Sura ya 27

Kamwe mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, daima Mimi huwa mkali kwake kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu. Hatimaye, kila kitu cha mwanadamu kinaanguka mbele Yangu bila mnong’ono; mwanadamu kimeporomoka polepole mbele Yangu, na ni katika nyakati kama hizi ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi. Hali ya mwanadamu haibadiliki kamwe. Kilicho ndani ya mioyo yao sio kulingana na mapenzi Yangu—sio Ninachohitaji. Jambo Ninalochukia zaidi ni ugumu na uhalifu sugu wa mwanadamu na ukaidi sugu, lakini ni nguvu zipi ambazo huwachochea wanadamu waendelee kushindwa kunijua, kuwafanya waniweke mbali na wao kila mara, na kutotenda kulingana na mapenzi Yangu mbele Yangu kamwe lakini kunipinga nyuma Yangu? Je, huu ndio uaminifu wao? Huu ndio upendo wao Kwangu? Mbona wasitubu dhambi zao na kuzaliwa mara ya pili? Mbona binadamu hupenda kuishi kwenye chemichemi badala ya kuishi mahali pasipo na matope? Inawezekana kuwa Mimi Nimewadhulumu? Inawezekana kuwa Mimi Nimewapotosha? Inawezekana kuwa Mimi nimewaelekeza kuzimu? Kila mtu anataka kuishi “kuzimu.” Mwangaza unapotokea, macho yao hupofuka ghafla, kwa kuwa kila chao kinatoka kuzimu. Ilhali watu hawana ufahamu wa mambo haya na wanafurahia tu “raha za motoni.” Wao hata hushikilia kwa nguvu karibu na vifua vyao kama hazina wakihofu kwamba Mimi nitazinyakua hazina hizi, hivyo kuwaacha bila kiini cha kuwepo kwao. Wanadamu wananiogopa na ndio maana wao hukaa mbali na Mimi na kutokaa karibu Nami Ninapokuja duniani kwa maana “hawapendi kujiletea madhara,” wakiwa na ombi la kuishi maisha ya amani katika familia yao ili wawe na “maisha ya furaha duniani.” Lakini Siwezi kuruhusu wanadamu watende vile wanavyotaka, kwa kuwa lengo Langu hasa ni kuziangamiza familia zao. Kunzia wakati Nifikapo, amani inatoweka katika nyumba zao. Nakusudia kusambaratisha mataifa yote yatawanyike, sembuse familia ya mwanadamu. Ni nani awezaye kuepuka mkono Wangu? Itawezekanaje kuwa wale wanaopokea baraka wataepuka kwa sababu ya kutonuia kwao? Itawezekanaje kamwe kuwa wale walioadibiwa watapata huruma Yangu kwa sababu ya wao kuwa na woga? Katika maneno Yangu yote, wanadamu wameona mapenzi Yangu na kuona matendo Yangu, lakini ni nani awezaye kuondokana na minyororo ya mawazo yake mwenyewe? Ni nani anaweza kupata njia kutoka ndani au nje ya maneno Yangu?

Mwanadamu ameshuhudia upendo Wangu, mwanadamu amenitumikia kwa dhati, na mwanadamu amenitii kwa kweli, akinifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Ilhali jambo hili haliwezi kutimizwa na watu ; wanalia tu katika roho zao kana kwamba wamenyakuliwa na mbweha mwenye njaa, na wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, wakinililia bila kukoma. Lakini mwishowe, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba. Ninakumbuka jinsi ambavyo watu wa kale waliweka ahadi mbele Zangu, wakiapa kwa mbingu na dunia mbele Zangu kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo, kigumu kuvumilia. Kwa sababu ya azimio lao, mara nyingi niliwapa watu msaada. Mara nyingi, wanadamu wamekuja mbele Zangu kunitii, mienendo yao ya kupendeza isiyoweza kusahaulika. Mara nyingi, wamenipenda bila kutikisika katika uaminifu wao, bidii yao ikiwa ya kupendeza. Mara nyingi, wamenipenda hadi kiwango cha kuhatarisha maisha yao, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe—na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara nyingi, wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kumekuwa na nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama kitu kinachothaminiwa, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hata hivyo, kile kilicho fikirani Mwangu hakiwezi kueleweka na mwanadamu. Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Lakini, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani anayeweza kutibu kidonda kilicho moyoni Mwangu? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayejitolea kushirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini kwamba hakuna lolote kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, haya yote si kwa sababu ya mwanadamu kupotoshwa na adui yake?

Malaika wanapocheza muziki wakinisifu, hii inasisimua huruma kwa ajili ya binadamu. Moyo wangu unajawa na huzuni ghafla, na inakuwa vigumu kujiondoa katika hisia hii ya kuhuzunisha. Katika furaha na huzuni ya kutengana na kisha kuunganika Kwangu na mwanadamu, hatuwezi kubadilishana mawazo. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, nyakati ambapo Mimi na mwanadamu tunaweza kukutana ni nadra sana. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hangetamani kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejaa wasiwasi mwingi. Licha ya sisi kuwa katika nafsi moja, hatuwezi kuwa pamoja mara kwa mara, na hatuwezi kuonana mara kwa mara. Kwa sababu hii, maisha ya wanadamu wote yamepata pigo kuu na hayana nguzo za nguvu muhimu, kwa sababu wamekuwa na hamu kuu Kwangu. Ni kana kwamba wao ni viumbe waliorushwa kutoka mbinguni, wakiliita jina Langu kutoka duniani, wakiinua macho yao Kwangu kutoka ardhini—lakini wanawezaje kuepuka kutoka kwa midomo ya mbwa mwitu mlafi? Wanawezaje kujiokoa kutokana na tishio na majaribu yake? Binadamu wanawezaje kukosa kujitolea kwa sababu ya kutii utaratibu wa mpango Wangu? Wanaponisihi kwa sauti, Ninageuza uso Wangu kutoka kwao, kwa maana Sitaki kushuhudia zaidi ya hayo; Lakini, itawezekanaje Nisisikie vilio vya watu hawa? Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakataza maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui Wangu wote waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni, hasira imechanganywa, Nitaukanyaga ulimwengu wote sawasawa, bila kumwacha yeyote, na kuwatia maadui Wangu hofu kubwa. Naiangamiza dunia nzima, na kuwafanya maadui Wangu waanguke katika maangamizo hayo, ili kuanzia sasa na kuendelea wasiwapotoshe wanadamu tena. Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeubadilisha. Ninapotembeatembea kwa fahari kuu ulimwenguni, wanadamu wote watafanywa wapya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwanadamu hatalia tena, hatanililia tena akitaka msaada. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo …

Leo hii, miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, Ninaendeleza kazi Niliyokusudia kukamilisha. Ninamtembelea kila mmoja, Nikifanya kazi Yangu jinsi Nilivyopanga, na binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine kulingana na mapenzi Yangu. Watu walio duniani wameweka mawazo yao kwa hatima zao wenyewe, kwa maana siku yenyewe hakika inakaribia na malaika wanacheza parapanda zao. Hakutakuwa na kuchelewa tena, na kila kiumbe ataanza kucheza kwa shangwe. Ni nani anayeweza kusongeza siku Yangu kwa uwezo wake? Inawezekana kiwe kiumbe cha duniani? Zinaweza kuwa nyota angani au malaika? Ninapotoa tamko la kuanza ukombozi wa wana wa Israeli, siku Yangu inawaelekea watu wote wa ulimwengu. Kila mwanadamu anahofia kurejea kwa taifa la Israeli. Israeli itakaporejea, hiyo itakuwa siku Yangu ya utukufu, na pia, itakuwa siku ambayo kila kitu kitabadilika na kuwa kipya. Hukumu ya haki inapoukaribia ulimwengu, watu wote watakuwa na woga na hofu, kwa maana ulimwengu wa mwanadamu haufahamu haki. Wakati ambapo Jua la haki litaonekana, Mashariki itaangazwa, kisha litaangaza ulimwenguni kote, likimfikia kila mtu. Iwapo mwanadamu atatenda haki Yangu, ni kitu gani kitakuwa cha kuogopesha. Watu Wangu wote wanangoja siku ya kurudi Kwangu, wanatarajia kwa hamu siku Yangu. Wanangoja Mimi niwaadhibu wanadamu wote na kupanga hatima ya wanadamu katika wajibu Wangu kama Jua la haki. Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya mamia ya milioni nyingi za watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Wanangu na watu Wangu wote wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama yoyote iliyolipwa? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, aidha, Nitashinda nguvu zote za adui. Wakati umewadia! Nitaianza kazi Yangu, Nitatawala miongoni mwa wanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nitawaruhusu binadamu wote watazame kufika kwa siku Yangu na wote watakaribisha siku Yangu kwa furaha tele!

Aprili 2,1992

Iliyotangulia: Sura ya 26

Inayofuata: Sura ya 28

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp