Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

281 Mungu Bado Anatupenda Leo

1

Mungu mwenye mwili amekuja kati ya binadamu,

na Amefanya kazi kwa muda mrefu kwa maficho ya unyenyekevu,

Akipitia mateso ya binadamu na kuonja uchungu

na utamu wote wa ulimwengu huu wa kidunia.

Yeye hutembea kati ya makanisa, Akipitia katika misimu mingi ya kuchipua,

ya joto, ya kupukutika kwa majani, na ya baridi.

Ameonyesha ukweli kututakasa na kutuokoa kutoka kwa Shetani.

Ni sasa tu kwamba tumekutana uso kwa uso na Kristo ndipo tunaona kuwa Mungu ndiye ukweli.

Mioyo yetu imeamshwa na Mungu,

na tunaona jinsi sisi ni wapotovu kwa kina.

Ni kwa ajili ya uvumilivu na ustahimilivu wa Mungu kwamba tuna nafasi hii ya kuokolewa.

Tunapitia ukuu wa wokovu wa Mungu;

Mungu hakika anastahili upendo na sifa zetu.

2

Ili kuwaletea binadamu wokovu, Mungu amepitia mateso ya kila aina,

kumwaga damu, jasho, na machozi.

Picha za zamani ni ngumu kusahau,

na upendo wa Mungu kwa wanadamu hauwezi kupimika.

Katika wakati wa udhaifu, Mungu aliniinua;

moyo wangu ulipouma, maneno ya Mungu yalinipa faraja.

Nilipokuwa mwenye kiburi, Mungu aliniadibu na kunifundisha nidhamu,

Akininongoza hadi leo hatua moja moja.

Mungu mara nyingi ametuletea hukumu adhimu,

na mara nyingi Ametupogoa na kutushughulikia,

Akitakasa upotovu wetu ili tuweze kuishi kama mwanadamu wa kweli anavyopaswa.

Tumepitia majaribu na dhiki, lakini Mungu amekuwa nasi,

akiandamana nasi na kutuongoza.

Tukiwa na Mungu, tumemshinda Shetani.

Shukrani kwa Mungu kwa wokovu Wake mkuu.

Mungu bado anatupenda leo; tunawezaje kuyasikitisha matarajio Yake?

Nakumbuka kusihi kwa Mungu,

na nitafanya bidii kutimiza wajibu wangu wa kuufariji moyo wa Mungu,

kwa hiari nikivumilia majaribu yote na mateso,

na kutoa ushuhuda wa nguvu na mkuu kwa Mungu.

Ingawa njia ya kumpenda Mungu imejaa mashimo na mitego,

katika uhasi naweza kuanguka, lakini kisha nasimama tena.

Haijalishi ni shida gani ambazo naweza kukutana nazo,

nitampenda Mungu daima bila kulalamika na bila majuto!

Iliyotangulia:Upendo Hukesha

Inayofuata:Upendo wa Mungu Hukaa Milele Miongoni mwa Wanadamu

Maudhui Yanayohusiana

 • Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

  I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo …

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…