286 Kuwa Jasiri Katika Njia ya Kumpenda Mungu

1

Njia yenye mabonde hufanya upendo wangu kwa Mungu safi zaidi.

Hukumu na usafishaji wa maneno ya Mungu ni marafiki zangu wa kila mara.

Haki Yake inanichoma kama moto.

Kupitia usafishaji mchungu hatimaye nimekuja kujijua,

na sasa ninaona jinsi nilivyopotoka.

Hukumu ya Mungu inatakasa tabia yangu potovu.

Mateso yamenifundisha jinsi ya kutii.

2

Kujua uzuri wa Mungu kunaniletea karibu na Yeye,

na kumshuhudia Yeye ni matamanio yangu.

Sasa naona kwamba hukumu ni baraka ya Mungu.

Ili kupata ukweli na kukamilishwa na Mungu, lazima tuteseke majaribu mengi.

Wavivu, waoga, na wenye hofu hawawezi kumshuhudia kamwe.

Natamani kuteseka hata zaidi ili kustahili kutumiwa na Mungu.

Mateso huimarisha upendo wangu Kwake.

3

Kristo wa siku za mwisho anatuletea njia ya uzima wa milele.

Hukumu ya Mungu na kuadibu ni upendo wa kweli.

Kwa kupitia hukumu, hatimaye nimejua haki na utakatifu wa Mungu.

Nina uchaji na utii kwa Mungu na nimehisi upendo wa kweli wa Mungu.

Hukumu na usafishaji mkali zaidi unanifaidi hata zaidi.

Baada ya kupitia mateso makubwa, napata ukweli na kuishi kama mwanadamu halisi.

Nitajitoa mwenyewe kulipiza upendo wa Mungu na kuwa mwaminifu Kwake.

Kiitikio

Kuwa wa akili moja na Mungu, tumia yote kwa ajili Yake.

Mpende, fuata mapenzi Yake,

jitahidi kufikia kile Anachotaka.

Kwa imani yangu thabiti, nakwenda kiaskari kuelekea maisha halisi ya kibinadamu.

Mafanikio yananiita.

Iliyotangulia: 285 Wimbo wa Kumpenda Mungu Bila Majuto

Inayofuata: 287 Sisi ni Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp