3. Tofauti ni ipi kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na kazi ya Roho?

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na Musa akasema, nakuomba, nionyeshe utukufu wako. Na Yehova alisema, Nitaufanya wema Wangu wote upite mbele yako, na nitalitangaza jina la Yehova mbele yako; na nitakuwa mwenye fadhili kwa yule nitakayekuwa mwenye fadhili, na nitaonyesha rehema kwa yule nitakayeonyesha rehema. Naye akasema, Huwezi kuuona uso wangu: kwani hakuna mtu atakayeniona, na kisha aishi” (Kutoka 33:18-20).

“Na Yehova akashuka chini kwenye mlima Sinai, katika kilele cha mlima: na Yehova akamwita Musa juu katika kilele cha mlima; na Musa akaenda juu. Na Yehova akasema kwa Musa, Nenda chini, waagize watu, ili wasipenye waende kwa Yehova kukazia macho, na wengi kati yao waangamie. Na makuhani pia, ambao humkaribia Yehova, wajitakase, ili Yehova asiwafurikie” (Kutoka 19:20-22).

“Na watu wote waliiona radi, na umeme, na sauti ya tarumbeta, na mlima ukitoa moshi: na watu walipoyaona, waliogopa, na kusimama mbali. Na wakasema kwa Musa, Wewe zungumza na sisi, na tutasikiza: lakini Mungu asizungumze nasi, ili tusife” (Kutoka 20:18-19).

“Kisha sauti ikaja kutoka mbinguni, ikisema, nimeitukuza, na nitaitukuza tena. Kwa hiyo, watu waliosimama hapo kando, na wakaisikia, walisema kwamba ilinguruma: wengine wakasema, Malaika alinena naye” (Yohana 12:28-29).

Maneno Husika ya Mungu:

Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguswa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Ikiwa Mungu hangevaa umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, kusingekuwa na njia kwa mwanadamu kupokea wokovu huu. Kwa maana mwanadamu hana njia ya kumkaribia, kama vile hakuna mtu aliyeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu aliyeumbwa tu, yaani, kwa kuweka tu neno Lake katika mwili wa nyama Ambao Anakaribia kuwa, Anaweza Yeye binafsi kulifanya neno ndani ya wote wanaomfuata. Ni hapo tu ndipo mwanadamu anaweza kuona na kusikia neno Lake kibinafsi, na zaidi ya hayo kuingia katika umiliki wa neno Lake, na kwa njia hii kuja kuokolewa kikamilifu. Ikiwa Mungu hangefanyika mwili, hakuna mtu wa nyama na damu ambaye angeweza kupokea wokovu mkuu hivyo, wala hakuna hata mtu mmoja angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inahusisha ugumu mwingi usiofikirika, matokeo ambayo yanapatikana mwishowe yanazidi kwa mbali sana kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Kazi ya mwili inahusisha taabu nyingi sana, na mwili hauwezi kuwa na utambulisho mkubwa kama wa Roho, hauwezi kufanya matendo ya kimiujiza kama Roho, sembuse kuwa na mamlaka kama ya Roho. Lakini bado kiini cha kazi inayofanywa na mwili huu usio wa ajabu ni bora zaidi ikilinganishwa na kazi inayofanywa moja kwa moja na Roho, na mwili huu Wenyewe ndio jibu la mahitaji ya wanadamu wote. Kwa wale watakaookolewa, thamani ya Roho ipo chini zaidi ikilinganiswha na ile ya mwili. Kazi ya Roho inaweza kuufikia ulimwengu wote, kuvuka milima yote, mito, maziwa, na bahari, lakini kazi ya mwili kwa ufanisi zaidi inahusiana na kila mtu anayekutana na Yeye. Aidha, mwili wa Mungu katika umbo la kushikika unaweza kueleweka vizuri na kuaminiwa na mwanadamu, na unaweza kuimarisha maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na unaweza kumwachia mwanadamu hisia ya kina zaidi ya matendo halisi ya Mungu. Kazi ya Roho imefungwa sirini, ni vigumu kwa viumbe wenye mwili wa kufa kuielewa, na ni vigumu zaidi kwao kuiona, na hivyo wanaweza kutegemea tu vitu vya kufikirika. Hata hivyo, kazi ya mwili ni ya kawaida, na imejikita katika uhalisi, na ina hekima kubwa sana, na ni ukweli unaoweza kuonekana kwa macho ya mwanadamu; mwanadamu anaweza kupitia uzoefu wa hekima ya Mungu, na hana haja ya kuwa na fikira zake kubwa. Huu ndio usahihi na thamani halisi ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Roho anaweza tu kufanya vitu ambavyo havionekani kwa mwanadamu na ni vigumu kwake kuvifikiria, kwa mfano nuru ya Roho, mguso wa Roho na uongozi wa Roho, lakini kwa mwanadamu mwenye akili, hivi havitoi maana inayoeleweka. Vinatoa tu mguso, au maana ya jumla, na havitoi maelekezo kwa maneno. Hata hivyo, kazi ya Mungu mwenye mwili, ni tofauti sana: Ina mwongozo sahihi wa maneno, ina nia ya wazi, ina malengo ya wazi yanayohitajika. Na hivyo mwanadamu hahitaji kupapasa, au kutumia fikra zake, au kufanya makisio. Huu ndio uwazi wa kazi katika mwili, na tofauti yake kubwa kutoka kwa kazi ya Roho. Kazi ya Roho inafaa tu kwa mawanda finyu, na haiwezi kuchukua kazi ya mwili. Kazi ya mwili inampa mwanadamu malengo halisi zaidi na yanayohitajika na maarifa ya kivitendo zaidi na yenye thamani kuliko kazi ya Roho. Ni kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo ya wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi halisi tu na mwongozo wa wakati sahihi kwa mahitaji ya mwanadamu, na kazi ya kivitendo pekee ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika tabia yake iliyopotoka na kusawijika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake ndiye Anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka. Ingawa Roho ni kiini cha asili ya Mungu, kazi kama hii inaweza tu kufanywa na mwili Wake. Kama Roho angefanya kazi peke Yake, basi haingewezekana kwa kazi Yake kuwa na ufanisi—huu ni ukweli ulio wazi kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kwa kuwa kila mtu anayetafuta ukweli na kutamani kuonekana kwa Mungu, kazi ya Roho inaweza tu kutoa mguso au msukumo, na hisia ya kuona maajabu ambayo hayaelezeki na kufikirika, na hisia ambayo ni kuu, ya juu sana kuliko uwezo wa mwanadamu, na inayotamanika, lakini ambayo pia haifikiwi na haipatikani kwa wote. Mwanadamu na Roho wa Mungu wanaweza tu kutazamana kwa mbali, kana kwamba kuna umbali mkubwa kati yao, na hawawezi kufanana kamwe, kana kwamba mwanadamu na Mungu wametenganishwa na mgawanyiko usioonekana. Kwa hakika, hizi ni fikra za uongo ambazo Roho amempa mwanadamu, ambazo ndiyo sababu Roho na mwanadamu sio wa aina moja, na Roho na mwanadamu hawawezi kuishi pamoja katika ulimwengu mmoja, na kwa sababu Roho hana kitu chochote cha mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hana haja ya Roho, maana Roho hawezi kufanya kazi inayohitajika sana na mwanadamu moja kwa moja. Kazi ya mwili inampatia mwanadamu malengo ya kivitendo ya kufuata, maneno halisi, na hisia kwamba Yeye ni halisi na wa kawaida, kwamba ni mnyenyekevu na wa kawaida. Ingawa mwanadamu anaweza kumwogopa, kwa watu wengi Yeye ni rahisi kuhusiana na Yeye: Mwanadamu anaweza kuuona uso Wake, na kuisikia sauti Yake, na hahitaji kumwangalia kwa kutokea mbali. Mwanadamu anahisi kuwa ni rahisi kuufikia mwili huu, sio wa mbali au usioeleweka, bali unaonekana na kushikika, maana mwili huu upo katika ulimwengu mmoja na mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Wakati Mungu alikuwa bado Hajafanyika mwili, watu hawakuelewa mengi kuhusu kile Alichosema, kwa sababu matamshi Yake yalitoka katika uungu kamili. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulionyeshwa kutoka katika ulimwengu wa kiroho ambao watu wasingeweza kuuona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika ulimwengu wa kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, na Alitoka na kuvuka upeo wa ulimwengu wa kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya kiungu, mapenzi, na mtazamo wake kupitia mambo ambayo wanadamu wangeweza kuyafikiria, vitu ambavyo wangeweza kuviona na kukutana navyo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kuzikubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kufahamu, ili kuwaruhusu wanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu nia Zake na viwango vyake vinavyohitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao, na kwa kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu katika ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa njia ya, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Hivi sasa mwanadamu anaona kuwa kazi ya Mungu kupata mwili ni ya ajabu kweli. Kuna mengi ambayo hayawezi kupatikana na mwanadamu, na kwamba ni mafumbo na maajabu. Kwa hivyo, wengi wamejiwasilisha. Wengine hawajawahi kujiwasilisha kwa mwanadamu yeyote kutoka siku za kuzaliwa kwao, ilhali wanapoyaona maneno ya Mungu siku hii, wanajiwasilisha kikamilifu bila kujua wamefanya hivyo, na hawajaribu kuchunguza au kusema chochote kingine. Binadamu wameanguka chini ya neno na wamesujudu chini ya hukumu ya neno. Kama Roho wa Mungu angewaongelesha wanadamu moja kwa moja, wote wangejiwasilisha kwa sauti hiyo, na kuanguka chini bila maneno ya ufunuo, vile Paulo alivyoanguka chini kukiwa na nuru alipokuwa akisafiri kwenda Damaski. Mungu angeendelea kufanya kazi kwa njia hii, mwanadamu hangeweza kutambua upotovu wake kupitia kwa hukumu ya neno na kupata wokovu. Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Mungu ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili; Ananena na kutekeleza hukumu kwa njia ya vitendo ili kupata matokeo ya hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa kiroho, bali miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Zaidi ya hayo, kazi kama hiyo ingekuwa ngumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hangeweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu Akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa asili na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na Yuko katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Kama kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi isingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa Ameinuliwa zaidi kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na Anaushinda mwili. Ikiwa Roho angefanya kazi hii moja kwa moja, Asingeweza kuhukumu uasi wote wa mwanadamu, na Asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kupitia dhana za mwanadamu kuhusu Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala Hawezi kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana na upinzani wa mwanadamu Kwake, Anafichua uasi wote wa wanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtiifu, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika dhana na kuwa na maarifa, na kutoka kwa kukataliwa hadi kupendwa—haya ndiyo matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anaokolewa tu kwa kukubali hukumu Yake, mwanadamu anakuja tu kumjua hatua kwa hatua kupitia maneno ya kinywa Chake, mwanadamu anashindwa na Yeye wakati wa upinzani wake Kwake, na anapata uzima kutoka Kwake wakati wa kukubali kuadibu Kwake. Hii yote ni kazi ya Mungu mwenye mwili, na sio kazi ya Mungu katika utambulisho Wake kama Roho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba, Anaweza kuacha maneno na mawaidha sahihi, na mapenzi Yake mahususi kwa ajili ya wanadamu kwa wale wanaomfuata, ili baadaye wafuasi Wake waweze kwa usahihi zaidi na kwa uthabiti zaidi kupitisha kazi Yake yote katika mwili, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote, kwa wale wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili Anahitimisha enzi ambapo ni mgongo wa Yehova pekee ndio ulioonekana kwa wanadamu, na pia Anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Hasa, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya kivitendo zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la muhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida, ambaye ni Mwenye haki na mtakatifu, ambaye Anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kufafanua mafumbo na hatima ya wanadamu, ambaye Aliwaumba wanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye Amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili kwa niaba ya Roho wa Mungu. Wakati Mungu anapofanya kazi katika mwili Wake, wale wanaomfuata wanakuwa hawatafuti tena na kupapasa vitu hivyo vinavyoonekana kuwa vipo na ambavyo havipo, na wanaacha kukisia mapenzi ya Mungu asiyeonekana. Mungu anapoeneza kazi Yake katika mwili, wale wanaomfuata wataieneza kazi ambayo Ameifanya katika mwili kwa dini na madhehebu yote, na watazungumza maneno Yake yote katika masikio ya wanadamu wote. Yote yanayosikiwa na wale wanaoipokea injili Yake yatakuwa ni ukweli wa kazi Yake, yatakuwa ni mambo ambayo mwanadamu ameyashuhudia na kuyaona binafsi, na utakuwa ukweli na sio uvumi. Ukweli huu ni ushahidi ambao kupitia huo Anaeneza kazi, na pia ni zana ambazo Anazitumia katika kueneza kazi. Bila uwepo wa ukweli, injili Yake isingeweza kuenea katika nchi zote na maeneo yote; bila ukweli bali tu kwa fikira za mwanadamu, Asingeweza kufanya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Roho hagusiki na mwanadamu, na wala Hawezi kuonekana na mwanadamu, na kazi ya Roho haiwezi kuacha ushahidi au ukweli wowote zaidi wa kazi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu kamwe hataweza kuuona uso halisi wa Mungu, na siku zote ataamini katika Mungu asiye yakini ambaye hayupo. Mwanadamu hataweza kuutazama uso wa Mungu, hataweza kusikia maneno yaliyozungumzwa na Mungu moja kwa moja. Mawazo ya mwanadamu, hata hivyo, ni matupu, na hayawezi kuchukua nafasi ya uso halisi wa Mungu; tabia ya asili ya Mungu, na kazi ya Mungu Mwenyewe haiwezi kuigwa na mwanadamu. Mungu wa mbinguni asiyeonekana na kazi Yake inaweza kuletwa tu duniani na Mungu mwenye mwili ambaye binafsi Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Hii ndiyo njia bora zaidi ya Mungu kuonekana kwa mwanadamu, ambayo kwayo mwanadamu anamwona Mungu na kuujua uso wa kweli wa Mungu, na haiwezi kufanikishwa na Mungu asiyekuwa katika mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Iliyotangulia: 2. Kupata Mwili Ni Nini? Ni Nini Kiini cha Kupata Mwili?

Inayofuata: 4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp