Sura ya 24

Wakati unakaribia hata zaidi. Amkeni! Watakatifu wote! Nitawatamkia ninyi. Wote wanaosikia wataamka. Mimi ni Mungu ambaye mmekuwa na imani katika kwa miaka hii mingi. Leo nimekuwa mwili na kuja mbele ya macho yenu, na hii inafichua yule ambaye ananitaka kwa kweli, ambaye yuko tayari kulipa gharama yoyote kwa ajili Yangu, ambaye husikiliza neno Langu kwa kweli, na yule ambaye yuko tayari kuuweka ukweli katika matendo. Kwa maana mimi ni mwenyezi Mungu, Ninaweza kuona siri zote za binadamu zilizofichwa gizani, Najua ni nani anayenitaka kwa kweli na Ninajua ni nani anayenipinga Mimi; Ninaweza kuchunguza mambo haya yote.

Sasa Ningependa kufanya kikundi cha watu ambao wanaupendeza moyo Wangu haraka iwezekanavyo, wale ambao wanaweza kuihurumia mizigo Yangu. Hata hivyo, Siwezi kuacha kusafisha na kutakasa kanisa Langu; kanisa ni moyo Wangu. Ninawadharau watu wote wabaya wanaowazuia msile na kunywa neno Langu. Hii ni kwa sababu kuna watu fulani wachache ambao hawanitaki Mimi kwa kweli. Watu hawa wamejaa udanganyifu, hawaji karibu na Mimi na moyo wao wa kweli, wao ni waovu, na ni watu ambao huzuia utekelezaji wa mapenzi Yangu; wao sio watu ambao huweka ukweli katika matendo. Watu hawa wamejaa kujidai na majivuno, wao ni wenye kutamani makuu vikali, wanapenda kutenda mema kwa nia ya kusimanga, na maneno wanayosema ni mazuri kusikia, lakini kwa siri hawatendi ukweli. Watu hawa waovu wote watakatwa na kuzolewa kabisa; watateseka katika majanga. Maneno haya ni kuwakumbusha na kuwaonya ili msalie kwenye njia inayoupendeza moyo Wangu. Daima rudini katika roho yenu, kwa sababu Ninawapenda wale wanaonipenda kwa moyo wao wote. Kwa kuwa mnanikaribia Mimi, nitawalinda na kuwaweka mbali na wale waovu, Nitawafanya msimame imara nyumbani Kwangu na kuwalinda mpaka mwisho.

Iliyotangulia: Sura ya 23

Inayofuata: Sura ya 25

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp