Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna anayemchukulia kama mwanadamu wa kawaida mwenye kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao humtendea kikawaida wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa “Kristo wa kweli.” Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.

Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia yako imebadilishwa kabisa, kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo zaidi. Pia kwamba, kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima utakuwa mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao huenda hujui: Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa “kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani” na “kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake.” Je, unathubutu kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unathubutu kusema kwamba wewe si muasi? Wengine watasema: Kila wakati ambao Mungu ananiweka katika mazingira mapya, mimi daima hutii na silalamiki na aidha siweki fikra zozote juu ya Mungu. Wengine watasema: Kazi zozote nilizopewa na Mungu mimi hufanya kadri ya uwezo wangu na kamwe mimi si mvivu. Kama ndivyo hali, Nawauliza hivi: Je, mnaweza kulingana na Kristo wakati mnaishi pamoja naye? Na ni kwa muda gani nyinyi mnaweza kulingana na Yeye? Siku moja? Siku mbili? Saa moja? Saa mbili? Imani yenu inaweza kuwa ya kustahili sifa, lakini hamna uthabiti wa kutosha. Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, kujidai kwako na kujigamba kwako kutawekwa wazi kwa maneno na matendo yako kidogo kidogo, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia, na akili yako isiyotii na kutoridhika kwako kutafichuka kwa kawaida. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, hadi wakati wewe utazozana sana na Kristo kama maji na moto, na basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Wakati huo, fikra zako haziwezi kufichika tena, malalamiko yako, pia, yataonekana kwa ghafla, na ubinadamu wako duni utakuwa wazi kabisa. Hata hivyo, hata wakati huo, utaendelea kukana uasi wako mwenyewe, ukiamini kwamba badala yake kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubaliwa na mwanadamu, ni mwingi wa madai kwa binadamu, na ungetii kikamilifu kwake kama Yeye angekuwa tu Kristo mwenye huruma zaidi. Mnaamini kwamba daima kuna sababu ya haki ya uasi wenu, na kwamba nyinyi mnamwasi tu baada ya Kristo amewafikisha hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufikiri kwamba mmekosa kumchukulia Kristo kama Mungu na katika nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na matakwa yako, na punde ambapo kuna jambo lolote ambamo Hafanyi hivyo, basi unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini hata hivyo? Na ni jinsi gani mnatafuta?

Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Ushirika wako na ndugu (au dada) huenda usionyeshe mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo? Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, ila kikundi cha washirika ambao wanaopigana dhidi ya Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye amefanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hajapokea upendo wa Mungu au fidia na utii wake. Je, hili si ni jambo la kusikitisha moyo?

Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ndiye mtu mwovu zaidi na mwenye nia mbaya zaidi duniani. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zaidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa ujanja? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja wenu anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na wote wanaona vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo, hata hivyo siku zote mnatangaza utiifu wenu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za ajabu na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kupatana na Kristo, wakati huo Mungu Atakuonekania kwa kawaida. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake. vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati; na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.

Baadhi ya watu wanaweza kuamini kwamba, kama kushirikiana na Mungu ni hatari sana, basi huenda likawa jambo la busara zaidi kukaa mbali na Mungu. Ni nini watu kama hawa wanaweza kupokea? Je, wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu? Hakika, kushirikiana na Mungu ni kugumu sana, lakini hiyo hasa ni kwa sababu mwanadamu amepotoka na si kwa sababu Mungu hawezi kushiriki naye. Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Kweli mnajua vyema kwamba hamstahili hata kidogo. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?

Iliyotangulia: Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Inayofuata: Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp