Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Tamko la Arubaini na Tisa

Ili kutumikia kwa uratibu, mtu lazima ajiunge kwa usahihi, na pia awe mchangamfu na dhahiri. Zaidi ya hayo, mtu lazima awe na uchangamfu, nguvu, na kujawa na imani, ili kwamba wengine waruzukiwe na watakuwa wakamilifu. Kunitumikia Mimi lazima utumikie Ninayonuia, sio tu kuupendeza moyo Wangu, lakini zaidi ya hayo kuridhisha nia Zangu, ili Niridhishwe na kile Ninachotimiza ndani yako. Jaza maisha yako na neno Langu, jaza usemi Wako na nguvu Yangu, hili ndilo Ninalohitaji kutoka kwako. Je, kufuata tamaa zako mwenyewe kunafichua mfano Wangu? Je, hilo litauridhisha moyo Wangu? Je, wewe ni mtu ambaye amechunguza nia Zangu kwa dhati? Je, wewe ni mtu ambaye amejaribu kwa kweli kuuelewa moyo Wangu? Je, wewe hakika umejitoa mwenyewe kwa ajili Yangu? Je, umejitumia mwenyewe kwa ajili Yangu? Je, umetafakari juu ya maneno Yangu?

Mtu lazima atumie hekima katika kila kipengele na kutumia hekima kutembea katika njia Yangu kamili. Wale wanaotenda kulingana na neno Langu ni wenye busara zaidi kuliko wote na wale wanaotenda kulingana na neno Langu ndio watiifu zaidi. Ninachosema kinakuwa na huhitaji kujadili na Mimi au kujaribu kunishawishi. Kila kitu Ninachosema Ninasema nikiwa na wewe akilini (bila kujali kama mimi ni mkali au mpole), ukilenga kuwa mtiifu hilo litakuwa jambo zuri, na hii ndiyo njia ya hekima ya kweli (na ndiyo njia[a] ya kuepuka hukumu ya Mungu kukupata). Leo katika nyumba Yangu usiwe na heshima mbele Yangu na kusema mambo mengine nyuma Yangu. Nataka uwe wa utendaji; huhitaji kutumia maneno ya kuvutia. Kwa wale ambao ni wa utendaji, kuna kila kitu. Kwa wale ambao sio, hakuna kitu. Hata mwili wao utarejeshwa kwa kutokuwepo pia, kwa sababu bila utendaji, kuna utupu tu; hakuna maelezo mengine.

Katika imani yenu katika Mungu Nawataka muwe wenye bidii na si kufanya mambo[b] kwa manufaa na hasara zenu wenyewe au kwa ajili yenu wenyewe tu; mnapaswa kutafuta tu kuweka miguu yenu katika njia ya kweli, na msitingike kwa ajili ya mtu yeyote au kudhibitiwa na mtu yeyote. Hii ndiyo inayojulikana kama kuwa nguzo ya kanisa, mshindi wa ufalme, lakini kufanya vinginevyo kunamaanisha wewe hustahili kuishi mbele Yangu.

Hali zinaweza kutofautiana, kama vile njia za kuwa karibu na Mimi. Watu wengine hupenda kusema maneno yanayosikika kuwa mazuri na kutenda kwa njia ya ibada mbele Yangu. Hata hivyo, nyuma ya matukio wao wamevurugika kabisa na maneno Yangu hayapo kabisa katika yale wanayoyatenda. Wao ni wa kuchukiza na wa kukasirisha; haiwezekani kwamba wangeweza kumletea mtu ujenzi wa maadili au kuwa na kitu cha kuruzuku. Ninyi hamwezi kuuzingatia moyo Wangu na hiyo ni kwa sababu tu hamwezi kuwa na ukaribu zaidi au kushiriki na Mimi, ninyi huniacha daima Niwe na wasiwasi na kufanya kazi kwa bidii kwa niaba yenu.

Tanbihi:

a. Maandishi asili yameacha "na ndiyo njia."

b. Maandishi asili yameacha "kufanya mambo."

Iliyotangulia:Tamko la Arubaini na Nane

Inayofuata:Tamko la Hamsini

Unaweza Pia Kupenda