Sura ya 36

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme akaliaye kiti cha enzi, Atawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yasiyohesabika na watu wasiohesabika, na utukufu wa Mungu unang’aa ulimwenguni kote. Viumbe vyote hai ulimwenguni na hadi miisho ya dunia vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari, na viumbe vyote viishivyo vimefungua pazia zao katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli, na wamesisimka kana kwamba wameamka kutoka ndotoni, kana kwamba wao ni chipuko zinazochipuka kutoka mchangani!

Ah! Mungu mmoja wa kweli anaonekana mbele ya watu wa dunia. Ni nani anayethubutu kumwelekea Yeye kwa upinzani? Wote wanatetemeka kwa hofu. Wote wameshawishika kabisa, na wote wanaomba msamaha kwa kurudia. Watu wasiohesabika wanapiga magoti mbele Yake, na vinywa visivyohesabika vinamwabudu! Mabara na bahari, milima, mito, na vitu vyote vinamsifu Yeye bila kikomo! Upepo mwanana wenye joto, ukiandamana na pumzi ya majira ya kuchipua, unaleta mwangaza, mvua isiyokoma ya majira ya kuchipua. Vijito vinavyotiririka na umati ni sawa, vyote vimejawa na huzuni na furaha, vikimwaga machozi ya kuhisi deni na kujilaumu. Mito, maziwa, mawimbi na dhoruba vyote vinaimba, vikilisifu jina takatifu la Mungu wa kweli! Sauti ya sifa inasikika kwa uwazi sana! Vitu vya zamani vilivyopotoshwa na Shetani wakati fulani—kila kimoja kitafanywa upya na kubadilishwa na kitaingia katika ulimwengu mpya kabisa …

Hii ni tarumbeta takatifu, na imeanza kulia! Isikilize. Sauti hiyo, tamu sana, ni tamko la kiti cha enzi. Inatangaza kwa kila taifa na watu kwamba wakati umefika, matokeo ya siku za mwisho yamewadia, mpango Wangu wa usimamizi umekamilika, ufalme Wangu umeonekana waziwazi duniani, na falme za dunia zimekuwa ufalme Wangu, Mimi ambaye ni Mungu. Tarumbeta Zangu saba zinalia kutoka katika kiti cha enzi, na mambo ya ajabu sana yatatukia! Watu katika miisho ya dunia watakurupuka pamoja kutoka kila upande kwa nguvu ya lundo na uwezo wa radi, baadhi yao baharini, baadhi yao wakiendesha ndege, baadhi yao watakuja kwa magari ya kila muundo na ukubwa, baadhi yao watakuja mgongoni mwa farasi. Angalia kwa karibu. Sikiliza kwa makini. Hawa wapandao farasi wa kila rangi, pepo kuchochewa, wenye majivuno na waadhimu, kama kuchukua uwanja wa vita, wao hawajali kifo. Katikati ya milio ya farasi na makelele ya watu ya kupiga mayowe wakimwita Mungu wa kweli, wanaume, wanawake na watoto wengi watakanyagwa na kwato zao mara moja. Baadhi yao watakufa, baadhi yao watakuwa wakivuta pumzi yao ya mwisho, baadhi yao watapondwa, pasipo na mtu wa kuwatunza, wakipiga kelele kwa kupagawa, wakilia kwa uchungu. Wana wa uasi! Je, hizi si hatima zenu za mwisho?

Ninawatazama watu Wangu kwa furaha, wanaoweza kuisikia sauti Yangu na kukusanyika kutoka kila taifa na nchi. Halaiki, wakimweka Mungu wa kweli vinywani mwao daima, wamsifu na kurukaruka bila kukoma! Wanatoa ushahidi kwa ulimwengu, na sauti ya ushahidi wao kwa Mungu wa kweli ni kama ngurumo ya maji mengi. Halaiki itasongamana katika ufalme Wangu.

Matarumbeta Yangu saba yatapaza sauti, kuamsha walio lala! Shughulika kwa haraka, muda hujakwisha. Angalia maisha yako! Fungua macho yako na uone ni wakati upi sasa. Unatafuta nini? Kuna nini cha kufikiria? Na kuna nini cha kushikamana nacho? Je, inaweza kuwa ninyi hamjazingatia tofauti ya thamani kati ya kupata maisha Yangu na vitu vyote ambavyo nyinyi mnavipenda na kung’ang’ania? Acha kuwa makaidi na kucheza kila mahali. Usikose nafasi hii. Wakati huu hautakuja tena! Simama mara moja, tenda kufanyisha roho yako mazoezi, kutumia zana mbalimbali kukuwezesha na kuzuia kila njama na hila za Shetani, na umshinde Shetani, ili kwamba uzeofu wako wa maisha uweze kuwa wa kina zaidi na uweze kuishi kwa kudhihirisha tabia Yangu, ili maisha yako yaweze kukomaa na yawe yenye tajriba na ili uweze daima kufuata nyayo Zangu. Ukiwa bila hofu, ukiwa usiye udhaifu, daima ukisonga mbele, hatua kwa hatua, moja kwa moja hadi mwisho wa njia!

Baragumu saba zitakapolia tena, itakuwa mwito wa hukumu, hukumu ya wana wa uasi, hukumu ya mataifa yote na watu wote, na kila taifa litajisalimisha mbele za Mungu. Uso wa utukufu wa Mungu hakika utaonyeshwa mbele ya mataifa yote na watu wote. Kila mtu atakuwa ameridhishwa kabisa, kupiga kelele kwa Mungu wa kweli bila kikomo. Mwenyezi Mungu Atakuwa Mtukufu zaidi, na wanangu watashiriki katika utukufu, kushiriki ufalme nami, kuhukumu mataifa yote na watu wote, kuadhibu maovu, kuokoa na kuwa na huruma juu ya watu ambao ni Wangu, kuleta uthabiti na utulivu kwa ufalme. Kupitia sauti ya matarumbeta saba, kundi kubwa la watu litaokolewa, kurudi mbele Yangu kupiga magoti na kuabudu, kwa sifa daima!

Wakati matarumbeta saba yatatoa sauti mara nyingine tena, hilo litakuwa tukio la hitimisho la mwisho wa enzi, mlipuko wa sauti wa tarumbeta ya ushindi dhidi ya ibilisi Shetani, saluti katika mwanzo wa maisha ya wazi wa ufalme duniani! Sauti hii ya kifahari sana, sauti hii inayonguruma pande zote za kiti cha enzi, mlipuko wa sauti ya tarumbeta inayotikisa mbingu na dunia, ni ishara ya mpango Wangu wa usimamizi, na hukumu ya Shetani, kuadhibu duniani hii ya zamani kwa kifo kabisa, jahanamu! Huu mlipuko wa sauti ya tarumbeta unaashiria kwamba lango la neema ni linafungika, kwamba uhai wa ufalme utaanza duniani, ambayo ni kamilifu kabisa. Mungu Huokoa wale wanaompenda. Mara tu watakaporudi kwa ufalme Wake, watu duniani watakabili njaa, ndwele ya kufisha, na mabakuli saba ya Mungu, tauni saba zitaanza kutumika kwa mfululizo. Mbingu na dunia zitapita, lakini neno Langu halitapita!

Iliyotangulia: Sura ya 35

Inayofuata: Sura ya 37

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp