Kazi na Kuingia (10)

Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu. Kazi ya Mungu imefikia upeo wake—na, kufuatia, “kuingia” kwa mwanadamu[1] pia kumefikia kilele chake. Mungu amejishusha kwa kadiri Anavyoweza, na kamwe Hajawahi kuwalalamikia wanadamu au kwa ulimwengu na vitu vyote. Mwanadamu, wakati ule ule, anasimama juu ya kichwa cha Mungu, akimnyanyasa hadi kilele; yote yamefikia kilele chake, ni wakati wa siku ambapo haki inaonekana. Kwa nini uendelee kuacha huzuni iifunike nchi, na giza kuwavaa watu wote? Mungu ameangalia kwa miaka elfu kadhaa—kwa makumi ya maelfu ya miaka, hata—na uvumilivu Wake umekwisha kufikia kikomo chake. Amekuwa akiangalia kila hatua za wanadamu, Amekuwa akiangalia kwa makini jinsi udhalimu wa mwanadamu utafanya fujo, na bado mwanadamu, ambaye amekuwa wa kutojali kwa muda mrefu, hahisi chochote. Na ni nani aliyewahi kuangalia kwa makini matendo ya Mungu? Nani aliyewahi kuinua macho yake na kutazama mbali sana? Nani aliyewahi kusikiliza kwa makini? Nani aliyewahi kuwa mikononi mwa Mwenyezi? Watu wote wanakerwa na hofu za kubuni[2]. Je, kuna faida gani kwa rundo la nyasi kavu na majani makavu? Kitu pekee wanachoweza kufanya ni kumtesa Mungumwenye mwili hadi kifo. Ingawa wao ni mafungu tu ya nyasi kavu na majani makavu, bado kuna kitu kimoja ambacho wao hufanya “bora zaidi”:[3] kumtesa Mungu hadi kifo na kisha kulia kwamba “hilo hufurahisha mioyo ya watu.” Kikundi cha jeshi lisilofaa kabisa! La ajabu, katikati ya mkondo usiokwisha wa watu, wao hulenga uangalifu wao juu ya Mungu, wakimzunguka Yeye na zingio lisilopenyeka. Hamasa yao daima ikiwaka moto zaidi,[4] wamemzunguka Mungu katika vikundi, ili Asiweze kusonga hata kidogo. Katika mikono yao, wanashikilia kila aina ya silaha, na kumtazama Mungu kana kwamba wanamwangalia adui, macho yao yakiwa yamejaa hasira; wana hamu ya “kumshambulia Mungu kwa nguvu.” Inafaidi kweli: Kwa nini mwanadamu na Mungu wamekuwa maadui wasioweza kupatanishwa? Inawezekana kwamba kuna chuki ya muda mrefu sana kati ya Mungu wa upendo sana na mwanadamu? Inawezekana kwamba matendo ya Mungu hayana faida kwa mwanadamu? Je, hayo humdhuru mwanadamu? Mtu hulenga jicho la hasira lisiloyumba juu ya Mungu, akiogopa sana kwamba Atapasua zingio la mwanadamu, Arudi mpaka mbingu ya tatu, na mara nyingine tena Amtupe mwanadamu ndani ya gereza. Mwanadamu anajihadhari na Mungu, yeye ni mwenye wasiwasi, na hufurukuta toka upande mmoja hadi upande mwingine wa ardhi kwa mbali, akishikilia “bombomu” ambayo inamlenga Mungu kati ya wanadamu. Ni kana kwamba, Mungu akijitikisa kidogo tu, mwanadamu atafuta kila kitu Chake—mwili Wake wote na yote Anayovaa—bila kuacha kitu chochote. Uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu hauwezi kurekebishwa. Mungu haeleweki kwa mwanadamu; mwanadamu, wakati ule ule, huyafunga macho yake kwa makusudi na kuchezacheza, asiyetaka kabisa kuona kuwepo Kwangu, na kutosamehe hukumu Yangu. Hivyo, wakati mtu hatarajii, Mimi huondoka kimya kimya, na Sitaweza tena kulinganisha nani aliye juu na nani aliye chini na mwanadamu. Wanadamu ni “wanyama” wa chini zaidi kuliko wote na Sitamani kumsikiliza tena. Kwa muda mrefu Nimerudisha neema Yangu yote mahali ambapo Mimi hukaa kwa amani; kwa kuwa mwanadamu ni mkaidi sana, ana sababu gani kufurahia zaidi neema Yangu ya thamani mno? Mimi siko tayari kutoa neema Yangu bure juu ya nguvu zilizo na uhasama Kwangu. Ningetoa matunda Yangu ya thamani juu ya wale wakulima wa Kanaani ambao ni wenye ari, na wanakaribisha kwa dhati kurudi Kwangu. Napenda tu mbingu ziendelee milele, na, zaidi ya hayo, mwanadamu asizeeke kamwe, mbingu na mwanadamu viwe vitulivu daima, na ile “misonobari na mivinje” iliyo na rangi ya kijani daima iandamane na Mungu, na daima iandamane na mbingu katika kuingia kwenye enzi kamilifu pamoja.

Nimetumia siku nyingi kuwa na mwanadamu, Nimeishi duniani pamoja na mwanadamu, na Sijawahi kutaka vitu zaidi kutoka kwa mwanadamu, Ninamwongoza tu mwanadamu kusonga mbele, Sifanyi chochote bali kumwongoza mwanadamu, na kwa ajili ya hatima ya binadamu, bila kuchoka Nafanya kazi ya kupangilia. Nani ambaye amewahi kuelewa mapenzi ya Baba wa mbinguni? Nani amewahi kusafiri kati ya mbingu na dunia? Sitamani kuishi tena na mwanadamu katika “uzee” wake, kwani mwanadamu ni “wa mtindo wa zamani sana,” hajui chochote; kitu pekee anachojua ni kula na kuvimbiwa kwenye sherehe Niliyoandaa, amejitenga na yote, hafikirii suala jingine lolote lile. Binadamu anateseka sana, makelele, huzuni, na hatari miongoni mwa wanadamu ni kubwa sana, na hivyo Natamani nisiwashirikishe matunda ya thamani ya kupata ushindi wakati wa siku za mwisho. Acha mwanadamu afurahie baraka tele ambazo ametengeneza mwenyewe, maana mwanadamu hanikaribishi—kwa nini Nimshurutishe binadamu kulazimisha tabasamu? Kila pembe ya dunia haina joto, hakuna hata chembe ya chemchemi katika ardhi yote ya nchi, maana, hana joto hata kidogo kama mnyama aishiye majini, ni kama maiti, na hata damu inayopita katika mishipa yake ni kama barafu iliyoganda inayofanya moyo kuwa baridi. Wema upo wapi? Mwanadamu alimsulubisha Mungu msalabani bila sababu yoyote, na baadaye hakuhisi wasiwasi wowote. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na majuto, na madikteta hawa makatili bado wanapanga “kumkamata Akiwa hai”[5] Mwana wa Adamu kwa mara nyingine na kumleta mbele ya kikosi cha kufyatua risasi, kukomesha chuki ndani ya mioyo yao. Kuna faida gani Kwangu, kubaki katika nchi hii ya hatari? Ikiwa Nitabaki, kitu pekee Nitakachomletea mwanadamu ni mgogoro na fujo, na hakutakuwa na mwisho wa shida, maana Sijawahi kumpatia mwanadamu amani, ni vita tu. Siku za mwisho za binadamu lazima zijae vita, na hatima ya mwanadamu lazima ipinduliwe katikati ya vurugu na migogoro. Na Sipo tayari kushiriki katika “furaha” ya vita, Sitaunga mkono umwagaji wa damu na mwanadamu kujitoa mhanga, maana kukataliwa na mwanadamu kumenipeleka katika hali ya kukata tamaa, na Sina moyo wa kuangalia vita vya mwanadamu—hebu mwanadamu apigane kuuridhisha moyo wake, Natamani kupumzika, Nataka kulala, acha mapepo wawe washirika wa binadamu wakati wa siku zao za mwisho! Nani ajuaye mapenzi Yangu? Kwa sababu Sijakaribishwa na mwanadamu, na hajawahi kunisubiri, Ninaweza tu kumuaga, na kumkabidhi hatima yake, na kumwachia mwanadamu utajiri Wangu wote, na kupanda maisha Yangu ndani yake, kupanda mbegu ya maisha Yangu ndani ya shamba la moyo wa mwanadamu, na kumwachia kumbukumbu za milele, Ninaweza kuacha tu upendo Wangu wote kwa binadamu, kumwachia yote ambayo mwanadamu anafurahia Kwangu, kama zawadi ya upendo ambayo tunaitamani iwe kwa kila mmoja. Ningependa tupendane milele, kwamba jana yetu iwe kitu kizuri sana tunachopeana, maana Nimejitoa kikamilifu kwa binadamu—ni malalamiko gani ambayo mwanadamu anaweza kuwa nayo? Tayari Nimeyaacha maisha Yangu yote kwa mwanadamu, na bila neno lolote, Nimetokwa jasho kwa kulima “ardhi nzuri ya upendo” kwa ajili ya binadamu; Sijafanya matakwa yoyote linganifu kwa mwanadamu, na Sijafanya chochote isipokuwa kujitiisha katika mipangilio ya mwanadamu na kutengeneza kesho nzuri zaidi ya binadamu.

Ingawa kazi ya Mungu ni yenye ukwasi na maridhawa, kuingia kwa mwanadamu kuna upungufu sana. Kwa “shughuli” ya pamoja kati ya mwanadamu na Mungu, karibu yote ni kazi ya Mungu; kuhusu kiasi gani mwanadamu ameingia, hana ushahidi wa chochote alichopata Mwanadamu, ambaye amechakaa sana na ni kipofu, hata hutathmini nguvu zake dhidi ya Mungu wa leo na “silaha za kale” mikononi mwake. Hawa “sokwe wa kale” huweza kutembea wima kwa shida, na hawaoni aibu katika miili yao iliyo “uchi.” Ni nini kinawastahilisha kutathmini kazi ya Mungu? Macho ya wengi wa sokwe hawa wa miguu minne hujaa ghadhabu, nao hujipambanisha na Mungu kwa silaha za kale za mawe mikononi mwao, wakijaribu kuanzisha mashindano ya sokwe watu ambao dunia haijawahi kuwaona kamwe hapo awali, kuwa na mashindano ya siku za mwisho kati ya sokwe watu na Mungu ambayo yatakuwa maarufu duniani kote. Wengi wa sokwe watu hawa walio nusu wima, zaidi ya hayo, hufurikwa na ridhaa. Nywele zikiwa zimefunika nyuso zao zilizofungamana, wamejaa nia ya kuua na huinua miguu yao ya mbele. Bado hawajageuka kwa ukamilifu kuwa mtu wa kisasa, kwa hiyo wakati mwingine wao husimama wima, na wakati mwingine wao hutambaa, shanga za jasho zikifunika paji la nyuso zao kama matone ya umande yaliyo karibu karibu, hamu yao ni dhahiri. Ukimwangalia sokwe mtu, wa asili, rafiki yake, akiwa amesimama kwa miguu yote minne, miguu yake minne ikiwa mikubwa na ya mwendo wa polepole, inayoweza kukwepa mapigo kwa shida na bila nguvu ya kupigana, anajizuia kwa shida. Kufumba na kufumbua—kabla ya kuwa na wakati wa kuona nini kilichotokea—“shujaa” katika ulingo huanguka chini ghafula, miguu ikiwa hewani. Miguu hiyo, iliyokaa vibaya juu ya ardhi kwa miaka yote hiyo, ghafula imegeuzwa juu chini, na sokwe mtu huyo hana tena hamu ya kupinga. Kuanzia wakati huu kuendelea, sokwe mtu kati ya sokwe watu wa kale zaidi anaondolewa kutoka kwenye uso wa dunia—ni la “kuhuzunisha” kweli. Huyu sokwe mtu wa kale alifikia mwisho wa ghafla. Kwa nini alikuwa na haraka kutoka katika ulimwengu wa ajabu wa mwanadamu mapema hivyo? Kwa nini hakuzungumzia hatua inayofuata ya mkakati na wenzake? Inasikitisha kwamba aliuaga ulimwengu bila kuacha siri ya kutathmini nguvu za mtu dhidi ya Mungu! Haikuwa busara kwa sokwe mtu huyo mzee kufa bila kunong’ona, kuondoka bila kupitisha “utamaduni wa kale na sanaa” kwa dhuria zake. Hakukuwa na wakati wa kuwaita wale walio karibu naye ubavuni mwake kuwaambia juu ya upendo wake, hakuacha ujumbe juu ya kibao cha mawe cha kuandikia, hakutambua jua la mbingu, wala hakusema chochote juu ya shida zake zisizoweza kuzungumziwa. Alipokuwa akipumua pumzi yake ya mwisho, hakuwaita wazao wake ubavuni pa mwili wake uliokuwa ukifa kuwaambia “msiingie ndani ya ulingo ili kumpinga Mungu” kabla ya kufumba macho yake, miguu minne migumu ikijitokeza juu daima kama matawi ya mti ikielekeza angani. Ingeonekana alikufa kifo cha uchungu.... Ghafla, kicheko cha kunguruma kinafoka kutoka chini ya ulingo; mmoja wa sokwe watu aliye nusu wima aliyejizuzua; akiwa ameshika “kigongo cha mawe” cha kuwinda paa au wanyama wengine wa mwitu kilichoendelea zaidi kuliko kile cha sokwe mtu wa kale, anaruka ndani ya ulingo, akiwa amejawa na hasira, akiwa na mpango alioufikiria kwa makini katika akili yake.[6] Ni kana kwamba amefanya kitu chenye kustahili. Kwa kutumia “nguvu” ya kigongo chake cha mawe anafanikiwa kusimama wima kwa “dakika tatu.” Ajabu jinsi “nguvu” ya huu “mguu” wa tatu ilivyo kuu! Alimshikilia sokwe mtu mkubwa, goigoi, mpumbavu aliye nusu wima akisimama kwa dakika tatu—si ajabu sokwe mtu huyu mzee wa kuheshimiwa[7] ni jeuri sana. Kwa kweli, kifaa cha jiwe cha kale “kilikuwa kizuri kama sifa zake”: Kuna mpini wa kisu, makali, na ncha, dosari pekee ni ukosefu wa mng’aro kuelekea ukingo—jinsi hilo linavyosikitisha. Tazama tena “shujaa mdogo” wa nyakati za kale, aliyesimama ulingoni akiwaangalia wale walio chini na kuwakazia macho kwa dharau, kana kwamba wao ni wadhaifu walio duni, na yeye ni shujaa hodari. Katika moyo wake, anawachukia kwa siri wale walio mbele ya jukwaa. “Nchi iko taabani na kila mmoja wetu anawajibika, kwa nini mnaepa? Inawezekana kuwa ninyi mnaona nchi inakabiliwa na maangamizi, lakini hamshiriki katika vita vikali? Nchi inakaribia kuangamizwa—kwa nini ninyi sio wa kwanza kushughulika, na wa mwisho kujifurahisha? Mnawezaje kusimama na kuiangalia nchi ikianguka na watu wake wakianguka katika uozo? Je, mko tayari kubeba aibu ya kutiishwa kwa taifa? Kikundi cha vinyangarika kweli!” Anapofikiria hili, ghasia zinatokea mbele ya jukwaa na macho yake yanakasirishwa hata zaidi, kana kwamba karibu kutupa[8] miale. Ana hamu ya Mungu kushindwa kabla ya vita, akiwa tayari kufanya lolote kumuua Mungu ili awafurahishe watu. Hajui hata kidogo kwamba, ingawa kifaa chake cha jiwe kinaweza kuwa cha sifa inayostahili, hakiwezi kamwe kumchokoza Mungu. Kabla hajapata wakati wa kujikinga, kabla hajapata wakati wa kulala chini na kusimama, anayumba nyuma na mbele, uwezo wa kuona umepotea kutoka kwa macho yote. Anaanguka chini ghafula kwa babu yake wa zamani na hainuki tena; akimshikilia kwa nguvu sokwe mtu wa kale, halii tena, na anakubali udhalili wake, hana tena tamaa yoyote ya kupinga. Sokwe watu hao wawili maskini wanakufa mbele ya ulingo. Ni jambo la kusikitisha kwamba mababu za wanadamu, ambao wamenusurika hadi siku hii, walikufa kijinga katika siku ambayo Jua la haki lilionekana! Ni upumbavu ulioje kuwa wameiacha baraka kubwa sana kama hiyo kuwapita—kwamba, katika siku ya baraka yao, sokwe watu ambao wamengoja kwa maelfu ya miaka wamepeleka baraka Kuzimu ili “kufurahia” na mfalme wa pepo! Kwa nini wasiweke baraka hizi katika ulimwengu wa walio hai ili wafurahie na wana na binti zao? Wanatafuta tu shida! Huku ni kupoteza tu kwamba, kwa ajili ya hadhi ndogo, sifa, na ubatili, wanateseka kwa kuchinjwa, kung’ang’ana kuwa wa kwanza kufungua milango ya jahanamu na kuwa wana wake. Gharama kama hiyo si lazima. Inasikitisha mababu wa zamani kama hao, waliokuwa “wamejawa sana na roho ya kitaifa,” wangekuwa “wakali sana kwao wenyewe lakini wenye kuwavumilia wengine sana,” wakijifungia jahanamu, na kuwafungia wale dhaifu walio duni nje. Ni wapi ambako “wawakilishi wa watu” kama hawa wanaweza kupatikana? Kwa ajili ya “ustawi wa uzao wao” na “maisha ya amani ya vizazi vijavyo,” hawamruhusu Mungu kuingilia kati, na hivyo hawatilii maanani maisha yao wenyewe. Bila kujizuia, wanajitolea kwa “kusudi la kitaifa,” kuingia Kuzimu bila kusema lolote. Utaifa kama huo unaweza kupatikana wapi? Wakipigana na Mungu, hawaogopi kifo, wala kumwaga damu, seuze kuwa na wasiwasi kuhusu kesho. Wanakwenda tu kwenye uwanja wa vita. Inasikitisha kwamba kitu pekee wanachopata kwa “roho yao ya kujitolea” ni majuto ya milele, na kuteketezwa na moto wa kuzimu uwakao milele!

Jinsi inavyovutia! Kwa nini kupata mwili kwa Mungu daima kumekataliwa na kushutumiwa na watu? Kwa nini watu hawawi na ufahamu wowote wa kupata mwili kwa Mungu kamwe? Inawezekana kuwa Mungu amekuja wakati mbaya? Inawezekana kuwa Mungu amekuja mahali pabaya? Inawezekana kwamba hili hutokea kwa sababu Mungu ametenda peke yake, bila “sahihi” ya mwanadamu? Inawezekana ni kwa sababu Mungu alifanya maamuzi Yake Mwenyewe bila ruhusa ya mwanadamu? Ukweli unasema kwamba Mungu alitoa taarifa ya awali. Mungu hakufanya makosa kuwa mwili—je, Anahitaji kuomba idhini ya mwanadamu? Zaidi ya hayo, Mungu alimkumbusha mwanadamu zamani, labda watu wamesahau. Hawapaswi kulaumiwa, kwa kuwa mwanadamu kwa muda mrefu amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hawezi kuelewa chochote kinachoendelea chini ya mbingu, sembuse matukio ya ulimwengu wa kiroho! Ni aibu iliyoje kwamba mababu wa mwanadamu, sokwe watu, walikufa katika ulingo, lakini hili halishangazi: Mbingu na dunia hazijawahi kulingana, na ni jinsi gani sokwe watu, ambao akili zao zimetengenezwa kwa mawe, wangeweza kudhani kwamba Mungu angeweza kupata mwili tena? Ni jambo la kusikitisha kwamba “mtu mzee” kama huyu ambaye yuko kwenye “miaka yake ya sitini” alikufa katika siku ya kuonekana kwa Mungu. Je, si jambo la kushangaza kwamba aliuacha ulimwengu bila baraka katika ujio wa baraka kubwa kama hiyo? Hali ya Mungu kupata mwili imesababisha mawimbi mazito katika dini na madhehebu yote, “imeparaganya” mpangilio wa awali wa jamii ya kidini, na imetikisa mioyo ya wale wanaotamani sana kujitokeza kwa Mungu. Ni nani asiyeabudu? Nani hatamani kumwona Mungu? Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi sana, lakini mwanadamu kamwe hajawahi kutambua. Leo, Mungu Mwenyewe amejitokeza, na Ameonyesha utambulisho Wake kwa watu—inawezekanaje hii isiupatie moyo wa mwanadamu furaha? Mungu aliwahi kushiriki furaha na huzuni pamoja na mwanadamu, na leo Ameunganika tena na mwanadamu, na kushiriki visa vya muda uliopita pamoja naye. Baada ya kutoka Uyahudi, watu hawakuweza kupata alama Yake yoyote. Wanatamani kukutana tena na Mungu, bila kujua kwamba leo wamekutana Naye tena, na kuungana Naye tena. Inawezekanaje hii isiamshe mawazo ya jana? Siku kama ya leo miaka elfu mbili iliyopita, Simoni mwana wa Yona, uzao wa Wayahudi, alimtazama Yesu Mwokozi, alikula meza moja pamoja Naye, na baada ya kumfuata kwa miaka mingi alihisi kumpenda sana: Alimpenda sana kwa dhati, alimpenda sana Bwana Yesu. Watu wa Uyahudi hawakujua chochote kuhusu vile mtoto huyu mwenye nywele za dhahabu, Aliyezaliwa katika hori la ng’ombe, Alikuwa ni sura ya kwanza ya Mungu kupata mwili. Wote walidhani kwamba Alikuwa ni mmoja wao, hakuna aliyedhani kwamba Yupo tofauti nao—watu wangewezaje kumtambua Yesu wa desturi na wa kawaida kabisa? Watu wa Uyahudi walidhani kwamba alikuwa ni mtoto wa Kiyahudi wa wakati huo. Hakuna aliyemtazama kama Mungu mwenye upendo, na watu hawakufanya chochote isipokuwa kufanya maombi bila kutambua, wakiomba Awape neema nyingi na maradufu, na amani, na furaha. Walijua tu kwamba, kama milionea, Alikuwa na kila kitu ambacho mtu angetamani kuwa nacho. Lakini watu hawakumchukulia kama mtu ambaye Alikuwa mpendwa; watu wa wakati huo hawakumpenda, na walimpinga tu, na walifanya maombi Kwake yasiyokuwa na mantiki, na Hakuwahi kupinga, Aliendelea kutoa neema kwa mwanadamu, ingawa mwanadamu hakumjua. Hakufanya chochote isipokuwa kwa kimya kumpatia mwanadamu wema, upendo, na huruma, na zaidi, Alimpatia mwanadamu njia mpya ya kutenda, kumwongoza mwanadamu kutoka katika vifungo vya sheria. Mwanadamu hakumpenda, alimhusudu tu na kutambua “talanta Zake za kipekee.” Inawezekanaje mwanadamu kipofu kujua jinsi Yesu Mwokozi alipitia mateso makubwa Alipokuja miongoni mwa wanadamu? Hakuna aliyejali shida Zake, hakuna mtu aliyejua upendo Wake kwa Mungu Baba, na hakuna ambaye angejua upweke Wake; ingawa Maria alikuwa mama Yake wa kumzaa, angewezaje kujua mawazo yaliyopo moyoni mwa Bwana Yesu mwenye huruma? Nani alijua mateso yasiyoweza kutamkika Aliyoyapitia Mwana wa Adamu? Baada ya kumwomba watu wa kipindi hicho walimweka nyuma ya akili zao, na kumtupa nje Akizungukazunguka mitaani, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, na kwenda bila mwelekeo kwa miaka mingi hadi Alipofikisha miaka thelathini na mitatu, miaka ambayo ilikuwa mirefu pia mifupi. Watu walipomhitaji, walimwalika nyumbani mwao wakiwa na nyuso za tabasamu, wakijaribu kumwomba kitu—na baada ya kuwa Ametoa mchango wake kwao, walimsukuma mara moja nje ya mlango. Watu walikula kile Alichokitoa mdomoni Mwake, walikunywa damu Yake, walifurahia neema Aliyowapatia, lakini bado walimpinga, maana hawakujua nani aliwapa uhai walionao. Hatimaye, walimsulubisha msalabani, lakini bado Hakutoa hata sauti. Hata leo, bado Anabakia kimya. Watu wanakula mwili Wake, wanakunywa damu Yake, wanakula chakula Anachowatengenezea, na wanapita njia Aliyofungua kwa ajili yao, lakini bado wanakusudia kumkataa, kimsingi wanamchukulia Mungu ambaye Amewapatia maisha yao kama adui, na badala yake wanawachukulia wale ambao ni watumwa kama wao kama Anavyofanya Baba wa mbinguni. Katika hili, je, hawampingi kwa makusudi? Yesu aliwezaje kufa msalabani? Je, mnajua? Je, Hakusalitiwa na Yuda, ambaye alikuwa karibu kabisa Naye, na akamla, akamnywa, na akamfurahia? Je, Yuda hakumsaliti Yesu kwa sababu Alikuwa tu mwalimu wa kawaida Asiye na umuhimu? Ikiwa watu walikuwa wameona kwamba Yesu alikuwa si wa kawaida kabisa, na Ambaye Alitoka mbinguni, wangewezaje kumsulubisha msalabani Akiwa hai kwa masaa ishirini na nne, hadi Alipoishiwa na pumzi yote katika mwili wake? Nani awezaye kumjua Mungu? Watu hawafanyi chochote isipokuwa kumfurahia Mungu kwa tamaa isiyotosheka, lakini hawajawahi kumjua. Walipewa inchi na wamechukua maili, na wanamfanya “Yesu” kutii kabisa amri zao, na maelekezo yao. Ni nani ambaye ameonyesha huruma kwa huyu Mwana wa Adamu, Ambaye hana mahali pa kuweka kichwa Chake? Ni nani ambaye amewahi kufikiria kushikana mikono Naye kukamilisha agizo la Mungu Baba? Ni nani amewahi kumuwaza? Ni nani mbaye amewahi kuyajali matatizo Yake? Bila upendo hata kidogo, mwanadamu anamvuta nyuma na mbele; mwanadamu hajui nuru na uhai wake unatoka wapi na hafanyi chochote isipokuwa kupanga kwa siri jinsi ya kumsulubisha tena “Yesu” wa miaka elfu mbili iliyopita, ambaye amepitia maumivu miongoni mwa wanadamu. Je, “Yesu” anawatia watu moyo kuwa na chuki ya namna hiyo? Je, yote Aliyoyafanya yamesahaulika zamani? Chuki ambayo ilichanganyika kwa maelfu ya miaka itaibuka tena juu. Nyinyi mfano wa Wayahudi! Ni lini “Yesu” amekuwa adui yenu, hadi mmchukie kiasi hicho? Amefanya mengi na kuzungumza mengi—je hakuna chochote chenye manufaa kwenu? Ameyatoa maisha Yake kwenu bila kuomba kurudishiwa kitu chochote, Amejitoa mzima kwenu—kweli bado mnataka kumla Akiwa mzima? Amejitoa kwenu kikamilifu bila kuacha kitu chochote, bila kufurahia utukufu wa kidunia, wema miongoni mwa wanadamu, na upendo miongoni mwa wanadamu, au baraka zote miongoni mwa wanadamu. Watu ni wabinafsi sana Kwake, hajawahi kufurahia utajiri wote wa duniani, Amejitoa kikamilifu, moyo wa upendo wa dhati kwa mwanadamu, Amejirithisha mzima kwa mwanadamu—ni nani ambaye amemfanyia wema? Ni nani aliyewahi kumpatia faraja? Mwanadamu amemjazia mashinikizo yote, balaa yote amempatia Yeye, shida zote mbaya Alizozipitia ni mwanadamu amempatia Yeye, anamtupia lawama kwa uonevu wote, na Amezikubali kimyakimya. Je, Amewahi kumpinga mtu yeyote? Je, Amewahi kuomba fidia hata kidogo kutoka kwa mtu yeyote yule? Ni nani amewahi kumwonyesha huruma yoyote? Kama watu wa kawaida, ni nani miongoni mwenu ambaye hajawahi kuwa na kipindi cha utotoni chenye mapenzi ya dhati? Ni nani ambaye hajawahi kuwa na ujana wa kupendeza? Ni nani ambaye hana joto la wapendwa? Ni nani ambaye hana upendo wa rafiki wa karibu? Ni nani ambaye haheshimiwi na wengine? Ni nani ambaye hana familia yenye upendo? Ni nani ambaye hana faraja ya wandani wao? Je, Amekwishawahi kufurahia moja ya haya? Ni nani ambaye amewahi kumtendea wema hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumpatia faraja hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumwonyesha angalau maadili hata kidogo ya kibinadamu? Ni nani ambaye amewahi kuwa mvumilivu Kwake? Ni nani ambaye amewahi kuwa pamoja naye katika nyakati za shida? Ni nani ambaye amewahi kupitia maisha ya shida pamoja Naye? Mwanadamu bado hajaacha kumwomba Yeye; anapeleka tu maombi Kwake bila hata haya, kana kwamba kuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alipaswa kuwa ng’ombe au farasi wake, na Alipaswa kumpatia mwanadamu kila kitu chake; Asipofanya hivyo, mwanadamu hatamsamehe, hatamtendea vizuri, hatamwita Mungu, na hatamheshimu kwa kiwango cha juu. Mwanadamu ni katili sana katika mtazamo wake kwa Mungu, kana kwamba yupo ili kumtesa Mungu hadi kifo, ni baada ya hapo tu ndipo anapunguza maombi yake kwa Mungu; kama sivyo, mwanadamu hatapunguza kiwango cha matakwa yake kwa Mungu. Inawezekanaje mwanadamu kama huyu asidharauliwe na Mungu? Je, hili si janga la siku hizi? Dhamiri ya mwanadamu haionekani popote. Anasema tu atalipa upendo wa Mungu, lakini anamchanachana Mungu na kumtesa hadi kifo. Je, hii sio “mbinu ya siri” kwa imani yake kwa Mungu, iliyorithishwa kutoka kwa mababu zake? Hakuna mahali ambapo huwezi kuwakuta “Wayahudi,” na leo bado wanafanya kazi ile ile, bado wanafanya kazi ile ile ya kumpinga Mungu, na bado wanaamini kwamba wanamwinua Mungu juu? Inawezekanaje macho ya mwanadamu yamjue Mungu? Inawezekanaje mwanadamu, anayeishi katika mwili, kumchukulia Mungu kama Mungu mwenye mwili ambaye Amekuja kutoka katika Roho? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kumjua? Ukweli upo wapi miongoni mwa wanadamu? Haki ya kweli ipo wapi? Ni nani anayeweza kuijua tabia ya Mungu? Ni nani anayeweza kushindana na Mungu mbinguni? Haishangazi kwamba, Alipokuwa miongoni mwa wanadamu, hakuna aliyemjua Mungu, na amekataliwa. Inawezekanaje mwanadamu kuvumilia uwepo wa Mungu? Anawezaje kuvumilia kuruhusu mwanga kuondosha giza la ulimwengu? Je, hii yote si kujitoa kwa heshima kwa mwanadamu? Je, huku sio kuingia adilifu kwa mwanadamu? Je, kazi ya Mungu haijajikita katika kuingia kwa mwanadamu? Ningependa muunganishe kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu, na kurekebisha uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu, na kufanya majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na mwanadamu kwa uwezo wako wote. Kwa njia hii, kazi ya Mungu hatimaye itafikia mwisho, ikiwa ni pamoja na utukufu Wake!

Tanbihi:

1. “Kuingia kwa mwanadamu” hapa inaonyesha tabia ya mwanadamu ya uasi. Badala ya kutaja kuingia kwa watu katika maisha—ambako ni kuzuri—kunahusu tabia na matendo yao mabaya. Inahusu kwa upana matendo yote ya mwanadamu yaliyo katika upinzani na Mungu.

2. “Wanakerwa na hofu za kubuni” inatumiwa kudhihaki maisha ya binadamu wa mwanadamu yasiyo na mwelekeo. Inahusu hali mbaya ya maisha ya wanadamu, ambayo watu huishi pamoja na pepo.

3. “Bora zaidi” inasemwa kwa dhihaka.

4. “Hamasa yao daima ikiwaka moto zaidi” inasemwa kwa dhihaka, na inahusu hali mbaya ya mwanadamu.

5. “Kumkamata akiwa hai” inahusu tabia ya vurugu na yenye kustahili dharau ya mwanadamu. Mwanadamu ni katili na hayuko tayari kumsamehe Mungu hata kidogo, na hufanya madai ya upuuzi Kwake.

6. “Mpango alioufikiria kwa makini katika akili yake” inasemwa kwa dhihaka, na hii inahusu jinsi watu hawajijui na hawajui kimo chao halisi. Hii ni kauli ya kimatusi.

7. “Wa kuheshimiwa” inasemwa kwa dhihaka.

8. “Kutupa” inaonyesha hali mbaya ya watu ambao hughadhabika kwa hasira wakati ambapo wanashindwa na Mungu. Inaonyesha kiwango cha upinzani wao kwa Mungu.

Iliyotangulia: Kazi na Kuingia (9)

Inayofuata: Maono ya Kazi ya Mungu (1)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp