Msimamo Wako Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu ni Upi?

Agano Jipya la Biblia lina nyaraka kumi na tatu za Paulo. Katika muda aliofanya kazi yake, Paulo aliandika barua hizi kumi na tatu kwa makanisa yaliyoamini katika Yesu Kristo. Yaani, Paulo aliinuliwa na akaandika barua hizi baada ya Yesu kupaa mbinguni. Barua zake ni ushuhuda wa kufufuka na kupaa mbinguni kwa Bwana Yesu baada ya kifo Chake, na pia zilieneza njia ya toba na kubeba msalaba. Bila shaka, ujumbe na ushuhuda huu wote ulinuiwa kuwafunza ndugu katika maeneo tofauti huko Yudea wakati huo, kwa sababu wakati huo, Paulo alikuwa mtumishi wa Bwana Yesu, na alikuwa ameinuliwa kumshuhudia Bwana Yesu. Katika kila kipindi cha kazi ya Roho Mtakatifu, watu mbalimbali huinuliwa kutekeleza kazi Zake tofauti, yaani kufanya kazi ya mitume ili kuendeleza kazi ambayo Mungu anakamilisha Mwenyewe. Ikiwa Roho Mtakatifu angeifanya moja kwa moja, na hakuna watu wangeinuliwa, basi ingekuwa vigumu sana kwa kazi hiyo kutekelezwa. Kwa hiyo, Paulo akawa yule ambaye aliangushwa akiwa njiani kuelekea Dameski, na ambaye baada ya hapo aliinuliwa kumshuhudia Bwana Yesu. Alikuwa mtume kando na wanafunzi kumi na wawili wa Yesu. Juu ya kueneza injili, pia alifanyia makanisa ya maeneo mbalimbali kazi ya uchungaji, ambayo ilihusisha kuwatunza ndugu wa makanisa hayo—yaani, kuwaongoza ndugu katika Bwana. Ushuhuda wa Paulo ulikuwa ili kujulisha kuhusu kufufuka na kupaa mbinguni kwa Bwana Yesu, na vilevile kuwafunza watu kutubu, kukiri, na kuitembea njia ya msalaba. Alikuwa mmoja wa mashahidi wa Yesu Kristo wa wakati huo.

Nyaraka kumi na tatu za Paulo zilichaguliwa ili zitumike katika Biblia. Aliandika hizo nyaraka zote kumi na tatu kuzungumzia hali tofauti za watu katika mahala mbalimbali. Aliguswa na Roho Mtakatifu kuziandika, na akawafunza ndugu kila mahali kutoka kwa nafasi ya mtume (kutoka kwa mtazamo wa mtumishi wa Bwana Yesu). Kwa hiyo, barua za Paulo hazikutoka kwa unabii au kutoka moja kwa moja kwa maono, bali zilitoka kwa kazi aliyoifanya. Barua hizi si za ajabu, wala si ngumu kuelewa kama unabii. Zinaandikwa tu kama barua, na hazina unabii wala mafumbo; zina maneno ya kawaida ya maagizo tu. Hata ingawa maneno yake mengi huenda yakawa magumu kwa watu kuyaelewa ama magumu kufahamu, yalitoka tu katika ufafanuzi wa Paulo mwenyewe na katika nuru ya Roho Mtakatifu. Paulo alikuwa mtume tu; alikuwa mtumishi aliyetumiwa na Bwana Yesu, si nabii. Alipokuwa akitembea katika nchi mbalimbali, aliwaandikia ndugu wa kanisa barua, ama, alipokuwa akiugua, aliyaandikia barua makanisa ambayo alikuwa akiyafikiria hasa lakini hakuweza kuyazuru. Kwa sababu hiyo, barua zake ziliwekwa na watu na baadaye zikakusanywa, kuratibiwa, na kupangwa baada ya Injili Nne katika Biblia na vizazi vya baadaye. Bila shaka, walichagua na kukusanya barua zote bora ambazo alikuwa ameandika. Nyaraka hizi zilinufaisha maisha ya ndugu wa kanisa, na hasa zilikuwa mashuhuri katika wakati wake. Paulo alipoziandika, lengo lake halikuwa kuandika kazi ya kiroho ambayo ingewawezesha ndugu zake wapate njia ya kutenda ama wasifu wa kiroho wa kuelezea aliyoyapitia yeye mwenyewe; hakunuia kuandika kitabu ili awe mwandishi. Alikuwa tu akiwaandikia ndugu zake wa kanisa la Bwana Yesu barua. Kutoka kwa nafasi yake kama mtumishi, Paulo aliwafunza ndugu zake, akiwaambia kuhusu mzigo wake, kuhusu mapenzi ya Bwana Yesu, na kuhusu kazi ambazo Alikuwa amewaaminia watu wa siku za baadaye. Hii ilikuwa kazi ambayo Paulo alitekeleza. Maneno yake yaliadilisha sana uzoefu wa ndugu wote wa baadaye. Ukweli aliowasilisha katika barua hizi nyingi ulikuwa kile ambacho watu katika Enzi ya Neema walipaswa kutenda, na ndiyo sababu barua hizi zilipangwa katika Agano Jipya na vizazi vya baadaye. Bila kujali matokeo ya Paulo yaliishia kuwa yapi, alikuwa mtu ambaye alitumiwa katika wakati wake, na ambaye aliwasaidia ndugu katika makanisa. Matokeo yake yaliamuliwa na asili yake, na vilevile yeye kuangushwa mwanzoni. Aliweza kuyazungumzia maneno hayo wakati huo kwa sababu alikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na Paulo aliyabebea makanisa mzigo kwa sababu ya kazi hii. Kwa hiyo, aliweza kuwaruzuku ndugu zake. Hata hivyo, kwa sababu ya hali fulani za kipekee, Paulo hakuweza kuenda kwa makanisa hayo kufanya kazi yeye binafsi, kwa hiyo aliyaandikia barua kuwaonya ndugu zake katika Bwana. Mwanzoni, Paulo aliwatesa wanafunzi wa Bwana Yesu, lakini baada ya Yesu kupaa mbinguni—yaani, baada ya Paulo “kuona mwangaza”—alikoma kuwatesa wanafunzi wa Bwana Yesu, na hakuwatesa tena wale watakatifu waliohubiri injili kwa ajili ya njia ya Bwana. Baada ya Paulo kumwona Yesu akimwonekania kama mwanga mkali, alikubali agizo la Bwana, na hivyo akawa mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu kueneza injili.

Kazi ya Paulo wakati huo ilikuwa tu kuwasaidia na kuwaruzuku ndugu zake. Hakuwa kama watu wengine, waliotaka kufanikiwa katika kazi yao ama kubuni kazi za fasihi, kuchunguza namna nyingine za mbadala, ama kupata njia kando na Biblia za kuwaongoza watu hawa katika makanisa ili wote waweze kuingia upya. Paulo alikuwa mtu aliyetumiwa; katika kufanya mambo aliyoyafanya, alikuwa tu akitimiza wajibu wake. Ikiwa hangeyabebea makanisa mzigo, basi angechukuliwa kuwa yule aliyetelekeza wajibu wake. Ikiwa jambo la kukatiza lingetokea, ama tukio la usaliti lingefanyika katika kanisa ambalo lingewasababisha watu hapo wawe na hali isiyo ya kawaida, basi angechukuliwa kuwa hakutekeleza kazi yake vizuri. Mfanyakazi akilibebea kanisa mzigo, na pia afanye kazi vyema kadiri ya uwezo wake, basi hili linathibitisha kwamba mtu huyu ni mfanyakazi anayestahili—anayestahili kutumika. Mtu asipohisi mzigo wowote kwa ajili ya kanisa, na asitimize matokeo yoyote katika kazi yake, na watu wengi anaowaongoza ni dhaifu au hata wanaanguka, basi mfanyakazi kama huyu hajatimiza wajibu wake. Paulo alikuwa vivyo hivyo, na ndiyo sababu ilimbidi ayatunze makanisa na kuwaandikia ndugu zake barua mara kwa mara. Aliweza kuyaruzuku makanisa na kuwatunza ndugu zake kwa namna hii; ni kwa njia hii pekee ndiyo makanisa yaliweza kupokea ruzuku na uchungaji kutoka kwake. Maneno ya barua alizoandika yalikuwa ya maana sana, lakini yaliandikiwa ndugu zake chini ya sharti la yeye kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, na alitia uzoefu wake binafsi na mzigo aliohisi ndani ya maandishi yake. Paulo alikuwa tu mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu, na maudhui yote ya barua zake yalichanganywa na uzoefu wake binafsi. Kazi aliyoifanya inawakilisha tu kazi ya mtume, siyo kazi iliyotekelezwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, na pia inatofautiana na kazi ya Kristo. Paulo alikuwa tu akitimiza wajibu wake, ambayo ndiyo sababu aliwaruzuku ndugu zake katika Bwana kwa mzigo wake na vilevile uzoefu na umaizi wake binafsi. Paulo alikuwa tu akitekeleza kazi ya agizo la Mungu kwa kutoa umaizi na ufahamu wake binafsi; bila shaka huu haukuwa mfano wa kazi iliyotekelezwa moja kwa moja na Mungu Mwenyewe. Kwa hiyo, kazi ya Paulo ilichanganywa na uzoefu wa binadamu na maoni ya binadamu na ufahamu wa kazi ya kanisa. Hata hivyo, ufahamu na maoni haya ya binadamu hayawezi kusemekana kuwa kazi ya roho mbaya ama kazi ya mwili na damu; yanaweza tu kusemekana kuwa maarifa na uzoefu wa mtu ambaye alikuwa ametiwa nuru na Roho Mtakatifu. Nikisema hivi namaanisha kwamba barua za Paulo si vitabu kutoka mbinguni. Barua hizi si takatifu, na hazikutamkwa ama kuonyeshwa na Roho Mtakatifu hata kidogo; ni maonyesho tu ya mzigo wa Paulo kwa ajili ya makanisa. Lengo Langu katika kusema haya yote ni kuwafanya muelewe tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu: Kazi ya Mungu inamwakilisha Mungu Mwenyewe, wakati kazi ya mwanadamu inawakilisha wajibu na uzoefu wa mwanadamu. Mtu hapaswi kuchukulia kazi ya kawaida ya Mungu kama mapenzi ya mwanadamu na kazi Yake ya mwujiza kama mapenzi ya Mungu; aidha, mtu hapaswi kuyachukulia mahubiri ya kiburi ya mwanadamu kama matamshi ya Mungu ama kama vitabu kutoka mbinguni. Maoni yote kama haya hayana maadili. Wanaponisikia Nikichambua nyaraka kumi na tatu za Paulo, watu wengi wanaamini kwamba barua za Paulo hazipaswi kusomwa, na kwamba Paulo alikuwa mtu mwenye dhambi sana. Hata kuna watu wengi wanaofikiri maneno Yangu hayana huruma, kwamba makadirio Yangu ya nyaraka za Paulo si sahihi, na kwamba barua hizo hazipaswi kuchukuliwa kuwa maonyesho ya uzoefu na mzigo wa mwanadamu. Wanaamini kuwa badala yake zinapaswa kuchukuliwa kuwa maneno ya Mungu, kwamba ni muhimu kama Kitabu cha Yohana cha Ufunuo, kwamba haziwezi kufupishwa ama kuongezewa, na, aidha, haziwezi kuelezwa kwa kugusia juujuu. Je, madai haya yote ya binadamu hayana makosa? Je, hilo halijasababishwa na watu kutokuwa na busara kabisa? Barua za Paulo zinawafaidi watu sana, na tayari zina historia ya zaidi ya miaka 2,000. Hata hivyo, hadi leo, bado kuna watu wengi wasioweza kuelewa alichosema wakati huo. Watu huziona barua za Paulo kuwa kazi bora zaidi katika Ukristo wote, na kwamba hakuna mtu anayeweza kuzifumbua, na kwamba hakuna mtu anayeweza kuzielewa kikamilifu. Kwa kweli, barua hizi ni kama tu wasifu wa mtu wa kiroho, na haziwezi kulinganishwa na maneno ya Yesu ama maono makuu aliyoyaona Yohana. Kinyume chake, aliyoyaona Yohana yalikuwa maono makuu kutoka mbinguni—unabii wa kazi ya Mungu mwenyewe—ambayo hayakuweza kutimizwa na mwanadamu, ilhali barua za Paulo ni maelezo tu ya kile mwanadamu aliona na kupitia. Ni yale ambayo mwanadamu anaweza kutimiza, lakini si unabii wala maono; ni barua tu zilizotumwa maeneo mbalimbali. Hata hivyo, kwa watu wa wakati huo, Paulo alikuwa mfanyakazi, na kwa hiyo maneno yake yalikuwa na thamani, kwa sababu alikuwa mtu aliyekubali alichoaminiwa. Kwa sababu ya hayo, barua zake ziliwanufaisha wale wote waliomtafuta Kristo. Ingawa maneno hayo hayakunenwa na Yesu binafsi, mwishowe yalikuwa na umuhimu kwa wakati wao. Kwa hiyo, watu waliokuja baada ya Paulo walipanga barua zake katika Biblia, hivyo kuziwezesha kupitishwa hadi leo. Je, mnaelewa Ninachomaanisha? Nawapa tu maelezo sahihi ya barua hizi, na kuzichambua bila kupinga manufaa na thamani zao kwa watu kama marejeleo. Ikiwa hampingi tu barua za Paulo baada ya kuyasoma maneno Yangu, ila kuzichukulia kuwa uzushi ama zisizo na thamani, basi inaweza tu kusemekana kwamba uwezo wenu wa kuelewa na vilevile umaizi wenu na jinsi mnavyoyaona mambo ni dhaifu sana; hakika haiwezi kusemekana kwamba maneno Yangu ni ya upendeleo kupita kiasi. Je, mnaelewa sasa? Mambo muhimu mnayopaswa kuelewa ni hali halisi ya kazi ya Paulo wakati huo na mazingira ambamo barua zake ziliandikwa. Ikiwa mna maoni sahihi kuhusu vipengele hivi, basi pia mtakuwa na maoni sahihi ya nyaraka za Paulo. Wakati uo huo, punde tu mnapoelewa kiini cha barua hizo, makadirio yenu ya Biblia yatakuwa sahihi, na kisha mtaelewa kwa nini nyaraka za Paulo zimependwa sana na vizazi vya baadaye vya watu kwa miaka mingi mno, na vilevile kwa nini hata kuna watu wengi wanaomchukulia kuwa Mungu. Je, hamngefikiria hivyo pia ikiwa hamngeelewa?

Mtu ambaye si Mungu Mwenyewe hawezi kumwakilisha Mungu Mwenyewe. Kazi ya Paulo inaweza tu kusemekana kuwa sehemu ya maoni ya binadamu na sehemu ya nuru ya Roho Mtakatifu. Paulo aliyaandika maneno haya kutoka kwa mtazamo wa binadamu, akiwa na nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hili ni jambo la kawaida. Hivyo haingeepukika kwamba maneno yake yalichanganywa na uzoefu kiasi wa binadamu, na baadaye alitumia uzoefu wake binafsi kuwaruzuku na kuwasaidia ndugu zake wakati huo. Barua alizoandika haziwezi kuainishwa kama uchunguzi wa maisha, wala haziwezi kuainishwa kama wasifu ama ujumbe. Aidha, hazikuwa ukweli uliotendwa na kanisa wala amri za utawala za kanisa. Kama mtu aliyekuwa na mzigo—mtu aliyepewa kazi na Roho Mtakatifu—hili ni jambo ambalo lazima tu alifanye. Roho Mtakatifu akiwainua watu na kuwapa mzigo, lakini wasifanye kazi ya kanisa, na wasiweze kusimamia shughuli zake vizuri, ama kutatua shida zake zote vyema kabisa, basi hili linathibitisha kwamba watu hao hawatimizi wajibu wao vizuri. Kwa hivyo halikuwa jambo la ajabu sana kwa mtume kuweza kuandika barua wakati wa kazi yake. Hii ilikuwa sehemu ya kazi yake; alilazimika kuifanya. Lengo lake la kuandika barua halikuwa kuandika uchunguzi wa maisha ama wasifu wa kiroho, na hakika halikuwa ili kuwafungulia watakatifu njia nyingine mbadala. Badala yake, alifanya hilo ili kutimiza kazi yake mwenyewe na kuwa mtumishi mwaminifu kwa Mungu, ili aweze kujieleza kwa Mungu kwa kukamilisha kazi Alizomwaminia. Ilimlazimu awajibike kwa sababu yake na kwa sababu ya ndugu zake katika kazi yake, na ilimlazimu afanye kazi yake vizuri na azingatie masuala ya kanisa: Haya yote yalikuwa tu sehemu ya kazi yake.

Ikiwa mmepata ufahamu wa barua za Paulo, pia mtakuwa na fikira na makadirio sahihi kuhusu nyaraka za Petro na Yohana. Hamtawahi tena kuziona barua hizi kuwa vitabu kutoka mbinguni ambazo ni takatifu na zisizokiukwa, sembuse kumchukulia Paulo kuwa Mungu. Hata hivyo, kazi ya Mungu ni tofauti na kazi ya mwanadamu, na aidha, maonyesho Yake yanawezaje kuwa sawa na ya mwanadamu? Mungu ana tabia Yake Mwenyewe ya pekee, ilhali mwanadamu ana wajibu ambao anapaswa kutimiza. Tabia ya Mungu inaonyeshwa katika kazi Yake, ilhali wajibu wa mwanadamu unadhihirishwakatika uzoefu wa mwanadamu na kuonyeshwa katika kazi za mwanadamu. Kwa hiyo inakuwa dhahiri kupitia kazi inayofanywa iwapo jambo fulani ni maonyesho ya Mungu ama maonyesho ya mwanadamu. Halihitaji kufafanuliwa na Mungu Mwenyewe, wala halihitaji mwanadamu ajitahidi kushuhudia; aidha, halimhitaji Mungu Mwenyewe kumkandamiza mtu yoyote. Yote haya yanakuja kama ufunuo wa kawaida; hayalazimishwi wala silo jambo ambalo mwanadamu anaweza kuingilia kati. Wajibu wa mwanadamu unaweza kujulikana kupitia uzoefu wake, na hauhitaji watu wafanye kazi yoyote ya ziada inayohusu uzoefu wao. Nafsi yote ya mwanadamu inaweza kufichuliwa wakati anapotimiza wajibu wake, wakati Mungu anaweza kuonyesha tabia Yake ya asili anapotekeleza kazi Yake. Ikiwa ni kazi ya mwanadamu basi haiwezi kufichika. Ikiwa ni kazi ya Mungu, basi haiwezekani hata zaidi kwa tabia ya Mungu kufichwa na yeyote, sembuse kudhibitiwa na mwanadamu. Hakuna mwanadamu anayeweza kusemekana kuwa Mungu, wala kazi na maneno yake kuonekana kuwa matakatifu ama kuchukuliwa kuwa yasiyobadilika. Mungu anaweza kusemekana kuwa mwanadamu kwa sababu Amejivika mwili, lakini kazi Yake haiwezi kuchukuliwa kuwa kazi ya mwanadamu ama wajibu wa mwanadamu. Aidha, matamshi ya Mungu na nyaraka za Paulo hayawezi kulinganishwa, wala hukumu na kuadibu kwa Mungu na maneno ya mwanadamu ya kuagiza kuzungumziwa kuwa sawa. Kwa hiyo, kuna kanuni zinazotofautisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Zinatofautishwa kulingana na viini vyao, sio kwa upana wa kazi ama ustadi wake wa muda. Watu wengi hufanya makosa ya kanuni kuhusiana na hili. Hii ni kwa sababu mwanadamu anaangalia mambo ya nje, ambayo anaweza kutimiza, ilhali Mungu anaangalia kiini, ambacho hakiwezi kuonekana na macho ya mwanadamu. Ukichukulia maneno na kazi ya Mungu kama wajibu wa mtu wa kawaida, na kuona kazi kubwa ya mwanadamu kama kazi ya Mungu aliyejivika mwili badala ya wajibu ambao mwanadamu anatimiza, je, basi hujakosea kimsingi? Barua na wasifu wa mwanadamu vinaweza kuandikwa kwa urahisi, lakini kwa msingi tu wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hata hivyo, matamshi na kazi ya Mungu haviwezi kufanikishwa kwa urahisi na mwanadamu ama kutimizwa kwa hekima na fikira za binadamu, na watu hawawezi kuvieleza kikamilifu baada ya kuvichunguza. Masuala haya ya kimsingi yasipowaletea hisia yoyote, basi ni dhahiri kwamba imani yenu si ya kweli ama safi sana. Inaweza tu kusemekana kwamba imani yenu imejaa mashaka, na imekanganyikiwa na ni isiyo na maadili. Bila hata kuelewa masuala ya msingi kabisa ya Mungu na mwanadamu, je, imani kama hii haijakosa utambuzi kabisa? Paulo anawezaje kuwa mtu wa pekee aliyetumika katika historia yote? Anawezaje kuwa mtu wa pekee aliyewahi kulifanyia kanisa kazi? Anawezaje kuwa mtu wa pekee aliyeyaandikia makanisa kuwasaidia? Bila kujali ukubwa ama ushawishi wa kazi ya watu hawa, au hata matokeo ya kazi yao, je, si kanuni na dutu yote ya kazi kama hiyo ni sawa? Je, hakuna mambo kuihusu ambayo ni tofauti kabisa na kazi ya Mungu? Hata ingawa kuna tofauti dhahiri kati ya kila hatua ya kazi ya Mungu, na hata ingawa mbinu Zake nyingi za kazi si sawa kabisa, je, zote hazina asili na dutu moja tu? Kwa sababu hiyo, ikiwa mtu bado hajaelewa mambo haya sasa, basi hana mantiki hata kidogo. Baada ya kuyasoma maneno haya, mtu bado akisema kwamba barua za Paulo ni takatifu na zisizokiukwa na ni tofauti na wasifu wa mtu yeyote wa kiroho, basi mantiki ya mtu huyu si ya kawaida hata kidogo na mtu kama huyu bila shaka ni mtaalamu wa maandishi ambaye hana akili kabisa. Hata kama unampenda Paulo sana, huwezi kutumia hisia zako changamfu kwake kugeuza ukweli wa mambo ama kukanusha kuwepo kwa ukweli. Aidha, kile ambacho Nimesema hakitupilii mbali kazi na barua zote za Paulo hata kidogo ama kukana kabisa thamani yao kama marejeleo. Bila kujali chochote, nia Yangu ya kuzungumza maneno haya ni ili mpate ufahamu mzuri na makadirio ya kutosha ya mambo na watu wote: Hili pekee ndilo mantiki ya kawaida; ni hili tu ndilo watu wenye haki walio na ukweli wanapaswa kujitayarisha nalo.

Iliyotangulia: Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Inayofuata: Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp