Kuingia Katika Uzima (III)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 444)

Unaelewa vipi umaalum katika roho? Roho Mtakatifu hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Shetani hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Roho waovu hufanya vipi kazi ndani ya mwanadamu? Na maonyesho ya kazi hii ni yapi? Wakati kitu kinakufanyikia, je, kinakuja kutoka kwa Roho Mtakatifu, na je, unapaswa kukiheshimu, au kukikataa? Utendaji halisi wa watu huibua mengi ambayo ni ya mapenzi ya kibinadamu ilhali ambayo watu daima huamini kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mengine hutoka kwa roho waovu, ilhali watu bado hudhani yanatoka kwa Roho Mtakatifu, na wakati mwingine Roho Mtakatifu huwaongoza watu kutoka ndani, ilhali watu wanaogopa kwamba mwongozo kama huo hutoka kwa Shetani, na hawathubutu kutii, wakati kwa kweli ni nuru ya Roho Mtakatifu. Hivyo, bila utofautishaji hakuna njia ya kupitia wakati uzoefu kama huo kwa hakika unakufanyikia, na bila utofautishaji, hakuna njia ya kupata maisha. Roho Mtakatifu hufanya kazi vipi? Roho waovu hufanya kazi vipi? Nini hutoka kwa mapenzi ya mwanadamu? Na ni nini hutoka kwa mwongozo na nuru ya Roho Mtakatifu? Kama unaelewa amri za kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mwanadamu, basi utaweza kukuza maarifa yako na kutofautisha katika maisha yako ya kila siku na wakati wa uzoefu wako halisi; utakuja kumjua Mungu, utaweza kumwelewa na kumtambua Shetani, hutachanganyikiwa katika kutii ama kufuatilia kwako, na utakuwa mtu ambaye fikira zake zi wazi, na ambaye hutii kazi ya Roho Mtakatifu.

Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wao daima hufuatilia ukweli na wanamiliki ubinadamu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwapa watu nuru na kuwaongoza katika maisha halisi; wakipitia maneno ya Mungu katika maisha yao tu ndipo wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.

Ni matokeo yapi yanayotimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu? Unaweza kuwa mpumbavu, na kunaweza kuwa hakuna utofautishaji wowote ndani yako, lakini Roho Mtakatifu anapaswa tu kufanya kazi ili kuwe na imani ndani yako, ili wewe daima uhisi kwamba huwezi kumpenda Mungu vya kutosha, ili uwe tayari kushiriki, uwe tayari kushiriki bila kujali ugumu mkuu ulio mbele. Mambo yatakufanyikia na haitakuwa wazi kwako iwapo yanatoka kwa Mungu ama kwa Shetani, lakini utaweza kungoja, na hutakuwa baridi wala mzembe. Hii ndiyo kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao, watu bado hukabiliwa na ugumu wa kweli, wakati mwingine wanalia, na wakati mwingine kuna mambo ambayo hawawezi kuyashinda, lakini hii yote ni hatua ya kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Ingawa hawashindi mambo hayo, na ingawa, wakati huo, wao ni dhaifu na hulalamika, baadaye bado wanaweza kumpenda Mungu na imani dhabiti. Ubaridi wao hauwezi kuwazuia kuwa na uzoefu wa kawaida, na bila kujali kile watu wengine husema, na jinsi wanavyowashambulia, bado wanaweza kumpenda Mungu. Wakati wa maombi, daima wanahisi kwamba walikuwa wadeni wa Mungu sana, na wanaamua kumridhisha Mungu na kuukataa mwili wakati wanakabiliwa na mambo kama hayo tena. Nguvu hii inaonyesha kuna kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao, na hii ndiyo hali ya kawaida ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia ndani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuja mbele ya Mungu katika hali ya kawaida. Hii ni kusema, punde tu kazi ya Shetani inapokuwa ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu au njia yao ya awali ya kuingia katika maisha, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 445)

Wakati kitu kinakufanyikia katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kutofautishaje kati ya iwapo kinatoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu ama kwa kazi ya Shetani? Wakati hali za watu ni za kawaida, maisha yao ya kiroho na maisha yao katika mwili ni ya kawaida, na mantiki yao ni ya kawaida na ya mpangilio; kwa jumla kile wanachokipitia na kuja kujua ndani yao wakati huu kinaweza kusemwa kutoka kwa kuguswa na Roho Mtakatifu (kuwa na umaizi au kumiliki maarifa ya juu juu wanapokula na kunywa maneno ya Mungu, au kuwa waaminifu wakati mambo yanawafanyikia, au kuwa na nguvu ya kumpenda Mungu wakati mambo yanafanyika—haya yote ni ya Roho Mtakatifu). Kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mwanadamu hasa ni ya kawaida: mwanadamu hana uwezo wa kuihisi, na inaonekana kuwa ni kupitia kwa mwanadamu mwenyewe—lakini kwa kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu. Katika maisha ya kila siku, Roho Mtakatifu hufanya kazi ndogo na kubwa kwa kila mtu, na ni tu kwamba kiwango cha kazi hii hubadilika. Watu wengine ni wa ubora mzuri wa tabia, wanaelewa mambo haraka, na nuru ya Roho Mtakatifu hasa ni kubwa ndani yao; watu wengine ni wa ubora duni wa tabia, na inachukua muda mrefu zaidi kwao kuelewa mambo, lakini Roho Mtakatifu huwagusa ndani, na wao, pia, wanaweza kutimiza uaminifu kwa Mungu—Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa wale wote wanaomfuatilia Mungu. Wakati, katika maisha ya kila siku, watu hawampingi Mungu, au kuasi dhidi ya Mungu, hawafanyi mambo ambayo yanazozana na usimamizi wa Mungu, na hawakatizi kazi ya Mungu, ndani ya kila mmoja wao Roho wa Mungu hufanya kazi kwa kiwango kikubwa au kidogo, na kuwagusa, kuwapa nuru, kuwapa nguvu, na kuwasisimua kuingia kimatendo, sio kuwa wazembe au kutamani raha za mwili, kuwa tayari kutenda ukweli, na kutamani maneno ya Mungu—hii yote ni kazi ambayo hutoka kwa Roho Mtakatifu.

Wakati hali ya watu si ya kawaida, wanatelekezwa na Roho Mtakatifu, kuna malalamishi ndani yao, motisha zao si sahihi, wao ni wazembe, wanajiingiza katika tamaa za kimwili, na mioyo yao huasi dhidi ya ukweli, na haya yote hutoka kwa Shetani. Wakati hali za watu si za kawaida, wakati wana uovu ndani yao na wamepoteza mantiki yao ya kawaida, wametelekezwa na Roho Mtakatifu, na hawawezi kumhisi Mungu ndani yao, huu ndiyo wakati Shetani anafanya kazi ndani yao. Ikiwa watu daima wana nguvu ndani yao na daima humpenda Mungu, basi kwa jumla wakati mambo yanawafanyikia yanatoka kwa Roho Mtakatifu, na yeyote wanayekutana naye ni tokeo la mipango ya Mungu. Ambayo ni kusema, wakati hali zako ni za kawaida, wakati upo katika kazi kubwa ya Roho Mtakatifu, basi haiwezekani Shetani kukufanya uyumbayumbe; juu ya msingi huu inaweza kusemwa kwamba kila kitu hutoka kwa Roho Mtakatifu, na ingawa unaweza kuwa na mawazo yasiyo sahihi, unaweza kuyakataa, na usiyafuate. Hii yote hutoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Shetani huingilia katika hali zipi? Wakati hali zako si za kawaida, wakati hujaguswa na Mungu, na uko bila kazi ya Mungu, na wewe ni mkavu na bure ndani, wakati unasali kwa Mungu lakini huelewi chochote, na kula na kunywa maneno ya Mungu lakini hujapewa nuru au mwangaza—wakati kama huo ni rahisi kwa Shetani kufanya kazi ndani yako. Kwa maneno mengine, wakati umeachwa na Roho Mtakatifu na huwezi kumhisi Mungu, basi mambo mengi hukufanyikia ambayo hutoka kwa majaribu ya Shetani. Shetani hufanya kazi wakati sawa na ule Roho Mtakatifu hufanya kazi, na huingilia kwa mwanadamu wakati sawa na ule Roho Mtakatifu hugusa ndani ya mwanadamu; wakati kama huo, hata hivyo, kazi ya Roho Mtakatifu huchukua nafasi ya kwanza, na watu ambao hali zao ni za kawaida wanaweza kushinda, ambao ni ushindi wa kazi ya Roho Mtakatifu juu ya kazi ya Shetani. Wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi, bado kuna tabia potovu ndani ya watu; hata hivyo, wakati wa kazi ya Roho Mtakatifu, ni rahisi kwa watu kugundua na kutambua uasi, malengo na ughushi wao. Ni hapo tu ndipo wanahisi majuto na wanakuwa tayari kutubu. Hivyo, uasi wao na tabia potovu zinaondolewa polepole ndani ya kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na Anapofanya kazi kwa watu bado wana shida, bado wanalia, bado wanateseka, bado ni dhaifu, na bado kuna mengi ambayo si dhahiri kwao, ilhali katika hali kama hiyo wanaweza kujisitisha kurudia mazoea mabaya, na wanaweza kumpenda Mungu, na ingawa wanalia na wana dhiki ndani, bado wanaweza kumsifu Mungu; kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na si ya mwujiza hata kidogo. Watu wengi sana huamini kwamba, punde tu Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi, mabadiliko hutokea katika hali ya watu na mambo muhimu kuwahusu yanaondolewa. Imani kama hizo ni za uwongo. Roho Mtakatifu afanyapo kazi ndani ya mwanadamu, mambo baridi ya mwanadamu bado yako hapo na kimo chake kinabaki sawa na awali, lakini ana mwangaza na nuru ya Roho Mtakatifu, na hivyo hali yake ni ya kimatendo zaidi, hali ndani yake ni za kawaida, na anabadilika kwa haraka. Katika uzoefu wa kweli wa watu, kimsingi wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu au Shetani, na iwapo hawawezi kuwa na madaraka juu ya hali hizi, na hawatofautishi, basi uzoefu wa kweli hauwezekani, sembuse mabadiliko katika tabia. Hivyo, ufunguo wa kuwa na uzoefu wa kazi ya Mungu ni kuweza kubaini mambo kama haya; kwa njia hii, itakuwa rahisi zaidi kwao kupitia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 446)

Kazi ya Roho Mtakatifu ni maendeleo mazuri, ilhali kazi ya Shetani ni kurudi nyuma kwa namna mbaya, uasi, kumpinga Mungu, kupoteza imani kwa Mungu, kutotaka hata kuimba nyimbo za kidini na kuwa dhaifu sana kiasi cha kutoweza kutimiza wajibu wa mtu. Kila kitu kitokacho kwa nuru ya Roho Mtakatifu ni cha kawaida sana; hakilazimishwi kwako. Ukikifuata, basi utakuwa na amani; usipokifuata, basi baadaye utakaripiwa. Ukiwa na nuru ya Roho Mtakatifu, basi hakuna ufanyacho kitakachoingiliwa au kuzuiliwa, utawekwa huru, kutakuwa na njia ya kutenda katika vitendo vyako, na hutapatwa na vizuizi vyovyote, na kuweza kutekeleza mapenzi ya Mungu. Kazi ya Shetani hukusababishia usumbufu katika mambo mengi; inakufanya kutotaka kusali, kuwa mzembe sana kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutotaka kuishi maisha ya kanisa, na inakutenganisha na maisha ya kiroho. Kazi ya Roho Mtakatifu haiingilii maisha yako ya kila siku, na haiingilii maisha yako ya kawaida ya kiroho. Huwezi kutambua mambo mengi katika wakati ambapo yanatokea, lakini, baada ya siku chache, moyo wako unakuwa angavu na akili yako inakuwa safi. Unakuja kuwa na ufahamu juu ya mambo ya roho, na polepole unaweza kutambua ikiwa wazo limetoka kwa Mungu au kwa Shetani. Mambo mengine kwa dhahiri yanakufanya umpinge Mungu na kuasi Mungu, au kukusitisha kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, na mambo haya yote hutoka kwa Shetani. Mambo mengine si dhahiri, na huwezi kujua ni nini wakati huo; baadaye, mnaweza kuona maonyesho yao, na kisha kufanya utambuzi. Kama mnaweza kutambua ni vitu vipi vinavyotoka kwa Shetani na ni vipi vinavyoelekezwa na Roho Mtakatifu, basi hamtapotoshwa kwa urahisi katika uzoefu wako. Wakati mwingine, hali zako zisipokuwa nzuri, una mawazo fulani yanayokutoa katika hali yako baridi—ambalo huonyesha kwamba wakati hali zako ni zisizofaa, mawazo yako mengine yanaweza pia kutoka kwa Roho Mtakatifu. Sio ukweli kwamba wakati wewe ni baridi, mawazo yako yote yanatumwa na Shetani; huo ungekuwa ukweli, basi ni lini ungeweza kugeukia hali ile nzuri? Baada ya kuwa baridi kwa kipindi cha muda, Roho Mtakatifu anakupa fursa kukamilishwa, Anakugusa, na kukutoa katika hali yako baridi.

Baada ya kujua kazi ya Roho Mtakatifu ni ipi, na kazi ya Shetani ni ipi, unaweza kulinganisha haya na hali yako mwenyewe wakati wa uzoefu wako, na uzoefu wako mwenyewe, na kwa njia hii kutakuwa na ukweli mwingi zaidi unaohusiana na kanuni katika uzoefu wako. Baada ya kuelewa mambo haya, utaweza kudhibiti hali yako halisi, utaweza kutofautisha kati ya watu na matukio, na hutahitajika kutumia nguvu nyingi sana katika kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Bila shaka, hiyo ni ilimradi motisha zako ziko sahihi, na ilimradi uko tayari kutafuta, na kutenda. Lugha kama hii—lugha inayohusiana na kanuni—inapaswa kuonyeshwa katika uzoefu wako. Bila hiyo, uzoefu wako utakuwa umejaa kukatizwa na Shetani, na umejaa maarifa ya upuuzi. Ikiwa huelewi jinsi Roho Mtakatifu hufanya kazi, basi huelewi jinsi unapaswa kuingia, na ikiwa huelewi jinsi Shetani hufanya kazi, basi huelewi jinsi unapaswa kuwa mwangalifu katika nyayo zako. Watu wanapaswa kuelewa jinsi Roho Mtakatifu hufanya kazi na jinsi Shetani hufanya kazi; ni sehemu ya lazima ya uzoefu wa watu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 447)

Ni nini kinashirikishwa ndani ya ubinadamu wa kawaida? Utambuzi, hisia, dhamiri na tabia. Iwapo unaweza kufanikisha ukawaida katika kila mojawapo ya vipengele hivi, ubinadamu wako uko katika kiwango kinachostahili. Unapaswa kuwa na mfanano wa binadamu wa kawaida na utende kama anayemwamini Mungu. Sio lazima ufikie viwango vya juu zaidi au kujishughulisha na diplomasia. Unapaswa tu kuwa mwanadamu wa kawaida, na hisia za kawaida za mtu, uweze kung’amua vitu, na kwa kiwango cha chini uonekane kama mwanadamu wa kawaida. Hiyo itakuwa imetosha. Kila kitu kinachohitajika kwako leo kiko katika uwezo wako, na huku si kukulazimisha ufanye kadri ya uwezo wako hata kidogo. Hakuna maneno yasiyo na maana au kazi isiyofaa yatakayotekelezwa kwako. Uovu wote ulioonyeshwa au kufichuliwa katika maisha yako lazima uondolewe. Ninyi mmepotoshwa na Shetani na mna sumu nyingi sana za Shetani. Yote ambayo yanahitajika kwako ni kuiepuka tabia hii potovu ya kishetani, si wewe kuwa mtu mwenye cheo cha juu, au mtu maarufu au mkuu. Hii haina maana. Kazi ambayo imefanyika kwenu inaafikiana na kile ambacho ni cha asili kwenu. Kuna mipaka ya kile Ninachohitaji kutoka kwa watu. Ikiwa watu wa leo wote wangeombwa kutenda kama maafisa wa serikali, na kujizoeza toni ya sauti ya maafisa wa serikali, kujifunza katika namna ya kuzungumza ya viongozi wa serikali wenye cheo cha juu, au kujifunza kwa namna na sauti ya kuzungumza ya waandishi wa insha na waandishi wa riwaya, basi hili halingekubalika pia. Halingeweza kufikiwa. Kwa mujibu wa ubora wa tabia zenu, mnapaswa angalau kuweza kuzungumza kwa hekima na busara na kuelezea mambo wazi. Ni wakati huo ndipo mtakapoyatosheleza mahitaji. Kwa kiwango kidogo sana, utambuzi na hisia vinapaswa kufikiwa. Kwa sasa jambo kuu ni kuitupilia mbali tabia potovu ya kishetani. Lazima uutupilie mbali uovu unaouonyesha. Ikiwa hujavitupilia mbali hivi, unawezaje kugusia hisia na utambuzi wenye mamlaka mkubwa kabisa? Watu wengi wanaona kwamba enzi imebadilika. Hivyo hawajizoezi unyenyekevu au uvumilivu wowote, na pengine pia hawana upendo wowote au mwenendo mwema wa kitakatifu pia. Watu hawa ni wajinga mno! Je, wana kiwango chochote cha ubinadamu wa kawaida? Je, wanao ushuhuda wowote wa kuzungumziwa? Hawana utambuzi na hisia zozote kamwe. Bila shaka, vipengele fulani vya utendaji wa watu vilivyopotoka na vyenye makosa vinapaswa kurekebishwa. Kama vile maisha ya watu ya kiroho yasiyopindika ya zamani au mwonekano wao wenye ganzi na upumbavu—vitu hivi vyote vinapaswa kubadilika. Mabadiliko hayamaanishi kukuruhusu uwe mpotovu au kujiingiza katika mwili, kusema chochote utakacho. Kuzungumza kiholela hakuwezi kukubalika. Kutenda kama mwanadamu wa kawaida ni kuzungumza kwa kueleweka. Ndiyo inamaanisha ndiyo, na la inamaanisha la. Kuwa mwenye ukweli kwa uhakika na uzungumze inavyofaa. Usilaghai, usidanganye. Inapaswa kujulikana ni mipaka gani mtu wa kawaida anaweza kufikia kuhusu mabadiliko ya tabia. Ikiwa hiyo haijulikani, hutaweza kuingia katika uhalisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuboresha Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 448)

Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa huduma ya mwanadamu hupunguzwa taratibu kupitia kwa uzoefu uongezekao na mchakato wa uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote. Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake. Mwanadamu akipoteza kile ambacho chaweza kutimizwa kiasili, hawezi kamwe kuitwa mwanadamu, na hafai kusimama kama kiumbe aliyeumbwa au kuja mbele za Mungu na kumtolea huduma. Aidha, hafai kupokea neema ya Mungu au kutunzwa, kulindwa na kukamilishwa na Mungu. Wengi waliopoteza imani ya Mungu hatimaye hupoteza neema Yake. Si kwamba wanachukia makosa yao tu bali pia hueneza wazo kuwa njia ya Mungu si sahihi. Na wale waasi hupinga hata uwepo wa Mungu; itakuwaje watu wenye uasi kama huo waendelee kupata neema ya Mungu? Wanadamu walioshindwa kutekeleza wajibu wao wameasi sana dhidi ya Mungu na wanawiwa mengi na Yeye, lakini wanageuka na kumkong'ota Mungu kwamba ni mkosaji. Je, mwanadamu kama huyo anastahili vipi kufanywa mkamilifu? Je, si huyu ni mmoja wa wale watakaoondolewa na kuadhibiwa? Mwanadamu asiyefanya wajibu wake mbele za Mungu tayari ana hatia ya makosa mazito sana ambayo hata kifo si adhabu stahili, ila bado mwanadamu ana ufidhuli wa kubishana na Mungu na kujilinganisha na Yeye. Pana faida gani kumkamilisha mwanadamu sampuli hiyo? Kama mwanadamu ameshindwa kutekeleza wajibu wake, anafaa kujihisi mwenye hatia na mdeni; anapaswa kuudharau udhaifu wake na kukosa umuhimu, uasi na uharibifu wake, na zaidi ya hayo, anafaa kujitolea maisha na damu sadaka kwa ajili ya Mungu. Hapo tu ndipo atakapokuwa kiumbe ampendaye Mungu kwa kweli, na ni mwanadamu kama huyu tu anayestahili baraka na ahadi za Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Na wengi wenu je? Mnamtendeaje Mungu aishiye miongoni mwenu? Mmefanyaje wajibu wenu mbele Zake? Je, mmefanya yote mliyoitwa kufanya, hata kwa gharama ya maisha yenu? Mmetoa sadaka gani? Je, hamjapokea mengi kutoka Kwangu? Mnaweza kuonyesha tofauti? Mna uaminifu kiasi gani Kwangu? Mmenitolea huduma vipi? Na kuhusu yote Niliyowapa na kuwafanyia je? Je, mmeyazingatia yote? Je, mmeyahukumu na kuyalinganisha haya yote kwa dhamiri yoyote ndogo mliyo nayo? Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa? Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna nia zenye uovu kunihusu na hamnipendi kwa dhati. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa hata kidogo? Mnawezaje kuchukuliwa kama kiumbe aliyeumbwa? Je, hamjui wazi mnachopaswa kuonyesha nakuishi kwa kudhihirisha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati. Wanadamu kama nyinyi, watu duni, hawastahili kufurahikia neema ya mbinguni. Ni ugumu tu wa maisha na adhabu isiyokoma vitayaandama maisha yenu! Ikiwa hamwezi kuwa waaminifu Kwangu, majaaliwa yenu yatakuwa matatizo. Ikiwa hamwezi kuyawajibikia maneno Yangu na kazi Yangu, kundi lenu litakuwa la kuadhibiwa. Kamwe hamtapata neema, na hamtakuwa na baraka na maisha ya kupendeza katika ufalme. Hii ndiyo hatima na matokeo mnayostahili kupata kwa kujitakia!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 449)

Hao watu wapumbavu na mafidhuli hawajafanya kila wawezalo wala kutimiza wajibu wao tu, bali wameinyoosha mikono yao wakitaka neema, kana kwamba wanastahili wanachoitisha. Na wakishindwa kupata wanachokiomba, wanakuwa wakosa imani zaidi. Watu kama hao wanawezaje kuchukuliwa kuwa wenye mantiki? Ninyi ni sampuli mbaya isiyokuwa na urazini, isiyoweza kabisa kutimiza wajibu mnaotakiwa kutimiza wakati wa kazi ya usimamizi. Thamani yenu tayari imeshuka pakubwa. Kushindwa kwenu kunilipa kwa kuwaonea imani tayari ni tendo la uasi mkuu litoshalo kuwahukumu na kuthibitisha uoga, uovu, uzembe na uduni wenu. Mnawezaje kuendelea kustahili kunyoosha mikono yenu? Hamwezi kuwa hata wa msaada kidogo kwa kazi Yangu, hamwezi kuahidi imani yenu, na hamwezi kunitolea ushuhuda. Tayari haya ni makosa na kushindwa kwenu, na bado mnanivamia, mnanisemea uongo na kulalama kuwa Mimi si mwenye haki. Je, huu ndio uaminifu wenu? Huu ndio upendo wenu? Ni kazi gani nyingine mnayoweza kufanya zaidi ya hii? Mmechangia vipi katika kazi yote ambayo imeishafanywa? Mmegharamia kiasi gani? Ni huruma kubwa tayari kwamba bado Sijawawekea lawama, na bado mnanipa visingizio na kulalama faraghani kunihusu. Kweli mna hata chembe ndogo ya ubinadamu? Ingawa wajibu wa mwanadamu umetiwa doa na fikira za mwanadamu na mitazamo yake, ni sharti ufanye wajibu wako na kuwa mwaminifu kwa imani yako. Uchafu katika kazi ya mwanadamu ni suala la ubora wa tabia yake, ilhali, ikiwa mwanadamu hafanyi wajibu wake, unajisi huu unaonyesha uasi wake. Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 450)

Ikiwa huna maarifa ya kazi ya Mungu, hutajua jinsi ya kushirikiana na Mungu. Ikiwa hujui kanuni za kazi ya Mungu, na hujui jinsi Shetani anavyofanya kazi kwa mwanadamu, hutakuwa na njia ya kutenda. Ufuatiliaji wenye ari pekee hautakuruhusu ufikie matokeo yanayohitajiwa na Mungu. Mbinu kama hiyo ya kupitia ni sawa na ile ya Lawrence: kutotofautisha hali yoyote kabisa na kusisitiza uzoefu tu, kutojua kabisa kazi ya Shetani ni nini, kutojua kazi ya Roho Mtakatifu ni nini, jinsi mwanadamu alivyo bila kuwepo kwa Mungu, na ni watu wa aina gani ambao Mungu anataka kuwakamilisha. Ni kanuni gani zinapaswa kukubaliwa wakati wa kushughulikia aina tofauti za watu, jinsi ya kuelewa vizuri mapenzi ya Mungu sasa, jinsi ya kujua tabia ya Mungu, na ni kwa watu, mazingira, na enzi gani ndiyo huruma, uadhama, na haki ya Mungu huelekezwa—hana utambuzi wowote kuhusu yoyote kati ya haya. Ikiwa watu hawana maono mengi kama msingi wa uzoefu wao, basi uzima haupo, sembuse uzoefu; wanaweza kuendelea kutii na kuvumilia kila kitu kwa upumbavu. Watu kama hawa ni vigumu sana kuwakamilisha. Inaweza kusemwa kuwa ikiwa huna maono yoyote yaliyotajwa hapo juu, hili ni thibitisho tosha kwamba wewe ni mpumbavu, wewe ni kama nguzo ya chumvi ambayo husimama daima katika Israeli. Watu kama hawa ni bure, vinyangarika! Watu wengine hutii kila mara bila kufikiri, wao daima hujitambua na hutumia njia zao wenyewe za kutenda wanaposhughulikia masuala mapya, au wanatumia “hekima” kushughulikia mambo madogo na yasiyofaa kutajwa. Watu kama hao hawana utambuzi, ni kama kwamba asili yao ni kukubali kuonewa bila kulalamika, na wao daima huwa vilevile, hawabadiliki kamwe. Watu kama hawa ni wapumbavu ambao hawana utambuzi hata kidogo. Kamwe hawajaribu kulinganisha matendo kwa hali au watu tofauti. Watu kama hawa hawana uzoefu. Nimewaona watu fulani ambao hushughulika sana katika ujuzi wao wenyewe kiasi kwamba wanapokabiliwa na watu walio na kazi ya pepo waovu, huinamisha vichwa vyao na kukiri dhambi zao, bila kuthubutu kusimama na kuwashutumu. Na wanapokabiliwa na kazi dhahiri ya Roho Mtakatifu, hawathubutu kutii. Wanaamini kwamba pepo hawa waovu pia wako mikononi mwa Mungu, na hawana ujasiri hata kidogo wa kusimama na kuwapinga. Watu kama hawa wanamwaibisha Mungu, na hawawezi kabisa kubeba mzigo mzito kwa ajili ya Mungu. Wapumbavu kama hawa hawaleti tofauti ya aina yoyote. Kwa hivyo, mbinu kama hiyo ya kupata uzoefu, inapaswa kusafishwa, kwani haiwezi kuthibitishwa machoni pa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Uzoefu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 451)

Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu. Wakati mwingine mnaweza kutekeleza aina moja ya kazi na wakati mwingine mnaweza kutekeleza mbili; mradi tu mnatoa nguvu zenu zote kujitumia kwa ajili ya Mungu, hatimaye mtafanywa wakamilifu na Mungu.

Vijana wana falsafa chache za maisha, na hawana hekima na ufahamu. Mungu amekuja hapa kukamilisha hekima na ufahamu wa mwanadamu, na neno la Mungu huyafidia mambo haya ambayo hawana. Hata hivyo, tabia za vijana si thabiti na hii inahitaji mbadiliko na Mungu. Vijana wana mawazo machache ya kidini na falsafa chache za maisha Wanafikiri kwa maneno rahisi, na fikira zao sio ngumu kufahamika. Hiki ni kipengele ambacho ubinadamu wao bado haujachukua umbo na ni kipengele cha kupendeza, lakini vijana hawajui na hawana hekima, na hii ni sehemu ambayo inahitaji kukamilishwa na Mungu. Kupitia kukamilishwa na Mungu, mnaweza kukuza utambuzi na kuweza kuelewa mambo mengi ya kiroho, na hatua kwa hatua mgeuke kuwa watu wanaostahili kutumiwa na Mungu. Ndugu na dada wakubwa pia wanaweza kutekeleza kazi fulani na hawajaachwa na Mungu. Na ndugu na dada wakubwa, wao pia wana mambo yanayofaa na baadhi ya mambo yasiyofaa. Ndugu na dada wakubwa wana falsafa zaidi za maisha, wana mawazo zaidi ya kidini, vitendo vyao vimekwama katika mfumo usiopindika, hufuata sheria kama roboti, wao huvitumia bila kufikiri, na hawawezi kubadilika. Hiki sicho kipengele kinachofaa. Hata hivyo, ndugu na dada wakubwa ni watulivu na wenye kijidhibiti nafsi kuelekea chochote kinachojitokeza; tabia zao ni imara, na hawana hisia kali zisizoweza kutabiriwa. Wanaweza kuwa wapole katika kukubali mambo, lakini hii siyo kasoro kubwa. Mradi mnaweza kutii; mradi mnaweza kuyakubali maneno ya sasa ya Mungu, ikiwa hamchunguzi maneno ya Mungu, ikiwa hamsiti kutii na kufuata, ikiwa hakika hutoi hukumu au kuwa na mawazo mengine mabaya, na ikiwa mnakubali maneno Yake na kuyaweka katika matendo—ikiwa mnakidhi hali hizi—mtaweza kukamilishwa.

Bila kujali kama ninyi ni ndugu au dada wadogo au wakubwa, mnajua kazi mnayopaswa kutekeleza. Wale walio katika ujana wao sio wenye kiburi; wale walio wakubwa zaidi sio wasioonyesha hisia na hawarudi nyuma. Nao wanaweza kutumia nguvu za kila mmoja kufidia upungufu wao, na wanaweza kuhudumiana bila ubaguzi wowote. Daraja la urafiki linajengwa kati ya ndugu na dada wadogo na wakubwa. Kwa sababu ya upendo wa Mungu mnaweza kuelewana vizuri zaidi. Ndugu wadogo hawawadharau ndugu wakubwa, na ndugu wakubwa sio wa kujidai. Je! Huu si ushirikiano patanifu? Ikiwa ninyi nyote mna uamuzi huu, basi mapenzi ya Mungu hakika yatatimizwa katika kizazi chenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 452)

Katika siku zijazo, ikiwa wewe unabarikiwa au kulaaniwa kutaamuliwa kulingana na matendo unayotekeleza leo. Ikiwa unafaa kukamilishwa na Mungu itakuwa ni sasa hivi katika enzi hii; hakutakuwa na fursa nyingine katika siku zijazo. Mungu kwa kweli Anataka kukukamilisha sasa, na hii sio njia ya kuzungumza. Katika siku zijazo, bila kujali majaribio gani yanayokufikia, matukio gani yanayofanyika, au maafa gani yanayokupata, Mungu anataka kukukamilisha—huu ni ukweli wa hakika na usio na shaka. Je, jambo hili inaweza kuonekana kutoka wapi? Kutokana na ukweli kwamba neno la Mungu katika enzi zote na vizazi halijawahi kufikia kiwango kikubwa kama lilivyo leo—limeingia katika ulimwengu wa juu, na kazi ya Roho Mtakatifu miongoni mwa wanadamu leo ni ya kipekee. Ni wachache sana kutoka vizazi vilivyopita wameonja hili. Hata katika enzi ya Yesu hapakuwa na ufunuo wa leo; viwango vikubwa vimefikiwa katika maneno yaliyosemwa kwenu, mambo mnayoyaelewa, na mambo mnayoyapitia. Hamuondoki katikati ya majaribu na kuadibiwa, na hii ni inatosha kuthibitisha kwamba kazi ya Mungu imefikia uzuri ambao haujawahi kutokea. Hiki si kitu ambacho mwanadamu anaweza kufanya na sio kitu ambacho mwanadamu anadumisha, lakini badala yake ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo, kutokana na ukweli mwingi wa kazi ya Mungu inaweza kuonekana kwamba Mungu anataka kumkamilisha mwanadamu, na Yeye hakika Anaweza kukufanya uwe mkamilifu. Ikiwa mnaweza kuona jambo hili, ikiwa unaweza kupata ugunduzi huu mpya, basi hutangoja kuja kwa pili kwa Yesu lakini badala yake, utamruhusu Mungu akufanye mkamilifu katika enzi ya sasa. Hivyo, kila mmoja wenu anapaswa kufanya kila linalowezekana na kujitahidi sana ili aweze kukamilishwa na Mungu.

Siku hizi hupaswi kuzingatia mambo hasi. Lazima kwanza uweke kando na kutojali kila kitu ambacho kinaweza kukufanya usihisi hasi. Unaposhughulikia mambo lazima udumishe moyo wa kutafuta na kupapasa papasa, na lazima udumishe moyo wa utii kwa Mungu. Wakati wowote mnapogundua udhaifu wowote ndani yenu, lakini hamko chini ya udhibiti wake na mnatenda kazi ambayo mnapaswa kutenda, hii ni hatua ya hakika kwenda mbele. Kwa mfano: Ndugu wana mawazo ya kidini, lakini unaweza kuomba, na unaweza kutii, kula na kunywa neno la Mungu, na kuimba nyimbo…. Kwa neno moja, chochote unachoweza kufanya, kazi yoyote unayoweza kutenda, jitolee kikamilifu kwa nguvu zote unazoweza kuzitumia. Usisubiri kwa kukaa tu. Kuweza kutimiza wajibu wako kwa ridhaa ya Mungu ni hatua ya kwanza. Kisha unapoweza kuuelewa ukweli na kuingia katika ukweli wa neno la Mungu, utakuwa umekamilishwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 453)

Kila mtu ambaye ameamua anaweza kumhudumia Mungu—lakini ni lazima iwe kwamba wale tu ambao wanayashughulikia kwa makini mapenzi ya Mungu na kuyafahamu mapenzi ya Mungu ndio wanaohitimu na walio na haki ya kumhudumia Mungu. Nimegundua hili kati yenu: Watu wengi wanaamini ya kuwa bora tu wanaeneza injili kwa bidii kwa ajili ya Mungu, waende barabarani kwa ajili ya Mungu, wajitumie na kuacha vitu kwa ajili ya Mungu, na kadhalika, basi huku ni kumhudumia Mungu; hata zaidi, watu wa kidini huamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kukimbia hapa na pale wakiwa na Biblia mikononi mwao, wakieneza injili ya ufalme wa mbinguni na kuwaokoa watu kwa kuwafanya watubu na kuungama; kuna wakuu wengi wa kidini wanaofikiri kwamba kumhudumia Mungu ni kuhubiri makanisani baada ya kusoma na kufunzwa katika chuo cha seminari, kuwafunza watu kwa kusoma sura za Biblia; pia kuna watu katika maeneo ya umaskini wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kupokea uponyaji na kufukuza mapepo, au kuwaombea ndugu, au kuwahudumia; miongoni mwenu, kunao wengi wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kula na kunywa maneno ya Mungu, kumwomba Mungu kila siku, na pia kutembelea na kufanya kazi katika makanisa kila mahali; kunao ndugu wengine wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kunamaanisha kutoolewa wala kulea familia kamwe, na kutoa nafsi zao zote kwa Mungu. Ilhali watu wachache wanajua maana ya kweli ya kumhudumia Mungu. Ingawa kunao wengi wanaomhudumia Mungu kama nyota angani, idadi ya wale wanaoweza kuhudumu moja kwa moja, na wanaoweza kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, ni hafifu—ndogo isiyo na maana. Kwa nini Ninasema hivi? Ninasema hivi kwa sababu wewe hufahamu kiini cha fungu la maneno “huduma kwa Mungu,” na unafahamu machache sana kuhusu jinsi ya kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu. Kuna hitaji la haraka kwa watu kuelewa hasa ni aina gani ya huduma kwa Mungu ndiyo inayoweza kulingana na mapenzi Yake.

Ikiwa ungependa kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanamfurahisha Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho. Isitoshe, unapaswa kujua malengo ya kazi ya Mungu, na kazi ambayo Mungu Ataitenda hapa na wakati huu. Baada ya kufahamu haya, na kupitia kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, kwanza unafaa kuingia, na kupokea agizo la Mungu kwanza. Unapopata uzoefu wa kweli kwa msingi wa maneno ya Mungu, na unapojua kweli kazi ya Mungu, utakuwa umehitimu kumhudumia Mungu. Na unapomhudumia ndipo Mungu hufungua macho yako ya kiroho, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa kazi Yake na kuiona dhahiri zaidi. Ukiingia katika ukweli huu, uzoefu wako utakuwa wa kina zaidi na wa kweli, na wale wote ambao wamepata uzoefu wa aina hiyo wataweza kutembea miongoni mwa makanisa mengi na kuwatolea ndugu zako, ili muweze kutumia nguvu za kila mmoja kufidia upungufu wako na kupata maarifa mengi zaidi ndani ya roho zenu. Ni baada tu ya kutimiza matokeo haya ndipo utakapoweza kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu na kufanywa mkamilifu na Mungu wakati wa kufanya huduma yako.

Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kumfurahisha Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu anataka kufanya kinathibitishwa katika ushuhuda wa watu kama hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu. Ukishakuwa rafiki mwema wa Mungu ndipo utakapoweza kabisa kutawala pamoja na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 454)

Yesu aliweza kukamilisha agizo la Mungu—kazi ya ukombozi wa wanadamu wote—kwa sababu alikabidhi kila tatizo kwa mapenzi ya Mungu, bila kufuata mipango na fikira Zake binafsi. Basi pia, Yeye Alikuwa rafiki mwema wa Mungu—Mungu Mwenyewe, jambo ambalo nyote mnalielewa vizuri sana. (Kwa kweli, alikuwa Mungu Mwenyewe aliyetolewa ushahidi na Mungu; Ninataja jambo hili hapa kwa kuutumia ukweli wa Yesu ili kuonyesha mfano wa suala hili.) Aliweza kuuweka mpango wa usimamizi wa Mungu katika kiini cha mambo yote, na kila mara alimwomba Baba wa mbinguni na kuyatafuta mapenzi ya Baba wa mbinguni. Aliomba, na kusema: “Mungu Baba! Timiza kile ambacho ni mapenzi Yako, na usitende kulingana na nia Zangu; ingekuwa heri ukitenda kulingana na mpango Wako. Mwanadamu anaweza kuwa dhaifu, lakini kwa nini unapaswa kumshughulikia? Ni vipi ambavyo mwanadamu anaweza kustahili kukuhangaisha, mwanadamu ambaye ni kama chungu mkononi Mwako? Ndani ya moyo Wangu, Ninatamani tu kutimiza mapenzi Yako, na Ninatamani Utende Unachotaka kutenda ndani Yangu kulingana na makusudio Yako mwenyewe.” Alipokuwa njiani kuelekea Yerusalemu, Yesu alihisi maumivu makali, kama kwamba kisu kilikuwa kimedungwa ndani ya moyo Wake, ilhali hakuwa na nia yoyote ya kwenda kinyume cha Neno lake; kila mara kulikuwa na nguvu zenye uwezo mkuu zilizomvutia Yeye kuelekea mahali ambapo Angesulubiwa. Mwishowe, alipigiliwa misumari juu ya msalaba na akawa mfano wa mwili wenye dhambi, akiikamilisha kazi hiyo ya ukombozi wa wanadamu, na kufufuka kutoka kwa pingu za kifo na Kuzimu. Mbele Yake, kifo, jehanamu, na Kuzimu vilipoteza nguvu zao, na vilishindwa Naye. Aliishi miaka thelathini na tatu, na katika miaka hiyo yote daima Alifanya kila Alichoweza kutimiza mapenzi ya Mungu kulingana na kazi ya Mungu wakati huo, bila kuzingatia atakachofaidi au kupoteza Yeye binafsi, na kila mara akiwaza kuhusu mapenzi ya Mungu Baba. Hivyo, baada ya Yeye kubatizwa, Mungu alisema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Kwa sababu ya huduma Yake mbele ya Mungu, iliyokuwa na upatanifu na mapenzi ya Mungu, Mungu aliuweka mzigo mzito wa kuwakomboa wanadamu wote juu ya mabega yake na akamfanya ajitolee kuutimiza, na Alikuwa na ujuzi na ustahiki wa kuikamilisha kazi hii muhimu. Katika maisha Yake yote, alivumilia mateso yasiyokuwa na kipimo kwa ajili ya Mungu, na alijaribiwa na Shetani mara nyingi, lakini hakufa moyo. Mungu alimpa kazi ya aina hiyo kwa sababu Alimwamini Yeye, na kumpenda Yeye, na hivyo basi Mungu mwenyewe alisema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Wakati huo, ni Yesu pekee ambaye angeweza kutimiza agizo hili, na hii ilikuwa sehemu moja ya Mungu kutimiza kazi Yake ya kuwakomboa wanadamu wote katika Enzi ya Neema.

Ikiwa, kama Yesu, unaweza kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu, na kuyakataa mambo ya mwili wako, Mungu atakuaminia kazi Zake muhimu, ili uweze kufikia masharti ya kumhudumia Mungu. Ni katika hali hizo pekee ndipo utakapothubutu kusema kwamba unafanya mapenzi ya Mungu na kukamilisha agizo Lake, hapo ndipo utakapothubutu kusema unamhudumia Mungu kweli. Ukilinganishwa na mfano wa Yesu, unaweza kuthubutu kusema kwamba wewe ni mwandani wa Mungu? Je, unaweza kuthubutu kusema kwamba unafanya mapenzi ya Mungu? Je, unaweza kuthubutu kusema kwamba kweli unamhudumia Mungu? Leo, hufahamu aina hii ya huduma kwa Mungu, unaweza kuthubutu kusema kwamba wewe ni rafiki mwema wa Mungu? Ukisema kwamba unamhudumia Mungu, humkufuru Yeye? Fikiria kuhusu hilo: Je, unamhudumia Mungu, au unajihudumia wewe mwenyewe? Unamhudumia Shetani, ilhali kwa ukaidi unasema kwamba unamhudumia Mungu—katika jambo hili humkufuru Mungu? Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, lakini wanalitumia kanisa vibaya, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao ni doezi katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila dhidi ya ndugu zao na kuwadanganya, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?

Nasema hivi ili uweze kujua masharti yanayohitajika kutimizwa ili kuhudumu kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu. Usipoutoa moyo wako kwa Mungu, usipoyashughulikia kwa makini mapenzi ya Mungu kama alivyofanya Yesu, basi huwezi kuaminiwa na Mungu, na mwishowe utahukumiwa na Mungu. Labda leo, katika huduma yako kwa Mungu, kila mara wewe huficha kusudi la kumdanganya Mungu na kila mara wewe humtendea kwa njia isiyo ya dhati. Kwa ufupi, bila kujali chochote kingine, ukimdanganya Mungu, hukumu isiyo ya huruma itakujia. Unapaswa kutumia vizuri nafasi ya kuwa umeingia katika njia sahihi ya kumhudumia Mungu kwa kumpa Mungu moyo wako kwanza, bila kugawanya uaminifu wako. Bila kujali iwapo uko mbele za Mungu, au mbele ya watu wengine, moyo wako unapaswa kuelekezwa kwa Mungu kila wakati, na unapaswa kufanya uamuzi wa kumpenda Mungu kama Yesu. Kwa kufanya hivi, Mungu atakufanya uwe mkamilifu, ili uwe mtumishi wa Mungu anayempendeza Mungu. Ikiwa ungependa kweli kufanywa mkamilifu na Mungu, na huduma yako iwe katika upatanifu na mapenzi Yake, basi unapaswa kubadilisha maoni yako ya awali kuhusu imani kwa Mungu, na kubadilisha jinsi ulivyokuwa ukimhudumia Mungu, ili nafsi yako yote iweze kufanywa kuwa kamilifu na Mungu; kwa kufanya hivi, Mungu hatakuacha, na, kama Petro, utakuwa katika kikosi cha mbele cha wale wanaompenda Mungu. Ukibaki kuwa mtu asiyetubu, basi utakutana na mwisho kama wa Yuda. Hii inapaswa kufahamika na watu wote wanaomwamini Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 455)

Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu amewaamulia kabla watu wengi kumhudumia, wakiwemo watu kutoka kila tabaka la maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni inatimia kwa urahisi. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia. Kila mtu anayemhudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na kudura ya Mungu, na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu kwa kweli anakuja ulimwenguni kufanya kazi Yake, kuwasiliana na watu, ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake. Leo, kundi hili la watu lina bahati kubwa kwa kundi hili lenu kumhudumia Mungu wa utendaji. Hii ni baraka isiyopimika kwenu. Kwa kweli ni Mungu anayewainua. Katika kumteua mtu ili amhudumie, Mungu siku zote huwa na kanuni Zake binafsi. Kumhudumia Mungu hakika, kama vile watu wanavyofikiria, si suala tu la kuwa na shauku. Leo mnaona kwamba mtu yeyote anayeweza kumhudumia Mungu akiwa mbele Yake anafanya hivyo kwa sababu wana mwongozo wa Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa sababu wao ni watu wanaofuata ukweli. Haya ndiyo mahitaji ya kiwango cha chini zaidi ambayo wote wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa nayo.

Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho. Makristo wa uwongo na wapinga Kristo waliozungumziwa watainuka kutoka miongoni mwa watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kuvitupa vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kidogo, hata kama utaivunja miguu yako au mgongo wako ukitia bidii, au hata ukifa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha mambo ni kwamba: Atasema kwamba wewe ni mtenda maovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 456)

Kufikia leo, Mungu atawakamilisha kirasmi wale wasiokuwa na fikira za kidini, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu kwa moyo wa kawaida, na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo hekima nyingi na isiyoisha. Kazi Yake ya kustaajabisha na matamshi Yake yenye thamani vinasubiri hata idadi kubwa ya watu waweze kuvifurahia. Kama ilivyo sasa, wale walio na fikira za kidini, wanaochukua hali ya ukubwa, na wale ambao hawawezi kujiweka pembeni wanaona vigumu sana kukubali vitu hivi vipya. Hakuna fursa ya Roho Mtakatifu kuwakamilisha watu hawa. Kama mtu hajaamua kutii, na hana kiu ya neno la Mungu, basi mtu huyo hataweza kupokea mambo mapya. Wataendelea tu kuwa waasi zaidi na zaidi, kuwa wajanja zaidi na zaidi, na hatimaye kujipata kwenye njia mbaya. Katika kufanya kazi Yake sasa, Mungu atawainua watu zaidi wanaompenda kwa kweli na wanaoweza kukubali mwangaza mpya. Na Atakatiza kabisa maafisa wa kidini wanaoonyesha ukubwa wao. Wale wanaokataa mabadiliko kwa ukaidi: Hataki hata mmoja wao. Je, unataka kuwa mmoja wa watu hao? Je, unatekeleza huduma yako kulingana na mapendeleo yako, au unafanya kile Mungu anachotaka? Hili ni jambo ambalo lazima ujijulie mwenyewe. Je, wewe ni mmojawapo wa maafisa wa kidini, au wewe ni mtoto mchanga anayefanywa kuwa mtimilifu na Mungu? Je, ni kiwango kipi cha huduma yako ambacho kinapongezwa na Roho Mtakatifu? Ni kiwango kipi ambacho Mungu hatasumbuka kukumbuka? Baada ya miaka mingi ya huduma, maisha yako yamebadilika kiasi kipi? Je, uko wazi kuhusu mambo haya yote? Kama unayo imani ya kweli, basi utaweka pembeni fikira zako za kale za kidini na utamhudumia Mungu kwa njia bora zaidi na kwa njia mpya. Hujachelewa sana kusimama sasa. Fikira za kale za kidini zitayakaba maisha ya mtu. Uzoefu ambao mtu anapata utamwongoza mbali na Mungu, kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe. Usipoviweka vitu hivi chini, vitakuwa kikwazo katika kukua kwa maisha yako. Mungu siku zote amewakamilisha wote wanaomhudumia. Hawatupilii mbali kwa urahisi tu. Kama tu utakubali kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo yako na sheria za kidini za kale, na kukoma kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo, ni hapo tu ndipo kutakuwa na mustakabali kwako. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hawatambui watu kama hao. Kama kweli unataka kukamilishwa, basi lazima uamue kutupilia mbali kabisa kila kitu cha kale. Hata kama kile kilichokuwa kimefanywa awali kilikuwa sahihi, hata kama ilikuwa ni kazi ya Mungu, ni lazima bado uweze kuiweka pembeni na uache kuishikilia. Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyo wazi, iliyofanywa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, leo lazima uiweke pembeni. Hufai kuishikilia. Hili ndilo Mungu anahitaji. Kila kitu lazima kifanywe upya. Katika kazi ya Mungu na neno la Mungu, Harejelei vitu vya kale ambavyo vilishapita, na vilevile Hafukui historia ya kale. Mungu siku zote ni mpya na kamwe si mzee. Hashikilii hata maneno Yake mwenyewe ya kitambo inayoonyesha kwamba Mungu hafuati mafundisho ya dini yoyote. Katika hali hii, kama mwanadamu, kama siku zote unashikilia kabisa vitu vya kale, ukikataa kuviachilia na kuvitumia kwa njia ya fomyula, huku naye Mungu hafanyi kazi tena katika njia Alizokuwa akifanya awali, basi maneno yako na matendo yako siyo ya kukatiza? Je, hujawa adui wa Mungu? Je, uko radhi kuyaacha maisha yako yote yaharibike kwa sababu ya mambo haya ya kale? Mambo haya ya kale yatakufanya kuwa mtu anayezuia kazi ya Mungu. Je, mtu kama huyo ndiye wewe unataka kuwa? Kama kweli hutaki kuwa hivyo, basi acha mara moja kile unachofanya na ubadilike; anza tena upya. Mungu hakumbuki huduma yako ya kale.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 457)

Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Ingawa imani hii ni sahihi, ni ya kuegemea upande mmoja sana; kile ambacho Mungu anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu; ni huduma zaidi na kujitoa ndani ya roho. Ndugu wengi hawajawahi kufikiria juu ya kumfanyia Mungu kazi hata baada ya miaka mingi sana ya uzoefu, maana kazi kama mwanadamu anavyoielewa haipatani na ile ambayo Mungu anaitaka. Kwa hiyo, mwanadamu havutiwi kwa namna yoyote ile na kazi ya Mungu, na hii ndiyo sababu kuingia kwa mwanadamu ni kwa kuegemea upande mmoja kabisa. Nyinyi nyote mnapaswa kuingia kwa kumfanyia Mungu kazi, ili muweze kupata uzoefu wa vipengele vyake vyote. Hiki ndicho mnapaswa kuingia ndani. Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu alio nao kwa Mungu na maarifa aliyo nayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu, na yote ambayo mwanadamu anapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupitia kazi ya Mungu hakumaanishi tu kwamba unajua jinsi ya kula na kunywa neno Lake; na muhimu zaidi, mnapaswa kuweza kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia na kumkimu mwanadamu. Hii ni kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza. Kuna watu wengi ambao wanatilia mkazo tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu, lakini hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuza kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu. Kwa miaka mingi sana, wale wanaomtumikia Mungu na kumhudumia mwanadamu wanaona kufanya kazi na kuhubiri kuwa ndio kuingia, na hakuna anayechukulia uzoefu wake binafsi wa kiroho kuwa kuingia muhimu. Badala yake, wanatumia nuru ya kazi ya Roho Mtakatifu kuwafundisha wengine. Wanapohubiri, wanakuwa na mzigo mkubwa sana na wanapokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kupitia hili wanatoa sauti ya Roho Mtakatifu. Wakati huo, wale wanaofanya kazi wanahisi kuridhika kana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wao binafsi wa kiroho; wanahisi kwamba maneno yote wanayoyazungumza wakati huo ni ya yao wenyewe, na pia kana kwamba uzoefu wao si wazi kama walivyoeleza. Kuongezea, wao hawana fununu ya nini cha kusema kabla ya kunena, lakini Roho Mtakatifu anapofanya kazi ndani yao, wao huwa na mtiririko wa maneno usioisha na usiosita. Baada ya kuwa umehubiri kwa namna hiyo, unahisi kwamba kimo chako halisi sio kidogo kama ulivyoamini. Baada ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yako kwa namna ile ile mara kadhaa, basi unaamini kwamba tayari una kimo na unaamini kimakosa kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuingia kwako na asili yako mwenyewe. Unapopitia uzoefu huu kwa mfululizo, unakuwa mzembe kuhusu kuingia kwako. Halafu unakuwa mvivu bila kujua, na kutozingatia kabisa kuingia kwako mwenyewe. Kwa hiyo, unapowahudumia wengine, unapaswa kutofautisha waziwazi kati ya kimo chako na kazi ya Roho Mtakatifu. Hii itasaidia zaidi kuingia kwako na kunufaisha zaidi uzoefu wako. Mwanadamu akidhani kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wake binafsi ndio mwanzo wa upotovu. Hivyo, kazi yoyote mnayoifanya, mnapaswa kuzingatia kuingia kwenu kama somo muhimu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 458)

Mtu anafanya kazi ili kutimiza mapenzi ya Mungu, kuwaleta wale wote wanaoutafuta moyo wa Mungu mbele Yake, kumleta mwanadamu kwa Mungu, na kuitambulisha kazi ya Roho Mtakatifu na uongozi wa Mungu kwa mwanadamu, kwa kufanya hivyo atakuwa anayakamilisha matunda ya kazi ya Mungu. Kwa sababu hii, ni muhimu kuelewa kiini cha kufanya kazi. Kama mtu anayetumiwa na Mungu, watu wote wanafaa kumfanyia kazi Mungu, yaani, wote wana fursa ya kutumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo kuna hoja moja mnayopaswa kuielewa: Mwanadamu anapofanya kazi iliyoagizwa na Mungu, mwanadamu anakuwa amepewa fursa ya kutumiwa na Mungu, lakini kile kinachosemwa na kujulikana na mwanadamu sio kimo cha mwanadamu kabisa. Mnaweza tu kujua vizuri kasoro zako katika kazi yenu, na kupokea nuru kubwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnaweza kupata kuingia kuzuri katika kazi yenu. Ikiwa mwanadamu anachukulia uongozi wa Mungu kuwa ni kuingia kwake mwenyewe na kile kilichomo ndani ya mwanadamu, hakuna uwezo wa mwanadamu kuongezeka kimo. Roho Mtakatifu humpatia mwanadamu nuru anapokuwa katika hali ya kawaida; katika nyakati kama hizo, mara nyingi mwanadamu anadhani nuru anayopokea ni kimo chake mwenyewe katika uhalisi, maana Roho Mtakatifu huangazia katika njia ya kawaida: kwa kutumia kile ambacho ni cha asili kwa mwanadamu. Mwanadamu anapofanya kazi na kuzungumza, au wakati mwanadamu anapofanya maombi katika shughuli zake za kiroho, ndipo ukweli utawekwa wazi kwao. Hata hivyo, katika uhalisi, kile ambacho mwanadamu anakiona ni nuru tu iliyoangaziwa na Roho Mtakatifu (kwa kawaida, hii inahusiana na ushirikiano kutoka kwa mwanadamu) na sio kimo halisi cha mwanadamu. Baada ya kipindi cha kupitia ambapo mwanadamu anakabiliwa na shida na majaribu fulani, kimo cha kweli cha mwanadamu hudhihirika katika mazingira kama hayo. Ni katika muda huo ndipo mwanadamu anagundua kwamba kimo cha mwanadamu sio kikubwa hivyo, na ubinafsi, fikira zake mwenyewe, na tamaa za mwanadamu vyote huibuka. Ni baada tu ya mizunguko kadhaa ya uzoefu kama huo ndipo wengi wa jinsi hiyo ambao wameamshwa ndani ya roho zao watatambua kwamba haukuwa uhalisi wao hapo nyuma, bali ni mwangaza wa muda tu kutoka kwa Roho Mtakatifu, na mwanadamu alipokea nuru tu. Roho Mtakatifu anapompa mwanadamu nuru ili aelewe ukweli, mara nyingi inakuwa katika namna ya wazi na tofauti, bila kueleza jinsi ambavyo mambo yalitokea au kule yanakoenda. Yaani, Hayajumuishi matatizo ya mwanadamu katika ufunuo huu, na badala yake Anatoa ufunuo moja kwa moja. Mwanadamu anapokabiliana na matatizo katika kuingia, basi mwanadamu anaijumuisha nuru ya Roho Mtakatifu, na huu unakuwa uzoefu halisi wa mwanadamu. … Kwa hiyo, mnapoipokea kazi ya Roho Mtakatifu, mnapaswa kujikita zaidi katika kuingia kwenu, na wakati huo huo, kuona kipi ni kazi ya Roho Mtakatifu na kipi ni kuingia kwenu, vilevile kujumuisha kazi ya Roho Mtakatifu katika kuingia kwenu, ili kwamba muweze kukalishwa Naye vizuri na kuruhusu hulka ya kazi ya Roho Mtakatifu kuletwa pamoja ndani yenu. Wakati mnapitia uzoefu wenu wa kazi ya Roho Mtakatifu, mnamjua Roho Mtakatifu, vilevile nyinyi wenyewe, na katikati ya mateso makali, mnajenga uhusiano wa kawaida pamoja na Mungu, na uhusiano baina yenu na Mungu unakuwa wa karibu siku kwa siku. Baada ya michakato mingi ya kupogolewa na kusafishwa, mnakuza upendo wa kweli kwa Mungu. Hii ndiyo sababu mnapaswa kutambua kwamba mateso, mapigo, na dhiki havitishi; kinachoogopesha ni kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tu lakini sio kuingia kwenu. Siku inapofika kwamba kazi ya Mungu imemalizika, mtakuwa mmefanya kazi bure; ingawa mmepitia uzoefu wa kazi ya Mungu, hamtakuwa mmemjua Roho Mtakatifu au kuwa na kuingia kwenu wenyewe. Nuru anayopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu si ya kudumisha hisia za mwanadamu; ni kufungua njia kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu, vilevile kumruhusu mwanadamu kumjua Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo anakuza moyo wa uchaji na ibada kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 459)

Kuna mkengeuko mdogo zaidi katika kazi ya wale ambao wamepitia kupogolewa, kushughulikiwa, hukumu na kuadibu, na uonyeshaji wa kazi zao ni sahihi zaidi. Wale wanaotegemea asili yao katika kufanya kazi wanafanya makosa makubwa sana. Kuna uasili mwingi sana katika kazi ya watu ambao si wakamilifu, kitu ambacho kinaweka kizuizi kikubwa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi ubora wa tabia ya mtu ulivyo mzuri, lazima pia apitie upogoaji, ashughulikiwe, na kuhukumiwa kabla aweze kufanya kazi ya agizo la Mungu. Kama hajapitia hukumu kama hiyo, kwa namna yoyote nzuri ile atakavyofanya, haiwezi kuambatana na kanuni za ukweli na ni uasili kabisa na uzuri wa mwanadamu. Kazi ya wale ambao wamepitia kupogolewa, kushughulikiwa, na hukumu ni sahihi zaidi kuliko kazi ya wale ambao hawajapogolewa, kushughulikiwa, na hukumiwa. Wale ambao hawajapitia hukumu hawaonyeshi chochote isipokuwa mawazo ya kibinadamu, yakiwa yamechanganyika na ufahamu wa kibinadamu na talanta za ndani. Sio maonyesho sahihi wa mwanadamu wa kazi ya Mungu. Watu wanaowafuata wanaletwa mbele yao kwa tabia yao ya ndani. Kwa sababu wanaonyesha vitu vingi vya kuona na uzoefu wa mwanadamu, ambavyo takribani havina muungano na nia ya asili ya Mungu, na hutofautiana sana nayo, kazi ya mtu wa aina hii haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, bali badala yake huwaleta mbele ya mwanadamu. Hivyo, wale ambao hawajapitia hukumu na kuadibu, hawana sifa za kufanya kazi ya agizo la Mungu. Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho. Kwa wafuasi kutambua endapo viongozi wana sifa, jambo la muhimu ni kuangalia njia wanayoiongoza na matokeo ya kazi yao, na kuangalia iwapo wafuasi wanapokea kanuni kulingana na ukweli, na kama wanapokea namna ya kutenda kunakowafaa wao ili waweze kubadilishwa. Unapaswa kutofautisha kati ya kazi tofauti za aina tofauti za watu; haupaswi kuwa mfuasi mpumbavu. Hili linaathiri suala la kuingia kwako. Kama huwezi kutofautisha ni uongozi wa mtu yupi una njia na upi hauna, utadanganywa kwa urahisi. Haya yote yana athari ya moja kwa moja katika maisha yako. Kuna mambo mengi ya asili katika kazi ya mtu ambaye hajakamilishwa; matakwa mengi ya kibinadamu yamechanganywa humo. Hali yao ni ya asili, kile walichozaliwa nacho, si maisha baada ya kupitia kushughulikiwa au uhalisia baada ya kubadilishwa. Ni kwa namna gani mtu wa aina hii ya mtu anaweza kuunga mkono utafutaji wa uzima? Maisha halisi ya mwanadamu ni akili au talanta yake ya ndani. Aina hii ya akili au talanta ni kinyume cha kile hasa ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Ikiwa mwanadamu hajakamilishwa na tabia yake potovu haijapogolewa na kushughulikiwa, kutakuwa na pengo kubwa kati ya kile anachokionyesha na ukweli; utachanganywa na vitu visivyoeleweka vizuri kama vile tafakari zake na uzoefu wa upande mmoja, n.k. Aidha, bila kujali jinsi anavyofanya kazi, watu wanahisi kwamba hakuna lengo la jumla na hakuna ukweli ambao unafaa kwa kuingia watu wote. Matakwa mengi yanawekwa kwa watu wakitakiwa kufanya kile ambacho ni nje ya uwezo wao, kumwingiza bata katika kitulio cha ndege. Hii ni kazi ya matakwa ya binadamu. Tabia potovu ya mwanadamu, mawazo yake na fikira vinaenea katika sehemu zote za mwili wake. Mwanadamu hakuzaliwa na tabia ya kutenda ukweli, na wala hana tabia ya kuuelewa ukweli moja kwa moja. Ikiongezwa kwa upotovu ya mwanadamu—mtu wa aina hii ya asili anapofanya kazi, je, si yeye husababisha ukatizaji? Lakini mwanadamu ambaye amekamilishwa ana uzoefu wa ukweli ambao watu wanapaswa kuuelewa, na maarifa ya tabia yao potovu, ili kwamba vitu visivyoeleweka vizuri na visivyokuwa halisi katika kazi yake vididimie kwa taratibu, ughushi wa binadamu upungue, na kazi na huduma yake yakaribie zaidi viwango vinavyohitajika na Mungu. Hivyo, kazi yake imeingia katika uhalisi wa ukweli na pia imekuwa halisi zaidi. Mawazo katika akili ya mwanadamu yanazuia kazi ya Roho Mtakatifu. Mwanadamu ana fikira nzuri na mwenye mantiki ya maana na uzoefu mkongwe katika kukabiliana na mambo. Kama haya yote hayatapitia kupogolewa na kusahihishwa, yote yanakuwa vizuizi katika kazi. Hivyo kazi ya mwanadamu haiwezi kufikia kiwango cha juu cha usahihi, hususan kazi ya watu ambao hawajakamilishwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 460)

Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wako unaegemea upande mmoja sana. Bila kujua hali yako ya kweli au kufahamu kanuni za ukweli, haiwezekani kufikia mabadiliko katika tabia. Bila kujua kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu au kuelewa matokeo yatokayo hapo, itakuwa vigumu kutambua kazi ya pepo wabaya. Lazima ufunue kazi ya pepo wabaya na mawazo ya wanadamu na uende moja kwa moja kwenye kiini cha suala hili; lazima pia uonyeshe mikengeuko mingi katika utendaji wa watu au matatizo katika kumwamini Mungu ili waweze kuyatambua. Kwa kiwango cha kidogo sana, lazima usiwafanye kuhisi hasi au wasiojishughulisha. Hata hivyo, lazima uelewe shida ambazo zipo kwa watu wengi bila upendeleo, hupaswi kuwa bila busara au “ujaribu kumfunza nguruwe kuimba”; hiyo ni tabia ya upumbavu. Ili kutatua matatizo mengi ya wanadamu, lazima uelewe elimumwendo ya kazi ya Roho Mtakatifu, lazima uelewe jinsi Roho Mtakatifu anavyotekeleza kazi kwa watu tofauti, lazima uelewe matatizo ya wanadamu, upungufu wa wanadamu, ubaini masuala muhimu ya shida, na kufikia chanzo cha tatizo, bila mkengeuko au makosa. Ni mtu wa aina hii tu ndiye aliyestahiki kuratibu kumhudumia Mungu.

Bila kujali kama unaweza kuelewa masuala muhimu na kuona kwa dhahiri mambo mengi hutegemea uzoefu wako binafsi. Namna ambavyo unapitia ndiyo pia namna ambavyo unaowaongoza wengine. Ikiwa unaelewa barua na mafundisho, basi unawaongoza wengine kuelewa barua na mafundisho. Njia ambayo unapitia ukweli wa maneno ya Mungu ndiyo njia ambayo unawaongoza wengine kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ikiwa unaweza kuelewa ukweli mwingi na kuona kwa dhahiri mambo mengi katika maneno ya Mungu, basi unaweza kuwaongoza wengine kuelewa ukweli mwingi, na wale unaowaongoza watakuwa na ufahamu wa wazi wa maono. Ukilenga kushika hisia zisizo za kawaida, basi wale unaowaongoza pia watalenga hisia zisizo za kawaida. Ikiwa unapuuza matendo na kusisitiza kuzungumza, basi wale unaowaongoza pia watazingatia kuzungumza, bila utekelezaji wowote, bila mbadiliko wowote katika tabia zao, na watakuwa tu na shauku kwa nje, bila kutenda ukweli wowote. Wanadamu wote huwatolea wengine kile walicho nacho wenyewe. Aina ya mtu huamua njia ambayo anawaongoza wengine kuingia, na aina ya mtu huamua aina ya watu anaowaongoza. Ili kuwa wa kufaa kwa matumizi ya Mungu, hamhitaji tu kuwa na matarajio, lakini mnahitaji pia nuru nyingi kutoka kwa Mungu, mwongozo kutoka kwa maneno ya Mungu, kushughulikiwa na Mungu, na usafishaji wa maneno Yake. Hili likiwa msingi, katika nyakati za kawaida, mnapaswa kutilia maanani uchunguzi, mawazo, kutafakari na hitimisho, na mjishughulishe na uingiaji au uondolewaji inavyopasa. Hizi zote ni njia za kuingia kwenu katika uhalisi na zote ni za msingi—hii ndiyo njia ambayo Mungu hufanya kazi. Ikiwa unapaswa kuingia katika njia hii ambayo Mungu hufanya kazi, basi utakuwa na fursa ya kukamilishwa na Mungu kila siku. Na wakati wowote, bila kujali kama ni mazingira magumu au mazingira mazuri, kama unajaribiwa au unashawishiwa, kama unafanya kazi au la, kama unaishi maisha kama mtu binafsi au kwa pamoja, utapata fursa za kukamilishwa na Mungu kila wakati, bila kukosa hata moja yao. Utakuwa na uwezo wa kugundua zote, na kwa njia hii utakuwa umepata siri ya kupitia maneno ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 461)

Siku hizi, watu wengi hawatilii maanani ni mafunzo yapi wanayopaswa kupata wakati wanaposhirikiana na wengine. Nimegundua kwamba wengi wenu hawawezi kupata mafunzo hata kidogo wakati wanaposhirikiana na wengine; wengi wenu huyashikilia maoni yenu wenyewe. Unapofanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na mtu mwingine anatoa yake, na maoni hayo hayana uhusiano; kwa kweli hamshirikiani hata kidogo. Ninyi nyote mnajishughulisha sana na kuwasiliana tu kuhusu utambuzi wenu wenyewe ama kuachilia “mizigo” mliyoibeba ndani yenu, bila kutafuta uzima kwa namna yoyote ile. Unaonekana kufanya kazi kwa njia ya uzembe tu, daima ukiamini kwamba unapaswa kuitembea njia yako mwenyewe bila kujali kile ambacho mtu mwingine anasema ama kufanya; unafikiria kwamba unapaswa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza, bila kujali hali za wengine zinaweza kuwa zipi. Hamwezi kugundua uwezo wa wengine, na wala hamwezi kujichunguza. Kukubali kwenu mambo kumepotoka na kuna makosa sana. Inaweza kusemwa kwamba hata sasa bado mnaonyesha unyoofu mwingi, kana kwamba mmerudia ugonjwa huo wa zamani. Kwa mfano, hamwasiliani kwa njia inayofanikisha uwazi kamili, kwa mfano, kuhusu aina ya matokeo ambayo mmepata kutoka kwa kazi katika makanisa fulani, ama kuhusu hali zako za ndani za siku hizi na kadhalika; kamwe hamwasiliani hata kidogo kuhusu mambo kama hayo. Hamshiriki hata kidogo katika vitendo kama kuyaacha mawazo yenu wenyewe ama kujikana. Viongozi na wafanyakazi wanafikiri tu kuhusu jinsi ya kuwazuia ndugu zao wasiwe hasi na jinsi ya kuwafanya waweze kufuata kwa juhudi. Hata hivyo, ninyi nyote mnafikiri kwamba kufuata kwa juhudi pekee kunatosha, na kimsingi, hamwelewi maana ya kujijua na kujikana, sembuse kuelewa maana ya kuhudumu kwa kushirikiana na wengine. Mnafikiri tu kuhusu ninyi wenyewe kuwa na nia ya kuulipiza upendo wa Mungu, kuhusu ninyi wenyewe kutaka kuishi kwa kudhihirisha mtindo wa Petro. Hamfikirii kuhusu kitu kingine isipokuwa mambo haya. Hata unasema kwamba bila kujali yale watu wengine wanayofanya, hutatii bila kufikiria, na kwamba bila kujali jinsi watu wengine walivyo, wewe mwenyewe utatafuta kukamilishwa na Mungu, na hiyo itatosha. Hata hivyo, ukweli ni kwamba kutaka kwako hakujapata maonyesho thabiti kwa kweli. Je, haya yote sio mwenendo ambao mnadhihirisha siku hizi? Kila mmoja wenu anashikilia utambuzi wake mwenyewe, na nyote mnatamani kukamilishwa. Naona kwamba mmehudumu kwa muda mrefu sana bila kufanya maendeleo mengi; hasa katika funzo hili la kufanya kazi pamoja kwa upatanifu, hamjafanikisha chochote hata kidogo! Unapokwenda katika makanisa unawasiliana kwa njia yako, na wengine wanawasiliana kwa njia zao. Ushirikiano wa upatanifu unafanyika mara chache sana, na hili ni kweli hata zaidi kwa wafuasi walio chini yako. Yaani, ni mara chache ambapo yeyote kati yenu anaelewa maana ya kumhudumia Mungu, ama jinsi mtu anavyopaswa kumhudumia Mungu. Mmekanganyikiwa na mnayachukulia mafunzo ya aina hii kama mambo madogo. Hata kuna watu wengi ambao hawakosi kutenda kipengele hiki cha ukweli tu, lakini ambao pia wanafanya makosa kwa makusudi. Hata wale ambao wamehudumu kwa miaka mingi wanapigana na kupangiana njama nao ni wenye wivu na wenye kupenda kushindana; ni kila mtu na wake, na hawashirikiani hata kidogo. Je, mambo haya yote hayawakilishi kimo chenu cha kweli? Ninyi watu mnaohudumu pamoja kila siku ni kama Waisraeli, ambao kila siku walimhudumia Mungu Mwenyewe moja kwa moja hekaluni. Inawezekanaje kwamba ninyi watu, mnaomhudumia Mungu, hamjui jinsi ya kushirikiana ama jinsi ya kuhudumu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 462)

Matakwa mnayohitaji kutimiza leo—kufanya kazi pamoja kwa upatanifu—ni sawa na huduma ambayo Yehova alitaka kutoka kwa Waisraeli: Vinginevyo, acheni tu kufanya huduma. Kwa sababu ninyi ni watu wanaomhudumia Mungu moja kwa moja, angalau lazima muweze kuwa waaminifu na watiifu katika huduma yenu, na pia lazima muweze kupata mafunzo kwa njia ya utendaji. Kwa wale kati yenu wanaofanya kazi kanisani hasa, je, kuna yeyote kati ya akina ndugu walio chini yenu anayeweza kuthubutu kuwashughulikia? Je, mtu yeyote anaweza kuthubutu kuwaambia makosa yenu ana kwa ana? Mko juu ya wengine wote, mnatawala kama wafalme! Hata hamchunguzi ama kuingia katika mafunzo ya utendaji ya aina hii, lakini bado mnazungumza kuhusu kumhudumia Mungu! Kwa sasa, unaombwa uyaongoze makanisa kadhaa, lakini hukosi tu kujitolea, bali hata unashikilia mawazo na maoni yako mwenyewe, ukisema mambo kama, “Nadhani suala hili linapaswa kutendwa kwa namna hii, kwa kuwa Mungu amesema kwamba hatupaswi kuzuiliwa na wengine na kwamba siku hizi hatupaswi kutii bila kufikiria.” Kwa hivyo, kila mmoja wenu anashikilia maoni yake mwenyewe, na hakuna anayemtii mwenzake. Ingawa unajua vyema kwamba huduma yako ina shida kubwa, bado unasema, “Jinsi nionavyo, njia yangu ni sahihi kiasi. Haidhuru, kila mmoja wetu ana upande wake: Wewe zungumzia upande wako, nami nitazungumzia upande wangu; wewe shiriki kuhusu maono yako, nami nitazungumzia kuingia kwangu.” Kamwe huwajibikii mambo mengi ambayo yanapaswa kushughulikiwa, ama unaridhika tu, kila mmoja wenu akijadili maoni yake mwenyewe na kuilinda hadhi, sifa na heshima yake mwenyewe kwa uangalifu. Hakuna yeyote kati yenu aliye tayari kujinyenyekeza, na hakuna atakayechukua hatua ya kwanza kujitolea na kufidiana kasoro zenu ili maisha yasonge mbele upesi zaidi. Mnaposhirikiana pamoja, mnapaswa kujifunza kuutafuta ukweli. Unaweza kusema, “Sielewi vyema kuhusu kipengele hiki cha ukweli. Je, una uzoefu upi kuuhusu?” Ama unaweza kusema, “Una uzoefu mwingi kuniliko kuhusu kipengele hiki; tafadhali unaweza kuniongoza kiasi?” Je, hiyo haitakuwa njia nzuri ya kulitatua? Mmesikiliza mahubiri mengi, na mna uzoefu kiasi kuhusu kufanya huduma. Msipojifunza kutoka kwa kila mmoja, msaidiane, na kufidiana dosari zenu mnapofanya kazi makanisani, basi mnawezaje kupata mafunzo yoyote? Wakati wowote mnapokabiliwa na chochote, mnapaswa kufanya ushirika ninyi kwa ninyi ili maisha yenu yaweze kufaidika. Aidha, mnapaswa kufanya ushirika kwa makini kuhusu mambo ya aina yoyote kabla kufanya maamuzi yoyote. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo mnawajibikia kanisa badala ya kutenda kwa uzembe tu. Baada ya kutembelea makanisa yote, mnapaswa kukusanyika pamoja na kushiriki kuhusu masuala yote mnayogundua na matatizo yoyote mliyokumbana nayo katika kazi yenu, na kisha mnapaswa kuwasiliana kuhusu nuru na mwangaza ambao mmepokea—huu ni utendaji wa msingi wa huduma. Lazima mfanikishe ushirikiano wa upatanifu kwa ajili ya kazi ya Mungu, kwa manufaa ya kanisa, na ili muwahimize ndugu zenu mbele. Mnapaswa kushirikiana, kila mmoja akimrekebisha mwenzake na kufikia matokeo bora ya kazi, ili kuyatunza mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo maana ya ushirikiano wa kweli, na ni wale tu wanaoshiriki katika ushirikiano huo ndio watakaopata kuingia kwa kweli. Mnaposhirikiana, baadhi ya maneno mnayozungumza yanaweza kuwa yasiyofaa, lakini hilo si muhimu. Shirikini kulihusu baadaye, na mlielewe vyema; msilipuuze. Baada ya ushirika wa aina hii, mnaweza kufidia kasoro za ndugu zenu. Ni kwa kusonga kwa kina daima katika kazi yenu kwa namna hii ndipo mnaweza kupata matokeo bora. Kama watu wanaomhudumia Mungu, kila mmoja wenu lazima aweze kulinda maslahi ya kanisa katika kila kitu mnachofanya, badala ya kuzingatia tu masilahi yenu wenyewe. Haikubaliki ninyi kutenda kila mtu peke yake, daima mkidhoofishana. Watu wanaotenda kwa namna hiyo hawafai kumhudumia Mungu! Watu kama hao wana tabia mbaya sana; hawana ubinadamu hata kidogo ndani yao. Wao ni Shetani asilimia mia moja! Wao ni wanyama! Hata sasa, mambo kama haya bado hutokea miongoni mwenu; hata mnafika kiasi cha kushambuliana wakati wa ushirika; mkitafuta visingizio kwa makusudi na kughadhabika sana mnapogombana kuhusu suala fulani lisilo la maana, pasiwe na mtu aliye radhi kujiweka kando, kila mtu akimfichia mwenzake fikira zake za ndani, akimtazama yule mwingine kwa makini na kuwa mwangalifu daima. Je, tabia ya aina hii inafaa katika kumhudumia Mungu? Je, kazi kama hiyo yako inaweza kuwapa ndugu zako chochote? Huwezi tu kuwaongoza watu kwenye njia sahihi ya maisha, lakini kwa kweli unawajaza ndugu zako tabia zako potovu. Je, huwadhuru wengine? Dhamiri yako ni mbaya na ni mbovu kabisa! Huingii katika uhalisi, wala huuweki ukweli katika vitendo. Aidha, unawafichulia wengine asili yako mbaya mno bila aibu. Huna aibu hata kidogo! Umeaminiwa ndugu hawa, lakini unawapeleka kuzimuni. Je, wewe si mtu ambaye dhamiri yake imekuwa mbovu? Huna aibu hata kidogo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 463)

Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo kwa njia inayofaa? Je, wewe unayepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho unaweza kueleza tabia ya Mungu yenye haki kwa utondoti? Je, unaweza kushuhudia kuhusu tabia ya Mungu kwa uwazi na usahihi? Utawezaje kupitisha kile ambacho umeona na kupitia kupitia kwa maskini hawa wa kuhurumiwa, na waumini wa kidini wa kumcha Mungu waliojitolea na waliojawa na njaa na kiu ya haki na wanaongoja uwe mchungaji wao? Ni watu wa aina gani ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Unaweza kuwaza kweli? Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? Utahudumu vipi kama kiongozi mzuri wa wakati unaofuata? Je, unao hisia nzuri ya uongozi? Utaeleza mkuu wa kila kitu kama nini? Je, ni mkuu wa kila kitu kilicho hai na viumbe vyote duniani? Una mipango ipi ya kuendelea kwa hatua inayofuata ya kazi? Ni watu wangapi ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Je, jukumu lako ni nzito? Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, “Njia iko wapi?” Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia, ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 464)

Binadamu anayo imani Kwangu Mimi lakini hawezi kunitolea ushuhuda Mimi; kabla ya Mimi Mwenyewe kujitambulisha, binadamu hawezi kunitolea ushuhuda Mimi. Binadamu anaona tu kwamba Mimi ninazidi viumbe na binadamu wote wengine watakatifu, na anaona kwamba kazi ninayofanya haiwezi kufanywa na binadamu wengine. Kwa hivyo, kuanzia kwa Wayahudi hadi kwa binadamu wa siku ya leo, yeyote ambaye ameyaona matendo Yangu yenye utukufu anajawa tu na uchu wa kudadisi mengi kuhusu Mimi, ilhali hakuna kinywa cha kiumbe kimoja ambacho kingeweza kunitolea ushuhuda. Baba Yangu tu ndiye Aliyenitolea ushuhuda Mimi; Alinitengenezea njia Mimi miongoni mwa viumbe vyote. Kwani, haijalishi ni namna gani Nilivyofanya kazi, binadamu asingewahi kujua Mimi ndimi Bwana wa viumbe, binadamu anajua tu kuchukua, na hajui kuwa na imani ndani Yangu Mimi kwa sababu ya kazi Yangu Mimi. Binadamu ananijua Mimi tu kwa sababu Mimi sina hatia wala si mtenda dhambi kwa vyovyote vile, kwa sababu Ninaweza kufafanua mafumbo mengi, kwa sababu Mimi niko juu ya wengine wote, au kwa sababu binadamu amefaidi pakubwa kutoka Kwangu. Ilhali wachache ndio wanaoamini kwamba Mimi ndimi Bwana wa viumbe. Hii ndiyo maana Ninasema ya kwamba binadamu hajui ni kwa nini anayo imani Kwangu mimi; hajui kusudio au umuhimu wa kuwa na imani Kwangu mimi. Uhalisia wa binadamu umekosekana, kiasi cha kwamba karibu hana thamani tena ya kuweza kunitolea ushuhuda Mimi. Unayo imani ya kweli ndogo sana na umefaidi kidogo sana, kwa hivyo una ushuhuda mdogo. Aidha, unaelewa mambo machache sana na unapungukiwa na mambo mengi sana kiasi kwamba hufai kushuhudia matendo Yangu. Azimio lako kwa hakika linaeleweka, lakini je una hakika kwamba utaweza kunitolea ushuhuda kwa ufanisi kuhusu hali halisi ya Mungu? Kile ambacho umepitia na kuona kinazidi kile ambacho watakatifu na manabii wengine wa awali walivyoshuhudia, lakini je unaweza kutoa ushuhuda mkubwa zaidi kuliko maneno ya hawa watakatifu na manabii waliotangulia? Kile Ninachokupa wewe sasa kinazidi kile Nilichompa Musa na ni kikubwa zaidi kuliko kile nilichompa Daudi, kwa hivyo vilevile Ninakuomba ushuhuda wako uzidi ule wa Musa na kwamba maneno yako yawe makubwa zaidi kuliko yale ya Daudi. Ninakupa vyote hivi mara mia moja, kwa hivyo vilevile ninakuomba nawe unilipe tena vivyo hivyo. Lazima ujue kwamba Mimi Ndimi ninayempa maisha mwanadamu, na kwamba wewe ndiwe unayepokea maisha kutoka Kwangu na lazima unitolee ushuhuda Mimi. Huu ndio wajibu wako, ambao Ninashusha kwako na ambao unastahili kunifanyia Mimi. Nimekupa utukufu Wangu wote, na kukupatia maisha ambayo watu wateule, Waisraeli, hawakuwahi kupokea. Bila kukosea, unastahili kunitolea ushuhuda, na kuutoa ujana wako kwa ajili Yangu na kuyatoa maisha yako. Yeyote yule ninayempa Mimi utukufu Wangu ataweza kunitolea Mimi ushuhuda na kunipatia maisha yake. Haya yote yametabiriwa mapema. Ni utajiri wako wewe ambao Ninawekea utukufu Wangu kwako wewe na wajibu wako ni kuutolea ushuhuda utukufu Wangu. Kama unaniamini tu Mimi ili kupata utajiri, basi kazi Yangu haitakuwa yenye umuhimu, na hutakuwa unatimiza wajibu wako. Waisraeli waliona tu huruma Yangu, upendo Wangu na ukubwa Wangu nao Wayahudi walitoa tu ushuhuda wa subira Yangu na ukombozi Wangu. Waliona kazi kidogo sana ya Roho Yangu; huenda ikawa kwamba kiwango chao cha uelewa kilikuwa sehemu ndogo sana ya ile ambayo wewe umesikia na kuona. Kile ulichoona kinazidi hata kile ambacho makuhani wakuu waliona miongoni mwao. Siku hii, ukweli ambao umeelewa umezidi wao; kile ambacho umeona siku hii kinazidi kile kilichoonwa kwenye Enzi ya Sheria pamoja na Enzi ya Neema na kile ambacho umepitia kinazidi hata kile ambacho Musa na Eliya walipitia. Kile ambacho Waisraeli walielewa kilikuwa tu sheria ya Yehova na kile ambacho waliona kilikuwa tu ni mgongo wake Yehova; kile ambacho Wayahudi walielewa kilikuwa tu ukombozi wa Yesu, kile walichopokea kilikuwa neema waliyowekewa na Yesu, na kile walichoona kilikuwa ni taswira ya Yesu ndani ya nyumba ya Wayahudi. Kile utakachoona siku hii ni utukufu wa Yehova, ukombozi wa Yesu na matendo Yangu yote ya siku hii. Umesikia pia maneno ya Roho Yangu, hekima Yangu teule, na ukaja kujua kuhusu maajabu Yangu, na umeweza kujifunza kuhusu tabia Yangu. Nimeweza pia kukuambia kuhusu mpango Wangu wa usimamizi. Kile ambacho umeona si tu Mungu mwenye upendo na huruma, lakini yule aliyejawa na haki. Umeiona kazi Yangu ya maajabu na kujua kwamba Nimejawa na hasira na adhama. Aidha, umejua kwamba Niliwahi kuzishusha hasira Zangu katika nyumba ya Israeli, na kwamba leo hii, umeshushiwa wewe. Umeelewa zaidi kuhusu mafumbo Yangu kule mbinguni kuliko vile alivyoelewa Isaya pamoja na Yohana; unajua zaidi kuhusu uzuri Wangu na kustahiwa Kwangu kuliko watakatifu wote wa vizazi vilivyotangulia. Kile ulichopokea si ukweli Wangu tu, njia Yangu, maisha Yangu, lakini maono na ufunuo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vile vya Yohana. Umeelewa mafumbo mengine mengi zaidi na pia umeona sura Yangu kamili; umekubali mengi kuhusu hukumu Yangu na tabia Yangu ya haki. Kwa hivyo, ingawaje ulizaliwa kwenye siku za mwisho, uelewa wako ni ule wa siku za awali na za kale; umeweza pia kupitia ni nini kilichomo kwenye siku hii, na kile kilichotimizwa na mkono Wangu. Kile Ninachokuomba kinawezekana, kwani kile Nilichokupa ni kingi mno na ni mengi ambayo umeona Kwangu mimi. Kwa hivyo, Ninakuomba kunishuhudia Mimi kama vile watakatifu wa awali walivyofanya na hili ndilo tamanio tu la moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 465)

Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu. Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu. Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yaani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote. Kwa hiyo unastahili kujua namna ya kunitosheleza Mimi sasa na namna unavyostahili kuwa kwenye njia iliyo sawa katika imani yako Kwangu. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwingine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili katika wakati ujao na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, lazima bado Nikuambie: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 466)

Ijapokuwa imani yenu ni ya kweli kabisa, hakuna kati yenu anayeweza kueleza kunihusu kabisa, na hakuna kati yenu anayeweza kushuhudia uhalisi mnaouona. Tafakari kuhusu jambo hili. Sasa hivi wengi wenu hamyatimizi wajibu wenu, mkifuata vitu vya mwili, mkishibisha mwili na kuburudika kwa mwili. Mnamiliki ukweli mdogo. Mnawezaje basi kushuhudia yote ambayo mmeyaona? Mna uhakika kuwa mtakuwa mashahidi Wangu? Iwapo siku moja utashindwa kushuhudia yote ambayo umeyaona leo, basi utakuwa umepoteza jukumu la kiumbe aliyeumbwa. Hakutakuwa na maana kabisa ya kuwepo kwako. Utakuwa hustahili kuwa binadamu. Mtu anaweza hata kusema kuwa wewe si binadamu! Nimefanya kazi isiyo na kifani kwako. Lakini kwa sababu kwa sasa hujifunzi chochote, hujui chochote, na kufanya kazi bure, Nikitaka kuipanua kazi Yangu utatazama bila kuelewa, bila kusema chochote na kuwa asiye na umuhimu wowote. Hiyo haitakufanya mtenda dhambi mkubwa zaidi? Wakati huo utakapofika, je, hutakuwa na majuto makuu? Hutazama katika huzuni kubwa? Sifanyi kazi hii yote sasa kwa sababu ya kukosa la kufanya na uchoshi, bali kuweka msingi kwa kazi Yangu ya baadaye. Sio kwamba Niko katika njia isiyopitika na Nahitajika kubuni kitu kipya. Unafaa kuelewa kazi ambayo Nafanya; si kitu kinachofanywa na mtoto anayecheza mtaani, bali ni kwa uwakilishi wa Baba Yangu. Unafaa kujua kuwa si Mimi tu Ninayefanya haya yote pekee Yangu bali Namwakilisha Baba Yangu. Wakati uo huo, jukumu lako ni kufuata, kuheshimu, kubadilika, na kushuhudia kwa makini. Unachofaa kuelewa ni kwa nini unafaa kuniamini. Hili ndilo swali muhimu kwa kila mmoja wenu kuelewa. Baba Yangu, kwa ajili ya utukufu Wake, ndiye Aliyewachagua ninyi kwa ajili Yangu kutoka wakati Alipoumba dunia. Haikuwa kwa ajili ya kitu kingine ila kwa ajili ya kazi Yangu na kwa ajili ya utukufu Wake, ndio maana Aliweka hatima yenu awali. Ni kwa sababu ya Baba Yangu ndio unaniamini; ni kwa sababu ya Baba Yangu kukuamua kabla ndio maana unanifuata Mimi. Hakuna kati ya haya ambayo ulichagua kwa hiari yako mwenyewe. La muhimu zaidi ni kwamba muelewe kuwa ninyi ni wale ambao Baba Yangu alinitawazia kwa ajili ya kushuhudia kwa niaba Yangu. Kwa sababu Aliwatawaza Kwangu, mnafaa kuzifuata njia ambazo Natawaza kwenu na njia na maneno ambayo Ninawafunza, kwani ni jukumu lenu kuzifuata njia Zangu. Hili ndilo kusudi la asili la imani yenu Kwangu. Kwa hivyo Nawaambieni, ninyi ni watu tu ambao Baba Yangu Alitawaza Kwangu ili mfuate njia Zangu. Hata hivyo, mnaamini tu Kwangu; ninyi si wa Kwangu kwa sababu ninyi si wa familia ya Wayahudi bali ni wa joka la zama. Kile Ninachowasihi ni muwe washahidi Wangu, lakini leo lazima mtembee kwa njia Zangu. Haya yote ni kwa ajili ya ushuhuda wa baadaye. Mkihudumu tu kama watu ambao wanasikiliza njia Zangu pekee, basi hamtakuwa na thamani yoyote na umuhimu wa Baba Yangu kuwatawaza Kwangu utapotea. Ninachosisitiza kuwaambia ni hiki: Mnapaswa kutembea katika njia Zangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 467)

Roho Mtakatifu Anafanya kazi vipi katika kanisa sasa? Je, una ufahamu wa hilo? Ni matatizo gani makubwa zaidi yanayowakumba ndugu na dada? Wamepungukiwa na nini zaidi? Kwa sasa, kuna watu ambao wako hasi katikati ya majaribio, na wengine wao hata wanalalamika, na wengine hawasongi mbele tena kwa sababu Mungu Hazungumzi tena. Watu hawajaingia njia sahihi ya imani katika Mungu. Hawawezi kuishi wakijitegemea, na hawezi kudumisha maisha yao ya kiroho. Kuna watu wengine ambao wanafuata, wanaofuatilia kwa nguvu, na wako tayari kutenda Mungu Akinena. Lakini Mungu Asiponena, hawasongi mbele tena. Watu bado hawajaelewa mapenzi ya Mungu katika mioyo yao na hawana mapenzi kwa Mungu moja kwa moja; kufuata kwao Mungu hapo awali ilikuwa kwa sababu walikuwa wamelazimishwa. Sasa kuna watu ambao wamechoka na kazi ya Mungu. Je, hawako hatarini? Watu wengi wako katika hali ya kuvumilia tu. Ingawa wanakula na kunywa maneno ya Mungu na kumuomba, yote ni kwa kusitasita. Hawana bidii waliyokuwa nayo mwanzoni, na watu wengi hawana shauku katika kazi ya Mungu ya uboreshaji na ukamilisho. Ni kana kwamba hawana bidii ya ndani kamwe, na wanalemewa na maasi hawahisi kuwa wana deni kwa Mungu, wala hawajuti wenyewe. Hawaufuatilii ukweli ama kuondoka kanisani. Wanafuata tu raha za muda. Huyu ni aina ya mjinga mkuu wa kipumbavu! Wakati utakapofika, wote watatupwa nje, na hakuna mmoja atakayeokolewa! Je, unafikiri kuwa kama mtu ameokolewa mara moja ataokolewa kila wakati? Hii ni kujaribu tu kuwapumbaza watu! Wale wote wasiofuata kuingia katika maisha wataadibiwa. Watu wengi hawana shauku hata kidogo ya kuingia katika maisha, katika maono, ama kuweka ukweli katika matendo. Hawafuati kuingia ndani, na kwa hakika hawafuati kuingia ndani zaidi. Je, hawajiangamizi wenyewe? Wakati huu, kuna sehemu ya watu ambao hali zao zinaendelea kuwa nzuri na nzuri zaidi. Roho Mtakatifu Anapofanya kazi zaidi, wanajiamini zaidi, na wanapozoea zaidi ndipo wanapohisi siri ya kushangaza ya kazi ya Mungu. Wanapoingia ndani zaidi, ndipo wanaelewa zaidi. Wanahisi kuwa upendo wa Mungu ni mkubwa sana, na wanahisi imara na kupata nuru ndani. Wana uelewa wa kazi ya Mungu. Hawa ni watu ambao Roho Mtakatifu Anafanya kazi ndani yao. Watu wengine wanasema, “Ingawa hakuna maneno mapya kutoka kwa Mungu, lazima bado niendelee kuingia ndani katika ukweli, lazima niwe na bidii katika kila kitu katika mazoea yangu na kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu.” Mtu kama huyu ana kazi ya Roho Mtakatifu. Ingawa Mungu Haonyeshi uso Wake na Amejifichika kutoka kwa kila mtu, na Haneni neno lolote, na kuna nyakati ambazo watu wanapitia usafishaji wa ndani, ilhali Mungu hajawaacha watu Wake kabisa. Kama mtu hawezi kudumisha ukweli ambao anafaa kutekeleza, hatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika wakati wa usafishaji, wa Mungu kutojionyesha, kama hujiamini na unaogopa, usipo lenga kuwa na uzoefu wa maneno Yake, hii ni kutoroka kutoka kwa kazi ya Mungu. Baadaye, utatupwa nje. Wale ambao hawatafuti kuingia katika neno la Mungu hawana uwezo wa kusimama kama shahidi Wake. Watu ambao wanaweza kutoa ushahidi kwa Mungu na kuridhisha mapenzi Yake wote wanategemea kikamilifu bidii yao kufuatilia maneno ya Mungu. Kazi ambayo Mungu Anaitekeleza katika watu ni kimsingi kuwawezesha kuupata ukweli; Kukufanya wewe kufuatilia maisha ni kwa ajili ya kukukamilisha, na yote ni ya kukufanya ufae kutumika na Mungu. Yote unayofuata sasa ni kusikia siri, kusikiliza maneno ya Mungu, kulisha macho yako, kuona kitu kipya ama kuona ni mwenendo upi, na kuridhisha udadisi wako. Kama hii ndio nia ya moyo wako, hakuna vile utafikia mahitaji ya Mungu. Wale ambao hawafuati ukweli hawezi kufuata mpaka mwisho kabisa. Wakati huu, si kwamba Mungu hafanyi kitu—ni kwamba watu hawashirikiani, kwa sababu wamechoka na kazi Yake. Wanataka tu kusikia maneno ya baraka Yake, na hawataki kusikia maneno ya hukumu Yake na kuadibiwa. Sababu ya hii ni nini? Ni kwa sababu tamaa ya watu kupata baraka haijatimizwa, na wako hasi na wanyonge. Si kwamba Mungu kimakusudi hakubali watu kumfuata, na si kwamba anapeana mapigo kimakusudi kwa wanadamu. Watu wako hasi na wanyonge kwa sababu nia zao hazifai. Mungu ni Mungu Ambaye Anampa mwanadamu maisha, naye hawezi kumleta mwanadamu katika kifo. Uhasi wa watu, unyonge na kurudi nyuma yote yanasababishwa na wao wenyewe.

Kazi ya Mungu ya sasa inawaletea watu usafishaji kiasi, na wale tu ambao wanaweza kusimama imara katika usafishaji huu watapata kibali cha Mungu. Haijalishi ni jinsi gani Anajificha, bila kuongea, ama kufanya kazi, bado unaweza kufuata kwa bidii. Hata kama Mungu Alisema angekukataa, bado ungemfuata Yeye. Hii ni kusimama kama shahidi kwa Mungu. Mungu Akijificha kutoka kwako nawe ukome kumfuata, hii ni kusimama shahidi kwa Mungu? Watu wasipoingia ndani kwa kweli, hawana kimo cha kweli, na wanapokabiliana na jaribio kubwa hasa, wanaanguka. Mungu Haneni kwa sasa, ama kile Afanyacho hakilingani na dhana zako, kwa hivyo hauko sawa. Kama Mungu angekuwa sasa anatenda kulingana na dhana zako kwa sasa, kama Angekuwa anayakidhi matakwa yako na ukawa na uwezo wa kusimama na kufuatilia kwa nguvu, basi ni nini ambacho kweli ungekuwa unatumia kuendelea kuishi? Nasema kuwa kuna watu wengi ambao wanaishi wakitegemea kabisa udadisi wa binadamu. Hawana kabisa moyo wa kweli wa kufuata. Wale wote wasiofuata kuingia katika ukweli lakini wanategemea udadisi wao katika maisha ni watu wenye kustahili dharau walio hatarini! Kazi za Mungu tofauti yote ni ya kuwakamilisha wanadamu. Hata hivyo, watu daima ni wadadisi, wanapenda kuuliza kuhusu tetesi, wana wasiwasi kuhusu kinacho endelea nje ya nchi—ni nini kinaendelea Israeli, kama kuna mtetemeko wa ardhi Misri—kila wakati wanatafuta kitu mpya, kitu kisicho cha kawaida kuridhisha tamaa zao za kibinafsi. Hawafuati maisha, wala kufuata kukamilishwa. Wanatafuta tu siku ya Mungu kufika haraka ili ndoto yao nzuri ijulikane na tamaa zao badhirifu zitimie. Mtu kama huyo si wa kweli—ni mtu aliye na mtazamo usio sawa. Kuufuata ukweli ni msingi wa imani ya wanadamu katika Mungu. Watu wasipofuata kuingia katika maisha, wasipotafuta kumridhisha Mungu, basi watatiishwa chini ya adhabu. Wale watakaoadhibiwa ni wale ambao hawajakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu katika wakati wa kazi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 468)

Watu wanafaa kushirikiana na Mungu vipi katika hatua hii ya kazi Yake? Mungu Anawajaribu watu kwa wakati huu. Haneni neno lolote; Anajificha na Hawasiliani na watu moja kwa moja. Kutoka nje, inaonekana kama Hafanyi kazi, lakini ukweli ni kwamba bado Anafanya kazi ndani ya mwanadamu. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ana maono kwa kufuata kwake maisha, na hana mashaka, hata kama haelewi kazi ya Mungu kikamilifu. Katikati ya majaribu, hata kama hajui ni nini Mungu Anataka kufanya na kazi gani Anataka kukamilisha, unafaa kujua kuwa nia za Mungu kwa wanadamu ni nzuri kila wakati. Ukimfuata na moyo wa kweli, Hatawahi kukuacha, na mwishowe kwa kweli Atakukamilisha, na kuwaleta watu katika mwisho unaofaa. Haijalishi ni vipi Mungu Anawajaribu watu kwa sasa, kuna siku moja ambayo Atawatolea watu matokeo yanayofaa na kuwapa adhabu inayofaa kulingana na kile ambacho wamefanya. Mungu Hatawaongoza watu hadi kituo fulani halafu Awatupe tu kando na kuwapuuza. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwaminifu. Katika hatua hii, Roho Mtakatifu anafanya kazi ya usafishaji. Anamsafisha kila mmoja. Katika hatua za kazi zilizoundwa na majaribu ya kifo na majaribu ya kuadibu, usafishaji katika wakati huo ulikuwa usafishaji kupitia maneno. Ili watu wapate uzoefu wa kazi ya Mungu, lazima kwanza waelewe kazi Yake ya sasa na kuelewa jinsi wanadamu wanafaa kushirikiana. Hili ni jambo ambalo kila mtu anafaa kuelewa. Haijalishi ni nini Mungu Anafanya, kama ni usafishaji ama kama Haneni, kila hatua ya kazi ya Mungu hailingani na dhana za wanadamu. Yote yanaenda mbali na kupenya katika dhana za watu. Hii ni kazi Yake. Lakini lazima uamini kwamba, kwa kuwa kazi ya Mungu imefika hatua fulani, Hatakubali wanadamu wote waangamie hata iweje. Anawapa ahadi na baraka kwa wanadamu, na wale wote wanaomfuata wataweza kupata baraka Yake, na wale wasiomfuata watatupwa nje na Mungu. Hii inategemea kufuata kwako. Haijalishi chochote, lazima uamini kuwa wakati kazi ya Mungu itakapomalizika, kila mtu atakuwa na mwisho unaofaa. Mungu Amewapa wanadamu matamanio mazuri, lakini wasipofuatilia, hawawezi kuyapata. Unafaa kuweza kuona hii sasa—Mungu kusafisha na kuwaadibu watu ni kazi Yake, lakini kwa watu, lazima wafuate badiliko katika tabia kila wakati. Katika mazoea yako ya kivitendo, lazima kwanza ujue jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu; lazima upate kile unachofaa kuingia ndani na mapungufu yako ndani ya maneno Yake, utafute kuingia katika mazoea yako ya kivitendo, na uchukue sehemu ya kazi ya Mungu inayofaa kuwekwa katika matendo na ujaribu kuifanya. Kula na kunywa maneno ya Mungu ni kipengele kimoja, maisha ya kanisa lazima pia yadumishwe, lazima uwe na maisha ya kiroho ya kawaida, na uweze kumkabidhi Mungu hali zako zote za sasa. Haijalishi ni vipi kazi Yake inabadilika, maisha yako ya kiroho yanapaswa kubaki kawaida. Maisha ya kiroho yanaweza kudumisha kuingia ndani kwako kwa kawaida. Haijalishi kile ambacho Mungu Anafanya, unapaswa kuendeleza maisha yako ya kiroho bila kukatizwa na kutimiza wajibu wako. Hiki ndicho watu wanapaswa kufanya. Yote ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini huku kwa wale walio na hali ya kawaida huku ni kukamilishwa, kwa wale wasio na hali ya kawaida ni majaribu. Katika hatua ya sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu ya kusafisha, watu wengine wanasema kuwa kazi ya Mungu ni kubwa sana na kwamba watu wanahitaji sana usafishaji, vinginevyo kimo chao kitakuwa ndogo sana na hawatakuwa na njia ya kufikia mapenzi ya Mungu. Hata hivyo, kwa wale walio na hali isiyo nzuri, inakuwa sababu ya kutomfuata Mungu, na sababu ya kutohudhuria mikusanyiko ama kula na kunywa neno la Mungu. Katika kazi ya Mungu, haijalishi ni nini Anafanya ama nini kinabadilika, kwa uchache sana watu lazima watu wadumishe hali ya chini zaidi ya maisha ya kawaida ya kiroho. Pengine umekuwa mwangalifu katika hatua hii ya sasa ya maisha yako ya kiroho, lakini bado hujapata mengi; hujavuna pakubwa. Katika hali za aina hizi lazima bado ufuate sheria; lazima ufuate sheria hizi ili usipate hasara katika maisha yako na ili uyakidhi mapenzi ya Mungu. Kama maisha yako ya kiroho si ya kawaida, huwezi kuelewa kazi ya sasa ya Mungu, badala yake kila wakati utahisi kwamba hayalingani kabisa na dhana zako mwenyewe, nawe una hiari ya kumfuata, lakini unakosa bidii ya ndani. Kwa hivyo haijalishi ni nini Mungu Anafanya sasa, lazima watu washirikiane. Watu wasiposhirikiana Roho Mtakatifu Hawezi kufanya kazi Yake, na kama watu hawana moyo wa kushirikiana, basi si rahisi wao kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Kama unataka kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani mwako, na kutaka kupata kibali cha Mungu, lazima udumishe moyo wako wa ibada asili mbele ya Mungu. Sasa, si lazima kwako kuwa na maelewano zaidi ya ndani, nadharia ya juu, ama vitu vingi—yote yanayohitajika ni kwamba ushikilie neno la Mungu juu ya msingi asili. Watu wasiposhirikiana na Mungu na wasipofuata kuingia zaidi, Mungu Atachukua kile walichokuwa nacho wakati mmoja. Ndani, watu wana tamaa kila wakati ya kilicho rahisi na afadhali wajifurahishe na kile ambacho kinapatikana. Wanataka kupata ahadi za Mungu bila kulipa gharama yoyote. Haya ni mawazo badhirifu ndani ya wanadamu. Kupata maisha yenyewe bila kulipa gharama—nini kimewahi kuwa rahisi? Mtu anapoamini katika Mungu na kutafuta kuingia katika maisha na kutafuta badiliko katika tabia yake, ni lazima alipe gharama na kufikia kiwango ambapo atamfuata Mungu daima bila kujali Anachofanya. Hiki ni kitu ambacho watu lazima wafanye. Hata kama unafuata haya yote kama sharti, ni lazima uyazingatie, na haijalishi majaribu yako ni makubwa kiasi gani, huwezi kuachilia uhusiano wako wa kufaa na Mungu. Unapaswa kuweza kuomba, udumishe maisha yako ya kanisa, na uishi na ndugu na dada. Mungu anapokujaribu, bado unapaswa kutafuta ukweli. Hiki ndicho kiwango cha chini cha maisha ya kiroho. Daima kuwa na moyo wa kutafuta na kujitahidi kushirikiana, kutumia nguvu zako zote—Je, hili linaweza kufanywa? Kwa msingi huu, utambuzi na kuingia katika uhalisi kitakuwa kitu ambacho unaweza kufanikisha. Ni rahisi kulikubali neno la Mungu wakati hali yako mwenyewe iko kawaida, na huhisi ugumu katika kuuweka ukweli katika matendo, na unahisi kuwa kazi ya Mungu ni kuu. Lakini kama hali yako ni duni, haijalishi kazi ya Mungu ni kuu vipi na haijalishi mtu anazungumza vizuri kivipi, hutasikiza chochote. Wakati hali ya mtu si ya kawaida, Mungu hawezi kufanya kazi ndani yao, na hawawezi kufanikisha mabadiliko katika tabia zao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 469)

Kama watu hawana imani yoyote, sio rahisi kuendelea katika njia hii. Kila mtu sasa anaweza kuona kuwa kazi ya Mungu hailingani hata kidogo na fikira za watu. Mungu amefanya kazi nyingi sana na kuzungumza maneno mengi sana, ambayo hayalingani kabisa na dhana za binadamu. Hivyo, lazima watu wajiamini na wawe na utashi kuweza kusimama na kile wameshakiona na kile wamepata kutoka kwa uzoefu wao. Haijalishi ni nini Mungu Anafanya kwa watu, lazima washikilie kile walicho nacho, wawe waaminifu mbele za Mungu, na wasalie wenye kujitolea Kwake hadi mwisho. Huu ni wajibu wa wanadamu. Lazima watu watetee kile wanachopaswa kufanya. Imani katika Mungu inahitaji utiifu Kwake na uzoefu wa kazi Yake. Mungu Amefanya kazi nyingi sana—inaweza semekana kuwa kwa watu yote ni kukamilishwa, yote ni usafishaji, na hata zaidi, yote ni kuadibu. Hakujakuwa na hatua hata moja ya kazi ya Mungu ambayo imelingana na dhana za binadamu; kile watu wamefurahia ni maneno makali ya Mungu. Mungu Atakapokuja, watu wanapaswa kufurahia enzi Yake na hasira Yake, lakini haijalishi maneno Yake yalivyo makali, Anakuja kuokoa na kukamilisha binadamu. Kama viumbe, watu wanapaswa watekeleze wajibu ambao wanafaa kufanya, na kusimama shahidi kwa Mungu katikati ya usafishaji. Katika kila jaribio wanapaswa washikilie ushahidi ambao wanapaswa washuhudie, na kushuhudia ushuhuda mkubwa kwa Mungu. Huyu ni mshindi. Haijalishi Mungu Anavyokuboresha, unabaki kuwa na imani kubwa na kutopoteza imani katika Mungu. Ufanye kile mwanadamu anafaa kufanya. Hiki ndicho Mungu Anahitaji kwa mwanadamu, na moyo wa binadamu unapaswa kuweza kurudi Kwake kikamilifu na kumwelekea katika kila wakati. Huyu ni mshindi. Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi. Kama kufuata kwako ni bora kabisa Mungu Anapokubariki, lakini unarudi nyuma bila baraka Zake, si huu ni utakaso? Kwa sababu una uhakika kuwa njia hii ni ya kweli, lazima uifuate hadi mwisho; lazima udumishe ibada yako kwa Mungu. Kwa sababu umeona kuwa Mungu Mwenyewe amekuja duniani kukukamilisha, lazima umpe moyo wako Kwake kabisa. Haijalishi ni nini Anafanya, hata kama Anaamua tokeo lisilofaa kwako mwishowe, bado unaweza kumfuata. Hii ni kudumisha usafi wako mbele za Mungu. Kupeana mwili wa kiroho mtakatifu na bikira safi kwa Mungu inamaanisha kuweka moyo mwaminifu mbele za Mungu. Kwa wanadamu, uaminifu ni usafi, na kuweza kuwa mwaminifu kwa Mungu ni kudumisha usafi. Hii ndiyo unafaa kuweka katika matendo. Unapopaswa kuomba, omba; unapopaswa kukusanyika pamoja katika ushirika, fanya hivyo; unapopaswa kuimba nyimbo za kidini, imba nyimbo za kidini; na unapopaswa kuunyima mwili, unyime mwili. Unapotekeleza wajibu wako hulimalizi kwa kubahatisha; unapokumbana na majaribu unasimama imara. Hii ni ibada kwa Mungu. Usiposhikilia kile ambacho watu wanapaswa kufanya, basi kuteseka kwako na maazimio ya hapo awali yalikuwa ya bure.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 470)

Kwa kila hatua ya kazi ya Mungu, kunayo njia ambayo watu wanapaswa washirikiane. Mungu Anawasafisha watu ili wawe na imani katikati ya usafishaji. Mungu Anawakamilisha watu ili wawe na imani ya kukamilishwa na Mungu na wako tayari kuukubali usafishaji Wake na kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Roho wa Mungu Anafanya kazi ndani ya watu ili kuwaletea nuru na mwangaza, na kuwafanya washirikiane Naye na kutenda. Mungu Haneni wakati wa usafishaji. Hatoi sauti Yake, lakini bado kuna kazi ambayo watu wanapaswa kuifanya. Unapaswa kushikilia kile ambacho unacho tayari, unapaswa bado kuwa na uwezo wa kumwomba Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kusimama shahidi mbele ya Mungu; hivi utatimiza wajibu wako mwenyewe. Nyinyi wote mnapaswa muone kwa dhahiri kutoka kwa kazi ya Mungu kuwa majaribu Yake ya imani ya watu na upendo inahitaji kuwa waombe zaidi kwa Mungu, na kwamba waonje maneno ya Mungu mbele Zake mara kwa mara. Mungu Akikupa nuru na kukufanya kuelewa mapenzi Yake lakini huyaweki katika matendo hata kidogo, hutapata chochote. Unapoyaweka maneno ya Mungu katika matendo, unapaswa bado kuwa na uwezo wa kumwomba, na unapoyaonja maneno Yake unapaswa utafute kila wakati mbele Zake na uwe umejaa imani Kwake bila kuvunjika moyo ama kuwa baridi. Wale wasioweka maneno ya Mungu katika matendo wamejawa na nguvu katika mikusanyiko, lakini wanaanguka katika giza wanaporudi nyumbani. Kuna wengine ambao hawataki hata kukusanyika pamoja. Kwa hivyo lazima uone kwa wazi ni wajibu gani ambao watu wanapaswa kutimiza. Unaweza kukosa kujua mapenzi ya Mungu ni nini hasa, lakini unaweza kutekeleza wajibu wako, unaweza kuomba inapopaswa, unaweza kuuweka ukweli katika matendo unapopaswa, na unaweza kufanya kile watu wanapaswa kufanya. Unaweza kushikilia maono yako asili. Hivi, utaweza kukubali zaidi hatua ya Mungu inayofuata. Ni shida ukikosa kutafuta wakati ambapo Mungu anafanya kazi katika njia iliyofichika. Anaponena na kuhubiri katika mabaraza, unasikiza kwa shauku, lakini Asiponena unakosa nguvu na kurudi nyuma. Mtu wa aina gani anafanya hivi? Huyu ni mtu ambaye tu anaenda na mkondo. Hana msimamo, hawana ushuhuda, na hawana maono! Watu wengi wako hivyo. Ukiendelea katika njia hiyo, siku moja utakapopitia jaribio kuu, utateremka katika adhabu. Kuwa na msimamo ni muhimu sana katika kukamilishwa kwa watu na Mungu. Kama huna shaka na hatua yoyote ya kazi ya Mungu, unatimiza wajibu ya mwanadamu, unashikilia kwa uaminifu kile Mungu Amekufanya ukiweke katika matendo, hiyo ni, unakumbuka mawaidha ya Mungu, na haijalishi Anachokifanya sasa husahau mawaidha Yake, huna shaka kuhusu kazi Yake, unadumisha msimamo wako, kushikilia ushahidi wako, na una ushindi katika kila hatua ya njia, mwishowe utakamilishwa kuwa mshindi na Mungu. Kama unaweza kusimama imara katika kila hatua ya majaribu ya Mungu, na bado unaweza kusimama imara hadi mwisho kabisa, wewe ni mshindi, na wewe ni mtu ambaye amekamilishwa na Mungu. Kama huwezi kusimama imara katika majaribu yako ya sasa, baadaye itakuwa hata vigumu zaidi. Ukipitia mateso kidogo yasiyo ya muhimu na usiufuate ukweli, hutapata chochote mwishowe. Utakuwa mkono mtupu. Kuna watu wengine ambao wanaacha kufuata wanapoona kuwa Mungu Haneni, na moyo wao unatawanyika. Je, si huyo ni mjinga? Watu wa aina hii hawana ukweli. Mungu Anenapo, wanakimbia huku na kule kila wakati, wakiwa na shughuli nyingi na kuwa na shauku kwa nje, lakini sasa Haneni, hawatafuti tena. Mtu kama huyu hana maisha ya usoni. Katika usafishaji, lazima uingie ndani kutoka kwa mtazamo halisi na usome masomo unayostahili kusoma; unapomwomba Mungu na kusoma neno Lake, unapaswa kulinganisha hali yako mwenyewe nayo, utambue pungufu zako, na ujue kuwa una somo mengi sana unayofaa kusoma. Unapotafuta kwa uaminifu katikati ya usafishaji, ndipo utakapojipata kuwa una pungufu. Unapokuwa unapitia usafishaji kunayo masuala mengi ambayo unapitia; hautayaona kwa wazi, unalalamika, unatambulisha mwili wako wenyewe—ni kwa njia hii pekee ndiyo unaweza kugundua kwamba una tabia nyingi sana potovu ndani yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 471)

Kazi ya Mungu katika siku za mwisho inahitaji imani kubwa—inahitaji imani kubwa zaidi hata kuliko ile ya Ayubu. Bila imani, watu hawataweza kuendelea kupata mazoea na hawataweza kukamilishwa na Mungu. Siku itakapokuja ambapo majaribu makuu yanakuja, watu wengine wataondoka kutoka kanisa hili, na wengine wataondoka kutoka kanisa lile. Kutakuwa na wengine ambao walikuwa wakifanya vizuri kiasi katika kufuata kwao katika siku za awali na haiko wazi mbona hawaamini tena. Vitu vingi vitafanyika na hutajua ni nini kinaendelea, na Mungu Hataonyesha dalili zozote ama ishara, ama kufanya chochote kisicho cha kawaida. Hii ni kuona kama unaweza kusimama imara—Mungu Anatumia ukweli kuwasafisha watu. Bado hujateseka sana. Hapo baadaye majaribu makuu yajapo, katika sehemu zingine kila mtu katika kanisa ataondoka, na wale umesikizana nao vizuri sana wataondoka na kuiacha imani yao. Utaweza kusimama imara wakati huo? Sasa, yale majaribu umepitia yamekuwa madogo, na pengine imekuwa vigumu kuyahimili. Hatua hii inajumuisha usafishaji na kukamilishwa kupitia neno pekee. Katika hatua inayofuata, ukweli utakuja juu yako kukusafisha, halafu utakuwa katikati ya hatari. Inapokuwa kubwa sana, Mungu Atakushauri uharakishe na uondoke, na watu wa kidini watajaribu kukushawishi ujiunge. Hii ni ili kuona kama unaweza kuendelea katika njia hiyo. Haya yote ni majaribu. Majaribu ya sasa ni madogo, lakini siku itakuja ambapo kunao wazazi nyumbani ambao hawaamini tena na kunao watoto nyumbani ambao hawaamini tena. Je, utaweza kuendelea mbele? Unapoenda mbele zaidi, ndivyo majaribu yako yanakuwa mengi zaidi. Mtu Anatekeleza kazi Yake ya kuwasafisha watu kulingana na mahitaji yao na kimo chao. Katika hatua ya Mungu kuwakamilisha wanadamu, haiwezekani kuwa idadi ya watu itaendelea kukua—itapunguka tu. Ni kwa kupitia usafishaji huu tu ndipo watu wataweza kukamilishwa. Kushughulikiwa, kuadhibiwa, kujaribiwa, kuadibiwa, kulaaniwa—ndipo unaweza kustahimili haya yote? Unapoona kanisa lililo na hali nzuri hasa, ndugu na dada wote wanatafuta kwa nguvu kubwa, wewe mwenyewe unahisi umetiwa moyo. Siku ikija ambapo wote wameondoka, wengine wao hawaamini tena, wengine wameondoka kufanya biashara ama kuolewa, na wengine wamejiunga na dini, utaweza kusimama imara wakati huo? Je, utaweza kubaki bila mabadiliko ndani? Kukamilishwa kwa wanadamu kwa Mungu siyo jambo rahisi! Anatumia vitu vingi kuwasafisha watu. Watu wanaona haya kama mbinu, lakini kwa nia asili ya Mungu hizi sizo mbinu hata kidogo, ila ni ukweli. Mwishowe, Atakapokuwa Amewasafisha watu kufikia kiwango fulani na hawana malalamishi yoyote tena, hatua hii ya kazi Yake itakuwa imekamilika. Kazi kuu ya Roho Mtakatifu ni kukukamilisha, na wakati ambapo Hafanyi kazi na Anajificha, hata zaidi ni kwa sababu ya kukukamilisha, na hivi inaweza kuonekana hasa kama watu wana upendo kwa Mungu, na kama wana imani ya kweli Kwake. Mungu Anaponena wazi, hakuna haja ya wewe kutafuta; ni wakati tu ambapo Amejificha ndipo unahitaji kutafuta, unahitaji kuhisi njia yako hadi upite. Unapaswa kuweza kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa, na haijalishi matokeo yako ya usoni na hatima yako inaweza kuwa ipi, unapaswa kuweza kufuatilia maarifa na upendo kwa Mungu katika miaka ambayo uko hai, na haijalishi jinsi Mungu anavyokutendea, unapaswa kuweza kuepuka kulalamika. Kuna sharti moja kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya watu. Bora wana hamu na wanatafuta na hawasitisiti ama kuwa na shaka kuhusu matendo ya Mungu, nao wanaweza kushikilia wajibu wao kila wakati, hivi tu ndivyo wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila hatua ya kazi ya Mungu, kinachohitajika kwa wanadamu ni imani kuu na kutafuta mbele za Mungu—kupitia tu kwa mazoea ndipo watu wataweza kugundua jinsi Mungu Anavyopendeka na jinsi Roho Mtakatifu Anavyofanya kazi ndani ya watu. Usipopata uzoefu, usipoihisi njia yako kupitia hayo, usipotafuta, hutapata chochote. Lazima uhisi njia yako kupitia mazoea yako, na kwa kupitia mazoea yako tu ndipo utaona matendo ya Mungu, na kugundua maajabu Yake na mambo Yake yasiyoeleweka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 473)

Lazima ukumbuke kwamba maneno haya sasa yamenenwa: Baadaye, utapitia dhiki kubwa na mateso makubwa! Kukamilishwa silo jambo rahisi au jepesi. Angalau lazima uwe na imani ya Ayubu, au hata labda imani kubwa kuliko yake. Unapaswa kujua kwamba majaribu katika siku zijazo yatakuwa makubwa kuliko majaribu ya Ayubu, na kwamba lazima bado upitie kuadibu kwa muda mrefu. Je, hili ni jambo rahisi? Ikiwa ubora wa tabia yako hauwezi kuboreshwa, ikiwa uwezo wako wa kuelewa umepungukiwa, na ikiwa unajua kidogo sana, basi wakati huo hutakuwa na ushuhuda wowote, lakini badala yake utakuwa kichekesho, kitu cha Shetani kuchezea. Ikiwa huwezi kushikilia maono sasa, basi huna msingi hata kidogo na katika siku zijazo utatupwa! Hakuna sehemu ya njia ambayo ni rahisi kutembea, kwa hivyo usiichukulie kwa urahisi. Lipime hili kwa uangalifu sasa na ufanye maandalizi ili uweze kuitembea vizuri sehemu ya mwisho ya njia hii. Hii ndiyo njia ambayo lazima itembewe katika siku zijazo, njia ambayo lazima watu wote waitembee. Lazima usikose kusikiliza maarifa haya; usifikirie kuwa kile Ninachokuambia si chote cha maana. Siku itakuja ambapo utayatumia vizuri—maneno Yangu hayawezi kunenwa bure. Huu ndio wakati wa wewe kujiandaa, wakati wa kuandaa njia kwa ajili ya siku zijazo. Unapaswa kuandaa njia ambayo unapaswa kuitembea baadaye; unapaswa kuwa na hofu na wasiwasi kuhusu jinsi utakavyoweza kusimama imara katika siku zijazo na ujiandae vizuri kwa ajili ya njia yako ya baadaye. Usiwe mlafi na mvivu! Lazima ufanye kila kitu uwezacho kabisa kutumia muda wako vizuri, ili uweze kupata kila kitu unachohitaji. Ninakupa kila kitu ili uweze kuelewa. Umeona kwa macho yako mwenyewe kwamba katika kipindi kisichozidi miaka mitatu, Nimenena mambo mengi sana na kufanya kazi nyingi sana. Sababu moja ya Mimi kufanya kazi kwa njia hii ni kwamba watu wamepungukiwa sana, na sababu nyingine ni kwamba muda ni mfupi sana; hakuwezi kuwa na kuchelewa zaidi. Unadhani kuwa watu lazima kwanza waweze kupata ufahamu kamili wa ndani kabla ya kushuhudia na kutumiwa—lakini hiyo haitakuwa polepole sana? Kwa hivyo, Nitalazimika kuandamana na wewe kwa muda gani? Ukinilazimisha niandamane na wewe hadi nitakapozeeka na niwe na mvi, hilo halitawezekana! Kwa kupitia dhiki kubwa zaidi, ufahamu wa kweli ndani ya watu wote utatimizwa. Hizi ni hatua za kazi. Punde unapofahamu kikamilifu maono yaliyoshirikiwa leo na ufikie kimo cha kweli, basi ugumu wowote utakaopitia katika siku zijazo hautakushinda na utaweza kuustahimili. Nitakapokuwa nimemaliza hatua hii ya mwisho ya kazi na kumaliza kunena maneno ya mwisho, katika siku zijazo watu watahitajika kutembea njia yao wenyewe. Hili litatimiza maneno yaliyonenwa hapo awali: Roho Mtakatifu ana agizo kwa kila mtu, na kazi ya kufanya ndani ya kila mtu. Katika siku zijazo, kila mtu ataitembea njia anayopaswa kuitembea, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ni nani atakayeweza kuwatunza wengine huku akipitia dhiki? Kila mtu ana mateso yake mwenyewe, na kila mmoja ana kimo chake mwenyewe. Hakuna kimo cha mtu yeyote kilicho sawa na cha mtu mwingine yeyote. Waume hawataweza kuwatunza wake zao, au wazazi kuwatunza watoto wao; hakuna mtu atakayeweza kumtunza mtu mwingine yeyote. Haitakuwa kama sasa, wakati ambapo kutunzana na kuhimiliana bado kunawezekana. Huo utakuwa wakati ambapo mtu wa kila aina amefunuliwa. Yaani, Mungu anapowapiga wachungaji, basi kondoo wa kundi watatawanyika, na wakati huo ninyi hamtakuwa na kiongozi yeyote wa kweli. Watu watakuwa wamegawanyika—haitakuwa kama sasa, wakati ambapo mnaweza kukusanyika pamoja kama mkutano. Katika siku zijazo, wale ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wataonyesha sura zao za kweli. Waume watawasaliti wake zao, wake watawasaliti waume zao, watoto watawasaliti wazazi wao, na wazazi watawatesa watoto wao—moyo wa binadamu ni usioeleweka kabisa! Kile kinachoweza kufanywa ni kwa mtu kushikilia tu kile mtu alicho nacho, na kuitembea vizuri sehemu ya mwisho ya njia. Sasa hivi, ninyi hamwoni hili wazi wazi; nyinyi nyote ni wasiofikiria mambo yajayo. Si jambo rahisi kupitia hatua hii ya kazi kwa mafanikio.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Sehemu ya Mwisho ya Njia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 474)

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu. Kwa njia hii, ingawa watu tofauti kila mmoja hufuatilia malengo yao binafsi, lengo la harakati zao na motisha yao yote ni sawa, na, zaidi ya hayo, kwa wengi wao, malengo yao ya ibada kwa kiasi kikubwa ni sawa. Katika kipindi cha elfu kadhaa za miaka iliyopita, waumini wengi wamekufa, na wengi wamekufa na kuzaliwa tena. Sio mtu mmoja au wawili ambao humtafuta Mungu, wala hata watu elfu moja au mbili, ilhali harakati ya wengi wa watu hawa ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe ama matumaini yao tukufu ya siku zijazo. Wale ambao ni waaminifu kwa Kristo ni wachache na nadra. Waumini wengi wanaomcha Mungu bado wamekufa wakiwa wametegwa na nyavu zao wenyewe, na zaidi ya hayo, idadi ya watu ambao wamekuwa washindi, ni ndogo mno. Hadi siku ya leo, sababu za watu kushindwa, au siri ya ushindi wao, bado haijulikani kwao. Wale ambao wamejawa na hamu ya kumtafuta Kristo bado hawajapata wakati wao wa ufahamu wa ghafla, hawajafikia kina cha mafumbo haya, kwa sababu hawajui. Ingawa wao wanafanya juhudi za mchwa katika harakati zao, njia ambayo wanatembelea ni njia ya kushindwa ambayo ilitembelewa na watangulizi wao, na si njia ya mafanikio. Kwa njia hii, bila kujali jinsi wanavyotafuta, je, si wao wanatembea katika njia ambayo inaelekea gizani? Je, si wanachopata ni matunda machungu? Ni vigumu vya kutosha kutabiri ikiwa watu ambao huiga wale waliofaulu katika nyakati za zamani hatimaye watapata utajiri au msiba. Uwezekano ni mbaya kiasi gani, basi, kwa watu ambao hutafuta kwa kufuata nyayo za wale ambao hawakufaulu? Je, si wao wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutofaulu? Ni thamani gani iliyoko katika njia wanayoipitia? Je, wao si wanapoteza wakati wao? Bila kujali iwapo mtu hufaulu ama hufeli katika harakati yake, kuna, kwa kifupi, sababu kwa nini wao wanafanya hivyo, na si kweli kuwa kufaulu kwao ama kushindwa kwao kunaamuliwa na kutafuta vyovyote watakavyo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 475)

Mahitaji ya msingi ya imani ya mtu kwa Mungu ni kuwa ni sharti awe na moyo mwaminifu, na kwamba ajitolee mwenyewe, na kutii kwa kweli. Kile kigumu sana kwa mwanadamu ni kupeana mwili wake ili abadilishe na imani ya kweli, ambapo kupitia hii anaweza kupata ukweli mzima, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Hili haliwezi kupatikana na wale ambao wanafeli, na halipatikani hata zaidi na wale ambao hawawezi kumpata Yesu. Kwa sababu mwanadamu si hodari kwa kujitolea mwenyewe kwa Mungu kabisa, kwa sababu mwanadamu hayuko tayari kutekeleza wajibu wake kwa Muumba, kwa sababu mwanadamu ameona ukweli lakini anauepuka na kutembea katika njia yake mwenyewe, kwa sababu mwanadamu daima anatafuta kwa kufuata njia ya wale walioshindwa, kwa sababu mwanadamu daima anaasi Mbingu, hivyo, mwanadamu daima hushindwa, huchukuliwa na hila za Shetani, na anakamatwa kwa hila na wavu wake. Kwa sababu mwanadamu hamjui Kristo, kwa sababu mwanadamu hana ustadi katika kuelewa na kushuhudia ukweli, kwa sababu mwanadamu ni wa kuabudu Paulo sana na mwenye tamaa nyingi ya mbinguni, kwa sababu mwanadamu daima anadai kuwa Kristo awe akimtii yeye na kuagiza kuhusu Mungu, hivyo mashujaa hao wakuu na wale ambao wamepitia mabadiliko mabaya ya dunia bado wamo na ubinaadamu, na bado hufa kwa kuadibu kwa Mungu. Yote Ninayoweza kusema kuhusu watu kama hawa ni kuwa wanakufa kifo cha kutisha, na athari yao—kifo chao—si bila haki. Je, si kushindwa kwao hakuvumiliki hata zaidi kwa sheria ya Mbinguni? Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hiki si kitu ambacho mwanadamu anaweza kufanya. Ilhali Kristo hutoa ukweli tu; Yeye haji kuamua ikiwa mwanadamu atafanikiwa katika harakati yake ya kufuata ukweli. Hivyo, kinachofuata ni kuwa mafanikio au kushindwa kwa kweli yote yanategemea harakati ya mwanadamu. Mafanikio au kushindwa kwa mwanadamu kwa kweli kamwe hakuna uhusiano na Kristo, lakini kwa mbadala kunategemea harakati yake. Hatima ya mwanadamu na mafanikio yake ama kushindwa haiwezi kurundikwa kichwani pa Mungu, ili Mungu mwenyewe afanywe wa kuibeba, kwa sababu sio jambo la Mungu mwenyewe, lakini linahusiana moja kwa moja na wajibu ambao viumbe wa Mungu wanapaswa kutekeleza. Watu wengi wana maarifa madogo ya harakati na hatima za Paulo na Petro, lakini watu hawajui lolote ila matokeo ya Petro na Paulo, na hawajui kuhusu siri ya mafanikio ya Petro, au mapungufu yaliyosababisha kushindwa kwa Paulo. Na kwa hivyo, kama ninyi hamwezi kabisa kuelewa kiini cha harakati zao basi harakati ya wengi wenu bila shaka haitafaulu, na hata kama wachache wenu watafaulu, bado hawatakuwa sawa na Petro. Ikiwa njia unayopitia katika kutafuta ni ya kweli, basi una matumaini ya mafanikio. Kama njia unayopitia katika kufuatilia ukweli ni mbaya, basi wewe milele hutaweza kufanikiwa, na utakuwa na hatima sawa na Paulo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 476)

Petro alikuwa mtu aliyefanywa mkamilifu. Ni baada tu ya kupitia kuadibu na hukumu, na hivyo kupata upendo safi kwa Mungu, ndipo alifanywa mkamilifu kabisa; njia ambayo alipitia ilikuwa ni njia ya kukamilishwa. Ambayo ni kusema kuwa, tangu hapo mwanzo kabisa, njia ambayo Petro alipitia ilikuwa ya haki, na motisha ya kumwamini Mungu ilikuwa sahihi, na kwa hivyo akawa mtu aliyekuwa amefanywa kamili na alifuata njia mpya ambayo mwanadamu kamwe hajawahi kuitembelea hapo awali. Hata hivyo, njia ambayo Paulo alitembea tangu mwanzo ilikuwa njia ya upinzani kwa Kristo, na ni kwa sababu tu Roho Mtakatifu alitaka kumtumia, na kufaidika na vipaji vyake na ustahili wake wote kwa kazi yake, kwamba alifanya kazi kwa ajili ya Kristo kwa miongo mingi. Alikuwa mtu tu ambaye alitumiwa na Roho Mtakatifu, na hakutumika kwa sababu Yesu alitazama ubinadamu wake kwa mapendeleo, lakini ni kwa sababu ya vipaji vyake. Aliweza kufanya kazi ya Yesu kwa sababu alipigwa, na sio kwa sababu alifurahia kufanya hivyo. Aliweza kufanya kazi kama hiyo kwa sababu ya kupata nuru na uongozi wa Roho Mtakatifu, na kazi aliyoifanya haikuwakilisha ufuatiliaji wake kwa njia yeyote, au ubinadamu wake. Kazi ya Paulo iliwakilisha kazi ya mtumishi, ambayo ni kusema kuwa yeye alifanya kazi ya mtume. Petro, hata hivyo, alikuwa tofauti: Yeye pia alifanya baadhi ya kazi; haikuwa kuu kama kazi ya Paulo, lakini alifanya kazi huku akiwa na harakati ya kuingia kwake mwenyewe, na kazi yake ilikuwa tofauti na kazi ya Paulo. Kazi ya Petro ilikuwa utekelezaji wa wajibu wa kiumbe wa Mungu. Yeye hakufanya kazi katika nafasi ya mtume, lakini alifanya kazi huku akifuatilia upendo kwa Mungu. Mwendo wa kazi ya Paulo pia ulikuwa na harakati yake binafsi. Ufuatiliaji wake ulikuwa tu kwa ajili ya matumaini yake ya siku za baadaye, na shauku yake ya hatima nzuri. Yeye hakukubali usafishaji wakati wa kazi yake, wala hakukubali upogoaji na ushughulikaji. Yeye aliamini kuwa alimradi kazi aliyoifanya iliridhisha mapenzi ya Mungu, na yote aliyofanya yalimpendeza Mungu, basi tuzo hatimaye ilikuwa inamsubiri. Hakukuwa na matukio ya kibinafsi katika kazi yake—yote yalikuwa kwa ajili yake mwenyewe, na hayakufanyika huku kukiwa na harakati ya mabadiliko. Kila kitu katika kazi yake kilikuwa shughuli, na hakukuwa na wajibu wowote au kujisalimisha kwa kiumbe cha Mungu. Wakati wa safari ya kazi yake, hakuna mabadiliko yaliyotokea katika tabia ya zamani ya Paulo. Kazi yake ilikuwa tu ya kufanya huduma kwa ajili ya wengine, na haikuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko katika tabia yake. Paulo alifanya kazi yake moja kwa moja, bila ya kufanywa mkamilifu ama kushughulikiwa, na alivutiwa na thawabu. Petro alikuwa tofauti: alikuwa mtu ambaye alikuwa amepitia upogoaji na ushughulikiaji na alikuwa amepitia usafishaji. Lengo na motisha za kazi ya Petro zilikuwa tofauti kimsingi na zile za Paulo. Ingawa Petro hakufanya sehemu kubwa ya kazi, tabia yake ilipitia mabadiliko mengi, na alichotafuta ni ukweli, na mabadiliko ya kweli. Kazi yake haikufanyika tu kwa ajili ya kazi yenyewe. Ingawa Paulo alifanya kazi nyingi, yote ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu, na ingawa Paulo alishirikiana katika kazi hii, yeye, hakuipitia. Kwamba Petro alifanya kazi ndogo ilikuwa tu kwa ajili Roho Mtakatifu hakufanya kazi kubwa kupitia yeye. Wingi wa kazi zao haukuamua iwapo walikuwa wamefanywa wakamilifu; harakati ya mmoja ilikuwa ili kupokea tuzo, na ile ya mwingine ilikuwa ili kufikia upendo wa mwisho kwa Mungu na kutimiza wajibu wake kama kiumbe cha Mungu, kwa kiasi kwamba angeweza kuishi kwa kudhihirisha picha inayopendeza ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Nje walikuwa tofauti, na pia vile vile viini vyao vilikuwa tofauti. Huwezi kuamua ni nani kati yao alifanywa mkamilifu kwa msingi wa kazi waliyofanya. Petro alitafuta kuishi kwa kudhihirisha picha ya yule ambaye hupenda Mungu, kuwa mtu ambaye alimtii Mungu, kuwa mtu ambaye alikubali ushughulikaji na upogoaji, na kuwa mtu aliyetekeleza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Aliweza kujitolea kwa Mungu, kuweka nafsi yake kamilifu katika mikono ya Mungu, na kumtii hadi kifo. Hilo ndilo alilokuwa ameamua kufanya na, zaidi ya hayo, hilo ndilo alilotimiza. Hii ndiyo sababu ya msingi ya kwani hatima yake ilikuwa tofauti na ile ya Paulo. Kazi ambayo Roho Mtakatifu alifanya ndani ya Petro ilikuwa kumfanya mkamilifu, na kazi ambayo Roho Mtakatifu alifanya ndani ya Paulo ilikuwa kumtumia. Hii ni kwa sababu asili zao na mitazamo yao kuhusu harakati hazikuwa sawa. Wote walikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Petro alitumia kazi hii kwake mwenyewe, na pia akawapa watu wengine; Paulo, kwa upande mwingine, aliwapa wengine kazi nzima ya Roho Mtakatifu, na mwenyewe hakufaidika na chochote kutoka kwa kazi hiyo. Kwa njia hii, baada ya yeye kushuhudia kazi ya Roho Mtakatifu kwa miaka mingi, mabadiliko ndani ya Paulo yalikuwa karibu na kutokuwepo. Yeye bado alibaki karibu katika hali yake ya asili, na bado yeye alikuwa yule Paulo wa awali. Ni baada tu ya kuvumilia ugumu wa miaka mingi ya kazi, ndivyo alikuwa amejifunza jinsi ya kufanya “kazi” na kujifunza uvumilivu, lakini asili yake ya zamani—ushindani wake mkuu na asili wa kimamluki—bado ilibaki. Baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi, hakufahamu asili yake potovu, wala hakuwa amejiondoa mwenyewe kutoka kwa asili yake ya zamani, na bado ilikuwa inaonekana katika kazi yake. Kwake, kulikuwepo tu na uzoefu wa kazi zaidi, lakini uzoefu mdogo kiasi hicho pekee haukuwa na uwezo wa kumbadilisha na hukuweza kubadilisha maoni yake kuhusu kuwepo au umuhimu wa harakati yake. Ingawa alimfanyia Kristo kazi kwa miaka mingi, na hakumtesa tena Bwana Yesu, ndani ya Moyo wake hakukuwa na mabadiliko katika elimu kuhusu Mungu. Hii ina maana kuwa hakufanya kazi ili awe mwaminifu kwa Mungu, lakini badala yake, alilazimika kufanya kazi kwa ajili ya hatima yake ya siku zijazo. Kwa kuwa, hapo mwanzo, alimtesa Kristo, na hakumtii Kristo; kiasili yeye alikuwa mwasi ambaye alimpinga Kristo kimakusudi, na mtu ambaye hakuwa na elimu kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi yake ilipokuwa inakaribia kukamilika, yeye bado hakujua kazi ya Roho Mtakatifu, na yeye tu alitenda kwa hiari yake mwenyewe kwa mujibu wa hulka yake mwenyewe, bila hata kidogo kutilia maanani mapenzi ya Roho Mtakatifu. Na hivyo asili yake ilikuwa katika uhasama na Kristo na haikutii ukweli. Mtu kama huyu, ambaye alikuwa ameachwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ambaye hakujua kazi ya Roho Mtakatifu, na ambaye pia alimpinga Kristo—je, ni jinsi gani mtu kama huyu angeokolewa? Iwapo mtu ataweza kuokolewa au la haitegemei kiasi cha kazi anayoifanya, au ni kiasi gani anajitolea, lakini badala yake kuamuliwa na iwapo anajua au hajui kazi ya Roho Mtakatifu, iwapo anaweza kuweka ukweli kwenye vitendo au la, na iwapo maoni yake kuhusu harakati yanalingana na ukweli au la.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 477)

Ingawa ufunuo wa asilia ulitokea baada ya Petro kuanza kumfuata Yesu, katika asili alikuwa, tangu mwanzo kabisa, mtu ambaye alikuwa tayari kujiwasilisha kwa Roho Mtakatifu na kumtafuta Kristo. Utiifu wake kwa Roho Mtakatifu ulikuwa safi: hakutafuta umaarufu na mali, lakini badala yake alikuwa amepewa motisha na utii wa ukweli. Ingawa kuna nyakati tatu ambapo Petro alikana kumjua Kristo, na ingawa alimjaribu Bwana Yesu, udhaifu kidogo kama huu wa kibinadamu haukubeba uhusiano wa asilia yake, na haukuathiri harakati zake za mbeleni, na huwezi kuthibitisha kikamilifu ya kuwa majaribu yake yalikuwa kitendo cha mpinga Kristo. Udhaifu wa kawaida wa kibinadamu ni kitu ambacho kimo kwa watu wote duniani—je, unatarajia Petro kuwa tofauti vyovyote vile? Je, si watu wana mtazamo fulani kuhusu Petro kwa sababu alifanya makosa mengi ya kijinga? Na je, si watu wanampenda Paulo kwa sababu ya kazi yote aliyoifanya, na nyaraka zote alizoandika? Itakuwaje mtu kuwa na uwezo wa kuona kupitia kiini cha mwanadamu? Hakika, je, wale ambao kwa kweli wana hisia wanaweza kuona kitu chenye thamani ndogo kama hiyo? Ingawa miaka mingi ya matukio ya uchungu ya Petro hayajanakiliwa katika Biblia, hii haithibitishi kuwa Petro hakuwa na matukio halisi, au kwamba Petro hakufanywa mkamilifu. Ni jinsi gani kazi ya Mungu inaweza kueleweka na mwanadamu? Kumbukumbu kwenye Biblia hazikuchaguliwa binafsi na Yesu, lakini zilikusanywa na vizazi vya baadaye. Kwa njia hii, si yote ambayo yaliandikwa katika Biblia yalichaguliwa kulingana na mawazo na mwanadamu? Zaidi ya hayo, hatima ya Petro na Paulo hazijaelezwa kwa dhati katika nyaraka, kwa hivyo mwanadamu anawahukumu Petro na Paulo kulingana na mtazamo wake mwenyewe, na kulingana na matakwa yake mwenyewe. Na kwa kuwa Paulo alifanya kazi kubwa sana, kwa sababu “michango” yake ilikuwa mikuu sana, yeye alipata imani ya umma. Je, si mwanadamu anamakinika tu na vitu vya juu juu tu. Inakuwaje mwanadamu kuwa na uwezo wa kuona kupitia kwa kiini cha mwanadamu? Bila kutaja, kwa kuwa Paulo amekuwa mlengwa wa ibada kwa maelfu ya miaka, ni nani ambaye atathubutu kukana kazi yake kwa haraka? Petro alikuwa mvuvi tu, hivyo ni jinsi gani mchango wake ungekuwa mkubwa kama ule wa Paulo? Kwa msingi wa mchango, Paulo angepaswa kuzawadiwa kabla ya Petro, na inapaswa kuwa yeye ndiye angekuwa amehitimu vyema zaidi kupata kibali cha Mungu. Nani angeweza kufikiri kuwa, katika kumtendea Paulo, Mungu alimfanya tu afanye kazi kupitia vipawa vyake, ilhali Mungu alimfanya Petro kuwa mkamilifu. Si kwa njia yoyote kweli ya kwamba Bwana Yesu alikuwa amefanya mpango kwa ajili ya Petro na Paulo tangu mwanzo kabisa: Badala yake, walifanywa wakamilifu au kuwekwa kazini kulingana na tabia zao za kiasili. Na kwa hivyo, kitu ambacho wanadamu wanachoona kama michango ya nje ya mwanadamu tu, ilhali anachoona Mungu ni kiini cha mtu, na vile vile kama njia ambayo mwanadamu hufuatilia tangu mwanzo, na motisha inayosukuma harakati ya mwanadamu. Watu hupima mwanadamu kulingana na dhana zao, na kulingana na mitazamo yao wenyewe, na bado hatima ya mwisho ya mwanadamu haiamuliwi kulingana na mambo ya nje ya mwanadamu. Na kwa hivyo Mimi ninasema kwamba kama njia unayochukua tangu mwanzo ni njia ya mafanikio, na mtazamo wako kuhusu harakati ni sahihi tangu mwanzo, basi wewe ni kama ya Petro; kama njia ambayo unatembea ni njia ya kushindwa, basi gharama yoyote ambayo unalipa, hatima yako itakuwa sawa na ile ya Paulo. Yawayo yoyote, hatima yako, na kama utafaulu ama hautafaulu, yote yanaamuliwa na kama njia unayotafuta ni sahihi ama si sahihi, badala ya kujitolea kwenu, au gharama ambayo wewe hulipa. Kiini cha Petro na kiini cha Paulo, na malengo ambayo walifuatilia, yalikuwa tofauti; mwanadamu hana uwezo wa kugundua vitu hivi, na Mungu pekee anaweza kuyajua kwa ujumla wao. Kwa kuwa kitu ambacho Mungu huona ni kiini cha mwanadamu, ilhali mwanadamu hajui chochote kuhusu kiini chake mwenyewe. Mwanadamu hana uwezo wa kukitazama kiini ndani ya mwanadamu ama kimo chake halisi, na hivyo hana uwezo wa kutambua sababu za kutofaulu ama kufaulu kwa Paulo na Petro. Sababu ya wanadamu wengi kumuabudu Paulo na wala si Petro ni kuwa Paulo alitumika katika kazi ya umma, na mwanadamu anaweza kutambua kazi hii, na hivyo watu wanakiri “mafanikio” ya Paulo. Matukio ya Petro, wakati huo huo, hayaonekani na mwanadamu, na kwamba kile alichotafuta hakipatikani na mwanadamu, na hivyo mwanadamu hana moyo wa kutaka kumjua Petro.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 478)

Petro alifanywa mkamilifu kwa kupitia ushughulishaji na usafishaji. Alisema, “Mimi ni lazima nikidhi mapenzi ya Mungu wakati wote. Kwa yote nifanyayo mimi natafuta tu kukidhi mapenzi ya Mungu, na kama mimi ninaadibiwa, au kuhukumiwa, bado nina furaha kufanya hivyo.” Petro alimpa Mungu kila kitu chake, na kazi yake, maneno, na maisha yote yalikuwa yote kwa ajili ya kumpenda Mungu. Alikuwa mtu ambaye alitafuta utakatifu, na alipopitia zaidi, ndivyo upendo wake wa Mungu ndani ya moyo wake ulikuwa mkubwa zaidi. Paulo, wakati huo huo, alifanya tu kazi ya nje, na ingawa alitia bidii katika kazi yake, juhudi zake zilikuwa kwa ajili ya kufanya kazi yake vizuri na hivyo kupata tuzo. Angalijua kuwa hatapokea tuzo, yeye angalikata tamaa katika kazi yake. Kitu ambacho Petro alijali mno ni upendo wa kweli moyoni mwake, na ule ambao ulikuwa wa vitendo na ungeweza kutimizika. Yeye hakujali kuhusu iwapo angepokea tuzo, lakini kuhusu iwapo tabia yake ingebadilishwa. Paulo alijali kuhusu kufanya kazi kwa bidii hata zaidi, yeye alijali kuhusu kazi ya nje na kujitolea, na kuhusu mafundisho ambayo hayashuhudiwi na watu wa kawaida. Yeye hakujali chochote kuhusu mabadiliko ndani yake wala kwa ajili ya upendo wa kweli kwa Mungu. Uzoefu wa Petro ulikuwa kwa ajili ya kupata upendo wa kweli na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Uzoefu wake ulikuwa ili kupata uhusiano wa karibu na Mungu, na kwa kuishi kwa kudhihirisha kwa vitendo. Kazi ya Paulo ilifanywa kwa sababu ya kile alichoaminiwa na Yesu, na ili apate vitu ambavyo alitamani, lakini haya hayakuwa na uhusiano na elimu yake mwenyewe na ya Mungu. Kazi yake ilikuwa tu kwa ajili ya kuepuka kuadibu na hukumu. Kitu ambacho Petro alitafuta kilikuwa ni upendo safi, na Paulo alitafuta taji ya hali ya kuwa mwenye haki. Petro alishuhudia miaka mingi ya kazi ya Roho Mtakatifu, na alikuwa na elimu ya vitendo kuhusu Kristo, na vile vile elimu ya kina kujihusu yeye mwenyewe. Na hivyo, upendo wake wa Mungu ulikuwa safi. Miaka mingi ya usafishaji ilikuwa imeinua elimu yake kuhusu Yesu na maisha, na upendo wake ulikuwa upendo usio na masharti, ulikuwa upendo wa hiari, na hakuagiza chochote akitarajia malipo, na wala hakutumainia kuwa na faida yeyote. Paulo alifanya kazi kwa miaka mingi, ilhali hakumiliki elimu kubwa ya Yesu, na elimu yake ya kibinafsi ilikuwa ndogo mno. Yeye kwa kifupi hakuwa na upendo kwa Kristo, na kazi yake na mwendo ambao alikimbia ilikuwa ili apate heshima na taji la mwisho. Kitu ambacho alitafuta kilikuwa taji zuri kabisa, wala si upendo safi. Yeye hakutafuta kikamilifu, lakini kwa kutoonyesha hisia; hakuwa anatekeleza majukumu yake, lakini alilazimika katika harakati yake baada ya kukamatwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, harakati yake haithibitishi kuwa yeye alikuwa kiumbe wa Mungu kilichokuwa na sifa zinazostahili; ilikuwa ni Petro ambaye alikuwa kiumbe wa Mungu aliyekuwa na sifa zilizostahili na ambaye alitekeleza wajibu wake. Mwanadamu anafikiri kuwa wale wote wanaotoa mchango kwa Mungu wanapaswa kupokea tuzo, na kwamba mchango unavyokuwa mkubwa zaidi, ndivyo mwanadamu anavyosadiki zaidi kuwa atapokea fadhila za Mungu. Kiini cha mtazamo wa mwanadamu ni wa shughuli, na hatafuti kikamilifu kutekeleza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Kwa Mungu, watu wanavyozidi kutafuta upendo kwa Mungu wa kweli na utii mkamilifu kwa Mungu, ambayo pia ina maana kutafuta kutekeleza wajibu wao kama viumbe wa Mungu, ndivyo zaidi wanaweza kupata kibali cha Mungu. Mtazamo wa Mungu ni kudai kwamba mwanadamu arejeshe hadhi na wajibu wake wa awali. Mwanadamu ni kiumbe wa Mungu, na kwa hivyo mwanadamu hapaswi kuvuka mpaka mwenyewe kwa kutoa madai yoyote kwa Mungu, na anapaswa asifanye lolote zaidi ya kutekeleza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Hatima ya Paulo na hatima ya Petro ilipimwa kulingana na iwapo wangeweza kutekeleza wajibu wao kama viumbe wa Mungu, na wala si kulingana na ukubwa wa michango yao; hatima zao ziliamuliwa kulingana na kile ambacho walitafuta tangu mwanzo, wala si kulingana na kiasi cha kazi waliyofanya, au makadirio ya watu wengine kuwahusu. Kwa hivyo, kutafuta kutekeleza kikamilifu wajibu wa mtu kama kiumbe wa Mungu ndiyo njia ya mafanikio; kutafuta njia ya upendo wa kweli kwa Mungu ndiyo njia sahihi kabisa; kutafuta mabadiliko katika tabia ya zamani ya mtu, na kutafuta upendo safi kwa Mungu, ndiyo njia ya mafanikio. Njia kama hii ya mafanikio ndiyo njia ya kurejeshwa kwa wajibu wa awali na vile vile pia kuonekana kwanza kwa kiumbe wa Mungu. Hiyo ndiyo njia ya kurejeshwa, na pia ni lengo la kazi yote ya Mungu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kama harakati ya mwanadamu inatiwa doa na madai badhirifu ya kibinafsi na tamaa isiyo ya akili, basi athari ambayo inatimizwa haitakuwa mabadiliko katika tabia ya mwanadamu. Hii ni kinyume na kazi ya kurejeshwa. Bila shaka siyo kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu, na hivyo hii inathibitisha kuwa harakati ya aina hii haikubaliki na Mungu. Harakati ambayo haijakubalika na Mungu ina umuhimu gani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 479)

Kazi iliyofanywa na Paulo ilionyeshwa mbele ya mwanadamu, lakini upendo wake wa Mungu ulikuwa safi kiasi gani, upendo wake kwa Mungu ulikuwa ndani ya moyo wake kiasi gani—haya hayaonekani na mwanadamu. Mwanadamu anaweza tu kutazama kazi ambayo aliifanya, ambapo mwanadamu hujua kuwa kwa hakika alitumika na Roho Mtakatifu, na hivyo mwanadamu hudhani kwamba Paulo alikuwa bora kuliko Petro, ya kwamba kazi yake ilikuwa kubwa zaidi, kwa kuwa alikuwa na uwezo wa kutoa kwa makanisa. Petro alitazama tu matukio yake binafsi, na akapata watu wachache wakati wa kazi yake ya mara kwa mara. Kutoka kwake kunazo lakini nyaraka chache zinazojulikana, lakini ni nani anayejua jinsi upendo wa Mungu ulivyokuwa mkubwa kiasi gani moyoni mwake? Siku zote, usiku na mchana, Paulo alimfanyia Mungu kazi: alimradi kulikuwepo na kazi ya kufanywa, yeye aliifanya. Yeye alihisi kuwa kwa njia hii angeweza kulipata taji, na angemridhisha Mungu, lakini hakutafuta njia za kujibadilisha mwenyewe kupitia kazi hii. Chochote katika maisha ya Petro ambacho hakikukimu mapenzi ya Mungu kilimfanya kuhisi wasiwasi. Kama hakikukidhi mapenzi ya Mungu, basi angehisi kujuta, na angetafuta njia mwafaka ambayo angejitahidi kuridhisha moyo wa Mungu. Hata katika masuala madogo kabisa maishani mwake yasiyokuwa na maana, bado alijishurutisha mwenyewe kukidhi mapenzi ya Mungu. Alikuwa pia mkali ilipofikia tabia yake ya asili na alikuwa daima mkali katika masharti yake mwenyewe ili kuelekea ndani zaidi kwa ukweli. Paulo alitafuta tu sifa na hadhi ya kijuu juu. Alitafuta kuringa mwenyewe mbele za mwanadamu, na hakutafuta kufanya maendeleo zaidi katika kuingia kwa maisha. Kile alichojali kuhusu ni mafundisho ya kidini, si uhalisi. Baadhi ya watu husema, “Paulo alimfanyia Mungu kazi nyingi, kwa nini yeye hakukumbukwa na Mungu? Petro alimfanyia Mungu kazi kidogo, na hakufanya mchango mkubwa katika makanisa, je, kwa nini yeye alifanywa mkamilifu?” Petro alimpenda Mungu hadi kiwango fulani, ambacho kilitakiwa na Mungu; ni watu kama hawa pekee wana ushuhuda. Na kuhusu Paulo? Ni kiwango gani ambacho Paulo alimpenda Mungu, je, wewe wajua? Kazi ya Paulo ilikuwa kwa ajili ya nini? Na kazi ya Petro ilikuwa kwa ajili ya nini? Petro hakufanya kazi kubwa, lakini, je, wafahamu ni nini kilikuwa moyoni mwake? Kazi ya Paulo inahusiana na utoaji makanisani, na msaada wa makanisa. Kile ambacho Petro alishuhudia ni mabadiliko ya tabia ya maisha yake; alishuhudia upendo kwa Mungu. Kwa kuwa sasa unajua tofauti katika kiini cha kila mmoja wao, unaweza kuona ni nani, hatimaye, kwa kweli alimwamini Mungu, na ni nani ambaye kwa kweli hakumwamini Mungu. Mmoja wao alimpenda Mungu kwa kweli, na mwingine hakumpenda Mungu kwa kweli; mmoja alipitia mabadiliko katika tabia yake, na mwingine hakupitia; mmoja alihudumu kwa unyenyekevu, na hakuonekana na watu kwa urahisi na mwingine aliabudiwa na watu, na alikuwa na picha nzuri; mmoja alitafuta utakatifu, na mwingine hakuutafuta, na ingawa hakuwa najisi, hakuwa amemilikiwa na upendo safi; mmoja alimilikiwa na ubinadamu wa kweli, na mwingine hakuwa nao; mmoja alikuwa na hisia ya kiumbe wa Mungu, na mwingine hakuwa na hisia hiyo. Tofauti kama hizi ndizo zilizo katika kiini cha Paulo sawa na Petro. Njia ambayo Petro alitembea ni njia ya mafanikio, ambayo pia ni njia ya kutimiza kupatwa tena kwa ubinadamu wa kawaida na wajibu wa kiumbe wa Mungu. Petro anawakilisha wote hao waliofaulu. Njia ambayo Paulo aliitembea ni njia ya kushindwa, na anawakilisha wale wote ambao wanajisalimisha na kujipa matarajio yao wenyewe ya kijuu juu, na hawampendi Mungu kwa dhati. Paulo anawakilisha wote ambao hawana ukweli. Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na kuwa bila kitu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake kwa Mungu. Je, huu haukuwa upendo mkamilifu kwa Mungu? Je, huku hakukuwa ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? Kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo kwa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki. Fikiria kwamba wewe unaweza kumfanyia Mungu kazi, ilhali wewe humtii Mungu, na huna uwezo wa kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa njia hii, wewe hutakuwa tu umekosa kutimiza wajibu wa kiumbe cha Mungu, lakini pia utalaaniwa na Mungu, kwa kuwa wewe ni mtu ambaye hana ukweli, ambaye hana uwezo wa kumtii Mungu, na ambaye si mtiifu kwa Mungu. Wewe unajali tu kuhusu kumfanyia Mungu kazi, na hujali kuhusu kuweka ukweli katika vitendo, ama kujifahamu. Wewe humfahamu ama kumjua Muumba, na humtii ama kumpenda Muumba. Wewe ni mtu ambaye asilia si mtiifu kwa Mungu, na hivyo watu kama hawa hawapendwi na Muumba.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 480)

Baadhi ya watu husema, “Paulo alifanya kazi kubwa kiasi cha ajabu, na alibeba mizigo mikubwa ya makanisa na aliwachangia mno. Nyaraka kumi na tatu ya Paulo zilizingatia miaka 2,000 ya Enzi ya Neema, na ni za pili tu baada ya Injili Nne. Nani anaweza kulinganishwa naye? Hakuna ambaye anaweza kufumbua maandiko ya Ufunuo wa Yohana, ilhali nyaraka za Paulo zinatoa maisha, na kazi ambayo alifanya ilikuwa na manufaa kwa makanisa. Ni nani mwingine angeweza kutimiza mambo kama haya? Na kipi ambacho Petro alikifanya?” Mwanadamu anapowapima wengine, ni kwa mujibu wa michango yao. Mungu anapompima mwanadamu, ni kwa mujibu wa asili yake. Miongoni mwa wale ambao hutafuta uzima, Paulo alikuwa mtu ambaye hakujua kiini chake mwenyewe. Hakuwa kwa njia yoyote mnyenyekevu ama mtiifu, wala kujua kiini chake, ambacho kilikinzana na Mungu. Na kwa hivyo, alikuwa mtu ambaye hakuwa amepitia matukio ya kina, na alikuwa mtu ambaye hakuweka ukweli katika vitendo. Petro alikuwa tofauti. Yeye alijua kutokamilika kwake, udhaifu, na tabia yake potovu kama kiumbe wa Mungu, na hivyo alikuwa na njia ya vitendo ambayo angebadilishia tabia yake; hakuwa mmoja wa wale ambao walikuwa tu na mafundisho ya kidini lakini hawakuwa na uhalisi. Wale ambao hubadilika ni watu wapya ambao wameokolewa, ni wale ambao wana sifa zinazostahili katika kufuatilia ukweli. Watu ambao hawabadiliki ni wa wale ambao hawafai kwa sasa kiasili; ni wale ambao hawajaokolewa, yaani, ni wale ambao wamechukiwa na kukataliwa na Mungu. Hawatakumbukwa na Mungu bila kujali jinsi kazi zao ni kubwa. Wakati unapolinganisha haya na harakati yako mwenyewe, kama wewe hatimaye ni mtu wa aina sawa na Petro au Paulo inapaswa kuwa dhahiri kibinafsi. Kama bado hakuna ukweli kwa yale unayotafuta, na kama hata leo bado wewe ni mwenye kiburi na jeuri kama Paulo, na bado wewe ni mwepesi wa kusema maneno matupu na mwenye kujisifu kama yeye, basi bila shaka wewe ni aliyeharibika tabia na ambaye hushindwa. Kama wewe hutafuta jinsi sawa na Petro, kama unatafuta vitendo na mabadiliko ya kweli, na usiwe mwenye kiburi au mkaidi, bali utafute kutekeleza majukumu yako, basi utakuwa kiumbe wa Mungu ambaye anaweza kufikia ushindi. Paulo hakujua kiini chake mwenyewe ama upotovu, vile vile hakujua kutotii kwake. Hakuwahi kutaja uasi wake kwa Kristo unaostahili dharau, wala yeye hakuwa mwenye kujuta kupindukia. Yeye tu alipeana maelezo mafupi, na, ndani katika moyo wake, hakujiwasilisha kwa Mungu kikamilifu. Ingawa alianguka barabarani akielekea Dameski, yeye hakuangalia nafsi yake kwa kina. Aliridhika tu kwa kuendelea kufanya kazi, na hakuzingatia kujijua mwenyewe na kubadilisha tabia yake ya zamani kuwa jambo la muhimu zaidi ya masuala yote. Yeye aliridhika tu kwa kusema ukweli, na kukimu wengine kama dawa ya dhamiri yake mwenyewe, na kwa kutowatesa tena wanafunzi wa Yesu kujifariji na kujisamehe kwa dhambi zake za zamani. Lengo ambalo yeye alifuatilia tu lilikuwa taji ya wakati ujao na kazi ya muda pekee, lengo ambalo alifuatilia lilikuwa neema tele. Yeye hakutafuta ukweli wa kutosha, wala hakutafuta kuendelea ndani katika kiini cha ukweli ambao hakuwa hapo awali ameufahamu. Na kwa hivyo elimu yake ya nafsi yake inaweza semwa kuwa ya uwongo, na hakukubali kuadibu au hukumu. Kwamba aliweza kufanya kazi haina maana alikuwa na elimu ya asili yake au kiini; lengo lake lilikuwa la vitendo vya nje pekee. Lile ambalo daima alijitahidi kwalo, zaidi ya hayo, halikuwa mabadiliko, laikini elimu. Kazi yake kwa ujumla ilikuwa matokeo ya kuonekana kwa Yesu njiani kuelekea Dameski. Hakikuwa kitu ambacho alikuwa ameamua kukifanya hapo awali, wala haikuwa kazi ambayo ilikuwa imetokea baada ya yeye kukubali upogoaji wa tabia yake ya zamani. Bila kujali jinsi ambavyo alifanya kazi, tabia yake ya zamani haikubadilika, na hivyo kazi yake haikulipia dhambi yake ya zamani lakini ilikuwa tu na wajibu fulani kwenye makanisa ya wakati huo. Kwa mtu kama huyu, ambaye tabia yake ya zamani haikubadilika—hivyo ni kusema, ambaye hakupata wokovu, na hata zaidi alikuwa bila ukweli—alikuwa hawezi kabisa kukuwa mmoja wa wale waliokubaliwa na Bwana Yesu. Hakuwa mtu ambaye alikuwa amejazwa na upendo na heshima kwa Yesu Kristo, wala hakuwa mtu ambaye alikuwa na ustadi katika kutafuta ukweli, na wala hakuwa mtu ambaye alitafuta fumbo la kupata mwili kwa Yesu Kristo. Alikuwa tu mtu ambaye alikuwa na ujuzi katika utata, na ambaye hangeweza kusalimu amri kwa yeyote ambaye alikuwa mkuu kwake au aliyekuwa na ukweli. Aliwaonea kijicho watu ama ukweli ambao ulikuwa tofauti naye, ama wenye uadui naye, na kupendelea watu wenye vipawa ambao walionyesha picha nzuri na kumiliki maarifa makubwa. Hakupenda kuingiliana na watu maskini ambao walitafuta njia ya ukweli na waliojali kuhusu ukweli pekee, na badala yake alijihusisha na viongozi mashuhuri kutoka mashirika ya kidini ambao walizungumza kuhusu mafundisho ya dini pekee, na walikuwa na elimu tele. Hakuwa na upendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, na hakujali kuhusu harakati za kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Badala yake, yeye alipendelea kanuni hizo na mafundisho ya dini ambayo yalikuwa juu kuliko ukweli wa ujumla. Katika kiini chake cha kiasilia na uzima wa kile alichotafuta, hastahili kuitwa Mkristo ambaye alifuatilia ukweli, wala mtumishi mwaminifu katika nyumba ya Mungu, kwa kuwa unafiki wake ulikuwa mwingi sana, na kutotii kwake kulikuwa kukubwa sana. Ingawa anajulikana kama mtumishi wa Bwana Yesu, hakustahili kamwe kuingia kwenye lango la ufalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake tangu mwanzo hadi mwisho hayawezi kuitwa yenye haki. Anaweza tu kuonekana kama mtu ambaye alikuwa mnafiki, na aliyefanya udhalimu, ilhali ambaye alimfanyia Yesu kazi. Ingawa hawezi kuitwa mwovu, yeye anaweza ipasavyo kuitwa mtu ambaye alifanya udhalimu. Alifanya kazi nyingi, ilhali ni lazima asihukumiwe juu ya wingi wa kazi aliyofanya, lakini tu kwa ubora na umuhimu wa kazi hiyo. Ni kwa njia hii tu ndiyo inawezekana kufikia kwenye kiini cha suala hili. Yeye siku zote aliamini: “Mimi nina uwezo wa kufanya kazi, mimi ni bora kuliko watu wengi; mimi ni mwenye kujali kuhusu mzigo wa Bwana kuliko mtu yeyote, na hakuna anayetubu sana kama ninavyotubu, kwa kuwa mwanga mkuu uling’aa kwangu, na nimeuona mwanga mkuu, na hivyo toba yangu ni kuu kuliko ya yeyote mwingine.” Wakati huo, hivi ndivyo alivyofikiria moyoni mwake. Mwishoni mwa kazi yake, Paulo alisema: “Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu.” Mapambano yake, kazi, na safari zilikuwa kwa ajili ya taji la haki, na yeye hakusonga mbele; ingawa yeye hakuwa wa juu juu tu katika kazi yake, inaweza kusemwa kuwa kazi yake ilikuwa kwa ajili tu ya kusahihisha makosa yake, na kusahihisha shutuma za dhamiri yake. Yeye tu alitumaini kukamilisha kazi yake, kumaliza safari yake, na kupigana vita vyake haraka iwezekanavyo, ili kwamba aweze kupata tuzo lake la haki alilotamani kwa haraka. Alilotamani halikuwa kukutana na Bwana Yesu na uzoefu wake na elimu ya kweli, lakini kukamilisha kazi yake haraka iwezekanavyo, ili kwamba aweze kupokea tuzo ambayo kazi yake ilikuwa imemwezesha kupata wakati alipokutana na Bwana Yesu. Alitumia kazi yake kujifariji, na kufanya makubaliano kwa ajili ya kupewa taji siku zijazo. Alichotafuta sio ukweli ama Mungu, lakini taji tu. Harakati kama hii inawezekanaje kuwa ya kiwangogezi? Motisha yake, kazi yake, gharama aliyolipa, na juhudi zake zote—ndoto zake za ajabu zilienea kote, na alifanya kazi kabisa kulingana na mapenzi yake. Katika ukamilifu wa kazi yake, hapakuwa na hiari kidogo ya gharama aliyolipa; alikuwa anashiriki kwenye mapatano tu. Juhudi zake hazikufanywa kwa hiari ili kutimiza wajibu wake, bali zilifanywa kwa hiari ili kutekeleza lengo la mapatano. Je, kuna thamani yoyote kwa jitihada kama hizo? Nani ambaye anaweza kusifu juhudi zake chafu? Nani ambaye ana moyo wa kujua juhudi kama hizi? Kazi yake ilijawa na ndoto za mbeleni, zilijawa na mipango ya ajabu, na hazikuwa na njia ya kubadilishia tabia ya kibinadamu. Ukarimu wake mwingi ulikuwa wa unafiki; kazi yake haikuleta maisha, lakini ilikuwa unyenyekevu bandia; lilikuwa tendo la maafikiano. Jinsi gani kazi kama hii kumwongoza mwanadamu kwenye njia ya kupata tena wajibu wake wa awali?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 481)

Yote ambayo Petro alitafuta yalikuwa kufuata Moyo wa Mungu. Alitaka kutimiza mapenzi ya Mungu, na licha ya taabu na mashaka, bado yeye alikuwa tayari kutimiza mapenzi ya Mungu. Hakuna ukimbizaji mkuu zaidi wa muumini katika Mungu. Kile ambacho Paulo alitafuta kilitiwa doa na mwili wake, na dhana zake mwenyewe, na mipango na mipangilio yake mwenyewe. Hakuwa kwa njia yeyote kiumbe wa Mungu aliyehitimu, hakuwa mtu ambaye alitaka kutimiza mapenzi ya Mungu. Petro alitaka kujiwasilisha kwenye mipango ya Mungu, na ingawa kazi aliyofanya haikuwa kuu, motisha ya harakati yake na njia ambayo alitembea zilikuwa sahihi; ingawa hakuweza kupata watu wengi, aliweza kufuata njia ya ukweli. Kwa hivyo inaweza kusemwa kwamba alikuwa kiumbe wa Mungu aliyehitimu. Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. Iwapo ulifanya kazi nyingi, na watu wengine walipata mafundisho yako, lakini wewe mwenyewe hukubadilika, na hukuwa na ushuhuda wowote, au kuwa na uzoefu wowote wa kweli, kwa namna kuwa katika hatima ya maisha yako, bado hakuna yoyote uliyofanya iliyo na ushuhuda, basi je, wewe ni mtu aliyebadilika? Je, wewe ni mtu ambaye hufuatilia ukweli? Wakati huo, Roho Mtakatifu alikutumia, lakini alipokutumia, alitumia sehemu yako ambayo ingeweza kutumika kufanya kazi, na wala hakutumia sehemu yako ambayo haingeweza kutumika kufanya kazi. Kama wewe ulitafuta kubadilika, basi ungeweza kufanywa mkamilifu hatua kwa hatua wakati wa mchakato wa kutumika. Hata hivyo Roho Mtakatifu hakubali jukumu la kama au la wewe mwishowe utapatwa, na hii inategemea na namna ya ukimbizaji wako. Iwapo hakuna mabadiliko katika tabia yako binafsi, basi hiyo ni kwa sababu mtazamo wako kuelekea kufuatilia ni mbaya. Kama hutatunukiwa tuzo, basi hilo ni tatizo lako, na kwa sababu wewe mwenyewe hujaweka ukweli katika vitendo, na huwezi kutimiza mapenzi ya Mungu. Na kwa hivyo, hakuna kitu cha umuhimu kama uzoefu wako wa kibinafsi, na hakuna kilicho cha maana kuliko kuingia kwako kibinafsi. Baadhi ya watu wataishia kusema, “Mimi nimefanya kazi nyingi kwa ajili yako, na ingawa kuna uwezekano kuwa hazikuwa na mafanikio ya kusherehekewa, bado nimekuwa mwenye jitihada kwenye juhudi zangu. Huwezi tu kuniruhusu niingie mbinguni ili nile tunda la uzima?” Ni lazima ujue aina ya watu ambao Ninataka; wale walio najisi hawakubaliki kuingia katika ufalme, wale walio najisi hawakubaliki kuchafua nchi takatifu. Ingawa unaweza kuwa umefanya kazi nyingi, na umefanya kazi kwa miaka mingi, mwishowe kama bado wewe ni mwovu kupindukia—hakuvumiliki kwa sheria ya Mbinguni kwamba wewe unataka kuingia katika ufalme wangu! Tangu mwanzo wa dunia hadi leo, kamwe Sijatoa njia rahisi ya kuingilia ufalme Wangu kwa wale wenye neema Yangu. Hii ni sheria ya Mbinguni, na hakuna awezaye kuivunja. Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao hutafuta mabadiliko katika tabia yao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee watakaofanywa wakamilifu. Kama wewe tu unatazamia tuzo, na hutafuti kubadilisha tabia ya maisha yako mwenyewe, basi juhudi zako zote zitakuwa za bure—na huu ni ukweli usiobadilika!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 482)

Kutoka kwa tofauti katika kiini cha Paulo na kiini cha Petro unapaswa kufahamu kuwa wale wote ambao hawafuati uzima wanafanya kazi ya bure! Unamwamini Mungu na unafuata Mungu, na kwa hivyo moyoni mwako ni lazima umpende Mungu. Ni lazima uache tabia yako potovu, lazima utafute kutimiza mapenzi ya Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako kama kiumbe wa Mungu. Kwa kuwa unamwamini na kumfuata Mungu, unapaswa kutoa kila kitu kwake, na hupaswi kufanya uamuzi au madai ya kibinafsi, na unapaswa kutimiza ukamilishaji wa mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa uliumbwa, unapaswa kumtii Bwana aliyekuumba, kwa kuwa wewe huna mamlaka kiasili juu yako mwenyewe, na huna uwezo wa kudhibiti hatima yako. Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye anamwamini Mungu, inapaswa utafute utakatifu na mabadiliko. Kwa kuwa wewe ni kiumbe wa Mungu, unapaswa kushika wajibu wako, na kuhifadhi nafasi yako, na ni lazima usivuke mpaka wa wajibu wako. Hii si kwa ajili ya kukuzuia, ama kukukandamiza kupitia mafundisho, bali ndiyo njia ambayo utaweza kutekelezea wajibu wako, na inaweza kufikiwa—na inapaswa kufikiwa—na wote wanaotenda haki. Ukilinganisha kiini cha Petro na kiini cha Paulo, basi utajua jinsi unapaswa kutafuta. Kati ya njia ambazo Petro na Paulo walitembea, njia moja ni ya kufanywa mkamilifu, na nyingine ni njia ya kutolewa katika mashindano; Petro na Paulo wanawakilisha njia mbili tofauti. Ingawa kila moja wao alipokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kila mmoja alipata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na kila mmoja alikubali kile alichokuwa ameaminiwa na Bwana Yesu, tunda lililozaliwa katika kila mmoja wao halikuwa sawa. Mmoja kwa kweli alizaa tunda, na mwingine hukuzaa tunda. Kutokana na kiini cha kila mmoja wao, kazi waliyofanya, hiyo walioonyesha kwa upande wa nje, na hatima yao ya mwisho, unapaswa kuelewa ni njia gani unayopaswa kuchukua, njia ambayo unapaswa kuchagua kuitembea. Walitembelea njia mbili ambazo dhahiri ni tofauti. Paulo na Petro, walikuwa mifano ya kila njia, na kwa hivyo tangu mwanzo walionekana kuwakilisha njia hizi mbili. Je, ni mawazo gani muhimu katika uzoefu wa Paulo, na ni kwa nini yeye hakufaulu? Je, ni pointi gani muhimu katika matukio ya Petro, na ni jinsi gani yeye alishuhudia kufanywa mkalifu? Ukilinganisha kile ambacho kila alijali kuhusu, basi utajua aina hasa ya mtu ambaye Mungu anamtaka, mapenzi ya Mungu ni gani, na tabia ya Mungu, ni mtu wa aina gani ambaye hatimaye atafanywa mkamilifu, na pia aina gani ya mtu hawezi kufanywa mkamilifu, nini tabia ya wale ambao watafanywa wakamilifu, na nini tabia ya wale ambao hawatafanywa wakamilifu—masuala haya ya kiini yanaweza kuonekana katika uzoefu wa Petro na Paulo. Mungu aliumba kila kitu, na hivyo yeye hufanya viumbe wote kuwa chini ya utawala wake, na kujiwasilisha kwenye utawala wake; Yeye ataamuru kila kitu, ili kila kitu kiwe mikononi mwake. Vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, pamoja na wanyama, mimea, mwanadamu, milima na mito, na maziwa—vyote ni lazima vije chini ya utawala Wake. Vitu vyote mbinguni na ardhini lazima zije chini ya utawala Wake. Haviwezi kuwa na hiari yoyote na vyote ni lazima vitii mipango Yake. Hii iliagizwa na Mungu, na ni mamlaka ya Mungu. Mungu huamuru kila kitu, na huagiza na kuainisha kila kitu, ambapo kila kimoja huainishwa kulingana na aina, na kutengewa nafasi zao zenyewe, kulingana na mapenzi ya Mungu. Bila kujali kitu ni kikubwa namna gani, hakuna kitu kinachoweza kumpita Mungu, na vitu vyote ambavyo vinamtumikia mwanadamu aliyeumbwa na Mungu, na hakuna kitu kinachothubutu kumuasi Mungu ama kumdai Mungu. Na kwa hivyo mwanadamu, kama kiumbe wa Mungu, ni lazima atekeleze wajibu wa mwanadamu. Bila kujali iwapo yeye ni bwana au mlindaji wa vitu vyote, bila kujali jinsi hadhi ya mwanadamu ni kuu miongoni mwa vitu vyote, bado yeye ni binadamu mdogo anayetawaliwa na Mungu, na si zaidi ya binadamu asiye na umuhimu, kiumbe wa Mungu, na kamwe hatawahi kuwa juu ya Mungu. Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji. Kama kile ambacho unatafuta ni ukweli, kile ambacho unatenda ni ukweli, na kile ambacho unafikia ni badiliko katika tabia yako, basi njia unayopitia ni sahihi. Iwapo utafutacho ni baraka za mwili, na kile unachoweka katika vitendo ni ukweli wa dhana zako mwenyewe, na iwapo hakuna mabadiliko katika tabia yako, na wewe si mtiifu kabisa kwa Mungu katika mwili, na bado unaishi kwenye mashaka, basi unachotafuta bila shaka kitakupeleka kuzimu, kwa kuwa njia ambayo unatembea ni njia ya kushindwa. Iwapo utafanywa mkamilifu ama utatolewa katika mashindano inategemea na harakati yako mwenyewe, ambayo pia ni kusema kuwa mafanikio au kushindwa kunategemea njia ambayo mwanadamu anapitia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Iliyotangulia: Kuingia Katika Uzima (II)

Inayofuata: Kuingia Katika Uzima (IV)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp