The Words the Holy Spirit Says to the Churches | "Sauti Nzuri Ajabu" | Filamu za Injili

20/08/2018

Dong Jingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina. Amemsadiki Bwana kwa miaka thelathini, na anapenda ukweli, mara kwa mara yeye husoma maneno ya Bwana na yanamsisimua. Anajitumia kwa ajili ya Bwana kwa shauku kubwa. Kwa sababu ya kazi yake ya kuhubiri, alikamatwa na polisi wa serikali ya Kikomunisti ya Kichina na akafungwa gerezani ambako alivumilia ukatili na mateso. Maneno ya Bwana ndiyo yaliyomwongoza kwa kustahamili miaka saba ya maisha ya gerezani yasiyokuwa ya kibinadamu . Baada ya kutoka gerezani, mfanyakazi mwenza Chenguang anakuja kumwona na kumsomea kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu, akishuhudia kwamba Mungu ameonekana na anafanya kazi katika siku za mwisho. Anampatia pia nakala ya Neno Laonekana katika Mwili. Baada ya kusoma kiasi kidogo cha maneno ya Mwenyezi Mungu, Dong Jingxin anahisi kwamba yana mamlaka na kwamba yanatoka kwa Mungu. Anakuwa na moyo wa kutamani kutafuta. Dong Jingxin na mumewe wanasoma ya maneno ya Mwenyezi Mungu kwa shauku na kugundua kwamba yote ni ukweli, na kwamba ni sauti ya Mungu. Wanaamua kwamba Mwenyezi Mungu kwa kweli ndiye kurudi kwa Bwana Yesu ambaye wamekuwa wakisubiri kwa miaka! Wakati tu hawa wawili wamejawa na furaha ya kukaribisha kurudi kwa Bwana, chifu wa polisi anawatembelea kuwaonya kutohudhuria mikusanyiko yoyote au kufanya mahubiri yoyote. Anawaonya kwamba lazima hasa wamripoti mtu yeyote anayehubiri Umeme wa Mashariki, na hili linampa wasiwasi Dong Jingxin. Baada ya hayo, pindi mchungaji wao anapogundua kwamba Dong Jingxin anaongoza ndugu kuichunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho, anaingilia pia na kuwazuia. Akiwa amechanganyikiwa na amevurugwa na nguvu za Shetani, Dong Jingxin anaweza kuona waziwazi hali ya kweli ya wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini kupitia kwa maombi, kutafuta, na ushirika. Hakati tamaa, lakini anaendelea kuwaongoza ndugu katika kuchunguza njia ya kweli, na anawaalika watu kutoka kwenye Kanisa la Mwenyezi Mungu ili kushiriki na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Mwishowe, kila mmoja anakubali kwamba maneno yaliyotamkwa na Mwenyezi Mungu kwa kweli ni sauti ya Mungu, na kwamba Yeye ni kuonekana kwa Mungu. Kila mmoja anasisimkwa kwa kina: Maneno ya Mwenyezi Mungu yanayo sauti nzuri ajabu!

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp