Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu

Nimewapa maonyo mengi na kutawaza juu yenu kweli nyingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyokuwa hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anapaswa awe, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata baada ya miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii kwenu kwingi na uasi dhidi Yangu hii miaka mingi, kwa sababu hakuna hata mtakatifu mmoja kati yenu, bila yeyote kuachwa nyuma nyinyi ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba Mimi daima Hujirudia mbele yenu. Sitaki kuishi hivi na nyinyi, lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, Mimi hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine tena. Natumai mtaniendekeza, na natumai hata zaidi kwamba mtakuwa na uwezo wa kuamini kila neno Nitakalosema, na hata zaidi, kwamba mtaweza kufahamu kwa kina maana ya maneno Yangu. Msiwe na shaka juu ya yale Ninayosema, au mbaya zaidi, kuchukua maneno Yangu mnavyotaka na kuyatupilia mbali kwa hiari, jambo ambalo mimi Ninapata haistahimiliki. Msiyahukumu maneno Yangu, sembuse kuyachukulia kirahisi, au kusema kwamba daima Nawajaribu, au mbaya zaidi, kusema kwamba kile ambacho Nimewaambia kinakosa usahihi. Mambo haya Ninapata kuwa hayavumiliki. Kwa sababu mnanichukulia Mimi na kuchukulia Ninayosema kwa shaka na kamwe hamyachukui ndani, Ninawaambia kila mmoja wenu kwa uzito wote: Msiunganishe kile Ninachosema na falsafa, msiyaweke pamoja na uongo wa matapeli, na hata zaidi, msiyajibu maneno Yangu kwa dharau. Labda hakuna mtu yeyote katika siku zijazo atakuwa na uwezo wa kuwaambia yale Ninawaambia nyinyi, au kuzungumza na nyinyi kwa huruma, sembuse kuwaeleza kuhusu mawazo haya kwa uvumilivu. Siku zijazo zitatumika katika kukumbuka nyakati zile nzuri, au kwa kulia kwa sauti kubwa, au kugumia kwa maumivu, au mtaishi katika njia ya usiku wa giza bila hata chembe cha ukweli au maisha kutolewa, au kusubiri tu bila matumaini, au katika majuto machungu kwamba nyinyi mmepita kiwango cha mantiki .... Hizi wezekano mbadala ni kweli (lakini si bayana) haziwezi kuepukika kwa mtu yeyote kati yenu. Kwa sababu hakuna hata mmoja wenu ambaye anamiliki kiti ambacho kwa kweli mnamwabudu Mungu; mnajitumbukiza katika dunia ya uasherati na maovu, kuchanganya katika imani yenu, ndani ya roho zenu, nafsi, na miili mambo mengi yasiyohusiana na maisha na ukweli na kwa kweli yana upinzani kwayo. Hivyo kile Natumai kwenu ni kuwa mnaweza kuletwa kwa njia ya mwanga. Tumaini Langu la pekee ni kwamba mna uwezo wa kujitunza wenyewe, uwezo wa kujihadhari wenyewe, si kuweka mkazo sana juu ya hatima yenu hadi mnatazama mienendo yenu na dhambi kwa kutojali.

Watu ambao wanaamini katika Mungu kwa muda mrefu sasa wametumainia hatima iliyo nzuri, watu wote ambao wanaamini katika Mungu wanatumai kwamba bahati nzuri ghafla itakuja kwao, na wote wanatumai kwamba bila kujua kwa amani watajikuta wameketi pahali pamoja au pengine mbinguni. Lakini Ninasema watu hawa pamoja na mawazo yao mazuri hawajawahi kujua kama wana uwezo wa kupokea bahati nzuri kama hiyo inayoanguka kutoka mbinguni, au kukaa juu ya kiti mbinguni. Kwa sasa nyinyi mna maarifa mazuri kujihusu, lakini bado mnatarajia kwamba mnaweza kuepuka maafa ya siku za mwisho na mkono wa mwenye Uweza ukiwaadhibu wale waovu. Inaonekana kana kwamba kuwa na ndoto tamu na kutaka maisha ya raha ni hulka ya kawaida ya watu wote ambao Shetani amewapotosha, sio kipaji cha ajabu cha mtu binafsi. Hata hivyo, bado Nataka kumalizatamaa zenu badhirifu na hamu zenu za kupata baraka. Kwa kuwa dhambi zenu ni nyingi na ukweli wa kutotii kwenu ni mwingi na kila wakati huongezeka, jinsi gani haya yatapatana na ramani yenu nzuri ya baadaye? Kama unataka kuendelea unavyotaka kukuwa katika ubaya, bila kitu kinachokuzuia, lakini bado unataka ndoto zitimie, basi Nakusihi uendele katika usingizi wako na kamwe usiamke, kwa sababu yako ni ndoto tupu, na haitatumika kukufanya usiye wa kawaida katika uso wa Mungu Mwenye haki. Kama unataka tu ndoto zitimie, basi kamwe usiote, lakini milele kabiliana na ukweli, kabiliana na ukweli. Hiyo ndio njia pekee ya kukuokoa. Je, kwa maneno thabiti, hatua za taratibu hizi ni zipi?

Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na kuchunguza mwenendo wako wote na mawazo ambayo hayafuati ukweli.

Hiki ni kipengee ambacho mnaweza kukifanya kwa urahisi, na Ninaamini kwamba watu wanaofikiri wana uwezo wa kukifanya. Hata hivyo, wale watu ambao hawajui ni nini maana ya dhambi na ukweli ni vikwazo, kwa sababu kimsingi wao sio watu wa kufikiri. Mimi Ninazungumza na watu ambao wamedhibitishwa na Mungu, ni waaminifu, hawajakosea amri za utawala vibaya, na kwa urahisi wanaweza kupata dhambi zao wenyewe. Ingawa hiki ni kipengee ambacho Ninahitaji kwenu ambacho ni rahisi kwenu, sio kipengee cha pekee Ninachohitaji kwenu. Haidhuru chochote, Ninatumai kwamba hamtalichecheka kwa siri hitaji hili, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kwa urahisi. Mlichukulie kwa umakini, na wala msilipuuze.

Pili, kwa kila moja ya dhambi zako na kutotii tafuta ukweli unaoambatana na utumie ukweli huu kuzitatua, kisha badilisha vitendo vyako vya dhambi na mawazo yako ya kutotii na vitendo na matendo ya ukweli.

Tatu, kuwa mtu mwaminifu, sio mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, daima mwenye hila. (Hapa Ninakuuliza tena uwe mtu mwaminifu.)

Kama unaweza kutimiza vipengee hivi vyote vitatu basi una bahati, ni mtu ambaye ndoto zake zinatimia na kupata bahati nzuri. Labda mtayachukulia maombi haya matatu yasiyovutia kwa umakini, au labda kuyachukulia bila kuwajibika. Haijalishi ni ipi, azma Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka maadili yenu katika matendo, sio kuwadhihaki au kuwadanganya.

Madai Yangu yanaweza kuwa rahisi, lakini kile Ninachowaambia si rahisi hivyo kama kujumlisha moja na moja upate mbili. Kama yote mnayofanya ni kuzungumza haya bila mpangilio, kuparaganya kwa taarifa tupu za mbwembwe, basi ramani yenu na matakwa yenu milele yatakuwa ukurasa mtupu. Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Hata sivyo, Mimi Huwachukulia wale ambao hawajatosheleza madai Yangu kwa adhabu, sio zawadi, sembuse huruma. Labda mnawaza kwamba kwa kuwa mfuasi kwa miaka mingi unaweka bidii katikabila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote unaweza kupata bakuli la mchele katika nyumba ya Mungu kwa kuwa mtendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu mmekuwa siku zote hadi sasa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani bila kuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa katika uzito wote: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kutunukiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unanifuata Mimi kwa karibu, jinsi una umashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile Ninachodai, kamwe hutaweza kushinda sifa Zangu. Futa yale mawazo hayo yote na hesabu zenu mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote kuwa majivuili Niitamatishe kazi Yangu, na kwa ubora zaidi Niifanye miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwautupu, kwa sababu Siwezi kuwaleta maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani katika ufalme Wangu, katika kipindi kijacho.

Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia zinazofaa na zenye mienendo mizuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, kuwa na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yaokwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu wenu na kutotii. Kama kila mmojawapo ya mazungumzo ambayo Nimekuwa nayo na nyinyi hayajawahi kutosha kuvuta nadhari yenu, basi huenda kila Ninaychoweza kufanya ni kutosema tena. Hata hivyo, nyinyi mnaelewa matokeo ya hayo. Mimi kamwe Sipumziki, hivyo basi Nisiponena, Nitafanya kitu ili watu watakitazame. Ningeweza kuufanya ulimi wa mtu uoze, au mtu afe bila viungo vyote, au kumpa mtu hisia zisizo za kawaida na kumfanya atende kama mwendawazimu. Au, basi tena, Naweza kufanya baadhi ya watu kuvumilia maumivu makali Nitakayochachisha kwa ajili yao. Kwa njia hii Ningejihisi Mwenye furaha, furaha sana na Mwenye kufurahashwa sana. Ilikuwa daima "Mema hulipizwa kwa mema, maovu kwa maovu," mbona isiwe hivyo kwa sasa? Kama unataka kunipinga Mimi na unataka kufanya hukumu fulani kunihusu, basi Mimi Nitauozesha mdomo wako, na hilo litanipendeza Mimi bila mwishod. Hii ni kwa sababu mwishowe hujafanya lolote linalohusiana na ukweli, sembuse kwa maisha, ilhali kila kitu Ninachofanya ni ukweli, kila kitu kinahusiana na kanuni za kazi Yangu na amri za utawala Ninazoweka chini. Kwa hiyo, Nawasihi sana kila mmoja wenu kujilimbikiza baadhi ya wema, wacha kufanya maovu mengi, na usikize madai Yangu katika wasaa wako wa mapumziko. Kisha mimi Nitahisi furaha. Kama mngekuwa wa kutoa (au kusaidia) kwa ukweli moja kwa elfu ya juhudi mnazoweka katika mwili, basi Nasema hungekuwa na dhambi mara kwa mara na midomo iliyooza. Je, hili sidhahiri?

Kadri dhambi zako zinavyoongezeka, ndivyo nafasi yako ya kupata hatima iliyo nzuri inapungua. Kinyume chake, kadri dhambi zako zilivyo ndogo, ndivyo nafasi zako za kusifiwa na Mungu zinazidi kuongezeka. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi mahali ambapo ni vigumu Kwangu kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa mjasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile yatakupa. Kama wewe ni mtu mwenye ari anayetenda ukweli basi kwa hakika una nafasi ya dhambi zako kusamehewa, na idadi ya kutotii kwako itakuwa chache zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu asiye radhi kutenda ukweli basi dhambi zako mbele ya Mungu kwa hakika zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitakua zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeharibiwa kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kufurahisha ya kupokea barakaitaharibiwa. Usuzichukue dhambi zako kama makosa ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, wala usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu tabia yako duni ulifanya isiwezekane kuitenda, na hata zaidi, usizichukulie dhambi zako ulizofanya kwa urahisi kama matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri. Kama unajua vizuri kujisamehe mwenyewe na uzuri wa kujitendea mwenyewe kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hatapata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukusumbua, lakini kukuzuia kabisa katika kutosheleza madai ya ukweli na kukufanya milele kuwa mwenzi mwaminifu wa Shetani. Ushauri Wangu kwako bado ni: Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa umakini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kwako kuhusu hatima yako.

Iliyotangulia:Maonyo Matatu

Inayofuata:Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Unaweza Pia Kupenda