35. Siku za Kutafuta Umaarufu na Faida

Na Li Min, Uhispania

Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu(“Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu” Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kuimba wimbo huu wa maneno ya Mungu kunanigusa sana, Nilikuwa nikiishi kwa kufuata sumu za Shetani kama vile “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake,” Na “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini.” Mara kwa mara nilitafuta umaarufu na hadhi, nikiwa nimedanganywa na kuharibiwa na Shetani, nikihangaikia faida na hasara za kujipatia sifa. Ilikuwa njia chungu ya kuishi. Mpaka nilipopata hukumu, kuadibu, na kufundishwa nidhamu na maneno ya Mungu ndipo nilikuja kuelewa kidogo kuhusu asili yangu potovu na nikapata uwazi kiasi kuhusu kiini na matokeo ya kutafuta umaarufu na hadhi. Mwishowe nilianza kugutuka na kuhisi majuto. Sikutaka tena kuishi kwa namna hiyo, lakini nilitaka tu kufuatilia ukweli na kufanya wajibu wangu vizuri ili kumridhisha Mungu.

Nakumbuka, ilikuwa mnamo Septemba ya 2016 ambapo nilijiunga na timu ya nyimbo kutimiza wajibu wangu. Muda mfupi baada ya hapo, kiongozi wetu alitujia kujadili kuhusu kuchagua kiongozi wa timu. Nilifurahi sana mara tu niliposikia hili na nikaanza kuwapima wagombea watarajiwa mawazoni mwangu. Ndugu wengine katika timu yangu walikuwa wachanga sana au hawakuwa na ujuzi wa kutosha. Kulikuwa tu na Ndugu Li—ushirika wake kuhusu ukweli ulikuwa wa vitendo kweli, na alielewa baadhi ya kazi hiyo. Pia, alikuwa na tabia ya utulivu. Nilihisi kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa wa yeye kuchaguliwa, lakini ushirika wangu haukuwa mbaya pia, na nilikuwa mwanafunzi mzuri hasa na mwenye kujifunza mambo mapya kwa haraka. Pia nilikuwa mzuri katika kuona taswira nzima ya mambo. Kwa hivyo, nilifikiri nafasi yangu ya kuchaguliwa ilipaswa kuwa bora kuliko yake. Lakini kila mtu katika timu alikuwa mgeni kwa wajibu huo na hatukuwa tumefanya kazi pamoja kwa muda mrefu, kwa hivyo hatukujuana vizuri sana. Kama wangenichagua ni jambo ambalo halikujulikana. Kwa hivyo, nilimpendekezea kiongozi kwamba ahesabu wajibu ambao kila mmoja wetu alikuwa ametimiza, na kisha achague mtu wa kuiongoza timu kwa muda mfupi. Kila mtu alikubali. Nilifurahi kwa siri; nilihisi kwamba nilikuwa na rekodi nzuri katika wajibu, kwa hivyo labda nilikuwa nimeshajizolea uchaguzi huu. Siku iliyofuata, nilienda kwenye mkutano nikiwa nimejiamini kabisa. Lakini nilishangaa kwamba Ndugu Li alichaguliwa mwishowe. Kweli nilikatishwa tamaa wakati huo, lakini ili kuficha aibu, nilijifanya kuwa sikuwa nimetatizika na nikasema, “Shukrani ziwe kwa Mungu. Kuanzia sasa na kuendelea, sote tufanye kazi kwa pamoja ili tutekeleze wajibu wetu.” Ndani kabisa, hata hivyo, sikuweza kukubali hilo kabisa. Nilihisi mchovu sana nilipokuwa nikitembea kwenda nyumbani. Sikuweza kuelewa lililofanyika. Ndugu Li alikuwa na nini kilichonishinda mimi? Sikuweza kukubali hilo kabisa. Nilihisi kuwa nilikuwa na talanta nyingi, kwa hivyo kwa kutonichagua, huko hakukuwa kuziharibu tu? Kwa hivyo nilihisi kwamba nilihitaji kujithibitisha, na kuwaonyesha wengine uwezo niliokuwa nao. Ingawa nilionekana mtulivu kwa juu baada ya hapo, nilikuwa nikipambana dhidi ya Ndugu Li kwa kimya. Nilijitosa katika kusoma ili kuboresha ujuzi wangu ili niweze kumshinda yeye. Nilishangilia kimya kimya nilipoona kwamba alikuwa mwanafunzi mpole, nikiwaza, “Kwa hivyo ukweli hujitokeza! Wewe sio mzuri sana hata hivyo! Baada ya muda, ndugu zetu wote wataona ni nani aliye bora pia.” Nilisherehekea kila kosa dogo alilofanya, nikijiwazia, “Je, una uwezo wa kufanya kinachohitajika? Sasa watakuona jinsi ulivyo kweli!” Kumwona Ndugu Li akitatua shida za wengine kulinifanya nihisi wivu. Nilihisi kuwa nilikuwa na uzoefu wa vitendo wa aina hii pia, na kama ningekuwa kiongozi wa timu, ningekuwa mzuri katika kufanya ushirika, pia. Hasa tulipokuwa tunajadili kuhusu kazi, haijalishi kile ambacho Ndugu Li alipendekeza, nilikimbia kusema kitu cha kina zaidi na chenye umaizi zaidi.

Nakumbuka katika mkutano mmoja, tulipokuwa tunajadili maoni ya wimbo, Ndugu Li alitoa maoni mazuri sana. Lakini nilifikiria kama ningeyakubali, je, hilo halingemfanya aonekane bora kuniliko? Kisha ningewezaje kukosa kuaibika? Niliropoka hoja ya kupinga na nikatoa maoni tofauti, lakini kikundi kiliishia kuunga mkono wazo lake. Ilikuwa kama kofi usoni. Nilipowaona ndugu wakijadili kuhusu hilo kwa furaha, nilihisi upinzani zaidi kwa Ndugu Li, na sikuwa na shauku yoyote ya kusikiliza zaidi. Nilikumbuka wajibu wa awali niliokuwa nimetimiza; hata hivyo, nilikuwa kiongozi wa timu zamani, na ndugu wote waliniheshimu. Lakini sasa, sikuwa kiongozi wa timu tena, na alikuwa anaonekana bora kuniliko mara kwa mara. Kama ningejua hili lingetendeka, singekuja hapa kutimiza wajibu wangu. Baada ya mkutano, mawazo yangu yalikuwa yamevurugika, na nilikuwa nikihisi mwenye giza ndani Nikiwa na ufahamu usio dhahiri kwamba sikuwa katika hali sahihi, nilimwomba Mungu, na kifungu hiki cha maneno Yake kilinijia mawazoni: “Najua kwa kina uchafu ndani ya mioyo ya kila kiumbe, na kabla ya Mimi kuwaumba ninyi, Nilijua tayari udhalimu uliokuwepo ndani ya kina cha mioyo ya binadamu, na Niliujua udanganyifu na uhalifu wote katika mioyo ya binadamu. Kwa hiyo, hata ingawa hakuna kabisa dalili zozote wakati ambapo watu hufanya mambo ya udhalimu, bado Najua kwamba udhalimu uliowekwa ndani ya mioyo yenu hushinda utajiri wa vitu vyote Nilivyoumba. Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote, mkitafuta mahali pa amani na mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya). Maneno ya Mungu yalifunua ubaya wote wa kupigania kwangu sifa na faida. Tangu nijiunge na timu ya nyimbo, nilikuwa nimememezwa na tamaa ya makuu, nikifanya kila niwezalo kufanikisha kitu ili ndugu na kiongozi wote waniheshimu na kwamba niweze kupata mahali pa usalama katika timu. Wakati wa mchakato wa uteuzi, nilikuwa nimejaribu kutumia akili yangu kwa faida yangu mwenyewe, nikimfanya kiongozi afanye uchaguzi wa mpito kulingana na wajibu ambao tulikuwa tumetimiza hapo awali. Nilikuwa na wivu wakati Ndugu Li alichaguliwa, na nikawa na mtazamo wa ushindani kwake. Nilipoona matatizo kadhaa katika kazi yake, sikutetea masilahi ya kanisa au kujaribu kumsaidia, lakini nilikuwa nataka tu abadilishwe kwa sababu ya kukosa uwezo, ambalo lingenipa uwezekano wa kupata kazi hiyo. Nilikuwa nimetatizika katika tabia za kishetani za kula njama, na kutafuta sifa na faida, na matendo yangu hayakuwa na dhamiri au mantiki. Lilikuwa jambo la kustahili dharau na lenye sumu. Nilikasirika sana na nikajisuta sana nilipogundua hili. Nilimwomba Mungu na nikamuuliza Aniongoze nitende ukweli ili kwamba nisifungwe na kuzuiliwa tena na tabia yangu potovu ya kishetani.

Siku moja, nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kwa kila mmoja wenu anayetimiza wajibu wake, haijalishi jinsi unavyoelewa ukweli kwa kina, iwapo ungependa kuingia katika uhalisi wa ukweli, basi njia rahisi zaidi ya kutenda ni kufikiria maslahi ya nyumba ya Mungu katika kila kitu unachofanya, na kuachana na tamaa zako za kibinafsi, nia zako binafsi, dhamira, heshima na hadhi. Yaweke maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza—hili ndilo jambo la msingi kabisa unalopaswa kufanya. Ikiwa mtu anayetimiza wajibu wake hawezi hata kufanya kiwango hiki, basi anawezaje kusemwa kuwa anatimiza wajibu wake? Huku si kutimiza wajibu wa mtu(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinielekeza kwa kanuni na mwelekeo katika kutekeleza wajibu wangu, ambayo ilikuwa kuacha tamaa yangu ya sifa na hadhi, na kuipa kazi ya kanisa kipaumbele bila kujali chochote, na kutekeleza wajibu wangu kadiri ya uwezo wangu. Ni hapo tu ndipo nitakuwa ninatimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa, na kuwa na mfano kiasi wa binadamu. Kama ningetafuta sifa na hadhi na nipuuze kazi yangu kuu, huko hakungekuwa kutimiza wajibu wangu; ningekuwa nakimpinga Mungu na kutenda maovu. Baada ya hapo, Niliwaambia ndugu zangu kuhusu haya yote katika mkutano na nikafichua upotovu wangu mwenyewe. Hawakunidharau, na kile kizingiti kati yangu na Ndugu Li kilipotea. Baada ya hapo nilishiriki kwa bidii ushirika wakati wa mikutano aliyokuwa akiendesha, na sikucheka kichinichini nilipoona dosari katika kazi yake. Badala yake, nilitoa maoni na uungaji mkono, na kila nilipomwona akiwasaidia ndugu kutatua shida zao, sikuona wivu kama hapo awali, lakini nilihisi kuwa ndani ya nyumba ya Mungu, ni majukumu yetu tu ambayo ni tofauti, si misimamo yetu. Nilitaka tu tufanye kazi pamoja ili kutekeleza wajibu wetu vizuri. Nilihisi mtulivu zaidi nilipoweka hayo katika vitendo, na baadaye niliona baraka za Mungu. Ingawa timu yetu hapo awali ilikuwa na misingi mibaya zaidi ya muziki, haikuchukua muda mrefu kabla hatujatoa wimbo wa kwanza wa Kihispania, na ulipokelewa vizuri sana na ndugu wengine.

Karibu mwaka mmoja ulipita na nilizidi kuizoea kazi hiyo. Ndugu walionekana kuyakubali maoni yangu tulipokuwa tukiijadili kazi. Na mimi kawaida niliongoza mabadilishano ya timu yetu ya kila mwezi. Nilihisi kwamba tamanio langu la sifa na hadhi lilikuwa limeridhishwa kwa kiasi kikubwa. Pia, papo hapo, kiongozi wetu aliniambia nifanye zaidi kuendesha kazi katika timu yetu. Kuheshimiwa sana na kiongozi wangu namna hiyo kulinifanya nihisi hata zaidi kuwa nilikuwa mtu mwenye talanta yenye thamani. Wakati mmoja, tulihitaji mtu achukue kazi ya ziada, na ingawa ilikuwa katika taaluma yangu, nilifanya hesabu kadhaa mawazoni: Haitaniletea umaarufu, na itachukua muda wangu. Kwa hivyo nikiifanya kazi hiyo, labda ningepoteza nadhari niliyokuwa nimeivuta kwangu. Lakini Ndugu Li akiifanya, ningeweza kujiwekea nafasi yangu mwenyewe katika timu… Nilitumia kila kisingizio kuikataa kazi hiyo, na nikapendekeza kwamba Ndugu Li aifanye badala yake. Ukweli ni kwamba nilihisi mwenye hatia na wasiwasi wakati huo, lakini nilibaki mkaidi, nikitaka kuilinda nafasi yangu. Ndugu Li alichukua kazi hiyo ambayo hakuwa na uzoefu nayo. Alikuwa hasi baada ya kukumbana na matatizo kadhaa, jambo ambalo baadaye ziliiathiri kazi yake. Baada ya kusikia kuhusu hili, bado sikutafakari kujihusu. Ndugu Li mara nyingi hakuweza kushiriki katika kazi iliyofanywa na timu yetu, hivyo mambo mengi, makubwa kwa madogo, yalikuwa jukumu langu. Kwa sababu hiyo, hamu yangu ya sifa na hadhi ilizidi kukua tu. Niliona kwamba kulikuwa na mikengeuko na upungufu katika kazi ya ndugu zangu ambayo yalikuwa yanazuia maendeleo yetu, na hili liliniacha nikiwa na wasiwasi sana. Nilikuwa msimamizi wa kazi hii, kwa hivyo kama kitu fulani kingeenda vibaya, sikujua kiongozi angefikiria nini kunihusu. Je, ningeonekana kuwa mtu asiyeweza? Sikuweza kujizuia ila kushikwa na hasira na kuwakaripia ndugu, “Mnawezaje kuita huku kufanya wajibu wenu? Je, hamwezi kushikilia malengo? Tafadhali acheni kufanya makosa ya kipumbavu.” Wote waliishia kuhisi waliozuiliwa sana na mimi. Wakati mwingine, nilikuwa nimesafiri kwa siku chache kutekeleza wajibu wangu, na niliporudi, niliona kwamba dada mmoja alikuwa ametengeneza mpangilio wa kazi bila kuujadili na mimi kwanza. Hili lilinikasirisha sana. Niliwaza, “Hii imezidi sana! Huniheshimu hata kidogo.” Nilimshambulia kabisa kwa maneno. Wakati huo huo, shida moja baada ya nyingine ilikuwa inaanza kuibuka katika timu. Maoni yangu hayakuwa yanakubaliwa na ndugu, na hata walikuwa wakinipa majibu fulani. Nilihisi huku kulikuwa tu kunifedhehesha, na hasira yangu ikalipuka. “Kwa kuwa nyinyi nyote mnaonekana kufikiria vinginevyo, fanyeni tu mnavyotaka! Na kisha mambo yanapoenda mrama, mnaweza kuyawajibikia ninyi wenyewe!” Baada ya kupiga kelele, nilihisi aina fulani ya hofu na kujishutumu. Niliwaza kuhusu jinsi nilivyokuwa nikiishi katika tabia ya kiburi, kila wakati kuwakasirikia ndugu zangu. Je, Mungu angekubali jambo hilo? Lakini kisha niliwaza, je, sikuwa nikifanya hivyo kwa sababu ya wajibu wangu? Na ni nani kati yetu ambaye hajawahi kufichua upotovu kiasi? Sikuwa kweli nimetafakari kujihusu. Siku iliyofuata, niliumia tindi ya mguu nilipokuwa nikicheza mpira wa vikapu; ilivimba kama puto na ikawa chungu sana. Sikuweza kutembea au kutekeleza wajibu wangu. Niligundua kabisa kwamba hii ilikuwa nidhamu niliyokuwa nikifundishwa na Mungu, na ni hapo tu ndipo nilianza kutafakari kujihusu. Wakati huo wote, nilikuwa nikitafuta sifa na hadhi, nikiwa mwenye kiburi, na kuwakaripia ndugu zangu. Picha hiyo ilinionekania akilini mwangu, tukio baada ya tukio, kama sinema. Nilijichukia na nikajiuliza: Kwa nini sikuwahi kubadilika kamwe? Je, Kwa nini sikujiepusha na kumwasi na kumpinga Mungu?

Siku chache baadaye, baadhi ya ndugu walikuja kuniona na wakafanya ushirika nami juu ya mapenzi ya Mungu. Pia, walisoma kifungu cha maneno Yake ambayo yaliishughulikia hali yangu hasa: “Wakimwona mtu aliye bora kuwaliko, wanamkandamiza, wanaanzisha uvumi kumhusu, au kutumia njia za uovu ili watu wengine wasimheshimu, na kwamba hakuna mtu aliye bora kuliko mtu mwingine, basi hii ni tabia potovu ya kiburi na yenye kujidai, na vile vile ya uovu, udanganyifu na kudhuru kwa siri, na watu hawa hawazuiwi na chochote katika kufikia malengo yao. Wanaishi namna hii na bado wanafikiria kuwa wao ni wazuri na kwamba wao ni watu wema. Hata hivyo, je, wana mioyo inayomcha Mungu? Kwanza kabisa, kuzungumza kutoka katika mtazamo wa asili za mambo haya, je, watu ambao hutenda hivi hawafanyi vile wapendavyo tu? Je, wao hufikiria masilahi ya familia ya Mungu? Wanafikiria tu kuhusu hisia zao na wanataka tu kufikia malengo yao wenyewe, bila kujali hasara inayopatwa na kazi ya familia ya Mungu. Watu kama hawa sio tu wenye kiburi na wa kujidai, pia ni wabinafsi na wenye kustahili dharau; hawajali kabisa kuhusu kusudi la Mungu, na watu kama hawa, bila shaka yoyote, hawana mioyo inayomcha Mungu. Hii ndiyo sababu wanatenda chochote wanachotaka na kutenda kwa utundu, bila hisia yoyote ya lawama, bila hofu yoyote, bila wasiwasi au shaka yoyote, na bila kuzingatia matokeo. Hawamchi Mungu, wanajiamini kuwa muhimu sana, na wanaona kila kipengele chao kuwa cha juu kumliko Mungu na cha juu kuliko ukweli. Mioyoni mwao, Mungu ndiye wa chini zaidi anayestahili kutajwa na Asiye na maana zaidi, na Mungu hana hadhi yoyote mioyoni mwao hata kidogo. Je, wale ambao hawana nafasi ya Mungu mioyoni mwao, na wasiomcha Mungu, wamepata kuingia katika ukweli? (Hapana.) Kwa hivyo, kwa kawaida wakati wao huzunguka wakijishughulisha kwa furaha na kuweka nguvu nyingi, wao huwa wanafanya nini? Watu kama hao hata hudai kuwa wameacha kila kitu ili kutumika kwa ajili Mungu na kwamba wamepitia shida nyingi, lakini kwa kweli, nia, kanuni, na lengo la vitendo vyao vyote ni kujinufaisha; wanajaribu tu kulinda masilahi yao yote. Je, mnaweza kusema kwamba mtu wa aina hii ni mbaya sana au la? Je, mtu asiyemcha Mungu ni mtu wa aina gani? Je, si yeye ni mwenye kiburi? Je, si yeye ni Shetani? Je, ni mambo ya aina gani ndiyo yasiyomcha Mungu? Kando na wanyama, wale wote wasiomcha Mungu ni pamoja na pepo, Shetani, malaika mkuu, na wale wanaobishana na Mungu(“Masharti Matano Ambayo Watu Wanayo Kabla ya Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya ukali ya Mungu kweli yalinitia wasiwasi. Niliona kwamba nilikuwa mwenye kiburi, mbinafsi, na mjanja, mwenye kukosa uchaji kwa Mungu kabisa. Wakati ushirikiano ulihitajika katika kazi ya kanisa, nilijua vizuri kabisa kuwa nilikuwa mwenye kufaa kabisa kufanya kazi hiyo kwa ulinganisho, lakini kwa sababu ya kudumisha sifa na hadhi yangu mwenyewe, sikufikiria chochote kuhusu kuhusika, jambo ambalo liliiathiri kazi ya nyumba ya Mungu. Nilipoona matatizo katika kazi ya ndugu ambayo yalizuia maendeleo yetu, sikushirikiana nao kutatua matatizo hayo; badala yake, nilifikiri walikuwa wakinivuta chini na kuathiri nafasi yangu ya kutokezea, kwa hivyo nilitumia nafasi yangu kuwakaripia, na wote walihisi kuzuiliwa na waliishi katika hali ya mateso. Singekubali maoni yao, pia. Nilianza kununa, nikakasirika na nikatumia wajibu wangu kutoa mawazo bila wazo, bila uzingativu wowote kuhusu jinsi kazi ya kanisa ingeweza kuathiriwa. Kwa kweli, sikuwa na talanta yoyote halisi; nilichokuwa nacho kilikuwa tu upendeleo wa muziki na shauku fulani— ilhali Mungu alikuwa na neema ya kutosha kunipa nafasi hii ili niweze kuendelea kitaaluma na katika ufuatiliaji wangu wa ukweli. Hata hivyo, badala ya kuithamini, mimi nilipigania tu hadhi na fahari kuu. Nilifuatilia masilahi yangu mwenyewe huku nikijifanya natekeleza wajibu wangu, nikiwanyanyasa ndugu zangu kama vifaa vya kunisaidia nisonge mbele. Nilikosa ubinadamu kabisa. Katika vitendo vyangu vyote, nilikuwa nikitenda uovu na kuikosea tabia ya Mungu. Lilikuwa chukizo na jambo la kumkera Mungu! Kugundua hilo kulinishtua na nilihisi kujisuta kwingi sana. Nilimwomba Mungu huku nikilia machozi: “Ee Mungu, nimekosea sana! Sitaki kuendelea kuwa mwasi na kushindana na Wewe, na sitaki kuendelea kupigania faida ya kibinafsi. Niko tayari kutubu.”

Baadaye nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI). Ufunuo huu kutoka katika maneno ya Mungu ulinipa ufahamu fulani wa mbinu za kustahili dharau za Shetani na nia mbaya ya kutumia umaarufu na faida kuwapotosha watu. Inawafunga na kuwadhuru watu kwa njia hii, kuwafanya wamsaliti na kujitenga mbali na Mungu. Sifa na hadhi ni zana ambazo Shetani hutumia kuwaangamiza watu. Nilikuwa nimeshawishiwa na kuelimishwa na Shetani tangu nilipokuwa mdogo, na kudanganywa na falsafa zake kama “Kila mtu ajitetee, ole wake ashikaye mkia” “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake” na “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini.” Nilikuwa nimezichukua kama wito wangu binfsi. Nilizidi kuwa mwenye kiburi, na katika kundi lolote daima ningepingania hadhi ili wengine waniheshimu. Hata baada ya kuwa muumini, siku zote nilifuatilia sifa na hadhi kwa sababu sikuwa nafuatilia ukweli. Niliteseka na nililipa gharama katika wajibu wangu kwa ajili ya vitu hivi, nikifanya kazi kwa bidii ili kuboresha ujuzi wangu mwenyewe. Nilishindana na kupingana na wengine, nilidhani kwamba nilikuwa mtu muhimu kila wakati nilipotimiza chochote, Niliwakemea ndugu kwa kiburi. Nilikuwa mwenye kiburi na majivuno mengi sana; sikuwa na mfano wowote wa binadamu katika jinsi nilivyoishi. Nilikuwa naishi kwa kufuata falsafa za kishetani, nikijitosa katika kupata sifa na hadhi. Sikuwaumiza wengine tu, bali pia nilifanya mambo mengine mengi ambayo yalikuwa chukizo kwa Mungu. Pia niliiathiri kazi ya kanisa kwa makosa yangu na vitendo viovu. Sifa na hadhi vimenidhuru vibaya sana. Ni hapo tu ndipo niliona kwamba falsafa za kishetani kama, “kuwa mwenye fahari,” na “kuwa bora kuliko wengine,” zote ni uwongo, na kuishi kwa kufuata uwongo huu kunasababisha upotovu na uovu zaidi tu, kukimfanya mtu amwasi na kumpinga Mungu na mwishowe, aadhibiwe na Yeye. Nilipogundua haya yote, nilihisi kwamba nilikuwa nikichukulia sifa na hadhi kana kwamba ndizo zilikuwa kamba kozi ambayo kwayo nililazimika kushikamana liwe liwalo. Kwa kweli nilikuwa kipofu na mjinga. Niliona pia kuwa ilikuwa njia ambayo ilienda kinyume na Mungu. Niliomba na kutubu mbele za Mungu. Baada ya hapo, kila nilipofikiria kuhusu kufuatilia vitu hivyo katika wajibu wangu, nilijihisi mwenye hofu sana, hivyo nilimwomba Mungu, na kuukana mwili. Kwa kuongezea, niliwaambia ndugu zangu wazi wasi nikifunua upotovu wangu mwenyewe. Baada ya muda, nilihisi kwamba nilikuwa na shauku kidogo zaidi ya kufuatilia sifa na hadhi, na nilianza kuwa na hisia ya amani ya ndani.

Baadaye, wakati kanisa lilikuwa likichagua kiongozi, tamaa yangu ya sifa na hadhi ilijitokeza kwa mara nyingine tena wakati wa upigaji kura, na vita vya ndani kwa ndani viliibuka: “Je, nimpigie Ndugu Li kura, au nijipigie mwenyewe? Kunihusu mimi, mimi si mzuri sana katika kutatua masuala kupitia ushirika kuhusu ukweli. Na yeye, basi kwa bahati mbaya ashinde, wengine watanionaje?” Niligundua kwamba nilikuwa nikitafuta umaarufu na hadhi tena, na nikahisi kwamba mawazo ya aina hiyo yalikuwa mabaya sana. Nilimwomba Mungu, nikiziacha na kuzilaani fikira kama hizo. Baadaye, kifungu kingine cha maneno ya Mungu kilinijia akilini: “Ikiwa moyo wako umejaa mawazo ya jinsi ya kufikia nafasi ya juu, au ni nini cha kufanya mbele ya wengine ili kuwafanya wakuheshimu, basi uko kwenye njia mbaya. Inamaanisha wewe unamfanyia Shetani mambo; unatoa huduma. Ikiwa moyo wako umejaa mawazo ya jinsi ya kubadilika ili uweze kupokea sura ya mwanadamu zaidi, unapatana na madhumuni ya Mungu, unaweza kumtii Yeye, una uwezo wa kumcha, unaonyesha kujizuia katika kila kitu unachofanya, na unaweza kukubali uchunguzi Wake kabisa, basi hali zako zitakuwa bora zaidi na zaidi. Hii ndiyo maana ya kuwa mtu anayeishi mbele za Mungu. Hivyo, kuna njia mbili: Moja inasisitiza tabia, kutimiza malengo ya mtu binafsi, matamanio, nia, na mipango tu; huku ni kuishi mbele ya Shetani na kumilikiwa na Shetani. Njia nyingine inasisitiza jinsi ya kutimiza mapenzi ya Mungu, kuingia katika uhalisi wa ukweli, kumtii Mungu, kutokuwa na suitafahamu au uasi Kwake, yote ili kufikia uchaji kwa Mungu na kutekeleza wajibu wa mtu vizuri. Hii ndiyo maana ya kuishi mbele za Mungu(“Mtu Akitenda Ukweli Tu Ndipo Anaweza Kuwa na Ubinadamu Wa Kawaida” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nikitafakari juu ya maneno ya Mungu, nilielewa kwamba kile Anachoangalia ni nia na mitazamo ya watu katika matendo yao—vitu hivi ni muhimu sana. Ikiwa msukumo wangu ni sifa na hadhi, na tamanio la kuwafanya wengine waniheshimu, basi hiyo itakuwa njia dhidi ya Mungu na kamwe haitanielekeza kwa ukweli, au kwa kukamilishwa na Mungu. Nilikuwa tayari kurekebisha nia zangu, na kama ningechaguliwa kama kiongozi wa kanisa au la, nilikuwa tayari kutii mipango ya Mungu na kutekeleza wajibu wangu vizuri. Baadaye, ilipofika wakati wa kupiga kura, nilizifikiria kanuni kwa makini na nikampigia Ndugu Li kura. Mwishowe, alichaguliwa kutumikia kama kiongozi wa kanisa. Sikuwa na tatizo na hilo. Hata ingawa sikuwa nimeshinda, sikuwa na majuto, kwa sababu hatimaye nilikuwa nimeutia ukweli katika vitendo, hivyo kutupilia mbali pingu za sifa na hadhi. Pia nilihisi amani ya ndani na utulivu kutokana na kutenda ukweli na kumridhisha Mungu, na kuona kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu kweli ni wokovu kwangu.

Iliyotangulia: 33. Pingu za Umaarufu na Faida

Inayofuata: 36. Kukombolewa Kutokana na Umaarufu na Utajiri

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

73. Wokovu wa Mungu

Na Yichen, UchinaMwenyezi Mungu anasema: “Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa...

31. Kushikilia Wajibu Wangu

Na Yangmu, Korea ya KusiniNilikuwa nikihisi wivu sana nilipowaona ndugu wakifanya maonyesho, wakiimba na kucheza kwa kumsifu Mungu....

62. Kuinuka licha ya kushindwa

Na Fenqi, Korea ya KusiniKabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi...

4. Jaribu la Uzao wa Moabu

Na Zhuanyi, UchinaMwenyezi Mungu anasema, “Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp