Sura ya 50

Makanisa yote na watakatifu wote wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita na kutumainia siku za usoni. Ni mangapi kati ya matendo yenu ya zamani ndiyo yanayostahili, na ni mangapi kati yao yalishiriki katika ujenzi wa ufalme? Usiwe mtu mwenye kujifanya kujua kila kitu! Unapaswa kuona wazi dosari zako na unafaa kuelewa hali zako mwenyewe. Najua kwamba hakuna yeyote kati yenu yuko tayari kuweka jitihada yoyote na kugharimika muda wowote kuhusu hili, kwa hivyo hamuwezi kupata ujuzi wowote. Mnaharibu muda wenu wote katika kula, kunywa na kustarehe. Wakati wachache wenu wanakuja pamoja mnafanya mchezo, bila kuwa makini kushiriki mambo ya kiroho maishani au kutoa maisha nyinyi kwa nyinyi. Siwezi kustahimili kuwaona mkicheka na kufanya mzaha mnapozungumza, ilhali nyinyi ni wapumbavu sana. Nimesema mara nyingi, lakini hamjui tu maana ya kile Ninachosema—je, hili si jambo ambalo liko wazi kabisa kwamba liko dhahiri kabisa kwenu? Nimesema mambo kama haya awali lakini bado hamjaridhishwa na hamkubali kile Ninachosema, mkifikiri kwamba Siwaelewi, mkifikiri kwamba kile Ninachosema sio halisi. Au yaweza kuwa kwamba hii sivyo ilivyo?

Ukishughulika na Mimi kwa uzembe basi nitakuweka upande mmoja. Wewe thubutu tu kuwa mzembe tena! Wewe thubutu tu kuwa mzembe na mvivu tena! Maneno Yangu ni kisu kinachochonga; chochote kisichopatana na mapenzi Yangu kitakatwa na kisu hiki, na hufai kuwa na nadhari sana kuhusu kujiheshimu. Ninakuchonga ili uweze kupata umbo na kufuata mapenzi Yangu. Usikose kuuelewa moyo Wangu; njia ya pekee inayokubalika ni kwa wewe kuwa mwenye kuujali moyo Wangu kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo. Ukionyesha kujali hata chembe, Mimi sitageuka mbali na wewe kwa dharau. Usilipuuze bila kufikiri kila mara; yaruhusu mapenzi Yangu siku zote yafanyike kwako.

Majeshi ya watakatifu yote yako katika nafasi tofauti, kwa hivyo bila shaka nyote mko na kazi tofauti. Lakini mnapaswa kufanya kila kitu katika uwezo wenu kugharimika kwa kweli kwa ajili Yangu, na wajibu wenu ni kufanya kila mnaloweza. Mnapaswa kuwa waaminifu katika hili, muwe na hiari kwa furaha, na kwa kweli ni sharti msiwe shingo upande. Vinginevyo, hukumu Yangu daima itakuwa juu yenu, miili yenu, roho na nafsi havitaweza kuistahimili, na kutakuwa na kulia na kusaga meno.

Iliyotangulia: Sura ya 49

Inayofuata: Sura ya 51

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp