Wewe Ni Mwaminifu kwa Nani Hasa?

Sasa hivi, kila siku mnayoishi ni muhimu sana, na ina umuhimu mkubwa kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo lazima mthamini kila kitu mlicho nacho leo, na mthamini kila dakika inayopita. Lazima mtwae kila fursa ili muweze kupata faida kubwa zaidi, na hivyo kuepuka kuishi maisha haya bure. Mnaweza kuhisi mmechanganyikiwa kuhusu kwa nini Ninanena maneno kama haya. Kusema kweli, Sipendezwi na tabia ya yeyote kati yenu, kwa maana matumaini Niliyokuwa nayo kwenu hayakuwa jinsi mlivyo leo. Hivyo, Ninaweza kusema hivi: Kila mmoja wenu yuko ukingoni mwa hatari, na vilio vyenu vya zamani vya kuomba msaada na matamanio yenu ya zamani ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho wake. Hili ni onyesho lenu la mwisho la kunilipa Mimi, na ni jambo ambalo Sikuwahi kutarajia. Sitaki kuzungumza kinyume na ukweli wa mambo, kwa maana mmenikatisha tamaa sana. Pengine hamtaki kukubali hili bila kupinga, hamtaki kukabiliana na uhalisi—lakini lazima Niwaulize hili kwa uzito: Katika miaka hii yote, mioyo yenu imejazwa na nini hasa? Ni miaminifu kwa nani hasa? Msiseme kwamba maswali haya yameibuka ghafla, na msiniulize kwa nini Nimeuliza mambo kama haya. Jueni hili: Ni kwa sababu Ninawajua vizuri sana, Ninawajali sana, na Nimewekeza moyo Wangu sana katika mwenendo na matendo yenu kiasi kwamba Nimewawajibisha bila kikomo na kuvumilia ugumu mchungu. Hata hivyo mnanilipa Mimi kwa kutojali tu na kukubali hali ilivyo bila kujiweza. Mmekuwa ajizi sana Kwangu; je, inawezekana kwamba Sijui chochote kuhusu hilo? Ikiwa hivi ndivyo mnavyoamini, inathibitisha zaidi ukweli kwamba hamnitendei Mimi kwa wema kwa kweli. Na hivyo Ninasema kwamba mnajidanganya. Ninyi nyote ni werevu sana kiasi cha kutojua hata mnachofanya—kwa hivyo mtatumia nini kunipa Mimi hesabu?

Swali Ninalojali kabisa kuhusu ni mioyo yenu ni miaminifu kwa nani hasa. Natumai, pia, kwamba kila mmoja wenu atajaribu kupanga mawazo yake, na kujiuliza yeye ni mwaminifu kwa nani hasa na anaishi kwa ajili ya nani hasa. Pengine hamjawahi kuzingatia kwa makini maswali haya, kwa hivyo vipi Nikiwafunulia majibu?

Mtu yeyote aliye na kumbukumbu atakubali ukweli huu: Mwanadamu huishi kwa ajili yake mwenyewe na ni mwaminifu kwake mwenyewe. Siamini majibu yenu kuwa sahihi kabisa, kwa maana kila mmoja wenu anaishi katika maisha yake na kupambana katikati ya mateso yake binafsi. Kwa hivyo, ninyi ni waaminifu kwa watu mnaowapenda na vitu mnavyovipenda; ninyi si waaminifu kwenu wenyewe kikamilifu. Kwa sababu kila mmoja wenu anashawishiwa na watu, matukio, na vitu vinavyomzunguka, ninyi si waaminifu kwenu wenyewe kwa kweli. Sisemi maneno haya ili kuunga mkono kuwa waaminifu kwenu wenyewe, bali ili kufichua uaminifu wenu kwa kitu chochote kile, kwa maana katika kipindi cha miaka mingi sana, Sijawahi kupokea uaminifu kutoka kwa yeyote kati yenu. Mmenifuata miaka hii yote, lakini hamjawahi kunipa hata chembe ya uaminifu. Badala yake, mmezunguka watu na vitu mnavyovipenda—sana kiasi kwamba wakati wote, na popote mnapoenda, mnaviweka karibu na mioyo yenu na hamjawahi kuvitelekeza. Kila mnapokuwa na hamu au shauku kuhusu kitu chochote kile mnachokipenda, mnafanya hivyo wakati huohuo mnaponifuata, au hata wakati huohuo mnaposikiliza maneno Yangu. Kwa hivyo, Ninasema mnatumia uaminifu Ninaouliza kutoka kwenu badala yake kuwa waaminifu kwa “vipenzi” vyenu na kuvithamini. Ingawa mnaweza kujitolea kitu kimoja au viwili kwa ajili Yangu, haliwakilishi kila kitu chenu, na halionyeshi kwamba ni Mimi ndimi Kwangu ninyi ni waaminifu kwa kweli. Mnajihusisha katika shughuli ambazo mna shauku nazo: Baadhi yenu ni waaminifu kwa wana na binti zenu, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wakubwa wenu, hadhi, au kwa wanawake. Hamhisi kamwe kuchoka au kuudhika kuelekea vitu ambavyo ninyi ni waaminifu kwavyo; badala yake, mnazidi kuwa na hamu zaidi ya kumiliki vitu hivi kwa wingi zaidi, na kuvimiliki kwa njia bora zaidi, na hamkati tamaa kamwe. Mimi na maneno Yangu kila mara tunasukumwa nyuma ya vitu ambavyo mna shauku navyo, na hamna budi ila kutuweka mwisho. Kuna hata wale ambao huacha nafasi hii ya mwisho kwa ajili ya vitu ambavyo wao ni waaminifu kwavyo lakini bado hawajavigundua. Hakujawahi kuwa na hata chembe Yangu mioyoni mwao. Mnaweza kufikiri kwamba Ninadai mengi mno kutoka kwenu au Ninawashutumu ninyi isivyo haki—lakini, je, mmewahi kufikiria ukweli kwamba wakati mnapitisha muda kwa furaha na familia yenu, hamjawahi kuwa waaminifu Kwangu hata mara moja? Wakati huu, je, hilo haliwapi ninyi maumivu? Wakati mioyo yenu imejawa na furaha kwa kulipwa kwa ajili ya kazi zenu, je, hamhisi kuvunjika moyo kwa kutojizatiti na ukweli wa kutosha? Ni lini mmelia kwa kutopokea kibali Changu? Mnajiumiza vichwa na kujitaabisha sana kwa ajili ya wana na binti zenu, lakini bado hamridhiki; bado mnaamini kwamba hamjakuwa na bidii kwa niaba yao, kwamba hamjafanya kila mwezalo kwa ajili yao. Hata hivyo, Kwangu Mimi, kila mara mmekuwa wa kijuujuu na wazembe; Mimi niko tu katika kumbukumbu zenu, lakini Sidumu mioyoni mwenu. Hamjawahi kujaribu kuelewa nia Zangu za uangalifu, au kuzijali. Mnajihusisha tu katika tafakari fupi na kuamini kwamba hili litatosha. “Uaminifu” kama huo si kile ambacho Nimekitamani kwa muda mrefu, bali kile ambacho Nimekichukia kwa muda mrefu. Hata hivyo, haijalishi Ninasema nini, mnaendelea kukubali jambo moja au mawili tu; hamwezi kukubali hili kikamilifu, kwa maana ninyi nyote “mnajiamini” sana, na kila mara mnachagua kile cha kukubali kutoka katika maneno ambayo Nimenena. Ikiwa bado mko hivi leo, Nina mbinu fulani za kushughulikia kujiamini kwenu—na, zaidi ya hayo, Nitawafanya mkubali kwamba maneno Yangu yote ni ya kweli, na kwamba hakuna hata moja linalopotosha ukweli wa mambo.

Kama Ningeweka pesa kiasi mbele yenu sasa hivi na kuwapa uhuru wa kuchagua—na Nisingewashutumu kwa uchaguzi wenu—basi wengi wenu mngechagua pesa na kuutelekeza ukweli. Walio bora zaidi miongoni mwenu wangeacha pesa na kuuchagua ukweli shingo upande, huku wale walio katikati wangeshika pesa katika mkono mmoja na ukweli katika mkono mwingine. Je, sura yenu halisi haingekuwa dhahiri hivyo? Mnapochagua kati ya ukweli na kitu chochote ambacho ninyi ni waaminifu kwacho, ninyi nyote mngechagua kwa namna hii, na mtazamo wenu ungebaki vilevile. Je, si hivyo ndivyo ilivyo? Wengi wenu mmeyumbayumba kati ya mema na mabaya, sivyo? Katika mapambano yote kati ya chanya na hasi, mema na mabaya—kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, upatano na mfarakano, utajiri na umaskini, hadhi na ukawaida, kuungwa mkono na kukataliwa, na kadhalika—hakika hamkosi kujua chaguzi ambazo mmefanya! Kati ya familia yenye upatano na iliyovunjika, mlichagua ya kwanza, na mlifanya hivyo bila kusita hata kidogo; kati ya utajiri na wajibu, mlichagua lililotangulia tena, hata mkikosa utashi wa kurudi ufuoni;[a] kati ya anasa na umaskini, mlichagua ya kwanza; mlipochagua kati ya watoto, wake, na waume zenu au Mimi, mlichagua wa kwanza; na kati ya mawazo na ukweli, bado mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, Nimepoteza imani nanyi kabisa, Nimeshangazwa kabisa. Mioyo yenu bila kutarajia haina uwezo kabisa wa kulainishwa. Damu ya moyo ambayo Nimeitumia kwa miaka mingi, la kushangaza, haijaniletea Mimi chochote zaidi ya ninyi kunitelekeza na hali yenu ya kutojiweza, lakini matumaini Yangu kwenu yanakua kila siku inayopita, kwa maana siku Yangu imewekwa wazi kabisa mbele ya kila mtu. Hata hivyo sasa bado mnafuatilia vitu vya giza na viovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu kwavyo. Basi, matokeo yenu yatakuwa yapi? Je, mmewahi kuzingatia hili kwa makini? Mngeambiwa mchague tena, basi msimamo wenu ungekuwa upi? Je, bado ungekuwa ule wa kwanza? Je, bado mngenilipa Mimi kwa masikitiko na huzuni yenye maumivu? Je, mioyo yenu bado ingekuwa na kiasi kidogo tu cha uchangamfu? Je, bado mngekosa kujua la kufanya ili kuufariji moyo Wangu? Wakati huu, mnachagua nini? Je, mtatii maneno Yangu au mtakuwa kinyume nayo? Siku Yangu imewekwa wazi mbele ya macho yenu, na kile mnachokikabili ni maisha mapya na mahali papya pa kuanzia. Hata hivyo, lazima Niwaambie kwamba mahali hapa pa kuanzia si mwanzo wa kazi mpya, kama ilivyokuwa zamani, bali ni hitimisho la kazi ya zamani. Yaani, hili ni tendo la mwisho. Nadhani ninyi nyote mnaweza kuelewa kile ambacho si cha kawaida kuhusu mahali hapa pa kuanzia. Hata hivyo, siku moja hivi karibuni, mtaelewa maana ya kweli ya mahali hapa pa kuanzia, kwa hivyo hebu tulipite jambo hilo pamoja na tukaribishe tamati inayokuja! Hata hivyo, kile kinachoendelea kunihangaisha Mimi kuwahusu ninyi ni kwamba, mnapokabiliwa na ukosefu wa haki na haki, kila mara mnachagua lililotangulia. Hilo, hata hivyo, sasa lipo katika wakati wenu uliopita. Natumai kusahau kila kitu cha wakati wenu uliopita, ingawa hili ni gumu sana kufanya. Hata hivyo, Nina njia nzuri sana ya kulifanya: Acha wakati ujao uchukue nafasi ya wakati uliopita, na kuruhusu vivuli vya wakati wenu uliopita vitawanywe ili kupata nafsi yenu ya kweli ya leo. Hivyo lazima Niwasumbue ninyi mfanye uchaguzi kwa mara nyingine tena: Je, ninyi ni waaminifu kwa nani hasa?

Maelezo ya chini:

a. Kurudi ufuoni: msemo wa Kichina, unaomaanisha “kugeuka kutoka katika njia mbaya za mtu.”

Iliyotangulia: Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Inayofuata: Juu ya Hatima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp