Sura ya 86

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia. Kwa wale Ninaowapenda, Nitawapenda daima mpaka mwisho kabisa na upendo hautabadilika kamwe. Kwa wale Ninaowachukia, moyo Wangu hauguswi hata kidogo bila kujali ni wazuri kiasi gani. Hii ni kwa sababu wao sio Wangu na hawana sifa Zangu na hawana uzima Wangu. Hiyo ni kusema, hawakuamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi, kwani Mimi siwezi kukosea. Hiyo ni kusema kwamba kila Ninachofanya kinaitwa kitakatifu na chenye heshima na Sina majuto yoyote kamwe. Katika macho ya watu, Mimi ni mkatili sana; lakini hujui kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye haki na uadhama? Kila kitu Changu ni sahihi; wale Ninaowachukia bila shaka watapata laana Zangu na wale Ninaowapenda kwa hakika watapokea baraka Zangu. Hii ni tabia Yangu takatifu na isiyokiukwa na hakuna mwanadamu atakayeibadilisha; hili ni bila shaka!

Leo, wale ambao kwa kweli wanakubaliana na nia Zangu hakika watakamilishwa na Mimi, kwa maana kazi Yangu ni wazi na kamilifu na Siachi chochote kisicho kamili; wale Ninaowalaani watachomwa. Hivyo kwa nini watu wengi wamelaaniwa na Mimi na bado Roho Mtakatifu bado anafanya kazi Yake juu yao (hili linasemwa kuhusiana na Mimi kutoishi katika hekalu chafu)? Je, mnaelewa maana halisi ya mambo yote na vitu vyote kuhusu kutoa huduma kwa Kristo? Roho Mtakatifu hufanya kazi Yake kupitia kwa wao Ninapotumia huduma yao, lakini kwa kawaida wakati hawako katika huduma Yangu kimsingi hawajapewa nuru katika roho yao. Hata wakinitafuta, ni kwa bidii, na hii ni hila ya Shetani, kwani kwa nyakati za kawaida, hawatilii maanani kazi Yangu hata kidogo na hawahurumii kabisa mizigo Yangu. Sasa wazaliwa Wangu wa kwanza wamekua, na hivyo Ninawafukuza na kwa hiyo Roho Wangu ameondoka kutoka kila mahali, na mkazo maalum unawekwa kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, unaelewa? Mambo yote yanabaki kwa matendo Yangu, yanabaki kwa majaaliwa Yangu, na kubaki kwa maneno yote kutoka kinywani Mwangu. Maeneo yote ambayo yamepokea baraka Zangu lazima yawe mahali ambapo Nafanya kazi, na pia mahali ambapo kazi Yangu inatekelezwa. China ni taifa ambapo Shetani anaabudiwa zaidi na hivyo Nimelilaani, na pia ni taifa ambalo limefanya mengi zaidi kunitesa. Mimi kabisa Sitafanya kazi Yangu kwa watu chini ya ushawishi wa joka kuu jekundu. Je, unaelewa maana halisi ya maneno Yangu? Hata hivyo, Wangu na watu Wangu ni wachache. Hakika kila kitu ki mikononi Mwangu; nguvu inapaswa kulenga na juhudi zaidi zinapaswa kutumiwa kwa wale ambao Nimewachagua na kuwaamulia kabla. Hiyo ni kusema, wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza wanapaswa kutenda haraka ili kubeba mizigo iliyo juu ya mabega Yangu mapema iwezekanavyo na kuweka jitihada zote katika kazi Yangu.

Wale wanaonitumikia, sikilizeni! Mnaweza kupokea baadhi ya neema Yangu wakati mnanitumikia. Yaani, ninyi mtajua kwa wakati kuhusu kazi Yangu ya baadaye na mambo ambayo yatatokea baadaye, lakini hamtafurahia hilo kabisa. Hii ni neema Yangu. Wakati huduma Yako imekamilika, ondoka mara moja na usikawie. Wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza hawapaswi kuwa wenye kiburi, lakini mnaweza kujivunia, kwa kuwa Nimewapa baraka za milele kwenu. Wale ambao ni walengwa wa uangamizaji hampaswi kujiletea shida au kuhisi huzuni kwa ajili ya hatima yenu; ni nani aliyekufanya kuwa mzawa wa Shetani? Baada ya kufanya huduma yako kwa ajili Yangu, unaweza kurudi tena kwenye shimo lisilo na mwisho kwa sababu hutakuwa tena na matumizi Kwangu na Nitaanza kuwashughulikia na kuadibu Kwangu. Mara Ninapoanza kufanya kazi, Nitaishughulikia mpaka mwisho; matendo Yangu yatakamilishwa, na mafanikio Yangu yatadumu milele. Hili linatumika kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanangu, watu Wangu, na hili linawahusu ninyi pia—Mimi kuwaadibu ninyi kutakuwa kwa milele. Nimewaambia mara nyingi kabla: Waovu wanaonipinga hakika wataadibiwa na Mimi. Unaponipinga bila ukaripiaji kutoka kwa Roho Mtakatifu, tayari umelaaniwa na baada ya hapo utapigwa chini na mkono Wangu. Ukipokea nidhamu ya Roho Mtakatifu unapokuwa na mawazo mabaya kunihusu, basi umepokea baraka Yangu. Hata hivyo, lazima uwe mwangalifu daima, usiwe mzembe kamwe, na usiwe mvivu kamwe.

Iliyotangulia: Sura ya 85

Inayofuata: Sura ya 87

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp