Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Siwezi Kusema Yote Yaliyo Moyoni Mwangu

I

Leo nimekutana na Wewe, matumaini yangu yote yametimia.

Nimefurahia utajiri wote katika kumbatio Lako la upendo na ukunjufu.

Moyo Wako hakika ni mzuri sana, upendo Wako unanivutia.

Kile Ulicho nacho na kile Ulicho, ni vya thamani sana kwangu.

Siwezi kuelezea, hakuna maneno:

Jinsi gani anavyopendeza Mwenyezi Mungu!

Unaishi hapa miongoni mwa wanadamu

na kuweka mifano kwa kila njia.

Upendo Wako ni mwenzi wangu.

Maneno Yako daima yananiruzuku.

Unasafisha na kunitakasa.

Katika kuteseka hukumu,

ninaonja utamu ulio ndani.

Katika upendo Wako wa kweli kwangu,

siwezi kusema yote yaliyo moyoni mwangu.

Nikiwa nimetakaswa, mimi ni Wako, nami nitakupenda milele!

II

Baada ya kustahimili dhoruba, nimeshikana na Wewe zaidi.

Kupitia mateso na usafishaji, moyo wangu umeamshwa.

Katika njia ya shida, nimejifunza kutii.

Sio tena baridi au mwasi, sasa ninajua mapenzi Yako.

Ingawa maneno Yako ni makali,

Una moyo wenye ukarimu zaidi.

Unafanya kazi kwa ajili ya hatima ya mwanadamu,

Unawasubiri warudi.

Upendo Wako ni mwenzi wangu.

Maneno Yako daima yananiruzuku.

Unasafisha na kunitakasa.

Katika kuteseka hukumu,

ninaonja utamu ulio ndani.

Katika upendo Wako wa kweli kwangu,

siwezi kusema yote yaliyo moyoni mwangu.

Nikiwa nimetakaswa, mimi ni Wako, nami nitakupenda milele!

Iliyotangulia:Kuwa Mtu Mpya na Uuliwaze Moyo wa Mungu

Inayofuata:Anga Hapa ni Samawati Sana

Maudhui Yanayohusiana

 • Njia Yote Pamoja na Wewe

  I Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini. Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza. Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako, nina ama…

 • Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  Ⅰ Mnyenyekevu na Uliyejificha, Wewe unaambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwe…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…

 • Nitampenda Mungu Milele

  Ⅰ Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Majaribu mengi na uchungu, dhiki nyingi s…