93 Katika Enzi ya Ufalme, Neno Linatimiza Kila Kitu

1 Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno.

2 Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno "maneno" linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana.

3 Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi.

Umetoholewa kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 92 Katika Siku za Mwisho, Mungu Anatimiza Yote Kupitia Maneno Yake

Inayofuata: 94 Katika enzi ya Ufalme Mungu Anakamilisha Mwanadamu Kwa Maneno

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp