Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

Ninyi nyote huketi kwenye viti vya umbuji, mkiwakaripia wale wa vizazi vidogo ambao ni wa namna yenu na mkiwafanya waketi pamoja nanyi. Ila hamjui kwamba “wazawa” wenu waliishiwa na pumzi kitambo sana na kuipoteza kazi Yangu. Utukufu Wangu unang’aa kutoka katika nchi ya Mashariki hadi katika nchi ya Magharibi, lakini utakapoenea hadi miisho ya dunia na kuanza kuinuka na kuangaza, Nitauchukua utukufu Wangu kutoka Mashariki na kuuleta Magharibi ili kwamba watu waovu, ambao wamenitelekeza huko Mashariki watanyimwa mwangaza kuanzia wakati huo na kuendelea. Hilo litakapofanyika, mtaishi katika bonde la kivuli. Hata ingawa watu siku hizi ni bora mara mia moja kuliko hapo awali, bado hawawezi kutimiza matakwa Yangu, na bado wao sio ushuhuda kwa utukufu Wangu. Kwamba mnaweza kuwa bora mara mia moja kuliko hapo awali ni matokeo ya kazi Yangu kabisa; ni matunda yatokanayo na kazi Yangu duniani. Hata hivyo, bado Ninahisi kuchukizwa na maneno na matendo yenu, na vile vile na tabia yenu, na Ninahisi chuki kubwa sana kuhusu jinsi mnavyotenda mbele Yangu, kwa kuwa hamna ufahamu wowote kunihusu. Basi, mnawezaje kuja kuishi kwa kudhihirisha utukufu Wangu, na mnawezaje kuwa waaminifu kabisa kwa kazi Yangu ya baadaye? Imani yenu ni ya kupendeza sana; mnasema kwamba mko tayari kutumia maisha yenu yote kwa ajili ya kazi Yangu, na kwamba mko tayari kutoa maisha yenu kwa ajili ya kazi hiyo, lakini tabia zenu hazijabadilika sana. Mnazungumza tu kwa kiburi, licha ya ukweli kwamba tabia yenu halisi ni mbovu sana. Ni kana kwamba ndimi na midomo ya watu iko mbinguni lakini miguu yao iko chini duniani, na kwa sababu hiyo, maneno na matendo yao na sifa zao bado ni mbovu na zisizoheshimika. Sifa zenu zimeharibiwa, tabia yenu imepotoka, njia yenu ya kuzungumza ni duni, na maisha yenu ni yenye kustahili dharau; hata ubinadamu wenu wote umezama katika hali duni ya chini kabisa. Ninyi ni wenye mawazo finyu kuhusu wengine, na ninyi hubishana kuhusu kila jambo dogo. Ninyi hugombana kuhusu heshima na hadhi zenu wenyewe, hadi kufikia kiwango ambapo mko tayari kushuka kuzimuni na kuingia kwenye ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha Mimi kubaini kwamba ninyi ni wenye dhambi. Mitazamo yenu kwa kazi Yangu inatosha Mimi kubaini kuwa ninyi ni wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kuonyesha kwamba ninyi ni watu wachafu mliojaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua vinatosha kusema kwamba ninyi ni watu ambao mmekunywa damu ya roho wachafu hadi mkatosheka. Kuingia katika ufalme kunapotajwa, hamfichui hisia zenu. Je, mnaamini ya kwamba jinsi mlivyo sasa inatosha kwa ninyi kupita katika lango la kuingia katika ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini ya kwamba mnaweza kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu, bila maneno na matendo yenu wenyewe kujaribiwa na Mimi kwanza? Ni nani anayeweza kunihadaa? Tabia na mazungumzo yenu yenye kustahili dharau na yaliyo duni yanaweza kuepukaje macho Yangu? Maisha yenu yamebainiwa na Mimi kuwa maisha ya kunywa damu na kula nyama ya roho hao wachafu kwa sababu ninyi huwaiga mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu, tabia yenu imekuwa mbaya hasa, kwa hiyo Ninawezaje kukosa kuwaona kuwa wenye kuchukiza? Maneno yenu yana uchafu wa roho wachafu: Mnabembeleza, kuficha na kujipendekeza kama tu wale wanaoshiriki katika uchawi na kama wale walio wadanganyifu na wanaokunywa damu ya wadhalimu. Maonyesho yote ya mwanadamu ni dhalimu mno, kwa hivyo watu wote wanaweza kuwekwaje katika nchi takatifu ambako wenye haki wako? Je, unafikiri kwamba hiyo tabia yako yenye kustahili dharau inaweza kukubainisha kama mtakatifu ikilinganishwa na wale wadhalimu? Ulimi wako ulio kama wa nyoka hatimaye utauangamiza huu mwili wako ambao huleta uharibifu na kutekeleza machukizo, na hiyo mikono yako iliyojaa damu ya roho wachafu pia hatimaye itaipeleka roho yako jahannamu. Basi, kwa nini huipokei kwa furaha nyingi fursa hii ili uitakase mikono yako iliyojaa uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kwa manufaa yako uukate huo ulimi wako unaozungumza maneno ya kudhulumu? Je, inawezekana kwamba uko tayari kuteseka katika moto wa jahannamu kwa ajili ya mikono, ulimi na midomo yako? Mimi huuchunga moyo wa kila mtu kwa macho yote mawili, kwa sababu muda mrefu kabla Niwaumbe wanadamu, Nilikuwa nimeifumbata mioyo yao mikononi Mwangu. Nilikuwa nimeibaini mioyo ya watu kitambo, kwa hiyo mawazo yao yangeyaepukaje macho Yangu? Muda utakosaje kuwa umewaishia wa kuepuka kuchomwa na Roho Wangu?

Midomo yako ni mikarimu zaidi kuliko njiwa, lakini moyo wako ni mwovu zaidi kuliko yule nyoka wa zamani. Midomo yako ni ya kupendeza hata kama wanawake wa Lebanoni, lakini moyo wako si mwema zaidi kuliko yao, na hakika hauwezi kulinganishwa na uzuri wa Wakanaani. Moyo wako ni mdanganyifu mno! Vitu Ninavyochukia ni midomo na mioyo ya wadhalimu tu, na matakwa Yangu kwa watu si ya juu zaidi ya yale Ninayotarajia kutoka kwa watakatifu hata kidogo; ni kwamba tu Natiwa kinyaa kwa ajili ya matendo maovu ya wadhalimu, nami Natumai kwamba waweze kutupilia mbali uchafu wao na kutoroka kutoka katika hatari waliyomo sasa ili waweze kusimama kutoka kwa hao wadhalimu na wawe watakatifu na kuishi na wale ambao ni wenye haki. Ninyi mko katika hali sawa na Yangu, lakini mmejaa uchafu; hamna hata mfano kidogo zaidi wa asili wa wanadamu walioumbwa hapo mwanzo. Aidha, kwa sababu kila siku mnaiiga mifano ya hao roho wachafu, mkifanya kile wanachofanya na kusema kile wanachosema, kila sehemu yenu—hata ndimi na midomo yenu—imelowezwa katika maji yao machafu, kiasi kwamba mmejaa madoa kama hayo kabisa, na hakuna sehemu yenu hata moja inayoweza kutumika kwa ajili ya kazi Yangu. Ni jambo la kusikitisha sana! Mnaishi katika dunia ya farasi na ng’ombe kabisa, lakini kwa kweli hamhisi kufadhaishwa; mmejaa furaha na mnaishi kwa uhuru na bila matatizo. Mnaogelea huku na kule katika maji hayo machafu, lakini kwa kweli hamtambui ya kwamba mmeingia katika hatari kama hiyo. Kila siku, mnaandamana na roho wachafu na kuingiliana na “kinyesi.” Maisha yenu ni ya kishenzi sana, ilhali hujui kweli kwamba haupo katika ulimwengu wa wanadamu kabisa na kwamba hujidhibiti. Je, hujui kwamba maisha yako yalikandamizwa na roho hao wachafu zamani, au kwamba tabia yako ilishachafuliwa na maji machafu zamani? Je, unafikiri kwamba unaishi katika paradiso ya duniani, na kwamba uko katikati ya furaha? Je, hujui kwamba umeishi maisha pamoja na roho wachafu, na kwamba umeishi pamoja kwa amani na kila kitu ambacho wamekuandalia? Jinsi unavyoishi inawezaje kuwa na maana yoyote? Maisha yako yanawezaje kuwa na thamani yoyote? Umekuwa ukikimbia huku na kule kwa ajili ya wazazi wako, wazazi wa roho wachafu, lakini hujui kweli kuwa wale wanaokutega ni hao wazazi wa roho wachafu waliokuzaa na kukukela. Aidha, huna habari kwamba kweli ni wao ndio waliokupa uchafu wako wote; kile unachojua tu ni kwamba wanaweza kukuletea “furaha”, hawakuadibu, wala hawakuhukumu, na hususani hawakulaani. Hawajawahi kukulipukia kwa hasira, lakini wanakutendea kwa upendo na fadhila. Maneno yao huusitawisha moyo wako na kukuvutia sana kiasi kwamba unakanganyikiwa, na bila kutambua, unafyonzwa na unakuwa tayari kuwahudumia, ukigeuka kuwa njia yao ya kutoka na kuwa mtumishi wao. Huna malalamiko hata kidogo, bali uko tayari kuwafanyia kazi kama mbwa, kama farasi; unadanganywa na wao. Kwa sababu hii, huna majibu yoyote kabisa kwa kazi Ninayoifanya. Si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kuponyoka kutoka Kwangu kwa siri, na si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kutumia maneno matamu kupata kibali kutoka Kwangu kwa njia danganyifu. Kama inavyotokea, tayari ulikuwa na mpango mwingine, na mpangilio mwingine. Unaweza kuona matendo Yangu kidogo kama mwenye Uweza, lakini huna ufahamu hata kidogo kuhusu hukumu na kuadibu Kwangu. Hujui kuadibu Kwangu kulianza lini; unajua tu jinsi ya kunidanganya—lakini hujui kwamba Sitastahimili ukiukaji wowote kutoka kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu anayechukia uovu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitakuvumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo Kwangu Mimi na ulimi wako? Je, ungewezaje kula kiapo kwa kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Nawaambia, hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya? Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?

Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichouliza kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina? Kazi Yangu kwa kweli ni ya nani? Inawezekana kuwa tu ni ya kuwapiga nyinyi nyote ili kufichua mamlaka Yangu? Je, si maisha yenu yameshikiliwa na neno moja kutoka Kwangu? Ni kwa nini Ninatumia maneno tu kuwaagiza na Sijayageuza maneno kuwa ukweli ili kuwapiga haraka iwezekanavyo? Je, maneno Yangu na kazi Yangu ni ya kuwapiga wanadamu tu? Je, Mimi ni Mungu ambaye huwaua wasio na hatia bila ubaguzi? Hivi sasa, ni wangapi wenu ambao wako hapo mbele Yangu ambao wanatafuta njia sahihi ya maisha ya mwanadamu na nafsi zao nzima? Ni miili yenu tu iliyo mbele Yangu, lakini mioyo yenu iko huru, na iko mbali, mbali na Mimi. Kwa sababu hamjui kwa kweli kazi Yangu ni nini, kuna baadhi yenu ambao mnataka kuondoka Kwangu, mnaojitenga na Mimi, na mnataka kuishi katika mahali hapo pa raha ambapo hakuna kuadibu, hakuna hukumu. Je, hili ndilo watu wanatamani katika mioyo yao? Mimi hakika sikulazimishi. Njia yoyote utakayoichukua ni uchaguzi wako mwenyewe, na njia ya leo huenda sambamba na hukumu na laana, lakini nyote mnapaswa kujua kwamba kile Niliyowapa, iwe ni hukumu au kuadibu, zote ni zawadi bora kabisa Ninazoweza kuwapa, na vyote ni vitu ambavyo mnahitaji kwa dharura.

Iliyotangulia: Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Inayofuata: Kazi katika Enzi ya Sheria

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp