Filamu za Kikristo “Tafakari Juu ya Wokovu” (Trela)

25/08/2023

Yang Mingyuan ni mzee wa kanisa la nyumbani. Siku moja, anasikia kwamba Mzee Xu, ambaye anaheshimika sana kanisani, amekubali Umeme wa Mashariki. Anaguswa sana, na anaamua kutafuta na kuchunguza Umeme wa Mashariki. Kupitia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, maswali ambayo yamemchanganya kwa miaka mingi kuhusu kumwamini Bwana yanatatuliwa, na anajifunza kwamba kuokolewa ni msamaha wa dhambi tu, si wokovu kamili. Ni kwa kukubali tu hukumu na utakaso wa Mungu katika siku za mwisho na kutatua kikamilifu asili yake ya dhambi ndiyo anaweza kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni. Anasoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu na kugundua kwamba hayo ni ukweli na sauti ya Mungu. Anaamini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, kwa hivyo anamkubali Mwenyezi Mungu kwa furaha. Baadaye, anahubiri injili kwa waumini walio chini yake, na ndani ya miezi michache, watu elfu tano au sita wanaikubali injili. Anafikiri ataendelea kuwa kiongozi, lakini anashangaa kanisa linapompangia kuhubiri injili huku wafanyakazi wenzake wakichaguliwa kuwa viongozi. Akiwa anahubiri injili, ushirika wake juu ya ukweli sio dhahiri au wa vitendo kama mshirika wake Ndugu Zhou. … Haridhishwi kuwa katika nafasi ya pili, na ili kuthibitisha nguvu zake na akitaka aheshimiwe na wengine, anafanya kazi kwa bidii ili kujitayarisha na ukweli, na mara nyingi anajidai mbele ya watu kiasi cha kazi ambayo amefanya na jinsi alivyoteseka. Anashangaa wakati hili linaposababisha akina ndugu zake kumpogoa na kumshughulikia na Mungu kumwadibu vikali na kumfundisha nidhamu…. Baada ya kupitia hukumu na kuadibu, kuadibiwa na kufundishwa nidhamu, Yang Mingyuan anapata nini hasa? Anabadilikaje? Tazama filamu hii ili ujue.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp