A. Mahitaji ya Mungu kwa Mwanadamu

605. Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza rasmi kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinavyotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kuna maana ya kuanza maisha ya watu wa Mungu—uko radhi kuyakubali mafunzo hayo? Uko radhi kuhisi kuthamini kwa umuhimu? Uko radhi kuishi chini ya nidhamu ya Mungu? Uko radhi kuishi chini ya kuadibu kwa Mungu? Wakati ambapo maneno ya Mungu yatakujia na kukujaribu, utafanyaje? Na utafanya nini wakati ambapo utakabiliwa na aina yote ya ukweli? Zamani, kulenga kwako hakukuwa juu ya maisha; leo, lazima uingie katika uhalisi wa maisha, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Hili ndilo lazima litimizwe na watu wa ufalme. Wale wote ambao ni watu wa Mungu lazima wawe na uzima, lazima wakubali mafunzo ya ufalme, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Hili ndilo Mungu huwashurutisha watu wa ufalme.

Masharti ya Mungu kwa watu wa ufalme ni kama yafuatayo:

1) Lazima wakubali maagizo ya Mungu, ambalo ni kusema, lazima wakubali maneno yote yaliyonenwa katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

2) Lazima waingie katika mafunzo ya ufalme.

3) Lazima wafuatilie kufanya mioyo yao iguswe na Mungu. Wakati ambapo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na una maisha ya kiroho ya kawaida, utaishi katika eneo la uhuru, ambalo lina maana kuwa utaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo wa Mungu. Ukiishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu tu ndipo utakuwa wa Mungu.

4) Lazima wapatwe na Mungu.

5) Lazima wawe dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani.

Haya mawazo makuu matano ni maagizo Yangu kwenu. Maneno Yangu yananenwa kwa watu wa Mungu, na kama hutaki kuyakubali maagizo haya, Sitakulazimisha—lakini ukiyakubali kwa kweli, basi utaweza kuyafanya mapenzi ya Mungu. Leo, anzeni kuyakubali maagizo ya Mungu, na kufuatilia kuwa watu wa ufalme na kufikia viwango vinavyohitajika kuwa watu wa ufalme. Hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia. Kama ungependa kufanya mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu, basi lazima uyakubali maagizo haya matano, na kama unaweza kuyatimiza, utaupendeza moyo wa Mungu na kwa hakika utatumiwa sana na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

606. Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la mwisho la kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili. Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu haipo bila sababu, na kutokana na hili inaonekana ni kwa nini Mungu kila mara hufanya kazi ya hali ya juu na yenye mahitaji makali. Ndiyo maana unafaa kujawa na imani katika Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu hufanywa kwa ajili yako, ili kwamba uweze kupokea urithi Wake. Hii sio kwa ajili ya utukufu wa Mungu bali ni kwa ajili ya wokovu wako na kufanya kundi hili la watu walioteswa na nchi najisi kuwa wakamilifu. Sharti uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo Nawahimiza wale wote wasiojua, wasio na hisia na ufahamu: Usimjaribu Mungu wala kumpinga tena. Mungu Ameshavumilia mateso yote ambayo mwanadamu hajaweza kupitia, na hapo awali Ameteseka na kudhihakiwa kwa niaba ya mwanadamu. Je, nini kingine ambacho huwezi kukiachilia? Je, ni nini muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu? Ni nini zaidi kuliko upendo wa Mungu? Ni kazi ambayo ina ugumu mara mbili zaidi kwa Mungu kufanya katika nchi najisi. Ikiwa mtu atatenda dhambi kimakusudi na akifahamu, kazi ya Mungu itaendelezwa kwa muda mrefu zaidi. Katika tukio lolote, hili silo pendeleo la yeyote wala si la maana kwa yeyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?

607. Maneno Ninayoongea ni ukweli unaoelekezwa kwa wanadamu wote, na wala hayajaelekezwa kwa mtu mahususi au aina fulani ya mtu. Kwa hiyo, mnapaswa kumakinikia kupokea maneno Yangu kutoka katika mtazamo wa ukweli, na vile vile mdumishe mtazamo wa uzingativu na uaminifu kamili. Msipuuze hata neno moja au ukweli Ninaoongea, na wala usichukulie maneno Yangu kwa dharau. Katika maisha yenu, Naona mengi ambayo mnafanya ambayo hayana uhusiano na ukweli, kwa hivyo Nawaambia moja kwa moja muwe watumishi wa ukweli na wala si kutawaliwa na maovu na ubaya. Msikanyage ukweli na kuchafua sehemu yoyote ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo onyo Langu kwenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

608. Natumai tu kwamba hamtapoteza juhudi Zangu zenye kujitahidi na zaidi ya hayo, kwamba mnaweza kuelewa utunzaji wote na fikira ambazo Nimetumia, mkiyachukulia maneno Yangu kama msingi wa jinsi mnavyotenda kama binadamu. Iwe ni maneno ambayo mko tayari kuyasikiliza au la, iwe ni maneno ambayo mnafurahia kuyakubali au mnayakubali bila raha, lazima muyachukulie kwa uzito. Vinginevyo, tabia na mielekeo yenu isiyokuwa ya kujali itanifadhaisha Mimi kweli na hata zaidi, kuniudhi. Natumai sana kwamba nyote mnaweza kuyasoma maneno Yangu tena na tena—mara elfu kadhaa—na hata kuyakariri. Ni kwa namna hiyo tu ndiyo hamtayaacha matarajio Yangu kwa ajili yenu. Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishi hivi sasa. Hata, nyote mmezama katika maisha fisadi ya kula na kunywa hadi kushiba, na hakuna yeyote kati yenu anayeyatumia maneno Yangu kuusitawisha moyo na nafsi yake. Kwa sababu hii ndiyo Nimehitimisha kuhusu uso wa kweli wa mwanadamu: Mwandamu anayeweza kunisaliti wakati wowote, na hakuna yeyote anayeweza kuwa mwaminifu kabisa kwa maneno Yangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)

609. Mungu anataka upendo mmoja wa mtu, naye humhitaji mtu amilikiwe na maneno Yake na upendo wa mtu Kwake. Kuishi ndani ya maneno ya Mungu, kugundua kile ambacho mtu anapaswa kutafuta kutoka ndani ya maneno Yake, kumpenda Mungu kama matokeo ya maneno Yake, kukimbiakimbia kwa ajili ya maneno ya Mungu, kuishi kwa ajili ya maneno ya Mungu—haya yote ni mambo ambayo mtu anapaswa kufikia. Kila kitu lazima kijengwe kulingana na maneno ya Mungu, na hapo tu ndipo mtu ataweza kukidhi matakwa ya Mungu. Kama mwanadamu hajatayarishwa na maneno ya Mungu, basi yeye ni funza tu ambaye amemilikiwa na Shetani. Yapime moyoni mwako mwenyewe—ni maneno mangapi ya Mungu ambayo umekita mizizi yake ndani yako? Ni katika mambo gani unaishi kulingana na maneno Yake? Ni katika mambo gani ndiyo hujakuwa ukiishi kulingana nayo? Kama maneno ya Mungu hayajakumiliki kikamilifu, basi ni nini hasa kilicho moyoni mwako? Katika maisha yako ya kila siku, je, unadhibitiwa na Shetani, au unamilikiwa na maneno ya Mungu? Je, maombi yako yameanzishwa kutoka kwa maneno Yake? Je, umeondoka katika hali yako mbaya kupitia nuru ya maneno ya Mungu? Kuchukua maneno ya Mungu kama msingi wa kuwepo kwako, hili ndio jambo kila mtu anapaswa kuingia ndani. Kama maneno ya Mungu hayapo katika maisha yako, basi unaishi chini ya ushawishi wa giza, wewe ni muasi dhidi ya Mungu, unampinga Mungu, na huheshimu jina Lake—imani ya watu kama hao katika Mungu ni uharibifu na usumbufu kabisa. Je, ni kiasi gani cha maisha yako kimeishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Ni kiasi gani cha maisha yako hakijaishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Je, ni kiasi gani cha kile ambacho maneno ya Mungu yamehitaji kwako kimetimizwa ndani yako? Ni mangapi yamepotea ndani yako? Je, umechunguza mambo kama hayo kwa karibu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

610. Je, mnayo nia ya kustarehe katika baraka Zangu duniani, baraka zilizo sawa na zile za mbinguni? Je, mko tayari kuchukua kuelewa kwao kunihusu, na kufurahia kwa maneno Yangu na ufahamu wako kunihusu, kama vitu vya thamani zaidi na vya muhimu zaidi katika maisha yenu? Je, kweli mnaweza kuwa watiifu Kwangu kikamilifu, bila fikira kwa matarajio yenu wenyewe? Je, kweli mna uwezo wa kujiruhusu kuuwawa na Mimi, na kuongozwa na Mimi, kama kondoo? Je, kunao kati yenu walio na uwezo wa kutimiza vitu kama hivi? Inawezekana kuwa wote wanaokubaliwa na Mimi na kupokea ahadi Zangu ndio wanaopokea baraka Zangu? Je, mmeelewa chochote kutoka katika maneno haya? Nikiwajaribu, je, mnaweza kweli kujiweka wenyewe katika huruma Yangu, na, katikati ya majaribu haya, mtafute nia Yangu na muelewe moyo Wangu? Mimi sitamani wewe uweze kuongea maneno mengi matamu, au utoe hadithi nyingi za kufurahisha; badala yake Ninauliza kuwa uweze kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu, na kwamba unaweza kuingia kikamilifu na kwa kina katika hali halisi. Kama Singezungumza moja kwa moja, je, ungewacha kila kitu kilicho karibu na wewe na ukubali kutumiwa na Mimi? Je, hii siyo hali halisi Ninayohitaji? Je, ni nani aliye na uwezo wa kuelewa maana iliyo katika maneno Yangu? Ilhali Ninauliza kuwa msishushwe na wasiwasi tena, kwamba mwe msitari ya mbele katika kuingia kwenu na muelewe kiini cha maneno Yangu. Hii itazuia hali ya nyinyi kutoelewa maneno Yangu, na hali ya kutokuwa na uwazi kuhusu maana Yangu, na hivyo kukiuka amri Zangu za utawala. Natumaini kuwa mtaelewa Nia Yangu kwenu katika maneno Yangu. Msifikiri juu ya matarajio yenu tena, na mtende vile ambavyo mmeamua mbele Yangu kutii mipango ya Mungu katika kila kitu. Wale wote wanaosimama miongoni mwa kaya Yangu wanapaswa kufanya mengi kiasi wanachoweza; unafaa utoe hali yako bora zaidi kwa sehemu ya mwisho ya kazi Yangu duniani. Je, unayo nia ya kuviweka vitu vya aina hii katika matendo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 4

611. Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani, walinde lango la nyumba Yangu kwa ajili Yangu, waweze kusaidiana na kupeana mahitaji, kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati mtakapokuwa na majuto ya kuchelewa sana. Kwa nini Ninawafundisha kwa hali hiyo ya dharura? Kwa nini Ninawaelezea ukweli wa ulimwengu wa kiroho? Kwa nini Ninawakumbusha na kuwaonya mara kwa mara? Je, mmewahi kufikiri juu ya hili? Je, mmewahi kulielewa? Hivyo, hamhitaji tu kuweza kuwa wazoefu kwa kutegemeza juu ya msingi wa zamani, bali, zaidi, kuondoa uchafu ndani yenu chini ya uongozi wa maneno ya leo, mkiruhusu kila maneno Yangu kukita mzizi na kustawi ndani ya roho zenu, na muhimu zaidi, kuzaa matunda zaidi. Hiyo ni kwa sababu kile Ninachokiomba si maua angavu yaliyostawi sana, bali matunda mengi—matunda, zaidi ya hayo, ambayo hayaharibiki. Je, mnaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu? Ingawa maua katika nyumba ya kioo ya kuhifadhi mimea ni yasiyohesabika kama nyota, na huwavuta watalii wote, mara yanaponyauka yanakuwa mabovu mabovu kama hila danganyifu za Shetani, na hakuna mtu anayevutiwa nayo. Lakini kwa wale ambao wamerushwa na upepo na kuchomwa na jua na kuwa na ushuhuda Kwangu, ingawa maua haya si mazuri, mara yanaponyauka, hapo panatokea tunda, maana haya ndiyo matakwa Yangu. Ninapozungumza maneno haya, mnaelewa kiwango kipi? Mara maua yanaponyauka na kuzaa matunda, na mara matunda haya yote yanaweza kutolewa kwa ajili ya furaha Yangu, Nitakamilisha kazi Yangu yote duniani, na Nitaanza kufurahia udhihirisho wa hekima Yangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 3

612. Watu ambao wanamwamini Mungu kwa muda mrefu sasa wametumainia hatima iliyo nzuri, watu wote ambao wanamwamini Mungu wanatumai kwamba bahati nzuri itawajia ghafla, na wote wanatumai kwamba bila kujua, watajikuta wameketi kwa amani pahali pamoja au pengine mbinguni. Lakini Ninasema watu hawa kwa mawazo yao mazuri hawajawahi kujua kama wana sifa ya kupokea bahati nzuri kama hiyo inayoanguka kutoka mbinguni, au kukaa juu ya kiti huko mbinguni. Kwa sasa nyinyi mna maarifa mazuri kujihusu, lakini bado mnatarajia kwamba mnaweza kuepuka maafa ya siku za mwisho na mkono wa mwenye Uweza ukiwaadhibu wale waovu. Inaonekana kana kwamba kuwa na ndoto tamu na kutaka vitu kama tu wanavyopenda ni jambo la kawaida la watu wote ambao Shetani amewapotosha, si kipaji cha ajabu cha mtu fulani binafsi. Hata hivyo, bado Nataka kukomesha tamaa zenu badhirifu na hamu zenu za kupata baraka. Kwa kuwa dhambi zenu ni nyingi na ukweli wa kutotii kwenu ni mwingi na unaongezeka kila wakati, haya yanawezaje kupatana na ramani zenu nzuri za baadaye? Kama unataka kuendelea unavyopenda kuwa mwenye makosa, bila chochote kinachokuzuia, lakini bado unataka ndoto zitimie, basi Nakusihi uendelee katika usingizi wako na usiamke kamwe, kwa sababu unaota ndoto isiyoweza kutimia, na haitatumika kukufanya uwe mtu usiye wa kawaida mbele ya Mungu mwenye haki. Kama unataka tu ndoto zitimie, basi usiote kamwe, lakini kabiliana na ukweli milele, kabiliana na mambo ya hakika. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuokoa. Je, kwa maneno thabiti, hatua za taratibu hizi ni zipi?

Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na kuchunguza mwenendo na mawazo yako yote ambayo hayafuati ukweli.

Hiki ni kipengee ambacho mnaweza kukifanya kwa urahisi, na Ninaamini kwamba watu wanaofikiri wanaweza kufanya hivi. Hata hivyo, wale watu ambao hawajui kamwe ni nini maana ya dhambi na ukweli ni tofauti, kwa sababu kimsingi wao si watu wa kufikiri. Mimi nazungumza na watu ambao wamethibitishwa na Mungu, ni waaminifu, hawajazikosea vibaya amri za utawala, na wanaweza kupata dhambi zao wenyewe kwa urahisi. Ingawa hiki ni kipengee ambacho Ninahitaji kwenu ambacho ni rahisi kwenu, sicho kipengee cha pekee Ninachohitaji kwenu. Lolote litokealo, Ninatumai kwamba hamtalicheka hitaji hili kwa siri, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kimzaha. Lichukulieni kwa umakini, na msilipuuze.

Pili, kwa kila moja ya dhambi na kutotii kwako tafuta ukweli unaoambatana na utumie ukweli huu kuzitatua, kisha badilisha vitendo vyako vya dhambi na mawazo yako na vitendo vya kutotii na kutenda ukweli.

Tatu, kuwa mtu mwaminifu, si mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, mwenye hila daima. (Hapa Ninakusihi tena uwe mtu mwaminifu.)

Kama unaweza kutimiza vipengee hivi vyote vitatu basi una bahati, wewe ni mtu ambaye ndoto zake zinatimia na ambaye hupata bahati nzuri. Labda mtayachukulia maombi haya matatu yasiyovutia kwa umakini, au labda mtayachukulia bila kuwajibika. Kwa vyovyote vile, azma Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka mawazo yenu katika matendo, si kuwadhihaki au kuwadanganya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

613. Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu. Kama kila mojawapo ya mazungumzo ambayo Nimekuwa nayo na nyinyi hayajatosha kuvuta nadhari yenu, basi huenda Sitasema mengine. Hata hivyo, nyinyi mnaelewa matokeo ya hayo. Sipumziki kamwe, kwa hiyo Nisiponena, Nitafanya kitu ili watu wakitazame. Ningeweza kuufanya ulimi wa mtu uoze, au mtu afe na viungo vyake kutolewa, au kumpa mtu kasoro za neva na kumfanya atende kama mwendawazimu. Au, basi tena, Ningeweza kufanya baadhi ya watu wavumilie maumivu makali Ninayowasababishia. Kwa njia hii Ningejihisi mwenye furaha, mwenye furaha sana na kufurahishwa sana. Imesemwa daima kwamba “Mema hulipizwa kwa mema, na maovu kwa maovu,” mbona isiwe hivyo sasa? Kama unataka kunipinga Mimi na unataka kutoa hukumu fulani kunihusu, basi Nitauozesha mdomo wako, na hilo litanipendeza Mimi sana. Hii ni kwa sababu mwishowe hujafanya lolote linalohusiana na ukweli, sembuse na maisha, ilhali kila kitu Ninachofanya ni ukweli, kila kitu kinahusiana na kanuni za kazi Yangu na amri za utawala Ninazoeleza rasmi. Kwa hiyo, Namsihi sana kila mmoja wenu kujilimbikiza wema kiasi, acha kufanya maovu mengi sana, na usikize madai Yangu katika wasaa wako. Kisha mimi Nitahisi furaha. Kama mngetoa (au kusaidia) kwa ukweli moja kwa elfu ya juhudi mnazoweka katika mwili, basi Nasema hungekuwa na dhambi mara kwa mara na midomo mbovu. Je, hili si dhahiri?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

614. Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

615. Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na wima, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, wakati siku itakuja, Mungu hatakosa kumjali mtu yeyote ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni tu kwa njia hii Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa malengo ya chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, msiwache jitihada zozote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutenga maisha ya jitihada za kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

616. Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo kwa njia inayofaa? Je, wewe unayepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho unaweza kueleza tabia ya Mungu yenye haki kwa utondoti? Je, unaweza kushuhudia kuhusu tabia ya Mungu kwa uwazi na usahihi? Utawezaje kupitisha kile ambacho umeona na kupitia kupitia kwa maskini hawa wa kuhurumiwa, na waumini wa kidini wa kumcha Mungu waliojitolea na waliojawa na njaa na kiu ya haki na wanaongoja uwe mchungaji wao? Ni watu wa aina gani ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Unaweza kuwaza kweli? Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? Utahudumu vipi kama kiongozi mzuri wa wakati unaofuata? Je, unao hisia nzuri ya uongozi? Utaeleza mkuu wa kila kitu kama nini? Je, ni mkuu wa kila kitu kilicho hai na viumbe vyote duniani? Una mipango ipi ya kuendelea kwa hatua inayofuata ya kazi? Ni watu wangapi ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Je, jukumu lako ni nzito? Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, “Njia iko wapi?” Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia, ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

617. Wewe ni kiumbe aliyeumbwa—unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu lakini unaishi ndani ya mwili wako mchafu, basi wewe si mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kwa kuwa wewe ni binadamu, unapaswa kujitumia kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso! Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu na Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kutoka kwa ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya uelekezi wa Shetani, na kukanyagiwa kabisa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au kupata njia ya kweli, basi kuna umuhimu gani katika kuishi kwa namna hii? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale mnaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (2)

618. Mnapaswa kutaka kufanya lote muwezalo kumpenda Mungu katika mazingira haya ya amani. Katika siku za baadaye hamtakuwa na nafasi zaidi za kumpenda Mungu, kwani watu huwa tu na nafasi ya kumpenda Mungu katika mwili; wanapoishi katika ulimwengu mwingine, hakuna atakayenena kuhusu kumpenda Mungu. Je, hili si jukumu la kiumbe aliyeumbwa? Kwa hiyo unapaswa kumpenda Mungu vipi katika siku zako za uhai? Umeshawahi kufikiri juu ya hili? Je, unangoja mpaka ufe ili umpende Mungu? Je, haya si maneno matupu? Leo, kwa nini hufuatilii kumpenda Mungu? Je, kumpenda Mungu huku ukiwa na shughuli nyingi kunaweza kuwa upendo halisi wa Mungu? Madhumuni ya kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu itafika mwisho hivi punde ni kwa sababu Mungu tayari ana ushuhuda mbele ya Shetani; hivyo, hakuna haja ya mwanadamu kufanya lolote, mwanadamu anatakiwa tu kufuatilia kumpenda Mungu katika miaka ambayo yuko hai—hili ndilo jambo muhimu. Kwa sababu masharti ya Mungu si mengi, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa kuna hamu kuu ndani ya moyo Wake, Amefichua muhtasari wa hatua inayofuata ya kazi kabla ya hatua hii ya kazi kumalizika, ambalo linaonyesha kwa dhahiri kuna kiasi gani cha muda: kama Mungu hangekuwa na hamu ndani ya moyo Wake, je, Angeyanena maneno haya mapema hivyo? Ni kwa sababu muda ni mfupi ndio maana Mungu anafanya kazi kwa njia hii. Inatarajiwa kwamba mnaweza kumpenda Mungu kwa mioyo yenu yote, kwa akili zenu zote, na kwa nguvu zenu zote, jinsi tu mnavyotunza maisha yenu wenyewe. Je, haya siyo maisha yenye maana kuu zaidi? Ni wapi pengine ambapo mngeweza kupata maana ya maisha? Je, ninyi si vipofu kabisa? Uko radhi kumpenda Mungu? Je, Mungu anastahili upendo wa mwanadamu? Je, watu wanastahili ibada ya mwanadamu? Kwa hiyo, unapaswa kufanya nini? Mpende Mungu kwa ujasiri, bila kusita, na uone kila ambacho Mungu atakufanya. Uone kama Atakuchinja. Kwa muhtasari, kazi ya kumpenda Mungu ni muhimu zaidi kuliko kunukuu na kuandika mambo kwa ajili ya Mungu. Unapaswa kukipa kipaumbele kilicho muhimu zaidi, ili maisha yako yaweze kuwa ya thamani zaidi na yajae furaha, na kisha unapaswa kusubiri “hukumu” ya Mungu kwako. Nashangaa iwapo mpango wako utahusisha kumpenda—Ningependa kwamba mipango ya watu wote iwe ile inayokamilishwa na Mungu, na iwe ya uhalisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 42

619. Mwanadamu lazima azingatie kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na hapaswi kuridhika na hali yake ya sasa. Kuishi kama mfano wa Petro, lazima awe na maarifa na uzoefu wa Petro. Mtu lazima ashikilie mambo ambayo ni ya juu na zaidi ya yaliyo makuu. Ni lazima yeye afuatilie kwa ndani zaidi, usafi zaidi wa upendo wa Mungu, na maisha ambayo yana thamani na umuhimu. Haya tu ndiyo maisha; hivi tu ndivyo mwanadamu atakuwa sawa na Petro. Lazima kuzingatia kuwa makini kwa kuingia kwako kwa upande mwema, na lazima uhakikishe kwamba haurudi nyuma kwa ajili ya urahisi wa kitambo na kupuuza mambo mengine makubwa, zaidi maalum, na zaidi kwa ukweli wa vitendo. Upendo wako lazima uwe wa vitendo, na lazima utafute njia ya kujitoa katika upotovu huu, maisha yasiyo na kujali ambayo hayana tofauti na ya mnyama. Lazima uishi maisha ya maana, maisha ya thamani, na usijipumbaze, au kufanya maisha yako kama kitu cha kuchezea. Kwa kila mtu ambaye anatumai kumpenda Mungu, hakuna ukweli usioweza kupatikana, na hakuna haki wasioweza kusimama imara nayo. Unafaa kuishije maisha Yako? Unapaswa kumpenda Mungu vipi na kutumia upendo huu ili kukidhi hamu Yake? Hakuna kubwa zaidi katika maisha Yako. Zaidi ya yote, lazima uwe na matarajio hayo na uvumilivu, na hupaswi kuwa kama wanyonge wasio na nia. Lazima ujifunze jinsi ya kupitia maisha ya maana, na kuuona ukweli wa maana, na hupaswi kujichukua kipurukushani katika njia hiyo. Bila wewe kujua, maisha Yako yatakupita tu; na baada ya hapo, je utakuwa una fursa nyingine ya kumpenda Mungu? Je, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu baada ya kufa? Lazima uwe na matarajio na dhamiri sawa na ya Petro; maisha Yako ni lazima yawe na maana, na usifanye mchezo na nafsi yako. Kama mwanadamu, na kama mtu ambaye anamfuata Mungu, ni lazima uweze kufikiria kwa makini jinsi unavyoendesha maisha yako, jinsi unapaswa kujitoa mwenyewe kwa Mungu, jinsi unapaswa kuwa na imani yenye maana zaidi katika Mungu, na jinsi, kwa kuwa wewe unampenda Mungu, unapaswa kumpenda Yeye kwa njia ambayo ni safi zaidi, nzuri zaidi, na bora zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

620. Mahitaji sahihi ya Mungu kwa wanadamu na wale ambao wanamfuata ni kama ifuatavyo. Mungu anahitaji mambo matano kutoka kwa wale wanaomfuata; imani ya kweli, ufuasi wenye uaminifu, utiifu kamili, ufahamu wa kweli na heshima za kutoka moyoni.

Katika mambo haya matano, Mungu anahitaji kuwa watu wasimshuku tena, wala kumfuata wakitumia fikira zao au mitazamo ikosayo uyakini na iliyo dhahania; Ni lazima wamfuate Mungu bila fikira au dhana zozote. Mungu anahitaji kuwa wote wanaomfuata wafanye hivyo kwa uaminifu, sio kwa shingo upande au bila kujizatiti. Mungu anapokupa mahitaji yoyote, au kukujaribu, kukuhukumu, kukushughulikia na kukupogoa, au kukuadhibu na kukuangamiza, unapaswa kuwa mtiifu kabisa Kwake. Hufai kuuliza kilichosababisha, au kuweka masharti, au hata uongee kuhusu sababu. Utiifu wako lazima uwe usio na shaka. Maarifa ya Mungu ni kipengele ambacho watu wengi wanakosea. Mara kwa mara wanamlazimishia Mungu misemo, matamshi, na maneno ambayo hayahusiani na Yeye, wakiamini kuwa haya maneno ndiyo ya kweli kuhusu kumfahamu Mungu. Kumbe hawajui kuwa hii misemo, ambayo inatoka kwa fikira za watu, ung'amuzi wao, na busara zao, havina uhusiano wowote na kiini cha Mungu. Na kwa hiyo, Ninataka kukwambia kuwa, katika ufahamu wa watu unaotamaniwa na Mungu, Mungu haulizi tu kwamba umtambue Mungu na maneno Yake, lakini kuwa ufahamu wako juu ya Mungu ni sahihi. Hata kama unaweza kusema sentensi moja tu, au una ufahamu mdogo tu, huu ufahamu mdogo ni sahihi na wa kweli, na unalingana na kiini cha Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hapendi sifa na wao kumtukuza Yeye kwa hali isiyo halisi na yenye nia mbaya. Zaidi ya hayo, Anachukia watu wanapomchukulia kama hewa. Anachukia ambapo, wakati wa majadiliano juu ya mada kuhusu Mungu, watu wanazungumza kimzaha, wakiongea kwa hiari bila ya kujali, wakiongea wapendavyo; zaidi ya hayo, anawachukia wale wanaojifanya wanamjua Mungu, na wanaringa kuhusu ufahamu wa Mungu, wakijadili mada kuhusu Mungu bila mipaka au kipimo. La mwisho Kati ya yale mahitaji matano lilikuwa ni kumheshimu Mungu kutoka moyoni. Hili ndilo hitaji kuu la Mungu kwa wale wote wanaomfuata. Wakati mtu ana ufahamu wa kweli na sahihi kumhusu Mungu, anaweza kumheshimu Mungu na kuepuka maovu. Heshima hii hutoka ndani ya moyo wake, ni ya hiari, na sio kwa sababu Mungu amemshurutisha. Mungu hataki utoe zawadi ya mwelekeo wowote wa kupendeza, au tabia, au mienendo ya nje Kwake; badala yake, anataka kwamba umheshimu na umwogope kutoka ndani ya moyo wako. Heshima hii inaafikiwa kutokana na mabadiliko katika tabia ya maisha yako, kwa sababu una ufahamu juu ya Mungu, kwa sababu unaelewa matendo ya Mungu, kwa sababu ya uelewa wako wa kiini cha Mungu, na kwa sababu umetambua ukweli kuwa wewe ni mmoja wa viumbe wa Mungu. Na kwa hiyo, nia yangu ya kutumia neno “kutoka moyoni” kwa kurejelea heshima hapa ni kwamba wanadamu waelewe kuwa heshima ya watu kwa Mungu inapaswa kutoka ndani ya mioyo yao.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

621. Nyote mnapaswa sasa kujichunguza haraka iwezekanavyo, ili muone ni kiasi gani cha kunisaliti kimebaki ndani yenu. Ninangojea jibu lenu kwa pupa. Msiwe wazembe katika kunishughulikia. Kamwe Mimi huwa sichezi michezo na watu. Nikisema Nitatenda jambo basi hakika Nitalitenda. Natumai kila mmoja wenu atakuwa mtu anayeyachukulia maneno Yangu kwa uzito, na asifikirie kana kwamba maneno hayo ni ubuni wa sayansi. Ninachotaka ni kitendo thabiti kutoka kwenu, siyo mawazo yenu. Baadaye, lazima mjibu maswali Yangu, ambayo ni kama ifuatavyo: 1. Ikiwa kwa kweli wewe ni mtendaji huduma, je, unaweza kutoa huduma Kwangu kwa uaminifu, bila dalili yoyote ya uzembe au mtazamo hasi? 2. Je, ukigundua kuwa Sijawahi kukuthamini, bado utaweza kusalia na kunitolea huduma ya maisha yote? 3. Ikiwa bado Ninakudharau sana licha ya wewe kutumia bidii nyingi, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika mashaka? 4. Ikiwa, baada ya wewe kufanya matumizi kwa ajili Yangu, Siyaridhishi mahitaji yako madogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi, au hata ukasirike na kunitukana kwa sauti kubwa? 5. Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana, ukinipenda sana, ilhali unateseka na ugonjwa, umaskini, na kutengwa na marafiki na jamaa zako, au ikiwa unavumilia taabu nyingine zozote maishani, bado uaminifu na upendo wako Kwangu utaendelea? 6. Ikiwa hakuna lolote kati ya yale ambayo umefikiria moyoni mwako linalingana na kile ambacho Nimefanya, je, utaitembea njia yako ya baadaye kwa namna gani? 7. Ikiwa hupokei lolote kati ya mambo ambayo ulitarajia kupokea, je, unaweza kuendelea kuwa mfuasi Wangu? 8. Ikiwa hujawahi kuelewa kusudi na umuhimu wa kazi Yangu, je, unaweza kuwa mtu mtiifu ambaye hatoi hukumu kiholela na kufanya maamuzi? 9. Je, unaweza kuthamini maneno yote ambayo Nimeyanena na kazi yote ambayo Nimeifanya wakati Nimekuwa pamoja na wanadamu? 10. Je, unaweza kuwa mfuasi Wangu mwaminifu, aliye tayari kuvumilia mateso ya maisha kwa ajili Yangu, ingawa hupokei chochote? 11. Je, unaweza kuachilia kuzingatia, kupanga, au kuandaa njia yako ya kuendelea kuishi ya siku za baadaye kwa ajili Yangu? Maswali haya yanawakilisha mahitaji Yangu ya mwisho ninayotaka kutoka kwenu, nami Natumai kuwa ninyi nyote mnaweza kunipa majibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

622. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwingine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili katika wakati ujao na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, lazima bado Nikuambie: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

Iliyotangulia: XIII. Maneno Juu ya Mahitaji, Ushawishi, Maliwazo na Maonyo ya Mungu

Inayofuata: B. Kushawishi kwa Mungu wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp