Kuhusu Majina na Utambulisho

Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu. Mtu fulani anaweza kukuuliza kuhusu kile Mungu wenu amesema kuhusu Biblia, Agano la Kale, na kazi na maneno ya Yesu ya wakati huo. Ikiwa huwezi kunena kwa hadithi ya ndani ya Biblia, basi hawatashawishika. Mwanzoni, Yesu alizungumzia sana Agano la Kale na wanafunzi Wake. Kila kitu walichosoma kilitoka Agano la Kale; Agano Jipya liliandikwa tu miongo kadhaa baada ya kusulubiwa kwa Yesu. Kueneza injili, mnapaswa hasa kufahamu ukweli wa ndani wa Biblia, na kazi ya Mungu katika Israeli, ndiyo kusema kazi Aliyoifanya Yehova. Na pia mnapaswa kuelewa kazi aliyoifanya Yesu. Haya ndiyo sanasana maswala ambayo watu wote wana wasiwasi nayo, na hadithi ya ndani ya zile hatua mbili za kazi ndiyo hawajasikia. Wakati wa kueneza injili, kwanza weka kando majadiliano juu ya kazi ya Roho Mtakatifu leo. Hii hatua ya kazi hawawezi kufikia, kwa sababu mnachotafuta ni kile kilicho juu kuliko zote: maarifa ya Mungu, na maarifa ya kazi ya Roho Mtakatifu, na hakuna kilichopandishwa cheo zaidi ya hizi mbili. Ukizungumzia kwanza kilicho juu, itakuwa ni kubwa mno kwao, kwani hakuna ambaye amepitia kazi kama hiyo ya Roho Mtakatifu; haina historia, na si rahisi kwa mwanadamu kukubali. Uzoefu wao ni mambo ya kale kutoka zamani, pamoja na baadhi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Wanayopitia si kazi ya leo ya Roho Mtakatifu, ama mapenzi ya Mungu leo. Bado wanatenda kulingana na mazoea ya kale, bila mwangaza mpya wala mambo mapya.

Katika enzi ya Yesu, Roho Mtakatifu hasa alifanya kazi Yake ndani ya Yesu, wakati wale waliomtumikia Bwana wakivaa mavazi ya kuhani hekaluni walifanya hivyo kwa uaminifu uliodumu. Wao pia walikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, lakini hawakuweza kuhisi mapenzi ya sasa ya Mungu, na wakabakia tu waaminifu kwa Yehova kulingana na mazoea ya kale, bila uongozi mpya. Yesu alikuja na kuleta kazi mpya. Wale watu waliohudumu hekaluni hawakuwa na uongozi mpya wala hawakuwa na kazi mpya. Wakihudumu hekaluni wangeweza tu kutetea mazoea ya kale; bila kuondoka hekaluni, hawangeweza kuwa na kuingia kupya. Kazi mpya ililetwa na Yesu, na Yesu hakuingia hekaluni kufanya kazi Yake. Alifanya kazi yake nje ya hekalu pekee, kwani wigo wa kazi ya Mungu ulikuwa umebadilika kitambo sana. Hakufanya kazi ndani ya hekalu, na mwanadamu alipomtumikia hapo ingeweza tu kuweka mambo yalivyokuwa, na haingeleta kazi yoyote mpya. Vivyo hivyo, watu wa dini bado huabudu Biblia leo. Ukieneza injili kwao, watakurushia maelezo ya juujuu ya maneno ya Biblia na watapata ushahidi mwingi, wakikuacha umezubaa na usijue la kusema; kisha watawawekea kipachiko and kuwaona kuwa wapumbavu katika imani yenu. Watasema, “Hujui hata Biblia, neno la Mungu, na unawezaje sema unamwamini Mungu?” Kisha watakudharau, na pia kusema, “Sababu mnayemwamini ni Mungu, mbona Asiwaeleze yote kuhusu Agano la Kale na Jipya? Sababu Ameleta utukufu Wake kutoka Israeli hadi upande wa Mashariki, mbona hajui kazi iliyofanywa Israeli? Mbona hajui kazi ya Yesu? Kama hamjui, basi inathibitisha kwamba hamjaelezwa; sababu Yeye ndiye kupata mwili kwa Yesu kwa mara ya pili, ingewezekanaje kuwa hajui mambo haya? Yesu alijua kazi aliyoifanya Yehova; Angekosaje?” Wakati utakapofika, wote watakuuliza maswali kama haya. Vichwa vyao vimejaa mambo kama haya; watakosaje kuuliza? Wale walio katika mkondo huu hawazingatii Biblia, kwa vile mmetazama hatua kwa hatua kazi aliyoifanya Mungu leo, mmeshuhudia hii kazi ya hatua kwa hatua kwa macho yenu, mmeona wazi hatua tatu za kazi, na kwa hivyo imewabidi kuweka chini Biblia na kukoma kuitafiti. Lakini hawawezi kukosa kuitafiti, kwani hawana ujuzi wa hii kazi ya hatua kwa hatua. Watu wengine watauliza, “Nini tofauti kati ya kazi aliyoifanya Mungu wa mwili na ile ya manabii na mitume wa zamani? Daudi pia aliitwa Bwana, na hivyo pia akawa Yesu; ingawa kazi waliyoifanya ilikuwa tofauti, waliitwa kitu kimoja. Mbona, unauliza, hawakuwa na utambulisho mmoja? Kile Yohana alichoshuhudia kilikuwa maono, moja iliyotoka pia kwa Roho Mtakatifu, na aliweza kuyasema maneno ambayo Roho Mtakatifu alikusudia kuyasema; kwa nini utambulisho wa Yohana ni tofauti na ule wa Yesu?” Maneno aliyoyasema Yesu yaliweza kumwakilisha Mungu kikamilifu, na kuwakilisha kikamilifu kazi ya Mungu. Kile alichokiona Yohana kilikuwa maono, na hakuweza kuwakilisha kikamilifu kazi ya Mungu. Ni kwa nini Yohana, Petro na Paulo walizungumza maneno mengi—kama alivyofanya Yesu—lakini bado hawakuwa na utambulisho sawa na Yesu? Ni hasa kwa sababu kazi waliyoifanya ilikuwa tofauti. Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe. Ilhali kwa Petro, Paulo na Daudi, bila kujali walichoitwa, waliwakilisha tu utambulisho wa kiumbe wa Mungu, na walitumwa na Yesu na Yehova. Kwa hivyo bila kujali kiasi cha kazi walichofanya, bila kujali jinsi walivyofanya miujiza kubwa, walikuwa bado tu viumbe wa Mungu, na hawakuweza kuwakilisha Roho Mtakatifu. Walifanya kazi kwa jina la Mungu ama baada ya kutumwa na Mungu; zaidi ya hayo, walifanya kazi katika enzi iliyoanzishwa na Yesu ama Yehova, na kazi waliyoifanya haikutengwa. Walikuwa, hatimaye, viumbe wa Mungu tu. Katika Agano la Kale, manabii wengi walizungumza utabiri, ama kuandika vitabu vya unabii. Hakuna aliyesema kuwa yeye ni Mungu, lakini punde tu Yesu Alipoanza kufanya kazi, Roho wa Mungu Alimshuhudia kuwa Yeye ni Mungu. Mbona hivyo? Kwa sasa, unapaswa kujua tayari! Awali, mitume na manabii waliandika nyaraka mbalimbali, na kufanya unabii mwingi. Baadaye, watu walichagua baadhi zao kuweka katika Biblia, na baadhi zikapotea. Kwa vile kuna watu wanaosema kuwa vitu vyote wanavyozungumza vimetoka kwa Roho Mtakatifu, mbona baadhi yavyo vinachukuliwa kuwa nzuri, na baadhi yavyo vinachukuliwa kuwa mbaya? Na mbona baadhi vilichaguliwa, na sio vingine? Kama kweli yalikuwa maneno Aliyoyasema Roho Mtakatifu, ingekuwa lazima kwa watu kuyachagua? Kwa nini akaunti ya maneno yaliyosemwa na Yesu na kazi Aliyoifanya ni tofauti katika kila moja ya Injili Nne? Makosa sio ya waliyoyarekodi? Watu wengine watauliza, “Sababu nyaraka zilizoandikwa na Paulo na waandishi wengine wa Agano Jipya na kazi walizozifanya zilitokana kidogo na matakwa ya mwanadamu, na zilichanganywa na dhana za mwanadamu, basi hakuna uchafu wa binadamu katika maneno ambayo Wewe (Mungu) unazungumza leo? Je, kweli hayana dhana hata moja za mwanadamu?” Hii hatua ya kazi aliyoifanya Mungu ni tofauti kabisa na zile walizozifanya Paulo na wengi wa mitume na manabii. Sio tu kwamba kuna tofauti na utambulisho, lakini, hasa, kuna tofauti kati ya kazi inayofanywa. Baada ya Paulo kupigwa chini na kuanguka mbele ya Bwana, aliongozwa na Roho Mtakatifu kufanya kazi, na akawa mtume. Na hivyo akaandikia makanisa nyaraka, na hizi nyaraka zote zilifuata mafundisho ya Yesu. Paulo alitumwa na Bwana kufanya kazi kwa jina la Bwana Yesu, lakini Mungu Mwenyewe alipokuja, Hakufanya kazi kwa jina lolote na Hakuwakilisha yeyote isipokuwa Roho wa Mungu katika kazi Yake. Mungu alikuja kufanya kazi Yake moja kwa moja: Hakukamilishwa na mwanadamu, na kazi Yake haikufanywa juu ya mafundisho ya mwanadamu yeyote. Katika hatua hii ya kazi Mungu haongozi kwa kuzungumza juu ya uzoefu Wake binafsi, ila Hufanya kazi Yake moja kwa moja, kulingana na Alicho nacho. Kwa mfano, jaribio la watoa huduma, nyakati za kuadibu, jaribio la kifo, nyakati za kumpenda Mungu…. Hii yote ni kazi ambayo haijawahi kufanywa mbeleni, na ni kazi ya enzi ya sasa, badala ya uzoefu wa binadamu. Kwa maneno Nimesema, ni yapi mazoefu ya mwanadamu? Je, yote hayatoki moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, na hayatolewi nje na Roho Mtakatifu? Ni vile tu aina yako ni maskini sana hadi huwezi kuona kupitia ukweli! Maisha ya vitendo Ninayozungumzia ni ya kuongoza njia, na hayajawahi zungumziwa na yeyote mbeleni, wala hakuna aliye na uzoefu wa njia hii, wala kujua ukweli huu. Kabla Niliyatamka maneno haya, hakuna aliyewahi kuyasema. Hakuna aliyezungumzia mazoefu haya, wala hakuna aliyewahi kusema maelezo hayo, na, zaidi ya hayo, hakuna aliyewahi kuonyesha hali kama hizo kufichua mambo haya. Hakuna aliyewahi kuongoza njia Ninayoongoza leo, na kama ingeongozwa na mwanadamu, basi isingekuwa njia mpya. Chukua Paulo na Petro, kwa mfano. Hawakuwa na uzoefu wao binafsi kabla ya Yesu aiongoze njia. Ilikuwa tu baada ya Yesu kuongoza njia ndipo walipopata uzoefu wa maneno aliyoyasema Yesu, na njia aliyoiongoza; kutoka hapa walipata mazoefu mengi, na kuziandika nyaraka, Na hivyo, uzoefu wa mwanadamu sio sawa na kazi Ya Mungu, na kazi ya Mungu sio sawa na maarifa yalivyoelezwa na dhana na uzoefu wa mwanadamu. Nimesema, tena na tena, kuwa leo Ninaongoza njia mpya, na kufanya kazi mpya, na kazi na matamshi Yangu ni tofauti na yale ya Yohana na wale manabii wengine wote. Kamwe, Sijawahi pata uzoefu kwanza, na kisha kuyazungumzia kwenu—hiyo sio ukweli hata kidogo. Kama ingekuwa hivyo, haingewachelewesha kitambo sana? Zamani, maarifa waliyoyazungumzia wengi yalipandishwa cheo pia, lakini maneno yao yote yalisemwa tu kulingana na hayo ya wanaoitwa takwimu wa kiroho. Hawakuiongoza njia, lakini walitoka kwa uzoefu wao, walitoka kwa walichokiona, na kwa maarifa yao. Zingine zilikuwa dhana zao, na mengine yalikuwa mazoefu waliyofupisha. Leo, asili ya kazi Yangu ni tofauti kabisa na yao. Sijapata uzoefu wa kuongozwa na wengine, wala Sijakubali kukamilishwa na wengine. Zaidi ya hayo, yote Nimesema na kushiriki ni tofauti na yale ya wengine, na hayajawahi kuzungumzwa na mwingine yeyote. Leo, bila kujali ninyi ni nani, kazi yenu inafanywa kulingana na maneno Nisemayo. Bila haya matamshi na kazi, nani angeweza kupata uzoefu wa mambo haya (majaribu ya watendaji huduma, nyakati za kuadibu…), na nani ataweza kuzungumzia maarifa kama haya? Kweli huna uwezo wa kuona haya? Bila kujali hatua ya kazi, punde tu maneno Yangu yasemwapo, mnaanza kushiriki kulingana na maneno Yangu, na kufanya kazi kulingana nayo, na sio njia ambayo yeyote kati yenu amefikiria. Baada ya kuja mbali hivi, huna uwezo wa kuona swali wazi na rahisi hivi? Sio njia iliyowazwa na yeyote, wala haijalinganishwa na mtu yeyote wa kiroho. Ni njia mpya, na hata maneno mengi yaliyosemwa mara kwanza na Yesu hayatumiki tena. Ninachozungumza ni kazi ya kufungua enzi mpya, na ni kazi inayosimama peke yake; kazi Nifanyayo, na maneno Nizungumzayo, yote ni mapya. Si hii ndiyo kazi mpya ya leo? Kazi ya Yesu pia ilikuwa hivi. Kazi Yake pia ilikuwa tofauti na hizo za watu wengine hekaluni, na pia ilitofautiana na kazi za Mafarisayo, na wala haikufanana na zilizofanywa na watu wote wa Israeli. Baada ya kuishuhudia, watu walishindwa kuamua: “Kweli ilifanywa na Mungu?” Yesu hakuzingatia sheria ya Yehova; Alipokuja kumfunza mwanadamu, yote Aliyoyanena yalikuwa mapya na tofauti na yale yaliyosemwa na watakatifu wa zamani na manabii wa Agano la Kale, na kwa sababu hii, watu walisalia bila uhakika. Hii ndiyo humfanya mwanadamu kuwa mgumu sana kushughulika naye. Kabla ya kukubali hii hatua mpya ya kazi, njia ambayo wengi wenu walitembelea ilikuwa ya kutenda na kuingia katika msingi wa watu hao wa kiroho. Lakini leo, kazi Ninayoifanya ni tofauti sana, na hivyo hamna uwezo wa kuamua kama ni sawa ama sio. Sijalishwi na njia uliyopitia mbeleni, wala Sijali ulikula “chakula” cha nani, ama uliyemchukua kama “babako.” Sababu Nimekuja na kuleta kazi mpya ya kumwongoza mwanadamu, wote wanaonifuata lazima watende kulingana na Ninachosema. Bila kujali jinsi ulivyotoka “familia” ya nguvu, lazima unifuate, hupaswi kutenda kulingana na mazoea yako ya awali, “Baba wa kambo” wako anapaswa kushuka nawe unapaswa kuja mbele ya Mungu wako kupata mgao wako halali. Uzima wako wote umo mikononi Mwangu, nawe hupaswi kuwa na imani kipofu nyingi kwa baba wako wa kambo, hawezi kukutawala kabisa. Kazi ya leo inasimama peke yake. Yote Nisemayo leo ni wazi hayajalinganishwa na msingi wa zamani; ni mwanzo mpya, na ukisema kuwa umetengenezwa na mkono wa mwanadamu, basi wewe ni mtu aliye kipofu sana kwamba huwezi kuokolewa!

Isaya, Ezekieli, Musa, Daudi, Ibrahimu na Danieli walikuwa viongozi ama manabii kati ya wateule wa Israeli. Mbona hawakuitwa Mungu? Mbona Roho Mtakatifu hakuwashuhudia? Mbona Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu punde tu Alipoanza kazi yake na kuanza kuzungumza maneno Yake? Na mbona Roho Mtakatifu hakuwashuhudia wengine? Wao, wanadamu waliokuwa na mwili, wote waliitwa “Bwana.” Bila kujali waliyoitwa, kazi yao inawakilisha utu wao na kiini chao, na utu wao na kiini chao kinawakilisha utambulisho wao. Kiini chao hakina uhusiano na majina yao, inawakilishwa na waliyoonyesha, na waliyoishi kwa kudhihirisha. Kwa Agano la Kale, hakuwa na chochote tofauti na kuitwa Bwana, na mtu angeitwa kwa njia yoyote, lakini kiini na utambulisho wake wa asili ulikuwa haubadiliki. Kati ya hao Kristo wa uwongo, manabii waongo na wadanganyifu, hakuna wanaoitwa “Mungu” pia? Na mbona hao sio Mungu? Kwa sababu hawana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu. Mizizini, wao ni wanadamu, wanaowadanganya watu, sio Mungu, na hivyo hawana utambulisho wa Mungu. Daudi pia hakuitwa Bwana miongoni mwa makabila kumi na mawili? Yesu pia aliitwa Bwana: mbona ni Yesu pekee aliyeitwa Mungu wa mwili? Yeremia pia hakujulikana kama Mwana wa Adamu? Na Yesu pia hakujulikana kama Mwana wa Adamu? Mbona Yesu alisulubiwa kwa niaba ya Mungu? Si kwa sababu kiini chake kilikuwa tofauti? Si kwa sababu kazi aliyoifanya ilikuwa tofauti? Je, jina lina umuhimu? Ingawa Yesu pia aliitwa Mwana wa Adamu, Alikuwa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya kwanza. Alikuwa amekuja kuchukua mamlaka, na kukamilisha kazi ya ukombozi. Hii inathibitisha kuwa utambulisho na kiini cha Yesu kilikuwa tofauti na kile cha wengine walioitwa pia wana wa wanadamu. Leo, nani kati yenu anathubutu kusema kwamba maneno yote yaliyotamkwa na wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kuna anayethubutu kusema mambo kama haya? Ukisema mambo kama haya, basi mbona kitabu cha Ezra cha unabii kiliondolewa, na mbona jambo hilo pia likafanyiwa vitabu vya watakatifu na manabii wa kale? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, basi mbona mnathubutu kufanya maamuzi ambayo yanabadilika kama haya? Umehitimu kuchagua kazi ya Roho Mtakatifu? Hadithi nyingi kutoka Israeli pia zilitolewa. Na ukiamini kwamba maandishi haya yote ya kale yalitoka Roho Mtakatifu, basi mbona baadhi ya vitabu vilitolewa? Kama yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu, yote yanapaswa kuwekwa, na kutumwa kwa ndugu na dada wa makanisa kuyasoma. Hayapaswi kuchaguliwa na kutolewa kwa matakwa ya mwanadamu; ni makosa kufanya hivyo. Kusema kwamba mazoefu ya Paulo na Yohana yalichanganywa na waliyoyaona binafsi hakumaanishi kwamba uzoefu na maarifa yao yalitoka kwa Shetani, ila tu walikuwa na mambo yaliyotoka kwa mazoefu na waliyoyaona wao binafsi. Maarifa yao yalilingana na asili ya mazoefu halisi ya wakati huo, na ni nani anayeweza kusema kwa ujasiri kwamba yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu? Kama Injili Nne zote zilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi ilikuwaje kwamba Mathayo, Marko, Luka na Yohana kila mmoja alisema jambo tofauti kuhusu kazi ya Yesu? Msipoamini haya, basi angalia akaunti tofauti kwa Biblia ya jinsi Petro alivyomkana Yesu mara tatu: Yote ni tofauti, na kila moja ina sifa yake yenyewe. Wengi walio wajinga husema, “Mungu wa mwili pia ni mwanadamu, kwa hivyo maneno Anayoyazungumza yanaweza kutoka kikamilifu kwa Roho Mtakatifu? Kama maneno ya Paulo na Yohana yalichanganywa na matakwa ya mwanadamu, basi maneno Anayoyasema kweli hayajachanganywa na matakwa ya mwanadamu?” Watu wanaosema mambo kama haya ni vipofu na wajinga! Soma Injili Nne kwa kina; soma iliyorekodi kuhusu alichofanya Yesu, na maneno Aliyoyasema. Kila akaunti ilikuwa kwa urahisi tofauti, na kila ilikuwa na mtazamo wake. Kama vilivyoandikwa na waandishi wa vitabu hivi vyote vilitoka kwa Roho Mtakatifu, basi yote yanapaswa kuwa sawa na thabiti. Basi mbona kuna tofauti? Si mwanadamu ni mjinga sana, kutoweza kuona haya? Ukiulizwa kutoa ushuhuda kwa Mungu, ni ushuhuda upi unaoweza kutoa? Njia hii ya kumjua Mungu inaweza kumshuhudia? Wengine wakikuuliza, “Kama rekodi ya Yohana na Luka yalichanganywa na matakwa ya mwanadamu, basi maneno yanayosemwa na Mungu wenu hayajachanganywa na matakwa ya mwanadamu?” utaweza kupeana jibu wazi? Baada ya Luka na Mathayo kuyasikia maneno ya Yesu, na kuona kazi ya Yesu, walizungumzia maarifa yao, kwa namna ya kumbukumbu walisema kwa kina baadhi ya mambo aliyoyafanya Yesu. Unaweza kusema kwamba maarifa yao yalifichuliwa kabisa na Roho Mtakatifu? Nje ya Biblia, kulikuwa na watu wengi wa kiroho wa maarifa ya juu kuwaliko; mbona maneno yao hayajachukuliwa na vizazi vya baadaye? Wao hawakutumika pia na Roho Mtakatifu? Jua kwamba kwa kazi ya leo, Sizungumzii juu ya kuona kwangu kunaolingana na msingi wa kazi ya Yesu, wala Sizungumzi juu ya maarifa Yangu dhidi ya usuli wa kazi ya Yesu. Ni kazi ipi Aliyofanya Yesu wakati huo? Na ni kazi ipi Ninayofanya leo? Ninachofanya na kusema hayana historia. Njia Nitembeleayo leo haijawahi kukanyagiwa mbeleni, haikuwahi tembelewa na watu wa enzi na vizazi vya kale. Leo, imefunguliwa, na hii sio kazi ya Roho? Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu, viongozi wote wa kale walifanya kazi yao juu ya msingi wa wengine. Hata hivyo, kazi ya Mungu Mwenyewe ni tofauti. Hatua ya kazi ya Yesu ilikuwa sawa: Aliifungua njia mpya. Alipokuja Alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni, na kusema kwamba mwanadamu anapaswa kutubu na kukiri. Baada ya Yesu kukamilisha kazi yake, Petro na Paulo na wengineo walianza kuendeleza kazi ya Yesu. Baada ya Yesu kusulubiwa na kupaa mbinguni, walitumwa na Roho Mtakatifu kueneza njia ya msalaba. Ingawa maneno ya Paulo yalipandishwa cheo, pia yalilingana na msingi uliolazwa na kile Yesu alisema, kama uvumilivu, upendo, mateso, kufunika kichwa, ubatizo, ama mafundisho mengine yakufuatwa. Haya yote yalikuwa juu ya msingi wa maneno ya Yesu. Hawakuwa na uwezo wa kufungua njia mpya, kwani wote walikuwa wanadamu waliotumiwa na Mungu.

Matamshi na kazi ya Yesu wakati huo hayakushikilia mafundisho, na hakufanya kazi Yake kulingana na kazi ya sheria ya Agano la Kale. Yalilingana na kazi iliyopaswa kufanywa kwa Enzi ya Neema. Alitenda kulingana na kazi Aliyokuwa ameleta mbele, kulingana na mipango Yake, na kulingana na huduma Yake; Hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale. Hakuna Alichofanya kilicholingana na Agano la Kale, na Hakuja kufanya kazi ili kutimiza maneno ya manabii. Kila hatua ya kazi ya Mungu haikuwa wazi ili kutimiza utabiri wa manabii wa zamani, na Hakuja kuyafuata mafundisho au kutambua makusudi utabiri wa manabii wa kale. Bado vitendo Vyake havikuvuruga utabiri wa manabii wa kale, wala havikuvuruga kazi Aliyokuwa amefanya awali. Hatua muhimu ya kazi Yake haikuwa kufuata mafundisho yoyote, na kufanya kazi ambayo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya. Yeye hakuwa nabii wala mwaguzi, ila mtendaji, aliyekuja kufanya hiyo kazi Aliyopaswa kufanya, na aliyekuja kufungua enzi Yake mpya na kufanya kazi Yake mpya. Bila shaka, Yesu alipokuja kufanya kazi Yake, pia Alitimiza maneno mengi yaliyosemwa na manabii wa zamani kwa Agano la Kale. Hivyo pia kazi ya leo imetimiza utabiri wa manabii wa zamani wa Agano la Kale. Ni vile tu Sishikilii hiyo “kalenda njano ya zamani,” hayo tu. Kwani kuna kazi zaidi ambayo lazima Nifanye, kuna maneno zaidi ambayo lazima Niwazungumzie, na kazi hii na maneno haya ni ya umuhimu mkubwa kuliko kueleza vifungu kutoka Biblia, kwa sababu kazi kama hiyo haina maana ama thamani kubwa kwenu, na haiwezi kuwasaidia, au kuwabadilisha. Ninanuia kufanya kazi mpya sio kwa ajili ya kutimiza kifungu chochote kutoka Biblia. Ikiwa Mungu alikuja duniani tu kutimiza maneno ya manabii wa Biblia, basi ni nani aliye mkuu, Mungu wa mwili ama hao manabii wa zamani. Na hata hivyo, hao manabii ni wasimamizi wa Mungu, ama Mungu ni msimamizi wa manabii? Unaweza kueleza haya maneno jinsi gani?

Mwanzoni, wakati Yesu alikuwa bado hajafanya rasmi huduma Yake, kama wanafunzi waliomfuata, wakati mwingine pia Yeye alihudhuria mikutano, na kuimba tenzi, Akasifu, na kusoma Agano la Kale kwa hekalu. Baada Yeye kubatizwa na kupanda, Roho alishuka rasmi juu yake na kuanza kufanya kazi, Akifichua utambulisho Wake na huduma Aliyokuwa afanye. Kabla ya haya, hakuna aliyejua utambulisho Wake, na mbali na Maria, hata Yohana hakujua. Yesu alikuwa 29 Alipobatizwa. Baada ya ubatizo wake kukamilika, mbingu zilifunguliwa, na sauti ikasema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Baada ya Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu alianza kumshuhudia kwa njia hii. Kabla ya kubatizwa Akiwa na umri wa 29, Alikuwa ameishi maisha ya ukawaida wa mtu, kula wakati Alipotakiwa kula, kulala na kuvaa kawaida, na hakuna chochote kumhusu kilikuwa tofauti. Bila shaka hii ilikuwa tu kwa nyama ya macho ya mwanadamu. Wakati mwingine Alikuwa mnyonge sana, na wakati mwingine Hakuweza kupambanua mambo, kama tu ilivyoandikwa kwa Biblia Akili Yake ilikua pamoja na umri Wake. Haya maneno yanaonyesha tu kwamba Alikuwa na ubinadamu na kwamba Hakuwa hasa na tofauti na watu wengine ambao ni wa kawaida. Alikuwa pia amelelewa kama mtu wa kawaida, na hakuwa na chochote maalum kumhusu. Hata hivyo Alikuwa chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu. Baada ya kubatizwa, Alianza kujaribiwa, baada yake Akaanza kufanya Huduma Yake na kufanya kazi, na Alimiliki nguvu, hekima, na mamlaka. Hii si kusema kwamba Roho Mtakatifu hakufanya kazi ndani Yake kabla ya ubatizo Wake, ama hakuwa ndani Yake. Kabla ya ubatizo Wake Roho Mtakatifu pia aliishi ndani Yake lakini Hakuwa ameanza rasmi kazi Yake, kwani kuna mipaka ya wakati Mungu afanyapo kazi Yake, na zaidi ya hayo, watu wa kawaida wana mwendo kawaida wa kukua. Roho Mtakatifu alikuwa daima anaishi ndani Yake, Yesu alipozaliwa, Alikuwa tofauti na wengine, na nyota ya asubuhi ilionekana; kabla Yeye kuzaliwa, malaika alimtokea Yusufu kwa ndoto na kumweleza kuwa Maria angejifungua mtoto wa kiume, na kwamba mtoto huyo alipatwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Baada ya Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu Alianza kazi Yake, lakini hili halimaanishi kwamba Roho Mtakatifu alikuwa tu amemshukia Yesu wakati huo. Huo msemo kwamba Roho Mtakatifu alishuka kama njiwa juu yake inamaanisha kuanza rasmi kwa huduma Yake. Roho wa Mungu alikuwa ndani yake mbeleni, lakini Hakuwa ameanza kufanya kazi, kwani wakati hukuwa umefika, na Roho hakuanza kazi upesi. Roho alimshuhudia kupitia ubatizo. Alipotoka nje ya maji, Roho alianza rasmi kufanya kazi ndani Yake, iliyoashiria kuwa Mungu wa mwili alikuwa ameanza kutimiza huduma Yake, na alikuwa ameanza kazi ya ukombozi, hiyo ni, Enzi ya Neema ilikuwa imeanza rasmi. Na hivyo, kuna wakati wa kazi Ya Mungu, bila kujali kazi Anayoifanya. Baada ya ubatizo Wake, hakukuwa na mabadiliko fulani kwa Yesu; Alikuwa bado ndani ya mwili wake kawaida. Ni kwamba tu alianza kazi Yake na kufichua utambulisho wake, na Alijawa na mamlaka na nguvu. Kwa swala hili, Alikuwa tofauti kuliko awali. Utambulisho wake ulikuwa tofauti, kusema kwamba kulikuwa na mabadiliko muhimu kwa hadhi Yake; huu ulikuwa ushahidi wa Roho Mtakatifu, na haikuwa kazi iliyofanywa na mwanadamu. Mwanzoni, watu hawakujua, na walikuja kujua kidogo wakati Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu kwa njia hiyo. Kama Yesu angekuwa amefanya kazi kubwa kabla ya Roho Mtakatifu kumshuhudia, lakini bila shuhuda ya Mungu Mwenyewe, basi bila kujali jinsi kazi Yake ilivyokuwa kubwa, watu hawangejua kuhusu utambulisho Wake, kwani jicho la mwanadamu halingekuwa na uwezo wa kuiona. Bila hatua ya ushuhuda wa Roho Mtakatifu, hakuna ambaye angemtambua kama Mungu wa mwili. Kama, baada ya Roho Mtakatifu kumshuhudia, Yesu angeendelea kufanya kazi kwa njia hiyo hiyo, bila tofauti yoyote, basi haingekuwa na athari hiyo, na hii hasa imeonyeshwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu pia. Baada ya Roho Mtakatifu kuwa na ushuhuda, Roho Mtakatifu alipaswa kujionyesha Mwenyewe, ili uweze kuona wazi kuwa Alikuwa Mungu, kwamba kulikuwa na Roho wa Mungu ndani Yake; ushuhuda wa Mungu hukukosea, na hii ingethibitisha kwamba ushuhuda Wake ulikuwa sahihi. Iwapo kazi ya kabla na baada ya ushuhuda wa Roho Mtakatifu ingekuwa sawa, basi huduma Yake ya mwili na kazi ya Roho Mtakatifu hazingekuwa maarufu, na hivyo mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kutambua kazi ya Roho Mtakatifu, kwani hakuwa na tofauti wazi. Baada ya kuwa na ushuhuda, Roho Mtakatifu alilazimika kutetea huu ushuhuda, na hivyo ilimlazimu kuonyesha hekima na mamlaka Yake ndani ya Yesu, ambayo ilikuwa tofauti na wakati wa kale. Bila shaka, hii haikuwa athari ya ubatizo; ubatizo ni sherehe tu, ni kwamba tu ubatizo ulikuwa njia ya kuonyesha kwamba ulikuwa wakati wa kufanya huduma Yake. Kazi hiyo ilikuwa ya kufanya wazi nguvu kubwa za Mungu, kufanya wazi ushuhuda wa Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu angechukua jukumu la ushuhuda huu mpaka mwisho. Kabla ya kufanya huduma Yake, Yesu pia alisikiliza mahubiri, Alihubiri na kueneza injili katika maeneo mbalimbali. Hakufanya kazi yoyote kubwa kwa sababu muda bado hukuwa umewadia ili Afanye huduma Yake, na pia kwa sababu Mungu Mwenyewe alijificha kwa unyenyekevu ndani ya mwili, na Hakufanya kazi yoyote hadi wakati ulipofika. Hakufanya kazi kabla ya ubatizo kwa sababu mbili: Kwanza, kwa sababu Roho Mtakatifu hakuwa ameshuka rasmi juu Yake kufanya kazi (ndiyo kusema, Roho Mtakatifu hakuwa amempea Yesu nguvu na mamlaka ya kufanya kazi kama hii), na hata kama Angekuwa anajua utambulisho Wake Mwenyewe, Yesu hangeweza kufanya kazi Aliyonuia kufanya baadaye, na ingembidi kusubiri hadi siku Yake ya ubatizo. Huu ulikuwa wakati wa Mungu, na hakuna ambaye angeweza kuikiuka, hata Yesu Mwenyewe; Yesu Mwenyewe hangeweza kuipinga kazi Yake Mwenyewe. Bila shaka, huu ulikuwa unyenyekevu wa Mungu, na pia sheria ya kazi ya Mungu; Kama Roho wa Mungu hangefanya kazi, hakuna ambaye angeweza kufanya kazi Yake. Pili, kabla Yeye kubatizwa, Alikuwa tu mwanadamu wa kawaida sana, bila tofauti na watu wa kawaida; hiki ni kipengele kimoja cha jinsi Mungu wa mwili alikuwa kawaida. Mungu wa mwili hakuenda kinyume na mipango ya Roho wa Mungu; Alifanya kazi kwa njia taratibu na kawaida. Ilikuwa tu baada ya kubatizwa ndipo kazi Yake ilikuwa na nguvu na mamlaka. Ambayo ni kusema, hata kama alikuwa Mungu wa mwili, Hakufanya matendo yasiyo ya kawaida, na Alikua kwa njia sawa na watu wa kawaida. Kama Yesu alikuwa ashaujua utambulisho wake, Alikuwa amefanya kazi kubwa eneo yote kabla ya ubatizo Wake, na Alikuwa tofauti na watu wa kawaida, kujionyesha Mwenyewe kuwa ajabu, basi haingewezekana tu kwa Yohana kufanya kazi yake, lakini pia hakungekuwa na njia ya Mungu kuanza hatua ifuatayo ya kazi Yake. Na hivyo hii ingethibitisha kwamba alichofanya Mungu kilienda mrama, na kwa mwanadamu, ingeonekana kuwa Roho wa Mungu na Mungu wa mwili hawakutoka mahali moja. Hivyo, kazi ya Yesu iliyorekodiwa kwa Biblia ni kazi iliyofanywa baada ya Yeye kubatizwa, kazi iliyofanywa katika kipindi cha miaka mitatu. Biblia haijarekodi Alichofanya kabla ya kubatizwa kwa sababu Hakufanya kazi hii kabla ya kubatizwa. Alikuwa tu mtu wa kawaida, na Aliwakilisha mtu wa kawaida; kabla ya Yesu kuanza kufanya huduma Yake, Hakuwa na tofauti na watu wa wenye ukawaida, na wengine hawangeona tofauti yoyote na yeye. Ilikuwa tu baada ya Yeye kufikia 29 ndipo Yesu alijua kwamba Alikuwa amekuja kukamilisha hatua ya kazi ya Mungu; kabla; Yeye Mwenyewe hakujua, kwani kazi Aliyoifanya Mungu ilikuwa kawaida. Alipohudhuria mkutano kwa sinagogi Akiwa na umri wa miaka kumi na miwili, Maria alikuwa akimtafuta, na alisema tu sentensi moja kwa namna sawa na mtoto mwingine yeyote: “Mama! Hujui kwamba ni lazima Niyaweke mapenzi ya Baba Yangu juu ya mengine yote?” Bila shaka, kwa vile alitwawa mwili na tendo la Roho Mtakatifu, Yesu hangeweza kuwa maalum kwa namna fulani? Lakini umaalum Wake hukumaanisha hakuwa kawaida, ila tu kuwa Alimpenda Mungu zaidi ya mtoto mwingine mdogo. Ingawa Alionekana kama mwanadamu, kiini Chake bado kilikuwa maalum na tofauti na cha wengine. Lakini, ilikuwa tu baada ya ubatizo ndipo Alipohisi Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani Yake, ndipo Alipohisi kuwa Mungu Mwenyewe. Ni baada tu na Yeye kuhitimu miaka 33 ndipo Alitambua kweli kuwa Roho Mtakatifu alinuia kufanya kazi ya usulubisho kupitia kwake. Akiwa na umri wa miaka 32, Alikuja kujua baadhi ya ukweli wa ndani, kama tu ilivyoandikwa kwa Injili ya Mathayo: “Naye Simoni Petro akajibu na kusema, Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aishiye. … Kutoka wakati huo kuendelea Yesu alianza kuwaonyesha wanafunzi Wake, jinsi ilivyompasa kwenda Yerusalemu, na kupitia mateso mengi ya wazee na makuhani wakuu na waandishi, na kufishwa, na afufuke tena siku ya tatu.” Hakujua awali kazi Aliyotakiwa kufanya, lakini kwa wakati maalum. Hakujua kwa kina punde tu Alipozaliwa; Roho Mtakatifu alifanya kazi polepole ndani Yake, na kulikuwa na mchakato wa kazi. Kama, hapo mwanzoni, Angejua kuwa yeye ni Mungu, na Kristo, na Mwana wa Adamu wa mwili, kwamba Alikuwa akamilishe kazi ya usulubisho, basi mbona Hakufanya kazi awali? Mbona tu baada ya kuwaeleza wanafunzi Wake kuhusu huduma Yake ndipo Yesu alipohisi huzuni, na kusali kwa bidii kwa ajili ya hii? Mbona Yohana alimfungulia njia na kumbatiza kabla ya Yeye kuelewa mambo mengi ambayo Hakuyaelewa? Kinachothibitishwa na hii ni kwamba ilikuwa kazi ya Mungu wa mwili, na hivyo ili aelewe, na kutimiza, kulikuwa na mwendo, kwani alikuwa Mungu wa mwili, na kazi Yake ilikuwa tofauti na ile iliyofanywa moja kwa moja na Roho.

Kila hatua ya kazi ya Mungu hufuata mkondo mmoja na sawa, na hivyo katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, kila hatua imefuatwa kwa karibu na ifuatayo, kutoka msingi wa dunia hadi leo. Kama hakungekuwa na mtu wa kupisha njia, hakungekuwa na mtu wa kuja baadaye; Kwani kuna wale wanaokuja baadaye, kuna wale wanaopisha njia. Kwa njia hii kazi imepitishwa chini, hatua kwa hatua. Hatua moja inafuata ingine, na bila mtu wa kufungua njia, haitawezekana kuanza kazi, na Mungu angekosa namna ya kupeleka kazi Yake mbele. Hakuna hatua inayopingana na nyingine, na kila hatua inafuata nyingine katika mlolongo kuunda mkondo; hii yote inafanywa na Roho Yule Yule. Lakini bila kujali iwapo mtu atafungua njia ama kuendeleza kazi ya mwingine, hii haiamui utambulisho wake. Hii si sawa? Yohana aliifungua njia, na Yesu akaendeleza kazi yake, hivyo hii inathibitisha kwamba utambulisho wa Yesu ni chini kuliko wa Yohana? Yehova alifanya kazi Yake kabla Yesu, hivyo unaweza kusema kuwa Yehova ni mkubwa kumliko Yesu? Iwapo waliopasha njia ama kuendeleza kazi za wengine sio muhimu; kilicho muhimu ni kiini cha kazi zao, na utambulisho unaowakilishwa. Hii si sawa? Kwa vile Yesu alinuia kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, ilimbidi Awainue wale ambao wangefanya kazi ya kupasha njia. Yohana alipoanza tu kuhubiri, alisema, “Itayarisheni ninyi njia ya Bwana, yafanyeni mapito Yake kuwa nyoofu.” “Ninyi tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu.” Aliongea hivi tangu mwanzoni, na mbona aliweza kuyasema maneno haya? Kwa suala la utaratibu ambao maneno haya yalisemwa, ni Yohana aliyezungumzia kwanza injili ya ufalme wa mbinguni, na Yesu aliyezungumza baadaye. Kulingana na dhana za mwanadamu, ni Yohana aliyeifungua njia mpya, na bila shaka Yohana alikuwa mkubwa kumliko Yesu. Lakini Yohana hakusema yeye ni Kristo, na Mungu hakumshuhudia kama Mwana mpendwa wa Mungu, lakini Alimtumia tu kufungua na kuandaa njia ya Bwana. Alimpisha Yesu njia, lakini hangefanya kazi kwa niaba ya Yesu. Kazi zote za mwanadamu pia zilidumishwa na Roho Mtakatifu.

Katika enzi ya Agano la Kale, ni Yehova aliyeongoza njia, na kazi ya Yehova iliwakilisha enzi nzima ya Agano la Kale, na kazi zote zilizofanywa Israeli. Musa tu alizingatia hizi kazi duniani, na kazi zake zinachukuliwa kuwa ushirikiano uliotolewa na mwanadamu. Wakati huo, Yehova ndiye aliyezungumza, na Akimwita Musa, na Alimwinua Musa miongoni mwa watu wa Israeli, na kumfanya awaongoze nyikani na kuendelea hadi Kanaani. Hii haikuwa kazi ya Musa mwenyewe, lakini hiyo iliyoagizwa kibinafsi na Yehova, na hivyo Musa hawezi kuitwa Mungu. Musa pia aliiweka chini sheria, lakini sheria hii iliamrishwa kibinafsi na Yehova. Ni kwamba tu alifanya Musa kuitaja. Yesu pia alitengeneza amri, na kuondoa sheria ya Agano la Kale na kuweka amri ya enzi jipya. Mbona Yesu ni Mungu Mwenyewe? Kwa sababu haya si mambo sawa. Wakati huo, kazi aliyoifanya Musa haikuwakilisha enzi, wala haikufungua njia mpya; alielekezwa mbele na Yehova, na alikuwa tu anatumiwa na Mungu, Yesu alipokuja, Yohana alikuwa amefanya hatua ya kazi ya kupisha njia, na alikuwa ashaanza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni (Roho Mtakatifu alikuwa ameanza hii). Yesu alipokuja, Alifanya moja kwa moja kazi Yake Mwenyewe, lakini kulikuwa na tofauti kubwa kati ya kazi Yake na kazi ya Musa. Isaya pia alizungumzia unabii mwingi, lakini mbona yeye hakuwa Mungu Mwenyewe? Yesu hakuzungumzia unabii mwingi lakini mbona Alikuwa Mungu Mwenyewe? Hakuna aliyethubutu kusema kwamba kazi zote za Yesu wakati huo zilitoka kwa Roho Mtakatifu, wala hawathubutu kusema zote zilitoka kwa matakwa ya mwanadamu, ama kwamba zilikuwa kabisa kazi za Mungu Mwenyewe. Mwanadamu hakuwa na njia yoyote ya kuchambua mambo haya. Inaweza kusemwa kwamba Isaya alifanya kazi kama hiyo, na kuzungumzia unabii huo, na yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu; hayakutoka moja kwa moja kwa Isaya mwenyewe, lakini yalikuwa ufunuo kutoka kwa Yehova. Yesu hakufanya kazi nyingi sana, na Hakusema maneno mengi sana, wala Hakuzungumzia unabii mwingi. Kwa mwanadamu, mahubiri Yake hayakuonekana hasa ya kupandishwa cheo, lakini alikuwa Mungu Mwenyewe, na mwanadamu hawezi kueleza haya. Hakuna aliyewahi kumwamini Yohana, ama Isaya, ama Daudi, wala hakuna aliyewahi kuwaita Mungu, ama Daudi Mungu ama Yohana Mungu, hakuna aliyewahi kuzungumza hivi, na ni Yesu tu aliyewahi kuitwa Kristo. Uainishaji huu umefanywa kulingana na ushahidi wa Mungu, kazi Aliyoifanya, na huduma Aliyoifanya. Kuhusu watu wakuu wa Biblia—Ibrahimu, Daudi, Yoshua, Danieli, Isaya, Yohana na Yesu—kupitia kazi waliyoifanya, unaweza kusema ni nani aliye Mungu Mwenyewe, na ni watu wapi walio manabii, na ni wapi walio mitume. Ni nani aliyetumiwa na Mungu, na nani aliyekuwa Mungu Mwenyewe, inatofautishwa na kuamuliwa na asili na aina za kazi walizozifanya. Iwapo huwezi kusema tofauti, basi hii inadhihirisha kwamba hujui maana ya kumwamini Mungu. Yesu ni Mungu kwa sababu Alizungumza maneno mengi, na kufanya kazi nyingi hasa maonyesho Yake ya miujiza nyingi. Vivyo hivyo, Yohana, pia alifanya kazi nyingi, na kuzungumza maneno mengi, Musa pia; mbona hawakuitwa Mungu? Adamu aliumbwa moja kwa moja na Mungu; mbona hakuitwa Mungu, badala tu ya kuitwa kiumbe? Mtu akikwambia, “Leo, Mungu amefanya kazi nyingi sana, na kuzungumza maneno mengi; Yeye ni Mungu Mwenyewe. Basi, vile Musa alivyozungumza maneno mengi, lazima yeye pia ni Mungu Mwenyewe!” inapaswa uwarudishie swali, “Wakati huo, mbona Mungu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana, kama Mungu Mwenyewe? Je, Yohana hakumtangulia Yesu? Ni ipi iliyokuwa kubwa, kazi ya Yohana ama Yesu? Kwa mwanadamu, kazi ya Yohana inakaa mkubwa kuliko ya Yesu, lakini mbona Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana?” Hiki kitu kimoja kinafanyika leo! Mwanzoni, Musa alipowaongoza watu wa Israeli, Yehova alimwongelesha kutoka miongoni mwa mawingu. Musa hakuzungumza moja kwa moja lakini badala yake aliongozwa moja kwa moja na Yehova. Hii ilikuwa kazi ya Israeli ya Agano la Kale. Ndani ya Musa hamkuwa na Roho, ama nafsi ya Mungu. Hangeweza kufanya kazi hiyo, na hivyo kuna tofauti kubwa kati ya aliyoifanya na Yesu. Na hiyo ni kwa sababu kazi walizozifanya zilikuwa tofauti! Iwapo mtu anatumiwa na Mungu, ama ni nabii, mtume, ama Mungu Mwenyewe, unaweza kubainishwa na asili ya kazi yake, na hii itakomesha mashaka yenu, Kwa Biblia, imeandikwa kwamba Kondoo peke yake ndiye anayeweza kuivunja mihuri saba. Kupitia zama zote kumekuwa na wachambuzi wengi wa maandiko miongoni mwa watu wakuu, na hivyo unaweza kusema kwamba wote ni Kondoo? Unaweza kusema kwamba maelezo yao yote yalitoka kwa Mungu? Walikuwa tu wachambuzi; hawana utambulisho wa Kondoo. Wanastahilije kuivunja mihuri saba? Ni ukweli kwamba “Kondoo peke yake anaweza kuivunja mihuri saba,” Lakini Hakuji tu kuivunja mihuri saba; hakuna umuhimu wa kazi hii, inafanywa kwa bahati. Yeye yu wazi kabisa kuhusu kazi Yake Mwenyewe; ni muhimu Kwake kutumia muda mwingi kutafsiri maandiko? Ni lazima “Enzi ya Mwanakondoo Akitafsiri Maandiko” iongezwe kwa kazi ya miaka elfu sita? Anakuja kufanya kazi mpya, lakini pia Anatoa ufunuo kadhaa kuhusu kazi za nyakati za zamani, kufanya watu waelewe ukweli wa kazi ya miaka elfu sita. Hakuna haja ya kueleza vifungo vingi kutoka Biblia; kazi ya leo ndiyo iliyo kuu, hiyo ni muhimu. Unapaswa kujua kwamba Mungu haji hasa kuivunja muhiri saba, ila kufanya kazi ya wokovu.

Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja.

Bila mwanzo wa hatua hii mpya ya kazi, ni nani ajuaye umbali upi ninyi wainjilisti, wahubiri, wachambuzi na wanaoitwa wanadamu wa kiroho wangeenda! Bila mwanzo wa hatua hii mpya ya kazi, mnachozungumzia ni cha zamani! Ama inapaa kwa kiti cha enzi, au kutayarisha kimo cha kuwa mfalme; ama kukanusha binafsi au kuhini mwili wa mtu; ama kuwa mtulivu au kujifunza masomo kutoka mambo yote; ama unyenyekevu au upendo. Hii ni kuimba wimbo sawa na zamani? Ni jambo tu ya kuita kitu kimoja na jina lingine! Ama kufunika kichwa cha mtu na kuvunja mkate, au kuweka mikono na kuomba, na kuponya wagonjwa na kutoa mapepo. Kunaweza kuwa na kazi ingine mpya? Kunaweza kuwa na matarajio ya maendeleo? Ukiendelea kwa njia hii, utayafuata mafundisho kwa upofu, ama ufuate mkataba. Mnaamini kazi yenu kuwa ya juu mno, lakini hamjui kwamba yote yalipitiwa na kufundishwa na hao “watu wazee” wa nyakati za zamani? Yote mnayoyasema na kufanya si maneno ya mwisho ya hao watu wazee? Siyo malipo ya hawa watu wazee kabla wafariki? Unafikiri kuwa vitendo vyenu vinashinda vile vya mitume na manabii wa vizazi vilivyopita, na pia kushinda mambo yote? Mwanzo wa hatua hii ya kazi umetamatisha kuabudu kwenu kwa kazi ya Mshahidi Lee ya kutaka kuwa mfalme, na kupaa kwa kiti cha enzi, na kukamata kiburi na fujo yenu, kwa hivyo hamna uwezo wa kuingilia hatua hii ya kazi. Bila hatua hii ya kazi, mngezama hata zaidi katika kutokombolewa. Kuna mengi yaliyo mzee miongoni mwenu! Kwa bahati nzuri, kazi ya leo imewarudisha; kama si hivyo, nani anajua mwelekeo ambao mngechukua! Kwa kuwa Mungu ni Mungu ambaye daima ni mpya na kamwe si mzee, mbona hutafuti mambo mapya? Mbona daima unakwamilia mambo ya kale? Na hivyo, kuijua kazi ya Roho Mtakatifu leo una umuhimu mkubwa!

Iliyotangulia: Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Inayofuata: Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp