Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Uhalisi—Kushiriki katika Kaida za Dini Si Imani

Je, ni matendo mangapi ya kidini unayofuata? Je, ni mara ngapi umeenda kinyume na neno la Mungu na umefuata njia yako? Je, ni mara ngapi umeweka neno la Mungu katika vitendo kwa sababu unajali mizigo Yake kweli na unatafuta kuziridhisha nia Zake. Unapaswa kuelewa neno la Mungu, utende kulingana nalo, na uwe mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; hili halimaanishi kufuata taratibu au kufanya kitu shingo upande kwa ajili ya kujionyesha tu, badala yake linamaanisha kutenda ukweli na kuishi kwa kutegemea neno la Mungu. Ni utendaji kama huu tu ndio unaomridhisha Mungu. Uamuzi wowote wa kutenda ambao unamridhisha Mungu sio taratibu, ila ni kutenda ukweli. Watu wengine wanapenda kujionyesha. Mbele ya ndugu na dada zao, wao huenda wakasema ni wadeni wa Mungu, lakini kwa siri, hawatendi ukweli na wanafanya kinyume kabisa. Je, hawa si Mafarisayo wa dini? Mtu anayempenda Mungu kwa kweli na anayemiliki ukweli ni mtu mwaminifu kwa Mungu lakini hajionyeshi kwa nje. Mtu kama huyu ako radhi kutenda ukweli hali zinapoibuka, na hazungumzi wala hatendi kwa njia ambayo inaenda kinyume na dhamiri yake. Mtu kama huyu anadhihirisha hekima mambo yanapotokea, na ni mwenye maadili katika matendo yake bila kujali hali. Huyu pia ni mtu wa aina ambaye anaweza kutoa huduma ya kweli. Kuna wengine ambao mara kwa mara husema maneno matupu kuhusu udeni wao kwa Mungu; wanajifanya kuwa na nyuso za wasiwasi, wakijionyesha na kujifanya wa kuhuzunisha. Ni jambo la kuchukiza kiasi gani! Ukimwuliza, “Hebu niambie kuhusu jinsi ulivyo mdeni wa Mungu?” kisha watabaki bila la kusema. Iwapo wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi hutaongea kwa nje kuhusu hilo; badala yake utadhihirisha upendo wako kwa Mungu kwa njia ya kutenda kwa uhalisi, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaosema maneno matupu tu kwa Mungu ni wanafiki! Wengine wanazungumzia udeni wao kwa Mungu kila mara wanapoomba, na kuanza kulia kila wakati wakiomba, wakati wowote ule, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wanamilikiwa na kaida na dhana za kidini; wanaishi kwa kutegemea kaida na dhana kama hizo, kila wakati wakiamini kuwa matendo hayo yanamfurahisha Mungu na kuwa Anapendelea ucha Mungu wa juujuu na machozi ya kusononesha. Je, watu wapumbavu kama hawa wanaweza kuwa wa maana? Ili kudhihirisha unyenyekevu, wengine wanajifanya wazuri wanapozungumza mbele ya wengine. Wengine wanajidhalilisha kwa makusudi wanapokuwa na wengine, wakijifanya wanakondoo wasio na nguvu hata kidogo. Je, huu ni mwenendo unaofaa watu wa ufalme? Watu wa ufalme wanapaswa kuwa wachangamfu na huru, safi na walio wazi, waaminifu na wa kupendeka, na wawe wanaishi katika hali ya uhuru. Wanapaswa kuwa na uadilifu na heshima na waweze kusimama imara katika ushahidi popote waendapo; watu kama hawa wanapendwa na Mungu na mwanadamu vilevile. Wale ambao ni limbukeni katika imani wana matendo mengi yanayoelelea nje; ni lazima kwanza wapitie kipindi cha kupogolewa na kuvunjwa. Kuwa na imani ya ndani katika Mungu si kitu ambacho wengine wanaweza kuona, lakini matendo na vitendo vya watu ambao wanaona ni vya kustahili kusifiwa. Ni watu kama hao tu ndio wanaoweza kuchukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukiwahubiria injili kila siku watu mbalimbali katika jitihada ya kuwaleta kwenye wokovu, lakini mwishowe bado uwe unaishi kwa kufuata taratibu na mafundisho, basi huwezi kumletea Mungu utukufu. Watu kama hao ni watu wa dini, na vile vile ni wanafiki. Kila wakati watu hao wa kidini wanapokutana, huenda wakauliza, “Dada, umekuwaje hivi karibuni?” Anaweza kujibu, “Ninahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu, na kwamba siwezi kuridhisha nia Zake.” Mwingine anaweza kusema, “Mimi, pia, ninahisi kuwa ni mdeni wa Mungu na kwamba siwezi kumridhisha.” Sentensi hizi na maneno haya machache pekee yanaonyesha vitu viovu vilivyo ndani mwao; maneno kama hayo ni ya kuchukiza mno, na ya kukirihi kupindukia. Asili ya watu kama hao ni ya kumpinga Mungu. Wale ambao hulenga uhalisi hufanya ushirika juu ya chochote kilicho mawazoni mwao, na wao hufanya hivyo kwa mioyo ya dhati. Hawajishughulishi na hata jambo moja la uongo, hawaonyeshi uungwana kama huo au mambo ya kufurahisha kama hayo. Wao huwa wanyofu, na hawafuati masharti yoyote ya kidunia. Watu wengine hupenda kuwa na maonyesho ya nje, hata kufikia hatua ya kukosa busara kabisa. Mtu anapoimba, wanaanza kucheza densi, bila hata kugundua kwamba wali ulio kwenye chungu chao umeungua tayari. Watu kama hao si wacha Mungu au wenye uungwana, na ni wa kipuuzi sana. Vitu hivi vyote ni udhihirisho wa ukosefu wa uhalisi. Watu wengine wanapofanya ushirika kuhusu mambo ya maisha ya kiroho, ingawa hawazungumzi kuhusu kuwa wadeni wa Mungu kwa namna yoyote, wao wana upendo wa kweli Kwake kwa dhati. Kuhisi kwako kuwa mdeni wa Mungu hakuwahusu watu wengine; wewe ni mdeni wa Mungu, si wa watu wengine. Kuna faida gani wewe kuwaambia wengine kuhusu hili siku zote? Ni lazima uweke umuhimu juu ya kuingia katika uhalisi, si kwa raghba au maonyesho yoyote ya nje. Mwenendo mzuri wa nje wa binadamu unawakilisha nini? Unawakilisha mwili; hata mwenendo mzuri kabisa kati ya mienendo ya nje hauwakilishi uzima, na inaweza tu kuonyesha silika yako binafsi. Matendo ya nje ya binadamu hayawezi kuziridhisha nia za Mungu. Unazungumza siku zote kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kukimu uzima wa wengine au kuchechemua mioyo yao impendayo Mungu. Je, unaamini kwamba hayo matendo yako yatamridhisha Mungu? Unahisi kwamba ni nia ya Mungu kwako kutenda kwa namna hii, na kwamba matendo yako ni ya kiroho, lakini kwa kweli, yote ni ya kipumbavu. Unaamini kwamba kile unachopenda na kile ambacho uko radhi kufanya ndivyo hasa vile ambavyo Mungu anafurahia. Je, vitu unavyopenda vinaweza kumwakilisha Mungu? Je, haiba ya mtu inaweza kumwakilisha Mungu? Kile unachopenda ndicho ambacho hasa Mungu anachukia, na mazoea yako ndiyo ambayo Mungu anabeua. Ukihisi kuwa mdeni, basi nenda uombe mbele za Mungu; hakuna haja ya kuzungumza kuhusu hilo kwa wengine. Usipoomba mbele za Mungu, na badala yake ujiweke siku zote katika kujionyesha mbele ya wengine, je, hili linaweza kuridhisha nia za Mungu? Ikiwa kila mara unalenga kufanya vitu kwa kuvionyesha kwa nje, basi hili linamaanisha wewe ni batili kuzidi kiasi. Hao ni watu wa aina gani walio na tabia nzuri ya kuonekana nje tu na wanakosa uhalisi? Wao ni Mafarisayo wanafiki na watu wa kidini! Msipoacha matendo yenu ya kujionyesha na mkose kufanya mabadiliko, basi vipengele vya unafiki vilivyo ndani yenu vitakua hata zaidi. Kadiri vipengele vyenu vya unafiki vilivyo vikubwa, ndivyo upinzani kumwelekea Mungu unavyokuwa mwingi. Mwishowe, watu kama hao hakika wataondoshwa.

Iliyotangulia: Tofauti ya Kimsingi Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Inayofuata: Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Sasa ya Mungu Ndio Wanaoweza Kumtumikia Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp