233 Thamini Sana Nyakati za Mwisho

1 Kufumba na kufumbua, sikugundua kuwa nilikuwa namwamini Mungu miaka hii yote. Ninapoona kwamba kazi Yake inakaribia kumalizika, natafakari ikiwa nimepata ukweli na uzima. Sijui la kusema, sijui naweza kujieleza vipi kwa Mungu. Nimesoma maneno ya Mungu mara nyingi sana, nimefanya mambo kwa namna isiyo ya dhati bila kutafakari kwa makini. Mara nyingi baada ya kupogolewa na kushughulikiwa, sijatafuta ukweli. Miaka mingi sana ya kujitoa na kujitumia, nilifikiria kuwa nilikuwa mwaminifu kwa Mungu. Kuchambua kwa uangalifu nia yangu, yote imekuwa kutafuta sifa na hadhi. Mungu alitamka maneno mengi sana, lakini nimeelewa ukweli mdogo tu. Nimekabili majaribio mengi sana, usafishaji mwingi sana, lakini tabia yangu haijabadilika. Sasa kwa kuwa Mungu yu karibu kuondoka, moyo wangu uliokufa ganzi umezinduka ghafla. Nimepoteza nafasi nyingi sana za kukamilishwa kutokana na kutofuatilia ukweli.

2 Mungu atarudi Sayuni, maafa makubwa yatatokea. Mungu bado ana wasiwasi juu ya uchanga wetu maishani. Anatusihi kwa bidii tufuatilie ukweli bila kupoteza wakati. Muda baada ya muda, hukumu na kuadibu vinaamsha moyo wangu uliokufa ganzi. Nalia kwa kuona maneno yote ya Mungu ya dhati. Ili kuwaokoa wanadamu Mungu amelipa gharama kubwa sana. Kama kweli ningekuwa na mantiki na dhamiri ningewezaje kuasi tena na kumjeruhi Mungu? Nisipofuatilia ukweli bado, nitakuwa nimepungukiwa na ubinadamu, nisistahili kuishi. Tabia ya Mungu ni ya haki na takatifu na haitavumilia makosa ya wanadamu. Kufanya tu kazi, kuhudumu, bila kupata ukweli, nawezaje kuokolewa? Ninaachwa na majuto mengi sana kutoka kwa mambo ya zamani, moyo wangu umejaa majuto. Nitathamini sana nyakati za mwisho, nitafuatilia ukweli ili kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu na kumridhisha Mungu.

Iliyotangulia: 232 Mungu Amengoja Kwa Muda Mrefu Sana

Inayofuata: 234 Kuwa Mtu Mpya na Uuliwaze Moyo wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp