Mtazamo Ambao Waumini Wanapaswa Kuwa Nao

Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepata tangu alipoanza kumwamini Mungu? Umekuja kujua nini kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako katika Mungu? Leo, ninyi nyote mnajua kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa nafsi na ustawi wa mwili pekee, wala si kwa ajili ya kutajirisha maisha yake kupitia kumpenda Mungu, na kadhalika. Kama hali ilivyo sasa, ukimpenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au raha ya muda mfupi, basi hata kama, mwishowe, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na hutaomba chochote zaidi, upendo huu unaoufuatilia bado ni upendo usio safi na usiompendeza Mungu. Wale wanaotumia kumpenda Mungu kutajirisha maisha yao yasiyovutia na kujaza pengo mioyoni mwao ni aina ya watu wanaotamani raha, si wale wanaotafuta kweli kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni wa kulazimishwa, ni ufuatiliaji wa raha ya kisaikolojia, na Mungu hauhitaji. Basi, upendo wako ni wa aina gani? Unampenda Mungu kwa ajili ya nini? Ni kiasi gani cha upendo wa kweli kwa Mungu ulio ndani yako sasa hivi? Upendo wa wengi wenu ni wa aina iliyotajwa hapo awali. Upendo kama huo unaweza tu kudumisha hali ilivyo; hauwezi kufikia hali ya kutobadilika, wala hauwezi kukita mizizi ndani ya mwanadamu. Upendo wa aina hii ni kama tu ua linalochanua na kunyauka bila kuzaa matunda. Yaani, baada ya kumpenda Mungu mara moja kwa njia kama hiyo, ikiwa hakuna mtu wa kukuongoza katika njia iliyo mbele, basi utaanguka. Ikiwa unaweza tu kumpenda Mungu wakati wa kumpenda Mungu lakini baadaye tabia yako ya maisha inabaki bila kubadilika, basi utabaki chini ya gubiko la ushawishi wa giza, usiweze kutoroka, na utabaki usiyeweza kujinasua kutoka katika utumwa wa Shetani na kutoka katika kudanganywa naye. Hakuna mtu kama huyu anayeweza kupatwa na Mungu kikamilifu; mwishowe, roho, nafsi, na mwili wake bado vitakuwa vya Shetani. Hakuwezi kuwa na shaka yoyote kuhusu hili. Wale wote wasioweza kupatwa na Mungu kikamilifu watarudi mahali pao pa asili, yaani, watarudi kwa Shetani, na watashuka kwenye ziwa la moto na kiberiti ili kupokea hatua inayofuata ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaopatwa na Mungu ni wale wanaoasi dhidi ya Shetani na kutoroka kutoka katika nguvu zake. Wanahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hapa ndipo ambapo watu wa ufalme wanatoka. Je, uko tayari kuwa mtu wa aina hii? Je, uko tayari kupatwa na Mungu? Je, uko tayari kutoroka kutoka katika nguvu za Shetani na kumrudia Mungu? Je, wewe sasa ni Shetani au wewe ni mmoja wa watu wa ufalme? Mambo haya tayari yanapaswa kuwa wazi, na hayahitaji maelezo zaidi.

Hapo zamani, wengi walifuatilia wakiwa na tamaa ya makuu na dhana, walifuatilia kwa sababu ya matumaini yao wenyewe. Hebu tuweke kando masuala kama hayo kwa sasa; kilicho cha muhimu sana sasa ni kupata njia ya utendaji itakayomwezesha kila mmoja wenu kudumisha hali ya kawaida mbele za Mungu na kujinasua polepole kutoka katika vifungo vya ushawishi wa Shetani, ili kwamba mweze kupatwa na Mungu, na kuishi kwa kukidhihirisha duniani kile ambacho Mungu anataka kwenu. Ni kwa njia hii pekee ndiyo mnaweza kuziridhisha nia za Mungu. Wengi wanamwamini Mungu, lakini hawajui kile ambacho Mungu anataka wala kile ambacho Shetani anataka. Wanaamini kwa njia ya kukanganyika, wakifuata mkondo wa mambo, na hivyo hawajawahi kuwa na maisha ya kawaida ya Kikristo; zaidi ya hayo, hawajawahi kuwa na mahusiano ya kawaida na watu, sembuse uhusiano wa kawaida na Mungu. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba matatizo na mapungufu ya mwanadamu, na mambo mengine yanayoweza kuzuia mapenzi ya Mungu, ni mengi. Hili linatosha kuthibitisha kwamba mwanadamu bado hajaingia katika njia sahihi ya imani katika Mungu, wala hajaingia katika upitiaji halisi wa maisha ya mwanadamu. Basi inamaanisha nini kuingia katika njia sahihi ya imani katika Mungu? Kuingia katika njia sahihi kunamaanisha kwamba unaweza kuutuliza moyo wako mbele za Mungu wakati wote na kushiriki katika ushirika wa kawaida na Mungu, ukija kujua polepole kile kinachokosekana ndani ya mwanadamu na polepole kumjua Mungu kwa kina zaidi. Kupitia hili, roho yako inapata ufahamu mpya na nuru mpya kila siku; shauku yako inakua, unatafuta kuingia katika ukweli, na kila siku kuna mwanga mpya na uelewa mpya. Kupitia njia hii, unajinasua polepole kutoka katika ushawishi wa Shetani na kukua katika uzima wako. Watu kama hao wameingia kwenye njia sahihi. Tathmini upitiaji wako halisi wewe mwenyewe na uchunguze njia ambayo umefuatilia katika imani yako: Unapolinganisha hayo na yale yaliyoelezwa hapo juu, je, unaona kuwa uko katika njia sahihi? Ni katika mambo gani ambayo umejinasua kutoka katika utumwa wa Shetani na kutoka katika ushawishi wa Shetani? Ikiwa bado hujaingia katika njia sahihi, basi uhusiano wako na Shetani haujakatwa. Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo, je, kutafuta kwako kumpenda Mungu kutakuongoza kuelekea upendo ambao ni wa kweli, wenye nia moja, na safi? Unasema kwamba upendo wako kwa Mungu ni thabiti na wa dhati, lakini bado hujajinasua kutoka katika utumwa wa Shetani. Je, hujaribu kumdanganya Mungu? Ukitaka kufikia hali ambayo upendo wako kwa Mungu haujachafuliwa, na unataka kupatwa na Mungu kikamilifu na kuhesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme, basi lazima kwanza ujiweke katika njia sahihi ya imani katika Mungu.

Iliyotangulia: Njia … (8)

Inayofuata: Kwenye Hatua za Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp