Swali la 3: Mbona Mungu amepata mwili katika siku za mwisho, akiwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu? Ni nini tofauti ya kweli kati ya mwili wa roho wa Bwana Yesu kufufuliwa kutoka kwa kifo na Mwana wa Adamu mwenye mwili? Hili ni suala ambalo hatulielewi—tafadhali shiriki ushirika kuhusu hili.

Jibu:

Wengi wa waumini huamini kwamba Bwana aliyerudi ataonekana kwao katika mwili Wake wa kiroho, yaani, mwili wa kiroho wa Bwana Yesu alioonekania kwa mwanadamu kwa siku arobaini baada ya kufufuka Kwake. Sisi waumini tunaelewa vizuri jambo hili. Juu juu, mwili wa kiroho wa Bwana Yesu baada yaYeye kufufuka unaonekana katika mfano sawa wa mwili Wake, lakini mwili wa kiroho hauzuiwi na ulimwengu yakinifu, anga, na mahali. Unaweza kuonekana na kutoweka upendavyo, ukimwacha mwanadamu ameshtuka na kushangaa. Maelezo ya hili yamerekodiwa katika Biblia. Kabla ya Bwana Yesu kusulubiwa, Alikuwa akizungumza na kufanya kazi katika ubinadamu wa kawaida wa mwili. Iwapo Alikuwa Anaonyesha ukweli, Anaingiliana na wanadamu, au Anafanya miujiza, wanadamu walihisi Alikuwa wa kawaida katika kila namna. Kile ambacho wanadamu waliona ni mwili huu ukifanya kazi kweli na kupitia mateso kweli na kulipa gharama. Mwishowe, ni mwili huu uliopigiliwa misumari msalabani kama dhabihu ya dhambu kwa mwanadamu, hivyo kukamilisha kazi ya Mungu ya ukombozi. Huu ni ukweli unaokubalika kwa kiasi kikubwa. Hebu fikiria kwa muda mfupi: Kama ungekuwa mwili wa kiroho wa Bwana Yesu unaofanya kazi, je, Angeweza kushirikiana na kuwa na mazungumzo ya kawaida na wanadamu? Angeweza kweli kupitia mateso na kulipa gharama? Angeweza kupigiliwa misumari msalabani? Hangeweza kufanya chochote kati ya hayo. Kama ungekuwa mwili Wake wa kiroho unaofanya kazi, je, sisi wanadamu tungeweza kuingiliana naye kwa urahisi? Tungezisaliti tabia zetu potovu? Tungeunda dhana kumhusu? Tungethubutu kumuasi na kumhukumu Mungu tupendavyo? Hilo halingewezekana! Wanadamu wote wamejaa ubinadamu wa kawaida, wote wanaweza kuzuiwa na ulimwengu yakinifu, anga, na mahali. Mchakato wa kufikiri kwa mwanadamu pia ni wa kawaida. Kama mwanadamu angekutana na kazi ya mwili wa kiroho, angeogopa na kushikwa na hofu kubwa. Mawazo yake yangegeuka kuwa yenye kichaa na wazimu. Akikabiliwa na aina hii ya hali, Mungu angeshinikizwa kutimiza ufanisi katika kazi Yake ya wokovu wa wanadamu. Kwa hivyo, matokeo yanayotimizwa kwa kufanya kazi ndani ya mipaka ya ubinadamu wa kawaida yanazidi mno yale ya ndani ya mwili wa kiroho. Kotekote katika enzi, wateule wa Mungu hawajawahi kupitia kazi ya mwili wa Mungu wa kiroho. Haingeifaa hakika kwa mwili wa kiroho kuonyesha ukweli moja kwa moja, kuingiliana na watu na kulichunga kanisa.

Kazi ya hukumu ambayo kuja kwa Mungu mara ya pili kunatimiza katika siku za mwisho inatumia onyesho la neno kumtakasa, kumwokoa, na kumkamilisha mwanadamu, lengo lake pia ni kuwafichua na kuwaondoa wanadamu, kumwainisha mwanadamu, kila mmoja katika aina yake mwenyewe, na kisha kutuza wema huku ikiadhibu waovu. Kama Mungu angeonekana kwa mwanadamu katika umbo la mwili Wake wa kiroho, wanadamu wote, wema au waovu, wangejiangusha chini mbele Zake, basi Angetengaje wema kutoka kwa waovu? Pia, kama Mungu angeonekana katika mwili Wake wa kiroho, mwanadamu angeingia katika hofu kubwa, na vurugu ingefoka kotekote ulimwenguni. Kama ingelikuwa hivyo, Mungu angeendeleaje kwa kawaida kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho? Pia, ni vipi ambavyo Mungu angeweza kutimiza mpango Wake wa kukikamilisha kikundi cha wanadamu ambao wanapatana na mapenzi ya Mungu kabla ya maafa? Kwa hiyo, katika siku za mwisho, Mungu bado lazima achukue mwili kama Mwana wa Adamu na ubinadamu wa kawaida. Ni kwa namna hii pekee ndipo Anaweza kufanya kazi na kuishi miongoni mwa ulimwengu wa binadamu. na ni namna hii pekee ndipo Anaweza kuonyesha ukweli na kuhukumu, kumtakasa mwanadamu katika njia halisi ili wanadamu waweze kupokonywa kutoka kwa ushawishi wa Shetani, waokolewa na Mungu, na wawe watu wa Mungu. Bwana Yesu mwenye mwili Alifanya kazi ndani ya ubinadamu wa kawaida kutimiza ukombozi wa wanadamu. Mwili wa kiroho wa Bwana Yesu uliofufuka ulionekana kwa mwanadamu ili kuthibitisha tu kwamba Bwana Yesu alikuwa kupata mwili kwa Mungu. Hili lilifanywa kuimarisha imani ya mwanadamu. Kwa hiyo, mwili wa kiroho wa Mungu ulikuja tu kuonekana kwa mwanadamu, sio kufanya kazi. Mwili wa Mungu lazima uwe na ubinadamu wa kawaida ili uweze kufanya kazi miongoni mwa wanadamu na utimize ukombozi na wokovu wa wanadamu. Kwa hiyo, kama Mungu anataka kuwaokoa wanadamu kabisa katika kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lazima Apate mwili na Afanye kazi Yake katika ubindamu wa kawaida kutimiza matokeo bora zaidi. Bila shaka Hataonekana kwa mwanadamu kama mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Hili ni jambo ambalo sisi, waumini, sote tunapaswa kulielewa vizuri.

…………

… Licha ya ukweli kwamba mwili wa kiroho wa Bwana Yesu unaweza kuonekana kwa mwanadamu na kuonana nao uso kwa uso, mwili wa kiroho bado unaonekana wa siri kwa kutofahamika, Anachochea woga na hofu ndani ya mioyo yao na kuwasababisha kudumisha umbali wenye heshima. Kwa kuwa mwili wa kiroho wa Bwana Yesu hauwezi kuingiliana na mwanadamu kwa kawaida na Hawezi kutekeleza kazi na kunena kwa kawaida miongoni mwa wanadamu, kwa hivyo Hawezi kuwaokoa wanadamu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti. Anaweza kuingiliana na mwanadamu katika namna halisi na ya kweli. Anaweza kumnyunyizia na kumruzuku mwanadamu, kama tu vile Bwana Yesu, Akiishi pamoja na wanadamu, Aliweza kuonyesha ukweli kumruzuku mwanadamu, wakati wowote na mahali popote. Wanafunzi wake waliketi naye mara nyingi, wakisikiliza mafundisho Yake na wakiwa na majadiliana ya dhati naye. Walipokea kunyunyizia na uchungaji Wake moja kwa moja. Matatizo au ugumu wowote waliokabiliana nao, Bwana Yesu aliwasaidia kutatua. Walijaliwa kiwango kikubwa sana cha ruzuku ya maisha. Walimwona Mungu kuwa mwema na wa kupendeza. Kwa sababu hii, waliweza kweli kumpenda na kumtii Mungu. Mara tu kupata mwili kwa Mungu anapokuja ndani ya ulimwengu wa mwanadamu ndipo tunapata nafasi ya kuingiliana naye, kuzoea na kumjua Mungu. Ni wakati huo tu ndipo tunaweza kuona ajabu na hekima na wokovu halisi wa Mungu wa wanadamu kwa macho yetu wenyewe. Hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu na thamani halisi ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwili wa kiroho hauwezi kabisa kuyatimiza matokeo haya.

Ushirika huu umeufanya ukweli mmoja kueleweka vizuri sana kwetu. Ni kwa kupata mwili tu kama Mwana wa Adamu na kufanya kazi katika ubinadamu wa kawaida ndipo Mungu anaweza kumhukumu, kumshinda na kumtakasa mwanadamu kwa uhalisi. Mwili wa kiroho wa Bwana Yesu haungeweza kutimiza takriban matokeo kama hayo katika kazi Yake. Kwanza, Mungu anapopata mwili kama Mwana wa Adamu kufanya kazi ya hukumu na utakaso miongoni mwa wanadamu, sisi wanadamu tutamchukulia Mungu kama mwanadamu wa kawaida kwa kuwa bado hatujabainisha kupata mwili kwa Mungu ni nani kweli. Hata tutaunda fikira kuhusu neno na kazi ya Mungu, tutamtendea Kristo bila heshima na kukataa kumtii. Tutanena uwongo kumdanganya, tutahukumu na hata kumpinga na kumshutumu. Kiburi, uasi, na upinzani wetu wanadamu utaonekana kwa ukamilifu mbele za Kristo. Kama tu anavyosema Mwenyezi Mungu: “Tabia potovu na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu kwa hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu—Mwana wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida—kwamba mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu hufichuliwa kikamilifu na kwa uwazi sana. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Huku kunaitwa ‘kumvuta chui mkubwa kutoka mlimani’ na ‘kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni pake’(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu). Mungu huwahukumu, huwafichua, huwapogoa na kuwashughulikia wanadamu kulingana na uhalisi wenye ukweli wa uasi na upinzani wao. Kazi ya Mungu ni halisi kweli na hufichua kweli wanadamu kwa kile walicho. Wanapokabiliwa na ushahidi kama huo wenye ukweli, wale ambao wanaweza kuukubali ukweli wataridhishwa kabisa na watakubali uasi na upinzani wao wenyewe. Pia watafahamu tabia ya Mungu takatifu, yenye haki na isiyokosewa. na wataweza kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa unyenyekevu, ili waweze kushindwa na kuokolewa na kazi halisi ya Mungu. Kama tu anavyosema Mwenyezi Mungu: “Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, bali hatua kwa hatua tu atamwelewa taratibu kupitia neno la mdomo Wake, ametwaliwa na Yeye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili). Kwa hiyo, mwanadamu atatakaswa na kuokolewa kabisa tu kama ni kupata mwili kwa Mungu ambaye Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: Swali la 2: Ingawa wale wanaomwamini Bwana wanajua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, watu wachache sana wanaelewa ukweli wa kupata mwili. Wakati ambapo Bwana atarudi, Akionekana tu kama Bwana Yesu alivyofanya, akiwa Mwana wa Adamu na kufanya kazi, watu kweli hawatakuwa na njia ya kumtambua Bwana Yesu na kukaribisha kurudi Kwake. Kwa hiyo kupata mwili kweli ni nini? Ni nini kiini cha kupata mwili?

Inayofuata: Swali la 4: Katika Enzi ya Sheria, Mungu alimtumia Musa kutenda kazi Yake, hivyo kwa nini Mungu hamtumi mtu kutekeleza kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lakini Mungu mwenye mwili Mwenyewe lazima aifanye?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp