Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 29

Siku hiyo ambayo vitu vyote vilifufuliwa, Nilikuja miongoni mwa wanadamu, na Nimeshinda naye kwa siku zilizokuwa za ajabu usiku na mchana. Ni katika hatua hii tu ndipo mwanadamu anaona wepesi Wangu wa kufikiwa, na vile uhusiano wake na Mimi unavyozidi kuwa mwingi, anaona baadhi ya kile Ninacho na Nilicho—na kwa sababu hii, anapata ufahamu kunihusu. Miongoni mwa watu wote, Ninainua kichwa Changu na kutazama, na wote wananiona. Hata hivyo, wakati maafa yanaikumba dunia, wanakuwa na wasiwasi mara moja, na sura Yangu inatoweka kutoka katika nyoyo zao; wakishikwa na hofu kutokana na kufika kwa maafa, hawasikii kusihi Kwangu. Nimepita kati ya wanadamu kwa miaka mingi, lakini hajawahi kufahamu hili, na hajawahi kunijua. Leo Namwambia hili kwa kinywa Changu mwenyewe, na kufanya watu wote waje mbele Yangu kupata kitu kutoka Kwangu, lakini bado wanaendelea kukaa mbali Nami, na hivyo basi hawanijui. Wakati nyayo Zangu zitaukanyaga ulimwengu mzima na hadi miisho ya dunia, mwanadamu ataanza kutafakari juu yake mwenyewe, na watu wote watakuja Kwangu na kusujudu mbele Zangu na kuniabudu. Hii itakuwa siku ya utukufu Wangu, siku ya kurudi Kwangu, na pia siku ya kuondoka Kwangu. Sasa, Nimeanza Kazi Yangu miongoni mwa watu wote, Nimeanza kirasmi, katika ulimwengu wote, ukamilishaji wa mpango Wangu wa usimamizi. Kuanzia sasa na kuendelea, wowote ambao si waangalifu wanastahili kutumbukizwa katikati ya kuadibu kusiko na huruma wakati wowote. Hii si kwa sababu Mimi sina utu, lakini ni hatua ya mpango Wangu wa usimamizi; zote lazima ziendelee kulingana na hatua za Mpango Wangu, na hakuna mwanadamu anayeweza kubadili hali hii. Ninapoanza kirasmi Kazi Yangu, watu wote wanatembea kama Mimi hatua kwa hatua, kiasi kwamba watu katika ulimwengu wote wanakuwa katika hatua na Mimi, kuna “shangwe” ulimwengu mzima, na mwanadamu anaendelezwa mbele na Mimi. Kwa sababu hii, joka kubwa jekundu mwenyewe anachapwa na Mimi mpaka anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na wazimu, na anahudumia Kazi Yangu, na, licha ya kutokuwa na nia, anashindwa kufuata tamaa zake mwenyewe, na kukosa njia nyingine ila kujiwasilisha kwa udhibiti Wangu. Katika mipango Yangu yote, joka kubwa jekundu ni foili[a] Yangu, adui Wangu, na pia mtumishi Wangu; kwa hivyo, Sijawahi kushusha “mahitaji” Yangu kwake. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya kazi Yangu katika mwili inakamilika katika nyumba ya joka huyu. Kwa njia hii, joka kubwa jekundu anapata uwezo zaidi wa kunitumikia Mimi vizuri, kwa njia ambayo Mimi Nitamshinda na kukamilisha Mpango Wangu. Ninapofanya kazi, malaika wote wanaanzisha vita vya maamuzi na Mimi na kuamua kutimiza matakwa Yangu katika hatua ya mwisho, ili watu walio duniani wajitoe Kwangu kama malaika, na wasiwe na haja ya kunipinga Mimi, na wasifanye chochote ambacho kinaniasi. Hii ndio elimumwendo ya kazi Yangu kotekote katika ulimwengu.

Madhumuni na umuhimu wa kuwasili Kwangu miongoni mwa mwanadamu ni kuwaokoa wanadamu wote, kuwaleta watu wote katika nyumba Yangu, kuunganisha mbingu pamoja na ardhi, na kufanya mwanadamu kufikisha “ishara” kati ya mbingu na dunia, kwa maana hiyo ndiyo kazi asili ya mwanadamu. Wakati Nilimuumba mwanadamu, Nilifanya mambo yote yawe tayari kwa ajili ya mwanadamu, na baadaye, Mimi Nikamruhusu mwanadamu kupokea utajiri Niliompa kulingana na masharti Yangu. Ndio maana Nasema ni kwa uongozi Wangu ndio maana wanadamu wote wamefikia siku hii. Na haya yote ni Mpango Wangu. Miongoni mwa watu wote, idadi kubwa ya watu ipo chini ya ulinzi wa Upendo Wangu, na idadi kubwa inaishi chini ya kuadibu kwa chuki Yangu. Ingawa watu wote wanaomba Kwangu, bado hawana uwezo wa kubadili hali yao ya sasa; mara tu wamepoteza matumaini, wanaweza tu kuwacha hali asili ichukue mkondo wake na kusitisha uasi Kwangu, kwa maana haya ndiyo yote yanayoweza kukamilishwa na mwanadamu. Inapokuja kwa hali ya maisha ya mwanadamu, mwanadamu bado hajapata maisha halisi, yeye bado hajaona kupita katika udhalimu, ukiwa, na hali duni ya dunia—na hivyo, kama haingekuwa ujio wa maafa, watu wengi bado wangekumbatia hali halisi ya dunia, na bado wangejishughulisha katika ladha ya “uzima.” Je, hii si hali halisi ya dunia? Je, hii si sauti ya wokovu Ninayonena kwa mwanadamu? Kwa nini, miongoni mwa wanadamu, hakuna kamwe aliyenipenda kwa kweli? Ni kwa nini mwanadamu ananipenda tu katikati ya kuadibu na majaribu, lakini hakuna mwanadamu Anayenipenda chini ya ulinzi Wangu? Mimi Nimetoa kuadibu Kwangu mara nyingi juu ya mwanadamu. Wao wanaiangalia, kisha wanaipuuza, na hawawezi kujifunza na kutafakari juu yake kwa wakati huu, na hivyo yote yanayokuja juu ya mwanadamu ni hukumu isiyo na huruma. Hii ni mojawapo tu ya mbinu Zangu za kazi, lakini bado ni kwa ajili ya kumbadili mwanadamu na kumfanya aweze kunipenda.

Mimi Natawala katika ufalme, na zaidi ya hapo, Ninatawala katika ulimwengu mzima; Mimi ni Mfalme wa ufalme na pia Mkuu wa ulimwengu. Kutoka wakati huu na kuendelea, Nitawakusanya wote wasio wateule na Nitaanza kufanya kazi Yangu katika mataifa, Na Nitatangaza amri Yangu ya utawala kwa ulimwengu mzima, ili kwa mafanikio Niweze kuingia katika hatua ifuatayo ya Kazi Yangu. Mimi nitatumia kuadibu ili kueneza kazi Yangu katika Mataifa, ambayo ni kusema, Nitatumia nguvu dhidi ya wale wote walio watu wa Mataifa. Kwa kawaida, kazi hii itafanyika kwa wakati mmoja na ile Kazi Yangu miongoni mwa wale waliochaguliwa. Wakati watu Wangu wanatawala na kushika madaraka duniani ndio pia itakuwa siku ambayo watu wote duniani watakuwa wameshindwa, na zaidi ya hayo, utakuwa wakati Wangu wa mapumziko—na hapo tu ndipo Nitawaonekania wale walioshindwa. Mimi huonekana kwa ufalme mtakatifu, na kujificha kutoka kwa nchi ya uchafu. Wote walioshindwa na kuwa watiifu mbele Yangu wana uwezo wa kuuona uso Wangu kwa macho yao wenyewe, na uwezo wa kusikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe. Hii ni baraka ya wale waliozaliwa katika siku za mwisho, hii ni baraka Niliyoamua kabla, na hii haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Leo, Ninafanya kazi kwa namna hii kwa ajili ya kazi ya baadaye. Kazi Zangu zote zinahusiana, katika yote kuna wito na mwitikio: Kamwe hakuna hatua yoyote iliyokoma kwa ghafla, na kamwe hakuna hatua yoyote iliyofanywa kwa kujitegemea kivyake. Je, hivi sivyo ilivyo? Je, kazi ya siku za nyuma siyo msingi wa kazi ya leo? Je, maneno ya zamani si utangulizi wa maneno leo? Je, hatua za zamani si asili ya hatua za leo? Wakati Ninafungua rasmi hati ya kukunjwa ndio wakati watu ulimwenguni kote wanaadibiwa, wakati watu wote duniani wanakabiliwa na majaribu, na ndicho kilele cha Kazi Yangu; watu wote wanaishi katika nchi bila mwanga, na watu wote wanaishi huku kukiwa na tishio la mazingira yao. Kwa maneno mengine, ni maisha ambayo mwanadamu hajawahi kupitia kutoka wakati wa uumbaji mpaka siku ya leo, na hakuna yeyote katika enzi zote aliyeweza “kustarehe” na aina hii ya maisha, na hivyo Ninasema kwamba Ninafanya kazi ambayo haijawahi kufanyika mbeleni. Hii ndiyo hali halisi ya mambo, na hii ni maana ya ndani. Kwa sababu siku Yangu inakaribia kwa wanadamu wote, kwa sababu haionekani kuwa mbali, lakini iko mbele ya macho ya mwanadamu, ni nani asiyeweza kuwa na uoga kwa sababu ya jambo hili? Ni nani asiyekuwa na furaha katika hili? Mji mchafu wa Babeli hatimaye umefika mwisho wake; mwanadamu amekutana na dunia mpya kabisa, na mbingu na dunia zimebadilishwa na kufanywa mpya.

Wakati Najitokeza kwa mataifa yote na watu wote, mawingu meupe yanaenea angani na kunifunika. Na pia, ndege duniani wanaimba na kunichezea kwa shangwe, wakiangazia hali duniani, na hivyo kusababisha vitu vyote duniani kuwa hai, kusiwe tena na “kuwa vumbi” lakini badala yake kuishi katika hali ya uzima. Wakati Niko mawinguni, mwanadamu anatambua uso Wangu na macho Yangu kwa umbali, na kwa wakati huu yeye anahisi uoga kidogo. Katika siku za nyuma, yeye alisikia “kumbukumbu za kihistoria” kunihusu katika ngano, na matokeo yake ni kuwa anayo imani nusu na nusu shaka Kwangu. Yeye hajui Niliko Mimi, au ukubwa wa uso Wangu—je ni mpana kama bahari, au kama usio na mwisho kama malisho ya majani mabichi? Hakuna anayejua mambo haya. Ni wakati tu mwanadamu anapouona uso Wangu katika mawingu leo ndipo anapohisi kwamba Mimi wa hadithi ni wa kweli, na hivyo anakuwa na upendeleo zaidi Kwangu, na ni kwa sababu tu ya matendo Yangu ndio upendo wake Kwangu unazidi kuwa mkubwa kidogo. Lakini mwanadamu bado hanijui, na anaona tu sehemu moja Yangu katika mawingu. Baada ya hapo, Ninanyosha mikono Yangu na kuionyesha kwa mwanadamu. Mwanadamu anashangaa, na kufunika mdomo kwa mikono yake, akiwa na uoga kuwa Nitampiga chini kwa mkono Wangu, na hivyo anaongeza heshima kidogo kwa upendo wake. Mwanadamu anaweka macho yake juu ya kila hatua Yangu, akiwa na hofu kuu kuwa Nitampiga chini wakati yeye hayuko makini-lakini kutazamwa na mwanadamu hakunizuii Mimi, na Ninaendelea kufanya kazi iliyo mikononi Mwangu. Ni tu katika matendo yote Ninayofanya ndipo mwanadamu ana upendeleo fulani Kwangu, na hivyo hatua kwa hatua anakuja mbele Zangu kujiunga Nami. Wakati ukamilifu Wangu unafichuliwa kwa mwanadamu, mwanadamu atauona uso Wangu, na kutoka hapo Sitauficha au kujikinga kutoka kwa mwanadamu. Katika ulimwengu, Nitaonekana hadharani kwa watu wote, na walio nyama na damu wote wataona matendo Yangu yote. Wale wote ambao ni wa roho hakika wataishi kwa amani katika Nyumba Yangu, na bila shaka watafurahia baraka za ajabu pamoja na Mimi. Wale wote ambao Ninawajali hakika wataepuka kuadibu, na kwa hakika wataepuka maumivu ya roho na maumivu makali ya mwili. Mimi Nitaonekana hadharani kwa watu wote na kutawala na kutumia mamlaka, ili harufu ya maiti isisambae tena ulimwenguni; badala yake, manukato Yangu yataenea katika dunia nzima, kwa sababu siku Yangu inakaribia, mwanadamu anaamka, kila kitu kilicho duniani kiko katika utaratibu, na siku za kunusurika kwa dunia hazipo tena, kwa maana Mimi Nimefika!

Aprili 6, 1992

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 26

Inayofuata: Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp