Sura ya 13

Katika hali yenu ya sasa nyinyi hushika dhana za nafsi zaidi kupindukia, na madakizo yenu ya dini ni mazito kiasi. Mmeshindwa kutenda katika roho, hamwezi kufahamu kazi ya Roho Mtakatifu, na mmekataa mwanga mpya. Huoni jua wakati wa mchana kwa sababu wewe ni kipofu. Huwaelewi watu, umeshindwa kuwaacha “wazazi” wako, umekosa utambuzi wa kiroho, huijui kazi ya Roho Mtakatifu, na huna wazo la jinsi ya kula na kunywa ya neno Langu. Ni tatizo kuwa hujui jinsi ya kula na kunywa peke yako. Kazi ya Roho Mtakatifu hupiga hatua siku baada ya siku kwa kasi ya kushangaza. Kuna mwanga mpya kila siku, na kuna mambo mapya na safi kila siku, lakini huelewi. Badala yake, unapenda kufanya utafiti, na wewe huangalia mambo kupitia lenzi ya mapendeleo yako ya kibinafsi bila kuyazingatia kwa makini na husikiliza kwa bumbuwazi. Huombi kwa bidii katika roho, wala hunitazami au kutafakari zaidi juu ya maneno Yangu. Hivyo, yote uliyo nayo ni elimu, sheria na mafundisho. Lazima ujue jinsi ya kula na kunywa kutoka kwa neno Langu na kuja mbele Yangu daima na neno Langu.

Watu siku hizi hawawezi kukubali kujiachilia wenyewe, wao siku zote hufikiri kwamba wao ndio sahihi. Wao wamekwama katika dunia yao wenyewe ndogo na hawawi watu sahihi. Wakiendelea kusisitiza kuwa na lengo lisilo sahihi basi hakika watahukumiwa, na kama ni mbaya basi wataondolewa. Lazima uweke juhudi zaidi katika kuwa na ushirika wa kudumu na Mimi na si kuwa na ushirika tu na yeyote umtakaye. Lazima uwe na ufahamu wa watu ambao huwa na ushirika nao na ushirika kuhusu masuala ya kiroho katika maisha, ni hapo tu unapoweza kuruzuku maisha kwa wengine na kufidia mapungufu yao. Hupaswi kuchukua sauti ya kuhubiri nao, ambao kimsingi ni msimamo mbaya kuwa nao. Katika ushirika ni lazima uwe na ufahamu wa mambo ya kiroho. Lazima uwe na hekima na kuwa na uwezo wa kuelewa ni nini kilicho katika mioyo ya watu wengine. Lazima uwe mtu mwafaka kama utawatumikia wengine na lazima ufanye ushirika na kile ulicho nacho.

Jambo la muhimu sasa ni kwako wewe kuwa na uwezo wa kufanya ushirika Nami, kuwasiliana kwa karibu Nami, kula na kunywa peke yako, na kuwa karibu na Mungu. Lazima uelewe haraka mambo ya kiroho na kuwa na uwezo wa kuona kwa njia ya mazingira na mambo yaliyopangwa katika eneo lako. Je, unaweza kuelewa kile Nilicho? Ni muhimu kwamba ule na kunywa kutegemea na kile unachokosa, na kuishi kwa kutegemea neno Langu! Tambua mikono Yangu, na wala usilalamike. Ukifanya hivyo na kujitenga, unaweza kupoteza nafasi ya kupokea neema ya Mungu. Anza kwa kunikaribia Mimi: Je, unakosa nini, unapaswa kunikaribia Mimi na kuuelewa moyo Wangu vipi? Ni vigumu kwa watu kuja karibu na Mimi kwa sababu hawawezi kuiachilia nafsi. Tabia yao daima haiwiani, kuwa moto na kisha baridi, na wao wanajivuna na kuridhika na wao wenyewe wanapopata ladha kidogo ya utamu. Baadhi ya watu bado hawajaamka, ni kiasi gani cha unayoyasema kina kile ulicho? Ni kiasi gani cha hayo ambacho ni kujitetea mwenyewe, au kuiga wengine ama tu kufuata kanuni? Sababu ya wewe kutofahamu au kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwa hujui jinsi ya kuwa karibu na Mimi. Kwa nje daima wewe hutafakari juu ya mambo, kutegemea dhana za nafsi na mawazo yako; wewe kwa siri hutafiti na kushiriki katika baadhi ya mipango midogo midogo, na huwezi hata kulileta hilo peupe. Hii inaonyesha kwamba kwa hakika huielewi kazi ya Roho Mtakatifu. Kama kwa hakika unaelewa kwamba jambo halitoki kwa Mungu, kwa nini usithubutu kusimama na kulikataa? Ni wangapi wangeweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Huonyeshi ujasiri wowote wa mtoto wa kiume.

Kila kitu ambacho kimepangwa sasa ni kwa lengo la kutoa mafunzo kwenu ili kwamba mkue katika maisha yenu, kuzifanya roho zenu ziwe na makali na zenye ncha, kuyafungua macho yenu ya kiroho na kuwafanya mtambue mambo yanayotoka kwa Mungu. Kitokacho kwa Mungu hukuwezesha kuhudumu kwa uwezo na mzigo na kuwa imara katika roho. Mambo ambayo hayatoki Kwangu yote ni matupu; hayakupi kitu, husababisha utupu katika roho yako na kukufanya upoteze imani yako, na kuweka umbali kati yako na Mimi, yakikufanya ufungiwe katika akili yako mwenyewe. Sasa unaweza kuvuka mipaka ya kila kitu katika ulimwengu wa kawaida unapoishi katika roho, lakini kuishi katika mawazo yako ni kuchukuliwa na Shetani na huu ni mwisho wa njia. Ni rahisi sana sasa: Nitegemee Mimi kwa moyo wako na roho yako mara moja itakuwa imara, utakuwa na njia ya kutenda na Mimi nitakuongoza katika kila hatua. Neno Langu litafichuliwa kwako wakati wote na katika maeneo yote. Bila kujali ni wapi au wakati upi, au mazingira yako ni mabaya namna gani, Mimi nitakuonyesha kwa uwazi na moyo Wangu kufichuliwa kwako ukinitegemea Mimi kwa moyo wako; kwa njia hii utaikimbilia barabara iliyo mbele bila kupoteza njia. Baadhi ya watu hujaribu kupapasa kwa nje, lakini kamwe hawafanyi hivyo kutoka ndani ya roho zao. Mara nyingi hawawezi kuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Wanapofanya ushirika na watu wengine, wao huchanganyikiwa zaidi, wakikosa njia ya kufuata na kutojua kitu cha kufanya. Watu hawa hawajui kinachowasumbua; wanaweza kuwa na mambo mengi na wawe wamejazwa sana ndani, lakini hilo lina maana yoyote? Je, kweli una njia ya kufuata? Je, umeangaziwa na kunurishwa? Je, una umaizi wowote mpya? Je, umefanya maendeleo au umerudi nyuma? Je, unaweza kujiendeleza na mwanga mpya? Huna utii; utii unaousema mara nyingi si kitu ila maongezi tu. Umeishi kwa kudhihirisha maisha ya utiifu?

Kikwazo cha mtu kujidai, kuridhika, majisifu, na kiburi ni kikubwa jinsi gani? Ni nani wa kulaumiwa usipoweza kuingia katika uhalisi? Lazima ujichunguze mwenyewe kwa makini ili kuona kama wewe ni mtu sahihi. Je, malengo yako hufanywa Nami katika mawazo? Je, maneno na matendo yako husimama mbele Yangu? Mimi huchunguza fikira na mawazo yako yote. Je, si unajihisi mwenye hatia? Unajitwika sura ya bandia ili wengine waone na wewe kwa upole unajifanya kujidai; hili hufanyika ili ujikinge mwenyewe. Wewe hufanya hili ili kuyaficha maovu yako, na hata kutafuta njia za kuusukuma huo uovu kwa mtu mwingine. Ni hila gani hukaa ndani ya moyo wako! Fikiria kila kitu ambacho umesema; haikuwa kwa faida yako kwamba ulikuwa na hofu kwamba roho yako mwenyewe ingepata madhara na hivyo ukamsitiri Shetani na kisha kuwaibia ndugu zako ulaji na unywaji wao kwa nguvu? Una nini la kusema juu yako mwenyewe? Je, unafikiri kwamba wakati mwingine utaweza kulipia kula na kunywa huko ambako Shetani amechukua wakati huu? Hivyo unaona wazi sasa, hiki ni kitu ambacho unaweza kufidia? Je, unaweza kuufidia wakati uliopotea? Lazima kwa bidii mchunguze wenyewe kuona ni kwa nini hapakuwa na kula na kunywa katika mikutano michache iliyopita na ni akina nani ambao walisababisha shida hii. Lazima mfanye ushirika mmoja kwa mmoja mpaka iwe wazi. Watu kama hawa wasipozuiwa bila huruma, akina ndugu hawataelewa, na basi itakuja kutokea tena tu. Macho yenu ya kiroho hayajafunguliwa na wengi wenu sana ni vipofu! Na wale ambao huona ni wa kutojali kuhusu hilo. Hawasimami na kuongea, nao, pia, ni vipofu. Wale ambao huona lakini hawaongei ni mabubu. Kuna wengi hapa ambao wana upungufu.

Baadhi ya watu hawaelewi ukweli ni nini, ni nini maisha, njia ni nini, na wao hawaielewi roho. Wao huangalia neno langu kama fomyula tu, na hili ni gumu mno kubadilika. Hawaelewi shukrani ya kweli na sifa ni nini. Baadhi ya watu hawawezi kufahamu mambo muhimu na ya msingi, badala yake, wao hufahamu tu ya upili. Inamaanisha nini kudakiza usimamizi wa Mungu? Inamaanisha nini kubomoa jengo la kanisa? Inamaanisha nini kudakiza kazi ya Roho Mtakatifu? Kikaragosi wa Shetani ni nini? Ukweli huu lazima ueleweke wazi na sio tu kusitiriwa kwa mashaka. Ni kwa nini hakukuwa na kula na kunywa wakati huu? Baadhi ya watu wanaona kuwa wao wanapaswa kumsifu Mungu kwa sauti kubwa leo, lakini ni kwa jinsi gani wamsifu Yeye? Je, wanapaswa kuimba nyimbo na kucheza ngoma ili kumsifu Yeye? Je, njia nyingine hazihesabiki kama sifa? Baadhi ya watu huja kwa mikutano na dhana kwamba sifa za shangwe ndiyo njia ya kumsifu Mungu. Watu wana dhana hizi, na hawatilii maanani kazi ya Roho Mtakatifu, matokeo yake yakiwa kuwa bado kuna madakizo. Hakukuwa na kula na kunywa katika mkutano huu; wote wamesema kwamba wangeweza kuudhukuru mzigo wa Mungu na kutetea ushuhuda wa kanisa. Ni nani ambaye kweli amefikiri kwa makini kuhusu mzigo wa Mungu? Jiulize: Je, wewe ni mtu ambaye ameonyesha nadhari kwa mzigo wa Mungu? Je, unaweza kutenda haki kwa ajili ya Mungu? Je, unaweza kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu? Je, unaweza bila kusita kuweka ukweli katika vitendo? Je, wewe ni jasiri vya kutosha kupambana dhidi ya matendo yote ya Shetani? Je, unaweza kuwa na uwezo wa kuweka hisia zako kando na kufichua Shetani kwa sababu ya ukweli Wangu? Je, unaweza kuyaruhusu mapenzi Yangu yatimizwe ndani yako? Je, umejitolea moyo wako wakati muhimu unapowadia? Je, wewe ni mtu ambaye hufanya mapenzi Yangu? Jiulize na kufikiri juu yake mara kwa mara. Zawadi za shetani zimo ndani yako na wewe ni wa kulaumiwa kwa hayo kwa kuwa huwaelewi watu na umeshindwa kuitambua sumu ya Shetani; unajiongoza mwenyewe kwa kifo. Shetani amekudanganya kabisa kiasi kwamba umekanganyika kabisa; umelewa kwa divai ya uasherati na unayumba mbele na nyuma bila uwezo wa kushikilia maoni dhabiti na bila njia ya kutenda. Huli na kunywa vizuri, wewe hupigana na kugombana ovyo ovyo, hujui mema na mabaya na humfuata yeyote aongozaye—je, una ukweli wowote? Baadhi ya watu hujitetea hata kushiriki katika udanganyifu, wao hufanya ushirika na wengine lakini hilo huwaongoza hadi mwisho wa njia. Je, ni kutoka Kwangu ambapo watu hawa hupata nia zao, malengo, motisha, na chanzo? Je, unafikiri kuwa unaweza kufidia ndugu hawa kwa kula na kunywa kwao kulikochukuliwa? Tafuta watu wachache ili kufanya nao na kuwauliza, na uwaache wajizungumzie wenyewe: Je, wao wamepewa kitu chochote? Au wamekunywa na kuyajaza matumbo na maji machafu na kujawa na takataka na sasa hawana njia ya kufuata? Je, si hilo litabomoa kanisa? Upendo uko wapi kati ya ndugu? Kwa siri, wewe unatafiti ni nani aliye sahihi na asiye sahihi, lakini kwa nini huubebi mzigo kwa ajili ya kanisa? Kwa kawaida wewe hufanya vizuri katika kupiga ukelele wa misemo, lakini mambo yanapotokea katika hali halisi wewe ni una mashaka kuyahusu. Baadhi ya watu huelewa lakini hunung’unika tu kimya kimya wakati wengine huongea yale wanayoyaelewa lakini hakuna mtu mwingine husema neno. Wao hawajui kinachotoka kwa Mungu na ni nini kazi ya Shetani. Ziko wapi hisia zenu za ndani kuhusu maisha? Kabisa hamuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu na hamuitambui kazi ya Roho Mtakatifu na ni vigumu kwenu kukubali mambo mapya. Nyinyi hukubali tu mambo ya kidini na ya kidunia, ambayo hupatana na dhana za watu. Kwa hivyo, nyinyi hupambana kitundu. Ni wangapi wanaweza kufahamu kazi ya Roho Mtakatifu? Ni wangapi ambao kwa hakika wamebeba mzigo kwa ajili ya kanisa? Je, unaufahamu? Kuimba nyimbo ni njia moja ya kumsifu Mungu, lakini huelewi kwa dhahiri ukweli wa kumsifu Mungu na wewe ni mgumu katika njia unayoitumia kumsifu Yeye. Si hilo ni wazo lako mwenyewe? Daima wewe hushika dhana zako mwenyewe bila kuachilia na huwezi kuzingatia kile Roho Mtakatifu atakachofanya leo, usiweze kuhisi yale ndugu zako wanahisi, na kushindwa kutafuta mapenzi ya Mungu kwa njia ya utulivu. Wewe hufanya mambo kwa upofu na kuimba nyimbo vyema, lakini matokeo yake ni machafuko kamili. Je, hiyo kweli ni kula na kunywa? Je, unaona ni nani hasa anayesababisha madakizo? Kimsingi wewe huishi katika roho, lakini badala yake hushikilia dhana mbalimbali—Hiyo kwa vyovyote vile, inawezaje kuwa kulibebea kanisa mzigo? Lazima muone kwamba kazi ya Roho Mtakatifu inaendelea hata kwa kasi zaidi sasa, kwa hivyo si nyinyi mnakuwa vipofu kama mnashikilia kikiki dhana zenu wenyewe na kupinga kazi ya Roho Mtakatifu? Si hilo ni kama nzi kuruka akigonga kuta na kuvuma pote? Mkiendelea kwa njia hii mtatupwa kando.

Wale ambao wamefanywa kuwa kamili kabla ya maafa ni watiifu kwa Mungu. Wao huishi wakimtegemea Kristo, humshuhudia Kristo, na humtukuza Yeye. Wao ni watoto wa kiume waliofanikiwa na askari wema wa Kristo. Ni muhimu sasa kwamba ujitulize mwenyewe na kuja karibu na Mungu na kufanya ushirika Naye. Kama huwezi kuja karibu na Mungu, una hatari ya kutekwa na Shetani. Kama unaweza kuja karibu na Mimi na kufanya ushirika na Mimi, ukweli wote utafichuliwa kwako, na wewe utakuwa na kiwango cha kufuata kwa maisha yako na vitendo. Kwa sababu wewe ni mmoja ambaye yu karibu na Mimi, neno Langu kamwe halitaondoka kando yako, na hutapotea kutoka kwa neno Langu katika maisha yako; Shetani hatakuwa na njia ya kukudanganya, na badala yake ataona aibu na kutoroka kwa kushindwa. Ukitafuta nje kile kinachokosa ndani yako, kunaweza kuwa na nyakati ambapo unapata baadhi yacho, lakini sehemu kubwa yacho itakuwa sheria na kinaweza kuwa kitu usichohitaji. Lazima ujiachilie mwenyewe na ule na kunywa kutoka kwa neno Langu zaidi na ujue jinsi ya kulitafakari neno Langu. Kama huelewi kitu, njoo karibu Nami na kufanya ushirika na Mimi mara nyingi; kwa njia hii, kile utakachokielewa kitakuwa halisi na cha kweli. Lazima uanze kwa kuwa karibu Nami. Hili ni muhimu! Vinginevyo, hutajua jinsi ya kula na kunywa. Huwezi kula na kunywa wewe mwenyewe—kimo chako kweli ni kidogo mno.

Iliyotangulia: Sura ya 12

Inayofuata: Sura ya 14

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp