Sura ya 87

Lazima uharakishe hatua na ufanye kile Nataka kufanya. Hii ni kusudi Langu lenye hamu kwenu. Inawezekana kuwa kwa wakati huu bado hamjaelewa maana ya maneno Yangu? Inawezekana kuwa bado hamjui kusudi Langu? Nimezungumza wazi zaidi na zaidi, na kusema mengi zaidi, lakini, je, ninyi hamjajitahidi kujaribu kuelewa maana ya maneno Yangu? Shetani, usifikiri kwamba unaweza kuharibu mpango Wangu! Wale wanaomtumikia Shetani, yaani, uzao wa Shetani (hii inahusu wale ambao wanamilikiwa na Shetani. Wale wanaomilikiwa na Shetani kwa hakika wana uhai wa Shetani, na kwa hivyo wanaitwa kuwa uzao wa Shetani) wanaomba rehema miguuni Pangu, wanalia na kusaga meno yao, lakini Siwezi kufanya kitu kama hicho cha kijinga! Ninaweza kumsamehe Shetani? Ninaweza kuleta wokovu kwa Shetani? Haiwezekani! Ninafanya kile Ninachosema na Siwezi kujuta kamwe!

Chochote Ninachosema kinakuja kutukia, si hivyo? Lakini ninyi bado kila mara hamniamini, mnashuku maneno Yangu, na kufikiri kwamba Ninawafanyia mzaha. Hiyo kwa kweli ya dhihaka. Mimi ni Mungu Mwenyewe! Mnaelewa? Mimi ni Mungu Mwenyewe! Ikiwa Sina hekima na sina nguvu, Ninaweza tu kufanya na kusema kama inavyonipendeza? Lakini bado hamniamini. Nimesisitiza mara kwa mara kwenu, na Nimewaambia mara kwa mara. Ni kwa nini wengi wenu bado hawaamini? Kwa nini bado mna mashaka? Kwa nini mnamshikilia kabisa mawazo yenu wenyewe? Yanaweza kukuokoa? Ninatenda kile ninachosema. Nimewaambia mara nyingi: Angalieni maneno Yangu kuwa ni ya kweli na msishuku. Je, mmechukulia maneno Yangu kwa uzito? Wewe peke yako huwezi kufanya chochote, lakini huwezi kuamini katika kile Ninachotenda. Ni nini kinaweza kusemwa juu ya mtu kama huyo? Kusema wazi wazi, ni kama kwamba Sikuwahi kuwaumba kamwe, ambayo ni kusema, wewe hujahitimu katika kila hali kuwa mtumishi Wangu. Kila mtu lazima aamini maneno Yangu! Wote wanapaswa kupitia jaribio—Sitamuacha mtu yeyote kukwepa. Bila shaka, hii ni isipokuwa wale wanaoamini. Watu wanaoyaamini maneno Yangu bila shaka watapata baraka Zangu, ambayo utapewa wewe na kutimizwa ndani yako kulingana na kile unachoamini. Wana Wangu wazaliwa wa kwanza! Sasa, Ninaanza kuwapa baraka Zangu zote. Mtaanza kuvitupa vifungo vyote vinavyochukiza vya mwili kidogo na kidogo: ndoa, familia, kula, kuvaa, kulala, majanga yote ya asili (upepo, jua, mvua, dhoruba inayouma, shida ya kuanguka kwa theluji, na mambo mengine yote mnayochukia). Ninyi mtasafiri baharini, ardhini, na angani bila kuathiriwa na vizuio vya anga, wakati, au jiografia, kujifurahisha kikamilifu katika kumbatio Langu la upendo, mkiwa na wajibu juu ya kila kitu chini ya utunzaji Wangu wa upendo.

Ni nani asiyejivunia wana Wangu wazaliwa wa kwanza ambao Nimewafanya wakamilifu? Ni nani asiyelisifu jina Langu kwa ajili ya wana Wangu wazaliwa wa kwanza? Kwa nini sasa Ninataka kuwaonyesha siri nyingi sana? Mbona si katika wakati uliopita, lakini leo? Hii yenyewe pia ni siri, wewe unajua? Kwa nini Sikusema hapo nyuma kuwa China ni taifa Nilililolilaani? Na kwa nini Sikuwafichua wale wanaonitumikia? Leo Nawaambieni hili: Leo, kwa maoni Yangu, kila kitu kimetimilika—Ninasema hili kuhusu wana Wangu wazaliwa wa kwanza. (Kwa kuwa leo wana Wangu wazaliwa wa kwanza wametawala pamoja nami, sio tu kuoneka, lakini kwa kweli wanatawala pamoja nami. Kwa sasa, ni kwa yeyote ambaye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake ambaye kwa hakika anatawala pamoja nami, na hii inafichuliwa sasa, sio jana, wala kesho.) Leo Ninafichua siri zangu Zangu zote katika ubinadamu wa kawaida kwa sababu wale watu ambao Nataka kuwafichua wamefichuliwa, na hii ni hekima Yangu. Kazi Yangu imeendelea hadi hatua hii: Yaani, kwa wakati huu ni lazima Nitekeleze mpango wa maagizo ya utawala Niliyoamua juu ya wakati huu. Kwa hiyo, Ninawatunukia wana Wangu wazaliwa wa kwanza, wana, watu, na watendaji huduma thibitisho linalostahili, kwa sababu Nina mamlaka na Nitahukumu na kutatawala kwa ukali. Ni nani anayethubutu kutonifanyia huduma kwa utii? Ni nani anayethubutu kunilalamikia? Ni nani anayethubutu kusema kwamba Mimi si Mungu wa haki? Najua, asili yenu ya kipepo imefichuliwa kwa muda mrefu mbele Yangu: Kwa yeyote Ninayekuwa mwema kwake, ninyi mnamwonea wivu na mnamchukia. Hii ni asili ya Shetani kabisa! Mimi ni mwema kwa wana Wangu—je, unathubutu kusema kuwa Mimi si mwenye haki? Naweza kukufukuza kabisa. Kwa bahati nzuri wewe unanifanyia huduma na sasa sio wakati; vinginevyo, Ningekuwa nimekufukuza!

Aina ya Shetani! Acheni kuwa washenzi! Msiseme tena! Msitende tena! Kazi Yangu imeanza kufanywa kati ya wana na watu Wangu waliochaguliwa, na tayari inaenea katika mataifa yote, makundi yote, madhehebu yote, na kazi zote za maisha nje ya China. Ni kwa nini wale wanaonipa huduma kila mara huzuiwa kiroho? Ni kwa nini hawaelewi kamwe mambo ya kiroho? Ni kwa nini kila mara Roho Yangu haifanyi kazi kwa watu hawa? Kwa ujumla, Siwezi kutumia nguvu nyingi sana juu ya wale ambao Sikuwaamulia kabla au kuwagua. Mateso Yangu yote ya awali, bidii Yangu ya kazi ya ulinzi imekuwa kwa wana Wangu wazaliwa wa kwanza na sehemu ndogo ya wana na watu, na zaidi ya hayo, pia wamekuwa kwa niaba ya kukamilika kwa ufanisi wa kazi Yangu ya baadaye, ili mapenzi Yangu yasizuiliwe. Kwa sababu Mimi ni Mungu Mwenye busara Mwenyewe, Nimepanga vizuri kila hatua. Mimi sijitahidi kwa vyoyote kubaki na mtu yeyote (hii inaelekezwa kwa wale ambao hawakuchaguliwa au kuamuliwa kabla), na Sitamuangusha mtu yeyote kwa bahati (hii inaelekezwa na waliochaguliwa na kuamuliwa kabla): Hii ni amri Yangu ya utawala, ambayo hakuna mtu anayeweza kuibadilisha! Kwa wale ambao Ninawachukia, Mimi ni mkatili; kwa wale Ninaowapenda, Ninawalinda na kuwahifadhi. Kwa hiyo, Ninatenda kile Ninachosema (Ninaowachagua, wamechaguliwa; Ninaowaamulia kabla, wameamuliwa kabla; haya ni mambo Yangu ambayo Nimeyapanga kabla ya uumbaji).

Nani anaweza kubadilisha moyo Wangu? Isipokuwa Mimi kufanya kulingana na mipango Ninayofanya Nitakavyo, ni nani anathubutu kutenda kwa pupa na kutotii amri Yangu? Hizi ni amri Zangu za utawala, na ni nani anayethubutu kuondoa moja yao kutoka Kwangu? Wote lazima wawe katika amri Yangu. Watu wengine wanasema, mtu huyo ameteseka sana, na ni mwaminifu na anafikiria moyo Wangu kabisa, lakini kwa nini hakuchaguliwa? Hii pia ni amri Yangu ya utawala. Nikisema mtu anaupendeza moyo Wangu, basi mtu huyo anaupendeza moyo Wangu na ni yule Ninayempenda; Nikisema kwamba mtu ni mtoto wa Shetani, basi mtu huyo ni yule Ninayemchukia. Usimpendekeze mtu yeyote! Je, unaweza kumng’amua? Haya yote yanaamuliwa na Mimi. Mwana ni mwana daima, na Shetani ni Shetani daima, ambayo ni kusema, asili ya mwanadamu haibadiliki. Isipokuwa Mimi Niwafanye wabadilike, wote watafuata aina yao wenyewe na hawawezi kamwe kubadilika!

Ninafichua siri Zangu kwenu kazi Yangu inavyoendelea. Leo, kazi Yangu imeendelea hadi hatua gani, je, mnajua kwa kweli? Je, mtafuata kwa kweli uongozi wa Roho Wangu kufanya kile Ninachofanya na kusema kile Ninachosema? Ni kwa nini Nasema kuwa China ni taifa ambalo Nimelilaani? Kwanza, Niliwaumba Wachina wa leo kwa sura Yangu. Hawakuwa na roho, na mwanzoni wao walipotoshwa na Shetani na hawangeweza kuokolewa. Kwa hivyo Niliwakasirikia watu hawa na nikawalaani. Ninawachukia watu hawa zaidi, na Ninakasirika wanapotajwa kwa sababu ni watoto wa joka kubwa jekundu. Kutokana na hili mtu anaweza kufikiria wakati ambapo nchi za dunia zimetwaa kwa nguvu China. Bado ni vivyo hivyo leo, na yote imekuwa laana Yangu—hukumu Yangu yenye nguvu zaidi dhidi ya joka kubwa jekundu. Hatimaye, Nikawaumba aina nyingine ya watu, ambao pamoja nao Niliwaamulia kabla wana Wangu wazaliwa wa kwanza, wana, watu, na wale wanaonifanyia huduma, kwa hivyo kile Ninachofanya leo Nilipanga kitambo kufanya. Kwa nini wale walio katika mamlaka nchini China wanatesa mara kwa mara na kuwadhulumu ninyi? Ni kwa sababu joka kubwa jekundu halifurahii laana Yangu na ananipinga. Lakini ni chini ya aina hii ya mateso na tishio hasa kwamba Mimi huwakamilisha wana Wangu wazaliwa wa kwanza kurudisha mashambulio dhidi ya joka kubwa jekundu na watoto wake. Baadaye Nitawaainisha. Baada ya kusikiliza maneno Yangu, je, mnaelewa umuhimu wa kuwaruhusu kutawala pamoja nami? Ninaposema kwamba joka kubwa jekundu limesononeshwa kabisa hadi kifo chake, pia ni wakati wana Wangu wazaliwa wa kwanza watawale pamoja nami. Mateso ya joka kubwa jekundu ya wana Wangu wazaliwa wa kwanza hutoa huduma sana Kwangu, na wakati wana Wangu wanapokua na wanaweza kusimamia masuala ya nyumba Yangu, basi watumishi waovu (watenda huduma) wataondolewa. Kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza watakuwa wakitawala pamoja nami na watakuwa wametimiza makusudi Yangu, Nitawasukuma watenda huduma mmoja baada ya mwingine kwenye ziwa la moto na kibiriti: Kwa vyovyote vile wanapaswa kwenda! Ninafahamu kikamilifu kwamba aina ya Shetani pia anataka kufurahia baraka Zangu, na asiyetaka kurudi chini ya miliki ya Shetani; hata hivyo, Nina amri Zangu ya utawala ambazo kila mtu lazima azingatie na ambazo zinapaswa kutekelezwa, na hakuna mtu anayeachiliwa. Baadaye, Nitawaambieni amri Zangu za utawala moja baada ya nyingine, msije kukosea.

Iliyotangulia: Sura ya 86

Inayofuata: Sura ya 88

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp