Waovu Hakika Wataadhibiwa

Jichunguzeni ili mwone kama mnatenda haki katika kila jambo mnalotenda, na iwapo matendo yenu yote yanachunguzwa na Mungu: Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo wale wanaomwamini Mungu wanafanya shughuli zao. Mtaitwa wenye haki kwa sababu mnaweza kumridhisha Mungu, na kwa sababu mnakubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji wa Mungu, na wale wanaopatwa na Yeye, ni wenye haki, na Yeye huwaona kuwa wenye thamani. Kadri mnavyozidi kuyakubali maneno ya sasa ya Mungu, ndivyo mtakavyozidi kuweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu, na ndivyo basi mtakavyoweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu na kuyakidhi mahitaji Yake zaidi. Hili ndilo agizo la Mungu kwenu na ndilo jambo ambalo nyote mnapaswa kuweza kufikia. Mkitumia fikira zenu wenyewe kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, na mkimwekea Mungu mipaka kabisa katika vigezo vya Biblia na kumweka katika mawanda ya kazi yenye mipaka, basi hii inathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu Wayahudi katika Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo lisilobadilika waliloshikilia mioyoni mwao, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yeye aliyeitwa Masihi pekee ndiye Angeweza kuwa Mungu, na kwa sababu binadamu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—hivyo Yesu asiye na hatia Alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na kosa lolote, mwanadamu alikataa kumsamehe, naye alisisitiza kumhukumu afe na basi Yesu akasulubishwa. Kila wakati mwanadamu huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu ana ufahamu wa kina kuhusu usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwanadamu anavyo vitu vyote atendavyo Mungu katika kiganja cha mkono wake. Wanadamu ni wapumbavu kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha kutia chumvi sana wanapoelezea jambo. Bila kujali jinsi kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu kilivyo, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba wewe ni mtu ambaye humpinga Mungu zaidi, na kwamba umemshutumu Mungu, kwa sababu huna uwezo kabisa wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kamilifu na Mungu. Kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana fikira nyingi sana, na kwa sababu maarifa yake kuhusu Mungu hayaafikiani na uhalisi hata kidogo, lakini badala yake hurudia tu mada ile ile bila mabadiliko na hutumia mwelekeo ule ule katika kila hali. Na hiyo, kwa kuwa Amekuja duniani leo, Mungu anasulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu. Wanadamu dhalimu! Kuwafumba watu macho na kula njama, kupokonyana na kunyang’anya mmoja kutoka kwa mwingine, kung’ang’ania umaarufu na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amezungumza, hakuna hata mmoja ambaye ameacha kufanya upumbavu. Watu hutenda kwa ajili ya familia zao, watoto wao, kazi zao, matarajio yao ya baadaye, cheo, majivuno, na pesa, kwa sababu ya chakula, mavazi, na mwili. Lakini kuna yeyote ambaye matendo yake kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao wanatenda kwa ajili ya Mungu, kunao wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni watu wangapi ambao hawatendi kwa ajili ya maslahi yao? Ni wangapi wasiowakandamiza na kuwatenga wengine ili kulinda vyeo vyao wenyewe? Na hivyo, Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, na mahakimu wakatili wengi mno wamemhukumu Mungu na kumsulubisha msalabani tena. Wangapi wanaweza kuitwa wenye haki kwa sababu wanatenda mambo kwa ajili ya Mungu kwa kweli?

Je, ni rahisi sana kukamilishwa mbele ya Mungu kama mtakatifu au mtu mwenye haki? Ni kauli ya ukweli kwamba, “hakuna wenye haki katika dunia hii, wenye haki hawapo katika dunia hii.” Mnapokuja mbele za Mungu, fikirieni kile mnachovaa, tafakarini kila neno na kitendo chenu, juu ya kila fikira na wazo lenu na hata ndoto mnazoota kila siku—vyote ni kwa manufaa yenu wenyewe. Je, hivi sivyo hali halisi ilivyo? “Haki” haimaanishi kuwatolea wengine sadaka wala haimaanishi kumpenda jirani yako vile unavyojipenda na haimaanishi kuepukana na mizozo na ugomvi, au kunyang’anya na kuiba. Haki inamaanisha kuchukua agizo la Mungu kama wajibu wako na kuiheshimu mipango na utaratibu wa Mungu kama wito wako utokao mbinguni, bila kujali wakati ama mahali, kama tu yote ambayo Bwana Yesu aliyafanya. Hii ndiyo haki ambayo amezungumzia Mungu. Kwamba Lutu aliweza kuitwa mwenye haki ni kwa sababu aliwaokoa wale malaika wawili waliotumwa na Mungu bila kuzingatia faida ama hasara yake mwenyewe; inaweza kusemwa tu kwamba alichotenda wakati huo kinaweza kuitwa haki, lakini hawezi kuitwa mwanadamu mwenye haki. Ilikuwa tu ni kwa sababu Lutu alikuwa amemwona Mungu ndipo akawatoa wasichana wake wawili badala ya malaika, lakini tabia yake yote ya hapo awali haikuwakilisha haki. Na hivyo Nasema “hakuna wenye haki katika dunia hii.” Hata kati ya wale ambao wako katika mkondo wa urejesho, hakuna hata mmoja anayeweza kuitwa mwenye haki. Haijalishi matendo yako ni mazuri vipi, haijalishi jinsi unavyoonekana kulisifu jina la Mungu, si kuwapiga na kuwalaani wengine, wala kuwaibia na kuwapora wengine, bado huwezi kuitwa mwenye haki, kwa sababu haya ndiyo mtu wa kawaida ana uwezo wa kuwa nayo. Kilicho muhimu sasa ni kwamba wewe humfahamu Mungu. Inaweza tu kusemwa kwamba kwa sasa una kiasi kidogo cha ubinadamu wa kawaida, lakini hakuna vipengele vya haki viliyozungumziwa na Mungu, na hivyo hakuna chochote unachotenda ambacho kinaweza kuthibitisha kwamba unamfahamu Mungu.

Hapo awali, Mungu alipokuwa mbinguni, mwanadamu alimtendea Mungu kwa namna ya udanganyifu. Leo, Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu—hakuna anayejua imekuwa ni kwa miaka mingapi—lakini katika kufanya mambo mwanadamu bado anatenda kwa namna isiyo ya dhati na anajaribu kumdanganya Yeye. Je, mwanadamu hayuko nyuma sana katika kufikiri kwake? Ndivyo ilivyokuwa na Yuda: Kabla Yesu aje, Yuda angesema uwongo ili kuwadanganya ndugu zake, na hata baada ya Yesu kuja, bado hakubadilika; hakumjua Yesu hata kidogo, na mwishowe alimsaliti Yesu. Je, hii haikuwa kwa sababu hakumfahamu Mungu? Kama leo bado hamumfahamu Mungu, basi kuna uwezekano kwamba mnaweza kuwa Yuda mwingine, na kufuatilia hili, msiba wa kusulubiwa kwa Yesu katika Enzi ya Neema maelfu ya miaka iliyopita unaweza kurudiwa tena. Je, hamwamini hili? Ni ukweli! Hivi sasa, watu wengi wako katika hali kama hiyo—Naweza kuwa Ninayasema haya mapema sana kiasi—na watu wa aina hii wote ni wahusika wanaochukua nafasi ya Yuda. Sizungumzi upuuzi, bali kwa msingi wa ukweli—na huna budi ila kuridhika. Ingawa watu wengi wanajifanya kuwa wanyenyekevu, katika mioyo yao hakuna kingine ila dimbwi la maji yaliyokufa, handaki la maji yanayonuka. Hivi sasa kuna wengi sana wa aina hii katika kanisa na mnafikiri Sina habari yoyote kuhusu hili. Leo, Roho Wangu huniamulia na kunishuhudia. Unafikiri kwamba Sijui lolote? Je, unafikiri Sielewi lolote kuhusu fikira za ujanja katika mioyo yenu, mambo mnavyoweka katika mioyo yenu? Je, ni rahisi hivyo kumdanganya Mungu? Je, unafikiri kwamba unaweza kumtendea kwa njia yoyote unayotaka? Hapo zamani, Nilikuwa na wasiwasi msije mkazuiwa, hivyo Niliendelea kuwapa uhuru, lakini binadamu hawakuweza kutambua kwamba Nilikuwa mzuri kwao, na Nilipowapa kidogo walitaka mengi. Ulizieni kati yenu: Sijawahi kumshughulikia yeyote, na Sijawahi kumkemea yeyote kijuujuu—na bado Sina tashwishi juu ya nia na fikira za mwanadamu. Je, unafikiri Mungu Mwenyewe, ambaye Mungu anamshuhudia, ni mjinga? Hivyo, Ninasema wewe ni kipofu sana! Sitakufunua, lakini hebu tuone tu jinsi unavyoweza kuwa mpotovu. Hebu tuone iwapo ujanja wako mdogo unaweza kukuokoa, ama iwapo kujaribu kadri uwezavyo kumpenda Mungu kutakuokoa. Leo, Sitakushutumu; hebu tungoje mpaka wakati wa Mungu tuone Atakavyokuadhibu. Sina wakati wa kupoteza kufanya maongezi madogo madogo na wewe sasa, na Sina nia ya kuchelewesha kazi Yangu kuu kwa ajili yako tu. Buu kama wewe hastahili muda utakaomchukua Mungu kukushughulikia—kwa hivyo hebu tuone tu jinsi unavyoweza kuwa mpotovu. Watu kama hawa hawafuatilii maarifa yaa Mungu hata kidogo, wala hawampendi Yeye hata kidogo, na bado wanataka Mungu awaite wenye haki—huu si utani? Kwa sababu idadi ndogo ya watu ni waaminifu kwa kweli, Nitalenga tu katika kuzidi kumpa mwanadamu uhai. Nitakamilisha tu kile Ninachohitaji kukamilisha leo, lakini katika siku zijazo Nitaleta adhabu kwa kila mmoja kulingana na kile ambacho amefanya. Nimesema yote yanayopaswa kusemwa, kwa sababu hii hasa ndiyo kazi Ninayoifanya. Ninafanya kile tu Ninachopaswa kufanya, na si kile Nisichopaswa kufanya. Hata hivyo, Natumai kwamba mtatumia muda zaidi katika kutafakari: Kiwango gani hasa cha ufahamu wako kuhusu Mungu ni cha kweli? Je, wewe ni mtu ambaye amemsulubisha Mungu kwa mara nyingine? Maneno Yangu ya mwisho ni haya: Ole wao wamsulubishao Mungu.

Iliyotangulia: Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Inayofuata: Jinsi ya Kuingia Katika Hali ya Kawaida

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp