Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Ili uwe na ushuhuda kwa Mungu na kuliaibisha joka jekundu ni sharti uwe na kanuni, na sharti: Katika moyo wako ni lazima umpende Mungu na uingie katika maneno ya Mungu. Kama huingii katika maneno ya Mungu, basi hutakuwa na njia ya kumuaibisha Shetani. Katika ukuaji wa maisha yako, unalikataa joka kuu jekundu na kuliletea aibu kamili, na ni hapo tu ndipo hili joka jekundu kweli linaaibika. Kadiri unavyohiari kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, ndivyo unavyothibitisha kwamba unampenda Mungu na kulichukia joka kuu jekundu; kadiri unavyotii maneno ya Mungu, ndivyo unavyothibitisha kwamba unautamani ukweli. Watu ambao hawayatamani maneno ya Mungu ni watu wasio na uzima. Watu kama hao ni wale walio nje ya maneno ya Mungu, walio ndani ya dini. Wanaomwamini kweli Mungu huwa na ufahamu wa kina wa maneno ya Mungu kupitia kula na kunywa maneno ya Mungu. Ikiwa huyatamani maneno ya Mungu, basi huwezi kweli kula na kunywa haya maneno ya Mungu, na kama huna ufahamu wa maneno ya Mungu, basi huna njia ya kumshuhudia Mungu au kumtosheleza Mungu.

Katika imani yako kwa Mungu, utamjuaje Mungu? Unapaswa kumjua Mungu kupitia maneno na kazi ya leo ya Mungu, bila upotovu au uwongo, na hata kabla jambo lolote lile ni sharti uijue kazi ya Mungu. Huu ndio msingi wa kumjua Mungu. Huo uwongo wa aina mbalimbali unaokosa ukubalifu wa maneno ya Mungu ni dhana za kidini, ni ukubalifu ambao ni potovu na wenye makosa. Ujuzi mkubwa zaidi wa watu mashuhuri wa kidini ni kuyachukua maneno ya Mungu yaliyokuwa yakikubalika zamani na kuyalinganisha na maneno ya Mungu ya leo. Unapomhudumia Mungu wa leo, ikiwa unashikilia vitu vilivyoangaziwa nuru na Roho Mtakatifu hapo zamani, basi huduma yako itasababisha hitilafu na vitendo vyako vitakuwa vimepitwa na wakati na havitakuwa tofauti na ibada ya kidini. Ikiwa unaamini kuwa wanaomhudumia Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wavumilivu…, na ukiweka ufahamu wa aina hii katika vitendo leo hii, basi vitendo kama hivi ni dhana ya kidini, na vitendo kama hivyo ni maigizo ya kinafiki. “Dhana za kidini” inarejelea vitu vilivyopitwa na wakati (kutia ndani ukubalifu wa maneno yaliyonenwa na Mungu zamani na kufichuliwa na Roho Mtakatifu), na vikiwekwa katika vitendo leo, basi vitahitilafiana na kazi ya Mungu na havitamfaidi mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kuyatakasa dhana za kidini yaliyomo ndani yake, basi yatakuwa kizuizi kizito katika kumuhudumia Mungu. Walio na dhana za kidini hawana njia ya kuendelea sawia na hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, watakuwa nyuma hatua moja, halafu mbili—kwani hizi dhana za kidini humfanya mwanadamu kuwa mtu wa kujitukuza na mwenye kiburi. Mungu hahisi kumbukumbu kwa ajili ya Alichokinena na kukifanya hapo zamani; kama kimepitwa na wakati, basi Anakiondoa. Hakika unaweza kuziacha dhana zako? Ukiyakatalia maneno aliyoyanena Mungu hapo zamani, je hili linadhihirisha kuwa unaijua kazi ya Mungu? Kama huwezi kukubali mwangaza wa Roho Mtakatifu leo na badala yake unashikilia mwangaza wa zamani, hili laweza kuthibitisha kuwa unafuata nyayo za Mungu? Je, bado huwezi kuziacha dhana za kidini? Ikiwa ndivyo ilivyo, basi utakuwa mpinga Mungu.

Mwanadamu akiacha dhana za kidini, basi hatatumia akili yake kuyapima maneno na kazi ya Mungu leo hii, na badala yake atatii moja kwa moja. Japokuwa kazi ya Mungu ya leo inaonekana wazi tofauti na ya zamani, unaweza kuiacha mitazamo ya zamani na kutii moja kwa moja kazi ya Mungu leo hii. Kama unaweza kuwa na ufahamu kama huu kwamba unaionea fahari nafasi ya kazi ya Mungu leo bila kujali Alivyofanya kazi zamani, basi wewe ni mtu aliyeyaacha dhana zake, anayemtii Mungu na anayeweza kuitii kazi na maneno ya Mungu na kufuata nyayo za Mungu. Katika hili, kwa hakika, utakuwa mtu anayemtii Mungu. Huichambui au kuitafiti kazi ya Mungu; ni kana kwamba Mungu amesahau kazi Yake ya zamani, nawe pia ukaisahau. Sasa ni sasa, na zamani ni zamani, na kwa sababu leo Mungu ameyaweka kando Aliyoyafanya zamani, haifai uendelee kuyashikilia. Hapo ndipo utakuwa mtu anayemtii kabisa anayemsikia Mungu na aliyeacha kabisa dhana zake za kidini.

Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na masuala mapya, kuna kazi ambayo inakuwa iliyopitwa na wakati na nzee kazi mpya inapoibuka. Hizi aina tofauti tofauti za kazi, nzee na mpya, hazikinzani, bali zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi yamekuwa ya kupendelea uundaji wa mwanadamu wa fikira kama hizo. Inaweza kusewa kwamba, katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa fikira mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu wote wa fikira kumhusu Mungu ndani ya watu, jambo ambalo limewafanya watu wengi wa kidini wanaomtumikia Mungu wageuke kuwa adui Zake. Hivyo, kadiri fikira za watu za kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti. Anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda tu Mungu wa zamani, ambaye ni mzee kwa umri, aliyejaa mvi na Asiyekwama papo hapo. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6000. Hawawezi kusaidika. Labda ni kwa sababu ya usumbufu wa mwanadamu, au kutokiukwa kwa kazi ya Mungu—ila hawa wahubiri bado wanashikilia vitabu vizee na karatasi ilhali Mungu anaendelea na kazi Yake ambayo haijakamilika ya usimamizi kana kwamba hana msaidizi. Japo huu utata unaleta uadui kati ya mwanadamu na Mungu, kiasi kwamba hawapatanishiki, Mungu haujali ukinzani huu. Hata hivyo mwanadamu bado anashikilia imani na dhana zake, na kamwe haiachilii. Ila kitu kimoja kiko wazi: Japo mwanadamu haachi misimamo yake, Mungu mara zote anapiga hatua na kubadilisha misimamo Yake kulingana na muktadha na hatimaye ni mwanadamu atakayeshindwa bila mapambano. Mungu ndiye adui mkubwa zaidi wa maadui wake walioshindwa na vilevile ni bingwa wa wale miongoni mwa wanadamu ambao wameshindwa na wale ambao bado hawajashindwa. Ni nani anaweza kushindana na Mungu na ashinde? Dhana za mwanadamu zinaonekana kutoka kwa Mungu kwani wengi wao walizaliwa kipindi cha kazi ya Mungu. Na bado Mungu hamsamehei mwanadamu kwa sababu ya hili na hata zaidi Hammiminii sifa mwanadamu kwa “kumzalishia Mungu” mazao baada ya mazao ambayo yamo nje ya kazi ya Mungu. Badala yake, Yeye hughadhabishwa sana na fikira na imani za zamani za uungu, za mwanadamu na hata hachukui hatua kufikira tarehe ambayo hizi fikira zilitokea mara ya kwanza. Hakubali kamwe kwamba hizi dhana zinaletwa na kazi Yake kwani dhana za mwanadamu husambazwa na mwanadamu; chanzo chao ni fikira na akili za mwanadamu, na si Mungu, ila ni Shetani. Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hamlielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwa sababu kuna maana kidogo sana ndani ya kazi ya Mungu, wala kwa sababu kazi ya Mungu inatofautiana na matakwa ya binadamu, wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu. Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzitoe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu, na kisha kubadilika na kukitumia kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa binadamu hawana sifa kabisa za kutoa maoni yao mbele za Mungu, na sembuse hawana sifa za kuonyesha hadharani maneno yao yasiyo na thamani, yanukayo, yaliyooza wapendavyo—bila kutaja chochote kuhusu hizo fikira zilizooza. Haina maana?

Mtu anayemhudumia Mungu kwa ukweli ni Yule anayeitafuta roho ya Mungu na anayefaa kutumiwa na Mungu na anayeweza kuacha dhana zake za kidini. Ikiwa unataka kunywa na kula kwako kwa maneno ya Mungu kuzaa matunda, basi ni sharti uache dhana zako za kidini. Ikiwa unataka kumhudumia Mungu, basi ni muhimu zaidi kuacha dhana zako za kidini na kutii maneno ya Mungu kwa kila unachokifanya. Hizi ni sifa za lazima kwa yeyote anayemhudumia Mungu. Ukikosa ufahamu huu, punde tu unapohudumu utasababisha hitilafu na usumbufu, na ukiendelea kushikilia dhana zako, basi bila shaka utagongwa chini na Mungu, usinyanyuke daima. Chukulia wakati wa sasa kama mfano. Mengi ya matamshi na kazi za leo hazilingani na Biblia pamoja na kazi zilizofanywa na Mungu hapo awali, na kama huna nia ya kutii, basi unaweza kuanguka wakati wowote. Ikiwa unataka kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kuziacha kwanza dhana zako za kidini na urekebishe mitazamo yako. Mengi ya yale yatakayosemwa katika siku za usoni hayatalingana na yaliyosemwa zamani na ikiwa sasa unakosa nia ya kutii, hutaweza kuipita njia iliyo mbele yako. Ikiwa njia moja ya Mungu ya kufanya kazi imechipuka ndani yako na huachii dhana zako, basi njia hii itakuwa dhana zako za kidini. Ikiwa kile Mungu Alicho kimekita mizizi ndani yako, basi umepata ukweli, na ikiwa maneno na ukweli wa Mungu unaweza kuwa maisha yako, kamwe hutakuwa na dhana kuhusu Mungu. Walio na ufahamu wa kweli kuhusu Mungu hawatakuwa na dhana na hawatatii mafundisho ya kidini.

Uliza maswali haya ili uwe macho:

1. Je, ufahamu ulio ndani yako unahitilafiana na huduma yako kwa Mungu?

2. Ni vitendo vingapi vya kidini vimo ndani ya maisha yako ya kila siku? Ikiwa unaonekana tu kama unamchaji Mungu, je, hili linamaanisha kuwa maisha yako yamekua na kukomaa?

3. Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, je, unaweza kuachia dhana zako za kidini?

4. Je, una uwezo wa kutupilia mbali ibada za kidini uombapo?

5. Je, unafaa kutumiwa na Mungu?

6. Ni kiwango gani cha ufahamu wako kuhusu Mungu kina dhana za kidini?

Iliyotangulia: Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Ukweli—Kujihusisha na Kaida za Dini Sio Imani

Inayofuata: Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp