Kazi na Kuingia (7)

Imemchukua mwanadamu mpaka siku hii kutambua kwamba kile mtu anachokosa si tu kuruzukiwa maisha ya kiroho na uzoefu wa kumjua Mungu, lakini, muhimu zaidi, mabadiliko katika tabia yake. Kutokana na ujinga kamili wa mwanadamu wa historia na utamaduni wa kale wa wanadamu, hana ujuzi wa kazi ya Mungu hata kidogo. Mwanadamu hutumaini kuwa ndani kabisa ya moyo, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu kwa kina moyoni mwake, lakini kwa kuwa mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kina sana, kwa kufa ganzi pamoja na kuwa usiohisi, hii imemsababisha kutojua chochote hata kidogo kumhusu Mungu. Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa mamilioni ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa. Kushughulika na nidhamu ni njia, na ushindi na kufanya upya ni malengo. Kuondoa mawazo ya kishirikina aliyonayo mwanadamu kuhusu Mungu asiye dhahiri ndilo limekuwa kusudi la Mungu milele, na hivi karibuni limekuwa suala la haraka kwake. Ingekuwa kwamba watu wote wangetafakari kwa kina kwa kuzingatia hali hii. Wabadilishe jinsi kila mtu anavyopitia uzoefu ili kwamba kusudi hili la haraka la Mungu liweze kufanyika hivi karibuni na hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani iweze kuhitimishwa kwa matokeo mazuri. Onyesheni uaminifu wenu kama mnavyopaswa, na ufariji moyo wa Mungu kwa mara ya mwisho. Ni matumaini Yangu kwamba hakuna mtu yeyote miongoni mwa kaka na dada atakayekwepa jukumu hili au kuzungukazunguka tu. Mungu Anakuja katika mwili wakati huu kwa mwaliko, na kutokana na hali ya mwanadamu. Yaani, Anakuja kumpatia mwanadamu kile alichokuwa anahitaji. Atakuja kumwezesha kila mwanadamu, wa tabia yoyote au jamii, kuona neno la Mungu na, kutoka katika neno Lake, kuona uwepo na udhihirishaji wa Mungu na kukubali ukamilishaji wa Mungu. Neno lake litabadilisha mawazo na mitazamo ya mwanadamu ili kwamba sura ya kweli ya Mungu ikite mizizi kabisa katika moyo wa mwanadamu. Hili ndilo tamanio pekee la Mungu duniani. Haijalishi jinsi gani asili ya mwanadamu ilivyo, jinsi gani asili yake ilivyo duni, au matendo yake yalivyokuwa huko nyuma, Mungu Hajali haya. Anatumainia tu mwanadamu kuisafisha kabisa taswira ya Mungu aliyonayo moyoni mwake na kuijua asili ya binadamu, na hapo Atakuwa Amebadilisha mtazamo wa kiitikadi wa mwanadamu. Anatarajia mwanadamu kuwa na shauku ya kina kwa Mungu na kuwa na mahusiano ya milele na Yeye. Hiki ndicho Mungu Anachomwomba mwanadamu.

Maarifa ya utamaduni wa kale na historia ambayo imekuwepo kwa maelfu kadhaa ya miaka imefunga fikra na mawazo na akili yake mwanadamu kwa nguvu sana kiasi cha kuzifanya kutowezakana kupenyezwa na kutoweza kuoza.[1] Watu wanaishi katika duara la kumi na nane la kuzimu, kana kwamba wamefukuziwa chini na Mungu, wasiweze kuona mwanga tena. Fikra za kishirikina hivyo zimewakandamiza watu kiasi kwamba hawawezi kupumua na wana shida ya kupumua. Hawana nguvu hata kidogo ya kupinga, kimya kimya wanaendelea kuvumilia na kuvumilia... Hakuna hata mmoja aliyewahi kujaribu kupigana au kusimama kwa ajili ya uadilifu na haki; watu wanaishi maisha ambayo ni mabaya zaidi ya mnyama, chini ya kugongwa na unyanyasaji wa maadili ya kishirikina, siku baada ya siku na mwaka baada ya mwaka. Wanadamu hajawahi kufikiria kumtafuta huyu Mungu ili kufurahia furaha katika ulimwengu wa mwanadamu. Ni kana kwamba mwanadamu amepigwa, kama majani yaliyoanguka ya majira ya kupukutika, yaliyonyauka na kukauka kabisa. Mwanadamu amepoteza kumbukumbu na anaishi bila matumaini kuzimu kwa jina la ulimwengu wa kibinadamu, akisubiri ujio wa siku ya mwisho ili kwamba waweze kupotea pamoja na kuzimu, kana kwamba siku ya mwisho wanayoitamani sana ni siku watakayofurahia pumziko la amani. Maadili ya kishirikina yamempeleka mwanadamu “Kuzimu,” hivyo kudhoofisha zaidi uwezo wa mwanadamu wa kupinga. Ukandamizaji wa aina mbalimbali umemlazimisha mwanadamu taratibu kuzama chini kabisa Kuzimu na kutanga mbali kabisa na Mungu. Sasa, Mungu Amekuwa mgeni kabisa kwa mwanadamu, na mwanadamu bado anafanya haraka kumwepuka wanapokutana. Mwanadamu hamtilii maanani na anamtenga kana kwamba mwanadamu hajawahi kumwona hapo kabla. Bado Mungu amekuwa mwenye subira kwa mwanadamu wakati wote katika safari ndefu ya maisha ya binadamu, kamwe harushi ghadhabu Yake isiyoweza kusitishwa kwake, Amekuwa Akisubiri tu kimya tu, bila kunena lolote, kwa mwanadamu kutubu na kuanza upya. Mungu zamani alikuja kwenye ulimwengu wa binadamu na Huvumilia mateso hayo hayo kama mwanadamu. Ameishi na mwanadamu kwa miaka mingi na hakuna aliyegundua kuwepo Kwake. Mungu huvumilia tu kwa kimya taabu ya uchakavu katika ulimwengu wa binadamu huku Akifanya kazi Aliyoleta yeye mwenyewe. Anaendelea kuvumilia kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na kwa ajili ya mahitaji ya wanadamu, Amevumilia, Akipitia maumivu ambayo kamwe mwanadamu hajawahi kupitia. Mbele ya mwanadamu, Amewahudumia kimya kimya na kujinyenyekeza Mwenyewe, kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na mahitaji ya wanadamu. Maarifa ya utamaduni wa kale kwa taratibu yamemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu na kumweka mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Bora[a] vimepeleka fikira za mwanadamu na mawazo yake katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Kwa ukosefu wa kujua wa mwanadamu, mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje ya moyo wake na kuumiliki yeye mwenyewe kwa furaha ya ushindi tangu wakati huo, mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na uso wa mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani ya mwanadamu hadi alipomalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa tena hata na chembe ya uhuru na hakuwa na njia ya kujikwamua kutokana na taabu za mfalme wa mashetani. Hakuwa na budi ila kuchukuliwa mateka papo hapo, kujisalimisha na kuanguka chini kwa kutii mbele yake. Hapo zamani, wakati moyo na nafsi ya mwanadamu vilikuwa vichanga, mfalme wa mashetani alipanda ndani yake mbegu ya saratani ya ukanaji Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, “kujifunza sayansi na teknolojia, kutambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani.” Si hivyo tu, ametangaza kwa kurudiarudia, “Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii,” akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kutumikia nchi yao. Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Ameshikilia binadamu mzima katika mikono Yake). Hajawahi kuwa na kuhisi aibu yoyote au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu amewanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, wakati akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Ni ujahili kabisa huu Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, “Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa ajili ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka chini kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?” Kuna wale hata wanaofoka kauli kama zifuatazo, kauli ambazo hazifai kutamkwa. “Mwanadamu alitoka kwa nyani katika nyakati zilizopita, na dunia leo inatoka kwa mfululizo wa jamii zizizostaarabika kuanzia takribani miaka mingi isiyohesabika. Iwapo nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake.” Kwa nyuma, inamfanya mwanadamu kuning’iniza kwenye ukuta au kuweka kwa meza ili kutoa heshima na kumtolea sadaka. Wakati huo huo anapiga kelele kwamba “Hakuna Mungu,” anajichukulia mwenyewe kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ni upuuzi mkubwa kiasi gani! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu Hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia huru na hajapatikana.[2] Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha katika matambara na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa,[3] kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi mmoja kati yao awe ameangamia. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza imefunuliwa toka zamani na sasa imevilia damu na kugongwagongwa,[4] ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira zake kwa Mungu, kana kwamba anatamani kummeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake. Tunawezaje kumvumilia, huyu adui wa Mungu anayechukiwa! Ni kumalizwa kwake na kuondolewa kabisa ndiko kutaleta kutimia kwa matamanio yetu ya maisha. Anawezaje kuruhusiwa kuendelea kukimbia ovyoovyo? Amemharibu mwanadamu kwa kiwango kama hicho mwanadamu hajui ’mahali pa raha zote, na amekuja kuwa mfu na asiye na hisia. Mwanadamu amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiri wa kibinadamu. Kwa nini tusitoe nafsi zetu zote kumwangamiza yeye na kumchoma ili kuondoa kabisa hofu yote ya hatari ya siku zijazo na kuruhusu kazi ya Mungu kuufikia uzuri usiotarajiwa mapema? Genge hili la waovu limekuja katika dunia ya wanadamu na kusababisha hofu na shida kubwa. Wamewaleta wanadamu wote katika ukingo wa jabali, wakipanga kwa siri kuwasukumia chini wavunjike vipande vipande na kumeza maiti zao. Wana matumaini ya kuharibu mpango wa Mungu na kushindana na Mungu katika pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda.[5] Hiyo kwa vyovyote vile ni rahisi! Msalaba umeandaliwa, mahususi kwa ajili ya mfalme wa mashetani ambaye ni mwenye hatia ya makosa maovu sana. Mungu si wa msalaba tena na Amekwishamwachia Shetani. Mungu Aliibuka mshindi muda mrefu uliopita, Hahisi tena huzuni juu ya dhambi za binadamu. Ataleta wokovu kwa binadamu wote.

Kutoka juu hadi chini na kutoka mwanzo hadi mwisho, Shetani amekuwa akivuruga kazi ya Mungu na kutenda katika upinzani Kwake. Mazungumzo yote ya “urithi wa utamaduni wa kale,” “maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale,” “mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius,” na “maandiko ya kale ya Confucius na ibada ya kishirikina” vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekeni popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kwa makusudi kabisa kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu. Sio tu amemtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[6] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wapo tayari kumpokea Mungu na kukaribisha kwa furaha ujio wa Mungu. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi linaloungua na ubani, ni harufu nzito sana inayomaliza hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo mwanadamu hawezi kuvumilia bali kutapika tu. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu ya furaha ya kutamanisha, wakati mfalme wa mashetani ameendelea kucheka vibaya, kana kwamba njama zake za kupotosha zimefanikiwa. Wakati huo mwanadamu hana habari naye, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwishamharibu kwa kiwango ambacho amekuwa hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani, kwa kishindo, kuangamiza kila kitu kuhusu Mungu, na kwa mara nyingine kuchafua na kumwangamiza; nia yake ni kubomoa na kuvunja kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “akiingilia” na kazi yake miongoni mwa wanadamu ulimwenguni? Anawezaje kumruhusu Mungu kuufichua uso wake wa kutisha? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya mahakama yake ya kifalme duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai![7] Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemchezea mwanadamu sana kiasi kwamba mwonekano wake umekuwa ule wa mnyama wa mashambani, mbaya sana, na kutoka athari ya mwisho ya mwanadamu asilia imepotea. Aidha, wanatamani kuwa wa nguvu za ukuu duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu kiasi kwamba isiweze kusonga mbele kiasi kidogo na wanamfunga mwanadamu kwa mkazo kama wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi mbaya sana na kusababisha majanga mengi sana, je, bado wanatarajia kitu tofauti na kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[8] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu kuliko mfalme wa wote, kujua kidogo kwamba wao si zaidi ya nzi wenye uvundo. Na bado, wanatumia vibaya uwezo wa nguruwe na mbwa ambao ni wazaziwe ili kukashifu uwepo wa Mungu. Kama nzi wadogo, wanaamini wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi wenye meno.[9] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, ilihali wazazi wao ni nguruwe wachafu mara mamia ya mamilioni kuliko wao wenyewe kwa ukubwa? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na kwa njia hizi wanaleta ukandamizaji kwa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea yale yanayoendelea kwa nyuma katika ulimwengu wa kidini). Ni jinsi gani mwanadamu angejua kwamba, licha ya urembo mzuri wa mbawa za nzi, nzi mwenyewe ni kiumbe mdogo tu, aliye na tumbo iliyojaa uchafu na mwili uliojaa vijidudu? Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza tena mkondo mwingine wa usaliti, wakianzisha kazi yao yenye miaka maelfu kadhaa iliyopita. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize. Kwa mwanadamu kumpenda Mungu ni lazima aelewe mapenzi Yake na furaha Yake na huzuni, vilevile na kile Anachokichukia zaidi. Hii itakuza zaidi kuingia kwa mwanadamu. Kadiri mwanadamu anavyoingia kwa haraka, ndivyo moyo wa Mungu unavyoridhika zaidi; kadiri mwanadamu anavyomtambua kwa uwazi mfalme wa mashetani, ndivyo mwanadamu anavyosogea karibu zaidi na Mungu, ili kwamba matamanio Yake yaweze kutimia.

Tanbihi:

1. “Kutoweza kuoza” imenuiwa kama tashtiti hapa, kumaanisha kwamba watu ni wagumu katika ufahamu, utamaduni na mitizamo yao ya kiroho.

2. “Huru na hajapatikana” inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.

3. “Hali ya shaghalabaghala kabisa” inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kuona.

4. “Imevilia damu na kugongwagongwa” inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.

5. “Pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda” ni istiara ya mipango mibaya ya shetani yenye kudhuru kwa siri, ya uovu. Inatumiwa kwa dhihaka.

6. “Kummaliza” inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.

7. “Washiriki jinai” ni wa namna moja na “kundi la majambazi.”

8. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

9. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

a. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Boara ni vitabu vyenye mamlaka ya Ukonfushashi nchini China.

Iliyotangulia: Kazi na Kuingia (6)

Inayofuata: Kazi na Kuingia (8)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp