Sura ya 22

Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu; mwanadamu anatafuta kitu fulani duniani, anaonekana akichakura, anayo nia, inaonekana, ya kusubiri kurudi Kwangu—ilhali yeye hajui siku Yangu, na anaweza tu kutegemea mara kwa mara mwanga unaong’aa mashariki. Miongoni mwa watu wote, Ninatafuta wale wanaoupendeza moyo Wangu kwa kweli. Natembea miongoni mwa watu wote, na kuishi miongoni mwa watu wote, lakini mwanadamu yuko salama salimini duniani, na kwa hivyo hakuna wanaopendeza nafsi Yangu kwa kweli. Watu hawajui jinsi ya kuyajali mapenzi Yangu, hawawezi kuona matendo Yangu, na hawawezi kutembea katika mwanga na kumulikwa na mwanga huo. Hata ingawa mwanadamu daima anayathamini maneno Yangu, yeye hana uwezo wa kuona katika mikakati ya udanganyifu ya Shetani; kwa kuwa kimo cha mwanadamu ni kidogo sana, hana uwezo wa kufanya vile ambavyo moyo wake unatamani. Mwanadamu hajawahi kunipenda kwa dhati. Ninapompandisha, yeye hujiona asiyefaa, lakini hili halimfanyi awe na ari ya kuniridhisha. Yeye hushikilia tu nafasi Niliyompa mikononi mwake na kukichunguza; bila hisia yoyote kwa uzuri Wangu, yeye anasisitiza badala yake kujijaza na baraka za kituo chake. Je, huu sio upungufu wa mwanadamu? Milima inaposonga, je, inaweza kubadili mkondo kwa ajili ya kituo chako? Maji yanaposonga, je, yanaweza kukoma kabla ya kufikia kituo cha mwanadamu? Je, mbingu na dunia zinaweza kubadilishwa na kituo cha mwanadamu? Wakati mmoja Nilikuwa mwenye huruma kwa mwanadamu, mara kwa mara—ilhali hakuna anayependa kwa dhati wala kuthamini haya, waliyasikiliza tu kama hadithi, au waliisoma tu kama tamthilia. Je, maneno Yangu hayauguzi moyo wa mwanadamu? Je, matamshi Yangu kwa kweli hayaleti mabadiliko yoyote? Inawezekana kuwa hakuna anayeamini katika kuwepo Kwangu? Mwanadamu hajipendi mwenyewe; badala yake, anaungana na Shetani ili kunivamia Mimi, na kumtumia Shetani kama “chombo” cha kunitumikia Mimi. Nitapenyeza katika mipango yote ya Shetani, na kuwazuia watu wote wa duniani dhidi ya kukubali uongo wa Shetani, ili wasije wakaniasi Mimi kwa ajili ya kuwepo kwa Shetani.

Katika ufalme, Mimi ni Mfalme—lakini badala ya kunichukulia kama Mfalme, mwanadamu ananichukulia kama Mwokozi aliyeshuka kutoka mbinguni. Kwa sababu hii, anasubiri kwa hamu Nimpe sadaka, na hafuatilii ufahamu Wangu. Wengi sana wamelia mbele Zangu kama waombaji; wengi pia wamenifungulia “mifuko” yao na kunisihi Niwape chakula ili waendelee kuishi; wengi wao wameniwekea macho yenye tamaa, kama mbwa mwitu wenye njaa, wakitamani wanibugie na kujaza matumbo yao; wengi pia wameinamisha vichwa vyao kwa sababu ya dhambi zao na kuona aibu, wakiomba huruma Yangu, au kukubali adhabu Yangu kwa hiari. Ninapozungumza, makosa kadhaa ya mwanadamu yanaonekana ya upuuzi, na umbo lake la kweli linaonekana katika mwanga, na katika mwangaza unaong’aa, mwanadamu hana uwezo wa kujisamehe mwenyewe. Hivyo, anakimbia na kuinama mbele Zangu na kutubu dhambi zake. Kwa sababu ya “uaminifu” wa mwanadamu, Mimi Namvuta tena kwa mara nyingine kwenye gari la wokovu, na kwa sababu hii mwanadamu ana shukurani Kwangu, na kunitupia jicho la upendo. Ilhali bado hana nia ya kujificha kikamilifu ndani Yangu, na hajautoa moyo wake wote Kwangu. Yeye anajigamba tu kwa ajili Yangu, ilhali hanipendi kwa kweli, kwa maana hajaweka mawazo yake Kwangu; mwili wake uko mbele Yangu, ilhali moyo wake uko nyuma Yangu. Kwa sababu kuelewa kwa mwanadamu kwa sheria ni kwa chini sana na hana haja ya kuja mbele Yangu, Mimi Nampa usaidizi unaofaa, ili aweze kugeuka upande Wangu kutoka kati ya upumbavu wake uliokita mizizi. Hii hasa ndiyo huruma ninayompa mwanadamu, na ndiyo njia ambayo nafanya bidii ili kumwokoa mwanadamu.

Watu ulimwenguni kote wanasherehekea kufika kwa siku Yangu, na malaika wanatembea miongoni mwa watu Wangu wote. Shetani anapoleta vurugu, malaika, kwa sababu ya huduma yao mbinguni, daima huwasaidia watu Wangu. Wao hawadanganywi na ibilisi kwa sababu ya udhaifu wa binadamu, ila wanapata uzoefu mwingi wa maisha ya mwanadamu yaliyojawa na ukungu unaosababishwa na uvamizi wa nguvu za giza. Watu wote wananyenyekea chini ya jina Langu, na hakuna wakati ambapo mtu huinuka kwa wazi kunipinga Mimi. Kwa sababu ya shughuli za malaika, mwanadamu anakubali jina Langu na wote wako katika mtiririko wa kazi Yangu. Dunia inaanguka! Babeli imelemaa! Dunia ya kidini—itakosa kuharibiwa vipi na mamlaka Yangu duniani? Ni nani bado anathubutu kuniasi na kunipinga? Waandishi? Wakuu wote wa kidini? Viongozi na wenye mamlaka wa duniani? Malaika? Ni nani asiyesherehekea ukamilifu na wingi wa mwili Wangu? Miongoni mwa watu wote, nani asiyeimba sifa Zangu bila kukoma, ni nani asiye na furaha isiyoshindwa? Ninaishi katika nchi ya kiota cha joka kubwa jekundu, ilhali hili halinifanyi Mimi nitetemeke kwa uoga wala kutoroka, kwa maana watu wa nchi hii wote wameanza kulichukia. Hakuna wakatia ambapo kitu chochote kimefanya “wajibu” wake mbele ya joka kwa sababu ya joka hili; badala yake, vitu vyote vinatenda kama vinavyoona kuwa bora, na kila kitu kinaenda kufanya shughuli zake. Je, mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuangamia? Mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuanguka? Watu Wangu watakosaje kushangilia? Watakosaje kuimba kwa furaha? Je, hii ni kazi ya mwanadamu? Je, ni tendo la mikono ya mwanadamu? Nilimpa mwanadamu mzizi wa kuwepo kwake, na Nikampa vitu halisi vya dunia, ilhali mwanadamu haridhiki na hali yake ya sasa na anauliza kuingia katika ufalme Wangu. Lakini atawezaje kuingia katika ufalme Wangu kwa urahisi vile, bila kulipa gharama yoyote, na bila nia ya kujitoa kwa kujinyima? Badala ya kulazimisha chochote kutoka kwa mwanadamu, Mimi huweka mahitaji kwake, ili ufalme Wangu duniani ujawe na utukufu. Mwanadamu ameongozwa na Mimi mpaka enzi ya sasa, anaishi katika hali hii, na anaishi katika mwongozo wa mwanga Wangu. Kama haingekuwa hivyo, nani kati ya watu wote duniani angejua matarajio yake? Ni nani ambaye angeelewa mapenzi Yangu? Ninaongeza matoleo Yangu katika mahitaji ya mwanadamu; je, hii haiambatani na sheria za hali asili?

Jana uliishi kati ya upepo na mvua, leo hii umeingia katika ufalme Wangu na kuwa watu wake, na kesho utafurahia baraka Zangu. Ni nani aliwahi kuwaza juu ya mambo kama haya? Je, ni dhiki na ugumu kiasi gani utakayopitia maishani mwako, je mnajua? Mimi naendelea kati ya upepo na mvua, na nimeishi mwaka baada ya mwingine miongoni mwa wanadamu, na hiyo inafuatwa na wakati wa sasa. Je, hizi sio hatua za mpango Wangu wa usimamizi? Ni nani amewahi kuongeza chochote katika mpango Wangu? Ni nani anaweza kuepuka hatua katika mpango Wangu? Naishi katika nyoyo za mamia ya mamilioni ya watu, Mimi ni Mfalme miongoni mwa mamia ya mamilioni ya watu, na nimekataliwa na kushutumiwa na mamia ya mamilioni ya watu. Mfano Wangu hauko kwa kweli ndani ya moyo wa mwanadamu. Mwanadamu anaona tu kwa umbali sura Yangu ya utukufu katika maneno Yangu, lakini kwa sababu ya hitilafu iliyo katika mawazo yake, haamini hisia zake mwenyewe; kuna uwepo Wangu usioeleweka vizuri ndani ya moyo wake, lakini uwepo huo haukai ndani yake kwa muda mrefu. Na kwa hivyo, upendo wake Kwangu pia uko vilevile: Upendo wake Kwangu unaonekana vizuri, ni kama kila mwandamu alinipenda kutokana na tabia yake, kana kwamba upendo wake ulikonyeza ndani na nje ya kuonekana chini ya mbalamwezi hafifu. Leo, ni kwa sababu tu ya upendo Wangu ndiyo maana mwanadamu bado yupo na ana bahati nzuri ya kunusurika. Kama haingekuwa hivyo, nani kati ya wanadamu, kwa sababu ya kunyauka kwa miili yao, asingeuawa na mwale wa moto? Mwanadamu bado hajielewi. Anajionyesha akiwa mbele Yangu, na kujigamba mwenyewe akiwa nyuma Yangu, ilhali hakuna anayethubutu “kuniasi” akiwa mbele Yangu. Hata hivyo, mwanadamu hajui maana ya upinzani Ninaozungumzia; badala yake, yeye anajaribu kunipumbaza Mimi, na anaendelea kujipandisha—na kwa hili, je, si ananipinga kwa wazi? Ninavumilia udhaifu wa mwanadamu, lakini Sina huruma hata kidogo kwa uasi ambao mwanadamu ameufanya mwenyewe kwa kujua. Hata ingawa anajua maana yake, yeye hana nia ya kutenda kulingana na maana hiyo na hutenda kutokana na kupenda kwake ananidanganya Mimi. Mimi huweka wazi mwenendo Wangu katika maneno Yangu kila wakati, ilhali mwanadamu hapataniki na kushindwa—na wakati uo huo, anadhihirisha mwenendo wake. Katika hukumu Yangu mwanadamu atashawishika kikamilifu, na katikati ya adhabu Yangu mwishowe ataweza kuishi kwa kudhihirisha mfano Wangu na kuwa udhihirisho Wangu duniani!

Machi 22, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 21

Inayofuata: Sura ya 23

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp