Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu
Kuna mambo mengi ambayo Ninatumai kuwa mtaweza kuyafikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kuridhisha matakwa Yangu kikamilifu, kwa hiyo ni lazima Niseme kile hasa Ninachotaka kusema na kuwafafanulia mapenzi Yangu. Kwa kuwa utambuzi wenu ni mdogo na ufahamu wenu pia ni mdogo, mpo karibu kabisa kukosa kuijua tabia Yangu na kiini Changu pia, na hivyo ni suala la dharura kwamba Niwafahamishe kuyahusu. Haijalishi hapo awali ulielewa kwa kiwango kipi, au kama uko tayari kujaribu kuelewa masuala haya, bado ni lazima Niyaelezee kwenu kwa undani. Masuala haya si mageni kabisa kwenu, lakini bado mnakosa uelewa mwingi, ufahamu mwingi, kwa maana iliyoko ndani yao. Wengi wenu mna ufahamu mdogo tu, na wa sehemu na ambao haujakamilika kwa hilo. Ili kuwasaidia kutenda ukweli kwa njia bora zaidi, yaani, kuweka maneno Yangu katika matendo kwa njia bora zaidi, Nafikiri kwamba ni masuala haya ambayo ni lazima kwanza myajue. Vinginevyo, imani yenu itabakia kuwa isiyo na uhakika, ya kinafiki, na iliyojawa na mambo ya kidini. Kama huielewi tabia ya Mungu, basi hautaweza kufanya kazi unayopaswa kufanya kwa ajili Yake. Kama hujui dutu ya Mungu, basi hautaweza kumwonyesha heshima na uchaji, lakini badala yake kutakuwa tu na uzembe wa kutokujali, na kuepuka kusema ukweli wote, na hata zaidi, kufuru isiyoweza kurekebishwa. Ingawa kuielewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, hakuna yeyote ambaye amewahi kuchunguza kwa umakini au kudadisi masuala haya. Ni wazi kuona kwamba nyote mmetupilia mbali amri za utawala Nilizotoa. Kama huielewi tabia ya Mungu, basi kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa wewe kuikosea tabia Yake. Kuikosea tabia Yake ni sawa na kuchochea hasira ya Mungu Mwenyewe, ambapo matunda ya mwisho ya matendo yako yatakuwa ni ukiukaji wa amri za utawala. Sasa unapaswa kutambua kwamba unapoelewa kiini cha Mungu, vivyo hivyo utaweza kuielewa tabia Yake—na unapoielewa tabia Yake, vivyo hivyo utakuwa umeelewa amri za utawala. Bila shaka, mengi ya yale yaliyoko katika amri za utawala yanahusisha tabia ya Mungu, lakini tabia Yake yote haijaonyeshwa ndani ya amri za utawala; kwa hivyo, ni lazima mpige hatua zaidi katika kuongeza ufahamu wenu wa tabia ya Mungu.
Ninaongea nanyi leo si katika hali ya mazungumzo ya kawaida, kwa hiyo inapaswa myachukulie maneno Yangu kwa uangalifu na, zaidi ya hayo, myatafakari kwa kina. Kile Ninachomaanisha kwa hili ni kwamba mmetoa jitihada ndogo sana kwa maneno ambayo Nimeyazungumza. Tunapokuja kwa tabia ya Mungu, hamko radhi hata zaidi kutafakari juu ya suala hili, na ni mara chache sana ambapo mtu anaweka juhudi katika hilo. Kwa hiyo, Nasema kwamba imani yenu ni mazungumzo ya kujionyesha tu. Hata sasa, hakuna hata mmoja wenu ametoa jitihada yoyote ya dhati kwa udhaifu wenu mkubwa zaidi. Mmeniangusha baada ya maumivu yote Niliyoyapitia kwa ajili yenu. Si ajabu kwamba hamjali kuhusu Mungu na mnaishi maisha yasiyo na ukweli. Watu kama hawa wanawezaje kuhesabiwa kama watakatifu? Sheria ya mbinguni haitavumilia jambo kama hilo! Kwa kuwa mna uelewa mdogo sana wa hili, basi itabidi Nitumie pumzi zaidi.
Tabia ya Mungu ni mada ambayo inaonekana kuwa ya dhahania sana kwa kila mtu na aidha ambayo haikubaliwi kwa urahisi, kwani tabia Yake ni tofauti na hulka ya binadamu. Mungu, pia, ana hisia za raha, hasira, huzuni, na furaha, lakini hisia hizo zinatofautiana na zile za binadamu. Mungu Mwenyewe ana milki na nafsi Yake. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukifichua ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Kila Alicho na anacho, pamoja na dutu na utambulisho Wake vyote ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, faraja kwa binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa binadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini chanya, changamfu, au isiyo na hisia. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai, na Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukuu, na zaidi ya yote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Zaidi ya hayo, tabia Yake ni ishara ya Yeye kutoweza kushindwa au kushambuliwa na giza au na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye kutoweza kukosewa (wala Hatavumilia kukosewa) na kiumbe chochote kilichoumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wenye uwezo au wanaoweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini sifa bainifu za mwanadamu ishara tu ya mamlaka madogo ya mwanadamu juu ya mnyama. Mwanadamu ndani yake na kwake hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuenda zaidi ya nafsi, lakini katika kiini chake ni mtu ambaye anajinyenyekeza chini ya kila aina ya watu, matukio, na vitu. Furaha ya Mungu inatokana na kuwepo na kuzuka kwa haki na nuru; kwa sababu ya uharibifu wa giza na uovu. Anafurahi kwa sababu Ameleta nuru na maisha mazuri kwa wanadamu; Furaha Yake ni furaha ya haki, ishara ya kuwepo kwa yote ambayo ni chanya na, hata zaidi, ishara ya fanaka. Ghadhabu ya Mungu ni n kwa sababu ya madhara ambayo kuwepo na kuingiliwa kwa dhulma kunaleta juu ya binadamu Wake, kwa sababu ya kuwepo kwa uovu na giza, kwa sababu ya kuwepo kwa vitu vinavyofukuza ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya kuwepo kwa vitu vinavyopinga vitu vilivyo vyema na vizuri. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote hasi havitakuwepo tena, na hata zaidi ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya wanadamu, ambao Amekuwa na matumaini nao lakini ambao wameanguka katika giza, ni kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya wanadamu wasio na hatia, kwa sababu ya yule ambaye ni mwaminifu lakini ni mjinga, na kwa sababu yule mwanadamu mzuri lakini ana upungufu katika maoni yake mwenyewe. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya uzuri na ukarimu. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda maadui Zake na kupata imani nzuri ya mwanadamu. Zaidi ya hayo, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na kwa sababu wanadamu wamepokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na raha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko raha. Furaha Yake ni ishara ya wanadamu kuwa huru dhidi ya mateso kuanzia wakati huu na kuendelea, na ni ishara ya wanadamu kuingia katika ulimwengu wenye mwanga. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote huibuka kwa ajili ya masilahi yake mwenyewe, na wala si kwa ajili ya haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, sembuse neema inayotolewa na Mbingu. Hisia za wanadamu zina ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa kwa njia sawa. Mungu ni mkuu milele na Anaheshimiwa milele, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote hana thamani. Hii ni kwa sababu daima Mungu anajitoa na kugharimika kwa ajili ya wanadamu, ilhali mwanadamu daima anatafuta na kujitahidi kwa ajili yake mwenyewe. Mungu daima anajitaabisha kwa ajili ya kuwepo kwa wanadamu, ilhali mwanadamu hachangii chochote kamwe kwa ajili ya haki au nuru, na hata kama mwanadamu atafanya jitihada ya muda, yeye ni dhaifu sana hawezi kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, wakati Mungu hana ubinafsi milele. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vizuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kuisaliti haki na kujiweka mbali na Mungu.
Kila sentensi Niliyoizungumza ina tabia ya Mungu ndani yake. Mtafanya vizuri endapo mtatafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka kwa maneno hayo. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuielewa, lakini Ninaamini kwamba angalau nyinyi nyote mna mawazo fulani kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatulizwa moyo. Kwa mfano, mweke Mungu moyoni mwako kila wakati. Unapochukua hatua, fanya hivyo kulingana na maneno Yake. Tafuta nia Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Hata zaidi usimweke Mungu nyuma ya akili yako ili ujaze utupu wa siku zijazo katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umeikosea tabia ya Mungu. Tena, ikitokea kwamba hutawahi kutamka matamshi ya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu maisha yako yote, na tena ikitokea kwamba unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho Amekuaminia wewe na pia kutii maneno Yake yote katika maisha yako yote, basi utakuwa umeweza kuepuka kuasi dhidi ya amri za utawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya ni nuru kiasi tu ya Roho Mtakatifu,” “Katika maoni yangu, si kila kitu ambacho Mungu anakifanya lazima ni sahihi,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukuu zaidi kuliko wangu,” “Maneno ya Mungu hayaaminiki kabisa,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakusihi wewe ukiri na kutubu dhambi zako mara nyingi zaidi. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani humkosei mwanadamu, ila Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unamhukumu mtu tu, lakini Roho wa Mungu haichukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia Yeye heshima. Kama hali ni hivi, basi si ni kweli kwamba umeikosea tabia ya Mungu? Lazima ukumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu kinafanywa ili kulinda kazi Yake katika mwili na ili kazi hii ifanywe vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ni mtu ambaye kamwe hataweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, kwa hivyo Atatumia adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.
Kupata kujua dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole na bila kujua, utaanza kujua dutu ya Mungu. Wakati umeingia katika maarifa haya, utajikuta unasonga mbele kwenye hali ya juu na nzuri zaidi. Mwishowe, utakuja kujisikia aibu kwa nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unahisi hakuna mahali pa kujificha. Wakati huo, kutakuwa na machache zaidi na zaidi katika mwenendo wako ya kukosea tabia ya Mungu, moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utaongezeka ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya wanadamu kuingia katika hali nzuri. Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Mnaposhughulika huku na kule kwa ajili ya majaaliwa yenu, ni nani anayependa kujaribu kujua dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, mtakiuka amri za utawala bila kujua, kwani mnafahamu kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, je, si kile ambacho mnafanya sasa kinaweka msingi wa makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaambia muielewe tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkikosea amri za utawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, basi kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Nawaambia kwamba, pamoja na kuchunguza mienendo yenu binafsi, muwe waangalifu zaidi na hatua mnazochukua. Haya ndiyo yatakuwa mahitaji ya juu zaidi Ninayotoa kwenu, na Ninatumai kwamba nyote mtayafikiria kwa umakini na kuyaona kuwa muhimu kabisa. Endapo siku itafika ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa ya kwenu peke yenu kuyafikiria, na hakutakuwa na mwingine yeyote atakayechukua adhabu hiyo kwa niaba yenu.