3. Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Katika kumwamini Mungu, angalau lazima utatue suala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Ikiwa huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi maana ya imani yako katika Mungu imepotea. Kuanzishwa kwa uhusiano wa kawaida na Mungu kunaweza kufikiwa kabisa kwa moyo ulio kimya katika uwepo wa Mungu. Kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu kunamaanisha kuweza kutokuwa na shaka na kutoikana kazi yoyote Yake na kuweza kuitii kazi Yake. Kunamaanisha kuwa na nia zisizo na makosa katika uwepo wa Mungu, kutofanya mipango kwa ajili yako mwenyewe, na kuzingatia masilahi ya familia ya Mungu kwanza katika mambo yote; kunamaanisha kukubali uchunguzi wa Mungu na kuitii mipango ya Mungu. Lazima uweze kuutuliza moyo wako katika uwepo wa Mungu katika yote ufanyayo. Hata kama huyaelewi mapenzi ya Mungu, bado unapaswa kutekeleza wajibu na majukumu yako kadiri uwezavyo. Mara tu mapenzi ya Mungu yanapofichuliwa kwako, lichukulie hatua, na hutakuwa umechelewa mno. Wakati ambapo uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa kwa msingi wa maneno ya Mungu. Kula na unywe maneno ya Mungu, kisha uyatie matakwa ya Mungu katika vitendo, rekebisha maoni yako, na uepuke kufanya chochote ili kumpinga Mungu au kulivuruga kanisa. Usifanye chochote ambacho hakifaidi maisha ya ndugu zako, usiseme chochote kisichowasidia wengine, na usifanye jambo lolote la aibu. Kuwa mwenye haki na mwenye heshima katika jambo unalotenda na uhakikishe kuwa kila kitendo chako kinapendeza mbele za Mungu. Ingawa wakati mwingine mwili unaweza kuwa dhaifu, lazima uweze kuweka masilahi ya familia ya Mungu kwanza, bila tamaa ya kupata faida ya kibinafsi, na lazima uweze kutenda kwa haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa namna hii, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?

Katika kila jambo unalofanya, sharti uchunguze ikiwa nia zako hazina makosa. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa. Chunguza nia zako, na ukiona kwamba nia mbaya zimejitokeza, uweze kuziacha na kutenda kulingana na maneno ya Mungu; hivyo utakuwa mtu aliye sawa mbele za Mungu, ambayo inaonyesha kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba yote unayoyafanya ni kwa ajili ya Mungu, si kwa ajili yako. Katika yote unayofanya na yote unayosema, uweze kuuweka moyo wako uwe sawa na uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, wala kutenda kulingana na mapenzi yako mwenyewe. Hizi ni kanuni ambazowaumini katika Mungu wanapaswa kutenda. Mambo madogo yanaweza kufichua nia na kimo cha mtu, na kwa hivyo, ili mtu aweze kuingia kwenye njia ya kukamilishwa na Mungu, lazima kwanza arekebishe nia zake na uhusiano wake na Mungu. Ni wakati tu uhusiano wako na Mungu unapokuwa wa kawaida ndipo unaweza kukamilishwa na Yeye; ni wakati huo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, ufundishaji nidhamu, na usafishaji wa Mungu vifanikisha athari zake zilizokusudiwa ndani yako. Hiyo ni kusema, ikiwa wanadamu wanaweza kumweka Mungu mioyoni mwao na wasifuatilie faida ya kibinafsi au kufikiria matarajio yao wenyewe (kwa njia ya mwili), lakini badala yake wabebe mzigo wa kuingia katika uzima, wajitahidi kabisa kuufuatilia ukweli, na kuitii kazi ya Mungu—ikiwa unaweza kufanya hivi, basi malengo unayoyafuatilia yatakuwa sawa, na uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Kuufanya uhusiano wa mtu na Mungu uwe muwafaka kunaweza kuitwa hatua ya kwanza ya kuingia katika safari ya kiroho ya mtu. Ingawa hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Mungu na imeamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na mwanadamu, kama unaweza kukamilishwa na Mungu au kupatwa na Yeye kunategemea ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Kunaweza kuwa na sehemu fulani ndani yako ambazo ni dhaifu au zisizotii—lakini mradi maoni yako na nia zako ni sawa, na mradi uhusiano wako na Mungu uko sawa na wa kawaida, basi unastahili kukamilishwa na Mungu. Ikiwa huna uhusiano muwafaka na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili au familia yako, basi bila kujali jinsi unavyotia bidii, itakuwa bure. Ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii kitu kingine chochote, lakini tu ikiwa maoni yako katika imani yako katika Mungu yako sawa: unamwamini nani, unaamini kwa ajili ya nani, na kwa nini unaamini. Ikiwa unaweza kuona mambo haya waziwazi na kutenda wakati maoni yako yakiwa na mwelekeo mzuri, basi utaendelea katika maisha yako, na pia utahakikishiwa kuingia kwenye njia muwafaka. Ikiwa uhusiano wako na Mungu si wa kawaida, na maoni ya imani yako katika Mungu yamepotoka, basi mengine yote ni bure, na haijalishi kadiri unavyoamini, hutapokea chochote. Ni baada tu ya uhusiano wako na Mungu kuwa wa kawaida ndipo utakapopata sifa kutoka Kwake unapoukana mwili, uombe, uteseke, uvumilie, utii, uwasaidie ndugu zako, ujitumie zaidi kwa ajili ya Mungu, na kadhalika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?

Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima kwanza umpe Yeye moyo wako, na kuutuliza moyo wako mbele za Mungu. Ni baada tu ya kuumimina moyo wako mzima kwa Mungu ndipo unaweza kuingia hatua kwa hatua katika maisha ya kiroho yanayostahili. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu. Mungu hawezi kupata kitu chochote kutoka kwa aina hii ya mtu; aina hii ya mtu anaweza tu kutumika kama foili[a] kwa kazi ya Mungu, kama pambo katika nyumba ya Mungu, kuchukua nafasi, naye hana manufaa—Mungu hamtumii aina hii ya mtu. Katika mtu kama huyo, sio tu kwamba hakuna nafasi kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu, hata zaidi hakuna thamani ya ukamilifu; aina hii ya mtu ni “mfu atembeaye” halisi—hana sehemu ambazo zinaweza kutumika na Roho Mtakatifu—wao wote wametwaliwa na Shetani, kupotoshwa kwa kiwango kilichokithiri na Shetani, ambao ni chombo cha kuondolewa na Mungu. Kwa sasa, katika kuwatumia watu, Roho Mtakatifu hatumii tu hizo sehemu zao zinazopendeza ili kufanikisha mambo, pia Anazikamilisha na kuzibadilish sehemu zao zisizopendeza. Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi na sifa za kuhitimu ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi, utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia dosari zako. Unapompa Mungu moyo wako, katika upande chanya, unaweza kupata uingiaji wa kina zaidi na ufikie kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa na dosari zako mwenyewe, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na hutakuwa katika hali ya kukaa tu, utaingia ndani kwa utendaji. Hii itamaanisha kuwa wewe ni mtu sahihi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Ikiwa unataka kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima moyo wako umgeukie Mungu. Hili likiwa msingi, pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu wengine. Iwapo huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi haijalishi unachofanya kudumisha uhusiano wako na watu wengine, haijalishi jinsi gani unafanya kazi kwa bidii au ni nguvu kiasi gani unaweka ndani yake, bado ni ya falsafa ya mwanadamu ya maisha. Unadumisha nafasi yako miongoni mwa watu kupitia mtazamo wa mwanadamu na falsafa ya mwanadamu ili kwamba watu wakupe wewe sifa, lakini hufuati neno la Mungu ili kuanzisha uhusiano wa kawaida na watu. Iwapo huzingatii uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, basi kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa wa kawaida. Kwa njia hii, uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwanadamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada zilizofanywa na binadamu. Unahitaji tu kutenda kulingana na maadili ya neno la Mungu. Je, unayo hiari ya kuwa mwenye kufikiria mapenzi ya Mungu? Je, uko tayari kuwa mtu “bila mantiki” mbele za Mungu? Je, uko tayari kuutoa moyo wako kwa Mungu kabisa, na kutofikiri kuhusu msimamo wako kati ya watu? Kati ya watu wote ambao una mawasiliano nao, ni gani ambao kati yao unayo mahusiano bora zaidi? Wepi kati yao ambao unayo mahusiano mabaya zaidi nao? Je, mahusiano yako na watu ni ya kawaida? Je, unawachukulia watu wote kwa usawa? Je, uhusiano wako na wengine umeimarishwa kwa mujibu wa falsafa yako ya maisha, ama umejengwa kwenye msingi wa upendo wa Mungu? Wakati mtu hautoi moyo wake kwa Mungu, basi roho yake inakuwa butu, inakufa ganzi na kutofahamu. Mtu wa aina hii kamwe hataelewa maneno ya Mungu na kamwe hatakuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu; tabia ya mtu wa aina hiikamwe haitabadilika. Kubadilisha tabia ya mtu ni mchakato wa mtu kuutoa kabisa moyo wake kwa Mungu, na wa kupokea nuru na mwangaza kutoka kwa maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu inaweza, kumruhusu mtu kuingia kwa utendaji, na pia kumwezesha kuepuka masuala yake hasi baada ya kupata maarifa. Unapoweza kuutoa moyo wako kwa Mungu, utaweza kuhisi kila harakati yenye hila ndani ya roho yako, nawe utajua kila nuru na mwangaza upokelewao kutoka kwa Mungu. Shikilia hili, nawe utaingia katika njia ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu hatua kwa hatua. Kadri moyo wako unavyoweza kuwa mtulivu mbele za Mungu, ndivyo roho yako itakavyokuwa makini zaidi na wa kutaka uangalifu mkubwa, na kadri roho yako itakavyoweza kutambua kuchochewa na Roho Mtakatifu, kisha uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida zaidi na zaidi. Uhusiano wa kawaida kati ya watu huundwa juu ya msingi wa kumpa Mungu mioyo yao haufanikishwi kupitia jitihada za binadamu. Bila Mungu mioyoni mwao, uhusiano kati ya watu ni uhusiano wa mwili tu. Sio uhusiano wa kawaida, lakini badala yake, ni utelekezaji kwa ajili ya tamaa za mwili. Ni uhusiano ambao Mungu anachukia, Asioupenda. Ukisema kuwa roho yako imeguzwa, lakini daima unataka kuwa na ushirika na watu wanaokupendeza, na wale unaowachukulia kwa hali ya juu, na iwapo kuna mtafutaji mwingine ambaye hakupendezi, ambaye huna upendeleo kwake na huwezi kujihusisha naye, huu ni ushahidi zaidi kuwa wewe uko chini ya hisia zako na kuwa huna uhusiano wa kawaida na Mungu kamwe. Unajaribu kumdanganya Mungu na kuficha ubaya wako mwenyewe. Hata ingawa unaweza kushirikisha uelewano kiasi lakini unabeba ubaya moyoni mwako, kila kitu unachofanya ni kizuri tu kwa kiwango cha mwanadamu. Mungu hatakusifu—unatenda kulingana na mwili, sio kulingana na mzigo wa Mungu. Iwapo unaweza kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu na kuwa na ushirikiano wa kawaida na wale wote wanaompenda Mungu, ni hapo tu ndipo utakuwa uko tayari kwa matumizi ya Mungu. Kwa njia hii, haijalishi jinsi unavyopatana na wengine, haitakuwa kulingana na falsafa ya maisha, lakini itakuwa kuishi mbele ya Mungu, kuufikiria mzigo Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Soma matamko yote ya Mungu na uyatie katika vitendo mara tu utakapoyaelewa. Labda kulikuwa na nyakati ambapo mwili wako ulikuwa dhaifu, au ulikuwa mwasi, au ulipinga; bila kujali jinsi ulivyotenda zamani, si muhimu, na haiwezi kuyazuia maisha yako kukomaa leo. Mradi unao uhusiano wa kawaida na Mungu leo, kuna matumaini. Ikiwa kuna mabadiliko ndani yako kila wakati unapoyasoma maneno ya Mungu, na wengine wanaweza kukuambia kuwa maisha yako yamebadilika na kuwa bora, inaonyesha kuwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida sasa, kwamba umerekebishwa. Mungu hawatendei watu kulingana na makosa yao. Mara tu unapoelewa na kufahamu, mradi unaweza kuacha kuasi au kupinga, basi bado Mungu atakuonea huruma. Unapokuwa na ufahamu na azimio la kufuatilia kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Haijalishi unachofanya, fikiria yafuatayo wakati unapofanya jambo hilo: Je, Mungu atafikiria nini nikifanya hili? Litawafaidi ndugu zangu? Litaifaidi kazi katika nyumba ya Mungu? Iwe ni katika sala, ushirika, hotuba, kazi, au kuwasiliana na wengine, zichunguze nia zako, na uchunguze ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Ikiwa huwezi kutambua nia na mawazo yako mwenyewe, hii inamaanisha kuwa huna upambanuzi, ambayo inathibitisha kwamba unaelewa ukweli kidogo sana. Ikiwa unaweza kuelewa vizuri kila kitu ambacho Mungu hufanya, na unaweza kuyatazama mambo kupitia katika maneno Yake, ukisimama upande Wake, basi maoni yako yatakuwa yamekuwa yasiyo na makosa. Kwa hivyo, kuanzisha uhusiano mzuri na Mungu ni muhimu sana kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuliona kama kazi muhimu sana na tukio kubwa kabisa katika maisha yake. Kila kitu unachofanya kinapimwa na kama una uhusiano wa kawaida na Mungu. Ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida na nia zako ni zisizo na makosa, basi chukua hatua. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupata hasara kwa masilahi yako ya kibinafsi; huwezi kumruhusu Shetani atawale, huwezi kumruhusu Shetani akununue, na huwezi kumruhusu Shetani akufanye uwe kichekesho. Kuwa na nia kama hiyo ni ishara kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida—si kwa ajili ya mwili, bali ni kwa ajili ya amani ya roho, kwa ajili ya kuipata kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali inayofaa, lazima uimarishe uhusiano mzuri na Mungu na urekebishe maoni ya imani yako katika Mungu. Hii ni ili Mungu aweze kukupata, na ili Aweze kudhihirisha matunda ya maneno Yake ndani yako na kukupa nuru na kukuangazia hata zaidi. Kwa njia hii, utakuwa umeingia katika njia inayofaa. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya leo, ingia katika njia ya sasa ya Roho Mtakatifu ya kufanya kazi, tenda kulingana na matakwa ya Mungu ya leo, usifuate mbinu za zamani za kutenda, usishikilie njia za zamani za kufanya mambo, na uingie katika njia ya leo ya kufanya kazi haraka iwezekanavyo. Hivyo, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utakuwa umeanza kutembea katika njia muwafaka ya imani katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?

Tanbihi:

a. “Foili” inahusu mtu au kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: 2. Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Inayofuata: 4. Adabu Takatifu Ambayo Waumini wa Mungu Wanapasa Kuwa Nayo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp