33. Pingu za Umaarufu na Faida

Na Jieli, Uhispania

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, nia zake husuda ni za kuchukiza? Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI). Ningependa kushiriki uzoefu na ufahamu wangu fulani unaohusiana na maneno ya Mungu.

Mnamo mwaka wa 2015, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa katika uchaguzi wa kila mwaka. Nilifurahi sana, nikidhani kwamba kuchaguliwa kuwa kiongozi kati ya ndugu wengi sana hakika kulimaanisha kwamba nilikuwa bora kuwaliko wengine. Katika wajibu wangu kuanzia wakati huo, ndugu walinijia kwa ajili ya ushirika walipokuwa na matatizo ya kuingia katika uzima, na viongozi wa timu walijadili nami masuala waliyokabiliana nayo katika kazi ya kanisa. Sikuweza kujizuia kuhisi kwamba nilikuwa bora. Nilitembea huku na kule kwa kujigamba, kifua changu kikiwa mbele, na nilijiamini sana nilipofanya ushirikia katika mikutano. Baada ya muda, niligundua kwamba Dada Liu, mfanyakazi mwenzangu, alikuwa na ubora mzuri wa tabia, ushirika wake kuhusu ukweli ulikuwa wazi sana, na aliweza kufahamu kiini cha matatizo ya watu ili kuyasuluhisha. Alionyesha pia njia za utendaji, na kila mtu alitaka kusikia ushirika wake. Nilivutiwa naye na kumwonea kijicho. Lakini sikutaka kushindwa, kwa hivyo nilijiandaa kwa uangalifu kabla ya kila mkutano, huku nikipiga bongo kuhusu jinsi ya kufanya ushirika kwa upana zaidi na kwa ufananuzi zaidi ili nionekane kuwa bora kumliko. Nilipowaona ndugu wakitikisa vichwa kwa kukubali nilipomaliza kufanya ushirika, niliridhika sana na nilihisi utimilifu. Baadaye, niligundua kuwa mfanyakazi mwenzangu Ndugu Zheng alikuwa na maarifa ya kitaalamu ya filamu na kwamba alikuwa hodari wa kutumia kompyuta. Ndugu waliofanya wajibu wa kufanyiza filamu walijadili naye masuala husika mara nyingi, na mimi kama kiongozi wa kanisa sikuwa na lolote la ziada la kusema. Nilihisi kama mtu asiye na maana, na hilo halikuniridhisha kabisa. Nilidhani kwamba kwa kumtafuta Ndugu Zheng wakati wowote walipokuwa na tatizo hakika walifikiri kwamba sikuwa mwenye uwezo kama wake. Nilifikiria kwamba itakuwa vyema nikijua kitu kuhusu filamu pia, kisha ndugu watajadili nami kuhusu masuala yao. Nilianza kuamka mapema na kukaa macho hadi usiku mkuu nikifanya utafiti na kujifunza jinsi ya kutengeneza filamu ili niweze kujua zaidi. Nilipuuza kabisa masuala yote yaliyokuwa kanisani na pia hali za ndugu. Baadaye kidogo, matatizo yalianza kutokea katika kazi ya timu kadhaa ambayo sikuweza kabisa kutatua bila kujali jinsi nilivyoshiriki au kufanya mikutano. Kwa kuwa hali za ndugu hazikuwa zimetatuliwa, maendeleo ya utengenezaji wa filamu yalizuiwa na matatizo yalikuwa yakitokea moja baada ya lingine. Nilishinikizwa sana kiasi kwamba sikuweza kupumzika. Niliteseka. Nilionea wasiwasi jinsi ambavyo wengine wataniona, iwapo watafikiri kwamba sikuwa kabisa na uwezo kama kiongozi na kwamba sikustahili kufanya wajibu huo. Ilionekana kana kwamba sikuweza kushikilia cheo changu kama kiongozi. Nilizidi kuwa hasi nilipokuwa nikifikiria hayo. Nilihisi kama baluni iliyotolewa pumzi na sikuwa na nguvu niliyokuwa nayo hapo awali. Kwa sababu ya kuishi katika uhasi na kuzembea katika wajibu wangu, nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu mwishowe. Kwa kuwa sikuwa nikifanikisha lolote katika wajibu wangu, nilibadilishwa na mwingine. Wakati huo nilihisi kama kwamba nilikuwa nimepoteza heshima kabisa na nilitaka ardhi inimeze. Nilikuwa nikijiuliza pia, “Je, ndugu watasema kwamba nilikuwa kiongozi wa uwongo ambaye hakufanya kazi ya vitendo?” Nilifadhaika zaidi nilipofikiria hilo sana.

Nililala kitandani huku nikigaagaa na kugeuka usiku huo, na sikuweza kulala. Nilimwomba Mungu tena na tena, nikimsihi Aniongoze ili nijue hali yangu. Kisha nikasoma maneno haya ya Mungu: “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na daima watu hawawezi kuondoa vishawishi hivi vya Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wao huwaza: ‘Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.’ … Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?). Nilitafakari kuhusu hali yangu ya hivi karibuni baada ya kusoma haya. Tangu nilipokubali wajibu wa kiongozi sikuwa nimefanya lolote ila kufuatilia sifa na hadhi na kutaka kuwapiku wengine. Nilipoona kwamba ushirika wa Dada Liu kuhusu ukweli ulikuwa bora kuliko wangu, niliogopa kwamba atanishinda. Nilifikiria jinsi ya kufanya ushirika bora kumliko ili wengine wanistahi na kunisifu. Nilipoona kwamba Ndugu Zheng alikuwa na ujuzi wa kitaalamu na ndugu wengi walizungumza naye juu ya matatizo yaliyokuwa katika wajibu wao, nilianza kuwa na wivu na nilimkataa. Nilijitahidi kujiandaa kwa maarifa ili nimshinde, na hata nilipuuza matatizo yaliyokuwa ndani ya timu. Wakati ambapo sikuweza kusuluhisha matatizo ya kina ndugu, sikumtegemea Mungu, wala kutafuta ukweli pamoja na kina ndugu ili kupata suluhisho kupitia ushirika. Nililenga tu faida na kupoteza hadhi, nikihofia kwamba sitaweza kushikilia cheo changu kama kiongozi ikiwa sitafanya wajibu wangu vizuri. Halafu hatimaye nikagundua kwamba sikuwa nikifanya wajibu wangu kwa kuzingatia mapenzi ya Mungu hata kidogo, bali ili kukidhi tamaa yangu kuu ya kuwa bora kuwaliko wengine na kuwatawala wengine. Ndugu waliniamini na kunichagua niwe kiongozi wa kanisa, lakini sikuzingatia kazi ya kanisa au kuingia kwao katika uzima hata kidogo. Sikuwa nikichukua wajibu wangu kabisa au kuwajibika, na hii iliishia kudhuru kazi ya kanisa. Nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau sana. Sikuwa nikifanya wajibu wangu—nilikuwa nikifanya uovu na kumpinga Mungu! Nilijutia kutokuwa kwenye njia sahihi katika imani yangu, lakini kila wakati nilipigania sifa na faida, na kumchukiza Mungu. Kuachishwa wajibu wangu kulikuwa hukumu ya Mungu ya haki na kuadibu Kwake. Hakuwa Akiniondoa, bali Alifanya nibadilishwe na mwingine ili nitafakari juu ya tabia yangu. Ni Mungu aliyekuwa Akinilinda na kuniokoa! Hali yangu ilianza kuboreka—kupitia kipindi cha ibada na kutafakari, kwa hivyo kiongozi wa kanisa alinipangia nifanye wajibu wa kawaida. Nilimshukuru Mungu sana kwa kunipa nafasi hiyo, na niliamua kimoyomoyo kwamba nitathamini wajibu huo, na kuacha kufuatilia sifa na hadhi kwenye njia impingayo Mungu.

Baada ya tukio hilo nilidhani kwamba nitaweza kuacha hamu yangu ya sifa na hadhi kidogo, lakini nilikuwa nimepotoshwa mno na Shetani. Aina hiyo ya tabia ya kishetani haiwezi kutatuliwa na ufahamu mdogo na kutafakari, kwa hivyo Mungu kwa mara nyingine aliandaa hali ili kunifunua na kuniokoa.

Siku moja miezi michache baadaye, kiongozi wa kanisa alituambia tuchague kiongozi wa timu. Mara niliposikia hayo nilianza kupima: “Je, nina nafasi ya kuchaguliwa kama kiongozi wa timu? Mimi ni mfanyakazi hodari sana, lakini sina ujuzi wowote wa kitaalamu, kwa hivyo pengine sina uwezekano mkubwa wa kuchaguliwa.” Kisha nilifikiri juu ya ndugu wengine wachache waliokuwa kwenye timu. Ndugu Zhang alikuwa bora kwa sababu ya ustadi wa kitaalamu na ushirika wake juu ya ukweli ulikuwa wa vitendo, na alijua haki na aliweza kuitetea kazi ya kanisa. Kwa jumla, ilionekana kana kwamba alikuwa na uwezekano mkubwa wa kuchaguliwa. Nilifikiria jinsi nilivyokuwa nikimpa kazi Ndugu Zhang nilipokuwa kiongozi wa kanisa, lakini akichaguliwa kuwa kiongozi wa timu, atakuwa akiniambia la kufanya. Je, hilo halitanifanya nionekane kuwa dhalili kumliko? Wazo hili lilinitia wasiwasi sana. Siku ya uchaguzi ilipofika, sikuweza kujizuia kuwa na wasiwasi, na vita vya ndani vilianza: “Nimpigie nani kura? Nimpigie kura Ndugu Zhang?” Nilifikiria jinsi ndugu wengi walivyojadili naye shida yoyote waliyokuwa nayo katika wajibu wao, na watu katika timu nyingine pia walijadili kazi zao naye wakati wote—ilimfanya aonekane kuwa mzuri sana. Je, akiwa kiongozi wa timu, je, hatakuwa wa ngazi ya juu kuniliko? Baada ya kufikiria hayo, sikutaka kumpigia kura tena, lakini sikuwa na maarifa ya kitaalamu na sikustahili kuwa kiongozi wa timu hiyo. Nilivunjika moyo na kufadhaika sana, na nilichukia kwamba sikujua zaidi kuhusu kazi hiyo. Wakati huo huo, wazo baya lilinijia akilini: “Iwapo siwezi kuwa kiongozi wa timu, nitahakikisha wewe pia hutakuwa.” Kwa hivyo, nilimpigia kura Ndugu Wu, ambaye hakuwa na ujuzi mwingi wa kitaalamu. Kwa mshangao wangu, Ndugu Zhang bado ndiye aliyeshinda. Sikufurahi nilipoona mambo yakiwa vile, lakini nilijawa na wasiwasi mara moja, kana kwamba nilikuwa nimefanya kitu cha aibu. Baadaye nilisoma maneno haya ya Mungu: “Wakimwona mtu aliye bora kuwaliko, wanamkandamiza, wanaanzisha uvumi kumhusu, au kutumia njia za uovu ili watu wengine wasimheshimu, na kwamba hakuna mtu aliye bora kuliko mtu mwingine, basi hii ni tabia potovu ya kiburi na yenye kujidai, na vile vile ya uovu, udanganyifu na kudhuru kwa siri, na watu hawa hawazuiwi na chochote katika kufikia malengo yao. Wanaishi namna hii na bado wanafikiria kuwa wao ni wazuri na kwamba wao ni watu wema. Hata hivyo, je, wana mioyo inayomcha Mungu? Kwanza kabisa, kuzungumza kutoka katika mtazamo wa asili za mambo haya, je, watu ambao hutenda hivi hawafanyi vile wapendavyo tu? Je, wao hufikiria masilahi ya familia ya Mungu? Wanafikiria tu kuhusu hisia zao na wanataka tu kufikia malengo yao wenyewe, bila kujali hasara inayopatwa na kazi ya familia ya Mungu. Watu kama hawa sio tu wenye kiburi na wa kujidai, pia ni wabinafsi na wenye kustahili dharau; hawajali kabisa kuhusu kusudi la Mungu, na watu kama hawa, bila shaka yoyote, hawana mioyo inayomcha Mungu. Hii ndiyo sababu wanatenda chochote wanachotaka na kutenda kwa utundu, bila hisia yoyote ya lawama, bila hofu yoyote, bila wasiwasi au shaka yoyote, na bila kuzingatia matokeo. Hawamchi Mungu, wanajiamini kuwa muhimu sana, na wanaona kila kipengele chao kuwa cha juu kumliko Mungu na cha juu kuliko ukweli. Mioyoni mwao, Mungu ndiye wa chini zaidi anayestahili kutajwa na Asiye na maana zaidi, na Mungu hana hadhi yoyote mioyoni mwao hata kidogo. Je, wale ambao hawana nafasi ya Mungu mioyoni mwao, na wasiomcha Mungu, wamepata kuingia katika ukweli? (Hapana.) Kwa hivyo, kwa kawaida wakati wao huzunguka wakijishughulisha kwa furaha na kuweka nguvu nyingi, wao huwa wanafanya nini? Watu kama hao hata hudai kuwa wameacha kila kitu ili kutumika kwa ajili Mungu na kwamba wamepitia shida nyingi, lakini kwa kweli, nia, kanuni, na lengo la vitendo vyao vyote ni kujinufaisha; wanajaribu tu kulinda masilahi yao yote. Je, mnaweza kusema kwamba mtu wa aina hii ni mbaya sana au la? Je, mtu asiyemcha Mungu ni mtu wa aina gani? Je, si yeye ni mwenye kiburi? Je, si yeye ni Shetani? Je, ni mambo ya aina gani ndiyo yasiyomcha Mungu? Kando na wanyama, wale wote wasiomcha Mungu ni pamoja na pepo, Shetani, malaika mkuu, na wale wanaobishana na Mungu(“Masharti Matano Ambayo Watu Wanayo Kabla ya Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilifadhaika sana niliposoma haya. Nilipokumbuka mawazo na matendo yangu wakati wa uchaguzi, nilihisi kana kwamba sitaweza kutokea mbele ya watu. Nilikuwa nimepiga kura kulingana na nia zangu za binafsi, ili kulinda cheo na sifa yangu njema, bila kukubali uchunguzi wa Mungu wa makini na bila kumcha Mungu hata kidogo. Nilijua kwamba Ndugu Zhang alikuwa stadi, ushirika wake juu ya ukweli ulikuwa wa vitendo, na yeye kuwa kiongozi wa timu kutafaidi kuingia katika uzima kwa kila mtu na kazi ya kanisa. Lakini niliona wivu, na niliogopa kuwa atakuwa wa ngazi ya juu kuniliko kama kiongozi wa timu, kwa hivyo sikumpigia kura kwa makusudi. Nilikuwa nimefuata kanuni ya joka kubwa jekundu ya “Udikteta usipofaulu, hakikisha demokrasia haifaulu.” Mbinu ya utendaji ya Joka kubwa jekundu ni kwamba, kama haliwezi kuwa madarakani, basi hakuna mtu mwingine awezaye. Ikilazimu, litatumia mapambano makali kuharibu pande zote. Je, sikuwa vilevile? Nisingetaka Ndugu Zhang apate cheo hicho kama singekipata mimi. Niliona kwamba ni afadhali mtu asiyestahili achukue wajibu huo na kazi ya kanisa iharibike ili nilinde sifa na hadhi yangu. Nilikuwa mbinafsi sana, mwenye kustahili dharau, mjanja, na mwovu, na asiyemcha Mungu hata kidogo. Nilikuwa nimefurahia ukweli ulioonyeshwa na Mungu, na kupata nafasi hiyo ya kufanya wajibu wangu kulikuwa Mungu kunionyesha wema. Lakini badala ya kufikiria jinsi ya kulipa upendo wa Mungu, niliona wivu na nilipania sifa na faida. Nilikuwa nikihudumu kama mtumishi wa Shetani, na kukatiza kazi ya nyumba ya Mungu. Je, sikuwa mpotovu na mdanganyifu? Nilifikiri kuhusu jinsi nilivyoachishwa wajibu wangu mwaka mmoja uliopita kwa sababu nilikuwa nikipigania sifa na faida, bila kufanya wajibu wangu vizuri, na sikuweza kufanya kazi ya vitendo. Na sasa, nilikuwa katika hali kama hiyo lakini bado nilikuwa nikifuatilia sifa na hadhi, wala si ukweli. Kama ningeendelea hivyo, ningedharauliwa na kuondolewa na Mungu.

Baadaye, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya). “Je, ni kwa nini Mungu husema kwamba watu ni ‘mabuu’? Machoni Pake, wanadamu hawa wapotovu bila shaka ni viumbe walioumbwa—lakini, je, wao hutimiza majukumu na wajibu ambao viumbe walioumbwa wanapaswa kutimiza? Ingawa watu wengi wanatekeleza wajibu wao, utendaji wao unaonyeshwaje vizuri? … Hakuna wanachofikiria kuhusu siku nzima kinachohusiana kwa vyovyote vile na ukweli au kufuata njia ya Mungu; wao hushinda siku nzima kula kwa pupa kupita kiasi, na hawafikirii chochote. Ingawa wanaweza kufikiria wafanye kitu, matendo yao bado husababisha usumbufu na vurugu. Wao hujiinua, kamwe wasifanye chochote kinachowafaidi wengine au nyumba ya Mungu. Akili zao zimejaa mawazo ya jinsi ya kutafuta chochote kinachoridhisha mwili, jinsi ya kupigania hadhi na umaarufu, jinsi ya kukubalika katika vikundi fulani vya watu, na jinsi ya kupata cheo na kuwa na sifa nzuri. Wanakula chakula ambacho Mungu amewapa, wakifurahia kila kitu Anachotoa, lakini hawafanyi kile ambacho wanadamu wanapaswa kufanya. Je, Mungu anaweza kuwapenda watu kama hao? … Zaidi ya yote, wale ambao ni mabuu hawana maana, hawana aibu, na machoni pa Mungu, hawana thamani! Je, kwa nini Nasema kwamba watu kama hao hawana thamani? Mungu alikuumba, na Akakupa uzima, lakini huwezi kutekeleza wajibu wako, ambao ndicho kitu cha kiwango cha chini zaidi unachopaswa kufanya; wewe unadoea tu. Machoni Pake, wewe ni mtu bure tu, na hakuna haja yoyote ya wewe kuwa hai. Je, watu kama hao sio mabuu? Kwa hivyo, watu wanapaswa kufanya nini ikiwa hawataki kuwa mabuu? Kwanza, tafuta mahali pako mwenyewe na ujaribu kwa kila njia inayowezekana kutekeleza wajibu wako, na utaunganishwa na Muumba; unaweza kumpa Yeye maelezo. Baada ya hayo, fikiria jinsi ya kufanikisha uaminifu katika kutimiza wajibu wako. Hupaswi kutenda kwa uzembe tu, au kumaliza wajibu kwa kubahatisha tu; badala yake, unapaswa kuufanya kwa moyo wako wote. Hupaswi kujaribu kumpumbaza Muumba. Unapaswa kufanya chochote ambacho Mungu anakwambia ufanye, na unapaswa kusikiliza na kutii(“Ishara Sita za Ukuaji katika Maisha” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, nilihuzunika mno. Niligundua kuwa Mungu aliona tabia yangu ya kishetani ya kupigania sifa na faida kama iliyo chafu na mbaya sana. Kuwa na bahati nzuri ya kutekeleza wajibu wangu katika nyumba ya Mungu kulikuwa kuinuliwa kwa kipekee na Mungu, lakini sikuwa nikitimiza wajibu wangu. Badala yake, nilifikiria tu sifa na hadhi yangu, na hata nilikatiza kazi ya nyumba ya Mungu kwa ajili ya vitu hivyo. Nilikuwa nimechukua nafasi ya Shetani. Hilo lilimchukiza Mungu na kumtia kinyongo! Mungu anasema, “Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi?” Naam. Mimi ni kiumbe, mtu mchafu na mpotovu asiye na thamani au hadhi hata kidogo, kwa hivyo hata nikipata cheo, hilo haliwezi kubadilisha utambulisho wangu. Sikuweza hata kutekeleza wajibu wangu vizuri, bali nilipigania sifa na faida kila mara, na nilitaka wengine wanistahi. Dhamiri na mantiki yangu vilikuwa wapi? Je, maisha yangu yalikuwa na thamani gani? Je, sikuwa mnyoo asiyefaa kabisa? Baada ya kupata ufahamu kiasi kuhusu asili na kiini changu kutoka kwa yale yaliyofichuliwa na maneno ya Mungu, nilijichukia na nikawa tayari kuukana mwili na kutenda ukweli.

Baadaye nilienda kumtafuta Ndugu Zhang na nilimweleza juu ya upotovu wangu, nikifichua nia na vitendo vyangu vya kustahili dharau katika uchaguzi huo. Mbali na kutonidharau, pia alishiriki juu ya uzoefu wake ili anisaidie. Baada ya kufanya ushirika, kizuizi kilichokuwa kati yetu kilitoweka na nilihisi mwenye amani na mtulivu kabisa. Katika wajibu wangu, kuanzia wakati huo, kila nilipokuwa na tatizo au wakati ambapo sikuelewa suala fulani, nilikwenda kwa Ndugu Zhang kutafuta, na kila mara alijibu maswali yangu kwa uvumilivu kupitia ushirika. Ujuzi wangu wa kitaalamu ulianza kuboreka baada ya muda. Nilipoacha sifa na hadhi na kutenda ukweli, nilipata raha na amani itokanayo na kutekeleza wajibu wangu kwa njia hiyo, na nilizidi kumkaribia Mungu. Nilikwepa tena pingu za sifa na hadhi kupitia hali hiyo na nilionja wokovu wa Mungu wa vitendo kwangu.

Uchaguzi wa kila mwaka wa kanisa ulianza mnamo Oktoba 2017, na kina ndugu walipendekeza kwamba niwe mgombea. Nilitetereka kihisia, nikiwaza, “Imekuwa zaidi ya miaka miwili tangu nilipoondolewa katika cheo changu cha uongozi, na nimesikia kwamba ndugu wengine wana maoni mazuri juu yangu. Wanasema kwamba ushirika wangu umekuwa wa vitendo zaidi na nimepitia mabadiliko fulani. Sijui kama nitaweza kupata cheo cha uongozi wakati huu.” Niligundua kwamba nilikuwa nikifuatilia sifa na hadhi tena na nilitafakari juu ya jinsi ilivyohuzunisha hapo zamani nilipozuiwa na vitu hivyo. Nilijua kwamba sikupaswa kuendelea na ufuatiliaji huo, kwamba nilipaswa kuukana mwili na kutenda ukweli. Kisha nilikumbuka kuhusu kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Mara unapoachilia ufahari na hadhi ambavyo ni vya Shetani, hutazuiliwa na kudanganywa tena na maoni na mitazamo ya kishetani. Utapata uhuru, na utahisi mtulivu zaidi na zaidi; utakuwa huru na uliyekombolewa. Siku hiyo itakapokuja ambapo wewe utakuwa huru na uliyekombolewa, utahisi kwamba vitu ambavyo umeacha vilikuwa mitego tu, na kwamba vitu ambavyo umepata kwa kweli ni vya thamani sana kwako. Utahisi kwamba hivyo ndivyo vitu vya thamani kuliko vyote, na ndivyo vitu vinavyostahili kuthaminiwa kuliko vyote. Hivyo vitu ulivyovipenda—anasa yakinifu, umaarufu na mali, hadhi, pesa, sifa, na heshima ya wengine—vitaonekana kuwa visivyo vya maana kwako; vitu hivyo vimekusababishia mateso makubwa, na hutavitaka tena. Hutavitaka tena hata ukipewa ufahari na hadhi ya kiwango cha juu zaidi; badala yake, utavichukia na kuvikataa kwa dhati!(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Moyo wangu ulichangamka, na nilijua kuwa kufuatilia sifa na hadhi hakukuwa na thamani, na kwamba kufahamu na kutenda ukweli na kutekeleza wajibu wa kiumbe ndivyo vitu vya thamani zaidi. Kwa kweli, kushiriki katika uchaguzi hakukuwa ili kupigania nafasi ya uongozi, lakini kulikuwa ili kutekeleza majukumu yangu kwa kushiriki katika mchakato huo. Ilinibidi niache tamaa zangu kuu za sifa na hadhi na kumpigia kura kiongozi aliyefaa kulingana na kanuni za ukweli. Hilo ndilo litakuwa la kufaa kwa kazi ya nyumba ya Mungu. Kama ningechaguliwa kama kiongozi, ningepaswa kufanya wajibu wangu vizuri. Iwapo singepata kuchaguliwa, singemlaumu Mungu, lakini ningefanya wajibu wangu kadiri niwezavyo. Mara niliporekebisha nia zangu kuhusu uchaguzi, kwa mshangao wangu, nilichaguliwa ili kuhudumu kama kiongozi. Nilipoona matokeo haya, sikufurahia tena kama nilivyofanya hapo zamani, nikidhani kwamba nilikuwa bora kuwaliko wengine, lakini nilihisi kwamba ni agizo na wajibu wangu, na ninapaswa kuzingatia kufuatilia ukweli na kutekeleza wajibu wangu vizuri ili niweze kustahili upendo na wokovu wa Mungu.

Kwa wakati huo, karibu miaka mitatu, hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake vimenionyesha waziwazi jinsi ambavyo sifa na hadhi hunidhuru, na nimeazimia kufuatilia ukweli. Hata ingawa wakati mwingine mimi bado hudhihirisha tabia hiyo hiyo upotovu, ninaweza kumwomba Mungu kimakusudi, kuzingatia kutenda ukweli, na kufanya wajibu wangu vizuri. Sizuiwi tena na tabia yangu potovu na ya kishetani. Nilipoacha sifa na hadhi, nilihisi kwamba si hayo pekee niliyoacha, bali nilikuwa pia nimeacha pingu nzito ambazo Shetani alikuwa amenifunga nazo. Ninahisi mtulivu na aliye huru sana.

Iliyotangulia: 32. Roho Yangu Yakombolewa

Inayofuata: 35. Siku za Kutafuta Umaarufu na Faida

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Katikati ya Jaribu la Kifo

Na Xingdao, Korea ya KusiniMwenyezi Mungu anasema, “Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo...

73. Wokovu wa Mungu

Na Yichen, UchinaMwenyezi Mungu anasema: “Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa...

29. Toba ya Afisa

Na Zhenxin, UchinaMwenyezi Mungu anasema, “Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, yote ambayo Mungu amefanya katika kazi Yake ni upendo, bila...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp