38. Wokovu wa Aina Tofauti

Na Huang Lin, China

Nilikuwa mwumini wa kawaida katika Ukristo wa Kipaji, na tangu nianze kuamini katika Bwana sikuwahi kukosa ibada. Ilikuwa hasa ni kwa sababu nilijua tulikuwa katika siku za mwisho na unabii katika Biblia kuhusu kurudi kwa Bwana ulikuwa kimsingi umetimia; Bwana angerudi hivi karibuni, na kwa hivyo nilihudhuria ibada hata kwa shauku zaidi, nikitazamia kwa hamu kurudi Kwake, nisije nikakosa nafasi yangu ya kukutana na Bwana.

Siku moja, dadangu mdogo alikuja na kuniambia kwa furaha, “Hujambo, nimekuja leo kukuambia habari njema kabisa—Bwana Yesu amerudi! Na zaidiya hayo, Amerudi katika mwili; Anaonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya siku za mwisho kumhukumu na kumtakasa mwanadamu, hivyo kutimiza unabii katika Biblia ‘Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Usipoteze muda wowote—ifuate kazi mpya ya Mungu!” Niliposikia habari kwamba Bwana alikuwa Amerudi, nilishtuka na kujawa na shaka. Nikasema, “Inasema katika Kitabu cha Ufunuo, ‘Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye(Ufunuo 1:7). Na wachungaji na wazee mara nyingi hutuambia kwamba Bwana atakaporudi, Atatujia juu ya wingu jeupe. Unasema kuwa Bwana amerudi na kwamba Amekuja katika mwili. Hilo linawezekanaje?” Dada yangu alisema kwa dhati, “Unasema kwamba Bwana Yesu atarudi na mawingu, lakini una uhakika kuhusu hili? Pia inatabiriwa katika Biblia: ‘Tazama, mimi nakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15), and ‘Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). Unathubutu kusema kwamba Bwana hangeweza kuja kwa siri? Kuna siri katika kurudi kwa Bwana, kwa hivyo lazima tutafute kwa uwazi wa fikira! Tukishikilia mawazo na fikira zetu wenyewe, tunawezaje basi kukaribisha kurudi kwa Bwana?” Lakini haijalishi jinsi alivyotoa ushirika, bado sikushawishika, nikiamini badala yake kwamba Bwana angerudi juu ya wingu jeupe na kwamba Hangeweza kuja katika mwili. Baadaye aliihubiria familia nzima injili, na baada ya kushiriki ushirika wake mara kadhaa, mume wangu, mwanangu mdogo na mkewe (ambao walikuwa wasioamini) wote walikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Lakini mimi niliendelea kushikilia maoni yangu mwenyewe, nikikataa kuikubali.

Baada ya hayo, niliendelea kuhudhuria ibada katika kanisa langu la zamani, huku mume wangu, mwanangu mdogo na mkewe wote walihudhuria mikutano katika Kanisa la Mungu Mwenyezi. Kila wakati nilipokuja nyumbani kutoka katika ibada, nilihisi mnyong’onyevu na nilihisi kwamba yote yalifanywa kwa ghibu; moyo wangu ulikuwa mtupu na sikuwa napata chochote. Wao, kwa upande wao, walikuwa wenye furaha sana kila wakati waliporudi kutoka kwenye mkutano na mara nyingi wangekuwa na ushirika na kutafuta pamoja kuhusu mambo kama vile ni tabia gani potovu walizofichua walipokumbana na masuala, jinsi wanavyopaswa kutafuta mapenzi ya Mungu, na jinsi wanavyopaswa kujijua na kujitafakari. Pia wangejadili jinsi ya kutenda ukweli na kuishi kwa kufuata maneno ya Mungu, jinsi ya kuondoa tabia zao potovu na kutakaswa, na kadhalika. Kuwasikia wakijadili mambo haya kulinishangaza, na niliwaza: “Wamekuwa na imani kwa muda mfupi sana; ni kwa nini wanajua kwamba wanahitaji kutafuta mapenzi ya Mungu wakati wanakumbana na masuala, kwamba wanaweza kupata njia ya kutenda, na kila kitu wanachosema kimefikiriwa vizuri sana? Nimemwamini Bwana Yesu kwa miaka hii yote; nimeomba, nimehudhuria ibada na kusoma Biblia bila kukoma, hivyo kwa nini huwa siwezi kamwe kuelewa mapenzi ya Bwana mambo yanaponipata? Na sio mimi tu—ndugu zangu wote katika kanisa langu ni vile vile. Tumefungwa na kila aina ya dhambi na hatuwezi kujikomboa; roho zetu zimenyauka, ni zenye giza na zisizo na tumaini, na tunahisi kama kwamba tunazidi kuwa mbali na Bwana. Ni nini hasa kinachoendelea?” Mada walizokuwa wakijadili zilikuwa safi na mpya, wakiongea kuhusu ni tabia zipi potovu walizokuwa wakifichua, kuhusu jinsi ya kutafakari na kujijua, kuhusu kutakaswa, na kadhalika. Nilikuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi sana lakini sikuwahi kuwasikia wachungaji au wazee kanisani mwangu wakihubiri kuhusu mambo hayo, na sikuweza kuelewa jinsi waliweza kuelewa mengi sana! Sikuelewa.

Kufumba na kufumbua, wakati wa mavuno ulikuwa umefika; wanangu wawili walivuna nafaka yao na kuileta nyumbani. Katika miaka iliyopita, nilikuwa nikimsaidia mwanangu mkubwa kumenya nafaka yake kwanza na kisha kumsaidia mwanangu mdogo, lakini mwaka huu mwanangu mdogo na familia yake waliifanya kazi hiyo wenyewe. Nilijiwazia: “Sijaisaidia familia ya mwanangu mdogo na kazi yao wakati huu, kwa hivyo mkewe lazima awe amenikasirikia. Atasema kuwa ninaonyesha upendeleo.” Lakini kilichonishangaza, sio tu kwamba hakuwa amekasirika, lakini aliniambia kwa moyo mkunjufu, “Mama, wewe na baba mnazidi kuwa wazee. Msijisumbue tena kuhusu kutusaidia na kazi yetu. Itunzeni tu afya yenu!” Nilishangaa sana kumsikia akisema hivi. Kwa kweli ilikuwa ni mara ya kwanza yeye kuwahi kusema kitu cha kudhukuru kutuhusu. Hakuwa amewahi kusema kitu kama hiki hapo awali! Na baadaye kikatokea tena—nikawaambia wanangu na wake zao, “Watoto wenu wataanza shule ya kati hivi karibuni, kwa hivyo nitamnunulia kila mmoja wao baiskeli.” Kwa hivyo nilimnunulia mtoto wa mwanangu mkubwa baiskeli, lakini kisha kitu kilitokea na ikanibidi nitumie pesa zote nilizobaki nazo; singeweza tena kuweza kumnunulia baiskeli mtoto wa mwanangu mdogo. Mamake mke wa mwanangu aliishia kumnunulia baiskeli. Nilihisi vibaya na kuwaza: “Mke wa mwanangu lazima awe amekasirikia na atasema kuwa sitimizi ahadi zangu.” Lakini kwa mshangao wangu, sio tu kwamba hakukasirika bali yeye alinifariji kwa kusema, “Mama, hakuna haja ya kujuta kutomnunulia mtoto wangu baiskeli. Wewe na baba wekeni pesa zenu kuanzia sasa na mzitumie wenyewe. Msijali kutuhusu!” Nilishangazwa sana na matukio haya mawili. Tangu binti mkwe wangu alipoanza kuamini katika Mwenyezi Mungu, hakubishana nami tena kuhusu mambo, lakini badala yake alionyesha kujali na kudhukuru—kweli alikuwa amebadilika. Na mume wangu alikuwa akinikasirikia kwa sababu ya jambo lolote dogo—kitu kidogo kingeibua hasira yake. Lakini sasa alikuwa na tabasamu kila alipozungumza nami, na hata wakati mwingine nilipokuwa nimemkasirikia, aliivumilia kwa upole na angeniambia kwa utulivu, “Tunamwamini Mungu yule yule. Uhusiano wetu wa mwili ni ule wa mume na mke, lakini tukiichukulia kiroho sisi ni ndugu na dada. Tunapaswa kupendana, kuelewana na kusameheana, na kuishi kwa kufuata neno la Mungu. Huoni hivyo? Nilikuwa mwenye hasira mbaya na ningekasirika kwa urahisi, na haya ndiyo yalikuwa matokeo ya tabia yangu potovu ya kishetani. Nilikuwa mwenye kiburi sana na mwenye kujivuna na nilikosa ubinadamu sahihi. Sasa, nimesoma maneno mengi ya Mungu Mwenyezi, na nimeelewa kuwa kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuwaokoa wanadamu kwa kuonyesha maneno Yake. Katika kutafuta kupata wokovu wa Mungu, watu wanahitaji kuweka maneno ya Mungu katika vitendo katika maisha halisi, na kushughulikia kila jambo kulingana na kanuni za ukweli. Lazima niuache mwili wangu, nitende kulingana na maneno ya Mungu, na niishi kwa kudhihirisha ubinadamu sahihi.” Nikiwaangalia mume wangu, mwanangu na mkewe, niliendelea kutafakari moyoni mwangu: “Walikubali tu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho miaka miwili tu iliyopita, kwa hivyo wamebadilikaje kiasi kikubwa hivi? Sina budi ila kusadikishwa na hii. Nimemwamini Bwana kwa miaka mingi sasa, na ninasoma Biblia na kusali kila siku, hivyo kwa nini sijabadilika hata kidogo wakati wote huu? Wakati kitu kinanitendekea, kwa nini mimi daima huzama katika dhambi ambayo siwezi kujiondoa katika? Ni Mungu tu aliye na nguvu ya kuwabadilisha watu. Inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu wanayemwamini ni Bwana Yesu alirudi? Ikiwa kweli hili ni kweli na ninaendelea kukataa kukubali, je, Bwana hataniacha? Je, si nitakuwa mtu mjinga kuwa na wokovu mkubwa kama huo mbele yangu lakini nishindwe kuupata?” Nikifikiria hili, sikuweza kujizuia ila kuhisi wasiwasi. Nilitaka kufuta na kuichunguza, lakini nilikuwa na aibu kuzungumza na familia yangu kuhusu hilo.

Siku moja mume wangu alipokuwa nje, kwa siri nilichukua kitabu alichokuwa akisoma kila wakati. Punde nilipoangalia kifuniko chake, maneno sita makubwa “Neno Laonekana Katika Mwili” yaliyoandikwa kwa dhahabu ya kung’aa yalinirukia, na nikawaza: “Kitabu hiki kina siri gani hasa? Kinaweza kuwabadilisha watu sana—lazima nikisome kwa uangalifu.” Kwa upole, nilifungua kitabu hicho na kuona maneno haya yameandikwa hapo: “Kupata mwili huku ni kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kufuatia kukamilika kwa kazi ya Yesu. Bila shaka, kupata mwili huku hakufanyiki kivyake, bali ni hatua ya tatu ya kazi baada ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kila hatua mpya ya kazi ya Mungu kila mara huleta mwanzo mpya na enzi mpya. Vivyo hivyo kuna mabadiliko yanayokubaliana katika tabia ya Mungu, katika njia Yake ya kufanya kazi, katika sehemu Yake ya kufanya kazi, na katika jina Lake. Ndiyo maana basi ni vigumu kwa mwanadamu kukubali kazi ya Mungu katika enzi mpya. Lakini licha ya jinsi anapingwa na mwanadamu, Mungu huendelea kufanya kazi Yake, na daima Yeye huwa Akiongoza wanadamu wote kuendelea mbele. Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Baada ya kusoma haya, nilitafakari: Ikiwa kupata mwili kwa pili kwa Mungu kulitamatisha kazi ya Enzi ya Neema, je, inaweza kuwa kwamba Mungu hafanyi kazi tena katika makanisa kutoka katika Enzi ya Neema? Je, sasa tumeingia katika Enzi ya Ufalme? Inasema hapa: “Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu.” Tangu mume wangu, mtoto wangu na mkewe waikubali kazi ya Mwenyezi Mungu, wamebadilika sana. Inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu wanayemwamini kweli ni Bwana Yesu aliyerudi? Je, wanafuata nyayo za Mungu kweli na kukubali mwongozo binafsi wa Mungu? Vinginevyo, wangeelewaje ukweli mwingi sana vile na wangewezaje kubadilika sana? Haya lazima yawe matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu—hiki si kitu ambacho wangeweza kupata wao wenyewe, bila kazi ya Roho Mtakatifu. Wazo hilo liliponitokea tu ghafla niliona kuwa mume wangu alikuwa anakuja nyumbani. Kwa haraka nilikirudisha kitabu kile pale kilipokuwa, na nikawaza: Lazima asijue kuwa nimekuwa nikisoma kitabu chake, la sivyo atanicheka.

Siku iliyofuata mume wangu alipoondoka kwenda kuhudhuria mkutano, nilichukua tena kitabu hicho na kuanza kusoma. Nilisoma kifungu hiki: “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Nilitafakari sana kuhusu kifungu hiki. Bwana Yesu aliwakomboa wanadamu wote kwa kusulubiwa, lakini Hakuondoa tabia potovu za wanadamu. Asili ya dhambi bado ipo ndani ya mwanadamu—hii ni kweli kabisa. Na kuhusu sisi ambao tunamwamini Bwana, mara nyingi sisi hushindwa kufuata mafundisho ya Bwana; na tunasema uwongo na kudanganya, na kila siku tunatenda dhambi na kisha kukiri, tukiwa katika dhambi bila kukoma na kutokuwa na uwezo wa kujikomboa kutoka katika minyororo ya dhambi. Huu ni ukweli usiopingika. Wakati huohuo maneno haya ya Mungu kwenye Biblia yalinijia mawazoni: “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45). Mungu anatutaka tufikie utakatifu, na bado mara nyingi sisi hutenda dhambi na kumchukiza Bwana—huko ni kuwaje watakatifu? Mungu ni mtakatifu, na ufalme Wake hauwezi kuchafuliwa. Kwa hivyo tunawezaje kuingia katika ufalme wa mbinguni sisi tunaotenda dhambi mara nyingi? Wazo hili liliniacha nikiwa nimechanganyikiwa kidogo, na nikasoma kifungu hiki tena: “Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani.” Inawezekana kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ni kazi kubwa hata zaidi iliyofanywa na Bwana Yesu aliyerudi? Je, ni kwa kukubali na kupitia hukumu ya Mwenyezi Mungu ndipo tunaweza kujiondolea dhambi, na kutakaswa na kubadilishwa? Je, inawezekana kwamba mabadiliko yaliyofanywa katika mume wangu na mke wa mwana wangu yametokana na kupitia kwao kwa kazi ya Mwenyezi Mungu ya kuadibu na hukumu? Mume wangu, mwanangu na mkewe walikuwa wameamini katika Mungu kwa muda mfupi sana lakini walikuwa wameelewa ukweli fulani, na pia wangeweza kueleza ufahamu wao kuhusu tabia zao potovu, kutafuta mapenzi ya Mungu wakati mambo yamewapata, na wangeweza kupata njia ya kutenda. Ilhali mimi, kwa upande mwingine, nilikuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi, na bado mtu angeniuliza imani katika Mungu ni nini hasa au mapenzi ya Mungu ni nini hasa, kusema kweli, singeweza kutamka lolote, sembuse kuweza kuzungumza kuhusu mabadiliko yoyote katika tabia yangu. Kujifikiria nikijilinganisha nao, nilihisi aibu kweli! Ilinionekania kwamba ilibidi niichunguze kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa bidii.

Kuanzia wakati huo, kila siku kwa sirir nilisoma kitabu Neno Laonekana katika Mwili bila mume wangu kujua, na kadiri nilivyosoma, ndivyo nilivyopata nuru moyoni mwangu na ndivyo nilivyosoma zaidi. Wakati mwingine sikutaka hata kuhudhuria ibada kanisani kwangu, lakini nilikaa nyumbani nikisoma kitabu hiki tu. Wakati mmoja, nilisoma maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Kwa hakika Mimi nitawaangazia na kuwapa nuru wale wote wenye njaa na kiu ya haki na ambao hutafuta kwa uaminifu. Mimi nitawaonyesha ninyi nyote siri za ulimwengu wa kiroho na kuonyesha njia ya kwenda mbele, Niwafanye mtupilie mbali tabia zenu mbovu za zamani haraka iwezekanavyo na mfikie ukomavu wa maisha ili kwamba muweze kuwa na manufaa Kwangu, na kwamba kazi ya injili hivi karibuni itaendelea bila kizuizi. Ni hapo tu mapenzi Yangu yatakaporidhishwa, ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita utatimizwa haraka iwezekanavyo. Mungu ataupata ufalme na atakuja chini duniani, na kwa pamoja tutaingia katika utukufu!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 8). Sikuwa na budi ila kufikiria maneno haya kutoka kwa Bwana Yesu: “Wamebarikiwa wale walio na njaa na kiu ya haki: kwa kuwa watapewa shibe(Mathayo 5:6). Kadiri nilivyosoma zaidi, ndivyo nilivyohisi kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Bwana Yesu yalikuwa na chanzo kimoja. Maneno kutoka kwa wote wawili yana mamlaka na nguvu, na kwa hivyo ilionekana sana kwangu kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa Bwana Yesu aliyerejeai! Nikiwa na mawazo haya, nilishangaa: Nilijua kwamba hii ingekuwa kweli, ningepaswa kuharakisha kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho, kwa maana kama ningeendelea kukataa kuikubali, ningeachwa nyuma kweli na kazi ya Mungu! Lakini ningewezaje kuiambia familia yangu? Walikuwa wameshiriki injili nami mara nyingi zamani, lakini siku zote nilikataa kuikubali. Ningesema sasa kwamba nilikuwa tayari kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, wangefikiria nini juu yangu? Wakati tu nilikuwa nikiyumbayumba katika hali ya kukosa uamuzi, Mungu alinifungulia njia.

Siku moja, mke wa mwanangu na dada mwingine walikuja kushiriki injili nami. Nilijua wakati huo kwamba hiyo ilikuwa nafasi niliyopewa na Mungu, kwa hivyo nikawaambia kwa uaminifu: “Kweli, nimekuwa nikisoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu kwa siri na nahisi kuwa maneno haya yanatoka kwa Mungu. Haiwezekani kwa mwanadamu yeyote kunena maneno ambayo yana mamlaka na nguvu kama hii.” Mke wa mwanangu alishangaa kunisikia nikisema hivi, na akamwangalia yule dada mwingine na kucheka kwa furaha. Niliendelea: “Lakini kuna kitu ambacho bado sielewi vizuri. Bwana Yesu alitabiri ‘Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu akiwa na nguvu na utukufu mwingi(Luka 21:27). Sisi waumini sote tunatamani sana kurudi kwa Bwana Yesu, Ashuke kati yetu juu ya wingu jeupe. Lakini mnasema kwamba Bwana amesharudi, kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi. Basi kwa nini hatujamwona Bwana akija juu ya wingu jeupe? Tafadhali fanya ushirika nami kuhusu hili.”

Dada huyo alijibu kwa dhati, “Shukrani ziwe kwa Mungu! Kama sote tunavyojua, kuna vifungu vingi kwenye Biblia vinavyotabiri kurudi kwa Bwana. Lakini tukitazama kwa uangalifu, tutaona kwamba kurudi kwa Bwana kunatabiriwa kwa njia mbili tofauti. Moja ni kwamba Bwana atakuja wazi juu ya wingu na kila mtu Atamwona, kama ilivyo katika Luka 21:27 ambayo inasema ‘Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu akiwa na nguvu na utukufu mwingi.’ Ya pili ni kwamba Bwana atakuja kwa siri, kama mwizi, na hakuna mtu atakayejua, kama ilivyo katika Mathayo 24:36: ‘Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni, isipokuwa Baba yangu tu.’ Tunaweza kuona kwamba ujio wa Bwana utatokea katika hatua mbili: Kwanza, Atakuja kwa siri, na baada ya Yeye kutekeleza hatua moja ya kazi Yake, ndipo kuja Kwake kutajulishwa. Unachoongelea ni unabii wa Bwana kuja wazi wazi, ilhali kwa sasa tuko katika hatua ambapo unabii wa kuja Kwake kwa siri unatimizwa. Hii ni hatua ambapo Mungu anapata mwili kutekeleza kazi Yake na kuwaokoa wanadamu. Punde Mungu atakapomaliza kufanya kazi katika mwili, basi Atakuja wazi wazi ili wote wamwone….”

Kusikia ushirika huu kuliupa moyo wangu nuru, na nikawaza: “Kama ilivyo, inatabiriwa katika Biblia kwamba Bwana atakuja kwa njia mbili tofauti. Kwanza, Atakuja kwa siri, na baadaye Atakuja kwa uwazi—kweli hii ni siri! Nimekuwa nikisoma Biblia miaka yote hii, ni vipi kwamba sijapata kugundua hili? Lakini sasa kwa kuwa nafikiria kulihusu, nina hakika kuwa hivi ndivyo ilivyo!”

Mke wa mwanangu aliniambia, “Mama, wakati ambao Mwenyezi Mungu anafanya kazi Yake katika mwili kumhukumu na kumtakasa mwanadamu kwa maneno ni hatua ambayo Mungu anakuja kwa siri, na ni wakati ambapo Mungu anawafunua watu na kututenganisha kulingana na aina yetu. Acha tusome maneno ya Mwenyezi Mungu ili nielewe vyema kipengele hiki cha ukweli.” Kisha akasoma: “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba ‘Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo’ watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia).

Dada huyo aliendeleza ushirika wake. “Kutoka katika maneno ya Mungu, tunaweza kuona kwamba wakati Mwenyezi Mungu anafanya kazi Yake kwa siri, Yeye anafanya tu kazi ya kuhukumu na kuwaadibu watu kwa maneno. Hiyo ni kusema, Anaonyesha ukweli wote kutupa kile tunachohitaji maishani, na wote wanaokubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, wanaopitia kuadibu na hukumu ya maneno ya Mungu, wanaokuja kuelewa ukweli na kumjua Mungu, na ambao tabia za maisha yao zimebadilika, ni washindi ambao wanafanyizwa na Mungu kabla ya majanga. Mara tu washindi hawa wanapofanyizwa, kazi kubwa ya Mungu itakamilishwa kwa mafanikio, na kazi Anayofanya kwa siri pia itakamilika. Ni baada ya hapo ndipo Mungu atakuja na mawingu na kuonekana wazi kwa mataifa na watu wote. Watu wengine hushikilia fikira zao wenyewe, wakingoja tu Bwana Yesu aje na mawingu, lakini wanakataa kukubali ukweli wowote unaoonyeshwa na Mungu wakati Anafanya kazi Yake kwa siri. Hawa wote ni watu wanaomwasi Mungu na kumdharau, na ikiwa hawawezi kumrudia Mungu na kukubali wokovu Wake wa siku za mwisho, basi watakuwa wakilia na kusaga meno yao katikati ya majanga makubwa. Imetabiriwa katika Ufunuo 1:7, ‘Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye. Hata hivyo, Amina.’ Fikiria kulihusu: Bwana atakapokuja na mawingu, kila mtu atamwona, na ni nini wanachoweza kufanya isipokuwa kukaribisha kuja Kwake kwa furaha kuu? Hivyo basi kwa nini watu wote wataomboleza? Ni kwa sababu, Mungu atakapokuja wazi, wataona kwamba Mwenyezi Mungu ambaye wamemdharau hakika ni Bwana Yesu aliyerudi, kwa hivyo wangekosaje kupiga vifua vyao, kuomboleza na kusaga meno yao?”

Niliendelea kutikisa kichwa changu huku nikisikiliza ushirika wa dada huyo, na nikasema, “Ah, sikuwahi kuelewa mstari huu hapo awali. Nilimuuliza mchungaji kanisani kwangu, lakini hakuueleza wazi. Inatokea kuwa mstari huu unawataja wale wote ambao wanakataa kukubali wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, kwa wale wote wanaomdharau Yeye.” Wakati huo, sikuweza kujizuia kufikiria jinsi muda baada ya muda familia yangu ilikuwa imeshiriki injili nami, lakini bado nilikuwa nimepinga na kukataa kuikubali—nilihisi kuvurugika sana. Kwa majuto, nilimwambia yule dada, “Kama singekuwa nimesoma maneno ya Mwenyezi Mungu, kama maneno ya Mwenyezi Mungu hayangeufungua mlango wa moyo wangu na kuniruhusu niwe na moyo wa kutafuta, nahofu bado singekuwa nasikiliza ushirika wenu, lakini bado ningekuwa nashikilia sana kungojea Bwana Yesu aje juu ya wingu jeupe na kujitokeza wazi kwa watu. Kwa kweli mimi ni mjinga na mpumbavu! Ni sasa tu ndipo ninaelewa kuwa hatua ya kazi ya siri ya Mungu kweli ni fursa nzuri kwa sisi kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kutupilia mbali tabia zetu potovu ili tuweze kupata wokovu kamili! Mungu anapokuja juu ya wingu na kuonekana wazi kwa mwanadamu, kazi Yake ya wokovu tayari itakuwa imekwisha, na Ataanza kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Na hilo linapofanyika, hata ikiwa nimejawa kabisa na majuto, nitakuwa nimechelewa sana. Nampa Mungu shukrani kwa kutoniacha na kunipa nafasi hii ya wokovu. Natamani kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho!”

Baadaye nilichukua hatua na kuuliza kujiunga na Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kama mume wangu, mwanangu na mke wa mwanangu, nilisoma maneno ya Mungu na kufanya ushirika kuhusu ukweli kila siku, na ninapitia hukumu, kuadibu, utakaso na wokovu wa maneno ya Mungu. Katika familia kubwa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, ninaishi maisha ya kweli ya kanisa, na roho yangu imejaa amani na furaha. Ninahisi kweli jinsi upendo wa Mungu kwangu ulivyo mkuu; ni kwamba nilikuwa baridi sana na nilimfanya Mungu asubiri muda mrefu sana. Namshukuru Mungu kwa kupanga kwa uangalifu watu, matukio na vitu vya kila aina ili kuniongoza na kunielekeza hatua kwa hatua kurudi katika familia ya Mungu—namshukuru Mungu kwa kuniletea wokovu wa aina tofauti!

Iliyotangulia: 37. Mungu Yuko Kando Yangu

Inayofuata: 39. Nimekaribisha Kurudi Kwa Bwana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

13. Sauti Hii Yatoka Wapi?

Na Shiyin, ChinaNilizaliwa katika familia ya Kikristo, na jamaa wangu wengi ni wahubiri. Nilimwamini Bwana pamoja na wazazi wangu tangu...

37. Mungu Yuko Kando Yangu

Na Guozi, MarekaniNilizaliwa katika familia ya Kikristo, na nilipokuwa na umri wa mwaka mmoja, mama yangu alikubali kazi mpya ya Bwana Yesu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp