2. Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Maneno Husika ya Mungu:

Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kwa maneno sawa. Kiini Chake na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Mungu asipofanya kazi Yake binafsi na kunena maneno Yake miongoni mwa wanadamu, basi, haijalishi chochote, mwanadamu hangeweza kuelewa nia za Mungu. Na hivyo, hata wale ambao wamejitolea maisha yao yote kwa Mungu hawangeweza kupokea kibali Chake. Mungu asipoanza kufanya kazi, basi haijalishi mwanadamu atafanya vizuri kiasi gani, yote yatakuwa bure, kwa sababu mawazo ya Mungu daima yatakuwa juu kuliko mawazo ya mwanadamu, na hekima ya Mungu haiwezi kueleweka na mtu yeyote. Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi” Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi? Tunafaa sote kujua kwamba watu, ambao ni wa mwili, wote wamepotoshwa na Shetani. Ni katika hali yao asili kumuasi Mungu, na hawako katika usawa na Mungu, sembuse kuweza kutoa mawaidha kwa kazi ya Mungu. Jinsi Mungu anavyomwelekeza mwanadamu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mwanadamu anafaa kunyenyekea, na hafai kuwa na wazo hili ama lile, kwani mwanadamu ni mchanga tu. Kwa sababu tunajaribu kumtafuta Mungu, hatufai kuwekelea dhana zetu katika kazi ya Mungu ili Mungu Aziwaze, na zaidi hatufai kutumia tabia zetu potovu kwa kupinga kazi ya Mungu kwa makusudi. Je hili halitatufanya wapinga Kristo? Je, watu kama hawa watawezaje kusema kuwa wanamwamini Mungu? Kwa maana tunaamini kuwa kuna Mungu, na kwa maana tunatamani kumtosheleza na kumwona, tunapaswa kutafuta njia ya ukweli, na tunapaswa kutafuta njia ya kulingana na Mungu. Hatupaswi kuwa katika upinzani sugu kwa Mungu; Matendo kama haya yatakuwa na matokeo gani mazuri?

Leo hii, Mungu amefanya kazi mpya. Unaweza kukosa kuyakubali maneno haya, na yanaweza kuonekana yasiyo ya kawaida kwako, lakini Ningekushauri usifichue asili yako halisi kwa sasa, kwa maana wale tu walio na njaa ya kweli na kiu cha haki mbele za Mungu ndio wanaweza kupata ukweli, na wale wanaomcha Mungu kwa ukweli tu ndio wanaoweza kupata nuru na kuongozwa na Yeye. Ni kwa kutafuta kwa utulivu ndio tunaweza kupata matokeo. Ninaposema kwamba “leo, Mungu Anayo kazi mpya,” Ninaashiria Mungu kurudi katika mwili. Pengine huyajali maneno haya, pengine unayachukia, au pengine una haja kubwa sana nayo. Haijalishi ni hali gani, Natumai kuwa wote walio na tamaa ya kweli ya kuonekana kwa Mungu wataweza kuukabili ukweli huu na kutafakari juu yake kwa makini. Ni vyema usiamue jambo upesi bila kuzingatia suala zima. Hivi ndivyo watu wenye hekima wanapaswa kutenda.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini muwe watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wana kiu na hamu ya kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua mambo kiholela bila kuzingatia suala zima; hata zaidi, msiwe wenye kuchukulia mambo kwa wepesi na msiwe hobelahobela katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaomwamini Mungu wanafaa kuwa na mioyo ya unyenyekevu na imwogopayo Mungu. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu ni watu wenye kiburi. Hakuna anayemwamini Yesu anayestahili kuwalaani au kuwashutumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Kwa kuwa tunatafuta hatua za Mungu, inatulazimu tutafute nia ya Mungu, maneno ya Mungu, na matamko Yake. Hii ni kwa sababu popote palipo na maneno mapya yanayonenwa na Mungu, sauti ya Mungu ipo hapo, na popote palipo na hatua za Mungu, matendo ya Mungu yapo hapo; popote palipo na maonyesho ya Mungu, Mungu anaonekana hapo, na popote anapoonekana Mungu, ukweli, njia, na uzima vipo hapo. Katika kutafuta hatua za Mungu, ninyi mmeyapuuza maneno “Mungu ni ukweli, njia, na uzima.” Na hivyo, watu wengi, hata wanapoupata ukweli, hawaamini kuwa wamepata hatua za Mungu, na sembuse kukiri kuonekana kwa Mungu. Hili ni kosa zito kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulingana na mawazo ya mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa jinsi mwanadamu anavyodai Yeye aonekane. Mungu anafanya uamuzi Wake mwenyewe na Ana mipango Yake mwenyewe Anapofanya kazi Yake; zaidi ya hayo, Ana malengo Yake, na mbinu Zake mwenyewe. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, sembuse kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na, zaidi ya hayo, inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Ikiwa unatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama unatamani kufuata nyayo za Mungu, basi ni sharti kwanza uzishinde dhana zako mwenyewe. Haupaswi kudai kwamba Mungu afanye hiki au kile, sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yako mwenyewe na kumzuia kwa dhana zako mwenyewe. Badala yake, unapaswa kujua jinsi utakavyotafuta nyayo za Mungu, na jinsi unavyopaswa kukubali kuonekana kwa Mungu, na jinsi unavyopaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.

Bila kujali kama wewe ni Mmarekani, Mwingereza, au mtu wa taifa jingine, ni lazima utoke nje ya mipaka ya utaifa wako, ni lazima ujivuke mwenyewe, na unapaswa kuitazama kazi ya Mungu kutoka kwa utambulisho wa kiumbe aliyeumbwa. Kwa njia hii, hutaweka mipaka katika nyayo za Mungu kwa upeo wowote ule. Hii ni kwa sababu, siku hizi, watu wengi wanafikiri kuwa haiwezekani Mungu kutokea katika taifa fulani au miongoni mwa watu fulani. Ni jinsi gani umuhimu wa kazi ya Mungu ulivyo wa kina, na ni jinsi gani kuonekana kwa Mungu kulivyo muhimu! Inawezekanaje hii iweze kupimwa kwa dhana na mawazo ya mwanadamu? Na ndio maana Ninasema kwamba, unapaswa kuvuka dhana zako za utaifa na kabila ili kutafuta kuonekana kwa Mungu. Ni kwa njia hii tu hautafungwa na dhana zako mwenyewe; kwa njia hii, utahitimu kukaribisha kuonekana kwa Mungu. Vinginevyo, daima utakuwa gizani na hutapata kibali cha Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Mungu ni Mungu wa jamii yote ya wanadamu. Hajichukulii kuwa mali binafsi ya taifa lolote au watu, bali Anaenda huku na huko kufanya kazi Yake jinsi Alivyoipanga, bila kuzuiliwa na mfumo wowote, taifa, au watu. Labda hujawahi kuufikiria mfumo huu, au pengine mtazamo wako kwa mfumo huu ni wa kukana, au pengine taifa ambalo Mungu anajidhihirisha Mwenyewe na watu ambao Anajidhihirisha miongoni mwao inatokea kuwa wanabaguliwa na kila mtu na inatokea kuwa ni watu walio nyuma sana duniani. Hata hivyo Mungu ana hekima Yake. Kwa uwezo Wake, kupitia ukweli Wake, na tabia Yake, kwa hakika Amepata kundi la watu ambao wana mawazo sawa na Yeye, na Amepata kundi la watu Aliotaka kuwakamilisha—kundi lililoshindwa na Yeye, ambao, wamevumilia kila aina ya majaribio na dhiki, na kila aina ya mateso, na wanaweza kumfuata Yeye mpaka mwisho. Lengo la kuonekana kwa Mungu, ambako hakuzuiliwi na mfumo au taifa lolote, ni ili kumwezesha Yeye akamilishe kazi Yake jinsi Alivyoipanga. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kukamilisha kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kufanyika mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu, na hatimaye kupelekea kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kwa nguvu zao zote kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, lakini wakati huo huo wanashutumu kuonekana Kwake; “haiwezekani” yao kwa mara nyingine tena inaweka kuonekana kwa Mungu ndani ya mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakiangua kicheko baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Lakini je, kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kufuru za Wayahudi? Huna heshima mbele ya ukweli, sembuse kuutamani ukweli. Nyinyi mnachunguza tu kama vipofu na kungoja bila kujali. Je, mtafaidi. Je, mtafaidi nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kutambua matamshi ya Mungu, ni kwa njia gani unastahili kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anaonekana, pana maonyesho ya ukweli, na pana sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni watu kama hao tu ndio waliohitimu kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Wekeni kando mitazamo yenu ya “haiwezekani”! Kadiri watu wanavyozidi kuamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo kulivyo zaidi na uwezekano wake wa kutokea, kwa kuwa hekima za Mungu ziko juu zaidi kuliko mbingu, mawazo ya Mungu ni ya juu zaidi kuliko mawazo ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inavuka mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kinavyokuwa zaidi na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kinavyokuwa nje ya mipaka ya dhana na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Hii ni kwa sababu, haijalishi ni wapi ambapo Anaonekana, Mungu bado ni Mungu, na kiini Chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali au jinsi ya kuonekana Kwake. Tabia ya Mungu hubaki kuwa vilevile bila kujali nyayo Zake ziko wapi. Bila kujali ni wapi nyayo za Mungu zilipo, Yeye ndiye Mungu wa wanadamu wote. Kwa mfano, Bwana Yesu si Mungu tu wa Waisraeli, lakini vilevile ni Mungu wa watu wote wa Asia, Ulaya, na Marekani, na hata zaidi, ndiye Mungu pekee wa ulimwengu mzima. Hivyo basi, tutafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake vipo kwa wakati mmoja, na tabia na nyayo Zake huonyeshwa hadharani kwa wanadamu kila wakati. Akina kaka na dada wapendwa, Natumaini kwamba mnaweza kuona kuonekana kwa Mungu katika maneno haya, na kwamba mnaweza kuanza kufuata nyayo Zake na kupiga hatua kuelekea enzi mpya, na kuingia katika mbingu mpya na dunia mpya nzuri ambayo Mungu ametayarisha kwa ajili ya wale wanaosubiri kuonekana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Iliyotangulia: 1. Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Inayofuata: 3. Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp