyo juu ya milima, wanyama katika misitu, na samaki majini. Badala ya kuwa na furaha kwa sababu ya haya, mwanadamu anasumbuliwa na wasiwasi. Maisha yake yote ni yale ya maumivu makali, na kukimbia hapa na pale, na raha kuongezwa kwa utupu, na katika maisha yake yote hakuna uvumbuzi na uundaji mpya. Hakuna anayeweza kujinasua kutoka katika utupu huu wa maisha, hakuna ambaye amegundua maisha ya maana, na hakuna ambaye amepitia maisha ya kweli. Ingawa watu wa leo wote wanaishi chini ya mwanga Wangu unaong’aa, hawajui lolote kuhusu maisha ya mbinguni. Nisipokuwa na huruma kwa mwanadamu na Nisipomwokoa binadamu, basi watu wote wamekuja bure, maisha yao duniani hayana maana, na wataondoka bure, bila chochote cha kujigamba nacho. Watu wa kila dini, nyanja ya jamii, taifa, na dhehebu wote wanajua utupu ulio duniani, na wote wananitafuta na kungoja kurejea Kwangu—ilhali nani ana uwezo wa kunifahamu nitakapofika? Nilitengeneza vitu vyote, niliumba binadamu, na leo nimeshuka kati ya mwanadamu. Mwanadamu, lakini, anagonga nyuma Yangu, na kulipisha kisasi Kwangu. Je, kazi Ninayofanya kwa mwanadamu haina faida yoyote kwake? Je, Mimi hakika sina uwezo wa kumtosheleza mwanadamu? Mbona mwanadamu ananikataa? Mbona mwanadamu ni baridi na hana hisia Kwangu? Mbona ardhi imejawa na maiti? Je, hii ndiyo hali ya dunia Niliyomtengenezea mwanadamu? Mbona Nimempa mwanadamu mali isiyo ya kufananishwa, ilhali ananipa Mimi mikono miwili mitupu? Mbona mwanadamu hanipendi kwa kweli? Mbona haji kamwe mbele Zangu? Maneno Yangu yote yamekuwa ya bure? Je, maneno yamepotea jinsi joto lipoteavyo kwa maji? Mbona mwanadamu hataki kushirikiana na Mimi? Je, wakati wa kufika kwa siku Yangu ni wakati wa kufa kwa mwanadamu kweli? Je, hakika Ningeweza kumwangamiza mwanadamu wakati ufalme Wangu utatengenezwa? Mbona, wakati wa mpango Wangu wa usimamizi wote, hakuna ambaye ameweza kuelewa nia Zangu? Mbona, badala ya kuyatunza matamshi ya kutoka kwa mdomo Wangu, mwanadamu anayachukia na kuyakataa? Simkashifu yeyote, ila tu Nawafanya watu wote watulie na kutekeleza kazi ya kujiangalia kwa undani.

Machi 27, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 24

Inayofuata: Furahini, Enyi Watu Wote!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp