B. Kushawishi kwa Mungu wa Mwanadamu

623. Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni utakuwa kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. Bila kujali jinsi ambavyo Mungu huwaokoa watu, yote hufanywa kwa kuwafanya wajitenge na asili yao ya zamani ya kishetani; yaani, Yeye huwaokoa kwa kuwafanya watafute uzima. Wasipotafuta uzima basi hawatakuwa na njia yoyote ya kukubali wokovu wa Mungu. Wokovu ni kazi ya Mungu Mwenyewe na kutafuta uzima ni kitu ambacho mwanadamu anapaswa kumiliki ili kupokea wokovu. Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa kwa baraka na neema Zake, ili kwamba waweze kumpa Mungu mioyo yao. Hivyo ni kusema, Yeye kumgusa mwanadamu ni kumwokoa. Aina hii ya wokovu inafanywa kwa kufanya makubaliano. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu atatiimbele ya jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Wokovu uliopewa leo unatokea wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, iwe hukumu ya haki au usafishaji na adhabu visivyo na huruma, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kila anaainishwa kulingana na aina yake, ama makundi ya wanadamu yanafichuliwa, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? Nyote mmeona Mungu mwenye mwili na kutambua kudura na hekima Yake; zaidi ya hayo, umepitia hali ya kupigwa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara. Lakini je, hujapokea pia neema kubwa? Je, baraka zako si kubwa zaidi kuliko za mtu yeyote mwingine? Neema zako ni nyingi zaidi kuliko utukufu na utajiri uliofurahiwa na Sulemani! Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, kuwaadhibu ninyi wanadamu wa kufa hakuwezi kufanywa kwa kutamka neon moja tu? Ningekuwa bado na haja ya kuwaangamiza baada ya kuwashutumu kwa makusudi? Je, bado hamwamini haya maneno Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

624. Nyinyi nyote mnaishi mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wapotovu na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kwa kusudi la kumkamilisha mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu. Iwapo huwezi kuona kuwa kila kitu unachofanyiwa ni mapenzi na wokovu, ukidhani kuwa ni mbinu tu, njia ya kumtesa mwanadamu na kitu kisichoaminika, basi ni bora urudi duniani mwako uendelee kupata mateso na ugumu wa maisha! Ikiwa uko tayari kuwa kwenye mkondo huu na kufurahia hukumu hii na wokovu huu wa ajabu, na kufurahia baraka hizi ambazo haziwezi kupatikana kokote katika ulimwengu wa wanadamu, na kufurahia upendo huu, basi kuwa mzuri: Salia kwenye mkondo huu ili kukubali kazi ya ushindi ili uweze kufanywa mkamilifu. Leo, unaweza kupitia mateso na usafishaji kidogo kwa sababu ya hukumu ya Mungu, mateso haya ni ya thamani na ya maana. Japo kuadibu na hukumu ni usafishaji na ufichuzi usio na huruma kwa mwanadamu, uliokusudiwa kuadhibu dhambi zake na kuadhibu mwili wake, kazi hii haijanuiwa kukashifu na kuuzima mwili wake. Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi. Ninyi wenyewe mmeipitia sana kazi hii na ni wazi, haijawaongoza kwenye njia mbaya! Yote ni ili kukufanya uishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na yote yanatimizwa na ubinadamu wako wa kawaida. Kila hatua ya kazi hufanywa kwa misingi ya mahitaji yako, kulingana na udhaifu wako, kulingana na kimo chako halisi, na hamjatwikwa mzigo msioweza kuubeba. Japo huwezi kuliona hili wazi kwa sasa, na unajihisi Ninakuwa mgumu kwako, japo unadhani kuwa Ninakuadibu na kukuhukumu na kukuadibu kila siku kwa kuwa Ninakuchukia, na ingawa unachokipokea ni kuadibu na hukumu, hali halisi ni kuwa yote ni mapenzi kwako, pia ni ulinzi mkubwa kwako. Ikiwa huwezi kung’amua maana ya ndani ya kazi hii, basi huna njia ya kuendelea katika uzoefu wako. Unapaswa kuliwazwa kwa sababu ya huo wokovu. Usikatae kuzirudia busara zako. Baada ya kusafiri umbali huu, unapaswa kuuona wazi umuhimu wa kazi hii ya kushinda. Hupaswi tena kushikilia mtazamo fulani kama huo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

625. Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake. Leo ni kwa sababu tu ya kutiwa moyo na Mungu na fadhili Zake ndio watu wamepokea usafishaji wa maneno Yake. Hii ni baraka ya kila mtu ambaye anazaliwa katika siku za mwisho—je, nyinyi binafsi mmepitia haya? Ni katika hali zipi watu wanapaswa kuteseka na kuwa na vipingamizi imekusudiwa na Mungu, na haitegemei mahitaji ya watu wenyewe. Hii ni kweli kamili. Kila muumini anapaswa kuwa na uwezo wa kupitia majaribio ya maneno ya Mungu na kuteseka ndani ya maneno Yake. Je, hili ni jambo mnaloweza kuliona dhahiri? Kwa hiyo kuteseka ulikopitia kumebadilishana na baraka za leo; ikiwa hutateseka kwa ajili ya Mungu, huwezi kupata sifa Zake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari

626. Kwamba wewe huweza kukubali hukumu, kuadibu, kuangamiza, na usafishaji wa maneno ya Mungu, na, aidha, unaweza kukubali maagizo ya Mungu, lilijaaliwa na Mungu mwanzoni mwa wakati, na hivyo lazima usihuzunishwe sana wakati ambapo wewe huadibiwa. Hakuna anayeweza kuondoa kazi ambayo imefanywa ndani yenu, na baraka ambazo zimetolewa ndani yenu, na hakuna anayeweza kuondoa yote ambayo mmepewa ninyi. Watu wa dini hawastahimili mlingano na ninyi. Ninyi hamna ubingwa mkuu katika Biblia, na hamjajizatiti na nadharia za kidini, lakini kwa sababu Mungu amefanya kazi ndani yenu, mmepata zaidi ya yeyote kotekote katika enzi—na kwa hiyo hii ni baraka yenu kuu zaidi. Kwa sababu ya hili, lazima mjitolee hata zaidi kwa Mungu, na hata waaminifu zaidi kwa Mungu. Kwa sababu Mungu hukuinua, lazima utegemeze juhudi zako, na lazima utayarishe kimo chako kukubali maagizo ya Mungu. Lazima usimame imara mahali ambapo Mungu amekupa, ufuatilie kuwa mmoja wa watu wa Mungu, ukubali mafunzo ya ufalme, upatwe na Mungu na hatimaye kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Je, wewe una maazimio haya? Kama una maazimio hayo, basi hatimaye una hakika ya kupatwa na Mungu, na utakuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba agizo kuu ni kupatwa na Mungu na kugeuka kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Haya ni mapenzi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

627. Kwa ndugu wote ambao wameisikia sauti Yangu: Mmeisikia sauti ya hukumu Yangu kali na mmevumilia mateso yaliyokithiri. Hata hivyo, mnapaswa kujua kwamba katika sauti Yangu kali kumejificha nia Zangu! Ninawafundisha nidhamu ili muweze kuokolewa. Mnapaswa kujua kwamba kwa wana Wangu wapendwa, Nitawafundisha nidhamu na kuwapogoa na kuwafanya muwe wakamilifu hivi karibuni. Moyo Wangu una hamu sana, lakini ninyi hamuelewi moyo Wangu na hamtendi kulingana na neno Langu. Maneno Yangu leo yanawajia ninyi na kuwafanya kutambua kweli kwamba Mungu ni Mungu mwenye upendo na nyote mmepitia upendo wa dhati wa Mungu. Hata hivyo, pia kuna idadi ndogo ya watu ambao wanajifanya na wanapoona huzuni ya watu wengine pia wao watakuwa na machozi machoni mwao. Kuna wengine ambao—kwa juu—wanaonekana kuwa wadeni wa Mungu na wanaonekana wenye majuto, lakini ndani yao, hawamwelewi Mungu kwa kweli na wala hawana uhakika kumhusu Yeye; badala yake, ni sura ya kinafiki tu. Ninawachukia watu hawa zaidi! Siku moja, watu hawa wataondolewa kutoka katika mji Wangu. Nia Yangu ni kwamba Nataka wale wanaonitaka kwa ari, na wale tu ambao wananifuatilia kwa moyo wa kweli wanaweza kunipendeza—kwani wao Nitawaunga mkono bila shaka kwa mikono Yangu mwenyewe na kuhakikisha kuwa hawatapata majanga yoyote. Watu wanaomtaka Mungu kwa kweli watakuwa tayari kujali mogo wa Mungu na kufanya mapenzi Yangu. Kwa hiyo, ninyi mnapaswa kuingia katika ukweli hivi karibuni na kukubali neno Langu kama maisha yenu—huu ndio mzigo Wangu mkubwa zaidi. Ikiwa makanisa na watakatifu wote wanaingia katika uhalisi na wote waweze kushiriki na Mimi moja kwa moja, wawe uso kwa uso na Mimi, na kutenda ukweli na haki, ni hapo tu ndipo wao ni wana Wangu wapendwa, wale ambao napendezwa nao sana. Watu hawa, Nitawapa baraka zote kubwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 23

628. Leo hii, huwezi tu kuridhika na jinsi wewe umeshindwa, lakini lazima pia uzingatie njia ambayo utatembelea siku zijazo. Lazima uwe na matarajio na ujasiri wa kufanywa mkamilifu, na hupaswi daima kufikiria kwamba huwezi. Je, ukweli una maonevu? Je, ukweli huwapinga watu kwa makusudi? Kama wewe utaufuata ukweli, je unaweza kukushinda? Kama wewe utasimama imara kwa ajili ya haki, je utakuangusha chini? Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli unakupuuza, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha; Iwapo unaishi katika mwanga, na hujaweza kuupata mwanga, hiyo siyo kwa sababu mwanga hauwezi kukuangazia, lakini kwa sababu wewe hujaweka makini kwa kuwepo kwa mwanga, na hivyo mwanga umeondoka kwa kimya. Kama huwezi kufuata, basi inaweza kusemwa kwamba wewe ni taka usiye na maana, na huna ujasiri katika maisha yako, na huna roho ya kupinga nguvu za giza. Wewe ni mdhaifu mno! Huwezi kutoroka nguvu za Shetani ambazo zimekuzingira, na kuwa uko tayari tu kuishi haya maisha ya usalama na kufa katika ujinga. Kile unachopaswa kufanya ni kutekeleza azma yako ya kuwa mshinde; huu ni wajibu wako uliokushikilia. Kama wewe umeridhika na kushindwa, basi unafukuza kuwepo kwa mwanga. Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya. Msitupilie mbali ukweli kwa ajili ya maisha ya amani ya familia, na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema, na unapaswa kufuatilia njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi. Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je, si huko ni kupoteza maisha Yako? Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii? Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja, na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima; hakuna maana ya kuwepo kwao!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

629. Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho. Lazima uwe na maono kama msingi wako. Kama siku ya kupatwa kwako na maafa itakapokuja, unapaswa kufanya nini? Bado ungeweza kufuata? Usiseme kwa wepesi kama utaweza kufuata hadi mwisho. Ni bora kwanza ufungue macho yako wazi kabisa ili uone wakati wa sasa ni upi. Ingawa sasa mnaweza kuwa kama nguzo za hekalu, wakati utakuja ambapo nguzo hizi zote zitatafunwa na funza, na kusababisha hekalu kuanguka, kwa sababu kwa sasa kuna maono mengi sana ambayo mmekosa. Mnachozingatia tu ni dunia zenu wenyewe ndogo, na hamjui njia iliyo ya kutegemewa kabisa, njia iliyo mwafaka zaidi ya kutafuta ni ipi. Hamtilii maanani maono ya kazi ya leo, na hamyashikilii mambo haya mioyoni mwenu. Je, mmefikiria kwamba siku moja Mungu atawaweka katika mahali pasipojulikana? Je, mnaweza kuwazia siku ambayo huenda Nikawapokonya kila kitu, ni kipi kingewakumba? Nguvu yenu siku hiyo ingekuwa vile ilivyo sasa? Je, imani yenu ingejitokeza tena? Katika kumfuata Mungu, lazima myajue maono haya makubwa ambayo ni “Mungu.” Hili ndilo suala muhimu zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!

630. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Katika njia hii, wanadamu wengi wanaweza kusema wana maarifa mengi, lakini katika wakati wao wa kufa, macho yao hujawa machozi, nao hujichukia wenyewe kwa kuharibu maisha yao yote na kuishi maisha yasiyo na mazao hadi uzeeni. Wanaelewa tu mafundisho lakini hawawezi kutia ukweli katika vitendo na kushuhudia kwa Mungu, badala yake wakikimbia huku na kule, wakiwa na kazi kama nyuki; mara wanapochungulia kaburi wao hatimaye huona kwamba hawana ushuhuda wa kweli, kwamba hawamjui Mungu kamwe. Je, si huku ni kuchelewa mno? Kwa nini usichukue nafasi hii na kufuatilia ukweli unaoupenda? Kwa nini usubiri hadi kesho? Iwapo katika maisha huwezi kuteseka kwa ajili ya ukweli au kutafuta kuupata, inaweza kuwa kwamba unataka kujuta katika saa yako ya kufa? Ikiwa hivyo, basi kwa nini umwamini Mungu? Kwa kweli, kuna mambo mengi ambayo mtu, iwapo ataweka juhudi kidogo tu, anaweza kuweka ukweli katika vitendo na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa binadamu daima umepagawa na mapepo na kwa hivyo hawezi kutenda mambo kwa ajili ya Mungu. Badala yake, yeye daima yumo katika safari ya huku na kule kwa sababu ya mwili, na hafaidiki na chochote mwishowe. Ni kwa sababu hizi ndio mtu hupata matatizo ya mara kwa mara na mateso. Je, haya sio mateso ya Shetani? Je, huu sio ufisadi wa mwili? Hufai kumdanganya Mungu kwa maneno ya mdomo. Badala yake, lazima uchukue hatua inayoonekana. Usijidanganye; ni nini maana katika hilo? Ni faida gani utakayopata kutokana na kuishi kwa ajili ya mwili wako na kufanya bidii kwa ajili ya umaarufu na mali ya dunia?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

631. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme? Ikiwa kusudi la kufuatilia kwako si kutafuta ukweli, basi afadhali utumie fursa hii na kurudi duniani ili kufanikiwa. Kupoteza muda wako hivi kwa kweli hakuna thamani—kwa nini ujitese? Je, si kweli kwamba unaweza kufurahia mambo ya aina yote katika dunia hii nzuri? Pesa, wanawake warembo, hadhi, majivuno, familia, watoto, na kadhalika—je, matokeo haya ya dunia siyo mambo mazuri zaidi ambayo ungeweza kufurahia? Kuna faida gani kuzurura zurura hapa ukitafuta mahali ambapo unaweza kuwa na furaha? Mwana wa Adamu hana pahali pa kulaza kichwa Chake, hivyo ungekuwaje na pahali pa utulivu? Angewezaje kukuumbia pahali pazuri pa utulivu? Hilo lawezekana? Kando na hukumu Yangu, leo unaweza kupokea tu mafundisho ya ukweli. Huwezi kupata faraja kutoka Kwangu na huwezi kupata kitanda cha starehe unachotamani sana usiku na mchana. Sitakupa utajiri wa duniani. Ukifuatilia kwa kweli, basi Niko tayari kukupa njia ya uzima yote, kukutaka uwe kama samaki aliyerudi majini. Usipofuatilia kwa kweli, Nitayafuta yote. Siko tayari kutoa maneno kutoka kwa kinywa Changu kwa wale ambao ni wenye tamaa ya faraja, ambao ni kama nguruwe na mbwa tu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?

632. Leo hii ni imani inayokuruhusu kushindwa, na kushindwa ndiko kunakufanya uamini kila tendo la Yehova. Ni kwa sababu tu ya imani unapokea kuadibu na hukumu ya aina hii. Kupitia kuadibu na hukumu hizi, umeshindwa na kukamilishwa. Bila aina hii ya kuadibu na hukumu upokeayo leo hii, imani yako ingekuwa bure, kwa sababu humtambui Mungu; haijalishi unamwamini kiasi gani, imani yako bado itakuwa maonyesho matupu yasiyokuwa na misingi katika uhalisi. Ni baada tu ya kupokea aina hii ya kazi ya kushinda inayokufanya mtiifu kabisa ndipo imani yako inakuwa kweli na inayotegemewa na roho yako kumrudia Mungu. Japo umehukumiwa na kulaaniwa sana kwa sababu ya hili neno “imani,” una imani ya kweli, na unapokea kitu cha kweli zaidi, halisi zaidi, na chenye thamani zaidi. Hii ni kwa sababu ni katika harakati ya hukumu tu ndipo unaona hatima ya viumbe wa Mungu; ni katika hukumu hii ndio unapata kuona kuwa Muumba anapaswa kupendwa; ni katika kazi kama hiyo ya kushinda ndio unapata kuona mkono wa Mungu; ni katika kushinda huku unapata kutambua kwa ukamilifu maisha ya mwanadamu; ni katika kushinda huku unapata kujua njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na kufahamu maana ya kweli ya “mwanadamu”; ni kupitia tu huku kushinda ndiko unaweza kuona tabia ya haki ya mwenye Uweza na uso Wake mzuri na mtukufu. Ni katika kazi hii ya kushinda ndiko unaweza kujifunza kuhusu asili ya mwanadamu na kufahamu “historia isiyokufa” ya mwanadamu; ni katika kushinda huku ndiko unapata kufahamu mababu za wanadamu na asili ya upotovu wa mwanadamu; ni katika kushinda huku ndio unapokea furaha na starehe pamoja na kuadibu, nidhamu, na maneno ya kuonya kutoka kwa Muumba kwa wanadamu ambao Aliwaumba; katika kazi hii ya kushinda, ndipo unapokea baraka na majanga ambayo mwanadamu anapaswa kupokea…. Je, haya yote si kwa ajili ya hiyo imani yako ndogo? Je, baada ya kuvipata vitu hivi vyote imani yako haijakua? Hujapata kiwango kikubwa ajabu? Hujasikia tu maneno ya Mungu na kuona hekima ya Mungu, lakini wewe binafsi umepitia pia kila hatua ya kazi. Labda utasema kuwa usingekuwa na imani, basi usingepata aina hii ya kuadibu au aina hii ya hukumu. Ila unapaswa kufahamu kuwa bila imani, usingeweza tu kupokea aina hii ya kuadibu na ulinzi kutoka kwa mwenye Uweza, bali pia daima ungepoteza fursa ya kumwona Muumba. Usingejua asili ya wanadamu na kufahamu umuhimu wa maisha ya mwanadamu. Japo mwili wako utakufa na roho yako kuondoka, bado hutayafahamu matendo yote ya Muumba. Aidha hutafahamu kuwa Muumba alifanya kazi kubwa kiasi hicho duniani baada ya kuwaumba wanadamu. Kama mmojawapo wa hawa wanadamu Aliowaumba, je, uko tayari kutumbukia gizani kiasi hiki bila fahamu na kukumbana na adhabu ya milele? Ukijitenga na kuadibu na hukumu ya sasa, utapatana na kitu gani? Je, unafikiri ukishajitenga na hukumu ya sasa, utaweza kuepukana na haya maisha magumu? Je, si kweli kwamba ukiondoka “mahala hapa,” utakachokipata ni mateso machungu au majeraha kutoka kwa ibilisi? Je, waweza kukumbana na mchana na usiku zisizostahimilika? Je, unafikiri kwamba kwa kuepuka hukumu leo, unaweza kukwepa milele yale mateso ya siku zijazo? Ni kitu gani kitakukumba? Inaweza kuwa paradiso ya duniani unayoitarajia? Unafikiri unaweza kuepuka kuadibu kwa milele kwa baadaye kwa kuukimbia uhalisi kama ufanyavyo? Baada ya leo, je, utawahi kuweza kuipata fursa na baraka kama hii tena? Je, utapata fursa na baraka utakapokuwa umekumbwa na misukosuko? Je, utapata fursa na baraka wanadamu wote waingiapo katika pumziko? Maisha yako ya furaha ya sasa na hiyo familia yako ndogo yenye amani—vyaweza kuwa kibadala cha hatima yako? Iwapo una imani ya kweli, na iwapo unafaidi pakubwa kwa sababu ya imani yako, basi hayo yote ndiyo—wewe kiumbe—unapaswa kufaidi na vilevile kile ambacho ulipaswa kuwa nacho. Aina hii ya kushinda ndiyo ya faida zaidi kwa imani na maisha yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

633. Musa alipougonga mwamba, na maji yaliyokuwa yametolewa na Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza kinubi kwa kunisifu Mimi, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake waliojaa kote milimani na mali nyingi sana, na mwili wake kujawa na majipu mabaya, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Sababu ya yanayodaiwa kuwa mataifa mengi yasiyo ya Kiyahudi kupata ufunuo Wangu, na yakajua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Je si wote ambao wamepigwa na maneno Yangu makali na bado wanafarijiwa nayo na wameokoka—wamefanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Wale wanaoamini Kwangu lakini bado hupitia mateso, je si pia wamekataliwa na dunia? Wale wanaoishi nje ya neno Langu, wakikimbia mateso ya majaribu, si wao wote wanazurura tu ulimwengu? Wao ni sawa na majani ya msimu wa kupukutika kwa majani yanayopeperuka hapa na pale, bila pahali pa kupumzika, sembuse neno Langu la kufutia machozi. Ingawa adabu na usafishaji wangu hauwafuati wao, je, wao si waombaji, wanaoelea kila mahali, ambao wakitangatanga katika mitaa iliyo nje ya Ufalme wa mbinguni? Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli? Je, unaweza kweli kupata tabasamu hata dhaifu ya kutosheleza kutoka kwa dunia kwa kuepuka adabu yangu? Je, unaweza kweli kutumia starehe zako za kidunia kuficha utupu ulio katika moyo wako usioweza kufichika? Unaweza kumdanganya mtu yeyote katika familia yako, ilhali huwezi kunidanganya Mimi kamwe. Kwa kuwa imani yako ni ndogo sana, mpaka wa leo huna uwezo wa kupata raha inayoletwa na maisha. Nakushauri: heri kutumia nusu ya maisha yako kwa ajili Yangu kwa dhati kuliko kuishi maisha yako yote katika hali hafifu na kujishughulisha kwa ajili ya mwili, kuvumilia mateso yote ambayo ni vigumu binadamu kuvumilia. Kuna faida gani ya wewe kujipenda sana na kuikimbia adabu Yangu? Kuna faida gani wewe kujificha kutoka kwa adabu Yangu ya muda mfupi tu, na mwishowe kupate aibu ya milele, na adabu ya milele? Mimi, kwa hakika, Simlazimishi yeyote kufanya mapenzi Yangu. Iwapo mtu kweli anayo nia ya kujiwasilisha kwa mipango Yangu yote, Sitamtendea vibaya. Lakini Nahitaji kwamba watu wote waamini ndani Yangu, kama vile Ayubu alivyoamini ndani Yangu, Yehova. Iwapo imani yenu inazidi ile ya Tomaso, basi imani yenu itapata pongezi Zangu, katika uaminifu wenu mtapata furaha Yangu, na hakika mtapata utukufu Wangu katika siku zenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi

634. Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba[a] sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilhali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Si ndivyo ilivyo? Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, mna uhakika na uchaguzi mlioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika. Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, nyinyi huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia mnachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni[b] kati ya starehe na umasikini, tena mlichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, mnachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa. Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu? Kwa wakati wa sasa, chaguo lenu ni nini? Mtayakubali maneno Yangu, au yatawachosha? Siku Yangu imewekwa wazi kabisa mbele ya macho yenu, na kile mnachokiona ni maisha mapya na mwanzo mpya. Hata hivyo, ni lazima niwaambie kwamba huu mwanzo mpya si mwanzo wa kazi mpya iliyopita, bali ni mwisho wa ya kale. Yaani, hili ni tendo la mwisho. Ninaamini nyote mtaelewa kitu ambacho si cha kawaida kuhusu mwanzo huu mpya. Lakini siku moja hivi karibuni, mtaelewa maana halisi ya huu mwanzo mpya, kwa hivyo hebu sote tuipite na kuikaribisha tamati inayofuata! Hata hivyo, kitu ambacho Ninaendelea kutofurahishwa nacho ni kwamba pale mnapokabiliwa na mambo ambayo si ya haki na mambo ya haki, daima mmekuwa mkichagua chaguo la kwanza. Lakini hayo yote yako katika maisha yenu ya zamani. Pia Ninatumai kuyasahau yale yote yaliyotokea katika maisha yenu ya zamani, kitu kimoja baada ya kingine, ingawa hili ni gumu sana kufanya. Lakini bado nina njia nzuri sana ya kulitimiza. Acha maisha ya baadaye yachukue nafasi ya maisha ya zamani na kuacha kivuli cha maisha yenu ya zamani kiondolewe badala ya utu wenu halisi wa leo. Hii ina maana kwamba nitawasumbua tena ili uweze kufanya maamuzi kwa mara nyingine tena na tutaona kabisa nyinyi ni waaminifu kwa nani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

635. Hawapaswi kuwa bila maadili, matarajio, au tabia ya maendeleo ya shauku; hawapaswi kuvunjika moyo juu ya matarajio yao wala hawapaswi kupoteza matumaini maishani au kupoteza imani katika siku zijazo; wanapaswa kuwa na uvumilivu kuendelea na njia ya ukweli ambayo sasa wamechagua kufanikisha matamanio yao ya kutumia maisha yao yote kwa ajili Yangu; hawapaswi kuwa bila ukweli, wala kuficha unafiki na udhalimu, bali wanapaswa kusimama imara katika msimamo unaofaa. Hawapaswi tu kuzurura, bali wanapaswa kuwa na roho ya kuthubutu kujitolea mhanga na kujitahidi kwa ajili ya haki na ukweli. Vijana wanapaswa kuwa na ujasiri wa kutoshindwa na ukandamizaji wa nguvu za giza na kubadili umuhimu wa uwepo wao. Vijana hawapaswi kukubali shida bila kulalamika, bali wanapaswa wawe wazi na wa kusema bila kuficha, na roho ya msamaha kwa ndugu wao. Bila shaka haya ni mahitaji Yangu ya kila mtu pamoja na ushauri Wangu kwa kila mtu. Hata zaidi, ni maneno Yangu ya kutuliza kwa vijana wote. Mnapaswa kutenda kulingana na maneno Yangu. Hasa vijana hawapaswi kuwa bila azimio la utambuzi katika masuala, na la kutafuta haki na ukweli. Yale mnayopaswa kufuata ni mambo yote mazuri na mema, na mnapaswa kupata uhalisi wa mambo yote mazuri, na pia kuwajibika juu yaa maisha yenu—hampaswi kuyachukulia kwa wepesi. Watu huja duniani na ni nadra kupatana na Mimi, na pia ni nadra kuwa na fursa ya kutafuta na kupata ukweli. Kwa nini msithamini wakati huu mzuri kama njia sahihi ya kutafuta katika maisha haya? Na ni kwa nini daima nyinyi hupuuza sana ukweli na haki? Kwa nini daima nyinyi hujikanyaga na kujiangamiza kwa ajili ya ule udhalimu na uchafu ambao huchezea watu? Na kwa nini mnajishughulisha na kile ambacho wadhalimu hufanya kama watu wazee? Kwa nini mnaiga njia za zamani za mambo ya kale? Maisha yenu yanapaswa kujaa haki, ukweli, na utakatifu; maisha yenu hayapaswi kupotoshwa katika umri mdogo hivyo, yakiwasababisha kuanguka kuzimuni. Je, hamhisi kwamba hili ni la kusikitisha sana? Je, hamhisi kwamba hili silo haki kwenu sana?

Nyinyi nyote mnapaswa kufanya kazi yenu sahihi kabisa na kuidhabihu juu ya madhabahu Yangu kama dhabihu bora zaidi, za kipekee ambazo mnanipa. Nyote mnapaswa kusimama imara katika msimamo wenu wenyewe na msipeperushwe peperushwe na kila upepo mwanana kama mawingu angani. Mnafanya kazi kwa bidii nusu ya maisha yenu, basi kwa nini msitafute hatima mnapaswa kuwa nayo? Mnafanya kazi kwa bidii kwa muda wa nusu ya maisha ilhali mnawaacha wazazi wenu walio kama nguruwe na mbwa kukokota ukweli na umuhimu wa maisha yenu binafsi ndani ya kaburi. Je, huhisi kwamba huu ni udhalimu mkubwa dhidi yako? Je, huhisi kuwa kuishi maisha kwa njia hii ni kusiko na maana kabisa? Kutafuta ukweli na njia sahihi kwa njia hii mwishowe kutasababisha matatizo ili kuwa majirani ni wa wasiwasi na familia nzima haina furaha, na hupata misiba ya mauti—je, si wewe kuwa hivi ni maisha yasiyo na maana kabisa? Maisha ya nani yanaweza kuwa na bahati zaidi kuliko yako, na maisha ya nani yanaweza kuwa ya mzaha zaidi kuliko yako? Kunitafuta kwako si kwa ajili ya kupata furaha Yangu na kwa maneno ya faraja kwako? Lakini baada ya wewe kukimbia kimbia kwa nusu ya maisha na kisha kunichokoza mpaka Ninapojawa na hasira na kukupuuza au kutokusifu, basi si maisha yako yote ni bure? Na ungewezaje kuthubutu kwenda kuona roho za wale watakatifu katika enzi zote ambao wameondolewa toharani? Wewe hunijali na hatimaye unasababisha msiba wa mauti—ingekuwa bora zaidi kutumia fursa hii na kuwa na safari ya furaha kuvuka bahari kubwa mno na kisha kusikiza “utoaji” Wangu. Niliwaambia zamani kwamba wewe leo, kama usiyejali ilhali hutaki kuondoka, hatimaye ungeingizwa na kumezwa na mawimbi yaliyoinuliwa na Mimi. Je, kwa kweli mnaweza kujilinda wenyewe? Je, una imani kwamba mbinu yako ya sasa ya ukimbizaji itahakikisha kuwa unakamilishwa? Je, moyo wako si mgumu sana? Kufuata kwa aina hii, ukimbizaji wa aina hii, maisha ya aina hii, na tabia ya aina hii—jinsi gani vingeweza kupata sifa Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno kwa Vijana na kwa Wazee

636. Mungu hataki kuwashinda watu kupitia kuwaadibu, Hataki siku zote kuwatawala watu kabisa. Anawataka watu watii maneno Yake na kufanya kazi kwa namna iliyo na nidhamu, na kwa kufanya hili, waridhishe mapenzi Yake. Lakini watu hawana aibu na wanamwasi kila wakati. Naamini kwamba ni bora kwetu kutafuta njia rahisi zaidi ya kumridhisha, yaani, kutii mipango Yake yote. Ikiwa kweli unaweza kutimiza hili, utakamilishwa. Je, hili si jambo rahisi na la furaha? Chukua njia unayopaswa kuchukua; usitilie maanani kile wanachosema wengine, na usifikirie sana. Je, si mustakabali na majaliwa yako viko mikononi mwako mwenyewe? Unajaribu daima kutoroka, ukitaka kuichukua njia ya dunia—lakini mbona huwezi kutoka? Kwa nini unasitasita katika njia panda kwa miaka mingi na kisha unaishia kuichagua njia hii tena? Baada ya kuzurura kwa miaka mingi, kwa nini sasa umerudi kwa hii nyumba bila kutaka? Je, haya ni mapenzi yako? Kwa wale kati yenu mlio katika mkondo huu, ikiwa hamniamini basi sikilizeni hili: Ikiwa umepanga kuondoka, ona kama Mungu atakuruhusu, ona jinsi Roho Mtakatifu anavyokugusa—lipitie mwenyewe. Kusema ukweli, hata ukipitia msiba, lazima uupitie katika mkondo huu, na kama kuna mateso, lazima uteseke hapa, leo; huwezi kuenda pengine. Je, unaelewa hili? Utaenda wapi? Hii ni amri ya Mungu ya utawala. Je, unafikiri kwamba Mungu kulichagua kundi hili la watu hakuna maana? Katika kazi Yake leo, Mungu hakasiriki kwa urahisi—lakini watu wakijaribu kuukatiza mpango Wake, uso Wake unabadilika mara moja, ukiacha kuwa mchangamfu na kugeuka wenye huzuni. Kwa hiyo, Nakushauri utulie na kutii mipango ya Mungu, na umruhusu Akukamilishe. Watu wanaofanya hili tu ndio werevu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia … (7)

637. Hatima yenu na majaliwa yenu ni muhimu sana kwenu—ni za matatizo makubwa. Mnaamini kuwa msipofanya mambo kwa uangalifu sana, itakuwa sawa na kutokuwa na hatima, na uharibifu wa majaliwa yenu. Lakini mmewahi kufikiri kwamba kama juhudi mtu hutumia ni kwa ajili ya hatima zao tu, hizo ni kazi tu zisizo na matunda? Juhudi za aina hiyo si halisi—ni bandia na danganyifu. Kama ni hivyo, wale ambao wanafanya kazi kwa ajili ya hatima yao watapokea maangamizo yao ya mwisho, kwa sababu kushindwa katika imani ya watu katika Mungu hutendeka kwa sababu ya udanganyifu. Hapo awali Nilisema kuwa Mimi Sipendi kusifiwa mno au kupendekezwa, au kuchukuliwa kwa shauku. Ninapenda watu waaminifu kukubali hali ilivyo kuhusu ukweli na matarajio Yangu. Hata zaidi, Ninapenda wakati watu wanaweza kuonyesha uangalifu mkubwa na kufikiria kwa ajili ya moyo Wangu, na wakati wanaweza hata salimisha kila kitu kwa ajili Yangu. Ni kwa njia hii tu ndipo Moyo wangu unaweza kuliwazwa. Sasa hivi, ni mambo mangapi yapo yanayowahusu ambayo Mimi Nachukia? Ni mambo mangapi yapo yanayowahusu ambayo Napenda? Je, hakuna kati yenu ambaye ametambua ubaya wote ambao mmeonyesha kwa ajili ya hatima zenu?

Katika moyo Wangu, Sitaki kuwa Mwenye kudhuru moyo wowote ambao ni chanya na wa motisha, na Mimi hasa Sitaki kupunguza bidii ya mtu yeyote ambaye anafanya wajibu wake kwa uaminifu; hata hivyo, ni lazima Niwakumbushe kila mmoja wenu juu ya upungufu wenu na roho chafu sana ndani ya mioyo yenu. Azma ya kufanya hivyo ni kutarajia kwamba mtaweza kutoa mioyo yenu ya kweli katika kukabiliana na maneno Yangu, kwa sababu kile Nachukia zaidi ni udanganyifu wa watu kuelekezwa Kwangu. Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mnaweza kutekeleza kwa kujitokeza, kujitoa kikamilifu, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote muwe na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwenu nyinyi mfanye uamuzi bora kabisa katika kujitoa Kwangu pekee na moyo wa ibada ya mwisho. Kama mtu hana moyo huo wa ibada pekee, mtu huyo hakika atakwenda kuwa thamani ya Shetani, na Mimi Sitaendelea kumtumia. Nitamtuma nyumbani akatunzwe na wazazi wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

638. Katika siku zijazo, ikiwa wewe unabarikiwa au kulaaniwa kutaamuliwa kulingana na matendo unayotekeleza leo. Ikiwa unafaa kukamilishwa na Mungu itakuwa ni sasa hivi katika enzi hii; hakutakuwa na fursa nyingine katika siku zijazo. Mungu kwa kweli Anataka kukukamilisha sasa, na hii sio njia ya kuzungumza. Katika siku zijazo, bila kujali majaribio gani yanayokufikia, matukio gani yanayofanyika, au maafa gani yanayokupata, Mungu anataka kukukamilisha—huu ni ukweli wa hakika na usio na shaka. Je, jambo hili inaweza kuonekana kutoka wapi? Kutokana na ukweli kwamba neno la Mungu katika enzi zote na vizazi halijawahi kufikia kiwango kikubwa kama lilivyo leo—limeingia katika ulimwengu wa juu, na kazi ya Roho Mtakatifu miongoni mwa wanadamu leo ni ya kipekee. Ni wachache sana kutoka vizazi vilivyopita wameonja hili. Hata katika enzi ya Yesu hapakuwa na ufunuo wa leo; viwango vikubwa vimefikiwa katika maneno yaliyosemwa kwenu, mambo mnayoyaelewa, na mambo mnayoyapitia. Hamuondoki katikati ya majaribu na kuadibiwa, na hii ni inatosha kuthibitisha kwamba kazi ya Mungu imefikia uzuri ambao haujawahi kutokea. Hiki si kitu ambacho mwanadamu anaweza kufanya na sio kitu ambacho mwanadamu anadumisha, lakini badala yake ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo, kutokana na ukweli mwingi wa kazi ya Mungu inaweza kuonekana kwamba Mungu anataka kumkamilisha mwanadamu, na Yeye hakika Anaweza kukufanya uwe mkamilifu. Ikiwa mnaweza kuona jambo hili, ikiwa unaweza kupata ugunduzi huu mpya, basi hutangoja kuja kwa pili kwa Yesu lakini badala yake, utamruhusu Mungu akufanye mkamilifu katika enzi ya sasa. Hivyo, kila mmoja wenu anapaswa kufanya kila linalowezekana na kujitahidi sana ili aweze kukamilishwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

639. Mapenzi ya Mungu ni kuwa kila mtu aweze kufanywa kamili, na kupatwa naye hatimaye, na kutakaswa naye kabisa, na kuwa mmoja anayependwa na Yeye. Haijalishi kama Ninasema nyinyi ni wa fikra za kurudi nyuma au wa kimo cha umaskini—hii yote ni ukweli. Huku kusema kwangu hakuthibitishi kuwa Mimi nina nia kukuacha wewe, kwamba Mimi Nimepoteza matumaini kwenu, au kwa kiasi kidogo kwamba sina nia ya kuwaokoa. Leo Nimekuja kufanya kazi ya ukombozi wenu, ambayo ni kusema kuwa kazi ambayo Mimi hufanya ni mwendelezo wa kazi ya ukombozi. Kila mtu ana nafasi ya kufanywa kamili: Ili mradi uko tayari, ili mradi ufuate, na mwishowe wewe utaweza kutimiza matokeo haya, na hakuna hata mmoja wenu ambaye ataachwa. Kama wewe ni mtu wa kimo cha umasikini, mahitaji Yangu kwenu yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha umaskini; kama wewe ni wa kimo cha juu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha juu; kama wewe ni mjinga na hujui kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa ujinga wako; kama wewe unajua kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa ukweli kwamba wewe unajua kusoma na kuandika; kama wewe ni mkongwe, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa umri wako; kama wewe una uwezo wa kutoa ukarimu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa hilo; kama wewe unasema huwezi kutoa ukarimu, na unaweza tu kufanya kazi fulani, iwe ni kueneza injili, au kuchunga huduma ya kanisa, au kuhudhuria mambo mengine kwa ujumla, Ukamilifu Wangu kwako utakuwa kwa mujibu wa kazi ambayo wewe hufanya. Kuwa mwaminifu, kutii hadi mwisho kabisa, na kutafuta upendo mkuu wa Mungu—mambo haya ni lazima uyakamilishe, na hakuna vitendo vizuri zaidi kuliko mambo haya matatu. Hatimaye, mtu anatakiwa kuyafikia mambo haya matatu, na kama anaweza kuyafikia hayo atafanywa kamili. Lakini, zaidi ya yote, ni lazima ujitahidi na kuendelea kwa bidii, na usiwe wa kukaa tu kuelekea hapo. Nimesema kwamba kila mtu ana nafasi ya kufanywa mkamilifu, na ana uwezo wa kukamilishwa, na hili ni kweli, lakini hujaribu kuwa bora zaidi katika ufuatiliaji wako. Kama huwezi kuvifikia vigezo hivyo vitatu, mwishowe lazima uondolewe. Nataka kila mtu afaulu kufikia wengine, nataka kila mtu awe na kazi na kupata nuru wa Roho Mtakatifu, na kuwa na uwezo wa kutii hadi mwisho kabisa, kwa sababu huu ni wajibu wa kila mmoja wenu ambao mnapaswa kufanya. Wakati nyinyi wote mmetimiza wajibu wenu, mtakuwa wote mmefanywa kamili, mtakuwa pia na ushuhuda wa kustaajabisha. Wale wote walio na ushuhuda ni wale ambao wamekuwa na ushindi juu ya Shetani na wanapewa ahadi ya Mungu, na wao ndio watakaobaki kuishi katika hatima ya ajabu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

640. Wanadamu, baada ya kuuwacha utoaji wa uzima kutoka kwa Mwenye uweza, hawajui azma ya kuishi, lakini hata hivyo wanaogopa kifo. Hawana usaidizi wala msaada, lakini bado wanasita kufumba macho yao, na wanajitayarisha kuendeleza uwepo wa aibu ulimwenguni humu, magunia ya miili wasio na hisia za roho zao wenyewe. Unaishi hivi, bila matumaini, kama vile wafanyavyo wengine, bila lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa watu ambao, wakiwa wanapiga kite katika mateso yao, wanatamani sana kufika Kwake. Hadi sasa, imani hii haijafikiwa kwa wale ambao hawana fahamu. Hata hivyo, watu bado wanaitaka sana. Mwenye uweza ana rehema kwa watu hawa ambao wameteseka sana. Wakati uo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na fahamu, maana imembidi Asubiri sana kupata jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako, kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo utarudisha ghafla kumbukumbu yako: ukitambua ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, lakini wakati fulani usiojulikana ukapoteza mwelekeo wako, wakati fulani usiojulikana ukaanguka barabarani ukiwa hujitambui na tena wakati fulani usiojulikana ukampata “baba.” Isitoshe, unagundua kuwa Mwenye uweza amekuwa hapo muda huo wote, akiangalia, akisubiri kurejea kwako, kwa muda mrefu sana. Amekuwa akitazama na tamanio kubwa, Akingoja itiko pasipo jibu. Kusubiri Kwake kunazidi thamani, na ni kwa ajili ya moyo na roho ya wanadamu. Pengine kusubiri huku hakuna mwisho, na pengine kumefikia mwisho. Lakini unapaswa kujua moyo wako na roho yako hasa viko wapi sasa hivi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

641. Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu wanaomilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

642. Wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu, wale wote ambao wanaweza kuokolewa wataokolewa kwa upeo wa juu zaidi, hakuna hata mmoja wao atakayeachwa, kwa kuwa kusudi la kazi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu. Wote ambao, wakati wa wokovu wa Mungu wa mwanadamu, hawawezi kufikia mabadiliko katika tabia zao, wote ambao hawawezi kumtii Mungu kabisa, wote watakuwa walengwa wa adhabu. Hatua hii ya kazi—kazi ya maneno—humwekea wazi mwanadamu njia na siri zote ambazo haelewi, ili mwanadamu aweze kuelewa mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, ili aweze kuwa katika ile hali ya kutia katika matendo maneno ya Mungu na kutimiza mabadiliko hayo katika tabia yake. Mungu huyatumia maneno tu kufanya kazi Yake, na hawaadhibu watu kwa sababu ni waasi kidogo, kwa sababu sasa ndio wakati wa kazi ya wokovu. Kama kila mtu ambaye alikuwa muasi angeadhibiwa, basi hakuna mtu ambaye angepata fursa ya kuokolewa; wote wangeadhibiwa na kuanguka kuzimuni. Kusudi la maneno ya yanayomhukumu mtu ni kumwezesha kujitambua na kumtii Mungu; sio kwao kuadhibiwa kwa njia ya hukumu ya maneno. Wakati wa kazi ya maneno, watu wengi watafunua uasi wao na kutotii kwao, na wataweka wazi kutotii kwao kwa Mungu mwenye mwili. Lakini Yeye hatawaadhibu watu hawa wote kwa sababu ya hili, badala yake Atawatupa kando wale ambao wamepotoka kabisa na ambao hawawezi kuokolewa. Atautoa mwili wao kwa Shetani, na katika hali kadhaa, kumaliza mwili wao. Wale ambao wanaachwa wataendelea kufuata na kupitia kushughulikiwa na kupogolewa. Ikiwa wanapofuata hawawezi kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na wanazidi kupotoka, basi watu hawa watapoteza nafasi zao za wokovu. Kila mtu ambaye amekubali ushindi wa maneno atakuwa na nafasi nzuri ya wokovu. Wokovu wa Mungu wa kila mmoja wa watu hawa huwaonyesha upole Wake mkubwa, kumaanisha kwamba wanaonyeshwa uvumilivu mkubwa. Mradi watu warudi kutokakatika njia mbaya, mradi kama waweze kutubu, basi Mungu atawapa fursa ya kupata wokovu wake. Watu wanapoasi dhidi ya Mungu kwanza, Mungu hana hamu ya kuwaua, lakini badala yake Anafanya yote Anayoweza kuwaokoa. Ikiwa mtu kwa kweli hana nafasi ya wokovu, basi Mungu atamtupa pembeni. Kwamba Mungu si mwepesi wa kumwadhibu mtu ni kwa sababu Anataka kuwaokoa wale wote ambao wanaweza kuokolewa. Yeye huwahukumu, huwapa nuru na kuwaongoza watu tu kwa maneno, na Hatumii fimbo kuwaua. Kutumia maneno kuwaokoa watu ni kusudi na umuhimu wa hatua ya mwisho ya kazi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

643. Katika upana mkubwa wa dunia hii, mabadiliko yasiyohesabika yamefanyika, bahari kujaa hadi kuziba mashamba, mashamba kufurika hadi baharini, tena na tena. Isipokuwa Yule ambaye anatawala kila kitu katika ulimwengu, Hakuna anayeweza kuongoza na kuelekeza jamii hii ya wanadamu. Hakuna yeyote hodari kufanya kazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya jamii hii ya binadamu, sembuse yule anayeweza kuiongoza jamii hii ya wanadamu hadi hatima ya mwanga na kuikomboa kutokana na udhalimu wa duniani. Mungu hulalamikia wakati ujao wa wanadamu, huhuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu na anaumizwa kwamba binadamu wanatembea, hatua baada ya nyingine hadi kuoza na katika njia ambayo hawawezi kurudi. Wanadamu ambao wameuvunja moyo wa Mungu na wakamkana kumfuata yule mwovu: je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaza kuhusu mwelekeo ambao wanadamu wa aina hii huenda wanafuata? Ni kwa sababu hii haswa kwamba hakuna anayehisi hasira ya Mungu, hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu au kujaribu kuja karibu na Mungu na isitoshe, hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu. Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu, binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mwenyewe, anazidi kwenda mbali na Mungu, kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli Wake, akiona heri kujiuza kwa Shetani, adui wa Mungu. Na ni nani amefikiri—iwapo mwanadamu ataendelea kuwa mkaidi—jinsi Mungu atakavyowatendea wanadamu hawa ambao wamempuuza bila kusita? Hakuna anayejua kwamba maana ya ukumbusho wa mara kwa mara na kusihi kwa Mungu ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake maafa yasiyokuwa ya kawaida ambayo ameandaa, maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili. Maafa haya siyo tu adhabu ya mwili bali pia ya roho. Unafaa kujua hili: Mpango wa Mungu utakaposhindikana na wakati makumbusho Yake na kusihi Kwake hakutapata majibu yoyote, atatoa hasira ya aina gani? Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali au hata kusikika na viumbe vyovyote. Na hivyo Nasema, majanga haya hayana mengine ya kulinganishwa nalo awali na kamwe hayatawahi kurudiwa. Hii ni kwa sababu ni mpango wa Mungu kuumba wanadamu mara hii moja tu na kuwaokoa wanadamu mara hii moja tu. Hii ndiyo mara ya kwanza na pia ni ya mwisho. Kwa hivyo, hakuna anayeweza kuelewa nia za bidii na hamu ya ari ambazo kwazo Mungu huokoa wanadamu wakati huu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Tanbihi:

a. Matini ya asili haina kauli “kuelewa kwamba.”

b. Kurudi ufuoni: nahau ya Kichina, ikiwa na maana kwamba “mtu kuacha njia zake za uovu.”

Iliyotangulia: A. Mahitaji ya Mungu kwa Mwanadamu

Inayofuata: C. Maonyo ya Mungu kwa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp