Sura ya 88

Watu hawawezi kabisa kuwazia kiwango ambacho mwendo Wangu umezidisha kasi: Hili ni jambo la ajabu ambalo limetokea ambalo ni zaidi ya kile ambacho mwanadamu anaweza kuwazia. Mwendo Wangu umeendelea tangu kuumbwa kwa dunia, na kazi Yangu haijawahi kusimama. Ulimwengu dunia mzima unabadilika siku baada ya siku, na watu, pia, wanabadilika kila wakati. Haya yote ni sehemu ya kazi Yangu, yote ni sehemu ya mpango Wangu, na, hata zaidi, ni sehemu ya usimamizi Wangu, na hakuna mwanadamu anayejua wala kuelewa mambo haya. Ni wakati tu Mimi Mwenyewe ninapowaambia, Ninapofanya ushirika nanyi uso kwa uso, ndipo mnajua kidogo; vinginevyo, hakuna mtu yeyote anayeweza kuwa na wazo lolote kuhusu ramani ya mpango Wangu wa usimamizi. Huo ndio uweza Wangu mkuu, na hata zaidi, hayo ndiyo matendo Yangu ya ajabu. Haya ni mambo ambayo hakuna anayeweza kuyabadilisha. Kwa hivyo, kile Ninachosema katika wakati wa sasa ndicho kinachokuwa, na hakiwezi kabisa kubadilika. Dhana za mwanadamu hazina hata chembe ndogo ya maarifa kunihusu Mimi—zote ni porojo tu zisizo na maana! Msifikiri kwamba mmepata vya kutosha na kuhisi kutosheka. Ninakuambia hili: Bado una safari ndefu! Kuhusu mpango Wangu wote wa usimamizi, mnajua kidogo tu, kwa hivyo lazima msikilize yale Ninayosema na mfanye chochote Ninachowaambia mfanye. Tendeni kulingana na matakwa Yangu katika kila kitu, na hakika mtapata baraka Zangu; yeyote anayeamini anaweza kupokea, ilhali kwa yeyote asiyeamini, huo “utupu” aliouwazia utatimizwa ndani yake. Hii ni haki Yangu, na, hata zaidi, ni uadhama Wangu, ghadhabu Yangu, na kuadibu Kwangu. Hakuna hata fikira wala tendo moja kutoka kwa kila mtu linalonipita Mimi.

Watu wengi wanaposikia maneno Yangu, wanaogopa na kutetemeka, na nyuso zao zinakunjamana. Je, kwa kweli Nimekukosea? Je, inawezekana kwamba wewe si mmoja wa uzao wa joka kuu jekundu? Hata unajifanya kuwa mwema! Hata unajifanya kuwa mzaliwa Wangu wa kwanza! Je, unafikiri Mimi ni kipofu? Je, unafikiri Siwezi kuwatambua watu? Mimi ndiye Mungu anayechunguza ndani kabisa ya mioyo ya watu: Hiki ndicho Ninachowaambia wana Wangu, na ndicho Ninachowaambia ninyi pia, uzao wa joka kuu jekundu. Ninaona kila kitu waziwazi, bila kukosea hata kidogo. Ninawezaje kutojua kile Ninachofanya? Ninalifahamu wazi kabisa! Kwa nini Ninasema kwamba Mimi ndiye Mungu Mwenyewe, Muumba wa ulimwengu na vitu vyote? Kwa nini Ninasema kwamba Mimi ndiye Mungu anayetazama ndani kabisa ya mioyo ya watu? Ninafahamu vyema hali ya kila mtu. Je, mnafikiri kwamba Sijui la kufanya au la kusema? Hili haliwahusu. Jihadharini msije mkapigwa chini na mkono Wangu; mtapata hasara kwa namna hiyo. Amri Zangu za utawala ni zisizosamehe. Mnaelewa? Yote yaliyo hapo juu ni sehemu za amri Zangu za utawala. Kuanzia siku Ninapowaambia haya, mkifanya ukiukaji wowote zaidi, kutakuwa na malipo, kwa sababu hapo awali hamkuelewa.

Sasa Ninatangaza amri Zangu za utawala kwenu (zitaanza kutumika kuanzia siku zinapotangazwa, zikitoa kuadibu tofauti kwa watu tofauti):

Ninatimiza ahadi Zangu, na kila kitu kiko mikononi Mwangu: Yeyote anayetilia shaka hakika atapigwa chini. Hakuna nafasi yoyote ya kufikiria; ataangamizwa mara moja, hivyo kuondoa chuki iliyo moyoni Mwangu. (Kutokana na hili inathibitishwa kwamba yeyote anayepigwa chini lazima asiwe mshiriki wa ufalme Wangu, bali lazima awe dhuria ya Shetani.)

Kama wazaliwa wa kwanza, mnapaswa kushika nafasi yenu wenyewe na kutimiza wajibu wenu wenyewe, na msiwe wadadisi. Mnapaswa kujitoa kwa ajili ya mpango Wangu wa usimamizi, na kila mahali mnapoenda, mnapaswa kunitolea Mimi ushuhuda mzuri na kulitukuza jina Langu, na hampaswi kufanya matendo ya aibu. Mnapaswa kuwa mifano kwa wana Wangu wote na watu Wangu; hampaswi kuwa wapotovu hata kwa muda mfupi, na lazima kila wakati mtokee mbele ya kila mtu mkiwa na utambulisho wa wazaliwa wa kwanza; na hampaswi kuwa wanyenyekevu kupita kiasi, bali mpige hatua mbele mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu. Ninawataka mlitukuze jina Langu, si kuliaibisha jina Langu. Wale ambao ni wazaliwa wa kwanza kila mmoja ana jukumu lake binafsi, na hawawezi kufanya kila kitu. Hili ndilo jukumu ambalo Nimewapa ninyi, na halipaswi kuepukwa. Lazima mjitoe kwa moyo wenu wote, akili zenu zote, na nguvu zenu zote, kutimiza kile ambacho Nimewakabidhi ninyi.

Kuanzia siku hii na kuendelea, katika ulimwengu dunia mzima, kazi ya kuwachunga wana Wangu wote na watu Wangu wote itakabidhiwa kwa wana Wangu wazaliwa wa kwanza kuitimiza. Na Nitamwadibu yeyote asiyeweza kuweka moyo wake wote na akili yake yote katika kuitimiza. Hii ni haki Yangu. Sitawaachilia wala kuwahurumia hata wazaliwa Wangu wa kwanza

Ikiwa kuna yeyote miongoni mwa wana Wangu au miongoni mwa watu Wangu anayemdhihaki na kumtukana mmoja wa wazaliwa Wangu wa kwanza, Nitamwadhibu vikali, kwa maana wazaliwa Wangu wa kwanza wananiwakilisha Mimi Mwenyewe; kile ambacho mtu anawafanyia, ananifanyia Mimi pia. Hii ndiyo kali zaidi kati ya amri Zangu za utawala. Nitawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza, kulingana na matakwa yao, kutekeleza haki Yangu dhidi ya yeyote miongoni mwa wana Wangu na watu Wangu anayekiuka amri hii.

Nitamtelekeza hatua kwa hatua yeyote anayenichukulia Mimi kwa mzaha na kulenga tu chakula, mavazi, na usingizi Wangu, anayezingatia tu mambo Yangu ya nje, na asiyezingatia kujali mzigo Wangu, wala kutimiza majukumu yake mwenyewe ipasavyo. Hili linaelekezwa kwa wote walio na masikio.

Yeyote anayemaliza kutumika kwa ajili Yangu lazima aondoke kwa utii bila fujo. Jihadhari, la sivyo Nitashughulika nawe. (Hii ni amri ya ziada.)

Wazaliwa Wangu wa kwanza watachukua fimbo ya chuma kuanzia sasa na kuanza kutekeleza mamlaka Yangu kutawala mataifa na watu wasiohesabika, kutembea miongoni mwa mataifa na watu wasiohesabika, na kutekeleza hukumu, haki, na uadhama Wangu miongoni mwa mataifa na watu wasiohesabika. Wana Wangu na watu Wangu wataniogopa Mimi, watanisifu Mimi, watanishangilia Mimi, na watanitukuza Mimi bila kukoma, kwa sababu mpango Wangu wa usimamizi umetimizwa na wazaliwa Wangu wa kwanza wanaweza kutawala pamojana Mimi.

Hii ni sehemu ya amri Zangu za utawala; baada ya hili, Nitawaambia zaidi kuzihusu kadiri kazi inavyoendelea. Kutokana na amri za utawala zilizo hapo juu, mnapaswa kuona mwendo ambao Ninafanya kazi Yangu, na vilevile hatua ambayo kazi Yangu imefikia. Huu ndio uthibitisho.

Nimemhukumu Shetani kitambo. Kwa sababu mapenzi Yangu hayazuiliwi na kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza wamepata utukufu pamoja na Mimi, tayari Nimetekeleza haki na uadhama Wangu juu ya dunia na vitu vyote vya kishetani. Sinyanyui kidole wala kumtilia maanani Shetani hata kidogo (kwa sababu hastahili hata kunena na Mimi). Ninaendelea tu kufanya kile Ninachotaka kufanya. Kazi Yangu inaendelea vizuri, hatua kwa hatua, na mapenzi Yangu hayazuiliwi kote duniani. Hili limemwaibisha Shetani kwa kiwango fulani, na ameangamizwa kabisa, lakini jambo hili lenyewe halijafikia nia Zangu. Pia Ninawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza kutekeleza amri Zangu za utawala juu yao. Kwa upande mmoja, kile Ninachomruhusu Shetani aone ni ghadhabu Yangu ikimshukia; kwa upande mwingine, Ninamwacha aone utukufu Wangu (aone kwamba wazaliwa Wangu wa kwanza ni mashahidi wenye nguvu zaidi wa kumwaibisha Shetani). Simwadhibu yeye Mimi binafsi; badala yake, Ninawaacha wazaliwa Wangu wa kwanza watekeleze haki na uadhama Wangu. Kwa sababu Shetani alikuwa akiwanyanyasa wana Wangu, akiwatesa wana Wangu, na kuwakandamiza wana Wangu, katika wakati wa sasa, baada ya huduma yake kumalizika, Nitawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza waliokomaa kummaliza. Shetani tayari hana nguvu na ameanguka. Kulemaa kwa mataifa yote duniani ndiko ushuhuda bora kabisa; watu kupigana na nchi kuwa vitani ni udhihirisho dhahiri wa kuporomoka kwa ufalme wa Shetani. Sababu ambayo Sikuonyesha ishara na maajabu yoyote hapo awali ilikuwa ili kumwaibisha Shetani na kulitukuza jina Langu, hatua kwa hatua. Shetani atakapokuwa amemalizwa kabisa, Nitaanza kutumia nguvu Zangu kuu: Kile Ninachosema kitafanyika, na mambo ya kupita maumbile ambayo hayalingani na dhana za mwanadamu pia yatatimia (haya yanarejelea baraka zinazokuja hivi karibuni). Kwa sababu Mimi ndiye Mungu wa vitendo Mwenyewe na Sina taratibu zozote, na kwa sababu Ninanena kulingana na mabadiliko katika mpango Wangu wa usimamizi, kile ambacho Nimesema hapo awali kwa hivyo si lazima kitumike wakati wa sasa. Msing'ang'anie dhana zenu wenyewe! Mimi si Mungu anayefuata taratibu; ndani Yangu, kila kitu ni huru, kinazidi maarifa ya dunia, na kimewekwa huru kabisa. Huenda kile kilichosemwa jana kimepitwa na wakati na kutupiliwa mbali katika wakati wa sasa (hata hivyo, amri Zangu za utawala, kwa kuwa zimetangazwa, hazitawahi kubadilika). Hizi ndizo hatua katika mpango Wangu wa usimamizi. Msing'ang'anie taratibu. Kila siku kuna nuru mpya na kuna ufunuo mpya, na huo ndio mpango Wangu. Kila siku nuru Yangu itafunuliwa ndani yako na sauti Yangu itaachiliwa kwa ulimwengu dunia mzima. Je, unaelewa? Huu ndio wajibu wako, jukumu ambalo Nimekukabidhi. Hupaswi kulipuuza hata kwa muda mfupi. Nitawatumia hadi mwisho watu Ninaowapata kuwa wanaostahili, bila kuwabadilisha kamwe. Hii ni kwa sababu Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, na Ninajua ni mtu wa aina gani anayepaswa kufanya jambo gani, na pia ni mtu wa aina gani anayeweza kufanya jambo gani. Huu ni uweza Wangu.

Iliyotangulia: Sura ya 87

Inayofuata: Sura ya 89

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp