Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Kazi yote ya miaka 6,000 imebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova bado hakuwa amepanga hatua ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; hatua ya pili ya kazi, ile ya neema; au hatua ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kupitia hili Angeweza kuushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi Yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima kwa usimamizi wa miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, kabla kuumba dunia, Hakuwa ameandika mpango kama huo kwa mtindo wa kitu kama “Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Binadamu.” Katika kazi ya Mungu, Anaonyesha moja kwa moja kile Alicho; Hapigi bongo kuunda mpango. Bila shaka, manabii wengi wameongea unabii mwingi, lakini bado haiwezi kusemekana kwamba kazi ya Mungu siku zote imekuwa ya upangaji mpango dhahiri; unabii ulitolewa kulingana na kazi halisi ya Mungu. Kazi Zake zote ni kazi halisi zaidi. Hufanya kazi Yake kufutana na maendeleo ya kila enzi, na inazingatia jinsi mambao yanabadilika. Kwake Yeye, kutekeleza kazi ni sawa na kutoa dawa kutibu ugonjwa; Akiwa anafanya kazi Yake, Anaangalia na kuendelea na kazi Yake kulingana na kile Alichoona. Katika kila hatua ya kazi Yake, Anaweza kuonyesha hekima Yake ya kutosha na kuelezea uwezo Wake wa kutosha; Anafichua hekima Yake ya kutosha na mamlaka Yake ya kutosha kulingana na kazi ya enzi hiyo husika na kuruhusu yeyote kati ya watu waliorudishwa na Yeye wakati wa enzi hizo kuweza kuiona tabia Yake nzima. Anawaruzuku watu na kutekeleza kazi Anayofaa kufanya kulingana na kazi ambayo lazima ifanywe katika kila enzi; Anawaruzuku watu kulingana na kiwango ambacho Shetani amewapotosha. Ilikuwa namna hii wakati Yehova aliwaumba Adamu na Hawa mwanzoni ili kuwaruhusu kumdhihirisha Mungu katika dunia na kuwa na mashahidi wa Mungu miongoni mwa uumbaji, lakini Hawa alitenda dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka; Adamu alifanya vivyo hivyo, na kwa pamoja wakiwa kwenye bustani wakalila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hivyo basi, Yehova alikuwa na kazi ya ziada ya kutenda miongoni mwao. Aliuona uchi wao na kuifunika mili yao kwa nguo ziliyotengenezwa kutoka kwa ngozi za wanyama. Kufuatia haya, Alimwambia Adamu “Kwa sababu umesikiliza sauti ya mkeo, na umekula kutoka kwa mti ule, ambao Nilikuamuru, nikisema, usile kutoka kwa mti huo: udongo umelaaniwa kwa sababu yako … mpaka urudi udongoni, kwani ulitolewa hapo: kwa kuwa wewe ni mavumbi, na utarudi mavumbini.” Kwa mwanamke Akasema, “Nitazidisha sana sikitiko lako na kupata kwako watoto; utazaa watoto kwa sikitiko; na ashiki yako itakuwa kwa mume wako, na atatawala juu yako.” Kuanzia hapo kuendelea, aliwafukuza kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuwafanya waishi nje ya bustani, kama vile binadamu wa kisasa afanyavyo duniani. Mungu alipomwumba mwanadamu mwanzoni kabisa, Hakupanga kumfanya binadamu ajaribiwe na nyoka baada ya kuumbwa na kisha kuwalaani binadamu na nyoka. Kwa hakika hakuwa na mpango wa aina hii; ilikuwa tu maendeleo ya mambo yaliyompa kazi hii mpya miongoni mwa uumbaji Wake. Baada ya Yehova kutekeleza kazi Yake miongoni mwa Adamu na Hawa kwenye ardhi, binadamu waliendelea kuimarika kwa miaka elfu kadhaa mpaka “Yehova aliona kwamba uovu wa mwanadamu ulikuwa mkubwa ulimwenguni, na kuwa kila wazo la fikira za moyo wake lilikuwa ovu tu daima. Na Yehova akajuta kwamba alikuwa amemwumba mwanadamu ulimwenguni, na akawa na huzuni moyoni mwake. … Lakini Nuhu alipata neema katika macho ya Yehova.” Wakati huu Yehova alikuwa na kazi mpya zaidi, kwa ajili binadamu Aliowaumba walikuwa wamezidisha dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka. Kwa mujibu wa hali hizi, Yehova aliichagua familia ya Nuhu kutoka miongoni mwa watu hawa na kuwanusuru, na kutekeleza kazi Yake ya kuuangamiza ulimwengu kwa gharika. Binadamu wameendelea kukua kwa njia hii mpaka siku ya leo, wakiendelea kupotoka kwa kukithiri, na wakati maendeleo ya binadamu yafikapo kilele, utakuwa ndio mwisho wa binadamu. Kuanzia mwanzo kabisa hadi mwisho wa ulimwengu, ukweli wa ndani wa kazi Yake siku zote umekuwa hivi. Hii ni sawa na namna ambavyo watu watakavyoainishwa kulingana na aina yao; hii ni mbali na hali ya kwamba kila mtu anayeamuliwa kabla kwa kikundi fulani; bali kila mtu anaainishwa polepole baada ya kupitia mchakato wa maendeleo. Mwishowe, yeyote ambaye hawezi kuokolewa kwa ukamilifu atarudishwa kwa mababu zake. Hamna kati ya kazi za Mungu miongoni mwa binadamu iliyokuwa tayari imetayarishwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu; badala yake, ilikuwa ni maendeleo ya mambo yaliyomruhusu Mungu kutekeleza kazi Yake hatua kwa hatua kwa uhalisia zaidi na kwa kimatendo zaidi miongoni mwa binadamu. Hivi ni kama ambavyo Yehova Mungu hakumwumba nyoka ili kumjaribu mwanamke. Haukuwa mpango Wake mahususi, wala halikuwa jambo ambalo Alikuwa ameliamua kimakusudi kabla; mtu anaweza kusema kwamba hili halikutarajiwa. Hivyo basi ilikuwa ni kwa sababu ya hili ndiyo Yehova aliwatimua Adamu na Hawa kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuapa kutowahi kumwumba binadamu tena. Lakini hekima ya Mungu inagunduliwa tu na watu kwenye msingi huu, kama tu ile hoja Niliyotaja awali: “Hekima Yangu hutumika kutokana na njama za Shetani.” Haikujalisha ni vipi ambavyo binadamu walizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Baada ya binadamu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayewapotosha binadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajaruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu waovu na kuwatuza wema. Amepambana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kitii mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu duniani kipumzike chini ya kigonda Chake na pia, Huwafanya wale waovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu wajipate katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake. Alikuwa hajawahi kufichua hekima Yake kabla ya uwepo wa binadamu, kwani Hakuwa na maadui kule mbinguni, juu ya dunia, au kwenye ulimwengu kwa ujumla, na hakukuwa na nguvu za giza zilizoshambulia chochote katika maumbile. Baada ya malaika mkuu kumsaliti, Aliwaumba binadamu kwenye dunia, na ilikuwa ni kwa sababu ya binadamu ndiyo Alianza rasmi vita Vyake vya milenia nzima dhidi ya Shetani, malaika mkuu, vita ambavyo vilizidi kushamiri kwa kila hatua iliyopigwa. Uweza Wake na hekima vinapatikana katika kila mojawapo ya awamu hizi. Ni katika muda huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na duniani huweza kushuhudia hekima ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu. Angali anatekeleza kazi Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake; Anawaruhusu kuona ule ukweli wa ndani katika kila hatua ya kazi, kuona hasa ni vipi mnaweza kuelezea uweza wa Mungu na hasa ni vipi mnavyoweza kuelezea uhalisia wa Mungu.

Kuhusu Yuda kumsaliti Yesu, watu wengine hushangaa: Je, hili halikuwa liamuliwa kabla ya uumbaji wa ulimwengu? Kwa hakika, Roho Mtakatifu alikuwa amepanga haya kulingana na uhalisi wakati huo. Ilitukia tu kwamba kulikuwepo mtu kwa jina la Yuda ambaye siku zote angebadhiri fedha. Hivyo basi alichaguliwa kutekeleza wajibu huu na kuwa mwenye huduma katika njia hii. Huu ni mfano halisi wa kutumia rasilimali za mahali palepale. Yesu hakujua hili kwanza; Alilijua hili tu Yuda alipolifichuliwa baadaye. Kama mtu mwingine angeweza kutekeleza wajibu huu, basi mtu mwingine angeweza kufanya hivi badala ya Yuda. Kile ambacho kiliamuliwa awali kiliweza hasa kufanywa wakati mmoja na Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu siku zote inafanywa kwa hiari; wakati wowote Anapopanga kazi Yake, Roho Mtakatifu ataitekeleza. Kwa nini sikuzote Nasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni ya uhalisi? Kwamba siku zote ni mpya na haijawahi kuwa zee, na siku zote inakuwa na uhai zaidi? Kazi Yake bado haikuwa imepangwa wakati ulimwengu ulipoumbwa; hivi sivyo kamwe ilivyofanyika! Kila hatua ya kazi hufikia athari yake bora kwa wakati wake mwafaka, nazo haziingiliani kati. Kunao wakati mwingi ambapo mipango katika akili zako hazilingani kamwe na kazi ya hivi punde ya Roho Mtakatifu. Kazi Yake si rahisi kama wanavyofikiria watu, wala si ngumu kama watu wengi wanavyofikiria; inajumuisha kuwaruzuku watu wakati wowote na mahali popote kulingana na mahitaji yao ya sasa. Hakuna aliye wazi zaidi kuhusu kiini halisi cha watu kama Yeye, na ni kwa sababu hii mahususi ndiposa hakuna kinachoweza kufaa mahitaji ya kihalisi ya watu kama vile ambavyo kazi Yake inavyofanya. Hivyo basi, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kazi Yake ilipangiwa milenia kadha mbele. Anavyofanya kazi miongoni mwenu sasa, kulingana na hali yenu, Yeye pia Anafanya kazi na kuongea wakati wowote na mahali popote. Wakati watu wako katika hali fulani, Yeye huongea maneno hayo ambayo hasa ndiyo wanayohitaji ndani yao. Ni kama hatua ya kwanza ya kazi Yake, nyakati za kuadibu. Baada ya nyakati za kuadibu, watu walionyesha tabia fulani, walikuwa na mienendo ya kuasi katika njia fulani, hali fulani nzuri ziliibuka, hali fulani hasi pia ziliibuka, na mipaka ya juu ya uhasi huu ikafikia kiwango fulani. Mungu alifanya kazi Yake kwa msingi wa mambo haya yote, na hivyo basi Alichukua haya yote ili kuweza kutimiza athari bora zaidi kwa ajili ya kazi Yake. Anatekeleza tu kazi Yake ya kuruzuku miongoni mwa watu kulingana na hali zao za sasa. Yeye Hutekeleza kila hatua ya kazi Yake kulingana na hali halisi za watu. Viumbe wote wamo mikononi Mwake; Angekosa kuujua? Kwa mujibu wa hali za watu, Mungu hutekeleza hatua inayofuata ya kazi inayofaa kufanywa, wakati na mahali popote. Kazi hii haikupangwa maelfu ya miaka kabla; hii ni dhana ya kibinadamu tu! Yeye hufanya kazi huku akiangalia athari za kazi Yake, na kazi Yake inaendelea kuwa ya kina na kukua; Anapoendelea kuangalia matokeo ya kazi Yake, Anatekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Yeye hutumia mambo mengi ili kuingia kwenye mpito hatua kwa hatua na kufanya kazi Yake mpya kuonekana na watu baada ya muda. Aina hii ya kazi inaweza kuruzuku mahitaji ya watu, kwani Mungu anawajua watu vizuri mno. Hivi ndivyo Anavyotekeleza kazi Yake kutoka mbinguni. Vilevile, Mungu mwenye mwili anafanya kazi Yake kwa njia iyo hiyo, Akipangilia kulingana na uhalisi na kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Hakuna yoyote kati ya kazi Zake iliyopangwa kabla ya ulimwengu kuumbwa, wala kupangwa kwa umakinifu kabla ya wakati. Miaka elfu mbili baada ya ulimwengu kuumbwa, Yehova aliona binadamu walikuwa wamepotoka sana kiasi cha kwamba Alikitumia kinywa cha nabii Isaya kutabiri kwamba baada ya Enzi ya Sheria kukamilika, Angetekeleza kazi Yake ya kukomboa binadamu katika Enzi ya Neema. Huu ulikuwa mpango wa Yehova, bila shaka, lakini mpango huu pia kufanywa kulingana na hali ambazo Aliangalia wakati huo; bila shaka Yeye hakuufikiria mara moja baada ya kumwumba Adamu. Isaya alitabiri tu, lakini Yehova hakuwa amefanya matayarisho ya mapema ya kazi hii wakati wa Enzi ya Sheria; badala yake, Alianza kazi hii katika mwanzo wa Enzi ya Neema, wakati mjumbe alipojitokeza katika ndoto ya Yusufu na kumpa yeye nuru, akimwambia kwamba Mungu angekuwa mwili, na hivyo kazi Yake ya kupata mwili ikaanza. Kama watu wanavyofikiria Mungu hakujitayarishia kazi Yake ya kuwa mwili baada ya kuumba ulimwengu; jambo hili liliamuliwa tu kulingana na kiwango cha maendeleo ya binadamu na hadhi ya vita Vyake na Shetani.

Mungu anapokuja kuwa mwili, Roho Wake anamshukia binadamu; kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauvaa mwili. Anafanya kazi Yake duniani, na badala ya kuleta naye hatua mbalimbali zilizozuiliwa, kazi hii haina mipaka kamwe. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya katika mwili bado inaamuliwa na athari ya kazi Yake, na Yeye hutumia mambo haya kuamua urefu wa muda ambao Atafanya kazi akiwa katika mwili. Roho Mtakatifu hufichua moja kwa moja kila hatua ya kazi Yake; Yeye huchunguza kazi Yake anapozidi kuendelea; si jambo la kimwujiza kiasi cha kupanua ile mipaka ya kufikiriwa na binadamu. Hii ni kama kazi ya Yehova katika kuumba mbingu na nchi na vitu vyote; Aliweza kupanga na kufanya kazi wakati huo huo. Alitenga nuru kutoka kwenye giza, na asubuhi pamoja na jioni vyote vikawepo—hii ilichukua siku moja. Siku ya pili Aliumba mbingu, ambayo pia ilichukua siku moja na kisha Akaiumba nchi, bahari na viumbe vilivyojaa ndani, pia ikichukua siku nyingine moja. Hili liliendelea hivyo hadi siku ya sita, wakati Mungu alipomwumba binadamu na kumwacha asimamie viumbe hivi vyote juu ya nchi, mpaka siku ya saba, Alipokuwa amemaliza kuumba viumbe vyote, na akapumzika. Mungu alibariki siku ya saba na kuitenga kuwa siku takatifu. Aliiamulia siku hii takatifu baada ya kuviumba viumbe vyote, na wala si kabla ya kuviumba. Kazi hii pia ilitekelezwa kwa hiari; kabla ya kuviumba viumbe vyote, Hakuamua kuumba ulimwengu kwa siku sita na kupumzika siku ya saba; ukweli hauko hivi hata kidogo. Hakusema hili, wala Hakupanga hili. Kwa vyovyote vile Hakusema kwamba uumbaji wa viumbe vyote ungekamilishwa katika siku ya sita na kwamba Angepumzika katika siku ya saba; badala yake, Aliumba kulingana na kile kilichokuwa kikionekana kizuri Kwake. Punde Alipomaliza kuumba kila kitu, tayari ilikuwa ni siku ya sita. Kama ingekuwa ni siku ya tano Alipomaliza kuumba kila kitu, Angepangilia basi siku ya sita kuwa siku takatifu; hata hivyo, Alimaliza kuumba kila kitu katika siku ya sita, na hivyo basi siku ya saba ikawa siku takatifu, ambayo imepitishwa hadi siku ya leo. Hivyo basi, kazi Yake ya sasa inatekelezwa kwa njia ii hii. Yeye huongea na kuwaruzuku kulingana na hali zenu. Yaani, Roho huongea na kufanya kazi kulingana na hali za watu; Roho huangalia kila kitu na kufanya kazi wakati wowote na mahali popote. Kile Ninachofanya, kwa mfano, kuwawekea na kuwapa bila kiwazo ni kile mnachohitaji. Kwa hivyo hakuna kazi Yangu iliyo tofauti na uhalisi; yote ni halisi, kwani nyinyi nyote mnajua ya kwamba “Roho wa Mungu hulinda vyote.” Kama haya yote yalikuwa yameamuliwa kabla ya wakati, huoni kwamba mambo yangekuwa yamekwisha amuliwa? Unafikiri kwamba Mungu alifanya kazi kwa milenia sita nzima na kisha kuamulia kabla binadamu kama waasi, wapingaji, waongo na wadanganyifu, kama kuwa na upotovu wa mwili, tabia za kishetani, ashiki za macho na kujihusisha kwao kwa mambo yasiyofaa. Haya yote hayakupangwa na Mungu, lakini yalitokana na upotoshaji wa Shetani. Baadhi watasema, “Shetani naye hakuwa ndani ya mfumbato wa Mungu? Mungu alikuwa amepanga awali kwamba Shetani angepotosha binadamu kwa njia hii, na baada ya hapo Akatekeleza kazi Yake miongoni mwa binadamu.” Je, Mungu kwa kweli angepanga awali Shetani kuwapotosha binadamu? Anayo hamu mno ya kuwaruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida na kibinadamu; Angenyanyasa maisha ya binadamu? Kama hali ni hivyo, kumshinda Shetani na kuokoa binadamu si kungekuwa jitihada za bure bilashi? Je, uasi wa binadamu ungeamuliwaje kabla? Ulitokana na kunyanyaswa na Shetani kwa hali halisi; ungepangwa vipi awali na Mungu? Shetani aliye ndani ya mfumbato wa Mungu ambaye mnamwelewa na Shetani ndani ya mfumbato wa Mungu ambaye Ninamzungumzia ni tofauti sana. Kulingana na kauli zenu kwamba “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake,” Shetani asingemsaliti Yeye. Je, wewe hujasema kwamba Mungu ni mwenyezi? Maarifa yenu ni ya kidhahania mno na hayaambatani na uhalisi; mwanadamu kamwe hawezi kuelewa fikira za Mungu, wala mwanadamu hawezi kamwe kuelewa busara ya Mungu! Mungu ni mwenyezi; huu si uwongo kamwe. Malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa sababu Mungu alimpa sehemu ya mamlaka awali. Bila shaka, tukio hili halikutarajiwa, kama vile Hawa kushindwa na jaribio la nyoka. Hata hivyo, bila kujali ni vipi ambavyo Shetani hutekeleza usaliti wake, tofauti na Mungu, yeye si mwenyezi. Kama vile mlivyosema, Shetani ni mwenye nguvu; haijalishi ni nini atakachofanya, mamlaka ya Mungu humshinda siku zote. Hii ndiyo maana ya kweli katika ule msemo “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake.” Hivyo basi, vita Vyake na Shetani lazima vitekelezwe hatua moja baada ya nyingine; aidha, Yeye hupanga kazi Yake katika kuitikia ujanja wa Shetani. Hivi ni kusema, kulingana na enzi, Anawaokoa watu na kufichua hekima na uweza Wake. Vilevile, kazi za siku za mwisho haikuamuliwa mapema, kabla ya Enzi ya Neema; kuamuliwa kabla hakufanywi kwa njia ya kawaida kama hii: mwanzo, kwa kuifanya tabia ya nje ya binadamu ibadilike; pili, kumweka chini ya uongozi binadamu apokee adabu na majaribio yake; tatu, kusababisha binadamu kupitia jaribio la kifo; nne, kumfanya binadamu apitie nyakati za kumpenda Mungu na aonyeshe uamuzi wa kiumbe kilichoumbwa; tano, kumruhusu binadamu kuweza kuona mapenzi ya Mungu na kumjua Yeye kikamilifu; na hatimaye, kisha kumkamilisha binadamu. Hakupanga mambo haya yote wakati wa Enzi ya Neema; badala yake, Alianza kuyapanga katika enzi ya sasa. Shetani yumo kazini, kama vile alivyo Mungu. Shetani huonyesha tabia yake potovu, huku naye Mungu huongea moja kwa moja na kufichua baadhi ya mambo muhimu. Hii ndiyo kazi inayofanywa leo, na kanuni ii hii ya kufanya kazi ilitumika zamani, baada ya ulimwengu kuumbwa.

Kwanza Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba nyoka. Miongoni mwa vitu vyote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu nyingi sana; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hii ili kufaidika naye. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa kisha waliweza kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova angejua kwamba nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini Akawaweka wote pale ndani ya bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya kwa nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Alinuia wao walile hilo tunda? Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kushikwa katika ujanja wa yule nyoka. Hatimaye Alimlaani nyoka, na Akamlaani Adamu na Hawa pia. Wakati hao wawili walilila tunda lile la mti, Yehova hakujua kabisa kwamba walikuwa wakifanya hivyo. Binadamu walipotoka hadi kufikia kiwango cha kuwa na uovu na uasherati wa kimapenzi, hadi kufikia hatua ambayo mambo yote waliyokuwa nayo katika mioyo yao yalikuwa maovu na yasiyo ya haki; yote yalikuwa machafu. Yehova hivyo basi alijutia kuumba binadamu. Baadaye Alitekeleza kazi Yake ya kuharibu ulimwengu kwa gharika, ambayo Nuhu na watoto wake wa kiume walinusurika. Baadhi ya mambo kwa hakika hayajaendelea na kuwa ya mwujiza kama vile watu wanavyoweza kufikiria. Baadhi wanauliza: “Kwa sababu Mungu alijua malaika mkuu angemsaliti Yeye, kwa nini Alimwumba?” Huu ndio ukweli: Wakati dunia haikuwepo bado, malaika mkuu ndiye aliyekuwa malaika mkuu zaidi mbinguni. Alikuwa na mamlaka juu ya malaika wote kule mbinguni; haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ambayo Mungu alimpa. Kando na Mungu, yeye ndiye aliyekuwa malaika mkubwa zaidi mbinguni. Wakati Mungu alipouumba binadamu baadaye, malaika mkuu alitekeleza usaliti mkuu zaidi dhidi ya Mungu duniani. Nasema kwamba alimsaliti Mungu kwa sababu alitaka kuwasimamia binadamu na kuzidi mamlaka ya Mungu. Ni malaika mkuu ambaye alimjaribu Hawa hadi akatenda dhambi; alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuanzisha ufalme wake duniani na kuwafanya binadamu wamsaliti Mungu na kumtii yeye badala yake. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo vilimtii; malaika walimtii sawa na vile ambavyo watu wa dunia walivyomtii. Ndege na wanyama, miti, misitu, milima, mito na vitu vyote vilivyo duniani vilikuwa chini ya utunzaji wa binadamu—yaani, Adamu na Hawa—huku nao Adamu na Hawa wakimtii. Malaika mkuu hivyo basi alitamani kuzidi mamlaka ya Mungu na kumsaliti Mungu. Baadaye aliwaongoza malaika wengi kumsaliti Mungu, ambao baadaye walikuja kuwa pepo wachafu mbalimbali. Je, maendeleo ya binadamu hadi siku ya leo hayajasababishwa na upotovu wa malaika mkuu? Binadamu wako tu namna walivyo leo kwa sababu malaika mkuu alimsaliti Mungu na kuwapotosha binadamu. Kazi hii ya hatua kwa hatua haiko karibu kuwa ya dhahania na rahisi kama vile watu wanavyofikiria hata kidogo. Shetani alitekeleza usaliti wake kwa sababu fulani, ilhali watu hawawezi kufahamu kitu rahisi kama hicho. Kwa nini Mungu akaziumba mbingu na dunia na vitu vyote, na pia kumwumba Shetani? Kwa sababu Mungu anamdharau Shetani sana, naye Shetani ni adui Wake, kwa nini akamwumba Shetani? Kwa kumwumba Shetani, hakuwa Anamwumba adui? Mungu kwa hakika hakuumba adui; badala yake, Alimwumba malaika, na baadaye malaika akamsaliti Yeye. Hadhi yake ilikuwa kubwa mno kiasi cha kwamba alitaka kumsaliti Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba hii ilikuwa ni sadfa, lakini ulikuwa pia mwelekeo usioepukika. Ni sawa na vile ambavyo mtu bila kuepuka atakufa akiwa na umri fulani; mambo yameendelea tayari hadi kwa hatua fulani. Kunao hata wapumbavu wengine wanaosema: “Kwa sababu Shetani ni adui Yako, kwa nini Ukamwumba? Kwani hukujua kuwa malaika huyu mkuu angekusaliti Wewe? Kwani Huwezi kukazia macho kutoka kwa milele hadi milele? Kwani Wewe huijui asili yake? Kwa sababu Ulijua waziwazi kuwa angekusaliti Wewe, basi kwa nini Ukamfanya kuwa malaika mkuu? Hata kama mtu atapuuza suala la usaliti wake, bado aliwaongoza malaika wengi sana na akashuka hadi kwa ulimwengu wa binadamu wenye kufa ili kuwapotosha binadamu; hadi siku ya leo Umeshindwa kukamilisha mpango Wako wa usimamizi wa miaka elfu sita.” Je, maneno haya ni sahihi? Unapofikiria kwa njia hii, hujiweki katika matatizo mengi zaidi kuliko yanayohitajika? Wengine bado husema: Kama Shetani asingewapotosha binadamu hadi siku ya leo, Mungu asingewaokoa binadamu kwa njia hii. Katika mfano huu, hekima na uweza wa Mungu vyote vingekuwa havionekani; hekima Yake ingejionyesha wapi? Hivyo basi Mungu alikiumba kizazi cha binadamu kwa minajili ya Shetani; katika siku za baadaye, Mungu angefichua uweza Wake—vinginevyo, binadamu angewezaje kugundua hekima ya Mungu? Kama binadamu asingempinga Yeye na kumwasi Yeye, isingehitajika kwa vitendo Vyake kujionyesha. Kama viumbe wote wangemwabudu Yeye na kumtii Yeye, Asingekuwa na kazi ya kufanya. Hali hii ni mbali zaidi na uhalisi wa mambo, kwani hakuna chochote kichafu kuhusu Mungu, na hivyo basi Hawezi kuumba uchafu. Yeye hufichua vitendo Vyake sasa ili kuweza tu kuwashinda kabisa adui Zake, ili kuokoa binadamu, ambao Aliwaumba, ili kuyashinda mapepo na Shetani, ambao wanamchukia, wanamsaliti na wanampinga, ambao walikuwa chini ya utawala Wake na alikuwa Wake mwanzoni kabisa; Anataka kuwashinda hawa mapepo na katika kufanya hivyo kuufichua uweza Wake kwa vitu vyote. Binadamu na vitu vyote vilivyomo duniani sasa hivi vinamilikiwa na Shetani na katika umiliki wa waovu. Mungu anataka kuvifichua vitendo Vyake kwa vitu vyote ili watu waweze kumjua Yeye, na hivyo kuishia kumshinda Shetani na kuwaangamiza kabisa adui Zake. Uzima wa kazi hii unakamilishwa kupitia kufichua matendo Yake. Viumbe Vyake vyote vimemilikiwa na Shetani, na hivyo basi Angependa kuufichua uweza Wake kwa viumbe hivyo, na hivyo kumshinda Shetani. Kama Shetani asingekuwepo, Asingehitaji kuyafichua matendo Yake. Kama usingekuwa usumbufu wa Shetani, Angewaumba binadamu na kuwaongoza kuishi katika Bustani ya Edeni. Kwa nini Hakuwahi kufichua vitendo Vyake vyote kwa malaika au malaika mkuu kabla ya kusalitiwa na Shetani? Kama malaika na malaika mkuu wangalimjua Yeye, na pia kumtii Yeye pale mwanzoni, basi Asingetekeleza vile vitendo vya kazi visivyo na maana. Kwa sababu ya uwepo wa Shetani na mapepo, watu humpinga na wanajazwa hadi pomoni na tabia ya uasi, na hivyo basi Mungu angependa kufichua vitendo Vyake. Kwa sababu Angependa kupigana vita na Shetani, lazima Atumie mamlaka Yake kumshinda Shetani na kutumia vitendo Vyake vyote kumshinda Shetani; kwa njia hii, kazi Yake ya wokovu Anayotekeleza miongoni mwa binadamu itawafanya watu waone hekima na uweza Wake. Kazi anayofanya Mungu leo ni yenye maana na haifanani hata kidogo kile watu wengine husema: “Je, kazi hii Unayofanya haihitilafiani? Je, hujisumbui tu na huu mfululizo wa kazi? Ulimwumba Shetani, kisha ukamruhusu Akakusaliti na kukupinga Wewe. Uliwaumba binadamu, na kisha ukawakabidhi kwa Shetani, na Ukaruhusu Adamu na Hawa wajaribiwe. Kwa sababu uliyafanya mambo haya yote kimakusudi, kwa nini Unawachukia binadamu? Kwa nini Unamchukia Shetani? Mambo haya si ya kujitungia Mwenyewe? Kuna nini cha Wewe kuchukia?” Watu wengi wa kipumbavu watasema hayo. Wanatamani kumpenda Mungu, lakini mioyoni mwao wanalalamika kumhusu Mungu—ukinzani kweli! Wewe huelewi ukweli, unazo fikira nyingi sana za kimiujiza, na pia unadai kwamba hili ni kosa la Mungu—wewe ni mpumbavu kweli! Ni wewe unayechezacheza na ukweli; si kosa la Mungu! Baadhi ya watu hata watalalamika na kulalamika: “Ni wewe uliyemwumba Shetani, na ni Wewe uliyemrusha Shetani hadi katika ulimwengu wa mwanadamu na uliyemkabidhi binadamu kwake. Binadamu wana tabia ya kishetani; badala ya kuwasamehe, Unawachukia sana kwa kiwango fulani. Mwanzoni Uliwapenda binadamu kwa kiwango fulani, na sasa Unawachukia sana binadamu. Ni Wewe unayewachukia sana na kuwapenda binadamu—maelezo ya haya ni yapi? Je, huu si ukinzani?” Bila kujali ni vipi mnavyoangalia suala hili, hili ndilo lililofanyika mbinguni; malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa njia hii, nao binadamu wakapotoshwa kwa njia hii, na wakaendelea mpaka leo kwa njia hii. Bila kujali ni vipi mnavyolisema, hii ndiyo hadithi yote. Hata hivyo, lazima muelewe kwamba Mungu anaifanya kazi ya leo ili kuwaokoa nyinyi, na ili kumshinda Shetani.

Kwa sababu malaika hasa walikuwa wanyonge na hawakuwa na uwezo wowote, walikuwa mwenye kiburi wakati walipewa mamlaka, hasa malaika mkuu, ambaye hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi kuliko ile ya malaika mwingine yeyote. Malaika mkuu alikuwa ndiye mfalme wa malaika wote. Aliwaongoza mamilioni ya malaika, na chini ya Yehova mamlaka yake yalizidi yale ya malaika yeyote mwingine. Alitaka kufanya hivi na vile, na kuwaongoza malaika hadi ulimwenguni mwa binadamu ili kuutawala ulimwengu. Mungu alisema kwamba Yeye huutawala ulimwengu; malaika mkuu akasema kwamba ulimwengu ulikuwa wake wa kutawala, na kuanzia hapo akamsaliti Mungu. Mbinguni, Mungu alikuwa ameuumba ulimwengu mwingine. Malaika mkuu akataka kuutawala ulimwengu huu na pia kushuka chini kwenye ulimwengu wa binadamu. Je, Mungu angemruhusu kufanya hivi? Hivyo basi, Alimpiga malaika mkuu na kumtimua chini hadi katikati ya anga. Tangu hapo alipowapotosha binadamu, Mungu amefanya vita dhidi yake ili kuwaokoa binadamu; Ametumia milenia hizi sita kumshinda. Dhana yenu ya mwenyezi Mungu hailingani na kazi ambayo Mungu anatekeleza sasa; haifanyi kazi katika kutenda na ni ya upumbavu ajabu! Kwa hakika, Mungu alitangaza malaika mkuu kuwa adui Yake baada tu ya malaika mkuu kumsaliti Yeye. Ilikuwa kutokana tu na kusaliti kwake Mungu ndiposa aliwakandamiza binadamu baada ya kuwasili katika ulimwengu wa binadamu, na ilikuwa kwa sababu hii ndiposa binadamu waliendelea hivyo hadi kwa hatua hii. Kufuatia haya, Mungu alikula kiapo na Shetani: “Nitakushinda wewe na kuwaokoa binadamu, viumbe Wangu.” Shetani hakushawishika wakati wa mwanzo na akasema, “Ni nini kwa hakika unachoweza kunifanyia mimi? Wewe kweli unaweza kuniangusha hadi katikati ya anga? Wewe unaweza kwa kweli kunishinda mimi?” Baada ya Mungu kumwangusha hadi katikati ya anga, Hakumtilia maanani tena na kisha Alianza kuwaokoa binadamu na kufanya kazi Yake mwenyewe, licha ya usumbufu ulioendelea kutoka kwa Shetani. Kila kitu ambacho Shetani angeweza kufanya kilitokana na nguvu alizopewa na Mungu; alichukua vitu hivi pamoja naye hadi katikati ya anga na amevihifadhi hadi leo. Alipomwangusha malaika mkuu hadi katikati ya anga, Mungu alimwangusha hadi angani lakini hakuchukua mamlaka yake, na hivyo basi aliendelea kuwapotosha binadamu. Mungu, kwa upande mwingine, Alianza kuwaokoa binadamu, ambao Shetani alikuwa amewapotosha baada ya kuumbwa kwao. Mungu hakufichua vitendo Vyake wakati akiwa mbinguni; hata hivyo, kabla ya kuiumba dunia, Aliwaruhusu watu katika ulimwengu Aliouumba mbinguni kuona vitendo Vyake na hivyo kuwaongoza watu juu mbinguni. Aliwapa hekima na akili, na kuwaongoza watu hao kuishi katika ulimwengu huo. Kiasili, hakuna kati yenu ambaye amewahi kusikia haya awali. Baadaye, baada ya Mungu kuumba binadamu, malaika mkuu alianza kuwapotosha binadamu; duniani, binadamu wote walikuwa katika machafuko. Ulikuwa ni wakati huu tu ambapo Alianza vita Vyake dhidi ya Shetani, na ulikuwa ni wakati huu tu ambapo watu waliona vitendo Vyake. Mwanzoni vitendo Vyake vilifichwa kutoka kwa binadamu. Baada ya Shetani kuangushwa hadi katikati ya anga, alijishughulisha na masuala yake, naye Mungu akajishughulisha Mwenyewe na kazi Yake binafsi, siku zote Akifanya vita dhidi ya Shetani, kila wakati mpaka siku za mwisho. Sasa ndio wakati ambapo Shetani anafaa kuangamizwa. Mwanzoni Mungu alimpa mamlaka, na baadaye Alimtimua hadi katikati ya anga, lakini Shetani alibaki mwasi. Baada ya hapo, aliwapotosha binadamu, lakini Mungu kwa hakika alikuwa ulimwenguni akiwasimamia binadamu. Mungu hutumia usimamizi Wake wa watu kumshinda Shetani. Kwa kuwapotosha watu, Shetani hutamatisha majaaliwa ya watu na kuinyanyasa kazi ya Mungu. Kwa upande mwingine, kazi ya Mungu ndiyo wokovu wa binadamu. Ni hatua gani ya kazi ya Mungu mwenyewe ambayo hainuii kuwaokoa binadamu? Ni hatua gani hainuii kuwatakasa watu, kuwafanya atende haki na kuwafanya kuishi kwa njia ambayo huunda taswira inayoweza kupendwa? Shetani, hata hivyo, hafanyi hivi. Yeye huwapotosha binadamu; siku zote anatekeleza kazi zake za kuwapotosha binadamu kote ulimwenguni. Bila shaka, Mungu pia hufanya kazi Yake mwenyewe. Hamtilii maanani Shetani. Haijalishi ni kiasi kipi cha mamlaka ambacho Shetani anacho, mamlaka yake bado yalitoka kwa Mungu; Mungu kwa hakika hakumpa mamlaka Yake yote tu, na hivyo basi haijalishi ni nini afanyacho, hawezi kuzidi Mungu na siku zote yuko mikononi mwa Mungu. Mungu hakufichua vitendo Vyake vyovyote akiwa mbinguni. Alimpa Shetani kiwango kidogo tu cha mamlaka ili kumruhusu kutekeleza udhibiti wake dhidi ya malaika. Hivyo basi, haijalishi kile anachofanya, hawezi kuzidi mamlaka ya Mungu kwa sababu mamlaka ambayo Mungu alimpa awali ni finyu. Huku Mungu akifanya kazi, Shetani hunyanyasa. Katika siku za mwisho, atamaliza unyanyasaji wake; vilevile, kazi ya Mungu itakamilika, na aina ya mtu ambaye Mungu angependa kumkamilisha atakuwa amekamilika. Mungu huwaelekeza watu kwa njia nzuri; maisha Yake ni maji yenye uzima, yasiyopimika na yasiyo na mipaka. Shetani amempotosha binadamu hadi kiwango fulani; hatimaye, yale maji hai ya uzima yatamkamilisha binadamu, na haitawezekana kwa Shetani kuingilia kati na kutekeleza kazi yake. Hivyo basi, Mungu ataweza kuwapata kabisa watu wake. Shetani angali anakataa kukubali haya sasa; siku zote hupambana na Mungu, lakini Mungu hamtilii maanani. Amesema, Nitakuwa mshindi dhidi ya nguvu zote za giza za Shetani na dhidi ya ushawishi wote wa giza. Hii ndiyo kazi ambayo lazima ifanywe katika mwili, na ndiyo pia maana ya kupata mwili kwa Yesu Kristo. Ni kukamilisha hatua ya kazi ya kumshinda Shetani katika siku za mwisho, kuondoa vitu vyote vinavyomilikiwa na Shetani. Ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani ni mtindo usioepukika! Shetani kwa hakika alishindwa kitambo sana. Wakati injili ilipoanza kuenezwa kote duniani mwa joka kubwa jekundu, yaani, wakati Mungu mwenye mwili alipoanza kufanya kazi na kazi hii ikafanywa kuendelea, Shetani aliweza kushindwa kabisa, kwani kupata mwili wa Kristo kulimaanisha kumshinda Shetani. Shetani aliona kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na alikuwa ameanza kutekeleza kazi Yake, na akaona kwamba hakuna nguvu ambazo zingeweza kukomesha kazi hii. Hivyo basi, alipigwa na bumbuazi alipoona kazi hii na hakuthubutu kufanya kazi yoyote nyingine zaidi. Kwanza Shetani alifikiria kwamba pia alimiliki hekima nyingi, na akaingilia kati na kunyanyasa kazi ya Mungu; hata hivyo, hakutarajia kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili, na kwamba katika kazi Yake, Mungu alikuwa ametumia uasi Wake kuhudumu kama ufunuo na hukumu kwa binadamu; na hivyo basi kumshinda binadamu na kumshinda Shetani. Mungu ni mwenye busara kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani kwa mbali. Hivyo basi, Niliwahi kutaja awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa Shetani. Mungu anapofanya kazi Yake, Shetani anamfuata unyo unyo kutoka nyuma mpaka mwishowe anaangamizwa—hatajua hata kilichomgonga! Ataweza kutambua tu ukweli baada ya kuvunjwa na kupondwapondwa; na wakati huo atakuwa tayari amechomwa kwenye ziwa la moto. Hatakuwa ameshawishika kabisa wakati huo? Kwani hatakuwa na njama zozote zingine za kutumia!

Ni kazi hii ya kihalisi ya hatua kwa hatua ambayo mara nyingi inaulemea moyo wa Mungu kwa huzuni ya binadamu, kiasi kwamba vita Vyake na Shetani vimedumu kwa sasa miaka 6,000. Hivyo basi Mungu alisema hivi: “Sitawahi tena kuumba binadamu, wala kuwahi tena kuwapa malaika mamlaka.” Kuanzia hapo, wakati malaika walipokuja kufanya kazi duniani, walimfuata tu Mungu ili kufanya kazi fulani. Hakuwahi kuwapa malaika mamlaka. Je, malaika ambao Waisraeli waliwaona walitekeleza vipi kazi yao? Walijifichua katika ndoto na kupitisha maneno ya Yehova. Wakati Yesu alipofufuka siku tatu baada ya kusulubishwa, ni malaika ndio waliolisukuma jiwe kando; Roho wa Mungu hakufanya kazi hii yeye binafsi. Malaika waliweza kufanya tu kazi ya aina hii; walifanya tu wajibu wa usaidizi na hawakuwa na mamlaka, kwani Mungu hangewahi tena kuwapatia mamlaka. Baada ya kufanya kazi kwa muda fulani, watu ambao Mungu alitumia hapa duniani walichukua nafasi ya Mungu na kusema, “Nataka kuzidi ulimwengu! Nataka kusimama kwenye mbingu ya tatu! Tunataka hatamu za mamlaka ya ukuu!” Wangekuwa na kiburi baada ya siku kadhaa za kazi; walitaka mamlaka ya ukuu duniani, walitaka kuanzisha taifa jingine, walitaka vitu vyote viwe katika utawala wao na walitaka kusimama katika mbingu ya tatu. Je, kwani hujui kwamba wewe ni binadamu tu unayetumiwa na Mungu? Unawezaje kupaa hadi kwenye mbingu ya tatu? Mungu huja duniani kufanya kazi, kimyakimya na bila ya kujitangaza, na Huondoka baada ya kukamilisha kazi Yake kimyakimya. Hajitangazi kama vile binadamu wanavyofanya, lakini badala yake Anatekeleza kazi Yake kwa uhalisi. Wala haingii kanisani na kujitangaza, “Nitawaangamiza nyinyi nyote! Nitawalaani na kuwaadibu!” Anatekeleza tu kazi Yake binafsi, na kuondoka mara Anapomaliza. Wale wachungaji wa kidini wanaowaponya wagonjwa na kupunga mapepo, wanawasomea wengine kutoka kwenye madhabahu, na kutoa hotuba ndefu na zenye makuu na kuzungumzia masuala yasiyo ya kihalisi, wana kiburi hadi moyoni! Wao ni vizazi vya malaika mkuu!

Baada ya kufanya kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, sababu ya kimsingi ikiwa ni kumshinda Shetani na kuleta wokovu kwa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Yeye huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu duniani, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Viumbe wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio Lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio duniani na viumbe wote walio duniani watauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na duniani vyote vitauona utukufu Wake, na Atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kumruhusu binadamu amsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani. Unaviona vitendo hivi vyote vya Mungu sasa, ilhali ungali unapinga na unakuwa mwasi na hutaki kunyenyekea; unayahifadhi mambo mengi ndani yako na unafanya utakacho; unafuata ashiki zako, na kile upendacho—huu ni uasi; huu ni upingaji. Imani katika Mungu ambayo inatekelezwa kwa ajili ya mwili, kwa ajili ya ashiki za mtu, na kwa ajili ya kile anachopenda mtu, kwa ajili ya ulimwengu, na kwa ajili ya Shetani ni chafu; ni upinzani na uasi. Kunazo aina zote tofauti za imani sasa: Baadhi hutafuta hifadhi dhidi ya janga, na wengine hutafuta kupokea baraka, huku baadhi wakitamani kuelewa mafumbo na bado wengine hujaribu kupata pesa. Hiyo yote ni mifumo ya upinzani; hiyo yote ni kukufuru! Kusema kwamba mtu anapinga au anaasi—huku si kwa mujibu wa mambo haya? Watu wengi sasa hivi wanalalamika, wanatamka manung’uniko au kutoa hukumu. Haya yote ni mambo yanayofanywa na waovu; wao ni binadamu wapinzani na waasi; watu kama hao wamemilikiwa na kujawa na Shetani. Watu ambao Mungu huwapata ni wale wanaonyenyekea Kwake kabisa, wale waliopotoshwa na Shetani lakini wameokolewa na kushindwa na kazi Yake sasa, wale waliovumilia majaribu na hatimaye wamepokelewa kabisa na Mungu na hawaishi tena katika umiliki wa Shetani na wamevunja minyororo ya udhalimu, walio radhi kuishi kwa kudhihirisha utakatifu—hawa ndio watu watakatifu zaidi; hawa ndio wale watakatifu. Kama matendo yako ya sasa hayalingani na sehemu moja ya mahitaji ya Mungu utaondolewa. Hili halipingiki. Kila kitu kinafanywa kulingana na leo; ingawa Amekuamulia awali na kukuchagua wewe, matendo yako leo bado yataamua matokeo yako. Kama huwezi kuenda sambamba sasa, utaondolewa. Kama huwezi kuenda sambamba sasa, utawezaje kuenda sambamba baadaye? Sasa kwa kuwa muujiza mkubwa kama huo umekufanyikia wewe, bado huamini. Basi, utamwamini vipi baadaye wakati Atakapomaliza kazi Yake na Hafanyi tena kazi kama hiyo? Wakati huo itakuwa vigumu zaidi kwako wewe kumfuata Yeye! Baadaye Mungu atategemea mwelekeo na maarifa yako katika kazi ya Mungu mwenye mwili na kile ulichopitia wewe ili kuamua kama wewe ni mwenye dhambi au mwenye haki, au kuamua kama wewe ndiwe uliyekamilishwa ama ni yule aliyeondolewa. Lazima uweze kuona wazi sasa. Roho Mtakatifu hufanya kazi hivyo: Yeye huamua matokeo yako kulingana na tabia yako leo. Nani anayeongea maneno ya leo? Nani anayefanya kazi ya leo? Nani anayeamua kama utaondolewa leo? Nani anayeamua kukufanya kuwa mtimilifu? Je, hiki sicho Ninachofanya Mimi mwenyewe? Mimi ndimi Ninayeongea maneno haya; Mimi ndimi Ninayetekeleza kazi hii. Kulaani, kuadibu na kuhukumu watu vyote ni sehemu ya kazi Yangu binafsi. Hatimaye, kukuondoa kutakuwa pia kazi Yangu binafsi. Yote ni shughuli Yangu binafsi! Kukufanya kuwa mtimilifu ni shughuli Yangu binafsi, na kukuruhusu kufurahia baraka ni shughuli Yangu binafsi pia. Hii yote ni shughuli Yangu binafsi. Matokeo yako hayakuamuliwa awali na Yehova; yanaamuliwa leo na Mungu wa leo. Yanaamuliwa sasa; hayakuamuliwa kabla ya ulimwengu kuumbwa. Baadhi ya watu wapumbavu husema, “Pengine kuna jambo mbaya na macho Yako, na Hunioni mimi kama vile Unavyofaa kuniona. Hatimaye mtaona namna Roho atakavyoonyesha kila kitu!” Yesu kwanza Alimchagua Yuda kama mwanafunzi Wake. Watu huuliza: “Angewezaje kumchagua mwanafunzi ambaye angemsaliti?” Mwanzo Yuda hakuwa na nia ya kumsaliti Yesu. Hili jambo lilifanyika tu baadaye. Wakati huo Yesu alikuwa amemchukua Yuda kwa upendo; Alimfanya mtu huyo amfuate Yeye na kumfanya awajibikie masuala yao ya kifedha. Kama Angejua kwamba Yuda angebadhiri pesa, Asingemwacha asimamie pesa hizo. Mtu anaweza kusema kwamba Yesu hakujua mwanzo kwamba mtu huyu hakuwa mwaminifu na alikuwa mdanganyifu, na kwamba aliwadanganya ndugu zake. Baadaye, baada ya Yuda kumfuata Yesu kwa muda fulani, Yesu alimwona Yuda akiwadanganya ndugu zake na kumrairai Mungu. Watu waligundua pia kwamba siku zote angetumia pesa kutoka kwenye mfuko wa fedha na kisha wakamwambia Yesu. Yesu alipata habari tu kuhusu haya yote wakati huu. Kwa sababu Yesu alikuwa atekeleze kazi ya kusulubishwa na Alihitaji mtu wa kumsaliti, na Yuda alitokea tu kuwa mhusika mzuri wa wajibu huu, Yesu akasema, “Kutakuwepo miongoni mwenu ambaye atanisaliti Mimi. Mwana wa Adamu atatumia usaliti huu kuweza kusulubishwa na baada ya siku tatu atafufuka.” Wakati huo Yesu hakuchagua hasa Yuda ili aweze kumsaliti Yeye; kinyume cha mambo ni kwamba, Alipenda kwamba Yuda awe mwanafunzi mtiifu. Bila kutarajia, Yuda aligeuka kuwa mlafi na aliyepotoka aliyemsaliti Bwana, na akatumia hali hii kumchagua Yuda kwa kazi hii. Kama wanafunzi wote kumi na wawili wa Yesu wangekuwa watiifu, na hakuna mtu kama Yuda angekuwa miongoni mwao, yule mtu wa kumsaliti Yesu angekuwa hatimaye mtu kutoka nje ya wale wanafunzi. Hata hivyo, wakati huo ilifanyika tu kwamba kulikuwa na mmoja miongoni mwao aliyefurahia kuchukua hongo—Yuda. Yesu kwa hivyo basi alimtumia mtu huyu kukamilisha kazi Yake. Jambo hili lilikuwa rahisi jinsi gani! Yesu hakuliamua awali mwanzoni mwa kazi Yake; Alifanya tu uamuzi huu punde tu mambo yalipoimarika hadi hatua fulani. Huu ulikuwa ni uamuzi wa Yesu, yaani, uamuzi wa Roho wa Mungu Mwenyewe. Wakati huo ni Yesu aliyemchagua Yuda; wakati Yuda alipomsaliti Yesu baadaye, haya yalikuwa ni matendo ya Roho Mtakatifu ili kuhudumia hatima Zake mwenyewe; ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo. Wakati Yesu alipomchagua Yuda, Hakuwa na wazo lolote kwamba Angemsaliti. Alijua tu kwamba alikuwa Yuda Iskariote. Matokeo yenu yanaamuliwa pia kulingana na kiwango chenu cha kunyenyekea leo na kulingana na kiwango chenu cha ukuaji wa maisha, na wala si kulingana na wazo miongoni mwa dhana za binadamu kwamba ilikuwa imepangiwa awali katika uumbaji wa ulimwengu. Lazima uelewe mambo haya waziwazi. Kazi hii nzima haitekelezwi kulingana na kufikiria kwako.

Iliyotangulia: Maneno kwa Vijana na kwa Wazee

Inayofuata: Kuhusu Majina na Utambulisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp