Sura ya 14

Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu. Unapaswa kujitayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru. Bila kujali jinsi ulivyo mpumbavu na mjinga, Mimi sioni vitu kama hivyo. Naangalia kuona jinsi unavyofanya kazi kwa bidii katika hali ya kujenga. Kama bado unashikilia dhana ya nafsi, kuzungusha duara katika dunia yako ndogo, basi Nafikiri uko katika hatari.… kuchukuliwa kuenda mbinguni ni nini? Inamaanisha nini kutelekezwa? Unapaswa kuishi vipi mbele ya Mungu leo? Unapaswa kushirikiana kikamilifu Nami vipi? Zitupilie mbali dhana zako mwenyewe, jichanganue mwenyewe, ivue barakoa yako, ona dhahiri ubainifu wa tabia yako halisi, jichukie mwenyewe, kuwa na moyo unaotafuta kwa njaa na kiu ya haki, amini kwamba wewe mwenyewe kwa kweli si kitu, kuwa tayari kujiachilia mwenyewe, kuwa na uwezo wa kuacha njia zako zote za kufanya mambo, jitulize mwenyewe mbele Yangu, yafanye maombi zaidi, jiegemeze Kwangu kwa unyofu, nitegemee Mimi, na usiache kuwa karibu na Mimi na kuwa na ushirika na Mimi—hili ni muhimu. Watu mara nyingi hujipata wamenaswa ndani ya nafsi zao wenyewe na hawako mbele ya Mungu.

Kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu kwa kweli ni ngumu kwa watu kuwaza na yote huingia katika uhalisi; kwa kweli haitakufaa kuwa mzembe. Kama moyo wako na mawazo si sahihi, basi hutakuwa na njia. Kutoka mwanzo hadi mwisho ni lazima uwe macho wakati wote na kuhakikisha kuwa umejikinga dhidi ya uzembe. Heri wale ambao daima huwa macho na kusubiri na ambao wako kimya mbele Yangu! Heri wale ambao daima hunitegemea Mimi kwa mioyo yao, ambao huhakikisha wameisikiliza kwa karibu sauti Yangu, ambao huzingatia matendo Yangu na ambao huweka maneno Yangu katika matendo! Wakati kweli hauwezi kuvumilia taahira; mabaa ya kila namna yataenea, yakifungua midomo yao mikali, yenye damu kuwala nyinyi nyote kama mafuriko. Wanangu! Wakati umefika! Hakuna nafasi zaidi ya kuwaza. Njia pekee itakayowaleta chini ya ulinzi Wangu ni kurudi Kwangu. Ni lazima muwe na nguvu ya tabia ya mwana wa kiume, msiwe wadhaifu au kuvunjika moyo; lazima mfuate unyounyo hatua Zangu, msikatae mwanga mpya na, kwa kuwaambia jinsi ya kula na kunywa, mnapaswa mtii na kula na kunywa vizuri. Je, bado kuna wakati sasa wa kupigana au kushindana na kila mmoja kiholela? Je, mnaweza kufanya vita kama hamli na kushiba na hamjatayarishwa kikamilifu na ukweli? Kama mnataka kuishinda dini, ni lazima mjitayarishe kikamilifu na ukweli. Kuleni na kunywa maneno Yangu zaidi na kutafakari juu ya maneno Yangu zaidi. Lazima mle na kunywa maneno Yangu kwa kujitegemea na kuanza kwa kujongea karibu na Mungu. Acha hili liwe ni onyo kwenu! Lazima mtie maanani! Wale ambao ni werevu lazima kwa haraka wauelewe ukweli! Achilia mambo yote ambayo huna nia ya kuyaacha. Nakwambia kwa mara nyingine tena kwamba mambo haya kwa kweli ni hatari kwa maisha yako na yasiyokuwa na manufaa! Natumaini unaweza kunitegemea Mimi katika matendo yako, vinginevyo njia tu iliyo mbele itakuwa njia ya kifo, na ni wapi basi utakakokwenda kutafuta njia ya maisha? Uondoe moyo wako ambao unapenda kujishughulisha na mambo ya nje! Uondoe moyo wako ambao huwakaidi watu wengine! Kama maisha yako hayawezi kukomaa na umetelekezwa, si wewe basi utakuwa ndiye ambaye amejikwaa mwenyewe? Kazi ya Roho Mtakatifu sasa si kama wewe unavyofikiria. Kama huwezi kuziachilia dhana zako basi utapata hasara kubwa. Kama kazi ingekuwa ni kwa kuambatana na dhana za mtu, je, asili yako ya zamani na dhana zingeweza kufichuka? Je, ungeweza kuwa na uwezo wa kujijua mwenyewe? Labda bado unadhani kuwa huna dhana, lakini wakati huu bado pande zako zote mbalimbali mbaya zitafichuka. Kwa makini jiulize:

Je, wewe ni mtu ambaye hunitii Mimi?

Je, una hiari na tayari kuiachilia nafsi yako na unifuate Mimi?

Je, wewe ni mtu ambaye huutafuta uso Wangu kwa moyo safi?

Je, unajua jinsi ya kujongea karibu na Mimi na kufanya ushirika nami?

Je, unaweza kujituliza mbele Yangu na kutafuta mapenzi Yangu?

Je, wewe huweka katika vitendo maneno ambayo Mimi hukufichulia?

Je, unaweza kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu?

Je, una uwezo wa kuona undani wa mipango ya hila ya Shetani? Je, wewe unathubutu kuifichua?

Ni jinsi gani unafanya busara kuhusu mzigo wa Mungu?

Je, wewe ni mtu ambaye hufanya busara kwa mzigo wa Mungu?

Je, wewe huielewaje kazi ya Roho Mtakatifu?

Je, ni jinsi gani wewe huhudumu kwa uratibu katika familia ya Mungu?

Je, wewe huwa na ushuhuda wa nguvu kwa ajili Yangu?

Je, wewe kupiganaje vita vizuri kwa ajili ya ukweli?

Lazima uchukue muda wa kutafakari ukweli huu kabisa. Ukweli ni wa kutosha kuthibitisha kuwa siku i karibu sana. Ni lazima ufanywe mkamilifu kabla ya maafa—hili ni suala la umuhimu mkubwa ambalo lazima litatuliwe haraka! Nataka kuwafanya wakamilifu, lakini Naona kwamba nyinyi kweli kwa kiasi fulani hamjadhibitiwa. Mna ushupavu lakini hamuuweki kwa matumizi bora na bado hamjaelewa mambo yaliyo muhimu zaidi, badala yake yote mnayoelewa ni mambo madogo. Kuna faida gani katika kujadili juu ya mambo haya? Je, si huku ni kupoteza wakati? Mimi huwaonyesha wema kwa njia hii lakini mnashindwa kuonyesha shukrani yoyote na nyinyi hupigana tu miongoni mwenu, hivyo si juhudi Zangu zote zimekuwa bure? Kama mtaendelea kwa njia hii, Sitachukua wakati kuwashawishi muendelee! Nawaambia, isipokuwa mzinduke kwa ukweli, kazi ya Roho Mtakatifu itaondolewa kutoka kwenu! Hamtapewa cha kula zaidi tena, na mnaweza kuamini kama mnavyoona inafaa. Maneno Yangu yamesemwa kwa kirefu; msikilize au la, ni juu yenu. Wakati utakapofika mnapokuwa mmechanganyikiwa na hakuna njia ya kwenda mbele na hamuwezi kuona mwanga wa kweli, mtanilaumu Mimi? Ujinga ulioje! Matokeo yanapaswa kuwa yapi iwapo utajigandamia kikiki na kukataa kujiachilia? Si kazi yenu itakuwa ilikuwa zoezi la bure? Ni sikitiko lililoje kutupwa kando wakati janga linapokumba!

Sasa ni awamu muhimu ya ujenzi wa kanisa. Kama huwezi kushirikiana na Mimi kwa kupanga na kujitoa mwenyewe Kwangu kwa moyo wote, kama huwezi kuacha kila kitu, basi utapata hasara; bado unaweza kuwa na nia zingine? Mimi Niliwaonyesha huruma kwa njia hii, Nikiwasubiri mtubu na kuanza upya. Lakini wakati kweli hauruhusu hili sasa na ni lazima Nizingatie jambo lote zima. Kwa ajili ya madhumuni ya mpango wa usimamizi wa Mungu, kila kitu kinasonga mbele na hatua Zangu zapiga hatua siku kwa siku, saa kwa saa, wakati kwa wakati, na wale ambao hawawezi kuendelea sawa watatelekezwa. Kila siku kuna mwanga mpya, kila siku matendo mapya hufanyika, kuna mambo mapya kila siku na wale ambao hawawezi kuona mwanga ni vipofu! Wale ambao hawawezi kufuata wataondolewa….

Iliyotangulia: Sura ya 13

Inayofuata: Sura ya 15

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp