164 Kupitia Shida, Upendo Wangu kwa Mungu Unaimarishwa

1 Nilitupwa katika gereza la CCP ya kishetani, nikikabiliwa na sura kali na za kishetani za polisi. Bila kujua kama ningeweza kuvumilia mateso yao ya ukatili, nilihisi nikiwa mwoga na dhaifu. Sikujua kama kamwe ningepata tena nafasi ya kuishi maisha ya kanisa na kutekeleza wajibu wangu. Sikujua kama kamwe ningeweza tena kufanya kazi pamoja na ndugu na kumtumikia na kumshuhudia Mungu. Moyo wangu ulimwita Mungu kwa bidii, nikimwomba Mungu aniokoe kutoka katika mtego wa Shetani. Licha ya ukatili mwovu wa Shetani, majaliwa yangu yalikuwa mikononi mwa Mungu. Nilipoelewa mapenzi ya Mungu, sikuhisi woga au hofu tena, nami nilikuwa na imani ya kuyakabili mateso yao ya ukatili. Kama ningeishi au kufa, ningetii mipangilio ya Mungu, na ningetoa ushuhuda mkuu kwa Mungu kwa hatari ya kupoteza maisha yangu.

2 CCP ya kishetani ni kali na ya kuchukiza, ilitumia mbinu kali na hafifu, ikijaribu kunilazimisha nimsaliti Mungu. Umeme ulipopita katika mwili mwangu mzima, nilihisi kuwa ningekosa hewa karibuni. Sindano zilipodungwa katika vidole vyangu, maumivu ya kuchoma yalifanya kifo kionekane kuwa afadhali kuliko maisha. Katika uchungu wangu, maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu na ujasiri wa kuyakabili hayo yote. Nilifikiria jinsi ambavyo sikuwa nimempenda Mungu kwa dhati hapo awali, na niliachwa na majuto mengi sana. Nilitamani tu kuutoa moyo wangu kwa Mungu wakati huo, na kama Mungu angenikubali basi moyo wangu ungehisi wenye kufarijika na huru. Ee Mungu! Natamani wakati usimame. Acha nikupende zaidi. Ningekuwa na kesho, kwa kweli ningefanya kila niwezalo niufuatilie ukweli na kukupenda Wewe kwa kina zaidi.

3 Pepo waliniumiza nusura nipoteze maisha yangu, Mungu alinilinda kwa siri kutokana na madhara makubwa. Shida ziliusababisha moyo wangu umkaribie Mungu. Nikiwa na Mungu kando yangu, uchungu uligeuka na kuwa utamu. Katika dhiki kuu, nilikumbana ana kwa ana na Mungu na nikatakaswa na kuokolewa na Mungu. Nikipitia mateso ya kikatili ya CCP, niliiona waziwazi sura yake ya uovu. Nilikuja kutofautisha kati ya haki na uovu, na nikaona hata zaidi kwamba Mungu pekee ndiye upendo. Nalichukia joka kubwa jekundu hata zaidi na ni afadhali nife kuliko kutii. Namfuata Mungu kwa dhamira ya ukakamavu. Ee Mungu! Njia ya kwenda mbinguni ni ngumu na isiyo imara, iliyojaa majaribu na hatari. Maneno Yako yakiniongoza, natamani kuwa niegemee karibu na Wewe kila wakati na upendo wangu Kwako usibadilike kamwe.

Iliyotangulia: 163 Watakatifu Katika Enzi Zote Wanazaliwa Upya

Inayofuata: 165 Amua Kuwa Mtu Mwaminifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp