Kazi na Kuingia (9)

Tamaduni za asili na mitazamo ya kiakili madhubuti vimeweka kivuli katika roho safi na ya kitoto ya mwanadamu, vimeshambulia roho ya mwanadamu bila ubinadamu hata kidogo kana kwamba anaondolewa hisia na hali yoyote ya nafsi. Mbinu za mashetani hawa ni za kikatili kupita kiasi, na ni kana kwamba “elimu” na “malezi” vimekuwa ni njia za kitamaduni ambazo kwazo mfalme wa mashetani anamchinja mwanadamu; kwa kutumia “mafundisho yake ya kina” anafunika kabisa roho yake mbaya, akivaa mavazi ya kondoo ili kupata imani ya mwanadamu na kisha kuchua fursa mwanadamu akilala fofofo kwa uchovu ili kummeza kabisa. Masikini binadamu—wangewezaje kujua kwamba nchi ambayo kwayo wamelelewa ni nchi ya Shetani, kwamba aliyewalea kimsingi ni adui ambaye anawaumiza. Lakini bado mwanadamu hazinduki kabisa; baada ya kushibisha hasira na kiu chake, anajiandaa kulipa “wema” wa wazazi wake kwa kumlea. Hivyo ndivyo mwanadamu alivyo. Leo, bado hajui kwamba “mfalme” ambaye alimlea ni adui yake. Nchi imechafuliwa na mifupa ya wafu, Shetani anafanya wazimu bila kutulia, na anaendelea kumeza mwili wa mwanadamu huko “kuzimu,” akishiriki kaburi pamoja na mifupa ya wanadamu na akijaribu waziwazi kuwamaliza masalia wa mwisho wa mwili wa mwanadamu uliobakia matambara. Lakini mwanadamu bado ni mjinga, na hajawahi kumchukulia Shetani kama adui yake, lakini badala yake anamtumikia kwa moyo wake wote. Watu kama hao waliokengeuka hawawezi kumjua Mungu. Ni rahisi kwa Mungu kuwa mwili na kuja miongoni mwa wanadamu, Akitekeleza kazi Zake zote za wokovu? Mwanadamu, ambaye tayari amekwishajiingiza Kuzimu, anawezaje kukidhi matakwa ya Mungu? Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amestahili vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kumlaumu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena? Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[1] na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haijakuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso haya na kunyanyaswa na nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku? Moyo wa upendo na matarajio ya shauku ya Mungu vimelipwa kwa mioyo ya baridi, na usugu, na macho yanayoonyesha kutojali, kwa makaripio ya kujirudia na matusi ya mwanadamu, kwa maneno ya mkato na dhihaka na udhalilishaji, vimelipwa kwa dhihaka ya mwanadamu, kwa kukanyagwa na kukataliwa, kwa kutokuwa na ufahamu, na kupiga kite, na farakano, na uepukaji, kwa uongo, mashambulizi na ukali. Maneno ya wema ya Mungu yamekutana na nyuso kali na ufidhuli wa vidole elfu moja vinavyotikisika. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa.[2] Miezi na jua nyingi sana, Amekabiliana na nyota mara nyingi sana, Ameondoka alfajiri na kurudi jioni mara nyingi sana, na kurushwarushwa na kugeuzwa, Akivumilia maumivu makubwa mara elfu moja kuliko maumivu Aliyoyapata Alipokuwa Anaondoka kwa Baba Yake, Akivumilia mashambulizi na “kuvunja” kwa mwanadamu, na “kumshughulikia” na “kumpogoa” mwanadamu. Unyenyekevu na kufichika kwa Mungu vimelipwa kwa upendeleo[3] wa mwanadamu, kwa mitazamo na vitendo vya mwanadamu visivyokuwa vya haki, na kutojulikana Kwake, ustahimilivu, na uvumilivu vimelipizwa kwa jicho la tamaa la mwanadamu, mwanadamu hujaribu kumkanyaga Mungu hadi afe, bila majuto, na anajaribu kumkanyagia Mungu ardhini. Mtazamo wa mwanadamu kwa namna anavyomtendea Mungu ni wa “ujanja adimu,” na Mungu ambaye Anachokozwa na kutwezwa na mwanadamu, Anakanyagwa na kuwa bapa kwa miguu ya makumi elfu ya watu wakati mwanadamu mwenyewe anasimama juu kabisa, kana kwamba angeweza kuwa “mfalme wa kasri,” kana kwamba anataka kuchukua mamlaka kamili,[4] “kuendesha mahakama akiwa nyuma ya skrini,” kumfanya Mungu kuwa makini na mwenye kanuni “mwongozaji nyuma ya matukio,” ambaye haruhusiwi kupigana au kusababisha shida; lazima Mungu achukue nafasi ya “Mtawala wa Mwisho,” ni lazima Awe “kibaraka,”[5] bila uhuru wote. Matendo ya mwanadamu hayasemeki, sasa ana sifa gani ya kutaka hili au lile kuhusu Mungu? Ana sifa gani ya kutoa mapendekezo kwa Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kumtaka Mungu amhurumie juu ya udhaifu wake? Anafaa kwa kiasi gani kupokea huruma ya Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kupokea ukarimu wa Mungu kila mara? Anafaa kwa kiasi gani kupokea msamaha wa Mungu kila mara? Dhamiri yake ipo wapi? Alivunja moyo wa Mungu muda mrefu uliopita, ni muda mrefu toka ameuacha moyo wa Mungu katika vipande. Mungu alikuja miongoni mwa wanadamu Akiwa na nguvu nyingi na mwenye shauku kubwa, Akitegemea kwamba mwanadamu atakuwa mkarimu Kwake, hata kama ni kwa wema kiasi kidogo tu. Bado moyo wa Mungu haujafarijiwa na mwanadamu, yote Aliyoyapokea ni mashambulizi na mateso ya kuongezeka haraka;[6] moyo wa mwanadamu ni wenye tamaa sana, tamaa yake ni kubwa sana, hawezi akatosheka, siku zote ni mwenye fitina na jasiri pasi busara, hawezi kamwe kumpatia Mungu uhuru au haki ya kuzungumza, na anamwacha Mungu bila budi ila kukubali unyanyasaji, na kumruhusu mwanadamu kumtawala vyovyote apendavyo.

Tangu uumbaji hadi leo, Mungu amestahimili maumivu mengi sana, na kupata mashambulizi mengi sana. Ilhali hata leo, bado mwanadamu hayalegezi matakwa yake kwa Mungu kwa urahisi, bado anamchunguza Mungu, bado hana uvumilivu Naye, na anachofanya ni kumpatia “ushauri,” na “kumkosoa,” na “kumfundisha nidhamu” kana kwamba Mungu atapotoka njia, kwamba Mungu duniani ni hayawani na Hana busara, au Atafanya fujo, au kwamba Hatafanya kitu chochote cha maana. Mwanadamu siku zote huwa na mtazamo wa aina hii kwa Mungu. Inawezekanaje isimhuzunishe Mungu? Kwa kuwa mwili, Mungu amevumilia maumivu na mateso mengi; ni vibaya kiasi gani, kumfanya Mungu akubali mafundisho ya mwanadamu? Kuwasili kwake miongoni mwa wanadamu kumemvua uhuru wote, kama vile Amefungwa Kuzimu, na Amekubali “uchunguzi” wa mwanadamu bila upinzani hata kidogo. Hii sio aibu? Katika kuja miongoni mwa familia ya wanadamu wa kawaida, “Yesu” amepitia uonevu mkubwa. Na kinachoumiza zaidi ni kwamba Amekuja katika ulimwengu huu wa vumbi na kujinyenyekeza Mwenyewe katika hadhi ya chini kabisa, na Amechukua mwili wa kawaida kabisa. Kwa binadamu kuwa mwembamba, je, Mungu Mwenyezi hapati shida? Na, je, Yeye hafanyi hivyo kwa ajili ya binadamu? Kuna wakati wowote ambapo alikuwa Anajifikiria Mwenyewe? Baada ya kukataliwa na kuuawa na Wayahudi, na kukejeliwa na kudhihakiwa na watu, Hajawahi kulalamika mbinguni au kupinga duniani. Leo, janga hili lenye umri wa milenia limetokea tena miongoni mwa watu hawa wanaofanana na Wayahudi. Je, hawafanyi dhambi ile ile? Nini kinamfanya mwanadamu kuwa na sifa ya kupokea ahadi za Mungu? Je, hampingi Mungu na kisha kukubali baraka Zake? Kwa nini haifikii haki, au kutafuta ukweli? Kwa nini havutiwi na kile ambacho Mungu anafanya? Haki yake iko wapi? Usawa wake uko wapi? Je, ana ujasiri wa kumwakilisha Mungu? Ziko wapi fahamu zake za haki? Ni kiasi gani ambacho kile kinachopendwa na mwanadamu ndicho kile kinachopendwa na Mungu? Mwanadamu hawezi kutambua tofauti muhimu, [7] siku zote anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe,[8] anakandamiza haki na ukweli, na anashikilia kutokuwa na haki wala usawa kwa kiwango kikubwa. Anafukuzia mbali mwanga na anarukaruka gizani. Wale wanaotafuta ukweli na haki badala yake wanafukuza mwanga, wale wanaomtafuta Mungu wanamkanyaga kwa miguu yao, na wanajipandisha angani. Mwanadamu hana tofauti na gaidi.[9] Sababu yake iko wapi? Nani anaweza kutofautisha kati ya jema na baya? Nani anaweza kushikilia haki? Nani yuko tayari kuteseka kwa ajili ya ukweli? Watu ni waovu na wana tabia za kishetani kabisa! Baada ya kumwangika Mungu msalabani wanapiga makofi na kufurahi, vilio vyao havikomi. Wako kama kuku na mbwa, wanashirikiana na kula njama, wameanzisha ufalme wao, udukuzi wao haujaachwa bila kusumbuliwa, wanafumba macho yao na kulia kwa maumivu makali zaidi na zaidi, wote wameungana pamoja, na hali ya kuvurugika imeenea kote, ni harakaharaka na hai, na wale ambao wanajishikamanisha kwa wengine kijinga wanazidi kuibuka, wote wakiwa wameshikilia majina “mashuhuri” ya mababu zao. Hawa mbwa na kuku wamemweka Mungu mbali na akili zao, na hawajawahi kuzingatia kabisa hali ya moyo wa Mungu. Si ajabu kwamba Mungu anasema mwanadamu ni kama mbwa au kuku, mbwa anayebweka anayewafanya mia wengine kutoa mlio mkali; kwa nia hii, kwa makelele mengi ameileta kazi ya Mungu katika siku ya leo, bila kujali kazi ya Mungu ni ya namna gani, bila kujali kuna haki, bila kujali Mungu ana nafasi Yake ya kuweka miguu Yake, bila kujali kesho itakuwaje, uduni wake, na hali yake ya kuwa mchafu. Mwanadamu hajawahi kufikiria juu ya mambo kiasi hicho, hajawahi kuhofia kesho, na amekusanya yale yote ambayo ni ya manufaa na ya thamani na kuyakumbatia, na bila kumwachia Mungu chochote isipokuwa mabaki na makombo.[10] Binadamu ni katili kiasi gani! Hana hisia hata kidogo kwa Mungu, na baada ya kuteketeza kila kitu cha Mungu, anamrusha Mungu nyuma yake na kuacha kujali kabisa kuhusu uwepo wake. Anamfurahia Mungu, halafu anampinga Mungu, na anamkanyagia chini ya miguu yake, wakati mdomoni mwake anamshukuru na kumsifu Mungu; anamwomba Mungu, na anamtegemea Mungu, wakati huo pia anamdanganya Mungu; “analiinua” jina la Mungu, na kuutazama uso wa Mungu, halafu pia bila haya na bila kuwa na aibu anakaa katika kiti cha enzi cha Mungu na “kuhukumu” “udhalimu” wa Mungu; kutoka katika kinywa chake yanatoka maneno haya “anapaswa kumshukuru Mungu,” na anatazama katika maneno ya Mungu, halafu katika moyo wake anavurumisha shutuma kwa Mungu; ni “mvumilivu” kwa Mungu halafu anamkandamiza Mungu, na kinywa chake kinasema ni “kwa ajili ya Mungu”; mikononi mwake ameshikilia vitu vya Mungu, na kinywani mwake anatafuna chakula ambacho Mungu amempatia, bado macho yake yanamtazama Mungu yakiwa hayana hisia kabisa, kana kwamba anatamani kummeza; anautazama ukweli lakini anasisitiza kuwa ni hila za Shetani; anatazama haki lakini analazimisha iwe kujikana nafsi; anatazama matendo ya mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni kile Mungu alicho; anatazama karama za asili za mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni ukweli; anatazama matendo ya Mungu lakini anasisitiza kuwa ni kiburi na majivuno, majigambo na haki binafsi; mwanadamu anapomwangalia Mungu anasisitiza kumpachika uanadamu, na anajitahidi sana kumweka katika kiti cha kiumbe aliyeumbwa akishirikiana na Shetani; anajua kweli kabisa ni matamshi ya Mungu, bado atasema si kitu chochote zaidi ya maandiko ya mwanadamu; anajua kabisa kwamba Roho anatambulika katika mwili, kwamba Mungu amekuwa mwili, lakini anasema mwili huu ni uzao wa Shetani; anajua kikamilifu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na hajionyeshi, lakini anasema kwamba Shetani ameaibishwa na Mungu ameshinda. Uzuri wa bure ulioje! Mwanadamu hata hafai kuwa mbwa mlinzi! Hawezi kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, na hata anachanganya kwa makusudi nyeusi ndani ya nyeupe. Je, nguvu za mwanadamu na husuru ya mwanadamu vinaweza kustahimili siku ya ukombozi wa Mungu? Baada ya kumpinga Mungu kwa kukusudia, mwanadamu hakuweza kujali sana, au hata kwenda mbali sana na kumuua, asimpatie Mungu nafasi ya kujionyesha Mwenyewe. Haki iko wapi? Upendo uko wapi? Anakaa kando ya Mungu na kumsukuma Mungu apige magoti ili Aombe msamaha, kutii mipango yake yote, kuridhia hila zake zote, na anamfanya Mungu kuchukua ishara Zake zote kutoka Kwake, la sivyo anaghadhibishwa[11] na kupandwa na hasira. Inawezekanaje Mungu asiwe na maumivu katika ushawishi huo wa giza, ambao unachanganya nyeusi kuwa nyeupe? Angewezaje kukosa kuwa na wasiwasi? Kwa nini inasemwa kwamba Mungu alipoanza kazi Yake ya hivi karibuni kabisa, ilikuwa ni kama kazi ya kuumba mbingu na dunia? Matendo ya mwanadamu “yana utajiri,” ni “chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima” bila kukoma “yanajaza tena” shamba la moyo wa mwanadamu, wakati “chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima” ya mwanadamu “inashindana” na Mungu bila haya;[12] wawili hawa hawapatani, na anawapa watu vitu kwa niaba ya Mungu bila hofu ya kuadhibiwa wala kuumia, wakati mwanadamu anashirikiana naye bila kujali hatari iliyopo. Na kwa athari gani? Anamtupilia mbali Mungu upande mmoja, na kumweka mbali sana, ambapo watu hawatamzingatia, akiogopa sana kwamba Atavuta usikivu wake, na anaogopa sana kwamba chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima ya Mungu itamteka mwanadamu, na kumpata mwanadamu. Hivyo, baada ya kupitia uzoefu wa miaka mingi wa masuala ya kidunia, anakula njama dhidi ya Mungu, na hata anamfanya Mungu kuwa mlengwa wa “adhabu.” Ni kana kwamba Mungu amekuwa gogo machoni mwake, na anatamani kumnyakua Mungu na kumweka motoni ili Atakaswe na kusafishwa. Mwanadamu anapoona mahangaiko ya Mungu, anapiga kifua chake na kucheka, anacheza kwa furaha, na kusema kwamba Mungu pia Amewekwa motoni, na anasema kwamba atausafisha uchafu wa Mungu, kana kwamba hili ni la urazini na lina maana, kana kwamba hizi tu ndizo njia za haki na zenye mantiki za Mbinguni. Tabia hii ya fujo ya mwanadamu inaonekana kuwa ni ya makusudi na ya kutofahamu. Mwanadamu anafichua uso wake mbaya na roho yake mbaya, vilevile sura ya kusikitisha ya ombaomba; baada ya kufanya ghasia sana, anavaa sura ya kuhurumiwa na kuomba msamaha wa Mbingu, akifanana na udongo wa kufinyangwa. Mwanadamu siku zote hutenda kwa namna asiyotarajiwa, siku zote “anamwendesha duma kuwatisha wengine,”[a] yeye daima huwa akiigiza sehemu fulani, hajali hata kidogo moyo wa Mungu, wala halinganishi hadhi yake mwenyewe. Kimyakimya anampinga Mungu, kana kwamba Mungu amemkosea, na Hapaswi kumtendea hivyo, na kana kwamba Mbingu haina macho na inafanya kwa makusudi mambo kuwa magumu kwake. Hivyo mwanadamu anapanga njama za siri, na hajali matakwa ya Mungu hata kidogo, anatazama kwa macho ya mnyama mkali, anatazama kwa hasira kila kitu Anachokifanya Mungu, hafikirii kwamba yeye ni adui ya Mungu, na ana matumaini kwamba siku itakuja ambapo Mungu atautawanya umande na kuviweka vitu wazi, na kumwokoa kutoka katika “kinywa cha duma” na kulipiza kisasa kwa niaba yake. Hata leo, watu bado hawafikiri kwamba wanatekeleza jukumu la kumpinga Mungu, jukumu ambalo limefanywa kwa enzi nyingi sana, wangewezaje kujua kwamba, katika yote wanayofanya, wamepotoka tangu zamani sana, kwamba yote waliyoyaelewa yamemezwa na bahari zamani sana.

Ni nani amewahi kukubali ukweli? Ni nani amewahi kumkaribisha Mungu kwa mikono yote? Nani amewahi kutamani uwepo wa Mungu? Tabia ya mwanadamu imeoza tangu zamani sana, na unajisi wake umefanya hekalu la Mungu lisitambulike tangu zamani sana. Mwanadamu, wakati akiendelea kufanya kazi yake, amekuwa akimdharau Mungu. Ni kana kwamba upinzani wake kwa Mungu umeandikwa kwenye jiwe, na haubadiliki, na matokeo yake ni bora alaaniwe kuliko kuendelea kuteseka “kwa kufanyiwa vibaya” na maneno na matendo yake. Inakuwaje watu kama hawa wamjue Mungu? Wanawezaje kupata pumziko kwa Mungu? Na wanawezaje kufaa kuja mbele za Mungu? Bila shaka, hakuna chochote kibaya kujitoa kwa mpango wa usimamizi wa Mungu—lakini kwa nini watu daima huweka kazi ya Mungu na ukamilifu wa Mungu akilini mwao huku wakitoa kwa dhati damu na machozi yao wenyewe? Roho ya watu ya kujitokea kwa dhati, bila shaka, ni ya thamani—lakini wangejuaje kwamba “hariri” wanayoisokota haiwezi kabisa kuwakilisha kile Mungu alicho? Nia nzuri za watu, bila shaka, ni za thamani na adimu—lakini wangewezaje kumeza “hazina ya thamani mno”?[13] Kila mmoja wenu anapaswa kufikiria juu ya maisha yenu ya zamani: Kwa nini hamjawahi kuwa mbali na kuadibu na laana ya kikatili? Kwa nini watu daima “huwa na uhusiano wa karibu” na maneno adhimu na hukumu yenye haki? Je, Mungu anawajaribu kwa kweli? Je, Mungu anawasafisha kwa makusudi? Na watu huingiaje katikati ya usafishaji? Je, wanajua kazi ya Mungu kweli? Ni mafunzo gani ambayo watu wamejifunza kutoka kwa kazi ya Mungu na kuingia kwao wenyewe? Watu wasisahau kusihi kwa Mungu, na wawe na ufahamu katika kazi ya Mungu, waitambue kwa uwazi kabisa, na kusimamia vizuri kuingia kwao wenyewe.

Tanbihi:

1. “Maangamizi” inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

2. “Anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa” ni kwa asili sentensi moja, lakini hapa imegawanywa mara mbili ili kuyafanya mambo wazi zaidi. Sentensi ya kwanza inahusu matendo ya mwanadamu, huku ya pili inaonyesha mateso aliyoyapitia Mungu, na kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyefichika.

3. “Upendeleo” unahusu tabia ya watu ya ukaidi.

4. “Kuchukua mamlaka kamili” inahusu tabia ya watu ya ukaidi. Wanajitukuza, huwafunga wengine, wakiwafanya wawafuate na kuteseka kwa ajili yao. Wao ni majeshi ambayo ni ya uadui kwa Mungu.

5. “Kibaraka” inatumiwa kuwadhihaki wale ambao hawamjui Mungu.

6. “Kuongezeka haraka” inatumiwa kuonyesha tabia duni ya watu.

7. “Hawezi kutambua tofauti muhimu” inaonyesha wakati ambapo watu wanageuza mapenzi ya Mungu kuwa kitu cha kishetani, ikitaja kwa upana tabia ambayo kwayo watu humkataa Mungu.

8. “Anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe” inahusisha kuchanganya ukweli na njozi, na haki na uovu.

9. “Gaidi” inatumiwa kuonyesha kwamba watu ni wapumbavu na hawana ufahamu.

10. “Mabaki na makombo” inatumiwa kuonyesha tabia ambazo kwazo watu humdhulumu Mungu.

11. “Anaghadhibishwa” inahusu uso mbaya wa mwanadamu aliye na hasira na aliyeudhika.

12. “Bila haya” inahusu wakati ambapo watu hawajali, na hawana uchaji kuhusiana na Mungu hata kidogo.

13. “Hazina ya thamani mno” inahusu ukamilifu wa Mungu.

a. Hili limetafsiriwa kulingana na maandishi asili “hú jiǎ hǔ wēi”, ambayo ni msemo wa Kichina. Yanarejelea hadithi ambamo mbweha anawafukuza wanyama wengine kwa kutembea kama pamoja na chui mwenye milia, hivyo “kuazima” hofu na hadhi ambayo chui mwenye milia anaibua. Hii ni istiara, inayotumiwa hapa kuashiria watu “wanaoazima” hadhi ya mtu mwingine ili kuwaogofya au kuwadhulumu watu wengine.

Iliyotangulia: Kazi na Kuingia (8)

Inayofuata: Kazi na Kuingia (10)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp