73. Wokovu wa Mungu

Na Yichen, Uchina

Mwenyezi Mungu anasema: “Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu, na inafaa kwa uhalisi. Kotekote katika enzi zote Mungu hajawahi kufanya kazi kama hii; leo, Yeye hufanya kazi ndani yenu ili muweze kufahamu hekima Yake. Ingawa mmepitia maumivu fulani ndani yenu, mioyo yenu inajisikia thabiti na kwa amani; ni baraka yenu kuweza kufurahia hatua hii ya kazi ya Mungu. Haijalishi kile mnachoweza kupata katika siku za baadaye, yote mnayoona kuhusu kazi ya Mungu ndani yenu leo ni upendo. Kama mwanadamu hapitii hukumu na kuadibu kwa Mungu, matendo yake na ari daima yatakuwa nje, na tabia yake daima itaendelea kutobadilika. Je, hii inahesabika kama kupatwa na Mungu? Leo, ingawa bado kuna mengi ndani ya mwanadamu ambayo ni yenye kiburi na yenye majivuno, tabia ya mwanadamu ni imara zaidi kuliko awali. Mungu kukushughulikia wewe ni ili kukuokoa, na ingawa unaweza kuhisi maumivu kidogo wakati huo, siku itafika ambapo kutatokea mabadiliko katika tabia yako. Wakati huo, utakumbuka ya nyuma na kuona vile kazi ya Mungu ni ya hekima, na huo utakuwa wakati ambao utaweza kufahamu kwa kweli mapenzi ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Ninaposoma kifungu hiki, siwezi kujizuia kufikiria jinsi nilivyokuwa na mazoea ya kujisifu. Nilikuwa na tamaa zisizozuilika kabisa, kila wakati nikitafuta umaarufu na hadhi, nikishindana na kujilinganisha na wengine. Niliishi bila mfano wowote wa kibinadamu. Baada ya kuhukumiwa, kuadibiwa, na kufundishwa nidhamu na maneno ya Mungu, nilianza kuelewa kidogo asili yangu ya kishetani. Niliweza kujuta na kujidharau, na nikawa mwaminifu na mnyenyekevu zaidi. Nilihisi kwa kweli kwamba hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ni wokovu kwa wanadamu.

Mnamo 2005, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kumkubali Mwenyezi Mungu, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Kwa kuwa nilikuwa nimeinuliwa na Mungu na kuaminiwa na kina ndugu, nilimwomba Mungu, nikiamua kufanya wajibu wangu vizuri ili kulipa upendo Wake. Nilizama katika kazi ya kanisa mara moja. Wengine walipoingia katika hali fulani au kupata shida, nilitafuta maneno fulani ya Mungu ya kuwasaidia, na ingawa kile nilichoshiriki kilikuwa finyu, bado nilipata matokeo kiasi. Kina ndugu walisema kwamba ushirika wangu uliwasaidia kidogo. Kwa kuwa nilikuwa na mafanikio kiasi katika wajibu wangu, baadaye kiongozi mmoja alinitaka nifanyie makanisa kadhaa kazi. Nilisisimka. Hasa nilipoona kwamba nilielewa maneno ya Mungu haraka kuliko yule dada niliyefanya naye kazi, na kiongozi huyo aliniheshimu sana, niliridhika sana. Nilidhani kwamba kiongozi aliniona kama mtu aliye na uwezo halisi, mtu mwenye talanta muhimu kanisani. Nilizidi kuwa mwenye kiburi kadiri muda ulivyozidi kusonga na nikadhani sasa nilikuwa na uhalisi kidogo wa ukweli. Niliacha kulenga kula na kunywa maneno ya Mungu au kutafakari juu yangu, na sikutafuta ukweli nilipokabiliwa na tatizo. Nilijipenda, nilijivuna, na kuwadharau ndugu zangu siku zote. Nilipoona kwamba baadhi yao walizuiwa na tabia zao potovu na hawakuweza kutekeleza wajibu wao vizuri, niliacha kushiriki kuhusu ukweli ili kuwasaidia kwa sababu ya upendo, lakini niliwakaripia bila uvumilivu: “Kazi ya Mungu imefikia hatua hii, lakini bado unafurahia mwili kwa tamaa. Je, huogopi kuwa utatumbukia katika maafa na kuadhibiwa? Usipoanza kufanya wajibu wako vizuri, utaondolewa.” Niliona kuwa walikuwa wakizuiwa na hawakutaka kuniona, lakini sikutafakari juu yangu, badala yake, nililalamika kuwa hawakuwa wakifuatilia ukweli.

Muda mfupi baadaye, kiongozi alikuja katika mkutano wetu. Nilidhani alikuja ili kunipandisha cheo. Ajabu ni kwamba, alisema kwamba kuingia kwangu katika uzima hakukuwa kwa kweli, kwamba ushirika wangu haukuweza kusuluhisha matatizo, na kwamba sikustahili kuendelea kuwajibikia kazi ya makanisa kadhaa. Niliposikia haya, nilishtuka—nilifadhaika. Sijui hata jinsi nilivyofika nyumbani baada mkutano. Nakumbuka tu nikilia njiani, nikiwaza: “Nimefanya kazi kwa bidii sana katika wajibu wangu, lakini badala ya kufanikiwa nimezama. Kina ndugu watanionaje? Inaonekana kana kwamba siwezi kuwajibikia kazi kubwa kama hiyo, lakini nawezaje kuwa tayari kukubali wajibu mdogo kama huu?” Kwa siku kadhaa sikuweza kula au kulala, lakini nililoweka katika taabu. Nilimwomba tu Mungu, nikimwomba Anitie nuru na kunielekeza ili niweze kuelewa mapenzi Yake. Nilihisi mtulivu zaidi baada ya kusali, na nikasoma maneno haya ya Mungu: “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. … Sasa nyinyi ni wafuasi, na mmepata ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujiondoa katika uhasi? Je, si jibu bila shaka ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo? … Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). Nilielewa mapenzi ya Mungu baada ya kusoma haya. Aliandaa hali hiyo ili kushughulikia tamaa yangu ya hadhi, kunifanya nitafakari juu yangu mwenyewe na nichukue njia sahihi katika kufuatilia ukweli. Niliwaza kuhusu iwapo ufuatiliaji wangu na kujitolea kwangu katika imani yangu vilikuwa kwa kweli ili kufuatilia ukweli na kufanya wajibu wa kiumbe. Ukweli ni kwamba vilikuwa tu vya kukidhi matamanio yangu ya kufanikiwa kuwaliko wengine, wala si kufuatilia ukweli kabisa! Kwa hivyo mara nilipopata cheo niliridhika na sikujaribu kuendelea. Nilipoachishwa kazi, mbali na kutotafakari juu yangu, pia nilikuwa hasi na dhaifu, na nilimlaumu Mungu. Hata nilifikiria kukubali kushindwa na kumsaliti Mungu. Sikuwa na dhamiri na mantiki, nilikuwa mbinafsi sana na mwenye kuleta hizaya. Kufukuzwa kazini kulikuwa Mungu kunilinda. Sikupaswa kuwa hasi na kumwelewa Mungu vibaya, lakini nilipaswa kutafuta ukweli ili kutatua upotovu wangu. Mara nilipogundua hilo, nilikuja mbele za Mungu katika maombi. “Ee Mungu, sitaki kufuatilia hadhi tena. Natamani kutii sheria na mipango Yako, kufuatilia ukweli kabisa, na kutimiza wajibu wangu ili kukuridhisha.” Katika siku zilizofuata, nililenga kula na kunywa maneno ya Mungu na kutafakari juu yangu, na nilipofichua tabia yangu ya kiburi tena, nlimwomba Mungu na kujikana makusudi. Nilihisi vyema zaidi baada ya kutenda kwa njia hii kwa muda, na niliweza kuingiliana vizuri na kina ndugu.

Baada ya miaka michache ya kufanya hivi, nilichaguliwa tena kuwa kiongozi wa kanisa. Muda mfupi baadaye, kanisa langu liliungana na lingine, hivyo tulihitaji kufanya uchaguzi wa viongozi tena. Tamaa yangu ya hadhi iliibuka tena kwa sababu ya hii, niliogopa sana kupoteza cheo changu. Katika mikusanyiko na viongozi wa hilo kanisa lingine, sikuona ufahamu wao kuhusu neno la Mungu na ushirika juu ya ukweli ukiwa wa ajabu, hivyo nilifikiria kuchaguliwa kuwa kiongozi kulikuwa kwa hakika kwangu. Ili kulinda cheo changu na kuwafanya watu zaidi waone jinsi nilivyokuwa hodari, nilijitolea kwenda kushughulikia baadhi ya matatizo katika kanisa lililokuwa dhaifu zaidi, nikiahidi kuyatatua haraka. Nilijishughulisha katika mikusanyiko kila siku, nikifanya ushirika na kutatua shida, na katika ushirika wangu nilizungumza kwa makusudi kuhusu jinsi nilivyofanya kazi yangu hapo zamani, ni mafanikio yapi makubwa niliyokuwa nimeyapata, na jinsi viongozi wakati huo walivyonithamini. Nilizungumza pia kwa makusudi kuhusu makosa na mikengeuko iliyokuwa katika kazi ya viongozi wa kanisa hilo lingine ili kujiinua na kuwadunisha kwa hila. Lakini Mungu huona ndani ya moyo na akili zangu, na kwa kuwa nia zangu katika wajibu wangu zilikuwa mbaya, Mungu alijificha mbali nami. Wakati huo, ingawa nilikuwa na shughuli nyingi kila wakati, sikufanikisha chochote katika kazi yangu. Nilipata vidonda kinywani mwangu, na hata kunywa maji kulikuwa chungu. Nilikuwa nikiteseka sana na nikafikiria jinsi ambavyo tangu niwe kule sikuwa nimetatua lolote na kazi yangu haikuwa na mafanikio na matokeo yoyote. Nilijiuliza viongozi wangenionaje, kama wangefikiria sikuwa hodari. Je, itakuwaje nikifutwa kazi hata kabla ya uchaguzi? Aibu iliyoje! Nilipofikiria haya nilikuwa na hamu ya kutatua shida zote mara moja, lakini bila kujali nilivyofanya ushirika, mambo yaliendelea tu kama awali. Nilihisi kuteseka sana, nilichoweza tu kufanya ilikuwa kuja mbele za Mungu na kumwita kwa kuomba: “Ee Mungu! Nimetumbukia gizani na sielewi tatizo lolote kabisa. Ee Mungu, hakika nimekuasi, kwa hivyo nakuomba Uniongoze. Niko tayari kutafakari juu yangu na kutubu Kwako.”

Baadaye nilisoma kifungu cha maneno ya Mungu. “Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia). Maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo yaliniacha nikitetemeka kwa woga! Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nikifikiri na kutenda. Ili kulinda cheo changu kama kiongozi na kuwafanya watu wengi zaidi wanistahi, nilijifanya kutatua shida kupitia ushirika ili kujionyesha na kuwavutia watu, nikijiinua na kuwadunisha wengine kila wakati. Niliwachukulia kina ndugu kama washindani, nikitumia hila na mbinu. Sikuwa na mfano wa mtu mwenye imani, sikuwa na ubinadamu. Nilikuwa na tofauti gani na mnyama anayepigania kipande cha chakula? Nilikuwa mbinafsi sana na mwenye kustahili dharau! Nilikuwa nikitenda uovu na kumpinga Mungu kwa matendo yangu na nilikuwa nimeikosea tabia Yake zamani. Kuumwa na vidonda hivyo na kutotimiza chochote katika kazi yangu kulikuwa Mungu kunirudi na kuniadhibu. Mapenzi Yake yalikuwa nitafakari kujihusu, nitubu na kubadilika. Niliwaza ni kwa nini nilikuwa nikifuatilia umaarufu na hadhi siku zote, nikiyathamini kuliko mengine yote. Ilikuwa tu kwa sababu ya kudanganyika na kupotoshwa na Shetani. Alitumia elimu na ushawishi wa kijamii kuujaza moyo wangu sumu na falsafa hizi, kama vile “Wenye ubongo hutawala wenye misuli,” na “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake.” Falsafa hizi za kishetani zilikuwa zimekita mizizi moyoni mwangu na zikawa asili yangu. Nilikuwa nikiishi kulingana na sumu hizi, nikizidi kuwa mwenye kiburi na majivuno, nikiabudu umaarufu na hadhi, kila wakati nikijaribu kufaulu na kuwa bora kuliko wengine. Kwa kuwa sikuwa katika njia sahihi, lakini nilikuwa nikiishi ndani ya tabia hii potovu na ya kishetani, nilipofushwa na sikuweza kuona chanzo cha matatizo yoyote, wala sikuweza kutatua matatizo ya watu wengine, na niliichelewesha kazi ya kanisa. Sikuwa nikifanya wajibu wangu, lakini nilikuwa nikifanya uovu. Nilisujudu mbele ya Mungu na nikatubu Kwake: “Mungu, nimetelekeza wajibu wangu kwa ajili ya sifa na faida, nikijaribu kukudanganya na kukulaghai. Napasawa kulaaniwa! Ee Mungu, sitaki kuwa hivi tena. Nataka kutubu Kwako.” Kisha nikasoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kwa kuwa nyinyi ni viumbe wa Mungu, lazima mtekeleze wajibu wa kiumbe. Hakuna mahitaji mengine kwenu. Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba: ‘Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na Wewe, na ikiwa iko chini ni kwa sababu ya mpango Wako. Kila kitu ki mikononi Mwako. Sina chaguzi zozote, wala malalamishi yoyote. … Sifikirii kuhusu hadhi; hata hivyo, mimi ni kiumbe tu. Ukiniweka kwenye shimo lisilo na mwisho, katika ziwa la moto wa jahanamu, mimi si chochote isipokuwa kiumbe. Ukinitumia, mimi ni kiumbe. Ukinikamilisha, mimi bado ni kiumbe. Usiponikamilisha, bado nitakupenda kwa sababu mimi si zaidi ya kiumbe’(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). Maneno ya Mungu yalinipa njia ya utendaji. Iwapo ningebadilishwa au kuwa na hadhi yoyote, bado ningehitaji kufuatilia ukweli na kufanya wajibu wangu vizuri, na kulenga kutenda ukweli katika wajibu wangu na kuacha tabia yangu ya kishetani. Baada ya hapo nilirekebisha nia zangu katika wajibu wangu na nikalenga kujituliza mbele za Mungu ili kusoma maneno Yake na kuomba. Niliyakabidhi matatizo ya kanisa mikononi mwa Mungu na nikamtegemea, na nikatafuta ukweli pamoja na kina ndugu. Yale matatizo yaliyokuwa kanisani yalitatuliwa kwa haraka sana. Nilijawa na shukrani kwa Mungu. Mungu ni wa kweli kabisa na Anapendeza sana, na Alikuwa pamoja nami, Akiandaa mambo ili kunitakasa na kunibadilisha. Pia niligundua jinsi ilivyo muhimu kufuatilia ukweli na mabadiliko ya tabia katika imani yangu.

Miezi sita baadaye, nilipewa jukumu la kazi ya makanisa mengine zaidi. Kwa kuwa nilijua jinsi tamaa yangu ya hadhi ilivyo kuu, na jinsi tabia yangu ivyokuwa ya kiburi, nilimwomba Mungu kwa dhati ili niweze kurekebisha nia zangu na kufanya wajibu wangu vizuri. Wakati huo, niliwekwa pamoja na Dada Wang, aliyekuwa na mtazamo mzuri kuhusu masuala na alikuwa mpevu katika kushughulikia matatizo. Niliomba ushauri wake mara kwa mara na kujifunza kutokana na uwezo wake. Baada ya miezi michache ya kufanya hivi, niliendelea sana katika kushiriki juu ya ukweli ili kutatua shida na kufanya kazi mbalimbali za kanisa. Kina ndugu walinistahi pia. Kufumba na kufumbua, nilianza tena kuridhika sana, nikifikiri kwamba, ingawa nilikuwa mgeni kiasi katika imani, ushirika wangu ulikuwa nzuri kama wa Dada Wang na uwezo wangu wa kushughulikia masuala ulikuwa umeongezeka. Nilidhani kimo changu kilikuwa kimeongezeka. Sikutambua kuwa kiburi changu kilikuwa kikidhihirika mara kwa mara na tamaa yangu ya umaarufu na hadhi ilikuwa imerudi ikiwa kuu kuliko hapo awali. Nilitaka Dada Wang anisikilize katika kila kitu. Sikuweza kuvumilia kuona wengine wakikubaliana na ushirika wake au kwamba aliongoza katika masuala ya kanisa. Nilihisi kuwa nilikuwa na utendaji kiasi na nilikuwa nimepata uzoefu mwingi, kwamba sikuwa mgeni asiyejua, na kwamba ubora wa tabia yangu ulikuwa sawa na wake. Sote tulikuwa viongozi, hivyo kwa nini yeye alikuwa akiongoza kila wakati? Kwa nini nimsikilize? Hili likiendelea, si nitakuwa kiongozi kwa jina tu? Nilianza kufanya kazi kwa bidii na kujiandaa na maneno ya Mungu ili niweze kumshinda, na wakati wa majadiliano yetu ya kazi ya kanisa katika mikutano ya wafanyakazi, alipoonyesha maoni yake, niliyachambua kwa makusudi na kupata makosa. Kisha nilishiriki “wazo langu zuri sana” ili kumdunisha na kujiinua. Muda mfupi baadaye, tulipokuwa tukijadili kazi ya kanisa, wafanyakazi wenzangu wachache walipenda maoni yangu na walianza kuja kwangu walipokuwa na matatizo na kusikiliza mapendekezo yangu. Nilipenda sana kuwaona wote wakinizingira. Baadaye, Dada Wang alishindwa kwenda kutekeleza wajibu wake kwa sababu CCP ilikuwa ikimsaka. kwa hivyo niliwajibika kazi ya kanisa kwa wakati huo pekee yangu. Sikuhisi kuzidiwa na kazi, lakini nilitulia kabisa, na nikadhani hatimaye ningeweza kuwa na kauli ya mwisho katika kila kitu. Wakati huo niligundua kuwa njia yangu ya kufikiria haikuwa sawa, lakini sikutafakari juu yangu au kuathiriwa na hilo hata kidogo.

Siku moja kiongozi aliniambia nilihitaji kuhudhuria mkutano katika eneo lingine, kwamba karibu watu 10 pekee walichaguliwa, ingawa ilijumuisha eneo kubwa. Pia nilisikia kwamba nilikuwa nipandishwe cheo. Nilihisi kweli kwamba nilikuwa muhimu sana, kwamba nilikuwa bora katika eneo letu. Nilipanda treni na dada wengine wanne tukiwa wachangamfu, lakini kitu cha ghafula kilitokea njiani. Tulifuatwa na kukamatwa na polisi wa CCP. Mahojiano yao hayakufua dafu, kwa hivyo walinihukumu miaka miwili ya kazi ngumu kwa “kuandaa na kutumia shirika la xie jiao kudhoofisha utekelezaji wa sheria.” Nilipitia wakati wa jaribio baada ya hukumu yangu. Suitafahamu na mashaka juu ya Mungu viliibuka moyoni mwangu: “Kwa nini nilikamatwa na kufungwa gerezani nilipokuwa karibu kupandishwa cheo? Si ni Mungu anayenikomesha, Akitumia hili kunifunua na kuniondoa? Je, nimepoteza nafasi yangu katika kutekeleza wajibu wangu na kuokolewa?” Nilisikitika sana, na nilikuwa nimepotea sana. Mara nyingi sana, nililia na kumwomba Mungu: “Ee Mungu, sielewi mapenzi Yako sasa. Inaonekana kwamba Unanikataa, ya kwamba Hunitaki. Mungu, nakuomba Unitie nuru na Uniongoze nielewe mapenzi Yako, ili nijue jinsi ya kuingia katika ukweli katika hali hii.” Namshukuru Mungu kwa kusikia ombi langu. Siku moja, dada aliyekuwa katika wadi hiyo ya gereza alinipa kisirisiri daftari lililokuwa na baadhi ya maneno Mungu aliyokuwa amenakili. Yalisema: “Kwa watu wote, usafishaji ni wa kutesa sana na ni mgumu sana kukubali—ilhali ni katika usafishaji ndipo Mungu huweka wazi tabia Yake ya haki kwa mwanadamu, na Huweka hadharani mahitaji Yake kwa mwanadamu, na Hutoa nuru zaidi, na upogoaji na ushughulikiaji halisi zaidi; kwa kulinganisha mambo ya hakika na ukweli, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi kujihusu na ukweli, na Humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu, hivyo kumruhusu mwanadamu kuwa na upendo wa kweli zaidi na safi zaidi wa Mungu. Haya ndiyo malengo ya Mungu katika kutekeleza usafishaji. Kazi yote Afanyayo Mungu kwa mwanadamu ina malengo yake na maana yake; Mungu hafanyi kazi isiyo na maana, wala Hafanyi kazi isiyo na manufaa kwa mwanadamu. Usafishaji haumaanishi kuondoa watu kutoka mbele ya Mungu, wala haumaanishi kuwaangamiza katika kuzimu. Unamaanisha kubadilisha tabia ya mwanadamu wakati wa usafishaji, kubadilisha motisha zake, mitazamo yake ya kale, kubadilisha upendo wake kwa Mungu, na kubadilisha maisha yake yote. Usafishaji ni jaribio la kweli la mwanadamu, na aina ya mafunzo halisi na ni wakati wa usafishaji tu ndipo upendo wake unaweza kutimiza wajibu wake wa asili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli). Moyo wangu ulichangamka mara moja. Hali hii ilikuwa jaribio la Mungu kwangu. Haikuwa mapenzi Yake kuniondoa, lakini kunifanya niweze kutafakari juu yangu na kujijua, na kuingia katika ukweli. Nilijua sikufaa kuwa hasi na dhaifu tena, na kwa kweli sikufaa kufuata mawazo yangu na kukisia mapenzi ya Mungu. Badala yake, nilifaa kujituliza na kutafuta ukweli, na kutafakari juu yangu na kujijua kwa dhati.

Usiku mmoja, sikuweza kulala, na ingawa sikutarajia, nilijiuliza ni kwa nini Mungu aliruhusu hili linipate? Kisha maneno ya Mungu yakanijia akilini: “Je, mnalichukia kwa kweli lile joka kuu jekundu? Mnalichukia kwa kweli? Mbona Nimewauliza mara nyingi? Mbona Nimewauliza swali hili, mara tena na tena?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 28). Nilijiuliza tena na tena: “Je, ninalichukia joka kubwa jekundu kweli? Je, nalichukia kabisa kweli?” Kisha nikafikiria kifungu hiki kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha: “Wengine husema: ‘Nimeliacha joka kubwa jekundu. Linanikandamiza na nalidharau sasa.' Unaweza kuliacha kwa maneno yako, lakini si kwa moyo wako. Labda unalichukia ndani ya moyo wako, lakini tabia na asili yako bado vipo chini ya udhibiti wake. Hiyo ni kwa sababu sumu, mawazo, mitazamo, falsafa, na matarajio ya joka kubwa jekundu ya maisha bado vimo moyoni mwako. Unavyoona mambo bado ndivyo linavyoona mambo. Mawazo yako na matarajio yako kuhusu maisha na mambo kwa ujumla ni sawa na mawazo na matarajio yake. Yote ni ya joka kubwa jekundu, hivyo bado upo chini ya nguvu zake. … Ikiwa kweli unataka kuepuka ushawishi wa Shetani lazima usafishe kabisa sumu zote za kishetani ndani yako. …” (Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha). Kwa kuzingatia maneno haya, niligundua nilichukia tu joka kubwa jekundu kwa kuwakamata na kuwatesa kina ndugu, na kuvuruga na kuhujumu kazi ya Mungu, lakini huko hakukuwa kulichukia na kuliacha kwa kweli. Kuchukia na kuacha kwa kweli kunaweza kutokana na kuona kikamilifu uovu wake na kiini chake cha kupinga maendeleo, ili tuweze kulichukia kwa dhati, na kukana sumu zake zilizomo ndani yetu. Kupitia mimi binafsi kukamatwa, kuadhibiwa, na kuteswa na joka kubwa jekundu, na kutiwa kasumba kwa nguvu, niliona kabisa kwamba ni pepo anayechukia ukweli na kumchukia Mungu. Niliona uso wake mbaya kama mdanganyifu na anayempotosha mwanadamu. Linapigia debe ukanaji Mungu na uyakinifu, likinuia kukana uwepo wa Mungu, na kufanya juu chini kujikuza na kujishaua kama lililo “kubwa, tukufu, na sahihi.” Linajisifu sana kama mwokozi wa watu na hutaka kila mtu aliabudu na kuliamini kana kwamba ni Mungu, likitumai kwa kiburi kuchukua nafasi ya Mungu mioyoni mwa watu. Joka kubwa jekundu linastahili dharau, ni ovu, na halina aibu. Na niligundua kiini changu kilikuwa sawa kabisa na kiini chake. Mungu aliniinua, Akinifanya nitende wajibu wa kiongozi, na nijifunze jinsi ya kusuluhisha matatizo kupitia ushirika juu ya ukweli ili wengine waweze kumjua na kumtii Mungu, lakini nilitumia fursa hiyo kujishaua sana iwezekanavyo, nikitaka tu wengine wanistahi na kufanya nilichosema. Je, si nilikuwa nikimpinga Mungu kwa kufanya hivyo? Nilimwonea wivu Dada Wang na nilimtenga, kila wakati nikishambulia makosa yake na kumdunisha. Nilikuwa hata nikitamani sana kumfanya aondolewe ili niweze kuwa na kauli ya mwisho kanisani. Je, sikuwa nikitenda kama dikteta? Je, sikuwa nikitawaliwa na sumu za joka kubwa jekundu, kama vile, “Kunaweza kuwa tu na ndume alfa mmoja” na “Mimi ni bwana wangu mwenyewe kotekote mbinguni na ardhini”? Amri za utawala za Mungu zinasema, “Mwanadamu hapaswi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu Katika Enzi ya Ufalme Wazitii). Ninapokumbuka yote niliyoonyesha, huko kunawezaje kuitwa kufanya wajibu wangu? Nilikuwa nikifanya uovu na kumpinga Mungu! Matendo yangu yalikuwa yamekiuka amri za Mungu za utawala zamani. na Mungu asingenifundisha nidhamu, Asingetumia hali hiyo kunizuia katika njia zangu mbaya, iwapo ningeendelea kulingana na asili yangu na malengo yangu, nina hakika kuwa ningefanya juu chini ili kupata umaarufu na hadhi hadi mwishowe nifanye uovu mkubwa na kuishia kuadhibiwa na Mungu. Kugundua hii kulikuwa zinduko halisi kwangu. Nilikuwa nimefikia hatua hatari sana, lakini sikutambua kabisa. Mwishowe nililazimika kutafakari juu yangu na kujijua kwa sababu ya kukamatwa kwangu. Bila pepo huyu, joka kubwa jekundu, kama foili, huenda singeona kamwe kiasi cha sumu zilizokuwa ndani yangu, kwamba mimi kwa kweli ni wa aina yake. Singeweza kabisa kuliacha kwa kweli na kutafuta kundokana na sumu yake. Niliona kwamba yote ambayo Mungu aliyafanya yalikuwa ya kunitakasa na nikamshukuru kwa dhati kwa kuniokoa.

Nilitafakari juu yangu sana gerezani na hasa nilijuta kuwa mimi sikuwa nimethamini nafasi zangu za kufanya wajibu wangu. Badala yake, nilikuwa nimesisitiza kutafuta umaarufu na hadhi na kuishi kulingana na sumu ya shetani. Nilifanya mambo mengi yaliyopingana na ukweli, yaliyowaumiza kina ndugu, na nilizuia na kuvuruga kazi ya kanisa. Nilikuwa nimemuumiza Mungu sana, nilikuwa na deni kubwa na nilijawa na majuto. Ni wakati huo tu ndipo nilipata hamu kubwa ya kufuatilia ukweli na kupitia hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake ili niweze kuondokana na hizo sumu na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu karibuni. Nilianza tena wajibu wangu baada ya kutoka, na nilipochaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa tena, sikuridhika mno wala kujivuna kama awali. Badala yake, nilihisi kuwa lilikuwa jukumu kubwa, kwamba lilikuwa agizo la Mungu kwangu nililopaswa kuthamini, na kwamba ninapaswa kutia bidii kufuatilia ukweli na kutekeleza wajibu wangu. Kurudiwa na kufundishwa nidhamu kila mara hatimaye kulizindua roho yangu iliyokuwa imehadaiwa na Shetani. Nilitambua kuwa kufuatilia tu ukweli, kutafuta mabadiliko katika tabia yangu, na kufanya wajibu wangu wa kiumbe vizuri ndio ufuatiliaji mzuri! Tamaa yangu ya umaarufu na hadhi si kuu kama ilivyokuwa zamani na ninazidi kuacha kuwa na majivuno. Naweza kufanya kazi vizuri na wengine na kutekeleza wajibu wangu vizuri, na sasa ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kibinadamu. Nahisi kabisa kwamba mabadiliko kidogo hayajatokea kwa urahisi. Haya yote yametimizwa na hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu. Nashukuru kwa wokovu wa Mwenyezi Mungu kwangu!

Iliyotangulia: 69. Kurudi kwenye Njia Sahihi

Inayofuata: 75. Hili Jaribu Langu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

57. Kuripoti Au Kutoripoti

Na Yang Yi, UchinaMwenyezi Mungu anasema, “Kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp