Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu
Kufahamu kusudi la kazi ya Mungu, matokeo ambayo kazi Yake inakusudiwa kuwa nayo kwa watu, na nia Zake kwa watu ni zipi hasa, ndicho kile ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kufikia. Ufahamu wa kazi ya Mungu ndio hasa ambao watu wote wanakosa siku hizi. Kile ambacho Mungu amefanya kwa watu, kazi yote ya Mungu, na nia za Mungu zimekuwa zipi hasa, tangu kuumbwa kwa dunia mpaka wakati wa sasa—watu hawafahamu na hawaelewi mambo haya. Huu ni upungufu unaopatikana sio tu katika ulimwengu wote wa kidini, lakini hata zaidi ndani ya wale wote wanaomwamini Mungu. Siku itakapofika ambapo utamwona Mungu kwa kweli, ambapo utathamini hekima Yake, ambapo utaona matendo yote ambayo Mungu amefanya, na ambapo utajua kile Mungu alicho na anacho—utakapoona utele, hekima, maajabu Yake, na kazi yote ambayo Amefanya juu ya watu—ni hapo tu ndipo utakuwa umemwamini Mungu kwa mafanikio ya kweli. Mungu anaposemwa kuwa Mwenye kujumuisha yote na tajiri katika utele, Yeye anajumuisha yote kwa njia gani hasa, na Yeye ni tajiri katika utele kwa njia gani hasa? Ikiwa huelewi hili, basi huwezi kuhesabiwa kuwa unamwamini Mungu. Kwa nini Ninasema kwamba wale walio katika ulimwengu wa kidini si waumini katika Mungu bali ni watenda maovu wa aina moja na ibilisi? Ninaposema wao ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi nia za Mungu na hawawezi kuona hekima Yake. Mungu kamwe hawafunulii kazi Yake. Wote ni vipofu, na hawawezi kuona matendo ya Mungu. Wametelekezwa na Mungu, na hawana kabisa utunzaji na ulinzi Wake, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale ambao hawana kazi ya Mungu wote ni watenda maovu na ni watu wanaompinga Mungu. Watu hawa wanaompinga Mungu ambao Ninawazungumzia wanarejelea wale wasiomjua Mungu, wale wanaomkiri Mungu kwa maneno huku wakiwa hawana ufahamu wowote kumhusu, wale wanaomfuata Mungu lakini hawamtii Yeye, na wale wanaofurahia neema Yake lakini hawawezi kusimama imara katika ushuhuda wao Kwake. Ikiwa mtu haelewi kusudi la kazi ya Mungu na haelewi kazi ambayo Mungu anafanya juu ya watu, mtu huyo hawezi kulingana na nia za Mungu, na hawezi kusimama imara katika ushuhuda wake kwa Mungu. Sababu ya watu kumpinga Mungu inatokana, kwa upande mmoja, na tabia zao potovu; kwa upande mwingine, ni kwa sababu hawamjui Mungu na hawaelewi kanuni ambazo kwazo Anafanya kazi au nia Zake kwa watu ni zipi. Vipengele hivi viwili, vikichukuliwa pamoja, vinaunda historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wale ambao wameanza kumwamini Mungu hivi punde wanampinga Yeye kwa sababu wanadamu wana asili inayompinga Mungu; kwa wale ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mingi, wanampinga Mungu kwa sababu hawamjui Yeye, na zaidi ya hayo wana tabia potovu. Katika wakati kabla ya Mungu kuwa mwili, kipimo cha iwapo mtu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo alishika amri zilizowekwa na Mungu aliye mbinguni. Katika Enzi ya Sheria, kwa mfano, yeyote ambaye hakushika sheria za Yehova alikuwa anampinga Mungu; yeyote aliyeiba sadaka za Yehova, au kuwapinga wale ambao Yehova aliwatazama kwa upendeleo, alikuwa anampinga Mungu na angepigwa mawe hadi kufa; yeyote ambaye hakuwaheshimu wazazi wake, au kuwapiga na kuwatukana watu wengine, alikuwa anakaidi sheria, na wote ambao hawakushika sheria za Yehova walikuwa wale waliompinga Yeye. Mambo yalikuwa tofauti katika Enzi ya Neema, ambapo wote waliompinga Yesu walikuwa wale waliompinga Mungu, na wote ambao hawakutii maneno yaliyotamkwa na Yesu walikuwa wale waliompinga Mungu. Ufafanuzi wa kipindi hiki wa “kumpinga Mungu” ulikuwa sahihi na wa vitendo zaidi. Kabla ya Mungu kuwa mwili, kipimo cha iwapo mtu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo alimwabudu na kumtazamia Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa kipindi hicho wa “kumpinga Mungu” haukuwa wenye uhalisi kabisa, kwa maana watu hawakuweza kumwona Mungu, na hawakujua hasa mfano wa Mungu ulikuwa vipi au Alifanya kazi na kuzungumza vipi hasa. Watu hawakuwa na dhana zozote kumhusu Mungu, na walimwamini Mungu katika hali isiyo dhahiri, kwa sababu Mungu alikuwa bado hajamwonekania mwanadamu. Kwa hivyo, haijalishi jinsi watu walivyomwamini Mungu kulingana na mawazo yao, Mungu hakuwahukumu au kuwawekea matakwa ya juu mno, kwa sababu hawakuweza kabisa kumwona Mungu. Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa watu, wote wanamwona Yeye, wanasikia maneno Yake, na wanaona matendo ya Mungu katika mwili, ambapo dhana za kila mtu hupasuka kama mapovu. Kuhusu wale wanaomwona Mungu akionekana katika mwili, hawatahukumiwa ikiwa watamtii Yeye kwa kudhamiria, ilhali wale wanaompinga kwa makusudi wataainishwa kama watu wanaompinga Mungu. Watu kama hao ni wapinga Kristo, maadui wanaompinga Mungu kwa makusudi. Wale wanaoshikilia dhana kumhusu Mungu lakini bado wanamtii kwa hiari hawatahukumiwa. Mungu huwahukumu watu kwa msingi wa nia zao na mambo wanayofanya, sio kwa mawazo na fikira zao. Ikiwa Angewahukumu watu kwa msingi wa mawazo na fikira zao, basi hakuna mtu hata mmoja ambaye angeweza kuepuka mikono ya hasira ya Mungu. Wale wanaompinga Mungu mwenye mwili kwa makusudi wataadhibiwa kwa ukaidi wao. Upinzani wa watu hawa unatokana na dhana walizo nazo kumhusu Mungu, jambo ambalo linawapelekea kufanya mambo yanayosumbua kazi ya Mungu. Watu wote kama hao wanapinga kwa makusudi na kujaribu kuvunja kazi ya Mungu. Sio tu kwamba wana dhana kumhusu Mungu—pia wanashiriki katika shughuli zinazosumbua kazi Yake, na kwa sababu hii wanahukumiwa. Wale ambao hawasumbui kazi ya Mungu kwa makusudi hawatahukumiwa kama wenye dhambi, kwa sababu wanaweza kutii kwa kudhamiria na kutofanya mambo yanayosababisha vurugu na usumbufu. Watu kama hawa hawatahukumiwa. Hata hivyo, wakati mtu amepitia kazi ya Mungu kwa miaka mingi huku akiwa bado na dhana kumhusu Yeye na akiwa hawezi kujua kazi ya Mungu mwenye mwili, na bado amejawa na dhana kumhusu Mungu na hawezi kumjua Yeye haijalishi amepitia kazi Yake kwa miaka mingapi, moyo wake ukiwa umejaa dhana kumhusu Yeye licha ya kwamba sio lazima awe amefanya chochote kinachosababisha usumbufu—na, ingawa dhana hizi huenda zisiweze kuwa dhahiri, mtu huyu hana msaada wowote kwa kazi ya Mungu, hawezi kuhubiri injili kwa ajili ya Mungu au kusimama imara katika ushuhuda wake Kwake—hiyo inamaanisha kwamba yeye ni mtu asiye na faida yoyote na mjinga. Kwa sababu hamjui Mungu na zaidi ya hayo hawezi kabisa kuachana na dhana zake kumhusu, anahukumiwa. Inaweza kuelezwa hivi: Ni kawaida kwa wale ambao wameanza kumwamini Mungu hivi punde kuwa na dhana kumhusu au kutomjua Yeye, lakini ikiwa mtu amemwamini Mungu kwa miaka mingi na amepitia kazi Yake nyingi, na bado ana dhana kumhusu, hiyo si kawaida, na ni isiyo ya kawaida hata zaidi ikiwa hana ufahamu wowote wa Mungu. Kwa sababu hii si hali ya kawaida, anahukumiwa. Watu hawa wasio wa kawaida wote hawana faida; wao ndio wanaompinga Mungu zaidi na ambao wamefurahia neema ya Mungu bure. Watu wote kama hao wataondoshwa mwishowe!
Wale ambao hawafahamu kusudi la kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu. Hili ni kweli hata zaidi kwa wale ambao wanafahamu kusudi la kazi ya Mungu lakini hawafuatilii kumridhisha Yeye. Kuna wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa na kukariri vifungu mchana kutwa, lakini hakuna hata mmoja miongoni mwao anayeelewa kusudi la kazi ya Mungu, wala hakuna yeyote miongoni mwao anayeweza kumjua Mungu—sembuse yeyote anayeweza kulingana na nia za Mungu. Wote ni watu wasio na thamani, waovu, ambao wanasimama juu ili kumhubiria “Mungu.” Wao ni watu wanaotenda chini ya bendera ya Mungu lakini wanampinga Mungu kwa makusudi, ambao wanabeba jina la kumwamini Mungu huku wakila nyama na kunywa damu ya mwanadamu. Watu wote kama hao ni ibilisi waovu wanaomeza roho za binadamu, mapepo wakuu wanaowasumbua watu kwa makusudi wasianze njia sahihi, na vikwazo vinavyowazuia watu kumtafuta Mungu. Wanaweza kuonekana kuwa “imara kimwili,” lakini wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaowaongoza watu kumpinga Mungu? Wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni ibilisi walio hai waliojitolea kumeza roho za binadamu? Wale wanaojiamini kuwa watukufu mbele za Mungu ndio wa chini kabisa kati ya wote, huku wale wanaojifikiria kuwa wa chini ndio watukufu kabisa. Na wale wanaojidai kujua kazi ya Mungu na ambao wanaweza kutangaza kazi Yake kwa wengine bila kizuizi wanapomtazama Yeye ndio wajinga kabisa kuliko wote. Watu kama hao hawana ushuhuda wa Mungu, na wote ni wenye kiburi na majivuno. Wale wanaoamini wanajua machache sana kuhusu Mungu lakini ambao kwa kweli wana upitiaji wa vitendo na ufahamu wa vitendo wa Mungu ndio wanaopendwa zaidi na Yeye. Ni watu kama hao tu ambao kwa kweli wana ushuhuda na kwa kweli wana uwezo wa kufanywa kuwa watimilifu na Mungu. Wale ambao hawaelewi nia za Mungu ni wale wanaompinga Mungu. Wale ambao wanaelewa nia za Mungu lakini hawatendi ukweli ni wale wanaompinga Mungu. Wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu, na bado wanakwenda kinyume na kiini cha maneno ya Mungu, ni wale wanaompinga Mungu. Wale walio na dhana kumhusu Mungu mwenye mwili, na zaidi ya hayo wanashiriki katika uasi kwa kudhamiria, ni wale wanaompinga Mungu. Wale wanaomhukumu Mungu ni wale wanaompinga Mungu. Na yeyote asiyeweza kumjua Mungu wala kumshuhudia Yeye ni mtu anayempinga Mungu. Kwa hivyo, Ninawahimiza ninyi: Ikiwa kwa kweli mna imani ya kuitembea njia hii, basi endeleeni kufuata. Lakini ikiwa hamwezi kujizuia kumpinga Mungu, basi ni afadhali mjiondoe kabla hamjachelewa, la sivyo mambo kwa kweli hayatakuwa mazuri kwenu, kwa kuwa asili yenu ni potovu mno. Hamna uaminifu, hamna utii, hamna moyo unaoonea kiu haki na ukweli, na hamna upendo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kwamba hali yenu mbele za Mungu kimsingi ni vurugu tupu. Hamwezi kushika kile mnachopaswa kushika, hamwezi kusema kile mnachopaswa kusema, hamwezi kutia katika vitendo kile mnachopaswa kutenda, na hamwezi kutimiza kazi mnayopaswa kutimiza; hamna uaminifu mnaopaswa kuwa nao, hamna dhamiri mnayopaswa kuwa nayo, hamna utii mnaopaswa kuwa nao, wala azimio mnalopaswa kuwa nalo; hamjavumilia mateso mliyopaswa kuvumilia, na hamna imani mnayopaswa kuwa nayo pia. Hamna sifa yoyote nzuri kabisa. Je, hamwoni aibu kuendelea kuishi? Ninawashauri kwamba ni afadhali mfunge macho yenu katika pumziko la milele mapema badala ya baadaye, na hivyo kumwepusha Mungu kuwa na wasiwasi kwa ajili yenu na kuteseka kwa ajili yenu. Mnamwamini Mungu na bado hamwelewi nia Zake; mnakula na kunywa maneno ya Mungu na bado hamwezi kutii matakwa ya Mungu kwa mwanadamu. Mnamwamini Mungu na bado hammjui Yeye, na mnaishi bila lengo la kujitahidi kufikia, bila thamani yoyote au maana yoyote ile. Ninyi ni binadamu na bado hamna dhamiri, uadilifu, au uaminifu hata kidogo—je, bado mnaweza kujiita binadamu? Mnamwamini Mungu na bado mnamdanganya Yeye; hata mnatamani pesa za Mungu na mnakula sadaka zinazotolewa Kwake. Na bado mwishowe mnashindwa kuonyesha hata chembe ya kujali hisia za Mungu au dhamiri ndogo sana Kwake. Hamwezi hata kutosheleza takwa moja dogo lililotolewa na Mungu. Je, bado mnaweza kujiita binadamu? Mnakula chakula ambacho Mungu anawapa, mnapumua oksijeni Anayowapa, na mnafurahia neema Yake, lakini mwishowe hamna ufahamu wowote wa Mungu hata kidogo. Kinyume chake, mmekuwa watu wasio na faida yoyote wanaompinga Mungu. Je, hilo haliwafanyi muwe wanyama ambao hawawezi hata kulinganishwa na mbwa? Miongoni mwa wanyama, je, kuna wowote wenye nia mbaya zaidi yenu?
Wachungaji na wazee hao wanaosimama juu wakiwahubiria wengine ni wale wanaompinga Mungu; wote ni washirika wa Shetani. Kuhusu ninyi mnaowahubiria wengine huku mkiwa hamjasimama juu, je, ninyi hamumpingi Mungu hata zaidi? Je, ninyi hamshirikiani na Shetani hata zaidi? Wale ambao hawafahamu kusudi la kazi ya Mungu hawajui jinsi ya kulingana na nia za Mungu. Je, hili linaweza kuwa kweli kwa wale ambao wanaelewa kusudi la kazi Yake? Kazi ya Mungu haina makosa kamwe; badala yake, tatizo liko katika ufuatiliaji wa watu. Je, wapotovu hao wanaompinga Mungu kwa makusudi si waovu na wenye nia ya kudhuru hata zaidi ya wachungaji na wazee hao? Wengi ni wale wanaompinga Mungu, lakini miongoni mwao hali tofauti ambazo kwazo wanampinga Mungu ni nyingi pia. Kama vile kuna kila aina ya waumini, vivyo hivyo kuna kila aina ya wale wanaompinga Mungu, kila mmoja akiwa tofauti na mwingine. Hakuna hata mmoja wa wale wanaoshindwa kutambua waziwazi kusudi la kazi ya Mungu anayeweza kuokolewa. Bila kujali jinsi mtu alivyompinga Mungu zamani, anapokuja kufahamu kusudi la kazi ya Mungu na anapoweza kujitahidi kumridhisha Mungu, Mungu atafuta dhambi zake zote za zamani. Mradi tu mtu anaweza kutafuta na kutenda ukweli, Mungu hatakumbuka yote aliyofanya. Zaidi ya hayo, Mungu atamwainisha kama mtu mwenye haki kwa sababu anaweza kutenda ukweli. Hii ndiyo haki ya Mungu. Kabla mtu hajamwona Mungu au hajapitia kazi Yake, bila kujali jinsi alivyomtendea Mungu, Yeye hakumbuki hilo. Hata hivyo, punde tu mtu anapomwona Mungu na anapopitia kazi Yake, matendo na vitendo vyake vyote vitaingizwa na Mungu katika “kumbukumbu,” kwa maana amemwona Mungu na ameishi katikati ya kazi Yake.
Wakati mtu ameona kwa kweli kile Mungu anacho na alicho, ametazama ukuu wa Mungu, na kwa kweli amepata kujua kazi ya Mungu—na, zaidi ya hayo, wakati tabia yake ya zamani imebadilishwa—atakuwa ametupa mbali kabisa tabia yake ya uasi inayompinga Mungu. Inaweza kuelezwa hivi: Kila mtu amempinga Mungu, na kila mtu amemwasi Mungu. Hata hivyo, ikiwa unaweza kumtii Mungu mwenye mwili kwa kudhamiria, na kuanzia wakati huu na kuendelea uuridhishe moyo wa Mungu kwa uaminifu wako, utende ukweli unaopaswa kutenda, ufanye wajibu unaopaswa kufanya, na ushike kanuni unazopaswa kushika, basi wewe ni mtu aliye tayari kutupa mbali uasi wako ili umridhishe Mungu na mtu anayeweza kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu. Ukishikilia kwa ukaidi njia zako zisizo sahihi, bila majuto moyoni mwako, na uendelee na mwenendo wako wa uasi bila nia hata kidogo ya kushirikiana na Mungu na kumridhisha Yeye, basi mtu mkaidi na asiyerekebishika kama wewe ataainishwa ili aadhibiwe, na ataainishwa kama mtu ambaye hatafanywa kuwa mtimilifu na Mungu. Ikiwa hili litatokea, utakuwa adui wa Mungu leo na adui wa Mungu kesho pia, na utabaki kuwa adui wa Mungu kesho kutwa—utakuwa daima mtu anayempinga Mungu, adui wa Mungu. Mungu anawezaje kukuacha uende zako basi? Watu wana asili inayompinga Mungu, lakini hawapaswi kutafuta kwa makusudi “siri” ya kumpinga Mungu kwa sababu ni vigumu sana kubadilisha asili ya mtu. Ikiwa utajaribu, itakuwa afadhali kwako kuondoka tu kabla hujachelewa, isijekuwa kuadibiwa kwako katika siku za usoni kukawa kukali zaidi, na isijekuwa asili yako ya kinyama ikalipuka na kuwa isiyodhibitika, na mwili wako wa nyama ukaangamizwa na Mungu mwishowe. Unamwamini Mungu ili kupokea baraka; lakini ikiwa mwishowe utakumbana na ole badala yake, imani yako kwa kweli haitakuwa na thamani. Ninawahimiza ninyi, ni afadhali mbuni mpango mwingine. Je, isingekuwa bora kwenu kufanya kitu kingine chochote kuliko kumwamini Mungu? Je, kweli mnaamini hii ndiyo njia pekee kwenu? Je, msingeendelea kuishi hata bila kutafuta ukweli? Kwa nini mjiweke kinyume na Mungu namna hii?