203 Neno la Mungu ni Nuru

1

Umeme kutoka Mashariki uliniamsha kutoka usingizini mwangu,

na kupitia katika ukungu wangu niliona neno la Mungu likionekana katika mwili.

Maneno ya hukumu na kuadibu vilinishinda na kuniokoa.

Kushindwa, majaribio na dhiki yalinirarua vipande vipande.

Upotovu wangu ulifichuliwa na mimi, niliyekuwa na majivuno, nikashusha kichwa changu.

Nilijua tu kutostahili kwangu kwa kuuona uchafu wangu uliokithiri.

Nikifikiria hadhi yangu na madeni ya zamani,

ningewezaje, mtu katili, mwovu na mpotovu, kustahili kumtumikia Mungu?

Vipingamizi vingi sana na kushindwa kwingi sana huniweka katika njia sahihi ya kumwamini Mungu.

Msururu wa mapigo, usafishaji na taabu vimekuwa mnyororo wa ukombozi wangu,

vikinifunga mimi mzima kwa karibu sana na upendo wa Mungu.

Kujua tabia ya haki ya Mungu ni baraka kuu sana.

2

Mungu katika mwili ni Mwokozi aliyerudi, Aliyerudi tena.

Kupitia hukumu, dhiki na majaribio, nimekutana uso kwa uso na Mungu.

Nimeonja wokovu na kumjua Mungu wa vitendo.

Mateso makali ya giza yameniruhusu kuelewa zaidi kile cha kuchukia na kile cha kupenda.

Nikipata nuru na mwanga wa maneno ya Mungu, naelewa siri za maisha.

Mwili mpotovu wa wanadamu ni Shetani mwenye mwili.

Kwamba naweza kumpenda na kumshuhudia Mungu ni uinuaji Wake wa pekee.

Kulipa upendo Wake ni tamanio la moyo wangu la pekee.

Hukumu na kuadibu kwa Mungu vina maana sana na vinafichua upendo wa Mungu.

Kumtii na kumpenda Mungu kwa moyo wa uchaji ni wajibu wangu.

Wajibu wangu wa lazima ni kumshuhudia na kuwa mwaminifu kwa Mungu.

Nitajitolea mzima kutekeleza mapenzi Yake kwa ajili ya utukufu Wake.

Maneno ya Mungu hunitakasa na kuniokoa, yakiniruhusu niishi kwa kudhihirisha maisha halisi.

Nimemjua Mungu, nikawa shahidi Wake. Nitampenda na kumtumikia Mungu milele.

Iliyotangulia: 202 Toba ya Dhati

Inayofuata: 204 Natamani Kusimama Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki