289 Mungu Daima Amemlinda Mwanadamu

1

Maelfu ya miaka imepita, na Umemlinda binadamu kwa muda wote.

Baada ya miaka ya mabadiliko, azimio Lako la kumwokoa binadamu halijabadilika.

Zamani Uliteswa na kusulubiwa msalabani, damu Yako ikimwagika kumwokoa binadamu.

Ulilipa gharama ya uzima, Ukimkomboa mwanadamu kutoka dhambini.

Umerudi kati ya binadamu katika siku za mwisho, Ukionekana katika mwili.

Unateseka pamoja na mwanadamu wakati wa upepo na mvua, kupita usiku mwingi bila usingizi.

Unatoa jasho la damu na kufanya kazi kwa moyo wote, Ukionyesha maelfu ya maelfu ya maneno.

Unawapa binadamu ukweli wa thamani na kuishinda mioyo ya umati.

2

Unatuadibu na kutuhukumu, tabia Yako yenye haki inaleta uchaji mioyoni mwetu.

Maneno Yako huleta faraja na kutia moyo, huruma na uvumilivu Wako huleta heshima kuu ndani yetu.

Tumepotoshwa sana na Shetani, tabia zetu za kiburi na za uasi zinauleletea moyo Wako uchungu.

Tumeshapoteza sura yoyote ya binadamu, tumeshuka dhambini kama wanyama.

Maneno Yako yanafichua na kuhukumu, yakituruhusu tujijue.

Taabu, majaribu, na shida zimetakasa tabia zetu za kishetani.

Kiitikio

Ee Mungu! Usiku na mchana Unatuhangaikia, daima Uko kando yetu Ukitulinda.

Unatupa ukweli na uzima, Ukituletea wokovu.

Upendo Wako ni mzuri zaidi, safi zaidi, unastahili sifa ya mwanadamu.

Tutakupa upendo ulio mioyoni mwetu, tutakushuhudia milele.

Iliyotangulia: 288 Mungu Bado Anatupenda Leo

Inayofuata: 291 Upendo wa Mwenyezi Mungu Ndio Safi Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp